Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Narudia kusema kuna editing imefanyika ili kuondoa maneno.

Pili, hiyo ya Ritz ameichukua kutoka kwa Adharusi kisha akafanya editing. Mkandara na Ritz hawakujua , wala hawajasikia hotuba, wamedandia(ushahidi upo wakikiri kutojua)

Tatu, huwezi kuwa na hotuba ya Shinyanga(Adharusi) na kisha Furahisha Mwanza(Ritz) ukasema mtu mmoja ameongea sehemu mbili katika wakati mmoja. Nadhani hapo tu unaona tatizo lilipo

Nitarudi kukuonyesha kwa umakini na uyakinifu neno hadi neno lengo ovu la Zitto juu ya mikoa ya kaskazini kwa kutumia hotuba hizo hizo ulizoleta. Hapa tunapiga kwa fimbo aliyoshika mtu, zetu zinaambiwa ni kubwa

Pamoja na hayo, tuweke rekodi sawa, kuna hotuba ya Zitto aliitoa shinyanga ambayo Mkandara amesahau kuiweka.

Naomba niiweke ili wakati wa kusasambua tuwe na hotuba 3.

Kwanza pata hotuba ya Mkandara aliyomnukuu Zitto kutoka Shinyanga
Tutarejea asubuhi
Nguruvi3.

Hii hotuba ya Zitto imekufanya umepagawa kabisa sasa hivi unakuja na madai mapya kuwa nimeifanyia editing teh teh teh!

Kwa faida ya Wanaukumbi wanaofautilia huu mnakasha tuwekee wewe hotuba original ya Zitto ambayo ulisikiliza tukate mzizi wa fitna weka yeyote kuanzia ile ya tarehe 5 mlikuwa mnajadili na Alinda.

Mimi sipo hapa kukufuraisha wewe na wafuasi wako mimi na deal na Wanaukumbi wanaofautilia huu mnakasha naweka tena Ulimbo.

Msome kiduchu hapa chini...

Zitto

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.

Mwambie Alinda akuletee twits za facebook kama utakubali zikufariji na kukuuliza nilidhani bado unaendelea kunipuuza kama ulivyosema mwanzo ukinitaja tu lazima nije ukumbini!
 
Last edited by a moderator:
Alicholeta Adharusi si takwimu. Chukua zile za Mchambuzi uweke sambamaba na za Adharusi! Mlima na Kichugu

Yaani imetia uvivu kujadili takwimu zake ndio maana tumeamua kukaa kimya.
Hivi unaweza kusema Dar inachangia 9% na K'njaro 1% ukaja na conclusion kweli! real!

Ndio maana tunapiga kelele, supreme si kuwa anapotosha tu bali anaharibu uwezo wa vijana kufikiri
Wewe kila ukiletewa ushahidi unapinga tu ndiyo maana nakuambia sisi wengine hatupo hapa kukufurahisha wewe tupo hapa kuwaeleza ukweli Wanaukumbi wanaofautilia huu mnakasha nimeleta hii hizi takwimu kwenye hotuba ya Zitto nazo hautaki ndiyo maana tunakuambia tuwekee basi hiyo hotuba ya Zitto ambayo ni original haijachakachuliwa Wanaukumbi waisome...

Zitto

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.

Hii hotuba imefinyanga finyanga hoja zenu kisha ikawapiga nazo usoni bora Mchambuzi karusha taulo mapema kakuacha wewe povu linakutoka ovyo!! Endelea kupambana...
 
Last edited by a moderator:
@Adharusi Ukurasa wa 38hoja #745

Nisome kwa umakini Nguruvi3magie3Mchambuzi

Naeleza kilichosemwa na Zitto na source ya Takwimu alizozizotoa

Source ya Takwimu alizotoa Zittozinatoka Tanzania Human Development Report 2014(THDR 2014).
Nanukuu maelezo ya Zitto

"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa

Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwanamba 4 katika kuchangia pato la Taifa,

Mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dares salaam.
Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato laTaifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.

Mchambuzi

" Zitto akasisitiza ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wasasa wa uchumi,huwezi kuwa na mkoa unashika nafasi ya 4 kuchangia Pato la Taifalakini unashika namna 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu,Shinyanga inamigodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi,ina Ng'ombe na Pamba.

Tunavita moja tu,kufanya Mapinduzi ya mfumowetu was uchumi kutoka mfumo wa
kinyonyaji nakifisadi na kujenga uchumi shirikishi,
Takwimu za watu wenye elimu ya sekondari simiyu ni 3.7%,na Dar ni 29% inaongoza nchi mzima.

Takwimu(THDR2014)

@RitzTanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia mkoa wa 8 kwa kiwango chamaendeleo ya watu wake.

Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dares Salaam.
Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato laTaifa na Arusha ni ya 7.

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagerana Tabora.

Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Patola Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi(1.89%) na Singida (1.92%).

Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juuya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato laTaifa ni 16.9%.

Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%.
Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wakutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi.

Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato laTaifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu.
Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Alma
si.
Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoanimwenu.

Mkandara;12735976]Basi hata wewe bado hujaelewa.Unachokitaza ni Kilimanjaro badala ya kuanza na Shinyanga.

Shinyanga wanachangia zaidi lakini hawapewi stahiki wakati Kilimanjarowanachangia kidogo wanapewa stahiki.

hakuna mahala Zitto kasema Kilimanjaro wanapewa zaidi ya stahiki,isipokuwa kuwepo na mfumo unaweza kugawanya keki ya taifa kiasi kwambawanaochangia zaidi wananufaika na kuwa shawishi wengine wazalishe na kuchangiazaidi.
Inadelea...
 
