Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Kwa hoja zako, we cant underestimate the power of social media katika kipindi hiki cha kiu ya mageuzi na mabadiliko. Awali ulipinga hilo katika mjadala wako na Nguruvi3, lakini sasa naona tupo upande mmoja wa hoja. Asante.

Mchambuzi:

Nope we aren't. You guys, the gate keepers of intellectual discourses, use JF as the only channel of communication. What's worse, you don't use your real identification. So why do you expect people to take your message very seriously? How do I know that Shayu, Mchambuzi, Nguruvi3 aren't the same person?
 
Unashindwa kuelewa hoja Ya msingi hapa juu ya ACT kuwa Mpini wa CCM kumaliza upinzani. Hiyo mifano Ya Akina Mbowe et al haina mashiko. Rejea hoja yangu huko juu.

Kuhusu hoja yako kwamba uzalendo ni kusema ukweli, je Superior leader wa ACT "Wazalendo" anasema ukweli jukwaani? Nitajie mambo matatu ambayo kayasema Songea, mwanza etc kwamba kwa mtazamo wako ni Ya kweli.

Kuhusu mimi na CCM, sikuzaliwa CCM, nilizaliwa mwanadamu na baadae kupewa uraia wa Tanzania kutokana na kuzaliwa katika ardhi Ya Tanzania. Kwahiyo kwangu, Nchi kwanza, vyama Vya Siasa baadae. Can't trade Nchi yangu na Chama cha Siasa, never.
Hoja ni ACT kuwa mpini,kwanini mnamjadili ZITTO,wakati ninyi mmekua mkisema amemfukuza LIMBU,Mara Kitila kachelewesha uchaguzi ili zitto agombee,oooh ACT kimeanzishwa na ZITTO,kama chama ni cha ZITTO,limbu hasingeng'ang'ania,kwanini awe mbishi wakati aliwekwa tu,mnatuchanganya sasa naomba unijibu ACT ni ya ZITTO au LIMBU,kama ni ya LIMBU naomba mtutake radhi kwa kutudanganya,kuwa imeanzishwa na Zitto,kama ni ACT ni ya ZITTO basi LIMBU hakutakiwa kujihusisha
 
Too much mkuu, sijasoma yote

Yes uko right, I hated chadema since 2009 pale mlipoamua kubaka demokrasia waziwazi!! pale mliposema zitto asigombee uenyekiti na kutoa sababu ambazo zilikuwa za kitoto na haziendani na maana ya demokrasia ( hapa utabwabwaja sana) ndio ukweli na nilitegemea kwa akili zako kuanzia muda huo neno 'DEMOKRASIA' ndani ya chadema is just either a new vocabulary au cosmetic!! sikuona sababu ya kuitisha uchaguzi wakati hamkuwa tayari kufanya uchaguzi wa mwenyekiti, kwa nn msingesema tu uchaguzi ngazi zote ila kwa hatua hizi za sasa hatutafanya uchaguzi wa mwenyekiti? kulikuwa na ugumu gani?? maana kuanzia muda huo Zitto akaanza kuchukiwa.....recall it...

nakupa pole tena mkuu Mag3
\
Waberoya, tafadhali uwe mkweli, kumbuka JF inatunza kumbukumbu!...dont be disingenuous, tofauti zetu wengine na Zitto hazikuanzia wala hazihusiki na kutaka kwake kugombea uenyekiti w Chadema. Je unakumbuka wakati Zitto alipotaka kususia JF baada ya kubanwa kutokana na mitambo ya Dowans/Richmond? Pamoja na mods kufuta matusi aliyoyamwaga kwa wana JF waliompa ukweli, baadaye ilibidi aombe msamaha na kweli wengi tulikuwa tuko tayari kumsamehe!

Unakumbuka wakati anajitapa anavyojiweza na kwamba kwa muda wa miaka miwili mitatu tu kwenye Ubunge ameweza kumiliki magari ya kifahari? Ni hapo wengine alianza kutupa wasiwasi. Unakumbuka alivyotamba kwamba yako majimbo yalikuwa yanamsihi akagombee Ubunge kwani wako tayari kumpa? Kigoma, Geita hadi Dar es Salaam? Juzi juzi hapa kaanza tena vitimbwi vyake. To you he might be a powerhouse, to us he is a blown fuse!
 
Mag3

issue ya UKAWA zote hizo ni zittophobia, level ya chadema at that time haikuwa ya kushirikiana na CUF au NCCR!!! BRAND POWER ya chadema ilikuwa juu mno.....ilijiuza kabisa, leo haiwezekani cocacola ikajiunga na azam cola ili iuze...stupid!

Hilo ndio tatizo lenu. Mnaweka personalities mbele, issues nyuma. Mnadhania Chama ni Viongozi, Ma degree yao, uwezo wao wa kujieleza, uwezo wa fedha na mengine yasiyokuwa na tija. Chama ni watu, kwahiyo ukipata kitu cha kuunganisha watu bila Ya kujalisha ukubwa au udogo wao, huo ni ushindi. Hakuna cha kuwaunganisha wananchi hivi sasa zaidi Ya constitutional reforms. Hata huko Chama cha kilaghai ACT Wazalendo, it's a matter of time, mtarudi kupigia magoti ukawa.

mbaya zadi katika UKAWA kuna mbunge wa kuteuliwa na CCM...tena rais kikwete mbaye wewe na wenzako mnaona dhambi kwa mtu kukaribiana naye!!? CUF na CCM zanzibar inaunda serikali moja in anycase lazima wabunge a CUF na CCM zanzibar wana ushirikiano wa kikazi ambao nyie ni sumu.....

