Kapwela;13135996]Maendeleo na uchumi ni jukumu mtambuka, serikali ina sehemu yake kwenye uchumi na maendeleo, na kuufanya uchumi huo uguze maisha ya watu, kuunganisha shughuli za kiuchumi na shughuli za watu wa maeneo husika, kuna jukumu la uwezeshaji katika nyanja tofauti n.k.
Mkuu. nadhani ungepaswa kutupongeza kwanza kabla ya kulaumu. UKisoma mwanzo kabisa wa hoja hii, utaona tulivyoongelea dhana ya maendeleo kwa ujumla wake tukionyesha vichocheo vinavyoleta tofauti baina ya eneo moja na jingine.
KUmbe tulikuwa sahihi na wale waliotusoma au kupitia mabandiko ya nyuma watakubaliana, tunaposemawarudi kusoma we mean it.
Kuhusu kuubadili mfumo, unachosema hakina tofauti na alichosema Zitto, alisema tuufumue huu mfumo maana haiwezekani sehemu yenye potential kama ile ya Shinyanga ikae kwenye lindi la umaskini.
Hapana, alisema haiwezekani mkoa namba Z katika uchangiaji uwe namba Z katika maendeleo(Shinyanga).
Hilo la potential ni jpya kwa wasomaji. Maneno mazito ndiyo yaliyozua swali, kuna uhusiano gani kati ya uchangiaji na maendeleo?
Na kwa mtazamo wa takwimu, mfano mzuri ulikuwa upi? Kuna mantiki gani ya random sampling ya mikoa abcd ambayo kiuhalisia haiangukii katika eneo lolote liwe uchangiaji au maendeleo katika kuleta maana ya talwi,u? Hapo ndipo hisia zilianza.
Ukichanganya na ukweli ni marudio ya mfano ule ule kwa njia nyingine, nadhani uliona hisia jukwaa la siasa.
Haihitaji kuwa mchumi kujua kuwa kama mkoa A una mchango mkubwa wa pato la taifa maana yake una uchumi wa jumla mkubwa, na kama mkoa B wenye mchango mdogo maana yake una uchumi wa jumla mdogo kuliko mkoa A. Sasa kama mkoa wenye uchumi mdogo una maendeleo ya watu makubwa kuliko mkoa wenye uchumi mkubwa maana yake kuna kuna potential ya mkoa A pia kuwa na maendeleo makubwa.Simple!
Yes, hoja inaweza kujengwa hivyo.
Kwa bahati mbaya haikujengwa hivyo. Unapokuwa na mikoa 21+ lazima sampling yako isiache maswali.
Kuna extremes unazoongelea, maendeleo na uchangiaji . Huwezi kuchukua mikoa ya kati ukaifanya sample, hapo utakuwa na biasness na prejudice.
Hata katika hilo lazima ueleze kwanini na kwa namba. Unaposema mikoa abc ina maendeleo ya juu, bila kuonyesha nafasi yao ukilinganisha na, wakati huo huo ukionyesha nafasi za uchangiaji wake ni deliberate move ya kutaka kupeleka ujumbe kwa njia za hisia.
Hilo kiongozi mkuu amefanikiwa na ndicho chanzo cha hisia kali kule jukwa la siasa na kwingineko.
Lakini pia utambue, watetezi wake wamesimama na kusema alichosema ni kweli, hakuna kosa na kuonyesha ukweli kwa njia zao.
Mkandara anasema, kuna mikoa imewezeshwa kufikia maendeleo. Huyu ni mtetezi namba moja anyejenga hisia hizo.
Anasema ipo mikoa ina umeme vijijini wakati mkoa x hauna maji.
Na yote hayo ni kutokana na mgawanyo wa rasilimali usiozingatia usawa.
Hawa ndio watetezi wake, kwanini ulaumu wanaojaribu kuonyesha si kweli?
Maana yake huo uchumi wa A hauna uhusiano na mwananchi wa kawaida, ndio maana akaongeza kuwa miongoni mwa sababu ni kuwa Shinyanga wanategemea dhahabu ambayo haihusiani na mwananchi wa Shinyanga.Ndio maana kama nawe unavyokiri lazima tuboreshe mfumo wetu wa kiuchumi ili huu uchumi umguse pia mwananchi wa kawaida. Hili ni jambo la kimfumo kuliko tulikolipeleka kwa hisia zetu hizi.Hatukuwaza hivi kwa sababu tu ya hisia zetu binafsi kama nilivyosema mwanzo.
Kumbuka aliweka takwimu kujenga hoja.
Shinyanga inachangia abcd kimaendeleo ni abcd, Kilimanjaro na Arusha ni namba ab kimaendeleo zipo juu.
Hivi unadhani wananchi ni wapuuzi wa kuelewa lugha?
Hakuna mwanasiasa yoyote aliyesema wananchi wa mkoa fulani wana shida kwa sababu ya mkoa mwingine na hakuna yoyote aliyesema kuna mikoa inapendelewa.
Takwimu zilikuwa na ulazima gani kulinganisha mikoa katika uchanguaji na maendeleo?
Ulitegemea nini kutokana na namba tena zikiwekwa nusu nusu na sehemu nyingine mikoa kuhukumiwa bila sababu.
Unaposema xz zipo juu kimaendeleo bila kuzipa nafasi, unaacha wazi hukumu kutoka kwa wasikilizaji.
Na hukumu hiyo tumeiona jukwaa la siasa jinsi vijana wanvyoparurana. Ni kwasababu kiongozi mkuu alilenga kufikisha ujumbe wake wa kisiasa wa kuungwa mkono kwa kutumia njia za kikanda. Kwa bahati mbaya hakuangalia madhara makubwa ya kauli zake
Ukisoma nyuzi hii bandiko la awali, tulimtahadharisha kwa nia njema kuwa kauli zake za sasa zitaangaliwa sana kwasababu amepoteza public trust na hana credibility mbele ya jamii.
