Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii hotuba aliyoweka Ritz, wewe umeanza kuiona lini?Ikiwa hotuba ya Zitto ni hiyo hapo juu aloiweka Ritz ebu nifafanulie ni wapi kasema Dhulma inafanywa na mikoa hiyo na sio mfumo (mrengo) wa serikali tawala, pengine mimi sielewi!
Alinda wanachotaka kunibadili mwelekeo wa mjadala.Wameingiza hadi udini, tumekataa, wameingiza gesi Mtwara, tumekataa! Spinning zinaendeleaHaya ni maneno ya Zitto Kabwe katika facebook yake tarehe 5 April..
Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.
Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.
Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu
Na hapa ni katika faceboo ya Zitto ya tarehe hiyo 5. April
Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.
Ritz kinachojadiliwa ni hicho kipengele ambacho Zitto aliamua kwa makusudi kukichomoa katika report kwa chuki zake kwa watu wa Kili/ARusha.
Kama hisinge kuwa chuki basi Mkoa wa kujadiliwa ulikuwa ni Lindi maana ni mkoa ambao unachangia kidogo sana katika pato la taifa lakini ni mkoa wa 9 kimaendeleo. Sasa tujiulize kwanini Lindi. Lakini si mikoa ambayo Kil/Arusha maana hii mikoa hiko katika mikoa 10 ya uchangiaji wa pato la taifa.
Mabandiko5 yalifuata Ritz akichangia vema sana, soma hitimisho lake@Adharusi, Mkandara:
Kwa mujibu wa Zitto (nimenukuu sehemu):
"Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu"].
Hapa Zitto ana maana gani na hili neno "Huwezi"? Analenga kufanikisha nini?
Walengwa hapa ni wananchi maskini wasio na uelewa mpana kuhusu maneno kama ‘pato la taifa'. Sidhani kama Zitto hatambui hilo. Wanachoelewa wananchi walio wengi katika hadhara hiyo ni kwamba wanapunjwa, wanaonewa, wanabaguliwa, wananyonywa. Wanafanyiwa haya na nani? Kwa hoja ya Zitto, wabaya hawa ni wananchi kutoka mikoa mingine iliyopiga hatua kimaendeleo. Ukweli ni kwamba adui wao namba moja ni sera mbovu za Chama Cha Mapinduzi lakini cha ajabu ni kwamba Zitto hakitaji kabisa CCM katika hoja hii wakati CCM ndio ‘the common denominator'. Ni Ni katika hili ndio maana Nguruvi3 anajadili jinsi gani ACT ni mpini wa CCM kumaliza upinzani kwani badala ya kuungana na ukawa kuelezea wananchi juu ya sera mbovu za CCM, Zitto anakilinda CCM na kuhamishia lawama wananchi wa mikoa mingine ambayo imekuwa na juhudi za aina mbalimbali kujiendeleza. Hii ni hatari sana.
Zitto anaendelea kusema:
"Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora".
Kwa kauli hii, Zitto anazidi kuwagawa wananchi. Kauli hii ‘mobilizes' wananchi wasio nacho waungane against wananchi walionacho. Vinginevyo, Zitto alishindwa nini kwenda katika kila mkoa na kujadili matatizo na changamoto zao individually huku akiwashirikisha katika mawazo juu ya the way forward ikiwa ni pamoja na kujadili fursa zilizopo ndani na nje ya mazingira yao?
Hoja hii ya Zitto is very ‘regressive and divisive'. Kwanini nasema hivyo? Ni hivi:
Watanzania ni watoto wa familia moja, kama ilivyo kwa watoto waliozaliwa, kukuzwa na kuishi katika nyumba moja. Kama tunakubaliana katika hilo, basi tutakubaliana pia kwamba haikuwa busara kwa Zitto kuwafananisha watoto wa nyumba moja kwa lugha za kuwagawanya, lugha yenye kuonyesha kwamba kuna watoto ambao wanapendelewa na ambao wanaendelea kwa kunyonya wengine. Nyumba inayoongozwa kwa namna hii kamwe haiwezi kudumu. Itabomoka kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zitto anaendelea:
"Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP."
