Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Ndio nilikuwa nataka kwenda huko huko na maswali yangu kwa Ritz ambayo anatujibu kwa copy and paste bila analysis. Kwa kuongezea katika orodha ya maswali yako, ningependa kumuuliza Ritz:

*Kama suala ni kodi ya shinyanga kutozwa DSM, Je, Arusha na Kilimanjaro wanahusika vipi na suala la kodi za Shinyanga kutozwa Dar-es-salaam badala ya Shinyanga?

*Kwanini sasa mnakubali kwamba tatizo ni kodi na sio GDP, lakini bado mnasema Zitto yupo sahihi na hoja yake ya GDP?

Hakuna aliyesema tatizo ni Kodi na siyo GDP, Usiwalishe wana Ukumbi Maneno.

Again, Tatizo siyo Kilimanjaro kama mkoa na watu wake, Tatizo ni serikali isiyo Fair, ambayo ina mipango mibovu katika ugawaji wa pato la taifa, Serikali ambayo hapo juu Ritz amekuonyesha hata Mbunge wa Shinyanga akilalamika kuwa Serikali imeuacha nyuma mno huo mkoa ktk suala la afya na Elimu.

Hakuna mwenye ugomvi na Kilimanjaro, kama serikali imepeleka maendeleo Kilimanjaro kuliko mikoa mingine, then wa kuwa questioned ajibu kwa nini ni serikali. Toka awali nafuatilia huu mjadala, hiki ndicho haswa ZZK alichokifanya.
 
Last edited by a moderator:
Nani kasema Arusha na Kilimanjaro wanahusika? Watu wanapinga huo mfumo.

Kwa maana hii, basi mnakubali kwamba kiongozi wenu Zitto alikosea kuhusisha mikoa ya kaskazini na hali ya maendeleo ya mkoa kama Shinyanga. Nashukuru kwamba hilo tumelimaliza, lakini muhimu zaidi kwamba - tatizo la msingi lipo kwenye Kodi na sio GDP.

copy and paste zangu ndiyo zinawakera? Lakini za kwako murua jamaa zako wanaziita madini au nikuonyeshe?
Mimi huwa sileti copy and paste na kuziongezea tu maneno ya "msome kiduchu", bali hutumia data husika kufanya analysis na kujenga hoja.
 
Hakuna aliyesema tatizo ni Kodi na siyo GDP, Usiwalishe wana Ukumbi Maneno.

Again, Tatizo siyo Kilimanjaro kama mkoa na watu wake, Tatizo ni serikali isiyo Fair, ambayo ina mipango mibovu katika ugawaji wa pato la taifa, Serikali ambayo hapo juu Ritz amekuonyesha hata Mbunge wa Shinyanga akilalamika kuwa Serikali imeuacha nyuma mno huo mkoa ktk suala la afya na Elimu.

Hakuna mwenye ugomvi na Kilimanjaro, kama serikali imepeleka maendeleo Kilimanjaro kuliko mikoa mingine, then wa kuwa questioned ajibu kwa nini ni serikali. Toka awali nafuatilia huu mjadala, hiki ndicho haswa ZZK alichokifanya.
Mkuu Gamba la Nyoka.

Tatizo ni mfumo na hicho ndicho Zitto alichofanya kuwafahamisha Watanzania jamaa zetu hawa wanataka kumuwekea maneno mdomoni.

Hata Chadema wenyewewe wanalalamikia huu mfumo msome Tundu Lissu anacholalamikia.

