Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Ritz,

Shukran sana sasa sina sababu ya kuendelea na ubishi huu baada ya kutazama bandiko lako na Adharusi kuwa sawa kabisa japo Adharusi kachukua vipande vipande. Tazama sehemu nilizo highlight.. Ama kweli nimeamini watu wamepania kumharibia jina kwa sababu wewe umetoa hotuba kamili, Adharusi kazungumzia wapi takwimu zake zinapatikana maana waliuliza Zitto kazipata wapi kwa sababu hawakuamini. sasa wamepewa bado wamekazania kipande ambacho hakipo ktk hotuba yake.. iweje wewe na Adharusi ndio muwe na hotuba lakini hawa jamaa na madai yao hawana hotuba hiyo? Kumbe alicholinganisha Zitto ni mkoa wa Lindi na Shinyanga sio kama walivyodai eeeh...

Hotuba ya zitto uloitoa wewe;-

" Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP. Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba. Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.'

Alichoandika Adharusi:-

Nanukuu maelezo ya Zitto

"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa

Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa,pia akasema Mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.

Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.

" Zitto akasisitiza ndio mana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi,huwezi kuwa na mkoa unashika nafasi ya 4 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namna 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu,Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi,ina Ng'ombe na Pamba.

Tunavita moja tu,kufanya Mapinduzi ya mfumowetu was uchumi kutoka mfumo wa kinyonyaji na kifisadi na kujenga uchumi shirikishi.

Zitto aligusia Takwimu za watu wenye elimu ya sekondari simiyu ni 3.7%, na Dar ni 29% inaongoza nchi mzima(THDR2014)
Mkuu Mkandara.

Hii hotuba ya Zitto ni ulimbo lazima unase kwenye mtego ndiyo maana makamanda hawataki hata kuiona achalia mbali kuisoma.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa Hotuba ya Zitto Shinyanga.. maana hayo aliyoleta Ritz hatufahamu aliyatoa wapi.. Zaidi ya kutwambia alimsikiliza yeye mwenyewe Mwanza..

Pili Kama wewe haukuona alichokuwa kaandika ZItto, na kwa bahati mbaya hatukuweza kukitoa Facebook na kukileta humu ndani haiondoi ukweli kuwa kilicholetwa na adharusi ndicho alichosema na ndicho kilisomwa na watu wengi na kuleta matusi kwa watu wa KLM/Arusha waliopata maendeleo yao kwa nguvu zao wenyewe.

tatu nafikiri hata wewe umeona kosa la Zitto ndo maana unajaribu kutuaminisha/kubadili mjadala kuwa "mnalisha/hakusema.. Na kama umeona hili basi unakubalina na hoja ya Nguvuri3 kuwa Zitto ni mchonganishi.

Na hata kwenye utetezi wenu sikuona mtu wa kumtoa Zitto katika tope aliloingia mwenyewe, zaidi ya mbona hata fulani alisema hivi... au sisi ni wabaguzi ndo maana umechomoa hiyo mikoa na. nk

NNe.. Ukweli ndio huo ukubali au ukatae lakni hicho ndicho alichoandika tarehe 5.4 Hakuna anayeongelea hotuba ya Shinyanga maana hakuna mwenye hotuba ya Shinyanga wala ya Tabora (zaidi ya kipande ambacho kinamuweka katika tope zaidi) na hakuna mwenye hotuba ya Mwanza....

Ushauri:Siku nyingine kabla hujaanza kuandika kitu chochote jaribu kufanya uchunguzi kufahamu kama unachojadili kinahusu nini, kimetoka wapi, na kimetoka kwa nani ni kweli humu mtu akisema hivi na nk.
Bibie kwani nimekataa alichokileta Adharusi? isipokuwa kwa kuelewa kwangu pale aliposema Zitto pia alisema ina maana sio maandishi ya Zitto ila mwandishi mwenyewe kwa jinsi alivyomsikia Zitto. Kwa hiyo mwandishi anaweza kupangilia anavyotaka kwa jinsi anavyokumbuka. na tulipoona Hotuba ya Zitto aloitoa Ritz haioneshi kuwa ni maneno ya mtu mwingine (third party), imejipanga vizuri kabisa kitakwimu ikieleza 1. Mikoa iliyo endelea, 2. Mikoa ilokuwa nyuma, 3. Mikoa inayochangia kidogo na mwisho 4. Mikoa inayochangia zaidi akilinganisha na nafasi zao ktk ngazi nyingine.

Kwa hiyo maadam nimepitwa na hilo na FB basi naomba mniache pembeni maana siwezi kujadili kitu ambacho hatuna ushahidi wake. Nitaweza tu kumsema mtu vibaya ikiwa nitapata ushahidi huo maana nakumbuka nyuma 2010 kuna hotuba ya Dr.Slaa akiwa Kilombero inadaiwa kuwa alisema "Atatoa Elimu bure na shule zote za kata atayakabidhi makanisa yaziendeshe" nikaivamia na kuomba nukuu zake watu wakasema Google, sijui alisema na kadhalika.
 
Kwa hiyo muda wote ulikuwa unajadili nini?
Hakuna aliyekuvuta kuja hapa, umekuja kwa hiyari yako kitu ambacho ni kizuri maana tumejifunza mengi kutoka kwako, na utaondoka kwa hiyari yako.. Hiyo ni haki yako ya msingi...

Pamoja ya hayo naona umekubali kiutuuzima... Kitu ambacho ni kizuri maana tusimuache huyu mtu akaharibu taifa. Tupiganie taifa letu ili kesho na keshokutwa wanao watoke Canada waje wawaone bibi na babu zao kwa amani kabisa bila wasiwasi wowote.

Usiku/Mchana wema tukutane katika mjadala mwengine... kumbuka Siku zote hoja usimama..