Zitto hapa anazidi kujenga uhasama na uadui mkubwa ambao moto wake kuuzima itakuwa ni vigumu sana mbeleni. Tumeshajadili kwamba wananchi hawa hawana uelewa mpana juu ya concepts anazotumia Zitto. Lakini awali tuliona pia jinsi gani Zakumi alivyojadili juu ya umuhimu wa wanasiasa to take advantage of illiteracy and ignorance of the masses for political and private gain. Walichoelewa wananchi hapa sana sana ni kwamba wapo wananchi mikoani ambao mchango wao ni mdogo sana lakini wanafaidika au wanakula zaidi kutokana na kuwanyonya wengine. Kwa mfano, zitto anawaeleza wananchi kwamba wana-Lindi hawana mchango wowote wa maana katika pato la taifa lakini wana maendeleo makubwa kuliko wasukuma wa Shinyanga ambao mchango wao ni mkubwa zaidi ya wana-lindi.
Zitto anazidi kusema kwamba:
"Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%."
Hapa, zitto hafafanui kwamba Dar-es-salaam ni mkoa wa wananchi wote kama ilivyokuwa kwa wananchi wa mikoa mingine. Hawaelezi wananchi kwamba wana ruhusiwa kwenda popote nchini kutumia fursa zilizopo. Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inatoa haki kwa raia yeyote kuishi mahali popote na kufanya shughuli yoyote ili mradi havunji sheria za nchi. Ndio maana ni kawaida kwa mikoa Fulani Fulani kuwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kipato au kiuchumi ingawa kiasili, hawatoki mikoa hiyo. Zitto akija kuhutubia Jangwani atawaeleza nini Wazaramo? Kwani ni wazi kwamba kwa DSM, wanao ongoza kwa mafanikio ya kiuchumi ni wananchi kutoka mikoa mingine kabisa, sio wazaramo?
Zitto anaendelea kusema:
"DSM inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%.
Kauli ya hatari sana. Maana ya ‘kabla haijagawanywa' ni nini? Na kabla haijagawanywa kwenda wapi au kuchukuliwa na nani na kwa sababu gani? Zitto haji na ufafanuzi wenye mantiki ya kiuchumi, badala yake anakuja na uchochezi wa kiwango kikubwa sana.
Zitto anaendelea kusema:
"…Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 kuchangia Pato la Taifa."
Huu ni mwendelezo wa ujenzi wa chuki, uadui, mgawanyiko na uhasama mkubwa sana baina ya wananchi wa Shinyanga na Mikoa mingine kama tulivyojadili.
Zitto anamalizia kwa kusema:
"Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7".
Hapa, Zitto haelezi ni kwanini mikoa hii ina maendeleo zaidi. Kwa uwazi kabisa, Zitto hapa anachonganisha mikoa ya Kilimanjaro na Arusha dhidi ya mikoa mingine. Kwa hoja hii, tafsiri nyepesi kabisa kwa wananchi husika ni kwamba Kilimanjaro na Arusha ni mikoa ambayo haina michango ya maana katika pato la taifa lakini wananchi wake wamepiga hatua kimaendeleo kwa njia za hila hila, unyonyaji na upendeleo.
Tusikubali Zitto atugawe kama taifa.
Leo Ritz anakuja na hotuba ‘mpya' ya Zitto.
Naona umehamaki kweli kweli lakini hotuba ya Zitto imefinyanga hoja zenu na kuzitupa kwenye takataka, umebakia kurusha ngumi hewani hauna pakushika tena nimefurahi sana na wewe unatafuta utetezi kupitia twitter na Facebook mwanzo ulikuwa unaponda, hivi mkuu haujui kama Mwanza aligawanywa na kutoka mkoa wa Geita nakuwekewa tena hotuba ya Zitto.Mabandiko5 yalifuata Ritz akichangia vema sana, soma hitisho lake
Leo Ritz anakuja na hotuba mpya ya Zitto.
Mkandara alichangia mabandiko (tunayo) halafu anamwambia Mag3 leo ameona hotuba ya Zitto kupitia Ritz!!!!
Alinda kaweka nukuu tarehe hadi twits za supreme, watuwamefumbia macho
Mtahamisha magoli sana, the bottom-line supreme anawajibika kwa kauli zake .
Tuta m-hold supreme responsible perfect and square.Msituondoe kwenye mada
Hatutakubalitaifa ligawanywe na genge la wenye uchu. Tutasema, tutakemea.