Kwanza tuweke rekodi sawa sawa. Hotuba unayosema ni Ritz, kwa mujibu wake aliitoa Mwanza.
Wanaukumbi. Narudia tenahii hotuba ya Zittoaliyoitoa Mwanza imekuwa mwiba sana maana imefinyanga hoja za wale waliokuwawanampinga.
Mkandara na wanamhaba wengine mnahangaika kutafuta mahali pa kushikiza.

Kwa minajili ya mjadala huu, tufanye assumption kuwa ndizo hotuba alizotoa.
Hotuba yako Mkandara haionekani kufanana na yoyote.Maana yake ulijaribu kutafuta maneno yako na kuyafanya hotuba ya Zitto.

Kitu hicho kinaitwa disingenuous yaani kutokuwa mkweli na mwaminifu kwa unachoandika.
Hotuba yako haipo popote isipokuwa ni mhangaiko, tuna tunaelewa

Pili, ''takwimu' za Adharusi zimeorodhesha mikoa 5 inayochangia pato la taifa. Ritz kaongeza wa 8 -Tanga.
Hakuna anayejua mkoa wa 6 ni upi

Angalia kwa Adharusi, baada ya kuonyesha mikoa 5 inayochangia, ikaja sentesi inayohusisha mikoa yenye maendeleo zaidi Dar/K'njaro/Arusha. Hakuna anayeeleza ni katika rank gani kimaendeleo.

Neno zaidi limetumika bila kuonyesha mtririk okama ule wa kuchangia. Lengo lilikuwa kuonyesha uchangiaji na maendeleo Arusha/Kilimanjaro/Dar zikihukumiwa kwa neno zaidi.

Baada ya kutumia neno ‘zaidi katika maendeleo' sentensiiliyofuata ni '' hata hivyo Kilimanjaro ni 9 kuchangia pato la taifa na Arusha ni ya 7. Hapa ameondoa Dar ili kuweza kuunganisha kauli ya ‘maendeleo zaidi' na namba za uchangiaji pato la taifa.

Lengo likiwa kuonyesha mikoa hiyo inachangia kidogo lakini ina ‘maendeleo zaidi' huu ni ushahidi wa shambulio la kukusudia!!

Nukuu ya Adharusi haionyeshi mikoa masikini, ya Ritz inaonyesha.Hapa kuna kupotosha kwasababu mtu mmoja hawezi kuwa na kauli tofauti katika wakati mmoja(kumbuka tunafanya assumption kuwa ile ya Mwanza na Shinyanga zoteni za Shinyanga) unaona?

Adharusi amenukuu supreme akisema … kufumua mfumo wauchumi wa kinyonyaji na kifisadi na kujenga uchumi SHIRIKISHI.

Nukuu ya Ritzimeondoa neno Shirikishi. Hii maana yake ilikuwa kuua hoja inayomshtaki supreme.

Huwezi kusema uchumi shirikishi katika mazingira tuliyo nayo. Tayari tuna uchumi shirikishi kupitia central gov.

Alichomaanisha Zitto, ni kuondoa mfumowa uchumi wa kinyonyanyaji na kifisadi unaotoa fursa sehemu moja ili uwe uchumi shirikishi.

Ukiangalia hapo juu jinsi alivyoondoa mkoa namba 6 na Dar na kuacha Kilimanjaro na Arushaz ikiwa na ‘maendeleo zaidi'
Zitto anatoa tuhuma za unyonyaji na ufisadi kwa mikoa hiyo miwili.

Angalia jinsi alivyoiondoa Dar na matumizi ya neno ‘maendeleo zaidi'

Nukuu ya Ritz inasema Tabora ni ya 10 kuchangia pato lataifa na Kagera ni ya 11 kuchangia GDP.
Sijui kama ni sentensi inayoeleweka kiuchumi, muhimu ni kuwa Adharusi hakuonyesha hayo.

Hiyo ni hotuba ‘moja' ya mtu mmoja!

Ukisoma nukuu ya Ritz, mikoa yenye michango kidogo n iPwani, Lindi na Singida.
Ukisoma maelezo ya Zitto Shinyanga inashika namba 16 na ina umasikini wa kutupwa.

Lindi inachangia 1.89% na ni ya 10 kwa maendeleo. Da rinachania 16.9%.

Kilimanjaro na Arusha hazikuwekewa kiwango cha uchangiaji.Wala hazikuwekewa nafasi ya maendeleo, zimehukumiwa moja kwa moja na Zitto kwakutumia maneno ‘maendeleo zaidi''

Kama Lindi ina mchango mdogo zaidi na ni ya 10 kwa maendeleo, iweje Kilimnjaro na Arusha 7 na 9 zitajwe kuwa na ''maendeleo zaidi''bila kupewa haki ya kitakwimu kwa namba?

Hapa ni wazi Kilimanjaro na Arusha zimelengwa makusudi, zikaminywa kupewa haki ya kupimwa, isipokuwa pale tuilipotajwa mikoa inayochangia 7 na 9 na kisha kushindiliwa msumari wa ‘maendeleo zaidi''

Orodha inaendelea ya mapugufu, inatosha kusema kuwa kama hicho ndicho mlidhani ni utetezi, basi mnazidi kumuumiza supreme.

Nukuu yaAdharusi imebana mambo muhimu, ya Ritz imeongeza na kunyoofoa sensitive areas,ya Mkandara haipo katika hizo mbili

Hizi zote ni desperate move za kutaka kumsalimisha supreme dhidi ya hasira za watu kutokana na matamshi yake.

