Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Nguruvi3.

JF ni jukwaa huru sasa unapowambia watu wanipuuze kisa nimeleta hotuba ya Zitto huo ni udhaifu wa fikra.

Ungefanya la maana ili watu wanipuuze ungekuja na hotuba ya kweli ya Zitto ungeeleweka zaidi sasa unakuja na maneno matupu mkuu.

Nimekusoma unasema umeanza kumjadili Zitto toka tarehe 5 huo ni uongo kumbukumbu zipo taziweka wanaukumbi waone au ulikuwa unajadili facebook.

Wewe endelea kunipuuza mimi sina tatizo na kupuuzwa, mimi nimejikita zaidi kuwafahamisha wanaofuatilia huu mnakasha siyo kukufurahisa wewe na imani siyo wote watakao nipuuza ni wafuasi wako tu.
 
Last edited by a moderator:

unachokisema Mkandara ni sahihi baada ya Mchambuzi na Nguruvi3 kupiga kelele kuwa tumekimbia mjadala au tunachungulia tu,na kusema tumekimbia Maswali ya Mage3 kila siku nikiingia katika Uzi utasikia jibu maswali ya Mage3 nikawaambia nipo mkoani,laptop sina, natumia simu Mchambuzi akaja kuniletea mizaa,nikaona niwajibu hivyo hivyo kwa kutumia simu maana walitaka na chanzo cha takwimu za Zitto nikawapa bado hawataki.
Mkandara nilichojifunza katika ishu ya Takwimu tusitegemeee Nguruvi3 Mchambuzi magie3 wataleta data zitakazo kuwa upande wa Zitto,na Takwimu zozote zitakazo kuwa kinyume na mtazamo wao Hawatazikubali Habadani
 
Last edited by a moderator:

Waberoya anawajua vizuri sana huyu Mchambuzi na Mwenzie kuwa wana Chuki kali mno dhidi ya Zitto!. Zitto afanye jema gani, hawa watu wawili watafukunyua, watafukunyua mpaka waone hata sehemu Zitto aliposahau kuweka kituo kwenye Sentensi., Then wataamplify hiyo kitu as if ni issue, kumbe siyo issue kabisa.
Hawa watu na Saed Kubenea ni type moja, wao wapo kama Walinzi wa Kusubiri Zitto apande mbegu wao wakapande magugu.

Hawana hoja za msingi, hoja zao ni uwongo, Mtima Nyongo, na sijui wananufaika na nini kwa hizi Character Assasination dhidi ya ZZK.
 
Ulisema utarudi kujibu maswali, ndiko huku. Takwimu umeleta mwenyewe, tumekuuliza umekimbia, uzi umesogea unaingia kati. Wewe nenda kafikirie majibu, halafu urudi hapa. Siyo mahali pa kutupa takwimu tumeze tu ikiwa wewe mwenyewe huwezi kuandika hata mstari mmoja wa kutetea.

Rejea bandiko langu ujibu hoja kwanzam huku kwingine tuachie. Hangaika na maswali uliyosema utarudi kujibu
 
Mkuu Gamba la Nyoka.

Kwa hii kauli yako lazima Supreme Leader wa ili jukwaa atatoa amri kwa vijana wake wakupuuze siyo kweli wewe muongo haujamsikiliza Zitto lakini nashukuru kumbe tupo wengi tunasimamia ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Sisi hatumezi tu. Soma uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wanyo-rasilimali-za-taifa-6.html#post12518131

Je, hao wote wana chuki na supreme leader.

Sisi tuna chuki na jinsi anavyotaka kuligawa taifa kwa misingi ya uhutu na utusi

Kilimanjaro haina uhusiano wa aina yoyote na matatizo ya Kigoma.

Hoja kwamba wao wameendelea kwasababu wanachangia kidogo wanapata sana ni kufilisika kisiasa.

Mkandara anasema hivi '' Zitto kasema, Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki, Shinyanga inachangia sana haipati stahiki' Hata hivyo K'njaro na Arusha ni 7 na 9 katika maendeleo na Shinyanga ni 16.

Mawazo kama haya ya supreme laeder na Mkandara ni hatari sana.

Kwamba mikoa isijiletee maendeleo ikimsubiri supreme leader aje na mgao wa pato la taifa kulingana na uchangiaji.

Hawa ndio wenye chuki hasa. siyo sisi. Tunataka supreme afanye siasa siyo kutugawa kwa Uhutu na Utusi. Hayo alipaswa kuyajua, ametoka Kigoma!

Jibu hoja, kuna uhusiano upi kati ya maendeleo ya mikoa ya kaskazini na uchangiaji wa pato na mgao wa pato

Hapo ndipo unatakiwa ujikite siyo hoja dhaifu cha chuki ambazo huna ushahidi nazo

Takwimu za Mchambuzi, Mkandara na Zitto sipo hapo, tusaidie kutuelewesha mahusiano ya kanda ya kaskazini na matatizo ya mikoa mingine
 
Hawana hoja za msingi, hoja zao ni uwongo, Mtima Nyongo, na sijui wananufaika na nini kwa hizi Character Assasination dhidi ya ZZK.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wanyo-rasilimali-za-taifa-6.html#post12518131

Ni hivi hoja za kusakama mikoa ya kaskazini hazikuanza leo. Nenda hansard za Bunge, supreme yupo akishambulia mikoa hiyo, tukampa benefit of doubt kama ulimi kuteleza. Alipoanza kuhusbiri kwenye twits kuhusu chuki na mikutanoni, hatuwezi kunyamaza

Tunajua lengo lao ni kuua upinzani, hilo wanaweza kulifanya, lakini si kuua taifa.
 
Kwani Kilimanjaro na Arusha ni mikoa Untouchable kiasi kwamba haitakiwi kutumiwa kama mifano katika ujenzi wa hoja?
Jibu ni hapana. Tatizo ni pale ana single out mikoa hiyo ambayo ukiangalia kimaendeleo ni ya 7 na 9. Vipi 1-6 mbona haiongelei.

Pili, ni pale anapotumia vigezo dhaifu kujenga hoja. Huwezi kulinganisha Kilimanjaro na Shinyanga kwa eneo na rasilimali.
Anapotuhumu mikoa hiyo bila kuangalia vigezo vingine ni uchochezi

Kama ungalisoma kuanzia mwanzo, tumeeleza nini maendeleo na nini vichocheo vyake

Hakuna sababu za aina yoyote kulaani mikoa inayojiendeleza eti kwa matatizo ya mikoa mingine

Thibitisha kuwa wananchi wa kanda ya kaskazini wanachukua pato zaidi, wanapanga hujuma dhidi ya wenzao

Soma hapa chini uone Watanzania wanavyomlaani, na ndilo hasa lililotulazimu kuangalia kwa hoja na mantiki
tukijua kuwa supreme ameliekeleza taifa kubaya

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wanyo-rasilimali-za-taifa-6.html#post12518131
 

Kauli ya Zitto ni hii hapa, hebu Tuelezee, katika kauli hii kasingle out vipi Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro?

"Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu".

Vipi Lindi Hamuioni?, Mbona mnasemea Kilimanjaro na Arusha tu, au ZZK Kapiga Ikulu nini ?
 
..kila mkoa na kila jamii hapa Tanzania ni untouchable unapoleta hoja za kufitinisha, kuchonganisha, na kuwagawa wa-Tanzania.

cc TRUVADA, Nguruvi3
Haswaa ndiyo maana tukasema, unaweza kuzungumzia mikoa kama taifa na siyo mikoa kadhaa dhidi ya kadhaa

Huwezi ku single out mikoa miwili, ukaisokomezea lawama na kuinyanynyasa bila ushahidi kama alivyofanya SL

Tumeuliza, iweje mifano ya supreme leader ijikite kwa mikoa miwili ambayo haipo katika top 6 za maendeleo?

Leo akienda Lindi atawaambia nini? Akienda Singida atawaambia nini?


Siasa za ukanda ndizo alizolaani, leo anasimama katika kilinge akihubiri. Huu ni ulaghai uliotamalaki na lazima tuamke sasa

Hatuwezi kulaani CCM kwa kuchochea habari za udini na Ukanda, ikiwa walioshika mpini tunawaacha, hapana! siasa za kijana zimepita kiwango. Akemewe kwa nguvu zote
 
Mkuu hiyo siyo kauli ya Zitto. Period! kama unataka nenda kasome nyuma nimemuuliza ile ya Adharusi vipi?

Pili, hiyo si kauli pekee tunayojadili. Tumeanza kuanzia April 5 alipoandika katika twits n.k.

Jibu hojazako na si kujadili mambo yaliyotengenezwa.
 
halafu soma hii Kitu kizuri tunawatandika na hoja zenu wenyewe

Huyo unayedhani amekupa kauli ya Zitto, alikuwa hana ufahamu hadi tarehe 13. Soma hapa chini
MkuuMkandara.

BahatinzurinduguyetuhapaukumbiniMkuuAdharusikutuliteaushahidiwatakwimualipozipataZittolakiniMchambuzihatakianaitaulaghaingojatumsubiriNguruvi3maanakapigasanakeleleakiombahizotakwimu.
Huyo anayeleta kauli hizo aliunga mkono kwa dhati kauli ya Adharusi kama alivbyomnukuu Zitto

Yaani wiki 3 alikuwa hana ufahamu, leo anakuja n akusema alisikiliza hotuba free Afrika radio

Unajua msidakie vitu msivyojua, spinning tumezipuuza sana kwa bahati mbaya wapo walioingia katika mtego, ona unavyoadhirika

Huna background ya mjadala kuanzia tarehe 5 jhadi hapa tulipo. Umekuja na hoja, zote huna majibu, sasa unadandia vitu vinakuacha ukiwa na tahayari.