ACT mpini inaendelea
Mag3, nilichogundua kumbe mnashikiana akili na wewe unapinga kuwa hiyo siyo hotuba ya Zitto mbona mnajidhalilisha kiasi hicho kuna watu wanawasoma kwa ukaribu mno mnajivunjia heshima zenu ili huamini kama hiyo hotuba ni ya Zitto nikuwekee nini audio au youtube.Pamoja na juhudi za kututoa kwenye mada ya Nguruvi3 inayosema; Re: Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani, naomba nikuulize Mkandara, kwa nini unaamini hayo ndiyo maneno aliyoyatamka Supreme Leader akiwa Shinyanga? Sijui kwa nini leo umwamini Ritz kwa kutoa nukuu anayodai ni ya Zitto...huu ushikaji umeanza lini! Kabla sijarudi kwenye mada na mimi naomba nikukumbushe kidogo onyo lililotolewa na Kamati ya Usaliti chini ya Samson Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo, nanukuu;
Mkuu Mkandara, mtu anayeongelewa hapa ni huyo huyo aliyekuwa anatengenezewa njia ili siku akitua chamani moja kwa moja atawazwe kuwa Kiongozi Mkuu (hata katiba ilikuwa inamsubiri!). Hapo tahadhari inatolewa jinsi asivyokuwa na busara na alivyo mwepesi katika kutoa matamshi bila kufikiria madhara yake katika jamii. Lakini kama nilivyotahadharisha hapo mwanzo haya tuyaache turudi kwenye mada iliyoko mezani...Re: Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani!
Supreme Leader hakuitaja mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa bahati mbaya, aliitaja kwa kukusudia lakini kama kawaida yake hakuzingatia ni jinsi gani matamshi yake yangepokelewa katika jamii. Ni katika mikakati hiyo hiyo aliwaita wana UKAWA wasakatonge bila kufikiria athari zake kwa watu wanaopigania mabadiliko ya kweli katika nchi hii. Yeye alichokusudia ni kuzidi kuwafurahisha wale ambao alikuwa na hakika wangempigia vigelegele kwa matamshi yake hayo...nasikia sasa anajuta, kasahau majuto ni mjukuu!
Nguruvi3.Alinda wanachotaka kunibadili mwelekeo wa mjadala.Wameingiza hadi udini, tumekataa, wameingiza gesi Mtwara, tumekataa! Spinning zinaendelea
Ahsante sanaRitz kuondoa mzizi wa fitina tupe chanzo cha hiyo habari..
Pia ni vizuri kuacha hizi kejeri na mipacho hisiyo kuwa na maana, Tuko hapa kushindana kwa hoja, kujifunza,kuelimisha na nk.
Kejeri, mipasho, matusi tuyaache katika jukwaa la siasa. Hatuko hapa kusoma mipasho maana kama mtu anataka kusoma mishapo najua sehemu ya kwenda. Tuko hapa kujifunza.
Katika huu uzi tumejifunza mambo mengi kupitia kwa Mchambuzi, nguvuri3, Mkandara, Barubaru, Zakumi, Alinda 🙂teeth🙂 Mag3 , JokaKuu, na wengineo. Hawa watu wameacha shughuli zao za maana na kuja hapa kushare na sisi elimu yao. Hivyo basi hatuna budi kuheshimu michango yao kwa kuwambia "Asante" na asante si kwa neno "asante" bali pale tunapojaribu kujenga hoja za kusaida taifa letu, kuuliza maswali kwa nia ya kujifunza. Kaka yangu Mkandara na Ngurur3 ninawakubali sana maana bila hawa hakuna mjadala.. Nimewasoma sana hawa watu na nimegundua kwamba huwa hawakubalini katika mambo mengi, lakini kutokubaliana kwao ni kwa ajili ya kujifunza.. leo hii nimepata ufahamu wa mambo mengi kwa kutokubaliana kwa hawa watu ,
Mf. Mwanzo sikuhufahamu kwanini Mtwara ni masikini ingawaje kuna gas/au Ni vipi Mtwara itafaidika na Gas lakini kutoka na michango ya hawa watu mbali mbali nimeelewa ni kwanini na ni vipi Mtwara wanaweza kufaidika na Gas. Hivyo hivyo kwa Shinyanga na nk. Hii elimu nisingeitapa kama mwanzo wa huu mjadala ungeanza na kejeri na mishapo. Kwa hili asante sana Mkandara na Ngururi3.
Pia tukumbuke pia watu wengi wanakuja kusoma na kujifunza kutoka kwetu, ukiangalia views wa hii thread ni zaidi ya elf 40 hii si kwamba ni mimi na wewe tu bali kuna watu mbali mbali wanakuja kutusoma na miongoni mwa hao ni wanasiasa na hawa wanajifunza vitu fulani kutoka kwetu. Hii topic inahusu Zitto na ACT lakni kimantiki inahusu kila mwanasiasa na kila chama aliyekuwa/chenye ana maono kama ya Zitto.