Ansate nguvuri3 na wengineo kwa shule yenu sina shaka kuwa tumejifunza mengi, Zitto amejifunza mengi na si Zitto tu bali wanasiasa waliopata bahati ya kuanza na sisi mwanzoni mwa mjadala huu watakubalina nami kuwa watanzania tuko macho, tunawasilikiliza na pale mwanasiasa yeyote akapoleta siasa zake za ukabila au dini hatutasita kumweka kikaangoni. Fanyani siasa zenu tuacheni nchi yetu yenye amani.

Nitabaki msomaji tu...
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna takwimu gani zinazoonyesha TRA kuna wachaga wengi kuliko makabila mengine? Pili kama hawa wanyakyusa wanasifa za kuajiriwa tatizo liko wapi? NI sekta gani hapa nchini unapokwenda ukakuta mlinganyo wa makabila? au dini? na kama kila sekta kuna watu wa kabila fulani wengi kuliko makabila mengine kwanini iwe BIMA tu? Nenda Mamlaka ya Pamba Mwanza kule ni wasukuma tupu tena hata mle ofisi lugha inayotumika ni kisukuma lakini hakuna mtu anayelalamika maana ni watanzani wenzetu, waliajiriwa kutoka na sifa zao si kabila yao sasa hapo tatizo ni nini?
Yaani unataka tufike wakati wa kuajiri tuangalie kabila la mtu si sifa za mtu? Hivi huko kwenye duani ya kwanza unapoishi ndivyo wanavyoajiri kwa kuangalia makabila (hivi wana makabila huko kweli) na kuwa kufanya hivi kweli Tanzania yetu inaweza kupiga hatua kwenda mbele?

(Nje ya topic) NImekuwa nikijiuliza hasa kuwa mchaga ni nani? ni yule mtu mwenye jina la kinyakyusa? au ni yule mtu alizaliwa Kagera na wazazi ambao ni wanyakyusa ila huyu mtu anafahamu kihaya, anaishi mila na desturi za kihaya, hajawahi kwenda unyakyusani zaidi ya kusikia simulizi? au ni yule aliyezaliwa unyakyusani, akajifunza mila na desturi za kinyakyusa, kaongea kinyakyusa ingawaje wazazi wake ni wahaya? Swali langu hapa Myakikyusa ni yupi?? (hili swali ni kwa kila mtu atakayependa kunipa ufafanuzi haliusiani na topiki iliyo mbele yetu)

Mkandara haya nimefuta wachaga na kuandika wanyakyusa kama ulivyotaka.. Je kuna kilichobadilika?

Naomba uonyeshe ungwana na ujibu maswali yangu..
Sana tu..Kwa mtu mwenye UKabila anajua Unyakyusa ni Nini maana Zitto kasema Kilimanjaro na Arusha tayari mkasema kauli yake ina Ukabila ndio maana nawashangaa!..Kwani wana KLM ni akina nani? wana Shinyanga ni kina nani iweje iwe ukabila wakati mikoa hiyo wanaishi watu wa makabila tofauti? Wewe umeweza kuwasema Wasukuma, miye nikatolea mfano Wachaga na Wanyakyusa, Mbowe aliwasema wasukuma sote hatukuwa na Ukabila isipokuwa tunajadili hali zilizopo.
 
Kwa hiyo muda wote ulikuwa unajadili nini?
Hakuna aliyekuvuta kuja hapa, umekuja kwa hiyari yako kitu ambacho ni kizuri maana tumejifunza mengi kutoka kwako, na utaondoka kwa hiyari yako.. Hiyo ni haki yako ya msingi...

Pamoja ya hayo naona umekubali kiutuuzima... Kitu ambacho ni kizuri maana tusimuache huyu mtu akaharibu taifa. Tupiganie taifa letu ili kesho na keshokutwa wanao watoke Canada waje wawaone bibi na babu zao kwa amani kabisa bila wasiwasi wowote.
Ooohooo! bibie mbona waenda mbali vipi? mimi najadili hotuba ya Zitto Shinyanga sijadili mambo ya FB kama ningetaka ningeenda huko huko FB. Kama mnajadili ya FB msiniulize miye tujadili tulonayo mkononi na ushahidi ndio huu. Yalonukuliwa na kuandikwa Pia akasema hii inapotosha mpangilio alosema Zitto maana sio yake, hivyo naamini hotuba aloitoa Ritz kuwa ndio maneno aloyasema Zitto kwa sababu yanalingana na msemaji.
 
Maswali hayajibiwi, Nimeshauliza maswali humu ndani mpaka nimekata tamaa. Sijui kama ili watalijibu ngoja tuwape muda.
Neno kuwezeshwa ina maana serikali inatoa sera na kujenga miundombinu inayowezesha ufunguzi wa miradi ya kukuza Uzalishaji. Kwa mfano, kama leo Kikwete atajenga bandari na Uwanja wa ndege Bagamoyo, ameuwezesha mkoa wa Pwani katika uzalishaji wa ajira na pato la Taifa maana miradi mingine itafunguliwa hapo kutokana na kuwepo tu Bandari na Uwanja wa ndege iwe Mahotel, maduka, nyumba za kupanga n.k.

Kazi kubwa ya serikali ni sera na Ujenzi wa miundombinu ambayo inawezasha uwekezaji katika jimbo, kwa mfano Mnyika kaomba mradi wa maji Ubungo hadi anaondoka bungeni ameshindwa kupewa jimbo kwake. Ubungo hawakuwezeshwa kupata maji hivyo maendeleo yake yamepwaya kutokana na kwamba sii rahisi viwanda kufunguliwa pasipo maji. Utakuta viwanda vingine vinakufa ama wanachimba visima vya maji jambo ambalo linaweza kuzua Ukame sehemu hiyo miti isiote. Wananchi watafikiria mara mbili kujenga Ubungo kwa sababu ya Maji. Hao CCM wenyewe wanashindwa kuhamia Dodoma kwa sababu hakuna maji ya kutosha.