Shallow argument. Nilishajibu hilo.

UKAWA was purely an art of Mbowe kumzika zitto asiende popote pale.....kweli alifanikiwa zitto hakwenda huko..leo yuko ACT mna kiaffiliate na CCM, wakati UKAWA kuna mbunge wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM.....!!!

Very shallow analysis. Chimbuko la ukawa ni alliance against Zitto? Jamani! Sasa kwanini sasa anataka kujiunga na hii alliance?

Mag3 unapojadili issues na watu kama akina waberoya, yaani mimi hapa lazima uwe smart kwa vitu vidogo kama hivi ambavyo huwezi ukawa na majibu navyo ila utazunguuuuuuka weeee; utarudi pale pale na utajiona mjinga kucheza michezo ya wanasiasa hawa na wamekamata akili zako ukashindwa kuwaza; that is cult, it is political seduction kuwa na mahaba ya kushindwa kuuliza, kujiuliza na kutoona dhaihiri..nilikataa
Waberoya, kama mada hii ni for mediocre, unatafuta nini humu? I will tel you once - wewe ni Zitto, na unashindwa kuvumilia facts presented humu.

ndio maana nasema mnafukuza watu JF maana tongotongo kama hizi bado mnazo hamzioni hata ukipewa kioo unaangalia pembeni unakalia kusema wa 2008 so what??

Nenda Basi kama hoja zetu zinakufukuza. And I promise I won't cc you again.
 
Last edited by a moderator:
Hoja ni ACT kuwa mpini,kwanini mnamjadili ZITTO,wakati ninyi mmekua mkisema amemfukuza LIMBU,Mara Kitila kachelewesha uchaguzi ili zitto agombee,oooh ACT kimeanzishwa na ZITTO,kama chama ni cha ZITTO,limbu hasingeng'ang'ania,kwanini awe mbishi wakati aliwekwa tu,mnatuchanganya sasa naomba unijibu ACT ni ya ZITTO au LIMBU,kama ni ya LIMBU naomba mtutake radhi kwa kutudanganya,kuwa imeanzishwa na Zitto,kama ni ACT ni ya ZITTO basi LIMBU hakutakiwa kujihusisha

ACT Wazalendo ni Ya Zitto na wenzake who are worshiping "Zitto almighty". ACT sio Ya wanachama wa ACT. Asante kwa kuona hilo.
 
Mchambuzi:

Nope we aren't. You guys, the gate keepers of intellectual discourses, use JF as the only channel of communication. What's worse, you don't use your real identification. So why do you expect people to take your message very seriously? How do I know that Shayu, Mchambuzi, Nguruvi3 aren't the same person?

Tangia 2007 nimekuwa naweka picha zangu halisi kwenye avatar Humu. Na kama unataka kujua jina langu, naitwa Mpoki Emmanuel Asajile Mwambulukutu. Na hii sio mara Ya kwanza kujitambulisha humu. Hilo ni jina la ubatizo na nililoandikishwa shule Ya chekechea Hadi chuo Kikuu. Sina haja Ya kuwa na majina mawili JF. Harakati za kutafuta mabadiliko hazihitaji multiple personalities, wala unafiki.
 
Adharusi, CHAMVIGA,

Mnalemewa na hoja, mnaanza kujadili watoa hoja. Mchambuzi na nguruvi3 ni mtu mmoja - that's the furthest you can go? Sijui hata huyo Nguruvi3 ni Nani, tumejikuta upande mmoja wa hoja, bila Ya kumsahau Mag3 kwa sababu tunaangalia maslahi Ya taifa kwanza kabla Ya personalities na vyama vya Siasa. CCM, Chadema, ukawa, ACT, Zitto, watapita lakini Nchi itabaki. Kuna hatari kwamba sasa Nchi itapasuka kutokana Na Siasa za kutugawanya za Zitto. Binafsi nipo hapa kujadili against that.

Trading Nchi kwa personalities au Chama cha Siasa? Never!
 
Last edited by a moderator:
Unashindwa kuelewa hoja Ya msingi hapa juu ya ACT kuwa Mpini wa CCM kumaliza upinzani. Hiyo mifano Ya Akina Mbowe et al haina mashiko. Rejea hoja yangu huko juu.

Kuhusu hoja yako kwamba uzalendo ni kusema ukweli, je Superior leader wa ACT "Wazalendo" anasema ukweli jukwaani? Nitajie mambo matatu ambayo kayasema Songea, mwanza etc kwamba kwa mtazamo wako ni Ya kweli.

Kuhusu mimi na CCM, sikuzaliwa CCM, nilizaliwa mwanadamu na baadae kupewa uraia wa Tanzania kutokana na kuzaliwa katika ardhi Ya Tanzania. Kwahiyo kwangu, Nchi kwanza, vyama Vya Siasa baadae. Can't trade Nchi yangu na Chama cha Siasa, never.

Mchambuzi:

Please call a spade spade. Nguruvi3 is deflecting the issue "Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani". CCM is very divided in many fronts. The question is how a divided political machine like CCM could have the nerves to go out out there and destroy the opposition? I don't get that.

CDM owns the entire Zitto saga and the party and its members shouldn't blame anybody else. If they didn't like him, they should have kicked him long time ago.

My point is if you have any issue, please own it. Blaming others is just a deflection. Followers of CDM can't bring a list of what Zitto has done wrong within the party since 2007 and then blame CCM for their unactions.
 
