Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
1. Tuseme basi hoja yako ya kodi za mipakani ina mashiko, hivyo we ignore CUSTOMS and EXCISE stats nilizowasilisha awali, how does that change the story?
2. Nimetoa mifano ya texas huko juu lakini nikajibiwa na Ritz kwamba wao wameendelea, kwahiyo tusiwajadili. Sasa kama wameendelea, na sisi tunafanyeje tuendelee kama sio kwa kujifunza kutoka kwa wenzetu walioendelea kupitia sekta ya mafuta na gesi?
Texas leads the US in oil reserves, lakini the major source of revenues in Texas is not oil and gas taxes but sales and use tax, by over 50%. Hoja yangu ya msingi hapa ni kwamba tuache kuwa wavivu wa kufikiri kwa vile tu kuna utajiri wa mafuta na gesi katika mkoa fulani. Tuache kupumbaza wananchi wa Mtwara kwamba wamejaliwa sana kuliko wenzao kwa hiyo walale kwa raha na starehe wasubiri serikali ikusanye kodi from oil and gas na kuwamwagia mapesa, na kuwapa huduma za bure. Mwanasiasa anayewaeleza wananchi hayo ni sumu ya hatari kwa mustakabali wa taifa letu.
Sambamba na kusubiria kodi kutoka oil and gas, wana mtwara sasa wajipange in terms of development of Human Capital ili watoto wao, wajukuu wao na vitukuu vyao waweze faidika kwa maana ya ajira za maana kwenye sekta ya oil and gas, ajira ambazo zitakatwa kodi na kuchangia maendeleo yao sambamba na kodi kutoka katika uzalishaji wa oil and gas. Pia wawe na skills za kuja wawezesha kutumia fursa zilizopo in the oil and gas value chain, kuwa suppliers, contractors n.k. Wana mtwara wana haja ya kujipanga ili oil and gas ivutie real estate development ili mkoa wao uanze kukusanya property taxes nzuri.
Siasa za kuwafanya wana Mtwara wawe na imani kwamba faida ya oil and gas sector will trickle down in the short to medium term, ni siasa hatarishi sana kwa wana mtwara, na taifa kwa ujumla. Wana mtwara wanahitaji viongozi wa kuwasaidia kujipanga ili sekta ya oil and gas itumike kama mbegu ya kupanda kuwafungulia katika maeneo mengine where they also have a comparative advantage over other regions. Pia wawe na fikra ya kuangalia investment opportunities zipo wapi na jinsi gani they can harness local and outside capital kuendelea. Kwa mfano:
1. Kilimo (Korosho)
2. Usafiri wa Anga na Maji.
3. Utalii.
4. Ufugaji nyuki.
5. Viwanda.
6. Pia maeneo ya social and economic infrastructure kama vile elimu, afya, mawasiliano, barabara kwa mtindo wa Build Operate and Transfer, na maeneo mengine mengi.
Mkuu maneno mazito! Watu wakumbuke jimbo lenye mafuta Nigeria ndilo masikini. Na kama mafuta na gesi yangekuwa mwarobaini basi Nigeria isingekuwa hapo ilipo.
Tuliwahi kusema huko nyuma na The Big Show akiwemo kuwa, wananchi wa Mtwara wapiganie faida za gesi si kwa kutaka ibaki bali kwa fursa zitakazopatikana.
Kwasasa Kiwanda cha Dngote kitaajiri watu. Ukiangalia ajira na shughuli za kiuchumi ni kubwa sana kuliko inavyodhaniwa
Wananchi wa Mtwara wajiandae kupokea fursa hizo wakiwa na maandalizi. Mimi ningewashauri wajiandae kwa elimu zaidi.
Kuongezeka kwa uwekezaji kuna kwenda sambamba na huduma za jamii kama elimu na afya.
Endapo hawatakuwa tayari, fursa za elimu na afya zitawafaidsha watu kutoka maeneo mengine na wao watafuata kauli za Zitto tu.
Kilimo mi eneo jingine. Huduma na ongezeko la shughuli za kibiashara na huduma linakwenda sambasamba na huduma za uzalishaji wa chakula n.k. Hapo wanapaswa kuwekeza maana embe wanalouza sh 50 ipo siku wataliuza sh 1000.
Hata hivyo lazima wajiandae kwa hilo vinginevyo fursa zilizopo ni za wote na katika ushindani watakuwa nyuma.
Hoja itakayosimama ni ya Zitto, wananchi wa kanda X wanakuja kuchukua fursa zetu
Uvuvi balo ni eneo la kuangalia. Kutakuwa na ongezeko la walaji tena wa viwango tofauti.
