Duh
Waberoya...kweli umeyatoa ya moyoni! Hebu ninukuu machache;
Mdogo wangu
Waberoya, hivi unakumbuka ni wapi pale mimi na wewe tulianza kuhitilafiana kimawazo na kimsimamo? Nimejiunga JF rasmi tarehe 31 May 2008 na wewe ukajiunga rasmi miezi mitatu baadaye tarehe 3 Agosti 2008. Uzuri wa JF ni kwamba inatunza kumbukumbu na ingawa kuna uwezekano wa mtu kufanyia marekebisho post zake za awali, si rahisi kurekebisha majibu ya walioku"quote".
Kuna watu wamebadilisha ID kwa aibu ya misimamo yao ya awali kuhusishwa na misimamo yao ya leo, kuna watu wameanzisha ID mpya baada ya kupigwa ban na kuna watu wanazo IDs kibao kuficha unafiki wao. Mimi Mag3, nakuhakikishia ni yule yule wa jana, leo na kesho...kupinga, kukemea na kulaani maovu yaliyopandwa, yakalelewa, yakastawi na sasa yamekuwa sugu ndani ya taifa letu hadi kutufikisha hapa tulipo.
Sisiti hata siku moja kuiita CCM adui nambari moja wa taifa hili kwa sababu bila CCM hatungefika hapa tulipo kwa mazuri au mabaya na bahati mbaya mabaya ndio yamekuwa kama dira kwa watawala wetu wa CCM. Mtu yeyote ambaye ananyooshea upinzani kidole kwa hapa tulipo hana tofauti na CCM, mtu yeyote anayeshirikiana na CCM katika kutetea mipango yake miovu, kwangu sina jina lingine kwake baki msaliti wa wananchi na taifa.
Kama wananchi wanakosa huduma za kijamii, kama ajira zinakosekana, kama tiba na dawa zinakosekana, kama elimu na waalimu ni haba, kama barabara hazipitiki, kama matiatizo ya maji na umeme yamekuwa sugu, kama hali ya uchumi inazidi kudidimia, kama vyombo vya dola vinashindwa kutoa uhuru, haki na usawa bila kuangalia itikadi, jinsia, rangi, dini na ukabila, wa kulaumiwa ni serikali inayoongozwa na CCM, period.
Kama atatokea mtu, badala ya kuelekeza malalamiko yake kunakohusika, akaamua kuyaelekeza sehemu ya jamii isiyo na mamlaka wala haijawahi kukamata madaraka ya nchi hii siwezi kumuelewa.
Waberoya naomba nikuulize...kwa nini unadhani mimi ni mwana Chadema? Kwa sababu naunga mkono jitihada zao? Kwa sababu nailaumu chama tawala CCM? Au ni kwa sababu sikubaliani na kipenzi chako,
Supreme Leader?
Kwa ufahamisho
Zitto tulikuwa naye bega kwa bega pale aliposimamia alichokiamini bila kuyumba lakini kama wote tunavyofahamu, katika nchi hii, watu wenye msimamo thabiti dhidi ya CCM usalama wao unakuwa katika hati hati na mifano ipo. Kwanza watajaribu kukushawishi kwa njia ya amani, pili watatumia vitisho mwisho na wakishindwa utawekewa mtego na ukinasa ujue huchomoki, usiponasa ukae tayari kujitoa mhanga.
Wapo watu walioshindwa kuvuka hatua ya mwanzo, wapo waliojitahidi wakafikia hatua ya pili wakasalimu amri na wapo walioweza kufikia hatua ya tatu and they have the scars to show for it. Hata hivyo CCM haijakata tamaa kwa watu hawa...it could be just a matter of time. Karata ya mwisho ni offer, offer one cannot refuse for refusing is tantamount to committing suicide. Sadly the few that did manage, their loved ones have but only bitter memories left!
Do you sincerely believe in your heart of hearts that Chadema can commit acts like you allege and get away with it? Do you really believe that opposition in general can get supoort from diehard CCM supporters without any repercussion? CCM imeapa, si mara moja, mara nyingi tu kwamba itabaki madarakani hata kwa miaka mia come what may. Na kweli mwaka 2010 they proved beyond any doubt that election results mean nothing!
you saw how out of 20,000,000 million registered voters Kikwete was declared President with 5,000,000 votes! You saw how the issue of a new constitution was handled yet when the Opposition formed a united front, UKAWA to challenge the whole process, one member from Opposition, Zitto Kabwe distanced himself calling them
wasaka tonge! But when matters got hot the cheek had the nerve to try to retract his steps...with no apology whatsoever!
Ukiunganisha utabiri wa watu kama Wassira na Mwigulu ni kama walikuwa wanasubiri tu kifo cha Chadema, ni silaha gani walipanga kuitumia kuua hilo zimwi lao Chadema? Nakumbuka mwishoni mwa mwaka 2014 yupo moja aliyesema mwezi wa nne 2015 ndio mwisho wa Chedema, je ni kitu gani ama tukio gani lilikuwa linasubiriwa kuisambaratisha Chadema? Hata kipofu ataona ni maamuzi ya kesi ya Zitto ndiyo yalikuwa yanasubiriwa!
Waberoya, admit it, you have never liked Chadema, you have never liked Mbowe, you have never liked Dr. Slaa...in short kama walivyoamini the Wassiras, the Lukuvis, the Napes...kwako Chadema bila Zitto si chochote si lolote and yet you have the nerve kudai wengine ni worshippers wa Mbowe. Well, for your info, Mbowe is the Chairman and Dr. Slaa is the Secretary General and whether you like it or not there is nothing you can do about that!
Waberoya, mimi sitakuita majina, huo ni utoto, ila nitakuambia ukweli...Zitto failed the test and Chadema had every right to show him the door. Afanye anayoyafanya huko ila kwa Chadema he is a reject na kwetu sisi watu tusioyumba katika vita yetu ya ukombozi, that's one more huddle crossed and the most we can wish him ni ushirika mwema na wenziye wa siku zote, chama cha wezi, wanafiki na wauaji wa CCM. Tahadhari moja tu kijana, CCM days are coming to an end for the birds are coming home to roost!