Utetezi mnaouleta,licha ya kuwa laini na uliofinyangwa, hakika unamweka supreme katika ubao kuliko mnavyodhani

Pamoja na spinning mnazofanya, bado picha inabaki palepale, hotuba ililenga kuwasumanga wananchi wa kaskazini.

Ni move ya kuligawataifa vipande pande kwa masilahi binafsi.

Hatudhani kama ni jambo jema kwajamii na kwa mwanasiasa kama Zitto

Njia nzuri ya kumsalimisha ni kujitokeza aombe radhi. Mnahokifanya ni kuchochea kuni bila kujua aliyeko jikoni ni mtu wenu.

Swali, kuna uhusiano gani kati ya maendeleo na uchangiajiwa pato la taifa?

Tutaendelea.

Wanaukumbi.

Narudia tena kesema nimemsikiliza Zitto kwenye mkutano wake aliofanya viwanja vya Furahisha Mwanza kupitia Radio Free Africa.

Hotuba za Zitto kanda ya ziwa zote zinafana angalieni kipande cha hotuba ya Tabora, ndicho hicho Zitto kakisema Shinyanga na Mwanza.

Tumemuomba Nguruvi3 aje basi na hotuba ya kweli ya Zitto hana kabakia kulalamika tu.
Nguruvi3 anasema mimi nimeongeza maandishi yangu siyo kweli huko ni kutapatapa tu.

Wanaukumbi kabla ya mimi sijaweka hii hotuba ya Zitto kuna mwenzetu jukwa la siasa aliiweka lakini yaye alikuwa anapinga na Zitto Wanaukumbi mkipata muda kiduchu pitieni hii link chini hapa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mikoa-yenye-maendeleo-zaidi-tanzania-8.html

Wanaukumbi sasa baada ya kupitia hii link nadhani mmejionea wenyewe naomba Nguruvi3 tuambie huyu alifungua huo uzi kumlalamikia Zitto naye kaongeza maandishi kama Ritz?

Nakuwekea tena hiyo hotuba halafu fananisha na hiyo kwenye uzi wa PISTO LERO.

Kisha tunakuomba kwa faida ya Wanaukumbi tuwekee hotuba ya Zitto ambayo ni originally!

Chini hapa mpini unaendelea najua kuna watu wanaumia kunisoma lakini vumilieni ndiyo faida za forum.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.
 
Last edited by a moderator:
Kumi, Ni utarataibu gani unaoweza kutumika kupendelea mikoa fulani katika serikali ya nchi moja kama Tanzania ikiwa Zitto alikuwa sehemu ya serikali hiyo na hakuweza kulizungumzia hilo akiwa mbunge?

Nguruvi3,

Nilitaka nikusahihishe kidogo hapo nilipo Underline.

Mh Zitto hajawahi kuwa sehemu ya Serikali bali yeye alikuwa mbunge.

Naomba nikufahamishe kuwa Mbunge au BUNGE sio sehemu ya Serikali BALI ni muhimili unaojitegemea.

Nchi yoyote inayofuata mfumo wa UTAWALA WA SHARIA (Rule of Law) Tz ikiwa moja wapo inakuwa inaongozwa ni mihimili mitatu nayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.

Na hyo yote ni mihimili inayojitegemea yenyewe na kila mmoja una kazi zake ambazo wanatekeleza bila kuingiliwa na muhimili mwingine.

Ahsantum
 
Wewe kila ukiletewa ushahidi unapinga tu ndiyo maana nakuambia sisi wengine hatupo hapa kukufurahisha wewe tupo hapa kuwaeleza ukweli Wanaukumbi wanaofautilia huu mnakasha nimeleta hii hizi takwimu kwenye hotuba ya Zitto nazo hautaki ndiyo maana tunakuambia tuwekee basi hiyo hotuba ya Zitto ambayo ni original haijachakachuliwa Wanaukumbi waisome...

Zitto

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.

Hii hotuba imefinyanga finyanga hoja zenu kisha ikawapiga nazo usoni bora Mchambuzi karusha taulo mapema kakuacha wewe povu linakutoka ovyo!! Endelea kupambana...

Acha kujifurahisha. Mnakimbia maswali, mkirudi, mnakuja na yale yale mkidhani kwamba tutafunika kombe mwana haramu apite. Kuna msururu mrefu wa hoja ambazo hamjajibu, kuanza kurudia humu ni kujaza tu server. Swali langu la mwisho kwenu lilihusu clip ya TUJITEGEMEE juu ya hotuba ya zitto Tabora. Kama kawaida, ukapotea. Je una majibu? Pia je, hivi unajua kwanini zitto amesitisha ziara zake za upotoshaji na ubaguzi?
 
Wanaukumbi.

Chini hapa mpini unaendelea najua kuna watu wanaumia kunisoma lakini vumilieni ndiyo faida za forum.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.
Ritz,

Ulichoandika hapa ni sawia kabisa na hilo ni tatizo la WIZARA YENU YAMIPANGO ambayo inapanga maendeleo kwa kufuata siasa na sio uchangiaji wkt pato la taifa.

Mgawanyo huo ndio tatizo kubwa sana tanzania na hili hata Mbowe aliwahi kulisema kuwa akipewa uongozi wa nchi ataigawanya katika majimbo ili kila jimbo lifaidike na uchangiaji wake katika mchango wake katika pato la tanzania.

Sioni kosa lolote hapo.

Dr. Barubaru.