Baadhi ya wabunge wamemshambulia Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, kwamba amekuwa akipendelea Jimbo lake la Mwanga lililopo mkoani Kilimanjaro kwa kulitengea kiasi kikubwa cha fedha za miradi ya maji huku majimbo yenye ukame mkubwa yakipewa fedha kidogo.Wabunge hao walitoa shutuma hizo wakati wakichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji Singida kwa mwaka wa fedha wa 2014/15. Hotuba ya wizara hiyo iliwasilishwa bungeni mjini Dodoma na Waziri Profesa Maghembe Jumamosi iliyopita.Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema Mkoa wa Singida ni mmoja kati ya mikoa yenye ukame mkubwa na isiyo na vyanzo vya uhakika vya maji.Lissu alisema katika Jimbo lake- lililopo Wilaya ya Ikugi mkoani Singida lenye kata 12, lina miradi miwili tu ya maji, jambo ambalo alieleza kuwa si sahihi.Alisema kumekuwapo na utaratibu wa ugawaji wa fedha za miradi ya maji katika majimbo, wilaya ama mikoa isiyo ya haki kutokana na upendeleo mkubwa sana.Kwa mujibu wa Mbunge huyo, mikoa yenye mahitaji makubwa ya maji, imekuwa ikitengewa fedha kidogo kwa kulinganisha na mikoa yenye unafuu wa upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.Aliitaja baadhi ya mikoa yenye ukame na ambayo kimsingi ilipaswa kutengewa fedha nyingi za miradi ya maji kuwa ni pamoja na Singida, Dodoma, Shinyanga na Simiyu. Hata hivyo, alisema licha ya mikoa hiyo kuongoza kwa ukame, lakini kila mwaka imekuwa ikitengewa bajeti ndogo ya miradi ya maji.Kwa mfano, alisema mkoa wa Singida umetengewa Sh. bilioni 3.304 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15, Simiyu Sh. bilioni 2.864, Shinyanga Sh. bilioni 3.296 na Dodoma Sh. bilioni 7.236.Aidha, Lissu aliitaja baadhi ya mikoa yenye unafuu wa upatikanaji wa maji kuwa ni Tanga ambayo kwa mwaka huu wa fedha imetengewa Sh. bilioni 10.791, Mbeya Sh. bilioni 9.293, Mtwara Sh. bilioni 7.571 na Kilimanjaro Sh. bilioni 6.322.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maana hii, basi mnakubali kwamba kiongozi wenu Zitto alikosea kuhusisha mikoa ya kaskazini na hali ya maendeleo ya mkoa kama Shinyanga. Nashukuru kwamba hilo tumelimaliza, lakini muhimu zaidi kwamba - tatizo la msingi lipo kwenye Kodi na sio GDP.

Mimi huwa sileti copy and paste na kuziongezea tu maneno ya "msome kiduchu", bali hutumia data husika kufanya analysis na kujenga hoja.

Kwa faida wanaukumbi weka hiyo kauli ya
Zitto kuhusisha Kaskazini na maendeleo ya Shinyanga hizi ndiyo hoja zako za uhongo.

Zitto yupo shahihi alichokisema hayo maneno ni yako na Nguruvi3.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna aliyesema tatizo ni Kodi na siyo GDP, Usiwalishe wana Ukumbi Maneno.

Again, Tatizo siyo Kilimanjaro kama mkoa na watu wake, Tatizo ni serikali isiyo Fair, ambayo ina mipango mibovu katika ugawaji wa pato la taifa, Serikali ambayo hapo juu Ritz amekuonyesha hata Mbunge wa Shinyanga akilalamika kuwa Serikali imeuacha nyuma mno huo mkoa ktk suala la afya na Elimu.

Hakuna mwenye ugomvi na Kilimanjaro, kama serikali imepeleka maendeleo Kilimanjaro kuliko mikoa mingine, then wa kuwa questioned ajibu kwa nini ni serikali. Toka awali nafuatilia huu mjadala, hiki ndicho haswa ZZK alichokifanya.

Huo ni mtazamo wako, na ni mtazamo sahihi, lakini haukuwa mtazamo wa zitto ambao ndio ulipelekea mjadala wote huu kuibuka. Pia haukuwa mtazamo wa akina Mkandara, ritz na wengine. Lakini zitto bado hajakiri kukosea. Ni wewe na wenzako ndio mnamtetea kama vile alimaanisha unachokisema. Vinginevyo maneno yake yatabakia kuwa ya upotoshaji, ubaguzi na uchonganishi.

Unachomfanyia zitto ni interpretation, not inference.
 
Wanaukumbi.

Tundu Lissu anahoji kwa nini Shinyanga wanatengewa bajeti ya maji bilioni 4.296 wakati Kilimanjaro wanatengewa bajeti ya maji bilioni 6.322.

Lakini hii kauli ingetolewa na Zitto angeshambuliwa sana kuwa ana chuki na Kaskazini.
 
Last edited by a moderator:
Wanaukumbi.

Tundu Lissu anahoji kwa nini Shinyanga wanatengewa bajeti ya maji bilioni 4.296 wakati Kilimanjaro wanatengewa bajeti ya maji bilioni 6.322.

Lakini hii kauli ingetolewa na Zitto angeshambuliwa sana kuwa ana chuki na Kaskazini.