Ni wakati sasa wajiandae kuhakikisha uvuvi wanaoufanya si wa ngalawa tena. Waende mbele zaidi
Kuna investment katika real estate. Watu wanahitaji makazi, je Mtwara wanajiandaa kwa hilo?
Orodha ni ndefu sana, hoja kubwa ni kuwa lazima wajiandae kwa vizazi vyao.
Maandalizi mazuri ni kuwekeza katika elimu, mengine yatafuata. Ni kuangalia fursa zilizopo na jinsi gani wataiztumia. Si kuangalia gesi na mafuta maana Williamson diamond ilikuwepo Shinyanga.
Hao Kilimanjaro na Arusha wanaosemwa na supreme, silaha yao kubwa ni uwekezaji katika elimu
Kwanini umlaumu mwananchi wa Kilimanajaro, Arusha, Kagera n.k. kwa kutumia fursa uliyoshindwa kuitumia hapo ulipo?
Matokeo yake, wanatumia fursa hizo na wanafanya 'remmitance' kwao, wanaendelea.
Supreme anasema, hapana, ni wanyonyaji!
![]()
Hivi tulikuwa tunajadili nini vile...!
kwani uongo si wenyewe kwa wenyewe,CCM ni jina tu,au Chadema ni jina tu,katika hivyo kuna watu ambao ni wanachama na n.k yeye anaeleza mfumo hana aja ya kutaja CHAMA kama unavyotaka,ujui zitto anazidi kupevuka kisiasa,huko amewaachia nyinyi
Mchambuzi:
I think I have answered this. Comparing US States and Tanzanian regions is to compare apple and orange. As I told you in my previous post, US states have full autonomy to enact their own laws and also enforce their own systems of taxation; whereas, Tanzanian regions are the extension of the center government bureaucracy.
Wrong, tax revenues collected by local government authorities are used for operational costs, mainly salaries and allowance of local government employees. Revisit your facts.Take for example the municipal governments in Tanzania. Even in Kilimanjaro and Arusha regions, where people build science labs for their secondary school children, the municipal governments there can't pay their own employees. So the comparison you try to make doesn't make sense at all.
I think you are confused. For those who live in the US will tell you that for the past six years the extraction of oil/gas has spurred economic activities in Texas, South Dakota, Oklahoma, and other states. What's more, the revenues of those states have gone up. So you can't say oil/gas isn't a major source of revenue. For example, after the financial crisis of 2008, many US states are struggling to balance their budgets, but oil/gas states are financially stable and some have experienced budget surplus.
If oil/gas can spur economic activities in Mtwara, why people of that region shouldn't claim the ownership? I believe you are the one who is struggling to think here. It seems to me you can't sustain your own life using your own environment. I don't envy what people of Mtwara, Kilimanjaro, Shinyanga for what they have. Development is all about taking advantage of what's available in your environment.
You say wana-Mtwara wajipange. How could they do that when they don't have any executive position and power to decide their own destiny? Every executive decision is made in Dar Es Salaam and Dodoma with people who have no tie to the region and who have no interest to develop the region.
Zakumi,Nguruvi3:
Any place in Africa where coffee is cultivated, people have experience economic growth. So education isn't a prerequite of development in Kilimanjaro, Kagera, or Mbeya region.
If education is the prerequite, people of Malawi could have experience robust economic growth because they love to go to school there.
If Nyerere, Mengistu, and Mugabe increase literacy rate in their countries to unprecendent levels, however their efforts didn't translate into any economic gain. So education isn't what give the people of Kilimanjaro an edge.
Furthermore, if Arusha was a such developed region, why did they divide it into two regions: Manyara and Arusha?
Mchambuzi, sijui kama Zakumi ni Mtanzania ama la ila matumizi ya Kiingereza katika michango yake katika hii mada yananipa mashaka juu ya uwezo wake ama wa kujielewa au kuelewa wanachosema wengine. Ni kama vile anajaribu kuficha mapungufu yake kwa kivuli cha lugha za watu na katika kufanya hivyo anazidi tu kujichanganya...haeleweki anatetea wala kusimamia nini katika huu mnakasha.
Mchambuzi sina haja ya kurudia yote uliyosema kwa sababu yako wazi kwa kila mtu huru anayeangalia mambo kwa macho yote mawili ila niongezee tu kidogo kuhusu hii ya Zitto kwenda mahakamani....Maswali kwenu:
· Iwapo Zitto asingefukuzwa Chadema, JE angeondoka na kwenda ACT?