Unachosema kuhusu Mbowe ni sahihi kabisa kwa faida ya Wanaukumbi tujikumbushe maneno ya Mbowe.

Tumsome Mbowe kiduchu hapa chini.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuwa utekelezaji wa sera ya Kanda inayoigawa Tanzania katika majimbo 10 kiutawala na hivyo kujenga mizizi ya chama hadi ngazi ya vitongoji na vijiji ni kihama cha Chama Cha Mapinduzi (CCM).Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema sera hiyo sasa itakiwezesha chama hicho kuking’oa CCM kuanzia ngazi ya chini kabisa baada ya kufanikiwa kufanya hivyo maeneo yote ya mijini ambako wagombea wake wote wa Chadema walishinda dhidi ya wale wa CCM.Akihutubia maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha katika mkutano wa hadhara kuzindua Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara, Mbowe alisema CCM inaogopa sera ya majimbo na kuamua kuipotosha makusudi kwa sababu itatoa fursa kwa wananchi kupanga na kuamua matumizi na mustakabali ya rasilimali zao.Alisema sera ya Kanda inahamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache walioko makao makuu Jijini Dar es Salaam na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini na hailengi kugawa nchi kama inavyopotoshwa na CCM iliyoshindwa kuongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru.“Hatuwezi kuendelea na mtindo wa kila jambo kuhusu maisha ya Watanzania zaidi ya 45 milioni kuamuliwa na watu wachache kutokea Ikulu ya Dar es Salaam. Madaraka haya sasa lazima yashuke kwa wananchi wenyewe,” alisema Mbowe.Alitaja migogoro ya ardhi iliyosambaa kila sehemu nchini kama moja ya matokeo ya sera ya mambo yote kuamuliwa na mtu mmoja, yaani waziri wa Ardhi akiwa ofisini Jijini Dar es Salaam.Alisema katika sera ya majimbo, kodi inayokusanywa kutokana na rasilimali zilizopo eneo moja zitatumika kuendeleza eneo hilo na maeneo mengine yasiyo na rasilimali.Mbowe alitumia fursa hiyo kuendeleza msimamo wa Chadema kuhusu nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya akisema hazina tija kwa maendeleo ya taifa kutokana na uteuzi wake kujaa uwahiba, kulipana fadhila kulingana na utashi wa mteuzi, jambo linalofanya viongozi hao kugeuka vibaraka badala ya watumishi wa umma.“Chadema hatuwataki wakuu wa mikoa na wilaya. Siyo kwamba tunawachukia, bali madaraka makubwa wanayopewa kama kuwa wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama pamoja na upatikanaji wao ndio chukizo kwa wananchi,” alisemaAlisema katika mfumo na sera ya majimbo. Viongozi wote wa umma na kisiasa watapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi wanaowaongoza.Hata hivyo aliwaonya wananchi wasionyeshe dharau kwa viongozi hao kwa sababu hivi sasa wapo kisheria nay eye ni mmoja wa wajumbe wa vikao vya kutunga sheria hivyo hawezi kushiriki kuhamasisha zivunjwe.Mbowa alitangaza kuwa iwapo katiba mpya itarejesha nafasi hizo, Chadema kitapinga kwa nguvu zote kwa kuwasha moto ambao hautazimika dhidi ya mapendekezo na rasimu ya katiba hiyo.Mwenyekiti huyo alisema kuanzia kesho Jumatano anaanza ziara ya kuzindua kanda zingine tisa akiania Kanda ya Ziwa Victoria atakakozindua Kanda za Ziwa magharibi na Mashariki zinazojumuisha mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Simuyu na Geita.Awali akimkaribisha Mbowe, Mwenyekiti wa muda wa Kanda ya Kaskazini, Israel Natse aliitaka serikali kutekeleza wajibu wake wa kulinda usalama wa maisha na mali ya wananchi dhdi ya vitendo vya mauaji yanayotokea nchini yenye sura ya tofauti za kidini kwani vikiachwa viendelee, taifa litaangamia kwa sababu hakuna vita mbaya kuliko inayohusiana na imani ya kidini.Alimpa changamoto Rais Jakaya Kikwete kujitokeza hdharani kukemea kwa nguvu tofauti zozote zinazojitokeza katika jamii kwa misingi ya ubaguzi wa aina yoyote kwa siyo tabia wala hulka ya Watanzania kubaguana.Alionya kuwa chokochoko za ubaguzi wa kidini zilizoanzishwa, kupaliliwa, kuenezwa na kushabikiwa na CCM na viongozi wake kulenga vyama vingine vya siasa ndiyo sasa inatafuna taifa.Mbunge Joshua Nassari wa jimbo la Arumeru Mashariki yeye licha ya kuwahimiza Watanzania wote wenye mapenzi mema kuunga mkono vuguvugu na harakati za kukiondoa madarakani CCM, pia alitangaza vita dhidi ya Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kama hajo yake binafsi kuhusu hali ya elimu inchini hakitajadiliwa kikao kijacho cha bunge.
 
Last edited by a moderator:
Hivi hawa watu wagumu kiasi gani kuelewa? Nimeandika wala sii mara moja ya kwamba bandiko la Adharusi ni usimulizi wake yeye kutokana na jinsi anavyokumbuka Zitto alisema nini na ndio maana akaongeza neno Pia akasema tofauti kabisa na bandiko la Ritz na mimi nimeelewa vizuri tu kwamba Adharusi alikuwa akijibu hoja ya Nguruvi3 kueleza wapi Zitto alizipata takwimu.

