Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Mchambuzi.ZITTO AENDELEZA UTAPELI WA KISIASA, SASA AMEUHAMISHIA KIGOMA
Zitto ametangaza rasmi nia yake kugombea ubunge Kigoma Mjini Kupitia ACT Wazalendo, chama ambacho ameshiriki kukipora huku kukiwa na kesi mahakamani. Kwa maana nyingine, wananchi wa Kigoma Kaskazini wanajiandaa kupigia kura chama ambacho matokeo ya uchaguzi yanaweza kutenguliwa huko mbeleni na mahakama kutokana na chama hicho kuwa ni cha kiujanja janja.
Akizungumza mara baada tu ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge, zitto alitamka kwamba ameamua kuwania ubunge jimbo la Kigoma mjini kwa sababu wananchi wa jimbo hilo wameshindwa kupata haki zao za msingi wanazostahili. Zitto akaenda mbali zaidi na kusema kwamba amemaliza kazi ya kuwahudumia wananchi wa Kigoma Kaskazini na kudai kwamba katika jimbo hilo hakuna shida tena ya maendeleo. Haya ni matusi makubwa sana kwa wananchi wa Kigoma Kaskazini. Zitto anadanganya na ushahidi upo. Maendeleo ni huduma bora za afya, elimu bora, miundo mbinu, kutaja machache. Maswali:
1. Je kuna hospitali ngapi zenye ubora wa kukidhi mahitaji kama vile upasuaji ndani ya jimbo la Kigoma Kaskazini? Jibu ni Hakuna hata moja.
2. Je, kuna barabara ngapi za lami ambazo zinazoweza kupitika mwaka mzima? Jibu ni Barabara ni moja tu, barabara ya Mwandiga Manyovu.
3. Je, Kigoma Kaskazini ina shule ngapi za sekondari zenye vidato vya tano na sita? Jibu ni Hakuna hata shule moja.
4. Je, wananchi wa Kigoma Kaskazini wamefanikiwa kumaliza tatizo la magonjwa ya milipuko? Jibu ni hapana kwani Kigoma Kaskazini ni eneo linalojulikana sana kama chanzo cha ugonjwa Kipindu Pindu.
5. Je Kigoma Kaskazini kuna soko kubwa la kusaidia wananchi kuuza mazao ya kibiashara (cash crops)? Hakuna soko hata moja.
Hivi karibuni katika ziara zake kama kiongozi mkuu wa ACT Tanzania, Zitto alitoa matamshi ya kubagua na kuchonganisha wananchi wa mikoa mbalimbali. Zitto aliwashambulia wananchi wa mikoa ya Kaskazini (Arusha na Kilimanjaro) kwamba wanawanyonya wananchi wa mikoa mingine kama vile Mwanza na Shinyanga. Zitto alitumia takwimu za GDP kama kipimo cha michango ya mikoa, na takwimu za HDI kama kipimo cha kuangalia returns za michango husika. Kwa vile Zitto anasema kwamba tatizo la umaskini kwa wananchi wa Kigoma Kaskazini halipo tena, je:
· Umaskini huo umetokomezwa kwa kutumia rasilimali zipi GDP?
· Kufuatia mafanikio hayo, Kigoma Kaskazini sasa ni jimbo hilo ni la ngapi kitaifa kimaendeleo?
Hii habari umeipata wapi mkuu wangu wakati Zitto anachukuwa fomu Kigoma Mjini wala akuita vyombo vya habari.
Last edited by a moderator:
