Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

[/QUOTE]

Hivi kwa akili zako tu za kawaida ulizojaliwa na Mwenyezi Mungu unaona hayo majibu yako yanaendana na maswali yangu? Yaani unataka kusema umeshindwa kujibu hayo maswali? Yaani umeshindwa kufafanua nini maana ya hiyo paragraf? Kweli?
 
Mimi nasubiri Nguruv, atuwekee hotuba ya ZZK akiwa kule " site" kwa wananchi ili tuone huo uchochezi wa ZZK, mambo ya Facebook amesema hayataki.

Hofu yangu mimi ni tusije tukaspin kauli halisi ya ZZK, ndiyo maana nataka hotuba neno kwa neno, ili kila mtu ajisomee mwenyewe, tumhukumu ZZK kihalali kabisa
 
Kweli hivi viloja,tuonyeshe kwa ushahidi usio na Shaka wapi Zitto alisema,Matatizo ya Shinyanga yanaletwa na Kilimanjaro, ukileta najitoa JF,nakuacha na Alinda wako
CC
Ritz Mkandara

Hivi mbona unataka kufanya huu mjadala ni wa kushinda na kushindwa? huu ni mjadala sisi tunaona hayo maneno yanajenga chuki miongoni wa watu wa mikoa husika.. Sasa kama wewe hukubaliani na sisi ni wajibu wako na wewe kujenga hoja inayoonyesha hayo maneno yanajenga umoja miongoni mwa watu wa mikoa husika... Hiki ndicho tunachotaka na ndo maana ya mjadala/majadiliano ni pande mbili zinazokidhana.

Hivyo basi baada ya hayo maelezo tupe maana ya hayo maneno kwa upande wako au kwa jinsi unavyoelewa.
Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.

Mimi nasubiri Nguruv, atuwekee hotuba ya ZZK akiwa kule " site" kwa wananchi ili tuone huo uchochezi wa ZZK, mambo ya Facebook amesema hayataki.

Kwa maana hiyo unakubaliana na mimi kuwa maneno ya Zitto ni ya kuchonganisha watu wa mikoa husika?
 
Nguruvi3.

Usipanic mkuu huu mnakasha tu weka sasa na wewe hotuba ya Zitto uliomsikia akiwafitinisha watanzania huko Shinyanga umma wa watanzania waisome.

Hawezi kukuonyesha hotuba kwa sababu hayo anayoyasema hayapo.

Hoja anayoifanya kuwa ni ya Zitto ni mawazo yake kichwani mwake yaliyotokana na ubaguzi wake na hofu kuwa Zitto atasababisha kushuka umaarufu wa chama chake anachoamini kuwa kitachoweza kuyabeba vizuri zaidi maslahi ya mkoa wake na taifa lake la kufikirika la Kaskazini, Mtu akiwa kwenye hofu ya namna hii hawezi kuelewa lolote.

Msubirini kwanza apone, siku akipona ugonjwa huu wa Zittophobia na akajisoma atajishangaa.
 
Last edited by a moderator:

Wakati ukisubiri hebu tufafanulie ni hapo kwenye nyekundu. Kwamba mkoa unaochangia sana unapata stahiki kubwa na mkoa unaochangia kidogo unapata stahiki ndogo??? au una maana gani?
 
Umeona swali langu hapo juu??
 
Kwa maana hiyo unakubaliana na mimi kuwa maneno ya Zitto ni ya kuchonganisha watu wa mikoa husika?

Hilo bandiko uliloliquote lilikuwa likimuaddress Nguruv, Data ulizoziweka umezitoa Facebook ambayo Nguruv ameikataa toka mapema, Nasubiri anipe Hotuba ya ZZK neno kwa neno ambayo anafanyia reference.
Kama wewe unayo hotuba ya ZZK live bila chenga tuwekee hapa.
 
Umeona swali langu hapo juu??

Kuna lolote jipya lolote miezi miwili sasa?kati ya vitu sipendi ni kuzunguka mbuyu daima dumu, kuzungumza kitu kilekile kwa mtu yuleyule kwa namna ileile alafu eti nitegemee uelewa tofauti.

Kuwa na akili ni pamoja na kujua kumsoma mtu.Na hapa sio tofauti.

Lakin natambua pia kuwa muda huponya, ndio maana nimeomba mpewe nafasi hiyo.
 
Wakati ukisubiri hebu tufafanulie ni hapo kwenye nyekundu. Kwamba mkoa unaochangia sana unapata stahiki kubwa na mkoa unaochangia kidogo unapata stahiki ndogo??? au una maana gani?

Juu kuna swali langu kuhusiana na stahiki.. naomba ufafanuzi ulichokusudia!!
 
Kuna lolote jipya lolote miezi miwili sasa?kati ya vitu sipendi ni kuzunguka mbuyu daima dumu.

Lakin natambua pia kuwa muda huponya, ndio maana nimeomba mpewe nafasi hiyo.

Kutakuwaje na jipya wakati tunasubiri majibu kutoka upande wa pili ili tusonge mbele? Miezi miwili umeshindwa kufafanua uchangiaji wa pato la taifa na huusika wa maendeleo sehemu husika? Sasa kama wewe great thinker hiki kitu kinakupa kigugumizi je inakuwaje kwa yule mama ambaye hata darasa la saba kamaliza kwa mbinde??

Husiwe na shaka muda tutakupa sie ni wavumilivu sana... Maana subira yavuta heri..
 
Kwa maana hiyo unakubaliana na mimi kuwa maneno ya Zitto ni ya kuchonganisha watu wa mikoa husika?

Hayo ya kusema kuwa eti maneno ya ZZK yanachonganisha watu wa mikoa husika ni ya kwako, siyo ya kwangu usinilishe maneno.

Je unakubaliana na Nguruv kuhusu kuchukua mabandiko kutoka Facebook?
 
Nikujibu kifupi sana, uchangiaji wa pato la Taifa ni ishara ya potential kiuchumi ya sehemu husika.

Uchangiaji mkubwa ni uthibitisho kuwa kuna shughuli za kiuchumi ambazo zikiboreshwa/zikitumiwa/zikipangwa vizuri zitaweza kuukuza zaidi uchumi wa Taifa na wa eneo husika.

Sasa hili ndio swali la kukesha miezi miwili humu great thinker!

Muda ninaokupa ni wa kupona huu ugonjwa,Zittophobia.
 
Ukianza kujibu hoja la mishapo tutaelewana tu..

NI jukumu la nani kuboresha shughuli za kiuchumi sehemu husika? Na ni jukumu la nani kuhakikisha kuwa wanakufaidii hiz shughuli za kiuchumi zinawanufaisha?

Na je unakubalina na kauli ya baadhi ya watu humu ndani kuwa kuna mikoa ambayo haipati stahiki zao? kama ni ndio kivipi hii mikoa inanyimwa stahiki zao na hizi stahiki za hii mikoa zinapelekwa mikoa ipi?

Kama haukubalini na hilo la stahiki huoni kulinganisha mikoa ya Shinyanga, Arusha na Kili kunajenga hizo "hisia" za dai la stahikii?
 
Hayo ya kusema kuwa eti maneno ya ZZK yanachonganisha watu wa mikoa husika ni ya kwako, siyo ya kwangu usinilishe maneno.

Je unakubaliana na Nguruv kuhusu kuchukua mabandiko kutoka Facebook?

Madhumuni ya mjadala ni kuelmishana, kuna kitu ambacho wewe unafahamu na mimi sifahamu hivyo hivyo kwako. hivyo basi tupe elimu kuhusu Stahiki ulikusudia nini?
 
NI jukumu la nani kuboresha shughuli za kiuchumi sehemu husika? Na ni jukumu la nani kuhakikisha kuwa wanakufaidii hiz shughuli za kiuchumi zinawanufaisha?

Ebu nyanyua bar, tusishuke chini kiasi hiki, hoja yako ni nin hapa?
 
Ebu nyanyua bar, tusishuke chini kiasi hiki, hoja yako ni nin hapa?

Tusikashifiane, tuelimishane...Tushuke tu chini, kumbuka sisi ni watu wenye maono tofauti.. Wewe unaweza kuona mawali hayo chini ya kiwango chako, lakini kwangu mimi na msomaji mwingine ni maswali ya msingi sana....

Turudi kwenye maswali yangu hapo juu.. Kama huna nafasi nitasubiri tena miezi 2.

Rudia hiyo post hapo juu kuna maswali zaidi.
.karibu
 
Nakushukuru kwa kuanza kutumia maneno hayo.

Baadhi ya watu...una maana sio Zitto tena bali ni "baadhi ya watu"?, Zinaleta "hisia" maana yake sio "halisia".

Toka siku ya kwanza nachangia mjadala huu nilisema hili, mjadala wooote,miezi miwili sasa umesimama kwenye huu msingi mbovu, msingi wa "hisia tu". Tukikaa kwenye hisia hakuna mwisho maana kila dakika bongo zetu zina millions of thoughts,hatutafika.
 
Husipende kujenga hoja kwa kunyofoa nyofoa sentensi ili kukidhi matakwa yako. maana hii ni mara ya pili unanyofoa maneno na kuyajengea hoja..

La sivyo naomba urudie tena nilichoandika na uone kama kinaendana na majibu yako..

Nimesema hivi:Ukianza kujibu hoja la mishapo tutaelewana tu..

NI jukumu la nani kuboresha shughuli za kiuchumi sehemu husika? Na ni jukumu la nani kuhakikisha kuwa wanakufaidii hiz shughuli za kiuchumi zinawanufaisha?

Na je unakubalina na kauli ya baadhi ya watu humu ndani kuwa kuna mikoa ambayo haipati stahiki zao? kama ni ndio kivipi hii mikoa inanyimwa stahiki zao na hizi stahiki za hii mikoa zinapelekwa mikoa ipi?

Kama haukubalini na hilo la stahiki huoni kulinganisha mikoa ya Shinyanga, Arusha na Kili kunajenga hizo "hisia" za dai la stahikii?

Husipende kujenga hoja kwa kunyofua nyofua sentensi ili kukidhi matakwa yako. maana hii ni mara ya pili unanyofoa maneno na kuyajengea hoja..

La sivyo unaomba urudie tena nilichoandika na uone kama kinaendana na majibu yako..

Tatizo lako Alinda unataka wote tufikiri unavyotaka.Kwenye hili, mie nimesoma na nimeona wewe mwenyewe umesema ni baadhi ya watu na ni hisia tu, ndio maana nikasema tukibase kwenye hizo hisia mjadala hautafika mwisho.

Natambua uwepo wa hisia hizo na mie binafsi siziamini, lakini kwa kuwa mjadala uliopo hapa ni juu ya ACT basi tungebase kwenye waliyosema wao ACT, lakini tukienda kwenye hisia za wengine hatutawatendea haki.Hisia hizi zipo na zitaendelea kuwepo kwa sababu hatuaminiani kwa dini,hatuaminiani kwa makabila, na hatuaminiani kwa maeneo tunayotoka.Tuna jamii inayohisiana tu wakati wote ndio maana ata kutaja tu jina la mkoa watu wanahisi mengine.

Muhimu tu tulichukulie hili positively kama kiashiria cha kazi ya kufanya zaidi kujenga umoja wetu, wenye jamii moja,ya watu wamoja,ndio msingi pekee wa kuepukana na hisia hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…