Na pia hii topic inamjenga Zitto zaidi kuliko kumbomoa maana watu wanasema mapungufu yake bila kumuonea haya na yeye ninavyomfahamu atayafanyia kazi.
Kukosoa mwanasiana au kusema mapungufu ya mwanasiasa si kwa ajili ya wivu au kutompenda bali ni katika kumjenga na kujenga chama chake. Tuchukulie mfn Chadema , sisi sote ni mashuhudu jinsi Chadema alivyokuwa inaingia kikaangoni, na kwa bahati nzuri chadema wakachukua zile "nagatives" wakazifanyia kazi leo tunaona matunda ya wanaJf waliokuwa hawasifii kila kitu bali wanasema ukweli kwa nia safi.
Ni kweli kuwa wakati mwingine unaweza kukwazika na kejeri za watu mbali mbali juu ya viongozi lakini hizo ndo siasa zetu na wasisi wa hizi siasa kwa bahati mbaya ni hawa hawa wanasiasa na mashabiki wao, hebu kila mtu ajifikirie ni kiongozi gani ambaye hajaingia katika kikaango cha kejeri? Tumeshuhudia rais walivyokuwa wanamvua nguo, tumeshuhudia jinsi Dr. Slaa na mkewe walivvyovuliwa nguo, na je kuna mtu amehonja matusi na kejeri kama Mbowe? ukisha pata jibu utaona ni kia mwanasiasa amepita katika kikaango hiki tena wengine tumeshuhudia makubwa zaidi ya haya mfn. Picha za Lema na nk.
Lakini ili litusifanye sisi watu wa jukwaa ili kuingia katika hii mitengo, haya mambo tuwaachie "watoto" sie ni watu wazima ni mfano kwao.
Na kwa hili nitamuomba mkuu Invisible atusaidie tusije anza kuharibu ili jukwaa kama jukwaa la siasa.
Hivyo basi wanaukumbi turudini kwenye hoja tuache viloja..
Jokakuu:
You are implying kuwa Zitto alisema hivyo. Na ingekuwa kweli kama Tanzania ingekuwa na mikoa mitatu tu: Shinyanga, Arusha na Kilimanjaro. Lakini kwa sababu Tanzania ina mikoa zaidi ya 25, Shinyanga haiwezi kudhulumiwa na Arusha na Kilimanjaro pekee yake.
Mkuu na ndio maana sipendi kabisa kujadili na wewe, leo naonekana Punguani, mbona mimi situmii matusi haya napojadili na wewe.. Pumbavu mkubwa. Usiniandikie lolote na wala sitaki kujadili na wewe tena. Shenzi mkubwa.Hii hotuba aliyoweka Ritz, wewe umeanza kuiona lini?
Kuna rekodi za kutosha kabisa, tuakuwekea za kwako na Zitto
Kuna nyakati unaonekana kama punguani. Umesahau hataulichokuwa unajadili kwa mwezi mzima.
Unaamini kabisa alicholeta Ritz,rudi nyuma uone kama kuna aliyejadili nukuu zake.
Unajua mkuu unakera. Yaani supreme ni kijana mdogo sana kiumri na exposure, kaukufanya unaonekana ze comedy.
Hebu tupitie kumbu kubu utaona jinsi unavyoadhirika. Mkuu kama huna cha kusema unaweza kujisitiri kwa kukaa kimya
Nawaomba radhi wanajamvi kwa kusoma hayo.Mkuu na ndio maana sipendi kabisa kujadili na wewe, leo naonekana Punguani, mbona mimi situmii matusi haya napojadili na wewe.. Pumbavu mkubwa. Usiniandikie lolote na wala sitaki kujadili na wewe tena. Shenzi mkubwa.
Mkuu wangu Mkandara pole sana nimeshangaa sana matusi uliyotukanwa watu wamejipa upofu kama hawayaoni na kwenda kunishambulia mimi kuwa naleta kejeli...Daaa!!! Mbaya zaidi kafahamishwa mpaka Invisible.Mkuu na ndio maana sipendi kabisa kujadili na wewe, leo naonekana Punguani, mbona mimi situmii matusi haya napojadili na wewe.. Pumbavu mkubwa. Usiniandikie lolote na wala sitaki kujadili na wewe tena. Shenzi mkubwa.