It's a matter of time before you learn kwamba CCM now ni Chama cha tycoons, sio cha wanachama. And it's the very same tycoons who are sponsoring ACT.

Zitto was recruited na Chama Akiwa chuo Kikuu. Waliona uzalendo, upeo na ujenzi mzuri wa hoja. Kwa sasa umemomonyoka kwani Baada Ya kujengwa na kufundwa, kageuka kutaka kuwa zitto almighty, na Msaliti. Swali Dogo tu kwako: Alikuwa na haja gani kutangaza kugombea urais Akiwa Chadema Wakati Chama kilikuwa kinachanja mbuga na operation M4C? Kama sio kutumika kama Mpini ni nini? Alijua kwamba hawezi kuteuliwa kwani katiba Ya Nchi hairuhusu mgombea chini Ya miaka 40. Lengo lake lilikuwa ni kutibua progress Ya Chadema kuelekea 2015, basi. Pamoja na hayo, alivumiliwa sana na pia juhudi nyingi zilifanywa kujaribu kusuluhisha matatizo, lakini wapi. Msome baregu juu ya hilo.

Nadhani umesahau kwamba anayecheza na dangerous blaming game on uneven development in Tanzania ni Huyo huyo mtu wenu Zitto.
 
Zitto kasema siasa za kwa kutaja vyama kwao ACT zimeshapitwa na wakati,anawaambia watanzania Ttatizo ni mfumo,hivo waipigie kura ACT ili ibadilishe na iuvunje mfumo wa kinyonyaji,mambo ya kutaja taja taja vyama amewaachia UKAWA

Basi Zitto hana uelewa juu ya role and functions of political parties in democracy. Ndio maana anawadanganya wananchi kwamba Adui wa maendeleo ni wenyewe kwa wenyewe na sio CCM na serikali yake.

Lakini alipokuwa Chadema alikuwa anataja sana CCM kama Adui, sasa hilo la kuachia kazi hiyo ukawa Akiwa ACT ni news ambazo zinaimarisha hoja kwamba ACT mpini wa CCM kumaliza upinzani. Kumbuka, kitila Yupo on records akisema kwamba kinahitajika Chama kipya cha upinzani kupambana na Chama Kikuu cha upinzani yani Chadema, sio CCM iliyotawala kwa miaka 50. How pathetic.
 
Nguruvi3 Zitto hafai hata kujadiliwa hapa manake kwanza kauli zake ni za kichonganish sana.
Nilijiuliza ivi amesahau kwamba KLM ndio mkoa ambao una ardhi ndogo sana na hivyo wengi wa wakazi wake wako mikoan hususan kigoma kutafuta maisha? Hivi amesahau kwamba kuhusu kilimo KLM haiwez hata kuskika manaked hakuna ardhi hivyo wakulima wengi huenda kulima nje ya mkoa na hurudi kwao kuwekeza tu?

KLM iko mbele kimaendeleo ni kwasabb ya vipaumbele vy wenyeji wake kwamba wanapenda nyumba nzuri, miundo mbinu bora ya bara bara na maji, hosp nk ndio mana wao kujichangia kuweza kutekeleza hayo sio shida.

sijui kwann aone eti KLM ni threat kwa maendeleo ya kigoma wakati amesahau wakazi wake utamaduni tu wa kupenda maendeleo hawakuwa nao. Ebu akawafundishe wenzie kupenda kwanza kwao kupenda maendeleo ya dhati mbona huku mijin wanajenga majumba makubwa lkn vijijin kwao hawajengi?

yaani hoja yake ni dhaifu sana mie akiniuliza nitamwambia nenda kwafundishe wenzio badala ya kukaa kulogana basi wakubali wawekeze kwao uone kama hawata piga hatua.

tusibaguliwe kwani sote tu wamoja, wawaige wachagga kwa kupenda kujenga kwao na waache sifa za kijinga
Nimewasoma nyote na kuja gundua kumbe watu hamuelewi kabisa Zitto alikuwa akizungumzia nini kiasi kwamba ndio maana mkachukua kuwa Shinyanga vs Kilimanjaro. Dadangu tunapozungumzia Umaskini wa Shinyanga haitokani na watu wake yaani WASUKUMA isipokuwa wao kama mkoa wanachangia kiasi gani na wanapewa kiasi gani kwa ajili ya mendeleo yake.

Kwa hiyo hapa kuna tofauti kubwa ya kimaelezo, labda nichukulie mfano mzuri baina yetu, tuseme mathlan wewe unachangia Tsh 20,000, Nguruvi3, Tsh 30,000, Mimi hapa Tsh 10,000, Mchambuzi Tsh 40,000 jumla katika mfuko wetu tunazo 100,000 lakini ili kila mmoja wetu ahudumie shughuli za uzalishaji wewe unapewa zaidi ya nguruvi3 ambaye tunakuja gundua kwamba hali ya maisha yake sio nzuri pamoja na kwamba anazalisha zaid yetu.

Kuna ubaya gani mimi nikimwambia Nguruvi3 kuwa unastahili zaidi ya gfsonwin na kuelezea sababu iwe uhasama baina yako na mimi wakait unajua kwamba kweli Nguruvi alistahili zaidi. hapa sii kwamba wewe ndiye mwenye matatizo yaani hukutaka ama hupendi Nguruvi3 apewe zaidi yako japo unajua kwamba huzalisha zaidi yako - yale yale ya UMIMI nayakuta hapa. Na rahisi sana kwako kutafuta sababu inayokupendeza wewe kuyaweka maneno yangu vibaya ukajiuliza kichwani mwako mwenyewe consciously - "Okay kwa sababu Nguruvi3 mwanamme mwenzake ana maana napendelewa kwa sababu? Mwanamke na kama mimi mwanamke huyu Mkandara anadhani mimi napataje upendeleo huu" Hivyo yote haya unayatunga wewe mwenyewe akilini mwako ukauacha ukweli pembeni.

