Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Ikiwa hotuba ya Zitto ni hiyo hapo juu aloiweka Ritz ebu nifafanulie ni wapi kasema Dhulma inafanywa na mikoa hiyo na sio mfumo (mrengo) wa serikali tawala, pengine mimi sielewi!
Hii hotuba aliyoweka Ritz, wewe umeanza kuiona lini?

Kuna rekodi za kutosha kabisa, tuakuwekea za kwako na Zitto

Kuna nyakati unaonekana kama punguani. Umesahau hataulichokuwa unajadili kwa mwezi mzima.

Unaamini kabisa alicholeta Ritz,rudi nyuma uone kama kuna aliyejadili nukuu zake.

Unajua mkuu unakera. Yaani supreme ni kijana mdogo sana kiumri na exposure, kaukufanya unaonekana ze comedy.

Hebu tupitie kumbu kubu utaona jinsi unavyoadhirika. Mkuu kama huna cha kusema unaweza kujisitiri kwa kukaa kimya
 
Alinda wanachotaka kunibadili mwelekeo wa mjadala.Wameingiza hadi udini, tumekataa, wameingiza gesi Mtwara, tumekataa! Spinning zinaendelea
 
Mabandiko5 yalifuata Ritz akichangia vema sana, soma hitimisho lake

Mkuu Mchambuzi.

Naona kumbe Zitto hizo takwimu akutoa kichwani mwake wote mmezitoa sehemu moja ingawa miaka tofauti.
Leo Ritz anakuja na hotuba ‘mpya' ya Zitto.

Mkandara alichangia mabandiko (tunayo) halafu anamwambia Mag3 leo ameona hotuba ya Zitto kupitia Ritz!!!!


Alinda kaweka nukuu tarehe hadi twits za supreme, watuwamefumbia macho

Mtahamisha magoli sana, the bottom-line supreme anawajibika kwa kauli zake .

Tuta m-hold supreme responsible perfect and square.Msituondoe kwenye mada

Hatutakubalitaifa ligawanywe na genge la wenye uchu. Tutasema, tutakemea.

ACT mpini inaendelea…

 
Naona umehamaki kweli kweli lakini hotuba ya Zitto imefinyanga hoja zenu na kuzitupa kwenye takataka, umebakia kurusha ngumi hewani hauna pakushika tena nimefurahi sana na wewe unatafuta utetezi kupitia twitter na Facebook mwanzo ulikuwa unaponda, hivi mkuu haujui kama Mwanza aligawanywa na kutoka mkoa wa Geita nakuwekewa tena hotuba ya Zitto.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.

Mpini unaendelea...
 
Last edited by a moderator:
Mag3, nilichogundua kumbe mnashikiana akili na wewe unapinga kuwa hiyo siyo hotuba ya Zitto mbona mnajidhalilisha kiasi hicho kuna watu wanawasoma kwa ukaribu mno mnajivunjia heshima zenu ili huamini kama hiyo hotuba ni ya Zitto nikuwekee nini audio au youtube.
 
Last edited by a moderator:
Alinda wanachotaka kunibadili mwelekeo wa mjadala.Wameingiza hadi udini, tumekataa, wameingiza gesi Mtwara, tumekataa! Spinning zinaendelea
Nguruvi3.

mkuu mbona Leo unapwelepweta sana kulikoni!? zitto kakuambia tatizo ni mfumo. unamtaka sasa aanze kueleza kila kitu kwenye mfumo hapana yeye amejikita kuliangalia hilo la utofauti wa maendeleo yakiuchumi kwenye mikoa yetu ni michango yake kwenye uchumi jumla wa taifa hili. wapi unakwazika mkuu? Sidhani kama kuna mtu kaingiza mambo ya udini zaidi ya jamaa zako kutuambia wadini.
 
Ritz kuondoa mzizi wa fitina tupe chanzo cha hiyo habari..

Pia ni vizuri kuacha hizi kejeri na mipacho hisiyo kuwa na maana, Tuko hapa kushindana kwa hoja, kujifunza,kuelimisha na nk.

Kejeri, mipasho, matusi tuyaache katika jukwaa la siasa. Hatuko hapa kusoma mipasho maana kama mtu anataka kusoma mishapo najua sehemu ya kwenda. Tuko hapa kujifunza.