Mara baada ya hoja yao kujibiwa kwamba takwimu zilitoka HDR wakabadilisha na kuchukua kipengele alichoandika Adharusi kuwa ndio maneno ya Zitto akiwa Shinyanga. Adharusi hakuitaja mikoa mingine yenye maendeleo madogo wala mikoa yenye mchango midogo kwa sababu haikuhusiana na hoja alopewa mwanzo kuitoa hotuba nzima ya Zitto ila kujibu kuwa Zitto hakusema Shinyanga inadhulumiwa na Kilimanjaro!. Na ndio maana kila alipoandika aliweka cc kwa Mchambuzi, Nguruvi3 Alinda na wengineo ikiwa ni maneno yake. Sasa mbona hamsemi Zitto aliwataja pia Mchambuzi, Nguruvi na Alinda katika hotuba yake ikiwa mnasoma bandiko la Adharusi neno kwa neno?\

NB Ritz shukran kwa kipande hiki cha mwisho ulokitoa, yule alopingana na Zitto kule kaweka hadi maneno haya:- Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu..
 
Nguruvi3 Mchambuzi mnafuatilia mjadala wa bunge la bajeti,bajeti ya wizara ya ujenzi,Mh lekule Laiza ametoa shilling sababu ya upendeleo miradi ya barabara,pia Ole sendeka ameunga mkono hoja,na emesema upendeleo kwa watu walisoma mapema,imetosha sasa,barabara zote mzuri zimeishia kwa hao
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Nilitaka nikusahihishe kidogo hapo nilipo Underline.

Mh Zitto hajawahi kuwa sehemu ya Serikali bali yeye alikuwa mbunge.

Naomba nikufahamishe kuwa Mbunge au BUNGE sio sehemu ya Serikali BALI ni muhimili unaojitegemea.

Nchi yoyote inayofuata mfumo wa UTAWALA WA SHARIA (Rule of Law) Tz ikiwa moja wapo inakuwa inaongozwa ni mihimili mitatu nayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.

Na hyo yote ni mihimili inayojitegemea yenyewe na kila mmoja una kazi zake ambazo wanatekeleza bila kuingiliwa na muhimili mwingine.

Ahsantum
Bunge ni mhimili wa nini?
 
Yes upo sahihi kwa mtazam huo. Ni kweli ipo mihimili 3 kama ulivyosema
Pengine ningesema Zitto alikuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania

Pamoja na ukweli huo, pia elewa kuwa mihimili hiyo hufanya kazi kwa kutegemeana ingawa ni huru katika maamuzi

Bunge lina kazi muhimu ya kuisimamia serikali iliyopo madarakani. Zitto alikuwa Mbunge, akiwa na nafasi ya kueleza duku duku lake dhidi ya mikoa ya kaskazini kupendelewa au kuwezeshwa kama anavyosema Mkandara

Pia alikuwa mwenyekiti wa PAC akishughulikia sana mambo ya serikali. Kwa mtazamo huo Zitto alikuwa ''in a way'' sehemu ya serikali ingawa hakuwa mtu wa serikali. Unaposimamia serikali kwa kuichunguza na kutoa mapendekezo ya kuisimami, hapo unakuwa sehemu ya'' na sio kuwa ni serikali

All in all, sikumaanisha kuwa alikuwa waziri, mkuu wa mkoa au vinginevyo
 
Bunge ni mhimili wa nini?
Kobello please. Bunge ni muhimuli wa Kidemokrasia wenye uwakilishi wa matakwa ya wananchi. Na ndani yake, matakwa ya wengi ndio huwa represented. Upande mwingine Serikali hushughulikia mambo ya utawala kulingana na mahitaji ya wananchi.
 
Hata tuendelee, ila binge ni mhimili wa serikali Kama ilivyo utendaji na mahakama.
Serikali Ina mihiimili mitatu (three branches of government).
 
Kobello please. Bunge ni muhimuli wa Kidemokrasia wenye uwakilishi wa matakwa ya wananchi. Na ndani yake, matakwa ya wengi ndio huwa represented. Upande mwingine Serikali hushughulikia mambo ya utawala kulingana na mahitaji ya wananchi.
Mkandara,

Bunge ni mhimili wa kidemokrasia? Umesoma Wapi hili.
Do you really know what "government" means? Kwanini unataka kuanzisha ubishi kwamba bunge sio sehemu Ya serikali? Do you know anything about separation of powers? Serikali ina mihimili mitatu - executive, legislative and judiciary. That's the bottom line.
 
Last edited by a moderator:
ZITTO AENDELEZA UTAPELI WA KISIASA, SASA AMEUHAMISHIA KIGOMA

Zitto ametangaza rasmi nia yake kugombea ubunge Kigoma Mjini Kupitia ACT Wazalendo, chama ambacho ameshiriki kukipora huku kukiwa na kesi mahakamani. Kwa maana nyingine, wananchi wa Kigoma Kaskazini wanajiandaa kupigia kura chama ambacho matokeo ya uchaguzi yanaweza kutenguliwa huko mbeleni na mahakama kutokana na chama hicho kuwa ni cha kiujanja janja.