Ukimsoma Zitto, Yeye anasema kuwa tatizo ni mfumo, Sasa nashangaa hawa Wenzetu wanachukulia issue as If ni Zitto against Kilimanjaro, Kumbe yeye yuko against Mfumo, Mfumo mbovu:

Msome Zitto anavyosema:

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

Ritz,
usiweweseke kwa mambo ambayo hayana msingi wowote. Kiongozi au mwanasiasa yoyote ambae anatoa kauli za utatanishi tutamhoji kama tunavyomhoji zitto. Akizungumza kitu ambacho kinapotosha na hakitujengi kama watanzania, tutamkosoa bila ya kujalisha jina lake ni nani, cheo chake ni nani au anatoka chama gani.

Kuhusu hoja ya Lissu. Ni vizuri ungeiwasilisha hoja nzima kuliko vipande vipande. Hata hivyo:

Kwanza elewa kwamba kinachozungumzwa na lissu hapo ni bajeti - mapato ya serikali (KODI) na sio pato la taifa (GDP).

Pili, wanaotenga bajeti ni akina nani? obviously ni mfumo, na sio wananchi wa Kilimanjaro. Kwa maana hii, Lissu anajadii mfumo wa bajeti na mapungufu yake, hajadili kwamba Kakazini wanawanyonya watu wa shinyanga kama alivyofanya Zitto.

Muhimu pia ni swali langu la awali kwako Ritz ni kwamba je - mchango wa Shinyanga kwenye kodi ya nchi ulitakiwa uwe ni kiasi gani? na je, hiyo 0.46% ya shinyanga kama mchango wake kwa kodi ya serikali, vyanzo au aina ya hizo kodi ni zipi?
 
Mchambuzi.

Mimi sipo hapa kukufurahisha wewe mimi na deal na wanaukumbi wanaofuatilia huu mnakasha mimi ndiyo nawalenga hao nyie ni kama daraja tu.

Majibu ya maswali yako nimekujibu nyema tu na nikawekea na bayana ya mbunge na waziri nikaweka na kiasi ambacho mgodi wa Buzwagi unatoa, ulikuwa unapinga kodi za mogodi hawalipi dar nimekuwekea ushahidi bado hutaki eboo!!

Sasa wewe unataka nikupe jibu utakalolipenda wewe

Teh teh teh.
 
Last edited by a moderator:
Ukimsoma Zitto, Yeye anasema kuwa tatizo ni mfumo, Sasa nashangaa hawa Wenzetu wanachukulia issue as If ni Zitto against Kilimanjaro, Kumbe yeye yuko against Mfumo, Mfumo mbovu:

Msome Zitto anavyosema:

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

Gamba la Nyoka kwanza nakukumbushia swali langu la "Stahiki"

Pili kama umemsoma Mchambuzi anasema kuwa Zitto anafanya makosa anapolinganisha uchangiaji wa pato la Taifa na maendeleo ya mkoa husika.. Sijui kama ulikuwa unafatiali mjadala kwa umakini au la..
 
Last edited by a moderator:
Alinda,

Mfano wako ni mzuri sana kutusaidia kuliweka suala hili sawa pengine for good. Wanakijiji wakilima na kuvuna mihogo yenye thamani ya soko ya shillingi milioni 20, huo utakuwa ni mchango wao kwa pato la mkoa na hata taifa (GDP). Na hiyo itatoa fursa kwa PATO LA SERIKALI (KODI) kupatikana kupitia tozo katika muktadha wa huo uzalishaji wa mihogo.
Tukirudi kwa wakulima hawa wa Mihogo - If it’s a business case, watatoa gharama zote na kubakisha faida. Wakulima hawa watakuwa na uhuru wa kutumia Faida itakayobakia kwa jinsi watakavyoamua, hata wakiamua kuachana na kilimo chao na kula mtaji wote. Lakini lipo jambo muhimu hapa, nalo ni kwamba – moja ya gharama katika uzalishaji wa bidhaa na huduma, tena gharama ambayo ipo kwa mujibu wa sheria, ni KULIPA KODI, unless kuna tax exemption ambayo pia nayo lazima iwe kwa mujibu wa sheria. Kwahiyo kama sehemu ya gharama za uzalishaji wa bidhaa (mihogo kwa mfano), wakulima hawa watalazimika kulipa kodi kabla ya kupiga mahesabu ya Faida ya jasho lao. Swali linalofuata ni je:

· Kwanini Kulipa kodi ni kwa mujibu wa sheria?