Na ndio maana sisi wengine tunasubiri kujua sera za vyama vinavyogombea kuongoza 2015, na ili kupambana na Umaskini lazima chama kionyeshe kiwawezeshaje mapambano haya maana raia ni askari tu wanaohitaji mitutu wakapigane. serikali haitaingia vitani bali huwezesha mafanikio ya vita hiyo. Mfano mdogo sana ni kwamba wewe huwezi jenga nyumba pasipo kibali cha kumiliki kiwanja, ramani na kadhalika ukikwamishwa na serikali ndio imetoka - Huna nyumba!.
 
Kwa hiyo muda wote ulikuwa unajadili nini?
Hakuna aliyekuvuta kuja hapa, umekuja kwa hiyari yako kitu ambacho ni kizuri maana tumejifunza mengi kutoka kwako, na utaondoka kwa hiyari yako.. Hiyo ni haki yako ya msingi...

Pamoja ya hayo naona umekubali kiutuuzima... Kitu ambacho ni kizuri maana tusimuache huyu mtu akaharibu taifa. Tupiganie taifa letu ili kesho na keshokutwa wanao watoke Canada waje wawaone bibi na babu zao kwa amani kabisa bila wasiwasi wowote.

Usiku/Mchana wema tukutane katika mjadala mwengine... kumbuka Siku zote hoja usimama..

Ansate nguvuri3 na wengineo kwa shule yenu sina shaka kuwa tumejifunza mengi, Zitto amejifunza mengi na si Zitto tu bali wanasiasa waliopata bahati ya kuanza na sisi mwanzoni mwa mjadala huu watakubalina nami kuwa watanzania tuko macho, tunawasilikiliza na pale mwanasiasa yeyote akapoleta siasa zake za ukabila au dini hatutasita kumweka kikaangoni. Fanyani siasa zenu tuacheni nchi yetu yenye amani.

Nitabaki msomaji tu...
Muda wote alikuwa hajui anajadili nini.
Ushahidi upo wazi, kwamba alikuwa na htuba ya Zitto iliyosema ''Kilimanjaro wanachangia kidogo wanapata stahiki, Shinyanga wanachangi zaidi hawapati stahiki''

Hiyo ndiyo hotuba ambayo Mkandara anayo peke yake na hataki kuijadili

Ile ya Adharusi ilipowekwa, Mkandara akajua Zitto kasema nini. Ukisoma hotuba zote mbili kuna maneno uameondolewa.
Nitakuonyesha, sasa Mkandara hajui atumie ipi, ya kwake, aliyotunga, ya Adharusi inayodhaniwa au ya kuumba anayotumia.

Kwakweli inafiki mahali inashangaza sana. Umma wote bila kujali itikadi unaalaani kauli za kichochezi, kichonganishi, chuki za Zitto. Mkandara anataka kufanya hilo kama halali. Tume m-quote mara nyingi kumuonyesha flip dlop, mkuu haelewi

Ukabila tumemuonyesha wake na si wa Zitto peke yake.
Hawa watu wamepania sana na vita yao dhidi ya mikoa ya kaskazini itakuwa mbaya.

Supreme atoke asahihishe makosa yaliyolenga kulivuruga taifa hili
Huyu mtu ni hatari sana, soma maoni ya watu uione walivyojaa chuki wenyewe kwa wenyewe na Zitto na watu

Kisiasa hili jambo linamuumiza sana, ataishi nalo katika maisha ya kisiasa.

Linaumiza chama chake kwasababu vita yao dhidi ya kanda sasa inachukua mkondo wa vita ya kisiasa ya ACT ikiongozwa na Zitto dhidi ya wananchi wasio na hatia wa kanda zingine.

Wananchi hawana hatia kwasababu hawapangi shughuli za maendeleo. Wanajiletea maendeleo kwa jitihada zao

Leo inapofikia mahali ACT/Zitto wanapita mbarabarani wakiwasumanga, wakiwatupia kauli kali kama za Zitto, ni jambo la kutisha

Muhimu, Zitto atuachie taifa letu lenye upendo na mshakamano.

Hatutakaa kimya hata siku moja akitumbukiza chuki bila sababu.

Ugomvi wake wa kisiasa usiingie katika taifa na utaifa.

Hatudhani wananchi wana chuki, na wote tutasimama bila kujali itikadi zetu za ina yoyote kumkemea, kumuonya aache siasa za uchochezi, uchonganishi na unafiki. Matatizo yake ya kisiasa ayamalize bila kushirikisha mkoa, kanda au taifa

Tutamkemea bila haya wala soni. Tunaamini katika taifa na si mtu au watu.
 
My take

Kwanza ni ngumu sana kukujibu kwa vile umekiri hoja zako zinatoka facebook ya Zitto.

Huko fb tunakuachia na pengine utupe nafasi kwavile hatufiki maeneo yako. Hoja zako zinajieleza wazi ni za kifb.

Ukisoma maelezo ya Zitto hapo juu, bila kujali alisema nini katika mkutano, bila kujali ana takwimu gani, tayari umeshamtia matatani na unazidi kuueleza umma kuhusu uhuni, uchochezi na uongo wa supreme. Yaani unamwanika hasa.

1 Huwezi kuweka asilimia ukasema ni data bila kutueleza zimepatikana kwa kuangalia nini

Kuna vitu vingi sana umeshindwa kujua havipo, na supreme alijua watu wa aina yako huko fb hawawezi kuona.
Wala sitajaribu kukueleza maana nitakuwa nakutwisha mzigo mzito.