Basically, umeyasema mwenyewe, kumbe hata Kilimo wana KLM hawafanyi kilimo mkoani kwao, wana ardhi ndogo na mengineyo sasa ni sababu zipi ambazo serikali yetu imetumia kama kigezo kuwapa KLM zaidi ya Shinyanga? Na unapotumia neno wanaKLM unanitia shaka vile vile kwa sababu ya kuhofia kilekile ulochomshutumu Zitto - UKABILA..Kwani ewanaShinyanga hawatoki mkoani mwao, hawatafuti riziki zao nje ya Shinyanga? laa kwa nni uweke tofauti hizi.. Kwa hiyo hatuwezi jenga ila kukisiana tuu na hatutapata jibu wala nani mkweli zaidi.

Mimi sioni tatizo kabisa kwa mwanasiasa ku raise swali hilo haswa anapokuwa anatangaza siasa za sera za chama chake kwa maana ya kwamba kama yeye akiingia madarakani atahakikishia kila anayechangia zaidi atanifaika zaidi. na huwezi kutolea mfano mzuri wa jambo hili pasipo kuwa na mifano halisi ambayo kaionesha japo hamkupenda. Je, angeweza vipi ulielezea jambo hili watu wakalielewa pasipo kutumia mikoa ambayo ni sehemu ya nchi ambayo ACT, given the change inataka kuiongoza.

Ndio maana nikawapa mfano ule mdogo wa kwamba wenzetu nchi zilizoendelea, swala kama hili wala sii la kujadiliwa na zaidi ya hapo wala hili sio swala la itikadi wa sera ni Mfumo wa Kitaifa katika uchangiaji na ugawanaji wa mapato hata ikiwa chama gani kimeingia madarakani mfumo huu haubadiliki. Yaani mfano mdogo hapa Canada kila states huchangia asilimia 5 ya kodi zake mfuko wa Taifa. na Alberta ambao wao ni matajiri wa mafuta hawana hata kodi za ndani yaani Provincial tax wakati Ontario mbali na kuchangia asilimia 5 ya mfuko wa Taifa wana kodi yao ya ndani ya asilimia 8 kwa sababu hawana maliasili za kutosheleza mahitaji yao.

Hivyo unapokuja mgawanyo na kwa sababu Alberta huchangia zaidi wao hupata zaidi vile vile maana kama zilivyoingia hutoka pia kwa Asilimia ni sawa kote zinagawanywa na kwa vigezo tofauti. Na Alberta tokana na mchango wao mgao huu huwatosha kuendesha shughuli za serikali yao hawana haja ya kuwatoza tena wananchi wake kodi nyingine za ndani kama Ontario ambako kutokana na mahitaji yake na pengine hawana vyanzo kama Alberta wameweka kodi zaidi za ndani. Kwa mwananchi anayeishi Alberta atalipa kodi ya mapato Asilimia 5 tu, wakati ukiishi Ontario utalipa kodi ya Asilimia 13 (5+8).

Kwa hiyo sii swala la kujadili hapa Zitto kasema nini na Mbowe kasema nini isipokuwa kinanichoshangaza miye ni kwa nini watu mnashindwa kuelewa kwamba tunayo mikoa, wilaya, majimbo na hatuwezi kuendelea pasipo kufanya kuhakikisha kuwa hizi ndizo huleta tofauti baina ya Mtu na mtu, jimbo kwa jimbo na mkoa kwa mkoa. na ndivyo tutakavyoweza kuzijua tofauti baina ya kiongozi mmoja kwenda mwingine lakini kama leo mimi nifanye kazi kwa bidii na kuzaliisha zaidi lakini kesho nanyimwa uwezo wa kuzalisha zaidi tumefanya nini. Ebu fikiria hivi unafanya vizuri darasani lakini marks zako huchukuliwa na kupewa mtu mwingine, Nguruvi akigundua haya atatumia lugha gani kuyasema wazi.

Kwa nini imefikia watu kumponda Zitto kwa kauli ambayo haina tofauti kabisa na ile ya Mbowe kwa kufikiria vile vile ikiwa sio fikra za uadui baina ya Chadema na ACT maanake mkumbuke tuna vyama 23 na hakunamalalamiko haya zaidi ya yale yalotoka Chadema tu. Binafsi kisiasa sioni tatizo kwa mwanasiasa yeyote kumponda/kumsifia JK sii kwa sababu ni Mkwere bali kwa sababu ya uongozi wake na wala hainamaana ukizungumzia Bagamoyo vs Kigoma basi ina maana ni juu ya Wakwere vs Wabembe au Wamanyema.

I think sisi wenyewe ndio tuko screwed up na hizi idea za Ukabila na Udini kiasi kwamba tunaufanya pasipo kujijua wenyewe. Unaposhinikiza maneno ya Zitto kuwa ya Kikabiila na ukaacha ya Mbowe alosema Wasukuma wako nyuma pasipo kufikiria yeye anayesema haya ni Kabila kgani basi hutakuwa umemtendea haki Zitto. kama Mbowe angekuwa msukuma asingesema aloyasema bali angesema sisi Wasukuma blaablaa blaaa.. NENO NYINYI tayari linamuondoa yeye katika kundi hilo. Ni Ukabila pia kama tutatazama kwa jicho lile lile mlomtazama Zitto.
 