Akizungumza mara baada tu ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge, zitto alitamka kwamba ameamua kuwania ubunge jimbo la Kigoma mjini kwa sababu wananchi wa jimbo hilo "wameshindwa kupata haki zao za msingi wanazostahili". Zitto akaenda mbali zaidi na kusema kwamba – amemaliza kazi ya kuwahudumia wananchi wa Kigoma Kaskazini na kudai kwamba katika jimbo hilo hakuna shida tena ya maendeleo. Haya ni matusi makubwa sana kwa wananchi wa Kigoma Kaskazini. Zitto anadanganya na ushahidi upo. Maendeleo ni huduma bora za afya, elimu bora, miundo mbinu, kutaja machache. Maswali:

1. Je kuna hospitali ngapi zenye ubora wa kukidhi mahitaji kama vile upasuaji ndani ya jimbo la Kigoma Kaskazini? Jibu ni Hakuna hata moja.
2. Je, kuna barabara ngapi za lami ambazo zinazoweza kupitika mwaka mzima? Jibu ni Barabara ni moja tu, barabara ya Mwandiga – Manyovu.
3. Je, Kigoma Kaskazini ina shule ngapi za sekondari zenye vidato vya tano na sita? Jibu ni Hakuna hata shule moja.
4. Je, wananchi wa Kigoma Kaskazini wamefanikiwa kumaliza tatizo la magonjwa ya milipuko? Jibu ni hapana kwani Kigoma Kaskazini ni eneo linalojulikana sana kama chanzo cha ugonjwa Kipindu Pindu.
5. Je Kigoma Kaskazini kuna soko kubwa la kusaidia wananchi kuuza mazao ya kibiashara (cash crops)? Hakuna soko hata moja.

Hivi karibuni katika ziara zake kama kiongozi mkuu wa ACT Tanzania, Zitto alitoa matamshi ya kubagua na kuchonganisha wananchi wa mikoa mbalimbali. Zitto aliwashambulia wananchi wa mikoa ya Kaskazini (Arusha na Kilimanjaro) kwamba wanawanyonya wananchi wa mikoa mingine kama vile Mwanza na Shinyanga. Zitto alitumia takwimu za GDP kama kipimo cha michango ya mikoa, na takwimu za HDI kama kipimo cha kuangalia returns za michango husika. Kwa vile Zitto anasema kwamba tatizo la umaskini kwa wananchi wa Kigoma Kaskazini halipo tena, je:

· Umaskini huo umetokomezwa kwa kutumia rasilimali zipi – GDP?
· Kufuatia mafanikio hayo, Kigoma Kaskazini sasa ni jimbo hilo ni la ngapi kitaifa kimaendeleo?
 
Acha kujifurahisha. Mnakimbia maswali, mkirudi, mnakuja na yale yale mkidhani kwamba tutafunika kombe mwana haramu apite. Kuna msururu mrefu wa hoja ambazo hamjajibu, kuanza kurudia humu ni kujaza tu server. Swali langu la mwisho kwenu lilihusu clip ya TUJITEGEMEE juu ya hotuba ya zitto Tabora. Kama kawaida, ukapotea. Je una majibu? Pia je, hivi unajua kwanini zitto amesitisha ziara zake za upotoshaji na ubaguzi?
Mchambuzi.

Wewe kuandika humu haujazi server pamoja wenzako? Ila sisi ndiyo tunajaza server sababu fikra zetu zipo tofauti na nyie daah!!..

Mchambuzi, mkikaa kwenye vikao vyenu mnajifariji na kupongezana na kudhani kuandika humu mnakwamisha harakati za ACT - Wazalendo na Zitto.

Unaniuliza kwa nini amesitisha ziara mikoani mimi sina majibu rasmi majibu rasmi soma kiduchu hapa chini.

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetangaza operesheni Majimaji katika majimbo 59 yaliyopo katika mikoa 19 nchini ikiwa na lengo la kukiwezesha kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa udiwani, ubunge na Rais wa Oktoba 25 mwaka huu.

Operesheni hiyo ni moja ya maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana Mei 23 na 24 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na kiongozi wake, Zitto Kabwe.

Taarifa iliyolewa jana na Ofisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, ilieleza kuwa kikao hicho pia kilifanya uteuzi wa nafasi za manaibu katibu wakuu bara na Zanzibar.

“Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Bara, Kamati Kuu imemteua Msafiri Mtemelwa ambaye ni mwanasiasa mzoefu katika siasa za Tanzania na kwa upande wa Zanzibar ameteuliwa Juma Said Sanani.

Khamis alisema kikao hicho kimefanya uteuzi wa makatibu mbalimbali ambako Peter Mwambuja (Fedha na Rasilimali), Habibu Mchange (Mipango na Mikakati), Richard Sabini (Mawasiliano na Uenezi).

Wengine ni Mohamed Masaga (Kampeni na Uchaguzi), Deus Chembo (Katiba na Sheria), Venance Msebo (Mambo ya Nje) na Gibson Kachinjwe (Katibu Kamati ya Maadili).

“Pia imemteua Estomih Mallah kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Rasilimali na Mwanasheria, Albert Msando, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria. Japhari Kasisiko na Hamad Mussa Yusuph wakuteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu,” alisema Khamis.

Kutokana na hali ya siasa nchini, Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, imewateua Profesa Kitilla Mkumbo na Tery Bermunda (mama Tery) kuwa washauri wa Chama.

Mpini unaendelea...
 
Last edited by a moderator:
Wanaukumbi.

Naona mwendelezo wa kumzulia Zitto bado unaendelea Mchambuzi kaja ma madai mpya kwa Zitto kuwa kasema tatizo la umasikini kwa wananchi wa Kigoma Kaskazini halipo tena.

Mchambuzi mkuu wangu unapat faida gani kumzulia Zitto kila kukicha unajifungua ndani na laptop yako unaaza kutunga uongo kisha unauleta JF bahati mbaya watu wanameza tu bila kutafuna kuona kama kuna mawe wateme.