Katika huu uzi tumejifunza mambo mengi kupitia kwa Mchambuzi, nguvuri3, Mkandara, Barubaru, Zakumi, Alinda 🙂teeth🙂 Mag3 , JokaKuu, na wengineo. Hawa watu wameacha shughuli zao za maana na kuja hapa kushare na sisi elimu yao. Hivyo basi hatuna budi kuheshimu michango yao kwa kuwambia "Asante" na asante si kwa neno "asante" bali pale tunapojaribu kujenga hoja za kusaida taifa letu, kuuliza maswali kwa nia ya kujifunza. Kaka yangu Mkandara na Ngurur3 ninawakubali sana maana bila hawa hakuna mjadala.. Nimewasoma sana hawa watu na nimegundua kwamba huwa hawakubalini katika mambo mengi, lakini kutokubaliana kwao ni kwa ajili ya kujifunza.. leo hii nimepata ufahamu wa mambo mengi kwa kutokubaliana kwa hawa watu ,

Mf. Mwanzo sikuhufahamu kwanini Mtwara ni masikini ingawaje kuna gas/au Ni vipi Mtwara itafaidika na Gas lakini kutoka na michango ya hawa watu mbali mbali nimeelewa ni kwanini na ni vipi Mtwara wanaweza kufaidika na Gas. Hivyo hivyo kwa Shinyanga na nk. Hii elimu nisingeitapa kama mwanzo wa huu mjadala ungeanza na kejeri na mishapo. Kwa hili asante sana Mkandara na Ngururi3.


Pia tukumbuke pia watu wengi wanakuja kusoma na kujifunza kutoka kwetu, ukiangalia views wa hii thread ni zaidi ya elf 40 hii si kwamba ni mimi na wewe tu bali kuna watu mbali mbali wanakuja kutusoma na miongoni mwa hao ni wanasiasa na hawa wanajifunza vitu fulani kutoka kwetu. Hii topic inahusu Zitto na ACT lakni kimantiki inahusu kila mwanasiasa na kila chama aliyekuwa/chenye ana maono kama ya Zitto.

Na pia hii topic inamjenga Zitto zaidi kuliko kumbomoa maana watu wanasema mapungufu yake bila kumuonea haya na yeye ninavyomfahamu atayafanyia kazi.

Kukosoa mwanasiana au kusema mapungufu ya mwanasiasa si kwa ajili ya wivu au kutompenda bali ni katika kumjenga na kujenga chama chake. Tuchukulie mfn Chadema , sisi sote ni mashuhudu jinsi Chadema alivyokuwa inaingia kikaangoni, na kwa bahati nzuri chadema wakachukua zile "nagatives" wakazifanyia kazi leo tunaona matunda ya wanaJf waliokuwa hawasifii kila kitu bali wanasema ukweli kwa nia safi.

Ni kweli kuwa wakati mwingine unaweza kukwazika na kejeri za watu mbali mbali juu ya viongozi lakini hizo ndo siasa zetu na wasisi wa hizi siasa kwa bahati mbaya ni hawa hawa wanasiasa na mashabiki wao, hebu kila mtu ajifikirie ni kiongozi gani ambaye hajaingia katika kikaango cha kejeri? Tumeshuhudia rais walivyokuwa wanamvua nguo, tumeshuhudia jinsi Dr. Slaa na mkewe walivvyovuliwa nguo, na je kuna mtu amehonja matusi na kejeri kama Mbowe? ukisha pata jibu utaona ni kia mwanasiasa amepita katika kikaango hiki tena wengine tumeshuhudia makubwa zaidi ya haya mfn. Picha za Lema na nk.

Lakini ili litusifanye sisi watu wa jukwaa ili kuingia katika hii mitengo, haya mambo tuwaachie "watoto" sie ni watu wazima ni mfano kwao.

Na kwa hili nitamuomba mkuu Invisible atusaidie tusije anza kuharibu ili jukwaa kama jukwaa la siasa.

Hivyo basi wanaukumbi turudini kwenye hoja tuache viloja..
 
Alinda.

Naona umeandika huku umehamaki sana na kunishambulia mimi unanionea bure mimi sijafanya kejeli wala kumtukana mtu yeyote hapa ukumbini.

Inawezekana haupendi ninachokiandika hapa ukumbini mimi takushauri kitu kimoja tu jifunze kusoma vitu usivyovipenda.

Vile vitu unavyovipenda kuvisoma hauombi source vile usivyovipenda ndiyo unaomba source. Alinda Nguruvi3 anamuita Mkandara The Comedy upo kimya au sababu aliyesoma una mahaba nae.
Zitto.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.