Ni kwa sababu, katika taifa au uchumi wowote ule, zipo aina mbili ya Goods namely - Public goods and Private goods. Awali tulijadili maana ya public goods na kwanini zinaitwa hivyo, kwa mfano taa za barabarani (security lights), traffic lights, bus station, national defense system, light house (for ships) n.k. Bidhaa hizi (Public goods) zina two main features namely (1) Non Excludable and (2) Non-Rivalrous. Kwa maana nyingine, in order for a good to qualify as a "public good", it must be non-excludable and non-rivalrous. Ni such feature ndio hupelekea umuhimu wa serikali kugharamia provision of such goods. Kwanini? Mfano mzuri ambao hutumiwa in classical economics ni light house(Mnara wa meli). Tuujadili mfano huu:

Mnara wa meli ni "non-excludable" kwa sababu its impossible kuzuia meli zisitumie au zisifaidike na mnara husika hata kama hazikuchangia katika kugharamia ujenzi wa mnara huo. Lakini pamoja na hayo, kwa usalama wa meli, abiria na mizigo, meli zote lazima zitumie na zifaidike na mnara huo. Mnara wa meli vile vile ni “Non‐rivalrous” kwa sababu kama tayari meli nyingi zinafaidika na mnara uliopo, hakuna extra cost itakayotokea kwa kuruhusu meli nyingine kufaidika nan a mnara husika. Hii ni tofauti na Private goods kama mkate, boksi la juisi ambazo zote ni “rivalrous good” kwa sababu the more these are provided to someone or to some people itahitaji more and more goods to be produced vinginevyo kutakuwa na shortage. Kwa private goods, such chaarcteritics ndio zinatoa incentives za kuzizalisha na kusambaza kibiashara. Lakini for public goods, the fact kwamba ni ‘non excludable’ and ‘non-rivalrous’, uzalishaji au provision yake by private sector huwa haina tija. Lakini kwa vile such goods ni muhimu sana, serikali lazima iingie gharama kwa maslahi ya taifa. Gharama za serikali katika jambo hili ni KODI, na sio GDP.

Nimetoa mfano huu kwa makusudi. Tukichukulia wananchi wa Shinyanga, Arusha n.k, wote wana mahitaji kama haya mengi tu ambayo bila ya ushiriki wa serikali, provision of such goods haitakuwepo, na italeta a huge crisis. Tukitumia mfano wa wakulima wa Mihogo, iwapo wakulima wa Mihogo uliowatolea mfano wanazalisha zao hili lenye market value tuseme ya T.sh 2,000,000, sasa ili mazao yaweze kufika Sokoni, watalazimika kutumia barabara. Barabara ni moja ya Public Goods, whether ni barabara chini ya Tanroads au zile chini ya Manispaa husika. Katika hali ya kawaida, wakulima hawa watahitajika kulipa kodi ya aina Fulani ili serikali iweze kuendelea kugharamia matumizi ya barabara husika na wakulima hawa lakini pia na watumiaji wengine. Provision of such services ndio maana halisi ya KEKI YA TAIFA. Na uwepo wa Fedha kugharamia mahitaji haya ndio maana hali ya SUNGURA MKUBWA au SUNGURA MDOGO, kule kwenye mijadala Bungeni.

Mgao halali kwa Wananchi?!!?

Mgao kwa wananchi maana yake ni kugawana kwa keko ya taifa. Kugawana kwa keki ya taifa maana yake ni uwepo wa sungura mkubwa na sio mdogo. Sungura hapa maana yake ni MAPATO YA KODI, Not GDP. Kwahiyo katika hali ya kawaida, mgao wa serikali kwa wananchi husika ni lazima utokane na michango ya wananchi husika kwenye PATO LA SERIKALI (KODI), ili wananchi hao wapate huduma wanazostahili. Vinginevyo kama wakulima hawa wamevuna mihogo yenye thamani ya shillingi milioni 20 (na huu ndio mchango wao kwa PATO LA TAIFA/GDP), lakini wakatumia pato hilo kugawana kwa matumizi binafsi na kukwepa kodi, wakulima hao watakuwa na uhalali gani wa kudai kwamba hawapati keki ya taifa? Ndio maana kodi ipo kwa mujibu wa sheria, na upatikanaji wa huduma za kijamii (keki ya taifa) ni lazima iendane na mchango wa wananchi au mkoa husika katika mapato ya serikali.