Halfu namnukuu Mkandara kuhusu kauli ya Zitto ili kukongezea hoja

''Zitto alisema, Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki, Shinyanganga inachangia sana haipati stahiki''

Huyu ni mtetezi wa supreme leader, na amemnukuu Zitto, sasa tuambie hiyo kauli unasemaje! Ni kweli au uongo?

Sasa angali nukuu tatu tofauti zingine zikinyofolewa ukweli

Hoja hii tumeizika

Mkuu mbona hujibu hoja?
Kuna uhusiano gani wa pato, uchangiaji na maendeleo kwa kuhusisha mikoa ya kanda ya kaskazini kama anavyohubiri Zitto

Kama hukubaliani na swali hilo, tueleze, wapi unasimama, kwa Mkandara, Adharusi au hiyo tuliyoipuuza au tuletee mpya

Data umeomba ukapewa, hukutia mguu. Tena zao na zetu
Hoja umeleta ukijibiwa unakimbia

Hatutakubali supreme leader aligawe taifa hili hata kidogo.

Kanda ya kaskazini haina tatizo na kand zingine.
 
Nguruvi3.

Ukiwa muongo lazima uwe na kumbukumbu unasema umeanza kujadali kauli ya Zitto toka terehe 5 mtu mzima kusema uongo ili kutimiza malengo siyo vizuri.

Hapa chini mchango wako wa kwanza kwenye hotuba ya Zitto tarehe 19 April 2015.

Nguruvi3.
ACT inakuja kutimiza malengo yaliyoshindikana walikotoka(Mag3).

Focus ya wananchi ni kuunga mkono upinzani ili kuondoa donda ndugu la miaka 50 linalowatafuta.

Jana Zitto anawaambia wananchi wa Shinyanga,mikoa ya Kilimanjaro na Arusha inachangia pato dogo lakini ipo katika kumi la kwanza la maeneo yaliyopiga hatua

Hakutumia busara kwasabau hoja yake haiungwi mkono na historia, jitihada na jiografia kwa uchache wa kusema.

Alitoa hoja ilikuwaaminisha wananchi wa Shinyanga kuwa yeye ni mtu wa eneo lao na hivyo wakatae watu wa ‘maeneo’ tajwa.

Lengo lilikuwa kuwazuia wananchi kuunga mkono upinzani kwa kutumbukiza hoja chafu, dhaifu na kipuuzi ya kuwagawa

Hoja aliyotumia ni ile ya CCM wanayotumia kuhusu vyama vyakikanda na kikabila.

Hapa Zitto akiwa ‘mpinzani’ kabeba mpini wa shoka la CCM kuondoa focus ya wananchi kuhusu CCM na kubomoa upinzani. Umeelewa.

Page ya 13...leo hii unawadanganya Wanaukumbi kuwa umeanza kujadili maneno ya Zitto toka tarehe 5 April 2015.

Ukiweka bandiko lako lalote la kujadili kauli ya Zitto kabla ya tarehe 19 achilia mbali tarehe 6 najitoa JF.

Teh teh teh teh.
 
Last edited by a moderator:
Wanaukumbi.

Nguruvi3 kaja na madai mapya kaingizwa chaka na Alinda.

Anadai kaanza kujadili kauli ya Zitto kuanzia tarehe 5 April 2015.

Pitie huu uzi nyuma mjionee wenyewe lini alianza kujadili kauli ya Zitto.
 
Last edited by a moderator:

niliitoa Facebook baada ya nyinyi kutaka source ya Takwimu zake
 
Hapa kuna chuki Gamba la Nyoka? Kuna tofauti gani na tunachojadili hapa?


Alichoongea Kimweri si ukweli?
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3.

Natafuta michango yako ya tarehe 5 April ambayo unasema mlikuwa mnajadili Zitto na kauli yake nimepata huu mchango wako wa tarehe 6 April 2015. Tufahamishe zile twits mlikuwa mnazijadili wapi mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Natafuta michango yako ya tarehe 5 April ambayo unasema mlikuwa mnajadili SL na kauli yake nimepata huu mchango wako wa tarehe 6 April 2015. Tufahamishe zile twits mlikuwa mnazijadili wapi mkuu.

Nadhani sasa unataka kunishawishi kwa nguvu nipuuze mabandiko yako...! Hoja kuu hapa ni Chama cha ACT-Mpini wa CCM kumaliza upinzani. Sub-hoja ni Kauli ya SL kuligawa taifa kwa kuwachonganisha watanzania aliyoitoa kanda ya Ziwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…