============================== ============================== ====
Nawashukuru nyote mlionisaidia kulielewa suala la Kodi na GDP kwa undani zaidi. Nimejua kuwa, kwa kutambua sehemu husika ilinapa kodi na tozo kiasi gani na inachangia kiasi gani kwenye GDP ndiyo unaweza kupima mchango wa sehemu hiyo katika maendeleo ya sehemu yenyewe na nchi kwa ujumla.
Baadaye nimeenda mbali kwenda kutafuta ubora wa kipimo hiki cha GDP. Kwanza nimeelezwa, GDP hutumiwa na wachumi kwa shughuli hii (kama nilivyoinukuu):
Economists use GDP to measure the relative wealth and prosperity of different nations, as well as to measure the overall growth or decline of a nation's economy.
Pia nikakumbana na vitu vinavyopunguza ubora wa kipimo hiki cha GDP (nanukuu):
But there are a number of shortcomings to using GDP. Here are just a few:
1. GDP doesn't count unpaid volunteer work: .......
2. Disasters can raise GDP: Wars require soldiers, oil spills require cleanup, and natural disasters require health workers, builders, and all manner of helping hands. Rebuilding after a disaster or war can greatly increase economic activity and boost GDP.
3.GDP doesn't account for quality of goods: Consumers may buy cheap, low-quality, short-lived products repeatedly instead of buying more expensive, longer-lasting goods (Hili nadhani limeelezwa).
Sasa kwenye namba mbili hapo ndiyo pamenistua kweli, kumbe yawezekana tunaambiwa (mfano) Shinyanga ama Kilimanjaro zinachangia sana kwenye pato la Taifa (GDP). Kumbe mikoa inaongeza matumizi tu ya kwenye pato hilo labda kutokana na majanga yaliyoikumba mikoa hiyo...!! Na bado mtu anakwambia Mkoa fulani unachangia sana kwenye GDP lakini hauna maendeleo...! lakini mwingine unachangia kidogo lakini unamendeleo! Kauli hii isipofafanuliwa zaidi kujua mikoa hiyo inachangiaje GDP (majanga ama uzalishaji?), inapotosha sana umma ambao hawajui maana ya pato la taifa (GDP). Na hapa ndipo S.L anapotiwa hatiani kuwa alitoa kauli za kichonganishi. Mimi siyo mchumi ila kama nimetafsiri maelezo yale ya wanauchumi kwa usahihi, basi na sisitiza S.L (Zitto) anahatia.
Chanzo cha nukuu zangu ni>>>>
What are the advantages and disadvantages of Gross Domestic Product?
Mkuu
TUJITEGEMEE hiyo video ya Mwl imekuja tukiambiwa wakati wa Nyerere hakukuwa na kodi!
Real, mtu anaandika hayo ili tu kujenga hoja za kumtetea SL. Unaweza kuona ukubwa wa tatizo!
Pili, watu wanasahau masharti ya IMF kwa serikali ilikuwa kukusanya kodi. Serikali ya Mwinyi inalaumiwa . Na Mkapa ilibidi atende.
Tatu, watetezi wa kiongozi mkuu hakuna hata mmoja anayetuonyesha uhusiano wa GDP na Maendeleo.
In fact wamekimbi huko sasa wamerudi kule Mchambuzi alipowaambia ni sahihi 1.e kodi.
Tunaulliza kodi zinaathiri vipi Shinyanga? Utetezi ni migodi ya madini 'kuwepo Dar' Tukauliza ile ya Arusha ina makao yao wapi? Kimya
Nne, tukauliza nini ambacho Shinyanga na Arusha wanatofautiana katika shughuli za kijamii.
Tunaona ufafanano. Tukahoji iweje Shinyanga ichangie kodi 0.46% tofauti na Arusha. Wamekimbia wanatafuta spelling
Tano, tukasema turudi kwenye GDP wanayoelewa wao. Tukauliza, kama GDP ni kigezo cha maendeleo, shughuli za kijamii zinahudumiwaje kwa kutumia GDP? Hakuna jibu, wote tutweee ! wanatafuta mistari yenye herufi waibuke
Sita, tukasema kama GDP inapima nani apate nini ili kuendelea, vipi Mbona Lindi ina GDP ndogo sana ukilinganisha na Kilimanjaro na Arusha, kimaendeleo ipo juu ya Shinyanga? Nako kimya, wamejibanza wanatafuta vijherufi vilivyokosewa waibuke
Saba, tukauliza tuelezwe mantiki za kauli za kiongozi mkuu kulinganisha mikoa, kuchagua baaadhi na kuinanika, kauli za ' hata hivyo, maendeleo zaidi, kuchangia zaidi au kidogo zililenga nini'' tunaambiwa asambaza uzalendo! Uhuni unapakwa rangi
Wengine tulishamtia hatiani siku nyingi. Kauli zake za takwimu za kulinganisha jamii, kwa mtu mwenye weledi na mature hawezi kuzikubali bila ushawishi. Ni kauli za kipuuzi sana kwa mwanasiasa mwenye miaka 15+ katika chombo kama bunge
Ni kauli zinazotakiwa zitolewe na mtu anayejiunga siasa. Kuanza comparison ya jamii ni kuleta 'uhutu na utusi' bila sababu
Tunadhani jamvi limeona wanavyotafuta nahau na methali . Hawana hoja, wamehamisha magoli sasa goli lipo karibu na jukwaa kuu
Ukirudi nyuma tulieleza makundi matatu , la kwanza linaloamini katika kiongozi mkuu.
Hili tulisema limelishwa yamini au limbwata. Lipo tayari kujitoa fahamu na kuuza utu na akili ilimradi tu kukaa mbele na kumsikiliza
Kundi la pili, ni lile lisilokubaliana naye kwasababu keshapoteza imani, haaminiki na linamuona ni laghai hatari kwa usalama na umoja
Kundi la tatu, ni lenye mashaka. Hili halimfahamu. Kundi lipo karibu kupotea, hakuna shaka tena juu yake.
Ni ima kundi la kwanza au la pili. Hakuna mashaka kwa mtu anayelenga kuchonganisha jamii
Leo tunaona ukweli, Shinyanga haina matatizo yoyote na Kilimanjaro au Arusha.
Na kwamba matatizo yapo katika dude la miaka 50. Tunaona hakuna ushahidi wa kitakwimu kuwa mkoa mmoja unaonya mwingine.
Tuna maelezo ya kichonganishi kuhusu hilo yakitolewa na mtu muflisi wa kisiasa, asiyejali nchi tna aliye tayari kuiutumbukiza katika matatizo.
Wamekmibia hoja, wamejificha, 'make no mistake'! uzi ukisonga hoja zikiwa mbali wataibuka na spelling check, watakuja wakiwa na wamebeba paste zao, na tutasikia 'mzee mawazo kasema haya.., Msikie Shemahonge, Hapa chini ni Maliwaza, Ngolile kasema'' n.k Hakuna uchambuzi wala utambuzi . Ni waviziaji,wapo bize wanatafuta vimistari na spelling vya kuanzia mada
Kwa hili Kiongozi mkuu alikuwa na nia ovu na mikoa ya kaskazini, nia ovu kabisa! Tunasema ni ovu kijamii, kimantiki, kisiasa na kitakwimu.
Wenye hoja waendelee, wenye viroja toeni nafasi