Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,149
sasa mbona niliyoyasema ndio haya haya. kwanza nimetofautsha baina ya Tax na Pato la Taifa kwa ujumla wake na imedhihirisha wazi kwamba mimi nilikuwa katika mjadala huu sikutaka kuchukua maneno ya nje. Nikataka kujua Zitto na Mchambuzi wametumia vigezo gani. na kikaweza tenganisha vizuri watu mpate kufahamu kwamba Tax collection sio kitu kizima, we collect taxes toka mapato yote ya ndani na nje lakini hii ni sehemu tu ya fedha zote maana kama wewe mfanya Biashara Ulozalisha billioni 10 na kulipa tax millioni 30 zitahesabiwa zote billioni10 na millioni 30 kama Pato la Taifa. Na mwisho wa siku tumeona kwamba Mchambuzi alitumia tax collection za TRA na Zitto alitumia GDP na HDI maana kumbuka vitu hivi vina mahusiano sana japo tofauti.
kitaalam na kiuchumi penye maskini wengi kuna upungufu wa MTAJI hivyo kuathiri ELIMU, AFYA na UZALISHAJI (Maendeleo) na ndio maana mara nyingi kuna hope ya kwamba nchi maskini yenye ongezeko kubwa la GDP mara nyingi kuna trickle down kuondoa Umaskini wao na Umaskini ukiondoka elimu, Afya, uzalishaji na maisha ya watu huboreka. hii hata iwe katika maisha yetu wenyewe unapopata ajira na mshahara mzuri unaweza kukabiri mahitajhi yako zaidi nakufuta umaskini. Utaweza wapeleka watoto wako shule na hata kuduma bora za Afya na kadhalika, Uzalishaji ukipungua huondoa ajira na hivyo shida kuendelea ama kuongezeka.
Sasa huwezi chukua moja ukalijengea hoja ukasahau kiini chake na ndicho tulichokuwa tukikitafuta. na mimi muda wote nimekuwa nikisema kosa ni la Kimfumo sio Zitto wala nani. na ndio mifano uloitumia hapo chini kunyesha jinsi mfumo mbovu unavyoweza athiri maendeleo ya watu. kama vile wazazi wanaopata mshahara mzuri lakini vipaumbele vyao vikawa Hovyo huwezi kuwalalamikia ndugu walowezeshwa ila wazazi.
Mkandara nilitaka kukuonyesha kuwa takwimu za Mchambuzi zililetwa hapa baada ya wewe kuziomba..Ni hilo tu turudi kwenye hoja.
Ukisoma maelezo ya Nguvuri3, unaona mjadala uliokuwa humu JF na ambao wewe ulishiriki ulizua sintofahamu nyingi, ulileta chuki za wazi, wachaga walidhalilishwa,kejeriuwa, baadhi ya watu walifikiri kuwa wao hawathaminiwi na taifa lao maana kila kitu kinakwenda KLM na nk. Na katika hili KAMA lengo la Zitto lilikuwa si kuchonganisha basi alitakiwa aje elezee alichomaanisha na awaombe watanzania kwa kuzusha uchonganishi miongoni mwao maana halikuwa lengo lake. Tungemuelewa na Tungemsamehe na kusonga mbele, lakini kinyume chake ZItto alikaa kimya akaacha watanzania wakiparuana wenyewe kwa wenyewe na si ajabu moyoni mwake alikuwa anasema "Matanzani majinga tu ona yanavyuparuana yenyewe kwa yenyewe huku akishusha moja moto moja baridi.. Siasa za namna hii ni za "KIITARAHAMWE"
Zitto ni mchumi tena mchumi Tanzania nzima hakuna mchumi kama yeye, Zitto ana akili sana, na Zitto ana siasa za kistaarabu, Sasa basi elimu yake ilishindwa kujua kuwa "uchangiaji wa pato la Taifa hauna usihano wa moja kwa moja na maendeleo ya mikoa husika? Alishindwa kujua kuwa Migodi kutosaidia kuleta vichocheo vya maendeleo si kwa sababu kuna mkoa unaoitwa KLM bali ni uzembe wa Mkapa na serikali yake? mbona wewe umegàmua hilo? Hivi alishindwa kuelewa kuwa umasikini wa Shinyanga hautokani na watu wa Arusha?