Ndio maana shughuli za uzalishaji zinatozwa kodi. Shughuli zote za uzalishaji (GDP Output) ambazo hazilipi kodi na kufanya hivyo kinyume cha sheria, maana yake ni kwamba mapato yake yanaenda kwenye mifuko ya wazalishaji kwa matumizi ambayo hayahusu umma bali maisha binafsi. Jamii ya aina hiyo haina uhalali wa kulalamika kwamba wanakosa keki ya taifa. Ndio maana suala la kodi katika demokrasia zilizokomaa ni suala muhimu sana katika chaguzi kuu. Mara nyingi, ceteris paribus, wananchi huwa more concerned zaidi with how their taxes are being spent kuliko suala la GDP.

Asante sana Mchambuzi kwa darasa lako lilishiba..
 
GDP ni kama suruali yenye mifuko minne.. haijalishi utaweka kiasi gani mfuko gani ila kila mfuko utabeba kiasi gani, unategemea weka fedha zaidi mfuko wa nyuma zaidi ya mingine lakini in Total fedha ulotegemea kuwa nazo ndizo tunazozungumzia.

Sawa hapa katika pato la taifa..Kwamba hizo mil 20 nikaa nazo nyumbani au benki au nizitoe kama zawadi katika pato la Taifa bado zitabaki hizo hizo mil.20

Mkandara;13165014]Kwa hiyo usipolipa kodi serikalini, bado fedha ulokuwa nayo itahesabika kuwa mchango wako katk GDP pengine wewe umeongeza ukubwa shamba na upo Shinyanga ina maana unategemea kutakuwa na ongezeko la mapato yako mwaka kesho. Ulipaji kodi ni muhimu kwa sababu unaiwezesha serikali kukabiri makadirio uloyafanya katika matumizi yake na kikubwa zaidi ni kutokuwa tegemezi la misaada ya nje badala ya wananchi wenyewe kuwa msingi wa pato lake. Lakini katika mipango yake haiwezi kuzuiwa kwa sababu Shinyanga wamechangia kidogo kwani asilimia kubwa ya mipango ama bajeti ya nchi inatangulia mapato ya kodi itakayo kusanya. Serikali inapanga mwaka 2015 - 2016 itafanya mambo gani mbele ya pato watalokusanya.
.
Kama nimekuelewa vizuri serikali inajiendesha/itajiendesha kwa makusanyo na kodi na makusanyo mengineo si kuangalia pato la Taifa.. (nimekuelewa vizuri?)(tuondoe misaada na pesa za wafadhili)

Na ili eneo fulani iliwe na maendeleo ni lazima liwe na huduma za jamii, na ili kupata huduma za jamii ni lazima ulipe kodi.(kama ulivyosema hapo juu matumizi ya serikali)Hapa sioni husiano wa uchangiaji wa pato la Taifa na maendeleo ya sehemu husika.

Tukirudi kwenye swali lingine ili linaweza kujibiwa na wewe, MCHumbuzi au mtu yeyote mwenye ufahamu (hapo kwenye ufahamu nina weka msisitizo la sivyo mtanichanganya)

Na kama kigezo cha maendeleo ni uchangiaji pato la Taifa inakuwaje Lindi mkoa ambao ni kati ya mikoa inayochangia kiasi kidogo sana ishike no.9?
 
Gamba la Nyoka kwanza nakukumbushia swali langu la "Stahiki"

Pili kama umemsoma Mchambuzi anasema kuwa Zitto anafanya makosa anapolinganisha uchangiaji wa pato la Taifa na maendeleo ya mkoa husika.. Sijui kama ulikuwa unafatiali mjadala kwa umakini au la..

Sijakujibu muda wote kwa sababu sikutumia neno "Stahiki" katika ile hoja yangu ya awali, bali nilitumia neno "Stahili"
Rekebisha kwanza swali halafu uniulize tena, tusilishane maneno!.
 
Mchambuzi.

Mimi sipo hapa kukufurahisha wewe mimi na deal na wanaukumbi wanaofuatilia huu mnakasha mimi ndiyo nawalenga hao nyie ni kama daraja tu.