2 Soma maelezo yako ambayo unasema ni ya supreme.
Hivi kuna uhusiano gani kati ya uchangiaji wa pato la taifa, umasikini na maendeleo ya mikoa ya Shinyanga, Kilimanjaro na Arusha?

Kama Arusha ni wa 7 na K’njaro ni wa 9, kipi kilikuwa bora, kulinganisha Shinyanga na namba 1 hadi 6 au kulinganisha Shinyanga na namba 7na 9. Kuna motive gani ya kuruka mikoa iliyotangulia kimaendeleo zaidi ya Kilimanjaro na Arusha?

Tatu, Kwa maneno yako, supreme alikuwa na maana gani aliposema ‘kujenga uchumi shirikishi?
Alimaanisha nani anamyonya nani na kwanini suluhu iwe shirikishi. Wapi kuna ombwe la shirikishi.

Nadhani unaona jinsi unavyozidi kuleta ushahidi kuhusu kauli za supreme za uchochezi, kuligawa taifa na shambulio kali la kisiasa dhidi ya mikoa miwili ya K’njaro na Arusha

Kwakweli kama ni wakili, basi utakuwa umemsaidia mwendesha mashtaka kumtia hatiani supreme.
Huko fb endeleeni, mkija huku mnamtafutia matatizo.

Soma tena maneno yake mwenyewe uliyomnukuu hapo juuhalafu fikiria mtu mwenye akili timamu atafikia conclusion gani.
Ni mbaya sana ndugu yangu, umemtia pabaya bora ungekaakimya! Rejea fb na ahsante sana kwa kushiriki nasi
Tuweke kumbukumbu sawa Alinda akikuletea habari za Facebook unazikubali lakini hapa huatakia hata kusikia habari za Facebook.

Mkuu Mkandara msome Nguruvi3 kiduchu na Habari za Facebook.

Kweli huuu mpini!
 
Last edited by a moderator:
Huki face mnapajua wenyewe. Ameeleza hivyo katika face, je ndivyo alivyosema katika mkutano? Kama anajisafisha sisi tuamini tu kama mazuzu

Usibebe kitu bila tafakuri ni hatari sana

Nguruvi3.

Mbona mnajichanganya wenyewe Alinda anasema toka tarehe 5 mnajadili kauli ya Zitto kutoka Facebook.

Wewe hapa kwa kauli yako unapakana tena Facebook.

Cc: Mkandara.
 
Last edited by a moderator:
Kuna uwezekano katoa clarification huko face book

Mkandara atakuwa shahidi mzuri tu kwasababu kuanzia jukwa lasiasa hadi hapa, yeye ni kinara wa hoja husika.

Msome hapo juu, ‘’ Shinyanga inachangia Zaidi haipati stahiki, Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki’’

Mwenzako team Adharusi kaja na data kabisa

Nashangaa hukuona hayo yote. All in all,tunajua alifanya shambulio la kisiasa dhidi ya mikoa ya kaskazini
Baada ya kuweka hotuba ya Zitto ukumbini Supreme Leader Nguruvi3 akajibu hivi lakini Alinda akitoa habari Facebook anameza tu daah!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu toa hotuba aliyotoa kule kwa wasukuma, achana na hotuba za facebook na redioni.
Hapa tena Facebook haitakiwi lakini Alinda akileta habari za Facebook hewalaa!!!. Nguruvi3 mimi nipo sijakimbia naenda mara moja Facebook kuangalia twits za Zitto tarudi ukumbini nikipata wasaa.

Cc; Mkandara
 
Last edited by a moderator:
Ritz na Mkandara asanteni sana kwa kuutendea haki mjadala huu. Mmeifanya jamii ijue kuwa kuna watu wako tayari kutumia majukwaa huru ya mitandao kudanganya Umma.

Ritz amefanikiwa kutuonyesha rangi halisi ya Nguruvi3 kwamba yuko tayari kujikana mwenyewe ili kushinda mijadala kwa mfano, yuko biased, kama kuna habari ya Facebook ina chembechembe za kumsaidia kushinda mjadala, hiyo anaikubali. Ila kama haimsaidii ktk azma hiyo basi anaikataa. Ushahidi ni hizo Quotes alizoziweka Ritz akinukuu flipflops za Nguruvi3
 
Mjadala haukuhusu nani ameshinda nani ameshindwa.

Ndio maana Mag3 alikueleza usome kwanza nini wenzako wamejadili kabla ya kuchangia.

Hatima ya taifa hili haiwezi kuwekwa mbele ya masilahi binafasi ya mtu au genge la wahuni.

Na wala hatutakaa kimya taifa likifinyangwa na kugawanywa kwa hoja muflisi za kisiasa. Kauli za Zitto zakuvuruga taifa.

Supreme leader hawezi kurudia maneno ya uchochezi. Mnachokifanya ni kufariji nafsi zenu baada ya umma kumkalia kooni kutokana na kauli zisizo na kipimo, zenye uchonganishi na zilizolenga kugawa jamii

Vita alivyotangaza na kanda ya kasakazini ataishinayo.

Tunasubiri kusikia atawaambia nini wananchi wa Mtwara,Singida na Sumbawanga kuhusu hali zao.

Atawaambia nini wananchi wa Morogoro naIringa kuhusu hatma yao.

Vita ya ACT/Zitto si ya kanda, ni pana zaidi. Sijui kama wananchi wanaridhika na kauli za mikoa fulani kunyonya mingine.

Kama Shinyanga inanyonywa na Kilimanjaro na Arusha, mkoa waMara, atasema nini.

Kisiasa, kilichofanyika ni ‘disfranchise'' kwamba kupitia matamko ya supreme, ameumiza chama chake vilivyo.

Hakuna anayetarajia kuwa kiongozi, akiwa ametenga wapigakura.