It's a matter of time before you learn kwamba CCM now ni Chama cha tycoons, sio cha wanachama. And it's the very same tycoons who are sponsoring ACT.

Zitto was recruited na Chama Akiwa chuo Kikuu. Waliona uzalendo, upeo na ujenzi mzuri wa hoja. Kwa sasa umemomonyoka kwani Baada Ya kujengwa na kufundwa, kageuka kutaka kuwa zitto almighty, na Msaliti. Swali Dogo tu kwako: Alikuwa na haja gani kutangaza kugombea urais Akiwa Chadema Wakati Chama kilikuwa kinachanja mbuga na operation M4C? Kama sio kutumika kama Mpini ni nini? Alijua kwamba hawezi kuteuliwa kwani katiba Ya Nchi hairuhusu mgombea chini Ya miaka 40. Lengo lake lilikuwa ni kutibua progress Ya Chadema kuelekea 2015, basi. Pamoja na hayo, alivumiliwa sana na pia juhudi nyingi zilifanywa kujaribu kusuluhisha matatizo, lakini wapi. Msome baregu juu ya hilo.

Nadhani umesahau kwamba anayecheza na dangerous blaming game on uneven development in Tanzania ni Huyo huyo mtu wenu Zitto.

Man I respect your contribution here, but I think now you have started to dwell into conspiracy theories. I think you try to connect dots so you could blame CCM and free CDM from its incompetency. CDM has blown away its chances (period) and that's what you should deal with.

With regard to Zitto's announcement, I don't know why the issue caused a major uproar within the party. It seems to me the leaders of CDM are mentally insecure. For God sake, the guy didn't even meet the age requirements. So there was nothing to afraid and discuss there. Furthermore, CDM is a democratic party and they shouldn't have anointed the candidacy for president position 5 years early. CCM don't do that. GOP don't that. Members of CDM let their emotions to take the best of them. Strategically they were just poor.
 
Tangia 2007 nimekuwa naweka picha zangu halisi kwenye avatar Humu. Na kama unataka kujua jina langu, naitwa Mpoki Emmanuel Asajile Mwambulukutu. Na hii sio mara Ya kwanza kujitambulisha humu. Hilo ni jina la ubatizo na nililoandikishwa shule Ya chekechea Hadi chuo Kikuu. Sina haja Ya kuwa na majina mawili JF. Harakati za kutafuta mabadiliko hazihitaji multiple personalities, wala unafiki.

Mpoki:

Based on the your profile, I can tell that the love of our country alone can't connect us. It seems you were born in a relative privileged family. You went to a boarding school where you met students from different backgrounds. To you, all Tanzanians are the same and one tribe. Your brain has been wired to think that way.

I, on other hand, have different experience. I didn't go to boarding school or university. I live in the area where majority are members of my tribe. If you don't come to our district to visit my people, I won't connect to you even though you are a sage person in JF. It's simple as that.
 
\
Waberoya, tafadhali uwe mkweli, kumbuka JF inatunza kumbukumbu!...dont be disingenuous, tofauti zetu wengine na Zitto hazikuanzia wala hazihusiki na kutaka kwake kugombea uenyekiti w Chadema. Je unakumbuka wakati Zitto alipotaka kususia JF baada ya kubanwa kutokana na mitambo ya Dowans/Richmond? Pamoja na mods kufuta matusi aliyoyamwaga kwa wana JF waliompa ukweli, baadaye ilibidi aombe msamaha na kweli wengi tulikuwa tuko tayari kumsamehe!

Unakumbuka wakati anajitapa anavyojiweza na kwamba kwa muda wa miaka miwili mitatu tu kwenye Ubunge ameweza kumiliki magari ya kifahari? Ni hapo wengine alianza kutupa wasiwasi. Unakumbuka alivyotamba kwamba yako majimbo yalikuwa yanamsihi akagombee Ubunge kwani wako tayari kumpa? Kigoma, Geita hadi Dar es Salaam? Juzi juzi hapa kaanza tena vitimbwi vyake. To you he might be a powerhouse, to us he is a blown fuse!
Indeed a blown fuse
 
Nimekuja kujadili hii maada kwa sababu umeniita, ila bahati mbaya, akina Mchambuzi mmeshusha kabisa hadhi ya kufikiri hapa JF na mmekuwa kama watoto, hayawani, wapuuzi, wapumbavu, sijui mmekula maharage ya wapi? sijui nani kawaroga?? maana sio kawaida kabisa
Mkuu unaweza kujenga hoja bila matusi.

Punguza jazba, vutafikra na jimwage ukumbini.

Jenga hoja tutakusoma, pangua hoja tutaelewa, nena hoja tutatafakari

Ahsante
 
Man I respect your contribution here, but I think now you have started to dwell into conspiracy theories. I think you try to connect dots so you could blame CCM and free CDM from its incompetency. CDM has blown away its chances (period) and that's what you should deal with.

With regard to Zitto's announcement, I don't know why the issue caused a major uproar within the party. It seems to me the leaders of CDM are mentally insecure. For God sake, the guy didn't even meet the age requirements. So there was nothing to afraid and discuss there. Furthermore, CDM is a democratic party and they shouldn't have anointed the candidacy for president position 5 years early. CCM don't do that. GOP don't that. Members of CDM let their emotions to take the best of them. Strategically they were just poor.