Majibu ya maswali yako nimekujibu nyema tu na nikawekea na bayana ya mbunge na waziri nikaweka na kiasi ambacho mgodi wa Buzwagi unatoa, ulikuwa unapinga kodi za mogodi hawalipi dar nimekuwekea ushahidi bado hutaki eboo!!

Sasa wewe unataka nikupe jibu utakalolipenda wewe

Teh teh teh.

Sijahoji Suala la kodi za Shinyanga Dsm. Hata Nguruvi3 kauliza kuhusu kodi za Tanzanite Arusha zinalipwa Wapi Kama sio dar. Haujajibu hoja.

Nilichokuuliza kwa nia ya kujenga mjadala na kwa vile wewe ndio ulioleta takwimu ni kwamba:

1. Shinyanga ilitakiwa ichangie kiasi gani Kwenye mapato ya serikali kitaifa?

2. Je, mchango wa Shinyanga wa 0.46%, vyanzo vya hizo kodi ni vipi kwa maana ni kodi za aina gani?

Mbona ni maswali marahisi sana and straightforward? Huyo waziri hajajibu maswali yangu kwa Sababu sikumuuliza waziri, unachofanya ni kulazimisha Hoja za Huyo waziri zijibu maswali yangu.
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo maana Mwl. Nyerere alikuwa anasisitiza ukusanyaji kodi na suala la miundombinu kwa ajiri ya maendeleo, na kulinda wafanyabihashara wenye viwanda hapa nchini kwa serikali kutoza kodi kwa haki. Mwl. Nyerere hakuimiza GDP...! Nadhani alikuwa amezielewa dhana hizi za Kodi na GDP. Waweza kumsikiliza katika clip mbili hapa chini. Clip ya kwanza isikilize yote na ya pili msikilize mwalimu kuanzia dk 2.40 mpaka ya 5.00.

Clip 1 (Kwa hisani ya Amilyimo>>>>https://www.youtube.com/watch?v=DXZEQGkXeyY )

Clip 2🙁Kwa hisani ya Michuzi>>>https://www.youtube.com/watch?v=idCCigo1L9w&feature=player_embedded )

============================== ============================== ====

Nawashukuru nyote mlionisaidia kulielewa suala la Kodi na GDP kwa undani zaidi. Nimejua kuwa, kwa kutambua sehemu husika ilinapa kodi na tozo kiasi gani na inachangia kiasi gani kwenye GDP ndiyo unaweza kupima mchango wa sehemu hiyo katika maendeleo ya sehemu yenyewe na nchi kwa ujumla.

Baadaye nimeenda mbali kwenda kutafuta ubora wa kipimo hiki cha GDP. Kwanza nimeelezwa, GDP hutumiwa na wachumi kwa shughuli hii (kama nilivyoinukuu): Economists use GDP to measure the relative wealth and prosperity of different nations, as well as to measure the overall growth or decline of a nation's economy.

Pia nikakumbana na vitu vinavyopunguza ubora wa kipimo hiki cha GDP (nanukuu): But there are a number of shortcomings to using GDP. Here are just a few:

1. GDP doesn't count unpaid volunteer work: .......
2. Disasters can raise GDP: Wars require soldiers, oil spills require cleanup, and natural disasters require health workers, builders, and all manner of helping hands. Rebuilding after a disaster or war can greatly increase economic activity and boost GDP.
3.GDP doesn't account for quality of goods: Consumers may buy cheap, low-quality, short-lived products repeatedly instead of buying more expensive, longer-lasting goods (Hili nadhani limeelezwa).

Sasa kwenye namba mbili hapo ndiyo pamenistua kweli, kumbe yawezekana tunaambiwa (mfano) Shinyanga ama Kilimanjaro zinachangia sana kwenye pato la Taifa (GDP). Kumbe mikoa inaongeza matumizi tu ya kwenye pato hilo labda kutokana na majanga yaliyoikumba mikoa hiyo...!! Na bado mtu anakwambia Mkoa fulani unachangia sana kwenye GDP lakini hauna maendeleo...! lakini mwingine unachangia kidogo lakini unamendeleo! Kauli hii isipofafanuliwa zaidi kujua mikoa hiyo inachangiaje GDP (majanga ama uzalishaji?), inapotosha sana umma ambao hawajui maana ya pato la taifa (GDP). Na hapa ndipo S.L anapotiwa hatiani kuwa alitoa kauli za kichonganishi. Mimi siyo mchumi ila kama nimetafsiri maelezo yale ya wanauchumi kwa usahihi, basi na sisitiza S.L (Zitto) anahatia.