Wananchi waliokasirishwa na kauli zake, bila shaka watamwangalia kwa jicho la ghadhabu.

Hao ni Watanzania wote waliosambaa kutoka eneo moja hadi jingine

Ni vema, mngemshauri atoke na kuisafisha nafasi,kukisaidiachama chake.

Kwa mwendo huu wa mijadala na utetezi usiozingatia hoja,safari itakuwa ngumu kuliko

Katika bandiko tumeeleza makundi 3, la kwanza halioni wala halisikii

Tulisema, supreme anakabiliwa na mambo kadhaa kuhusu mustakabali wake

1 Kwamba, amekosa public trust
2 kwamba, kauli zake zitaangaliwa na wale wenye mashaka wakundi la 3

Kwa kauli ya supreme dhidi ya uchonganishi wa mikoa, ni dhahiri tuliyomuonya yanatimia.

Hakuna mwenye shaka tena kuhusu azma na ni yake.

Kilichobaki ni kuona shoka litakata wapi baada ya kupata mpini.

Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
Ritz na Mkandara asanteni sana kwa kuutendea haki mjadala huu. Mmeifanya jamii ijue kuwa kuna watu wako tayari kutumia majukwaa huru ya mitandao kudanganya Umma.

Ritz amefanikiwa kutuonyesha rangi halisi ya Nguruvi3 kwamba yuko tayari kujikana mwenyewe ili kushinda mijadala kwa mfano, yuko biased, kama kuna habari ya Facebook ina chembechembe za kumsaidia kushinda mjadala, hiyo anaikubali. Ila kama haimsaidii ktk azma hiyo basi anaikataa. Ushahidi ni hizo Quotes alizoziweka Ritz akinukuu flipflops za Nguruvi3
Mkuu wangu hawa jamaa viumbe wa ajabu wapo kama vinyonga wanabadlika kutokana na mazingira, ndiyo maana Supreme Leader Nguruvi3 anawambia wafuasi wake wanipuuze anajua nawaharibia mipango yao.

Sasa hivi kageuka kuwa msemaji wa Watanzania sijui hayo mamlaka kayatoa wapi mkuu chunguza sana Supreme Leader Nguruvi3 wa ili jukwaa ana wafuasi wake ukimgusa tu wote wanakuvamia.

Mimi namjua sana huyu jamaa tumefanya naye minakasha mingi tu alichobakisha sasa hivi ni kurusha ngumi hewani na kujifariji.

Watanzania siyo wapuuzi kushikiwa akili wanapima mambo na wenyewe ndiyo wanaamua wafanye nini siyo Supreme Leader wa ili jukwaa Nguruvi3 na wenzake wanataka nini.
 
Last edited by a moderator:
Nawaomba radhi wanajamvi kwa kusoma hayo.

Kwa kawaida duru tuna utulivu, yanapotokea kama haya tunavumiliana.

Kuna nyakati wanadamu wanaghafilikiwa, wajibu wetu si hamaki wala taharuki ni kuangalia wapi kuna mghafala.

Nawaomba asiwepo yoyote atakayetaharuki au kujibu kauli hizo.

Mkuu Mkandara, tunakuombea kwa mola akujaze hekma na busara, akupe utulivu na subra katika kipindi hiki kigumu cha majadiliano.

Nguruvi3,

Wabondei wana usemo mmoja '' Sizaki kuona nguku akakoza '' wakiwa na maana kuwa hawajawahi kumuona kuku anajisaidia haja ndogo (anakojoa).

Hii mada mnayoijadili ina vichwa vikuu viwili au watu wana ueleo na kuijibu kwa majibu ya aina mbili kwani imejikikita hivi
1. Je mikoa inayochangia zaidi katika Pato la Taifa ni laazima ipewe kipaumbele zaidi katika maendeleo yake?
2. Zitto anaamini kuwa kuna baadhwi ya mikoa kuidhulumu mikoa mingine kiuchumi au kwa kifupi anabainisha kuwa kuna upendeleo wa wazi wa Serikali kuipendelea baadhwi ya mikoa japo inachangia pato dogo kwa Taifa na kuikandamiza mingine.

Nawashauri ili msichanganye mada ni vizuri kuzitofautisha kimtazamo na kujipambanua wazi kabisa nini mnachotaka ili nasisi wengine tuchangia kwa kina.

Kwani hata mimi nilichangia hapo awali kwa mtazamo wa namba moja hapo juu lakin nikiendelea kusoma zaidi naona kuna mkanganyiko na mwisho mnafikia kuhamakiana.

Tuweke wazi mwelekeo wa mada yako ni upi kati ya hizo juu.

Ahsantum

Shukran mkuu nadhani ndipo tunapopingana katika haya maana wapo wanaoamini la kwanza na wapo wanaochukua la pili lakini habari yote hii inatokana na Hotuba ya Zitto aidha kama aliandika Facebook ilikuwa baada ya Hotuba au tuseme kabla jambo ambalo sisi wengine hatukujaliwa kulisoma huko FB.

Mimi natazama maelezo ya hapa JF maana tupo ktk mjadala na vyanzo tunavyopewa ni hivi hapa yaani bandiko la Adharusi na Ritz ndio kichecheo cha mjadala huu hadi tumepata takwimu za kila aina na zimetusaidia sana. Mimi niliposoma habari zote mbili nikaona zinafanana sana, moja inaonyesha ni maneno ya Zitto mwenyewe na nyingine inaonyesha kuwa Adharusi anamnukuu Zitto katika hotuba yake hivyo sio lazima hotuba ilikuwa vile isipokuwa kile anachokumbuka na ndio maana kaweka neno Zitto pia akasema..ktk kujibu hoja aloulizwa.Hii ni kawaida kabisa ya uandishi kuchukua sehemu muhimu za Hotuba na kuzisherehesha na hoja sio lazima aindike hotuba nzima. Na ukitazama tofauti baina ya Adharusi na Ritz, utaona kwamba mikoa mingine ilotajwa na Zitto Adharusi hakuiweka kwa sababu haihusiani na hoja ilotangulia kuuuliza zile takwimu Zitto kazitoa wapi? ndipo alipoiweka Hotuba kwa kuzingatia takwimu kazipata wapi. Wakati Ritz kajibu swali la watu ambao walitaka Hotuba ya Zitto akiwa Shinyanga na akaiweka. Kwa msomaji mwelewa ataelewa tofauti hizi pasipo kuumiza kichwa.