I considered mr. Zitto as just a kid who is dreaming to be a pilot or a Doctor.....he just dreamed to be a president!! that was a taboo to CDM leaders....the Kid that all CDM elders participated in raising him up and who is considered as their 'child'

I see nothing wrong for my son to dream big!!

Thanks Zakumi
 
Hilo ndio tatizo lenu. Mnaweka personalities mbele, issues nyuma. Mnadhania Chama ni Viongozi, Ma degree yao, uwezo wao wa kujieleza, uwezo wa fedha na mengine yasiyokuwa na tija. Chama ni watu, kwahiyo ukipata kitu cha kuunganisha watu bila Ya kujalisha ukubwa au udogo wao, huo ni ushindi. Hakuna cha kuwaunganisha wananchi hivi sasa zaidi Ya constitutional reforms. Hata huko Chama cha kilaghai ACT Wazalendo, it's a matter of time, mtarudi kupigia magoti ukawa.

Shallow argument. Nilishajibu hilo.

Very shallow analysis. Chimbuko la ukawa ni alliance against Zitto? Jamani! Sasa kwanini sasa anataka kujiunga na hii alliance?

Waberoya, kama mada hii ni for mediocre, unatafuta nini humu? I will tel you once - wewe ni Zitto, na unashindwa kuvumilia facts presented humu.

Nenda Basi kama hoja zetu zinakufukuza. And I promise I won't cc you again.

Mchambuzi uliniita ha ha ha! I have just done what you expected!!

sasa ukisema mimi Zitto na mtu nishawahi kutumia my true verified ID naweza kukusaidiaje hapo??

kwa hili tu, unazidi kujidharaulisha......kwa hiyo wewe ni Nguruvi? au Mag3? au wewe mbowe??

poor you!!
 
Kinachonishangaza mimi mfuatiliaji wa minakasha ya hapa jukwaani kuna majina kadhaa wao huwa wanakubaliana kila jambo litakaloletwa na mmojawao.

Wakati huohuo watu hao ni mashabiki/wanachama wa CHADEMA. Hivi kipi kinawafanya muwe na mawazo yanayofanana wote linapokuja suala la kupambana na mh Zitto lakini pia mnanyamazia maovu ya kina Mbowe,Slaa, Ndesamburo wanaofanya yaleyale aliotuhumiwa kuyafanya zitto? Nguruvi3, Mag3, Mchambuzi n.k Mnamchukia ZZK Kwasababu gani hasa? Ukanda atokao,dini yake,kabila lake au mafanikio yake kisiasa Tanzania na duniani kwa ujumla? Msiniambie ni usaliti kama walivyolishwa uongo huo na wanavyouimba wimbo huo kwa ustadi BAVICHA.
Kuna tatizo gani dunia nzima ikukubaliana kuwa jualinazunguka jua na si vinginveyo?

Kuna tatizo gani wakitokea watu 50 wakakubaliana kwa pamoja sisi ni nchi masikini?

Kuna tatizo gani watu 3 au 4 wakiona Zitto ni tatizo?Kwanini 50 wanaomuona ni masiah wasiwe tatizo?
Je, ni lazima tu watu wapingane bila sababu?

Kuhusu Mbowe, Slaa, Ndesamburo, kwanini usianzishe mada kuhusu wao tukachangia kama unavyochangia hii?
Kwani ni lazima hao uliowataja waanzishe mada? Je, mabaya ya Mbowe yanasafisha uchafu wa supreme leader?

Kuhusu uanachama wa CDM, una haki pia ya kusema Nguruvi3 ni mdogo wake Dovutwa, na ni mwanachama wa TPP ya Kuga mziray. Hiyo ni haki yako,ndio starehe ya JF. Unaweza kusema tu

Kuhusu chuki kwa Zitto, jukumu la kumtia hatiani mshtakiwa lipo kwa mwendesha mashtaka ‘the onus is on the complainant to prove guilty'Unalo jukumu la kuonyesha Chuki zetu kwa Zitto.

Kamahuwezi, chuki haipo unachofanya ni udhaifu wa kujibu hoja zinazomkabili

Hatukusema Wananchi wa Shinyanga wanachangia sana na kupata kidogo kuliko wa KLM wanaochangia kidogo na kupata sana. Kasema Zitto, sisi tunajadili. Nani mwenye chuki hapo?

Yule aliyelianzisha au sisi tunaosimama katika utaifa?

Kuhusu chuki kama ni kutokana na ukanda, ukabila au dini,wewe unayesema tuna chuki unadhima ya kuthibitisha madai yako kwa kutumia vigezo hivyo. Hivyo, nafasi ipo unaweza kulieleza jamvi.

Hata hivyo, ukiona mtu anakimbilia hayo mambo ujue kuna ombwe la hoja.

Ukanda, ukabila na udini ndio silaha nyepesi na rahisi kwa wasiona hoja kama supreme
 
Waberoya

Katika ndoto za supreme, tungependa asichonganishe wananchi

Mkuu, matatizo ya watu wa Shinyanga na Mwanza yanasababishwana watu wa Kilimanjaro na Arusha?

Ndipo hoja ilipo.

Nimewasoma nyote na kuja gundua kumbe watu hamuelewi kabisa Zitto alikuwa akizungumzia nini kiasi kwamba ndio maana mkachukua kuwa Shinyanga vs Kilimanjaro. Dadangu tunapozungumzia Umaskini wa Shinyanga haitokani na watu wake yaani WASUKUMA isipokuwa wao kama mkoa wanachangia kiasi gani na wanapewa kiasi gani kwa ajili ya mendeleo yake.