Chanzo cha nukuu zangu ni>>>>What are the advantages and disadvantages of Gross Domestic Product?
 
Last edited by a moderator:
Gamba la Nyoka kwanza nakukumbushia swali langu la "Stahiki"

Pili kama umemsoma Mchambuzi anasema kuwa Zitto anafanya makosa anapolinganisha uchangiaji wa pato la Taifa na maendeleo ya mkoa husika.. Sijui kama ulikuwa unafatiali mjadala kwa umakini au la..

Asante Alinda. Hoja ya zitto ni kwamba kuna mikoa maskini na ambayo haistahili kuwa maskini kwa Sababu michango ya mikoa hii (GDP) Kwenye pato la taifa (National GDP) ni mikubwa sana. Akaenda mbali na kufananisha mikoa Kama Arusha na Kilimanjaro kwamba michango Yao Kwenye GDP ni midogo kuliko shinyanga lakini imeendelea zaidi.

Kwa hiyo mikoa hii ni wanyonyaji wa mikoa mingine kwa logic ya ovyo Kabisa kwamba eti - michango Yao kwa GDP ya taifa ni midogo lakini viwango vyao kimaendeleo ni vikubwa zaidi. Tuka challenge Hilo ka kuingiza Suala la Kodi katika equation. Akina Ritz, Mkandara, adhurusi na wafuasi wengine wa zitto wakapinga hoja ya kodi na kusema GDP is supreme na ndio iwe kigezo Cha kuinua Hali za wananchi husika. Tukasema kwamba kwa Hali ya Sasa, GDP pekee is misleading, na mapato ya kodi ni more practical katika kuelewa Nini kinaendelea. Leo wote wanaimba wimbo wa kodi kodi kodi na wanaenda mbali zaidi na kumsafisha zitto kwamba aliposema "pato la taifa", alimaanisha mfumo wa kodi. Ni Kama vile kusifia mfalme amevaa Nguo nzuri kumbe yupo utupu.
 
Last edited by a moderator:
Sijahoji Suala la kodi za Shinyanga Dsm. Hata Nguruvi3 kauliza kuhusu kodi za Tanzanite Arusha zinalipwa Wapi Kama sio dar. Haujajibu hoja.

Nilichokuuliza kwa nia ya kujenga mjadala na kwa vile wewe ndio ulioleta takwimu ni kwamba:

1. Shinyanga ilitakiwa ichangie kiasi gani Kwenye mapato ya serikali kitaifa?

2. Je, mchango wa Shinyanga wa 0.46%, vyanzo vya hizo kodi ni vipi kwa maana ni kodi za aina gani?

Mbona ni maswali marahisi sana and straightforward? Huyo waziri hajajibu maswali yangu kwa Sababu sikumuuliza waziri, unachofanya ni kulazimisha Hoja za Huyo waziri zijibu maswali yangu.
Maswali nimeishakujibu maswali mengine ukiona sijajibu basi hujue nimeyapuuza kama wewe ulivyoshindwa kujibu tuhuma za Zitto kuwa anajenga chuki na Kaskazini, hapa hamna mjadala tena saizi kuna viroja tu lakini tunashukuru Zitto yupo sahihi baada ya watanzania wenye uchungu na nchi yao kulisimamia ili hapa ukumbuni nakuuliza swali rahisi unayo hotuba ya Zitto akiwashambuliwa watu wa Kaskazini?
 
Last edited by a moderator:
Asante Alinda. Hoja ya zitto ni kwamba kuna mikoa maskini na ambayo haistahili kuwa maskini kwa Sababu michango ya mikoa hii (GDP) Kwenye pato la taifa (National GDP) ni mikubwa sana. Akaenda mbali na kufananisha mikoa Kama Arusha na Kilimanjaro kwamba michango Yao Kwenye GDP ni midogo kuliko shinyanga lakini imeendelea zaidi.