Source: Radio Free Africa Mkutano wa ACT - Wazalendo Viwanja vya Furahisha Mwanza.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana
 

..Zitto ndiye anayeamini ktk hayo mambo ya mikoa fulani kudhulumu mikoa mingine. mambo ya kuchonganisha jamii moja vs nyingine.

..mimi siamini kama kuna mkoa au jamii fulani hapa Tz inaishi kinyonyaji na kudhulumu mikoa na jamii nyingine.

..hata mikoa ambayo iko nyuma kimaendeleo au jamii ambazo ziko nyuma kimaendeleo naamini zinapaswa kusaidiwa ili maendeleo yamfikie kila Mtanzania.
 
Mkuu na ndio maana sipendi kabisa kujadili na wewe, leo naonekana Punguani, mbona mimi situmii matusi haya napojadili na wewe.. Pumbavu mkubwa. Usiniandikie lolote na wala sitaki kujadili na wewe tena. Shenzi mkubwa.
 
Mkuu na ndio maana sipendi kabisa kujadili na wewe, leo naonekana Punguani, mbona mimi situmii matusi haya napojadili na wewe.. Pumbavu mkubwa. Usiniandikie lolote na wala sitaki kujadili na wewe tena. Shenzi mkubwa.
Nawaomba radhi wanajamvi kwa kusoma hayo.

Kwa kawaida duru tuna utulivu, yanapotokea kama haya tunavumiliana.

Kuna nyakati wanadamu wanaghafilikiwa, wajibu wetu si hamaki wala taharuki ni kuangalia wapi kuna mghafala.

Nawaomba asiwepo yoyote atakayetaharuki au kujibu kauli hizo.

Mkuu Mkandara, tunakuombea kwa mola akujaze hekma na busara, akupe utulivu na subra katika kipindi hiki kigumu cha majadiliano.
 
Mkuu na ndio maana sipendi kabisa kujadili na wewe, leo naonekana Punguani, mbona mimi situmii matusi haya napojadili na wewe.. Pumbavu mkubwa. Usiniandikie lolote na wala sitaki kujadili na wewe tena. Shenzi mkubwa.
Mkuu wangu Mkandara pole sana nimeshangaa sana matusi uliyotukanwa watu wamejipa upofu kama hawayaoni na kwenda kunishambulia mimi kuwa naleta kejeli...Daaa!!! Mbaya zaidi kafahamishwa mpaka Invisible.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Mkandara pole sana nimeshangaa sana matusi uliyotukanwa watu wamejipa upofu kama hawayaoni na kwenda kunishambulia mimi kuwa naleta kejeli...Daaa!!! Mbaya zaidi kafahamishwa mpaka Invisible.
Unajua kuna watu hushindwa kujenga hoja na wewe ndio unakuwa hoja yao na huyu jamaa ndio kawaida yake siku zote. Kibaya zaidi tumejadili vizuri tu humu, ghafla matusi yanakuja wala sielewi kwa nini. Huyu Zitto sijui kawafanya nini kiasi kwamba amekuwa mwiba kwao kiasi hiki hata wanaojaribu kuwa na mawazo tofauti basi nao Punguani.

Kama ndivyo, kuna sababu gani ya mjadala huu ikiwa sote tutakubaliana kuwa ACT ni mpini wa CCM au Zitto ni msaliti?. Kazi yake huyu jamaa anataka ku control watu waseme nini, waandike nini na maandishi yake tu ndio yapite bila kupingwa..Nashukuru sintomjibu mtu huyu ktk mada yoyote maana sii muungwana.
 
Mkandara , kwanza uelewe shughuli ya kauli za maudhi umeifanya sana huko nyuma. Zipo kumbu kumbu. Kwa sisi wenye kujali wenzetu na kuwatazama kama wanadam huwajibu hivi Pili, kuna tatizo la lugha linajitokeza, kwa minajili ya mjadala na ufahamu siku za baadaye, tunaomba tuweke sawa.

Umekereka na neno supreme leader, tukakuomba tafasiri nyingine maana tuliyo nayo inamaanisha kiongozi mkuu.
Hukuweza kusema hata kwa kuparaza. Tunafahamu ni lugha tu inayotatiza has ainapochanganywa na hisia na mahaba

Na ni mwendo huo huo ndio unaozaa tafasiri nyingine mbovu.

