Nimewasoma nyote na kuja gundua kumbe watu hamuelewi kabisa Zitto alikuwa akizungumzia nini kiasi kwamba ndio maana mkachukua kuwa Shinyanga vs Kilimanjaro. Dadangu tunapozungumzia Umaskini wa Shinyanga haitokani na watu wake yaani WASUKUMA isipokuwa wao kama mkoa wanachangia kiasi gani na wanapewa kiasi gani kwa ajili ya mendeleo yake.
Kwa hiyo hapa kuna tofauti kubwa ya kimaelezo, labda nichukulie mfano mzuri baina yetu, tuseme mathlan wewe unachangia Tsh 20,000,
Nguruvi3, Tsh 30,000, Mimi hapa Tsh 10,000,
Mchambuzi Tsh 40,000 jumla katika mfuko wetu tunazo 100,000 lakini ili kila mmoja wetu ahudumie shughuli za uzalishaji wewe unapewa zaidi ya
nguruvi3 ambaye tunakuja gundua kwamba hali ya maisha yake sio nzuri pamoja na kwamba anazalisha zaid yetu.
Kuna ubaya gani mimi nikimwambia Nguruvi3 kuwa unastahili zaidi ya
gfsonwin na kuelezea sababu iwe uhasama baina yako na mimi wakait unajua kwamba kweli Nguruvi alistahili zaidi. hapa sii kwamba wewe ndiye mwenye matatizo yaani hukutaka ama hupendi Nguruvi3 apewe zaidi yako japo unajua kwamba huzalisha zaidi yako - yale yale ya UMIMI nayakuta hapa. Na rahisi sana kwako kutafuta sababu inayokupendeza wewe kuyaweka maneno yangu vibaya ukajiuliza kichwani mwako mwenyewe consciously - "Okay kwa sababu
Nguruvi3 mwanamme mwenzake ana maana napendelewa kwa sababu? Mwanamke na kama mimi mwanamke huyu Mkandara anadhani mimi napataje upendeleo huu" Hivyo yote haya unayatunga wewe mwenyewe akilini mwako ukauacha ukweli pembeni.
Basically, umeyasema mwenyewe, kumbe hata Kilimo wana KLM hawafanyi kilimo mkoani kwao, wana ardhi ndogo na mengineyo sasa ni sababu zipi ambazo serikali yetu imetumia kama kigezo kuwapa KLM zaidi ya Shinyanga? Na unapotumia neno wanaKLM unanitia shaka vile vile kwa sababu ya kuhofia kilekile ulochomshutumu Zitto - UKABILA..Kwani ewanaShinyanga hawatoki mkoani mwao, hawatafuti riziki zao nje ya Shinyanga? laa kwa nni uweke tofauti hizi.. Kwa hiyo hatuwezi jenga ila kukisiana tuu na hatutapata jibu wala nani mkweli zaidi.
Mimi sioni tatizo kabisa kwa mwanasiasa ku raise swali hilo haswa anapokuwa anatangaza siasa za sera za chama chake kwa maana ya kwamba kama yeye akiingia madarakani atahakikishia kila anayechangia zaidi atanifaika zaidi. na huwezi kutolea mfano mzuri wa jambo hili pasipo kuwa na mifano halisi ambayo kaionesha japo hamkupenda. Je, angeweza vipi ulielezea jambo hili watu wakalielewa pasipo kutumia mikoa ambayo ni sehemu ya nchi ambayo ACT, given the change inataka kuiongoza.
Ndio maana nikawapa mfano ule mdogo wa kwamba wenzetu nchi zilizoendelea, swala kama hili wala sii la kujadiliwa na zaidi ya hapo wala hili sio swala la itikadi wa sera ni Mfumo wa Kitaifa katika uchangiaji na ugawanaji wa mapato hata ikiwa chama gani kimeingia madarakani mfumo huu haubadiliki. Yaani mfano mdogo hapa Canada kila states huchangia asilimia 5 ya kodi zake mfuko wa Taifa. na Alberta ambao wao ni matajiri wa mafuta hawana hata kodi za ndani yaani Provincial tax wakati Ontario mbali na kuchangia asilimia 5 ya mfuko wa Taifa wana kodi yao ya ndani ya asilimia 8 kwa sababu hawana maliasili za kutosheleza mahitaji yao.
Hivyo unapokuja mgawanyo na kwa sababu Alberta huchangia zaidi wao hupata zaidi vile vile maana kama zilivyoingia hutoka pia kwa Asilimia ni sawa kote zinagawanywa na kwa vigezo tofauti. Na Alberta tokana na mchango wao mgao huu huwatosha kuendesha shughuli za serikali yao hawana haja ya kuwatoza tena wananchi wake kodi nyingine za ndani kama Ontario ambako kutokana na mahitaji yake na pengine hawana vyanzo kama Alberta wameweka kodi zaidi za ndani. Kwa mwananchi anayeishi Alberta atalipa kodi ya mapato Asilimia 5 tu, wakati ukiishi Ontario utalipa kodi ya Asilimia 13 (5+8).
Kwa hiyo sii swala la kujadili hapa Zitto kasema nini na Mbowe kasema nini isipokuwa kinanichoshangaza miye ni kwa nini watu mnashindwa kuelewa kwamba tunayo mikoa, wilaya, majimbo na hatuwezi kuendelea pasipo kufanya kuhakikisha kuwa hizi ndizo huleta tofauti baina ya Mtu na mtu, jimbo kwa jimbo na mkoa kwa mkoa. na ndivyo tutakavyoweza kuzijua tofauti baina ya kiongozi mmoja kwenda mwingine lakini kama leo mimi nifanye kazi kwa bidii na kuzaliisha zaidi lakini kesho nanyimwa uwezo wa kuzalisha zaidi tumefanya nini. Ebu fikiria hivi unafanya vizuri darasani lakini marks zako huchukuliwa na kupewa mtu mwingine, Nguruvi akigundua haya atatumia lugha gani kuyasema wazi.
Kwa nini imefikia watu kumponda Zitto kwa kauli ambayo haina tofauti kabisa na ile ya Mbowe kwa kufikiria vile vile ikiwa sio fikra za uadui baina ya Chadema na ACT maanake mkumbuke tuna vyama 23 na hakunamalalamiko haya zaidi ya yale yalotoka Chadema tu. Binafsi kisiasa sioni tatizo kwa mwanasiasa yeyote kumponda/kumsifia JK sii kwa sababu ni Mkwere bali kwa sababu ya uongozi wake na wala hainamaana ukizungumzia Bagamoyo vs Kigoma basi ina maana ni juu ya Wakwere vs Wabembe au Wamanyema.
I think sisi wenyewe ndio tuko screwed up na hizi idea za Ukabila na Udini kiasi kwamba tunaufanya pasipo kujijua wenyewe. Unaposhinikiza maneno ya Zitto kuwa ya Kikabiila na ukaacha ya Mbowe alosema Wasukuma wako nyuma pasipo kufikiria yeye anayesema haya ni Kabila kgani basi hutakuwa umemtendea haki Zitto. kama Mbowe angekuwa msukuma asingesema aloyasema bali angesema sisi Wasukuma blaablaa blaaa.. NENO NYINYI tayari linamuondoa yeye katika kundi hilo. Ni Ukabila pia kama tutatazama kwa jicho lile lile mlomtazama Zitto.