Mchambuzi, huu huzi utawachia majeraha mengi sana ya mishale ya migongoni mwenu mkuu hauwezi kuingia vitani na pisto ya maji mkuu wangu, kwa faida ya Wanaukumbi tuwekee hotuba ya Zitto alichosema wakati anawaanga wananchi wa Kigoma Kaskazini.

Zitto.
Mwanamapinduzi na Rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara alisema kuwa ili kuleta mabadiliko ya kimapinduzi ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu. Ila tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja na changamoto nyingi.Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka kuboresha maisha ya wanakigoma, mwaka 2005 nilikuja kwenu kuwaomba ridhaa ya kuwatumikia kama mwakilishi wenu Dodoma. Nikiwa na umri wa miaka 29 tu. Labda ulikuwa ni msukumo wa matumaini yangu makubwa yanayoambatana na ujana yaliyowashawishi, kwani mliniamini na kunipa kazi hiyo ya heshima kubwa ya kuwawakilisha.Mwaka 2010 mliniamini tena, naamini kutokana na utekelezaji wangu mzuri wa kazi na mafanikio tuliyoyaweza kuyapata katika jimbo letu. Hivyo kwa miaka kumi tumekuwa bega kwa bega katika safari hii ya pamoja ya kujenga na kuiendeleza jimbo letu, na leo nimekuja kuwashukuru kwa fursa mliyonipa kwani safari yetu inafikia mwisho. Fursa mliyonipa ni ya kipekee kwani ilikuwa fursa si tu ya kuwatumikia ninyi bali kulitumikia Taifa langu.Katika miaka kumi hii kuna mambo makubwa tumeyafanya pamoja na kufanikiwa; na kuna mambo ambayo hatukuweza kuyafanya. Kwa yale ambayo hatukuweza kuyafanya naomba radhi. Kwa yale ambayo tumeweza kuyafanya naomba kuwapongeza sana kwa kufanikisha. Kwani kama Mwalimu Nyerere alivyotuambia kuhusu Uhuru na Maendeleo: “Uongozi ni kuongea na kujadili na wananchi, kuwaelewesha na kuwashawishi. Uongozi ni kufanya kazi pamoja na wananchi na kuonyesha kwa vitendo mnachotaka kufikia. Uongozi ni kuwa mmoja wa wananchi na kutambua kuwa mko sawa…. Wananchi hawawezi kuendelezwa bali wanajiendeleza.” Na ndivyo tulivyofanya kwa miaka kumi, na kwa ushirikiano wenu tumeweza kufanikisha miradi mikubwa katika Jimbo letu.Mwaka 2005 tulikuwa hatuna barabara ya lami hata moja. Leo hii, ninapoongea nanyi tuna barabara za lami zenye zaidi ya kilomita 100 kuunganisha Jimbo letu na majimbo mengine kwa pande zote za nchi kavu. Vilevile tuna mradi mkubwa wa kuunganisha vijiji vya ufukweni mwa Ziwa Tanganyika kwa barabara. Kiujumla kwa mkoa wa Kigoma tumefanikiwa kumaliza daraja la Malagarasi na hivyo kuunganisha mkoa wetu na mkoa wa Tabora kwa lami jambo ambalo lilikuwa kilio chetu cha muda mrefu sana tokea enzi na enzi. Muhimu zaidi ni kuwa barabara hizi zinatumika na wananchi, wafanyabiashara na wakulima ili kuwasiliana, kufanya biashara na kupanua masoko.Tumefanikiwa kuongeza huduma ya Nishati ya Umeme kwa kuunganisha vijiji zaidi ya 16 hivi sasa. Changamoto kubwa iliyobakia mkoani kwetu ni uzalishaji mdogo wa umeme na wenye gharama kubwa sana. Suluhisho la kudumu ni kufanikisha mradi wa Malagarasi wenye uwezo wa kuzalisha 44MW ambao utakuwa nafuu na kuwezesha pia kusambaza umeme mikoa jirani ya Katavi na Tabora, na hata kuuza nchi jirani ya Burundi. Viongozi wa kisiasa wa mkoa wa Kigoma watakaoingia kwenye uongozi baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka 2015 hawana budi kuweka kipaumbele kikubwa kwa mradi huu. Bila ya umeme wa uhakika na nafuu hatuwezi kupiga hatua ya kuongeza thamani ya mazao yetu kwa kujenga viwanda vya usindikaji na kuongeza ajira ya vijana wetu.Tumefanikiwa kuanza miradi ya Bandari na Soko kubwa kijiji cha Kagunga. Lengo likiwa ni kukuza biashara ya bidhaa kati yetu na nchi ya Burundi. Kigoma ni mji wa biashara kiasili na biashara ilichukua nafasi kubwa ya uchumi wa mkoa huu kwa miaka mingi sana. Kuimarishwa kwa miundombinu ya Biashara ni sehemu ya miradi ya kimkakati katika kuuweka mkoa kuchukua nafasi yake ya kiuchumi katika nchi yetu. Katika muktadha huo ndio maana tunaendelea na miradi ya Bandari Kibirizi na Bandari ya Nchi Kavu Katosho. Ndio maana tunaendelea na mradi wa Kituo cha Usafirishaji Mwandiga ( Mwandiga International Transportation Terminal ) na eneo maalumu la kiuchumi Ujiji. Haya yote tuliyaanzisha kwa pamoja nanyi ili kuhakikisha kuwa uchumi wetu unazalisha ajira kwa watu.Tumefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi wa sekondari kwa kuwa na shule katika kata na baadhi ya kata tumejenga shule kila kijiji. Hata hivyo, tuna changamoto kubwa sana ya ubora wa elimu katika mkoa wetu. Katika