Kwa hiyo hapa kuna tofauti kubwa ya kimaelezo, labda nichukulie mfano mzuri baina yetu, tuseme mathlan wewe unachangia Tsh 20,000, Nguruvi3, Tsh 30,000, Mimi hapa Tsh 10,000, Mchambuzi Tsh 40,000 jumla katika mfuko wetu tunazo 100,000 lakini ili kila mmoja wetu ahudumie shughuli za uzalishaji wewe unapewa zaidi ya nguruvi3 ambaye tunakuja gundua kwamba hali ya maisha yake sio nzuri pamoja na kwamba anazalisha zaid yetu.

Kuna ubaya gani mimi nikimwambia Nguruvi3 kuwa unastahili zaidi ya gfsonwin na kuelezea sababu iwe uhasama baina yako na mimi wakait unajua kwamba kweli Nguruvi alistahili zaidi. hapa sii kwamba wewe ndiye mwenye matatizo yaani hukutaka ama hupendi Nguruvi3 apewe zaidi yako japo unajua kwamba huzalisha zaidi yako - yale yale ya UMIMI nayakuta hapa. Na rahisi sana kwako kutafuta sababu inayokupendeza wewe kuyaweka maneno yangu vibaya ukajiuliza kichwani mwako mwenyewe consciously - "Okay kwa sababu Nguruvi3 mwanamme mwenzake ana maana napendelewa kwa sababu? Mwanamke na kama mimi mwanamke huyu Mkandara anadhani mimi napataje upendeleo huu" Hivyo yote haya unayatunga wewe mwenyewe akilini mwako ukauacha ukweli pembeni.

Basically, umeyasema mwenyewe, kumbe hata Kilimo wana KLM hawafanyi kilimo mkoani kwao, wana ardhi ndogo na mengineyo sasa ni sababu zipi ambazo serikali yetu imetumia kama kigezo kuwapa KLM zaidi ya Shinyanga? Na unapotumia neno wanaKLM unanitia shaka vile vile kwa sababu ya kuhofia kilekile ulochomshutumu Zitto - UKABILA..Kwani ewanaShinyanga hawatoki mkoani mwao, hawatafuti riziki zao nje ya Shinyanga? laa kwa nni uweke tofauti hizi.. Kwa hiyo hatuwezi jenga ila kukisiana tuu na hatutapata jibu wala nani mkweli zaidi.

Mimi sioni tatizo kabisa kwa mwanasiasa ku raise swali hilo haswa anapokuwa anatangaza siasa za sera za chama chake kwa maana ya kwamba kama yeye akiingia madarakani atahakikishia kila anayechangia zaidi atanifaika zaidi. na huwezi kutolea mfano mzuri wa jambo hili pasipo kuwa na mifano halisi ambayo kaionesha japo hamkupenda. Je, angeweza vipi ulielezea jambo hili watu wakalielewa pasipo kutumia mikoa ambayo ni sehemu ya nchi ambayo ACT, given the change inataka kuiongoza.

Ndio maana nikawapa mfano ule mdogo wa kwamba wenzetu nchi zilizoendelea, swala kama hili wala sii la kujadiliwa na zaidi ya hapo wala hili sio swala la itikadi wa sera ni Mfumo wa Kitaifa katika uchangiaji na ugawanaji wa mapato hata ikiwa chama gani kimeingia madarakani mfumo huu haubadiliki. Yaani mfano mdogo hapa Canada kila states huchangia asilimia 5 ya kodi zake mfuko wa Taifa. na Alberta ambao wao ni matajiri wa mafuta hawana hata kodi za ndani yaani Provincial tax wakati Ontario mbali na kuchangia asilimia 5 ya mfuko wa Taifa wana kodi yao ya ndani ya asilimia 8 kwa sababu hawana maliasili za kutosheleza mahitaji yao.

Hivyo unapokuja mgawanyo na kwa sababu Alberta huchangia zaidi wao hupata zaidi vile vile maana kama zilivyoingia hutoka pia kwa Asilimia ni sawa kote zinagawanywa na kwa vigezo tofauti. Na Alberta tokana na mchango wao mgao huu huwatosha kuendesha shughuli za serikali yao hawana haja ya kuwatoza tena wananchi wake kodi nyingine za ndani kama Ontario ambako kutokana na mahitaji yake na pengine hawana vyanzo kama Alberta wameweka kodi zaidi za ndani. Kwa mwananchi anayeishi Alberta atalipa kodi ya mapato Asilimia 5 tu, wakati ukiishi Ontario utalipa kodi ya Asilimia 13 (5+8).

Kwa hiyo sii swala la kujadili hapa Zitto kasema nini na Mbowe kasema nini isipokuwa kinanichoshangaza miye ni kwa nini watu mnashindwa kuelewa kwamba tunayo mikoa, wilaya, majimbo na hatuwezi kuendelea pasipo kufanya kuhakikisha kuwa hizi ndizo huleta tofauti baina ya Mtu na mtu, jimbo kwa jimbo na mkoa kwa mkoa. na ndivyo tutakavyoweza kuzijua tofauti baina ya kiongozi mmoja kwenda mwingine lakini kama leo mimi nifanye kazi kwa bidii na kuzaliisha zaidi lakini kesho nanyimwa uwezo wa kuzalisha zaidi tumefanya nini. Ebu fikiria hivi unafanya vizuri darasani lakini marks zako huchukuliwa na kupewa mtu mwingine, Nguruvi akigundua haya atatumia lugha gani kuyasema wazi.