Kwa hiyo mikoa hii ni wanyonyaji wa mikoa mingine kwa logic ya ovyo Kabisa kwamba eti - michango Yao kwa GDP ya taifa ni midogo lakini viwango vyo kimaendeleo ni vikubwa zaidia. Tuka challenge Hilo ka kuingiza Suala la Kodi katika equation. Akina Ritz, Mkandara, adhurusi na wafuasi wengine wa zitto wakapinga hoja ya kodi na kusema GDP is supreme na ndio iwe kigezo Cha kuinua Hali za wananchi husika. Tukasema kwamba kwa Hali ya Sasa, GDP pekee is misleading, na mapato ya kodi ni more practical katika kuelewa Nini kinaendelea. Leo wote wanaimba wimbo wa kodi kodi kodi na wanaenda mbali zaidi na kumsafisha zitto kwamba aliposema "pato la taifa", alimaanisha mfumo wa kodi. Ni Kama vile kusifia mfalme amevaa Nguo nzuri kumbe yupo utupu.

Hayo maneno niliyoyapigia msitari ni Zitto aliyeyatamka au UNADHANI Zitto anamaanisha hivyo?
Kama unadhani basi you are wrong dhana yako ni potofu.

Soma tena bandiko tunalolijadili la ZZK utaona yeye anaulamu mfumo na si mkoa kama mkoa
 
Asante Alinda. Hoja ya zitto ni kwamba kuna mikoa maskini na ambayo haistahili kuwa maskini kwa Sababu michango ya mikoa hii (GDP) Kwenye pato la taifa (National GDP) ni mikubwa sana. Akaenda mbali na kufananisha mikoa Kama Arusha na Kilimanjaro kwamba michango Yao Kwenye GDP ni midogo kuliko shinyanga lakini imeendelea zaidi.

Kwa hiyo mikoa hii ni wanyonyaji wa mikoa mingine kwa logic ya ovyo Kabisa kwamba eti - michango Yao kwa GDP ya taifa ni midogo lakini viwango vyao kimaendeleo ni vikubwa zaidi. Tuka challenge Hilo ka kuingiza Suala la Kodi katika equation. Akina Ritz, Mkandara, adhurusi na wafuasi wengine wa zitto wakapinga hoja ya kodi na kusema GDP is supreme na ndio iwe kigezo Cha kuinua Hali za wananchi husika. Tukasema kwamba kwa Hali ya Sasa, GDP pekee is misleading, na mapato ya kodi ni more practical katika kuelewa Nini kinaendelea. Leo wote wanaimba wimbo wa kodi kodi kodi na wanaenda mbali zaidi na kumsafisha zitto kwamba aliposema "pato la taifa", alimaanisha mfumo wa kodi. Ni Kama vile kusifia mfalme amevaa Nguo nzuri kumbe yupo utupu.

Tena si kuwa wanaimba wimbo wa kodi kodi kodi, wameacha kabisa kuzungumzia GDP

Kila hoja wanayotaka tuiongelee kwa mtazamo wao sisi tunakubali, baada ya dakika tano wanahamisha goli, hatujui watasingizia nini sasa. Twambieni tuongelee hoja za kiongozi mkuu kwa kutumia nini GDP au Kodi? Tupo tayari kwenda mnakotaka

1. Alinda kaibua lingine, anauliza hivi kama DGP alizotumia supreme kuonyesha unyonyanyaji wa mikoa ya Aeusha na Kilimanjaro kwa kuchangia kidogo na kuwa na maendeleo, vipi Lindi ambayo inachangia kidogo lakini ipo juu ya Shinyanga?
(Hii ni kwa mujibu wa maelezo ya Adharusi, Ritz(hotuba ya Shinyanga) Kapwela n.k. Hapa ''hatujamwekea maneno'' ni yenu

2. Nimeshangazwa na mkuu mmoja akisema mipango ya serikali na bajeti inategemea wafadhaili.
Huyu anaishi first world, sijui huko Canada bajeti inategemea wafadhili na ni wapi hao. Nimeskikitila sana , naye aje kuhamisha goli

3. Mchambuzi kasema, kwani Shinyanga inapaswa ipate kiasi gani cha kodi ili kuongeza 0.46% ya sasa?

4. Nguruvi3 anauliza kama kigezo ni madini na corporate tax, zile xa Tanzanite zinaachwa Arusha au zinakwenda Dar?

5 Alinda akauliza, Gamba la Nyoka aliposema Shinyanga haipati 'stahili'(Alinda nasahihisha kwa niaba) au stahiki kama Mkandara anavyosema alimaanisha nini? Tunaona wanatafuta hifadhi ya spelling na maneno!

Hadi hapo kama hakuna majibu ya maana(uchambuzi na utambuzi), basi watu wakae kimya wenye hoja tuendelee
 
Back
Top Bottom