Mimi binafsi kutokana na Hotuba hiyo, sidhani kuwa Zitto alikuwa na maana Mkoa unaochangia zaidi mfuko wa Taifa upewe kipaumbele zaidi, ila Kiuchumi mkoa unaochangia zaidi pato la Taifa hautakiwi kuwa mkoa maskini kuna makosa makubwa hapa yanafanyika. Ni sawa kabisa na Tanzania yenye maliaasili na rasilimali kubwa kuliko nchi nyingi Afrika lakini bado ni nchi maskini kuliko hata zisizokuwa na Utajiri kama Ethiopia na hakuna visingizio nje ya Utawala ni lazima Umaskini huu utokane na vitu viwili tu - SIASA CHAFU na UONGOZI MBAYA hivyo kuonyesha kuna uwezo mdogo wa CCM kuleta mageuzi ya Maendeleo.

Na tukiendekeza habari hizi za siasa chafu tukasahau haswa lengo la Zitto ni kuonyesha Ubovu wa mfumo mzima tulonao, mfumo ambao sisi tunapewa tu na nchi za magharibi ktk miradi ya IMF pasipo kuzingatia hali halisi ya nchi yetu, Tanzania itaendelea kuwa maskini miaka nenda miaka rudi maana wao IMF na WB wanataka nchi kama zetu ziendelee kuwa Taifa tegemezi. Na ndio maana ya mfumo wa Kibepari sisi wengine tunaishi maisha haya na madeni kila siku ya Mungu.

Tunatumikishwa kulipia madeni ya Credit card na mikopo hivyio tunaishi maisha ya kusadikika. Ni wajibu wetu sisi Watanzania wenyewe kutambua unyonge wetu, kutambua interest zetu pasipo kupangiwa maisha kwa kuelewa tunataka taifa la aina gani. Hii kuwaamini wazungu na IMF ndio athari kubwa inayotawala uozo tulokuwa nao kwa sababu viongozi wetu wenyewe ni reflection yetu. Tusipojiamini wenyewe tumekwisha.

Kutegemea misaada huja na masharti, huja na kupangiwa mipango ya biashara na Uchumi sasa kuna haja gani ya kusomesha watoto wetu? tunasomesha watoto wetu ili wawe kina nani kesho? leo hii tunaamini na kuajiri Wakenya kuwa wafanyakazi wazuri kuliko sisi kwa sababu wanazungumza Kiingereza! Kwa nini Viongozi wasiamini wazungu wataweza kutupangia Mikakati ya Uchumi japo kwa interest zao.

Kama tutawajaza wananchi fikra za UKABILA na UDINI kwa sababu za kisiasa ndani ina maana tutapoteza dira zaidi kwa kuwajaza wananchi Ukabila na Udini. Mada hii inalengo la kuwajaza ujinga wananchi sio kutafuta ukweli ili waamini kwamba Umaskini wetu ni wa kujitakia maana Shinyanga wana ng'ombe, Pamba na sijui Dhahabu kwa nini wawe maskini?.anawashangaa wa Shinyanga!. Halafu mtu huyo huyo utamkuta akisema Tanzania tuna maziwa mengi, ardhi yenye rutuba, madini, vito na kadhalika kwa nini bado maskini? hapo atakuwa na jibu tofauti kabisa...Hajishangai yeye mwenyewe!

Mimi nawaomba tuondokane na hizi siasa za majitaka, Zitto mlomkataa kisha ondoka na kisha anza maisha mapya. ACT ni uzao wa Chadema chama kilichoendekeza siasa za majitaka wakasahau kwamba wana muda mfupi sana kufikia Uchaguzi wa mwaka 2015, hivyo wakaona bora chama kuliko kutafuta Ushindi. Sasa Zitto kawakalia kooni kwa maamuzi yao wenyewe wanashindwa hata kuishambulia CCM wakati imebakia miezi 4 tu kufikia Uchaguzi mkuu.

- What a waste!
 
Mkuu Mkandara , kwanza tuweke rekodi sawa

Hotuba aliyoweka Ritz si ya Shinyanga kwa mujibu wake, ni ya viwanja vya furahisha(ushahidi upo yeye mwenyewe kusema) na si Shinyanga kama unavyodai

Pili, huwezi kuchukua hotuba mbili zikawa na takwimu zisizo na ulinagnifu, na baadhi ya maneno kunyofolewa ukadai ni maelezo sahihi ya mhusika. Ndio maana tulipomuuliza Adharusi maswali yanayotokana na hotuba ile ile aliyoleta hakuweza kuandika mstari hata mmoja.

Tatu, hotuba unayosema, si kweli yeye amechukua kutoka kwa Adharusi akabadilisha maneno.
Tena amekushirikisha wewe kumshukuru Adharusi. Hiyo ilikuwa tarehe 13 May.

Wiki iliyofuata akaja na kauli kuwa amesikia mwenyewe radio Afrika.
Ina maana alisikia hotuba kwanza, hakuelewa, hadi pale aAdharusi alipoileta. Huoni uumbaji wa maneno hapo?