Unajua kuna watu hushindwa kujenga hoja na wewe ndio unakuwa hoja yao na huyu jamaa ndio kawaida yake siku zote. Kibaya zaidi tumejadili vizuri tu humu, ghafla matusi yanakuja wala sielewi kwa nini. Huyu Zitto sijui kawafanya nini kiasi kwamba amekuwa mwiba kwao kiasi hiki hata wanaojaribu kuwa na mawazo tofauti basi nao Punguani.
Mkandara , kwanza uelewe shughuli ya kauli za maudhi umeifanya sana huko nyuma. Zipo kumbu kumbu. Kwa sisi wenye kujali wenzetu na kuwatazama kama wanadam huwajibu hiviUnajua kuna watu hushindwa kujenga hoja na wewe ndio unakuwa hoja yao na huyu jamaa ndio kawaida yake siku zote. Kibaya zaidi tumejadili vizuri tu humu, ghafla matusi yanakuja wala sielewi kwa nini. Huyu Zitto sijui kawafanya nini kiasi kwamba amekuwa mwiba kwao kiasi hiki hata wanaojaribu kuwa na mawazo tofauti basi nao Punguani.
Kama ndivyo, kuna sababu gani ya mjadala huu ikiwa sote tutakubaliana kuwa ACT ni mpini wa CCM au Zitto ni msaliti?. Kazi yake huyu jamaa anataka ku control watu waseme nini, waandike nini na maandishi yake tu ndio yapite bila kupingwa..Nashukuru sintomjibu mtu huyu ktk mada yoyote maana sii muungwana.
Pili, kuna tatizo la lugha linajitokeza, kwa minajili ya mjadala na ufahamu siku za baadaye, tunaomba tuweke sawa.Mkandara;12717003]Mkuu wakati mwingine mnabisha vitu kiupuuzi sana wakait mnajua tofauti baina ya GDP na Renevue..Sielewi kwa nini mnataka takkwimu wakati mnaweza zipata kirahisi kabisa. haya nenda hapa tafuta table namba 26 kisha angalia mwaka 2010.
Na hata hadi kufikia 2014 au kesho, bado Shinyanga inachangia sana GDP kutokana na madini lakini kidogo tu kinaingia kama revenue kwa sababu madini hayatoi ajira nyingi wala kuanzishwa miradi mingine itknayo na madini hayo.. Kuna mengi unaweza jifunza pia kupitia hapaNguruvi: Mkuu ni katika upuuzi wetu tunafaidika na huduma za ujanja wako.
Mkuu tusaidie sasa, ingawa hizo si takwimu alizotumia supreme na hata unaona WanaMahaba wake mnavyopingana, tungependa utufahamishe, kipi hasa kimetumika katika kauli ya supreme, Revenue au GDP?
Usichoke tusiadie, ndilo lengo la elimu kwa umma
Na historia ipo wazi, wakati wa kujadili EAC na tume ya Kamala, supreme leader yupo ubaoni akisema ''Msiogope EAC,maana hata sisi tuna tofauti ya maendeleo kati ya Kigoma na Kilimanjaro.P
Supreme Leader hakuitaja mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa bahati mbaya, aliitaja kwa kukusudia lakini kama kawaida yake hakuzingatia ni jinsi gani matamshi yake yangepokelewa katika jamii. Ni katika mikakati hiyo hiyo aliwaita wana UKAWA wasakatonge bila kufikiria athari zake kwa watu wanaopigania mabadiliko ya kweli katika nchi hii. Yeye alichokusudia ni kuzidi kuwafurahisha wale ambao alikuwa na hakika wangempigia vigelegele kwa matamshi yake hayo...nasikia sasa anajuta, kasahau majuto ni mjukuu!
Alinda.
Naona umeandika huku umehamaki sana na kunishambulia mimi unanionea bure mimi sijafanya kejeli wala kumtukana mtu yeyote hapa ukumbini.
Inawezekana haupendi ninachokiandika hapa ukumbini mimi takushauri kitu kimoja tu jifunze kusoma vitu usivyovipenda.
Vile vitu unavyovipenda kuvisoma hauombi source vile usivyovipenda ndiyo unaomba source. Alinda Nguruvi3 anamuita Mkandara The Comedy upo kimya au sababu aliyesoma una mahaba nae.
Tena kuna sehemu Nguruvi3 anamuita Mkandara punguani na ilo Alinda hajaliona,unawezaje kumtukana anaetumia verified I'd wakati yeye amevaa mask