Kwa nini imefikia watu kumponda Zitto kwa kauli ambayo haina tofauti kabisa na ile ya Mbowe kwa kufikiria vile vile ikiwa sio fikra za uadui baina ya Chadema na ACT maanake mkumbuke tuna vyama 23 na hakunamalalamiko haya zaidi ya yale yalotoka Chadema tu. Binafsi kisiasa sioni tatizo kwa mwanasiasa yeyote kumponda/kumsifia JK sii kwa sababu ni Mkwere bali kwa sababu ya uongozi wake na wala hainamaana ukizungumzia Bagamoyo vs Kigoma basi ina maana ni juu ya Wakwere vs Wabembe au Wamanyema.

I think sisi wenyewe ndio tuko screwed up na hizi idea za Ukabila na Udini kiasi kwamba tunaufanya pasipo kujijua wenyewe. Unaposhinikiza maneno ya Zitto kuwa ya Kikabiila na ukaacha ya Mbowe alosema Wasukuma wako nyuma pasipo kufikiria yeye anayesema haya ni Kabila kgani basi hutakuwa umemtendea haki Zitto. kama Mbowe angekuwa msukuma asingesema aloyasema bali angesema sisi Wasukuma blaablaa blaaa.. NENO NYINYI tayari linamuondoa yeye katika kundi hilo. Ni Ukabila pia kama tutatazama kwa jicho lile lile mlomtazama Zitto.
Mkandara kuna jambo ambalo labda sikuliweka sawa kwenye hoja yangu ya mwanzoni.
KLM imetajwa kama mkoa ambao unamchango mdogo kwenye GDP lakin ukawa na maendeleo makubwa sana.............mind you huu ndio mkoa ambao kweli mchango wake kwenye GDP ni mdogo sana wkasabb kwanza hauna viwanda, kilimo sio cha biashara zaid ya subsistance, ukame/mafuriko huathiri sehem kubwa ya mkoa, kibiashara bado biashara zake sio kubwa kwani mzunguko wa hela na mwingiliano wa watu ni mdogo zadi.............ufugaji ndo kabisa huu mkoa hauwez kufuga zaid ya kufuga kwa ndani ambako ni kwaajili ya chakula cha familia tu...........

tatizo linakuja kwenye huu mkoa kuwa na manedeleo makubwa zaid kuliko mikoa mingine mie ndipo nikasema huu mkoa uko ivo kwasabb watu wake wengi hasa vijana wametoka leo hii ukienda hukuti vijana huko wako mijini kwenye mikoa tofauti kutafuta maisha na wanaporudi nyumban huwekeza wako kama vile ujenzi wa mahosp, mashule, barabara na miundo mbinu ya maji achilia mbali ujenzi wanyumba bora za kisasa.
Mkandara mie sidhan kwamba hata huu mkoa inabidi uwe ni point of discussion kwan tunawajua wachagga leo hii ukienda sehem kama machame lami iliyojengwa na mjeruman kwa kuchangisha wanachi ndo inabomolewa na kujengwa ingine ambayo kila household imetoa mchango wa sh 40000/=kuijenga................ni km kama 20 tu lakn kila familia imetoa huo mchango. wengine wakijenga shule za kata kwa kulumbana KLM walionyesha mfano kwa kujenga kwa kuchanga kwa hiari miskitini na makanisani na risiti wakapewa. Mbona wao wenyewe walichanga kuongeza ubora wa hosp na ukweli baadhi ya hosp zao zikapandishwa madaraja kama vile Kilema hosp na nkwarungo kuwa hosp teule??

Kumbuka kinachobishaniwa hapa ni kwamba kwann wana kasi kubwa ya maendeleo lkn mchango wao kwenye GDP ni mdogo, mie nasema ni kwasabb wao priority yao ni maendeleo yao na sio kitu kingine. Ukiongelea miundo mbinu ya majisafi na salama hadi kwenye vijiji yapo sishangai manake mamlaka husika zilijitahd kuelimisha watu na kila mtu aliona umuhimu wa kuchangia ili aunganishiwe maji na ndivyo ilivyo hali mpaka sasa.

KLM mfano hupata ruzuku kubwa (ambayo pia huwa siamini saana) kwasabb ya kuwa na miradi mingi ya maendeleo ambayo hutokana na nguvu ya wananchi wenyewe. Serikali kwa kuona umuhimu wa miradi hii basi hulazimika kuwaongezea nguvu of which ni jambo jema.

Ilipojengwa lami toka kwasadala hadi masama Rais alipokwenda kuifungua ulimskia akisema kwamba hii ni mali yenu manake mmetoa hela zenu mifukon kuijenga, na serikal iliwaoambea msaada kidogo ili kufanikisha lkn nakumbuka kila familia ilichonga sh 10000/= sjui kama akina Nguruvi3 na @mchambuzi wamewah kufika huko mfano machame watu wakienda kanisan ama mskitin baada aya ibada hupenda kuskia barua za kiutawala (yaani kutoka kweney serikali nk) na hapo huskiliza unahitajka mchango wa nini ili waweze kujiandaa. utashangaaa kumkuta mtu sokoni anaenda kuuza debe la ndizi za kupika mbege lkn ni ili apate elfu moja ya kudunduliza ili alipe mchango unaotakiwa manake anajua anatakiwa kulipa nia sio hiari ni lazima

nafkir badala ya kueneza kuwa KLM inapata ruzuku kubwa mchango wake ni mdogo angeeleza wanafanayaje wao wa klm ili na wo waige mbona wao hatuwaskii wakilalama kuchangishwa sana kweney shughuli za maendeleo?
 
Back
Top Bottom