Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Nguruvi3,
Yaani wewe huwezekaniki wala hueleweki.Ulipoandika haya ulikuwa na maana gani
Ahaa , nimekuelewa sasa. Ngoja nikuambie kitu. Baada ya kubaini nafasi ni chache, wakazi wa Kilimanjaro wakahamia maeneo mengine. Huko waliendelea kufaulu kwasababu ushindani wa kule walikotoka ulikuwa mkubwa na uliwajenga watoto. Hutapenda hii lakini ni ukweli mtupu.

Unahitaji mfano mzuri ?

Hapa hoja si shule tena, hayo yalikuwa kujenga hoja. Kilichopo mbele yetu ni kuhusu takwimu za supreme ambazo si kuwa hazipo sawa, bali hakuzifanyia uchambuzi, wala hakutumia maarifa kufafanua kama kipo kizuri alichokusudia

Kilichomuongoza kufikia hatua ya shambulio ni ACT na Zitto kuwa na chuki dhidi ya wananchi wa mikoa waliyoishambulia kisiasa. Hakuna ushahidi mikoa hiyo ilitenda lipi baya, hakuna! Ni shambulio tu

Leo wanarudi kusaidia mount Meru Hospitali baada ya kubaini kuwa hoja zao zimeudhi umma, zimekera na zimeonyesha rangi zao kamili.

Mkuu, tetea hoja. Kama Zitto alisoma tu data mkutanoni, hivi unategemea mwanakijiji angeelewa nini tofauti na tunavyosema?

Je, ilikuwa sahihi kusoma data zinazohitaji uchanganuzi kama alivyoonyesha Mchambuzi hapo juu kwa average Tanzanian

Wewe umeshindwa kuzijibu seuse mkulima!
 
Mkuu acha uchizi mimi sio mjinga kiasi hicho. Wewe umesema shule za Mwanga zilikuwa na wanafunzi 6000 walokaa mtihani na wakafaulu 62 nafasi nyingine wakapewa wa mikoani hata kama viwango vya ufaulu vilikuwa vodogo.

Inahusiana nini na wana Kilimanjaro kuhama ati wakaenda mikoani ili wapate marks ndogo? hujui hata kudanganya..Kwa mwana saikologia kama mimi huwezi nipaka mafuta ya mgongo mkuu, nimeshajua wewe ni mtu wa aina gani na una upeo gani kama wabaguzi wengine wanaoogopa kuambiwa ukweli. Kwa hiyo inatosha. Endelea na mada yako ya ACT dhidi ya Chadema sijui UKAWA..
 
Mkuu Mkandara.

Hii data ya Mwanga sijui kaipata wapi ngoja aje atufahamishe.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu fanya marekebisho kiduchu kwenye ili bandiko lako kisha tuendelee na mjadala wetu ACT – Wazalendo na Supreme Leader.

Kuna watu wanaweza kutumia ili bandiko lako kama reference na hizo data za Mwanga.

Ahsante.
 
Nikisoma hoja za Mchambuzi , Barubaru , nguvuri3 , Mkandara hoja #433 , #439 na #440 Zakumi na wengineo wote mnakubaliana kuwa maendeleo hayapimwi kwa GPD tu bali kwa kuangalia zaidi Tax Revenues, Historia ya eneo fulani, mwamko, idadi ya mashule, idadi ya watu, hosp na nk. na katika uchambuzi yakinifu wa mchambuzi amesema kuwa GPD inapatikana kwa kuchukua jumla ya uzalishaji kugawanya na idadi ya watu. Hivyo basi kila mtu anaelewa kama GPD ni kigezo pekee cha maendeleo basi mikoa yoote yenye wakazi wachache ingekuwa imepiga hatua mbele kimaendeleo kuliko mikoa yenye watu wengi.

Hivyo basi kama tunakubaliana kuwa GPD si kigezo cha kuangalia maendeleo katika mikoa yetu, basi tutakuwa tunakubali kuwa Zitto alifanya makosa kutoa mfn ya Arusha na Kilimanjora kuwa inamaendeleo kuliko Shinyanga kwa vile tu Shinyanga wanachangia zaidi katika pato la Taifa.