Hoja hapa ni kuwa kauli iliyoamsha hisia kali katika jamii si ile ya Zitto, ni zile zilizosika na umma ambazo wewe umechangia sana. Inashangaza ulikuwa unachangia kitu usichokijua na hapa kuna question mark kuhusu michango yako

Nne, kuna hotuba yako iliyosema 'Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki, Shinyanga inachangia sana haipati stahiki''
Hili nalo linaongeza mchanganyiko kwa wale wanaotaka kumuwekea Zitto maneno badala ya yale aliyosema

Tano, video ya Tabora inaonyesha Zitto akizungumza na alipoanza Kilmanjaro ilikatwa.
Hii inatia shaka sana nini kilifuata baada ya kutaja Kilimanjaro

Sita, kama ilibidi kutumia mifano, bado mikoa 1-6 kwa maendeleo ingekuwa imepewa nafasi zaidi kuliko 7 na 9.
Hivyo kuichagua mikoa fulani katika mfano ilikuwa delibarate kwa ku target mikoa hiyo katika kuonyesha 'maliciuous intent' ya Zitto dhidi ya mikoa hiyo

Saba, kama uchangiaji unaambatana na maendeleo, vipi Lindi inayochangia kidogo kabisa iwe katika nafasi ya 10?
Mfano upi ungekuwa mzuri, Kilimanjaro inayochangia katika top 10 au Lindi isiyoonekana.

Nane, maendeleo yanahusiana vipi na uchangiaji wa pato la taifa

Tisa, Je, historia, mazingira ya kiuchumi yana nafasi gani katika maendeleo ya eneo husika?

Kumi, Ni utarataibu gani unaoweza kutumika kupendelea mikoa fulani katika serikali ya nchi moja kama Tanzania ikiwa Zitto alikuwa sehemu ya serikali hiyo na hakuweza kulizungumzia hilo akiwa mbunge?

Na mwisho, hatujui una maana gani unaposema Zitto kawakalia kooni.

Kama kusumanga mikoa ni njia muafaka kisiasa basi anachokifanya ni 'political sucide'

Kwa mfano, leo akisimama mikoa ya kaskazini, lazima atawajibika kuwaambia, wanapendelewa vipi, wanaonea wenzao vipi

Kama kukalia kooni ni kufanya 'disfranchise' Zitto atakuwa amefanikiwa kwasababu hatudhani Lindi watasimama naye kwa kuzingatia Mchango wao kidogo, lakini wapo juu kwa maendeleo.

Hii maana yake ni kuwa Zitto atawajibika kuwaambia katika mfumo wa ACT nini wanatakiwa wafanye la sivyo, wanachopata sasa kitakwenda kunakostahiki

Na pia itabidi aende Morogoro na Dodoma akawaeleza kuhusu hali zao

Ukiangalia kwa picha pana, supreme leader atakuwa amekalia mikoa ya kaskazini kooni, lakini hoja zake zitamkalia kooni

Itakuwa ngumu sana kueleweka kwa wananchi waliosambaa nchi nzima.

Kama anadhani kooni ni kaskazini basi ni mkakati mbaya si kwake tu bali kwa chama chake
 
Ama kweli wachekeshaji sio lazima wapewe kipaza sauti na ukumbi wa kuchekesha… Yaani tulikoanzia Mada ilikuwa ACT mpini wa CCM, ikiwa kosa ni Zitto kafukuzwa na kujiunga na ACT ni Msaliti Ushahidi hawana.

Zitto Supreme Leader ndiye kaanzisha ACT wakati akiwa bado Chadema –Ushahidi hawana. Oooh kapanda madaraka haraka sana haya tukawapa mfano wa Dr.Slaa alohama CCM na kuingia Chadema akiwa bado na kadi ya CCM na kupewa madaraka haraka toka mbunge hadi makamu mwenyekiti wakapinga. Tukawapa Ushahidi wakameza mate ya uchungu.

Wakaja na jingine kuwa Dr. Slaa alishinda kura za wanachama wa CCM katika uchaguzi wa mgombea wa Karatu. Nikawajibu kuwa hapakuwa na kitu kama hicho wakabisha wee bila ushahidi mara ghafla uchungu wa mimba wakageuza game kuwa Zitto kasema haya..

By Mkandara
Mimi naamini na nitaendelea kuamini kwamba Zitto ni mpinzani mkubwa wa mfumo wa Fisi uliopo. na anapigwa vita na CCM, Chadema na vyama vingi vyenye wenyewe kwa sababu Uongozi wa chama na taifa ni utajirisho mkubwa kwao na Zitto ameonekana kuwa mwiba kuwapinga sana iwe ktk Ufisadi, Rushwa, Kujilimbikiza mali kupitia Ubunge, uwaziri na kadhalika.

Zitto akifanikiwa kuondoa Mfumo huu ama wananchi wakishtuka na kumsikiliza itakuwa hatari kubwa kwa siasa hizi za Ubwanyenye. Nasikia leo huko Bungeni, wabunge wanajiongezea kiinua Mgongo mbali kabisa na Transition Allowance kiasi kwamba mbunge ataondoka na zaidi ya millioni 200. Hakuna cha CCM, Chadema wala UKAWA walolaani mpango huu, wote wanachekelea kupata fedha ili kujiandaa kugombea tena Ubunge wakati fedha hizo zinatoka mfukoni mwa wananchi. Kama sio wizi huu ni kitu gani? Zitto akisema kuwatetea nyie, oooh anapenda sana U Supreme! Sasa kama ataboresha mfumo huu huo U supreme wake utatukomboa ama utadumaza uchumi. Ndio maana hata Sokoine hakupendwa hadi baada ya kifo chake ndio tunasikia sifa.. Unafiki mtupu.