Neno punguani si tusi, ni hali ya mtu kuwa na mapungufu. Miongoni mwetu kila mmoja ana mapungufu.
Mapungufu yako ni kubadilika badilika katika hoja au kutokuwa na uaminifu katika kile unachosimamia(spinning)

Mfano, wakati supreme leader anasema UKAWA ni wasaka tonge ulijitokeza na kusema hakuwa na maana hiyo hata pale kila ushahidi ulionyesha supreme alikusudia hilo.

Adharusi alipokuja na takwimu, ulisimama kidete kusema supreme leader yupo sahihi kwa yale aliyosema

Baada ya muda ukaja na data zako, na ghafla ukahamia zingine. Kote huko unabadilika badilika, usichobadilika ni utetezi wako dhidi ya supreme. Haya ndiyo mapungufu tunayosema, si kosa ni mapungufu na ndiyo yanazaa neno punguani( pungufu)

Kuhusu supreme leader, katiba ya ACT/Wazalendo/Wajamaa/Watanzania inasema 'kiongozi mkuu ndiye nuru na taswira ya chama''. Hapa kinachoongelewa ni kauli zake kama kiongozi mkuu wa ACT akiwa supreme. Kauli zake haziwezi kutengwa na supremacy yake

Imeshangaza, ulipokuja na kumweleza Mag3 uwepo wa data mpya zaidi ya zile ulizotetea mwezi mzima.

Wiki mbili ziilizopita ni MKandara alituambia '' Zitto alisema, Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki, Shinyanga inachangia sana haipati stahiki''

Hukuchukua muda wa kujibu hoja za Mchambuzi na Alinda zenye vyanzo.

Ndipo tukasema supreme anawajibika kwa kauli zake na si vema kuleta utetezi katika upungufu.

Hakuna shaka, kauli za Kitila kuhusu supreme na mapungufu yake ya kauli tata inazidi kupata nguvu.

Historia ya kauli zake inaanzia mbali. Tumeonyesha na hansard za bunge zinaonyesha jinsi alivyoshambulia Kilimanjaro

Tumehoji, iweje takwimu zake zilenge Kilimanjaro ambayo kitakwimu haipo katika kundi la kuangaliwa? Hakuna jibu

Tunakubaliana kupingana, hata hivyo ni muhimu sana kuwa na mjadala ongofu na wenye uaminifu zaidi ya mahaba

Ni kwanini tunasema huu ni mpini wa CCM? Yale waliyokuwa wanasema CCM ndiyo anayafanyia kazi.
Takribani mwezi na kitu CCM wapo likizo, kule jukwaa la siasa vijana wakirushiana maneno machafu katika ukanda

Na wewe hapa(kumbu kumbu zipo) umesimama kutetea kwa dhati mgawanyo usio sawa wa pato na rasilimali dhidi ya mikoa iliyowezeshwa kama Kilimnjaro vs Shinyanga.

Nyote wawili mnatuondoa katika focus dhidi ya dudumizi na kuchanganya umma. CCM wapo likizo, mkuu huoni mpini huo?

Labda tukuulize, bado unasimama na kauli ya ''Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki, na Shinyanga inachangia sana haipati stahiki"" au unasimama na Adharusi na takwimu au haya mengine yanayoibuka?
 
Na historia ipo wazi, wakati wa kujadili EAC na tume ya Kamala, supreme leader yupo ubaoni akisema ''Msiogope EAC,maana hata sisi tuna tofauti ya maendeleo kati ya Kigoma na Kilimanjaro.

Kauli hii haikwenda uzuri masikioni mwa wananchi hasa walioguswa nayo wa kanda husika

Katika takwimu zote zilizoletwa na watetezi hapa jamvini, hakuna hata moja inayo onyesha K'njaro ipo katika 5 bora za mendeleo.
Hii maana yake ni kuwa Kilimanjaro kwa supreme ni zaidi ya maendeleo, kuna kitu nyuma yake

Inapokuja suala la takwimu ambazo hazinyumbulishwi, huku akiendelea na kauli zile zile za Kuilamu Kilimanjaro dhidi ya mikoa mingine, supreme anajenga hoja isiyo na shaka kuhusu chuki yake dhidi ya maeneo hayo.

Mchambuzi alisema hivi '' Sumbawanga inachangia GDP kubwa Reveneu kidogo. Kigoma inachangia Revenue kubwa GDP kidogo'' kwanini supreme asiangalie kwa mtazamo mpana wenye mantiki kama huo?

Kwanini asilinganishe Shinyanga na Kagera, aende moja kwa moja katika namba 9 kimaendeleo?
 
Last edited by a moderator:
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…