Na kama tunakubalina na hili basi hapa ndipo hoja ya nguvuri3 inaposimama kuwa pamoja na kuwa Zitto ni mchumi mzuri lakini anatumia lugha za kilaghai kufarakanisha watu. Labda kama Zitto au Adharusi wana maelezo tofauti na haya.. Natumaini Adharusi pindi atakapopata nafasi atakuja kutoa ufafanuzi ni nini Zitto alikusudia na kujibu maswali yangu no.#767
 
Mnatafuta namna ya kuondoka katika zinazomkabili supreme.

Nimeeleza kwa ufasaha kuwa nafasi ziligawanywa kwa mikoa baada ya mitihani ya kitaifa kubadilishwa na kuwa ya mikoa.
Hadi hapo kama huelewei basi tena

Tunasema hivi data za Zitto kama alivyoleta Adharusi na Mkandara ndizo tunajadili

Mchambuzi kaonyesha bila chembe ya shaka nini HDI. Watetezi wa supreme hakuna anayejaribu kugusa huko.

Tumeuliza, Mkandara anaposema supreme anaonewa kwa kwasababu tu kasoma data mkutanoni, tunamuuliza je ilikuwa sahihi kwa supreme kusoma data nzito na pana kama za HDI katika mkutano wa wananchi wa kawaida kabisa?

Je, Supreme alifafanua kile kilichomo ndani ya HDI?

Ni kwanini alitumia ufanano wa mikoa ya Shinyanga(16) na Kilimanjaro(9) na Arusha(7) na wala si Shinyanga na mikoa namba 1-6? Hamgusi huko
Alinda kamuuliza Adharusi na Mkandara, kuna uhusiano gani wa ato la taifa na maendeleo ya Shinyanga/Mwanza/K'njaro/Arusha? Mumekimbia

Mchambuzi kauli kama data ni za HDI kwanini zisitumike kwa Sumbawanga vs Kigoma ikiwa Sumbawanga inachangia GDP kubwa na Kigoma wana Revenue kubwa? Mumekimbia

Tumemuuliza Mkandara, baada ya uhuru kuna ushahidi gani wa wananchi wa Kilimanjaro kupewa fursa zaidi ya Shinyanga? Tumepewa jibu wao wana maji hivyo ni rahisi kuwekeza. Tumeuliza hayo maji yanaletwa na malori kutoka hazina? Mitini

Sasa watu waatafuta namna ya kufionyanga maneno. Hamtuondoi katika hoja hata kidogo.

Mchambuzi kaweka data mkasema zimepitwa na wakati. Adharusi kaweka, hamuwezi kutetea. Mkandara katupa zake zinamshatkai supreme.

Kauli ya supreme ni shambulio kwa taifa. Ulaghai hauwezi kufichwa kwa ujanja ujanja.

Jambo jema, hata ninyi mnatambua kwa hoja na takwimu ''supreme aliteleza ulimi'' na sasa kilichopo mbele yake ni kuueleza umma nia ya kulimega taifa imekusudia nini na kwanini? Hii si vita ya kanda kama anavyotaka iwe ni vita ya walaghai dhidi ya taifa

Hatutakaa kimya
 
Alinda, tumeshawishiwa kuwa data za Mchambuzi hazifai. Tukaomba halisi kwa mujibu wao

Wameleta za HDI, Mchambuzi kazifinyanga finanyanga hakuna jibu.

Mkandara anasema Zitto alisoma tu katika mkutano, asilaumiwe
 
Nakubaliana nacho au laa kwamba nini? Sijaelewa, tupe mtazamo wako wa kiuchambuzi. Vinginevyo naona kama ni kiwewe cha kulemewa hoja.

NB: pitia pia kipande hiki bofya database kushoto kisha tazama basic demographic and social economic indicators - upate kuona serikali ina wajibu gani sio wananchi, wao ni matunda ya serikali ilowajibika kwao.

Kwanini nibofye badala ya wewe kutueleza hilo? Na iwapo ni kweli kwamba serikali ina wajibu kwa wananchi, wajibu huo unatekelezwa na kipi kati ya GDP na Tax Revenues za wananchi?