Kauli zake ziwe za bahati mbaya au makusudi haziwezi kupuuzwa. Keshaondoa benefit of doubt na sasa anaishi katika mazingira halisi. Mzigo huo asilaumiwe mtu, aubebe mwenyewe
Pia epuka hizi lugha,hakuna mkoa wowote ambayo wananchi wake ni wavivu na ambao wananchi wake wana fikra tegemezi, wala hakuna mkoa wowote ambao wananchi wake ni wajuzi na mahiri kudai haki kuliko mkoa mwingine. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo thread hii imefanikiwa sana na kuishia kukera watu na kujenga chuki ambazo zinaongeza hisia za kuvunja utaifa wetu, kumbuka hakuna mtu atafurahi kusoma hapa kuwa kwao ni wavivu na wenye fikra tegemezi kwa sababu tu hawatoki Arusha au Kilimanjaro.Tuangalie hizi lugha. Kote Tanzania wananchi wanajitafutia maendelo yao binafsi, lakini kuna changamoto mbalimbali na changamoto hizi wakati mwingine ni tofauti kutoka sehemu moja na nyingine, ndio maana solutions zake sio lazima ziwe universal.
Lugha inayotumika ni kuonyesha kuwa jitihada zinaofanywa zikubalike na ziigwe. Je, kuna makosa wanakijiji wa Nronga kujiletea maendeleo?
Je kuna makosa wananchi kujiwezesha kulipia huduma za umeme vijijini?
Je, si kweli kuwa wapo wananchi wanahama makwao na ndio wanaolalamika mwakwao kuwa nyuma?
Je, si kweli kuwa kuna jamii zinazjitegemea zaidi kuliko kusubiri kufyeka barabara?
Kuna jamii zimechimba majabali milimani kupitisha barabara, kuna jamii haziwezi kufyeka nyasi kupata barabara.
Hii ni taboo kweli kusema ukweli. Kuna jamii shule zinafungwa kwa kukosa wanafunzi. Kuna jamii shule zimejaa watoto na madarasa ni machache! kuna kosa la kuonyesha ukweli huo!
Nini kinakera, kusema watu wapeleke watoto shule?Kipi bora kuwapongeza watoto wanaoachishwa shule?
Kama hatuwezi kusimama na kujifunza kwa njia za mifano bora yenye ukweli uwazi na kujenga, tutabaki na taboo hiyo, miaka mingine 10 waliotangulia hatuwaoni, tunarudi kulalama.
Mfano, kijana aliyeishia darasa la 7 arusha au kilimanjaro bado utalii unaweza kumgusa lakini kijana wa darasa la 7 aliye pembezoni mwa katavi nation park hawezi kuguswa kabisa na utalii, mazingira lakini pia priority za serikali kwenye kujenga miundo mbinu ya kuvutia watalii n.k.Hii inaweza kuleta tofauti ya maisha ya vijana hao wawili.
Tumeyasema haya miezi mingi katika nyuzi hii.
Tukaeleza kuwa umuhimu si kuona wivu kwanini fulani anaendelea kwa utalii.
Muhimu ni kuangalia pale penye tatizo panaweza kufanikiwa vipi?
Kwa mfano, huyo wa Kilimanjaro utalii utamsaidia na miundo mbinu ni muhimu kwa hilo.
Yule wa Katavi hahitaji utalii, anahitaji miundo mbinu ya kupeleka mahindi Kilimanjaro ili achukue pesa za utalii kwa njia hiyo.
Hapa wenzentu wanasema ' mikoa fulani imependelewa au kuwezeshwa''
Nadhani ungemwalika Mkandara afadidike na elimu yako badala ya kukinga kifua kwenye tope! kusafisha sahani chafu na maji ya uani
Huu ni mfano tu, kuna maeneo mengi ambayo yanaweza kuboreshwa kuchochea maendeleo pande zote za Tanzania.Kila eneo la Tanzania lina kitu ambacho kinaweza kikashushwa kuwagusa watu
Ndiyo maana tupo hapa kulaani na kukemea hizi siasa majitaka za kutupa vijinamba kwa wananchi kujenga hisia na chuki.
Kama kiongozi angekuwa mtu makini, angejitokeza na kuweka sawa kauli zake.
Kwa vile nia na kusudio lilikuwa kuamsha hisia na kujenga chuki, hilo halina kipaumbele kwake.
Tumelichukua ili kuileta jamii pamoja, kwa kusema kuwa matatizo ya wananchi yapo ndani ya miaka 50.
Hayajaletwa na mkoa fulani kuchangia kidogo na maendeleo zaidi au kinyume.
Tupo hapa kumaliza hisia zilizozuka jukwa la siasa zenye lengo la kugawa taifa. Nia hii ovu ipigwe vita kabisa
Tanzania ni yetu sote, si ya mtu wala watu. Tanzania yetu haina ibaguzi.
Tusipokaa mkao mzuri na kuwakemea , kuwakataa na kuwaonya hawa wanasiasa uchwara tutaishia pabaya
Mwanasiasa anayezusha hisia katika jamii na kukaa kimya, kamwe nia yake haikuwa nzuri.
Ni wakti watu wamshauri atoke na kukanusha, kufafanua, au kuweka sawa kauli.
Vinginevyo ataishi na hizi kauli kama mzigo mgongoni.
Yes wananachi wanaona na wana hisi nia ovu sana ya kuligawa taifa