hapana sio kosa la zitto ni kosa la sisi kuelewa, yaani tunarukia mambo pasipo kuyaelewa wala kupima kwanza. Sasa tazama basi wakati zitto alizungumzia hdi kutokana na pato la taifa sisi tukaenda moja kwa moja ktk revenues na gdp wakati ni mchanganuo tofauti kabisa. Kwa kutazama mchango wa shinyanga katika pato la taifa (national income) zitto kaweza kutupa data zinazoonyesha shinyanga wapo chini wakati wanachangia zaidi, hivyo ni msukumo kwa wananchi kuelewa haja ya kufumua mfumo uliopo na kuweka mfumo ulokuwa bora zaidi.
hapo ndipo nilipomba ufafanuzi wako wa swali langu la no.#835 lakini ulinipa web. Ambayo nayo haikunisaidia sana kuona uchangiaji wa pato la taifa unahusiana na nini na maendeleo ya mikoa husika?? Je kinachoangaliwa katika maendeleo ni uchangiaji wa pato la taifa tu au kuna vigezo vingine?
pengine swali la kumuuliza zitto, katika muundo wa act na ujamaa, serikali yake ingeweza vipi kuhakikisha shinyanga wanafaidika zaidi kwa mchango wao maana kumbukeni nchi zote za magharibi majimbo yalochangia zaidi hufaidika zaidi na mchango wao, na majimbo mengine huwezeshwa zaidi ili nao wachangie zaidi ktk miradi inayoongeza productivity na hivyo kukiuza pato la taifa.
Hakuna loser, ndio maana nikamwambia
nguruvi ya kwamba ukiomba ongezeko la mshahara kutokana na uzalishaji wako haina maana unataka mtu mwingine apunguziwe mshahara kwa sababu tu umetaja jina lake kuwa na pato zaidi yako. Au ni kuzua uadui baina yenu hii akili ni ya kibongo tu siku zote tunaogopana. Lakini ni lazima mtu utumie kigezo baina yako na wafanyakazi wengine na ndivyo madai ya wanawake kuhusu mishahara sawa na wanaume haina maana kuwa mshahara wa wanaume utakatwe ili wanawake walipwe..ni kutoelewa tu kwa watu.