Je unakubali kwamba Kodi ya serikali ni fedha za wananchi? Ikiwa unakubali kwamba fedha za serikali chanzo chake wananchi, kuna ubaya gani wananchi ku - mobilze fedha zao kwa njia nyingine mbadala kama vile michango kwa ajili ya miradi ya maendeleo badala ya kusubiri mgao wa kodi kwa ajili ya kila kitu?
 
Mkuu kuna maswali mengine hayajibiki kwasababu hapa si mahala pake.

Kwa mfano, uliuliza kwanini tunapata marais kutoka makabila madogo, sijui nikujibu nini maana unatakiwa utueleze kabila la Mwinyi ni lipi? Pili, utueleze tatizo ni Rais au ni rank nzima ya uongozi. Tutakapokujibu tayari umeshaanda dhana ya dini. Huko hatutaki kwenda

Kwa mtazamo wa haraka kuna kitu zaidi unachotaka kuzungumzia. Unaposema kwanini hatupigi vita nepotism, nashangaa maana sijui kama uliwahi kuona tulivyo na tunavyosimama kidete dhidi ya uhuni na wahuni kama BoT n.k.

Hatujafiki nepotism ya kiwango unachotaka tuamini, ndio maana tunapiga vita sana watu wanaosimama katika majukwaa kama supreme leader wakianzisha mijadala ya hovyo kama ule wa Kili Vs Shinyanga

Pili, umekubali kuwa maendeleo ni tatizo kwa nchi nzima hata katika mkoa mmoja.

Kama unakubali tofauti hizo, basi tuungane kukemea kauli za upotoshaji za supreme kuwa wapo walioendelea zaidi ya wengine kwasababu za kinyonyaji

Tatu, unakosea unaposema tukiongelea Shinyanga Vs Kili ni wasukuma na Wachagga.
Nimempa Mkanadara darsa la Kilmanjaro. Ni uelewa finyu kudhani kuwa wazaliwa wa Kilimanjaro ni wachagga. Inasikitisha.

Nne, labda utueleze prerequist ya maendeleo ni kitu gani.

Mimi nasimama kuwa ni elimu, si Tanzania bali dunia nzima. Wenzetu wenye akili wanajua hilo ndio maana hawachezi makida na elimu kama sisi. Tafuta mkoa mmoja, angalia wilaya hadi kijiji halafu uje tutaongea kwa kuchepuka chepuka

Hata supreme leader anajua hilo
 
Alinda, tumeshawishiwa kuwa data za Mchambuzi hazifai. Tukaomba halisi kwa mujibu wao

Wameleta za HDI, Mchambuzi kazifinyanga finanyanga hakuna jibu.

Mkandara anasema Zitto alisoma tu katika mkutano, asilaumiwe

Hivi unatumia akili zote hizi kumjadili Ayatollahh!!?? Nadhani haujetendei haki hili linawafaa labda kwa watu wa karibu yake kama Mkandara na wale wa Deen yetu.
 
walanalimegaje Taifa,wakati wewe ndio uliemlisha Maneno kwa kujitoa uelewa kwa chuki zako, Mchambuzi na Nguruvi3 kazi yao kutafsiri kwa chuki maelezo ya watu wasiowapenda,wako tayali wakusingie neno,ata kama ujasema.
 
Last edited by a moderator:
Alinda:
Kiasi kikubwa cha matumizi ya serikali kinaenda kwenye sehemu yenye watu wengi.

Katavi ina idadi Ya wananchi Karibia sawa na Mbozi, au Kwimba, Au Nzega au Kilosa. Lakini hizi Ni Wilaya, huku Katavi ikipewa hadhi Ya mkoa. Je kati Ya wilaya Hizi nne na mkoa wa Katavi, Ni Wapi kiasi kikubwa cha matumizi Ya serikali yanaenda? Je Ni kutokana na idadi Ya wakazi wa maeneo husika kweli?
 
walanalimegaje Taifa,wakati wewe ndio uliemlisha Maneno kwa kujitoa uelewa kwa chuki zako, Mchambuzi na Nguruvi3 kazi yao kutafsiri kwa chuki maelezo ya watu wasiowapenda,wako tayali wakusingie neno,ata kama ujasema.