· Iwapo itikadi na falsafa ya chadema kwake ilikuwa ni tatizo, kwanini aliendelea kutafuta haki mahakamani, haki ndani ya chama ambacho itikadi na falsafa zake haziendani na ndoto yake?
Msome John Mnyika kiduchu.Mchambuzi sina haja ya kurudia yote uliyosema kwa sababu yako wazi kwa kila mtu huru anayeangalia mambo kwa macho yote mawili ila niongezee tu kidogo kuhusu hii ya Zitto kwenda mahakamani.
Lengo la Zitto toka awali ilikuwa ni moja tu nalo ni kuisambaratisha Chadema, chama pekee kilichotokea kuhatarisha maslahi ya mafisadi ndani ya chama tawala, CCM, waliokiteka. Zitto angeweza kujiondoa Chadema mapema sana baada ya kuona itikadi na falsafa zake ni tatizo na haziendani na ndoto yake. Kwa muda wote Zitto alipokuwa ndani ya Chadema, mgogoro wa kimawazo haukuweza kumpa nafasi ya kuupa ushirikiano uongozi wa Chadema kama ilivyotakiwa.
Chama tawala, CCM, waliweza kugundua toka mapema sana kwamba ndani ya Chadema kuna weakest link kupitia kijana huyo ambaye kiukweli alionesha kipaji cha kujieleza. Kupitia sakata la Buzwagi, CCM iliweza kutumia kipaji chake kumnasa Zitto na baada ya hapo matamko yote aliyokuwa akiyatoa, yalikuwa ni kama vile anaongea kupitia mnong'onezi (prompter) mambo yaliyofurahisha pande zote, akiuma na kupuliza bila kuacha madhara kwa Chadema au chama tawala.
Hali iliendelea hivyo hadi akajenga fikra kichwani kwamba yeye ni zaidi ya Chadema na kuuona uongozi kama unampotezea muda kutimiza ndoto yake kama aliyoaminishwa na CCM. Zitto angeweza kujiondoa Chadema muda mrefu tu lakini hakuwa na uhuru huo, chama tawala bado kilimhitaji katika kufanikisha malengo yao akiwa Chadema. Alitakiwa aondoke muda muafaka ukiwadia Chadema ikiwa imedhoofika kutokana na mgogoro uliopangwa kuukumba.
Juzi amesikika Zitto akidai Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam iliingiliwa baada ya kutupilia mbali kesi aliyokuwa ameifungua dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho. Kwa maana nyingina ni kuwa Zitto alijua na aliamini ataibwaga Chadema mahakamani na swali linalofuatia ni je kama maamuzi yangekuwa tofauti, angeendelea kubaki Chadema? Kama kikulacho ki nguoni mwako?
Zitto kubaki Chadema kungekuwa na maana mbili...kuendeleza kufukuta kwa mgogoro ndani ya Chadema na kusogezwa mbele uzinduzi wa ACT ambao haungewezekana bila ya Zitto. Baada ya kuisambaratisha Chadema ndipo Zitto kwa mbwembwe angeitisha vyombo vya habari na kuitangazia dunia kujiondoa akiiacha Chadema vipande vipande. Kwamba mpango huo haukufanikiwa lilikuwa pigo si kwa Supreme Leader tu bali kwa chama tawala na utabiri wao.
Kama mada inavyosema Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza Upinzani hakuhitajili akili za ziada kuona ripple effect iwapo mpango huu ungefanikiwa. Kwanza swala la Katiba Mpya lingekuwa limezikwa na Katiba ya Chenge ingepita bila pingamizi. Pili UKAWA ingesambaratika kwani mgogogoro ambao ungeikumba Chadema ungetikisa hadi umoja huu na kuuacha nyang'anyang'a. Tatu mwezi wa kumi na moja CCM ingeunda tean serikali, Zitto akiwa ndani.