Watu wanashindwa kutazama Itikadi na sera za chama badala yake wanampima yeye. Kiongozi wa siasa tofauti na dini hutaka kuwakomboa wananchi wakati kiiimani ya dini unajikomboa mwenyewe kwanza. Viongozi Kama Lema anayediriki kusema hawezi somesha watoto wake shule za kata huku akidai elimu bure kwa wote! sijui hawezi kuishi kimaskini kwa sababu jirani zake ni maskini wakati akitumia fedha ya maskini hao hao kuishi vizuri ni kutuonyesha wazi kwa nini yeye hayupo kuwasaidia wananchi bali anachukulia siasa kama dini kujikomboa yeye..Miafrika bana!
Mkuu kabla sijajibu hoja zako, hebu tupe takwimu alizotumia Zitto kufikia hitimisho kuwa wananchi wa kanda fulani wanawapora wa kanda nyingine. Kama hiyo kauli si sawa, basi tupe kauli yake sahihi na takwimu alizotumia.

Twende taratibu mkuu

Mkuu kabla nami sijakujibu.. Labda nikuulize moja ili tuwe msitari mmoja. Je Wanawake wanapopigania mishahara sawa huwa wana maana huporwa na wanaume? Pili, tunapozungumzia Haki za Wanawake, je, unadhani kwamba hawa wanawake hakandamizwi na mfumo dume bali wanaume wenyewe? Kisha turudi kwa Zitto with open mind..
cc Alinda

Zile takwimu za supreme alizotumia Shinyanga na Mwanza ulizoahidi kuzileta zipo wapi mkuu. Huko kwingine hatujafika. Yakafuatia ya #738

Kama huna takwimu, muombe radhi mkuu Mag3 na jamvi kwa usumbufu uliosababisha

Ok, tueleze amesema nini kwa ufasaha. Pili, tuletee zile data alizotumia kwa hoja ya kwanza.

Kwa yoote haya sina sababu wala haja ya kuongeza neno mwenye kujua kusoma na kuchambua atasoma na kuelewa tofauti na mwisho naweka hizo taarifa mbili zenye kuonyesha takwimu ama maelezo ya Zitto na mchambue wenyewe kilichosemwa.

@Adharusi Ukurasa wa 38 hoja #745

Nisome kwa umakini Nguruvi3 magie3 Mchambuzi

Naeleza kilichosemwa na Zitto na source ya Takwimu alizozizotoa
Source ya Takwimu alizotoa Zitto zinatoka Tanzania Human Development Report 2014(THDR 2014).
Nanukuu maelezo ya Zitto
"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa

Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa,pia akasema Mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa. (Sijaona Zitto aliposema Arusha,Kilimanjaro zinapora utajili wa Shinyanga) kinachofanywa na Nguruvi3 nikuleta uchochezi na chuki ili watu wa Arusha na KLM wamchukie Zitto,na ikiwezekana wamletee fujo,ili aje aandike si tulisema...narudia tena ulistahili ban kwa kupotosha kwa lengo unalolijua mwenyewe
Mchambuzi nawe naomba usome maelezo ya Zitto hapo chini,maana wewe unataka Zitto ataje CCM.

" Zitto akasisitiza ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi,huwezi kuwa na mkoa unashika nafasi ya 4 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namna 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu,Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi,ina Ng'ombe na Pamba.

Tunavita moja tu,kufanya Mapinduzi ya mfumowetu was uchumi kutoka mfumo wa kinyonyaji na kifisadi na kujenga uchumi shirikishi,pia Zitto aligusia Takwimu za watu wenye elimu ya sekondari simiyu ni 3.7%, na Dar ni 29% inaongoza nchi mzima.

Wapi Zitto kasema Arusha,Kilimanjaro,zinaipokony a Shinyanga,bora weredi wenu mngeonyesha kujadili Takwimu(THDR2014).Kuliko kumlisha maneno Zitto kwa Chuki zenu bila sababu.

@Ritz

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.
 
Narudia kusema kuna editing imefanyika ili kuondoa maneno.

Pili, hiyo ya Ritz ameichukua kutoka kwa Adharusi kisha akafanya editing. Mkandara na Ritz hawakujua , wala hawajasikia hotuba, wamedandia(ushahidi upo wakikiri kutojua)

Tatu, huwezi kuwa na hotuba ya Shinyanga(Adharusi) na kisha Furahisha Mwanza(Ritz) ukasema mtu mmoja ameongea sehemu mbili katika wakati mmoja. Nadhani hapo tu unaona tatizo lilipo

Nitarudi kukuonyesha kwa umakini na uyakinifu neno hadi neno lengo ovu la Zitto juu ya mikoa ya kaskazini kwa kutumia hotuba hizo hizo ulizoleta. Hapa tunapiga kwa fimbo aliyoshika mtu, zetu zinaambiwa ni kubwa

Pamoja na hayo, tuweke rekodi sawa, kuna hotuba ya Zitto aliitoa shinyanga ambayo Mkandara amesahau kuiweka.

Naomba niiweke ili wakati wa kusasambua tuwe na hotuba 3.

Kwanza pata hotuba ya Mkandara aliyomnukuu Zitto kutoka Shinyanga
Mkandara;12735976]Basi hata wewe bado hujaelewa. Unachokitaza ni Kilimanjaro badala ya kuanza na Shinyanga.

Shinyanga wanachangia zaidi lakini hawapewi stahiki wakati Kilimanjaro wanachangia kidogo wanapewa stahiki.

hakuna mahala Zitto kasema Kilimanjaro wanapewa zaidi ya stahiki, isipokuwa kuwepo na mfumo unaweza kugawanya keki ya taifa kiasi kwamba wanaochangia zaidi wananufaika na kuwa shawishi wengine wazalishe na kuchangia zaidi.

Tutarejea asubuhi
 
Back
Top Bottom