Vipi, Laptop bado ipo kibiti? Nilitarajia utakuja kupangua hoja kwa hoja za kitakwimu.
 
Last edited by a moderator:
Sawa kabisa sasa inajulikana kwamba Zitto alitumia GDP kuonyesha jinsi mfumo mbovu wa mikataba unavyoweza kuwagharimu wananchi wa Shinyanga!
Zitto hajui uchumi basi, Ni mbabaishaji mbali Ya kuwa mlaghai na mbaguzi. Tukijikita Katika ukweli unaojitokeza kwamba Zitto hajui uchumi, je:

Matatizo yetu Ni volume of output (GDP) contribution Ya sekta Ya Madini au mapato Ya Kodi katika sekta Ya Madini? Tanzania sasa Ni top three in terms of output Ya mining sector in Africa. Tanzania sasa inavutia wawekezaji wakubwa kutoka kila pande ya dunia Kuja kuwekeza Kwenye mining sector, lakini kwa kauli yako japo juu hence Ya supreme zitto, hilo Ni tatizo. Nini kigumu kujua kwamba Kilio Chetu Ni low revenues and not large output Ya sekta Ya Madini?

Kwa kweli mnasikitisha sana na mchumi wenu uchwara Zitto Kabwe.
 
Last edited by a moderator:
Vipi, Laptop bado ipo kibiti? Nilitarajia utakuja kupangua hoja kwa hoja za kitakwimu.
Kawaida yao, wakiona jiko moto wanatulia.Uzi ukisonga mbele utaona wanachomoa bandiko na kuanza kulijadili kana kwamba hawakuona ya nyuma

Huyu tulikubaliana na data zake za fb, nashangaa kashidwa kusimama kuzitetea
Anasema watu wana chuki, yaani alitaka tumeze fb style
 

Nguruvi3:

Usiseme kwa mfano wakati nimeuliza swali moja mara nne na kukuomba utoe maoni au majibu yako. Ulishindwa kufanya hivyo. Nitakuelewa ukisingizia sababu za kiufundi kwa sababu naona bado unashindwa kujibu swali lenyewe na yale ya zaida.

Vilevile kuna maswali mengine ni rethorical questions. Yanaulizwa kujenga hoja na sio kupata majibu. Kuhusu Mwinyi, Yeye kazaliwa mwanalomango, Kisarawe na ni Mzaramo.

Kuhusu kukemea sina mamlaka ya kukemea mtu na vilevile sina mamlaka ya kuzuia haki za mtu za kikatiba. Zitto ana haki zake za kikatiba ambazo ni zilezile zilizokupa wewe na Mchambuzi uwezo wa kumwita Zitto Supreme Leader, Evil, mlaghai, --------- na kadharika.

Hakuna democracy tambarare.
 

Supreme Mchumi unalazimisha point. Ni vyombo vingapi vya kiserikani vipo kwenye eneo lenye watu wengi? Afu umekimbia swali langu. Ngoja nirudie.

Je umerudisha kadi ya yanga (CCM)?
 

Alendi:

Hiyo definition ni GDP au GDP per capital? Ufafanuzi. Sisi wengine shule tulikimbia.

Kuhusiana na maneno ya Zitto, wengi hapa mko trained kuchambua facts. But you have to understand that politics isn't about facts, but narratives. Those who control narratives always win.
 


Mchambuzi:

Naomba uonyeshe sehemu niliyosema kuwa GDP tells the whole story. Ama sivyo hayo ni maneno yako.

Pili kumbuka kuwa hata wenye mawazo unayoyaona ya kibaguzi na hatari kwa usalama wa taifa ni watanzania na wana haki zao ya kitaifa na kikatiba. Hivyo mtazamo wako haukufanyi kuwa more Tanzanian than others.

Mada kamili ni ACT - mpini wa CCM kumaliza upinzani. Wewe si CCM, tuambie kwanini mnataka kuua upinzani? Usiwe unamlaumu Zitto wakati Taasisi yako ndio yenye kuendesha hujuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…