Ritz, sina hakika kama unafuatilia mada iliyoletwa mezani na kwa nini Zitto tunamlaumu kwa hujuma zake dhidi ya upinzani. Kama angeelekeza lawama zake kunakohusika, mipango ya hovyo ya serikali ya CCM, hatungelalamika kwamba anatumiwa lakini anapofika Shinyanga na kuwaaminisha kuwa matatizo yao yanasababishwa siyo na serikali bali Mikoa mingine, anatuacha hoi. Kwa nini ataje kanda ya Kaskazini bila kuitaja Serikali Kuu ambayo kila siku ndio inahubiri na kujivuna kutekeleza sera za CCM ambazo hasa ndizo kiini cha tatizo na ndizo zimetufikisha hapa tulipo?Wanaukumbi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki kuu ya Tanzania(BOT),Dsm ndio mkoa unaoongoza kwa kuchangia pato la taifa.-1. Dar-es-salaam(GDP-7.5 trilion)2. Mwanza(GDP-4.09 trilion)3. Mbeya(GDP-3.2 trilion)4. Shinyanga5. Iringa6. Morogoro7. Arusha(GDP-2.1 triliom)8. Tanga(GDP-2.09 trillion)9. Kilimanjaro(GDP-2.03 trillion)http://www.thecitizen.co.tz/News/Rev...z/-/index.htmlCha kushangaza ni kuwa mkoa wa Lindi ambao umezungukwa na gesi yenye ujazo wa mabilioni ndio mkoa wa pili kwa umaskini baada ya mkoa wa Pwani.Lakini swali ni je,kwanini arusha haipo hata katika top 3 ya mikoa tajiri yenye kuchangia pato la taifa? Inaonekana makampuni mengi ya utalii yanamilikiwa na wageni au mengi yanatokea katika mkoa wa Dsm.
Ritz, sina hakika kama unafuatilia mada iliyoletwa mezani na kwa nini Zitto tunamlaumu kwa hujuma zake dhidi ya upinzani. Kama angeelekeza lawama zake kunakohusika, mipango ya hovyo ya serikali ya CCM, hatungelalamika kwamba anatumiwa lakini anapofika Shinyanga na kuwaaminisha kuwa matatizo yao yanasababishwa siyo na serikali bali Mikoa mingine, anatuacha hoi. Kwa nini ataje kanda ya Kaskazini bila kuitaja Serikali Kuu ambayo kila siku ndio inahubiri na kujivuna kutekeleza sera za CCM ambazo hasa ndizo kiini cha tatizo na ndizo zimetufikisha hapa tulipo?
Ukimsoma Mnyika, moja kwa moja shutuma zake anazielekeza kwa sera mbovu za CCM zinazotekelezwa na Serikali Kuu na hapo ndipo ninapotofautiana na wewe. Zitto hakutaja kanda ya Kaskazini kwa bahati mbaya bali kwa lengo lile lile la kupandikiza sumu ya kubaguana baina ya wananchi na wananchi. Mkazi wa Shinyanga akitoka kwenye mkutano wa ACT anaamini kabisa kwamba kama si kanda ya Kaskazini, wangeweza kuwa na maendeleo zaidi. Kwa vyovyote vile hapa ni wazi kakosa busara kama isemavyo methali, shimo la ulimi mkono haufutiki...sumu ya neno ni neno.
Mkuu Mag3, kwani unadhani Ritz hatambui hilo! anachokifanya ni spinning tu katika kuhakikisha ima ana 'adulterate' hoja nzito zinazomkabili supreme au anabadili mwelekeo. Tunamsoma tuRitz, sina hakika kama unafuatilia mada iliyoletwa mezani na kwa nini Zitto tunamlaumu kwa hujuma zake dhidi ya upinzani. Kama angeelekeza lawama zake kunakohusika, mipango ya hovyo ya serikali ya CCM, hatungelalamika kwamba anatumiwa lakini anapofika Shinyanga na kuwaaminisha kuwa matatizo yao yanasababishwa siyo na serikali bali Mikoa mingine, anatuacha hoi. Kwa nini ataje kanda ya Kaskazini bila kuitaja Serikali Kuu ambayo kila siku ndio inahubiri na kujivuna kutekeleza sera za CCM ambazo hasa ndizo kiini cha tatizo na ndizo zimetufikisha hapa tulipo?
Ukimsoma Mnyika, moja kwa moja shutuma zake anazielekeza kwa sera mbovu za CCM zinazotekelezwa na Serikali Kuu na hapo ndipo ninapotofautiana na wewe. Zitto hakutaja kanda ya Kaskazini kwa bahati mbaya bali kwa lengo lile lile la kupandikiza sumu ya kubaguana baina ya wananchi na wananchi. Mkazi wa Shinyanga akitoka kwenye mkutano wa ACT anaamini kabisa kwamba kama si kanda ya Kaskazini, wangeweza kuwa na maendeleo zaidi. Kwa vyovyote vile hapa ni wazi kakosa busara kama isemavyo methali, shimo la ulimi mkono haufutiki...sumu ya neno ni neno.