Kama swala ilikuwa ni kuongelea mikoa yenye maendeleo/uchangiaji wa pato la Taifa mbona ameiacha Lindi mkoa ambao ni kati ya mikoa inayochangia kwa kiasi kidogo sana katika pato la Taifa lakni ni mkoa wa 9 kimaendeleo? Sikiliza hiyo Video kataja Tabora inachangia pato la Taifa ikiwa ya 10 baada ya hapo kaenda kupanga mikoa yenye maendeleo, katafuta Klm ilipo kaikuta ni 9 kuchangia pato la Taifa kaishiki bango, mbona asitumwambie mkoa wa 10 ni hupi? si kaanzia chini? kwa hiyo utaona hapa alichokuwa anatafuta Kilimanjaro tu si kingine.
Na kama angekuwa anamaanisha kitu kingine angekuwa ameisha ingia humu na kutueleza lengo lake likuwa nini? maana mara ya mwisho kuingia humu ilikuwa jana tu. Haji hapa maana lengo lilikuwa chuki zake kwa watu hawa.
Kama hisingekuwa chuki basi angeanza na Lindi mkoa ambao ni kati ya mikoa inayochangia kwa kiasi kidogo sana katika pato lakni ni ya 9 kimaendeleo.. Na hapa kama mwanasiasa angejiuliza ni kwanini Lindi wanaweza na Tabora, Shinyanga wasiweze hali wanalima pamba, mchele, wana mifungo na nk.
Kwa hiyo tatizo angelikuta kwa wenyeji wa mkoa huu elimu bado ni ndogo sana, pia miundo mbinu ni kikwazo kwa ajiri ya kusafirishaji wa mazao yao, Na sote tunafahamu bila elimu hakuna maendeleo ndo maana dada yangu gfwinson ametueleza kuwa watu wa vijijini wakati mwingine wanapesa kuliko watu wa mjini lakini kutoka na elimu ndogo mtu hafahamu hizo hela hazitumieje. matokeo yake ni kuongezea wanawake, kulewea pombe na nk. Sasa hapa ndipo tunapotegemea viongozi ambao ni wanasiasa kuwaeleza watu muhimu wa kujiletea maendeleo badala ya kuanza kuwachonganisha.
Hebu niambie leo Shinyanga ni maskini lakni wakazi wa vijijini wana mali yenye thamani kubwa kuliko wa watu wa mjini. unakuta mtu wa kijijini ana ardhi kubwa tu, ana mifungo mtu mmoja ana zaidi ya Ng'ombe 1000 mbuzi husiseme, kuku na nk. Hivi huyu mtu ni masikni kweli? au amekosa elimu ya kufahamu vitu alivyonavyo vinaweza kumsaidia kuwa na maisha mazuri kuliko mtu wa mjini. maana anaweza kabisa kujenga nyumba ya kisasa, kuweka solar, kupeleka mtoto wake shule kusaidia shughuli mbali mbali katika eneo analoishi kama kujenga barabara (si lami) kujenga visima,choo na nk. kwa mtaji wa Ng´ombe 500, mbuzi, na kuku pamoja na uuzaji wa maziwa.
Tanzania kama Kilimanjaro wameweza, kama Lindi wameweza nina imani hata mikoa mengine wakipata viongozi ambao wanauchungu na matatizo ya wananchi wao basi wataweza kujiletea maendeleo.
Wanasiasa waache uchonganishi, waache porojo wao ndo wanakomba hazina ya taifa kwa kujilimbikizia mIshahara minono na malulupa yasiokuwa na maana. Kama hiyo mil200 wanazokopeshwa kila mbunge zingepelekwa kwa wakulima, kwa wafugaji, kwa vijana wenye viwanda vidogo vidogo, wakapewa elimu, wakapewa watu wa kuwasimamia, miundo mbinu ikatengenezea basi Tanzania tungepiga hatua tena kubwa tu katika swala zima la maendeleo. Sasa anapojitokeza wanasiasa anayelipwa mamilioni ya shilngi hasiyostahili na akaona hilo halitoshi na kuanza kutuchonganisha huyu HATUTAMPA NAFASI.