jimbo la Kigoma Kaskazini zaidi ya 90% ya watahiniwa wa Kidato cha Nne wanapata madaraja ya mawili ya chini, wakati ule daraja la nne na daraja la sifuri. Tumeanzisha mradi wa majaribio ya kutoa motisha kwa Walimu ili kuona namna bora zaidi ya kuhakikisha elimu inaboreshwa. Shirika la Twaweza linaendesha mradi mkubwa wa motisha kwa walimu na baada ya mwaka huu tutakuwa tumejifunza njia bora za kuongeza ubora wa elimu kwa watoto wetu. Bila Elimu bora miradi yote niliyoeleza hapo awali haina maana yeyote. Serikali imetoa Sera mpya ya Elimu, ni wajibu wetu kuona namna ya kuitekeleza katika ngazi yetu ili kupata mafanikio. Hata hivyo, uongozi wa kisiasa utakaoingia baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu hauna budi kujielekeza vya kutosha katika elimu ya ufundi ili kujenga stadi za kazi kwa vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.Tumefanikiwa kupanua huduma ya Afya kwa kuboresha Zahanati zetu chache zilizokuwepo na kujenga zahanati kadhaa mpya na miradi ya vituo vya afya vya Mahembe na Nyarubanda. Hata hivyo nasisitiza sana umuhimu wa kinga kuliko tiba kwani gharama za afya zimekuwa kubwa sana. Ndiyo maana tulipojadili hili suala, ilionekana kuwa suluhisho linatakiwa lipatikane kwa kufanya kile ambacho hatujawahi kufanya ili kuleta maendeleo ya kweli. Na mniruhusu hapa kunukuu wosia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alipotuasi kuwa “Maendeleo ni maendeleo ya watu. Barabara, Majengo, kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao na masuala mengi kama haya si maendeleo, bali ni vitendea kazi tu vya maendeleo” Ndiyo maana kulikuwa na umuhimu wa kutafuta njia mpya na mbadala kuboresha maisha ya mwananchi, hususan kwa upande wa afya. Uthibitisho wa ubunifu wetu ni kuwa katika kipindi hiki cha miaka 10 tumefanikiwa kuanzisha hifadhi ya jamii kwa wakulima.Tulianza na Ushirika wa Wakulima wa Kahawa wa RUMAKU ambapo wananchi walijiunga na NSSF na hivyo kupata mikopo ya muda mfupi, huduma za afya bure na kujiwekea akiba kwa ajili ya mafao ya muda mrefu. Mafanikio makubwa yaliyopatikana yamewezesha wazo hili kusambaa nchi nzima na hivi sasa wakulima wa Korosho, Chai, Pamba, Tumbaku wanafuata nyayo za Wakulima wa Ushirika wa RUMAKU. Hapa Kigoma wazo hili sasa linatekelezwa kwa wavuvi wa mwambao mwa Ziwa Tanganyika. Ndoto yetu ni wananchi zaidi ya theluthi moja kwenye nguvu kazi wawe na Hifadhi ya Jamii. Natoa wito kwa wananchi wengine wenye uwezo wa kuchangia hifadhi ya jamii wajiunge na vikundi vya ushirika na kuchangia ili kufaidika na mafao ya muda mrefu kama pensheni lakini pia yale ya muda mfupi kama bima ya afya, mikopo kupitia SACCOS na mengine yatakayoanzishwa kama bima ya mazao.Tumefanikiwa kujenga heshima ya watu wa Kigoma hapa nchini. Hivi sasa watu wa Kigoma tunatembea kifua mbele bila woga kuliko hapo awali. Kujiamini na kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano ni wajibu wetu kama raia. Changamoto za kujiona raia wa daraja la pili zimeondoka na zinaendelea kutokomezwa. Juhudi zetu ni silaha kubwa katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya Jamhuri yetu katika kila Nyanja za maisha yetu. Nafurahi kupata fursa ya kushiriki nanyi katika kujenga heshima hiyo ya Mkoa wetu. Nitaendelea kushiriki katika kudumisha heshima hiyo.Nimejifunza mengi sana katika safari hii ya utumishi kwenu. Kama nilivyosema hapo awali, mliamua kufanya kile kisichozoeleka katika siasa ya nchi yetu kwa kunipa jukumu hili nikiwa kijana mdogo. Naamini kuwa ule ukichaa wangu mzuri wa kusimamia misingi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wangu na kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia nimezipigania. Na katika safari hii nimejenga marafiki wengi sana na pengine hata maadui ingawa hao ni wachache. Lakini haijalishi kwani mi binafsi sina uhasama na binadamu mwenzangu.Katika utumishi wangu kwenu, bungeni nimejifunza namna nchi yetu inaendeshwa. Katika kujifunza huko kuna mambo kadhaa nimefanya ya kujivunia na mengine ni makosa. Mliniruhusu kufanya makosa na kuyarekebisha makosa hayo kwa hiyo kukomaa zaidi. Shukrani za dhati ziwaendee wazee wangu ambao mliniongoza mpaka hapa tulipofika na kunishauri hata kunionya pale palipohitajika. Kwa ujumla nimejifunza kuwa mzalendo zaidi kwa nchi yangu na kuwatumikia watu wa nchi hii. Ndio maana hamkunisikia tu kutetea watu wa Kigoma pekee, bali watu maeneo mengine ya nchi yetu na makundi mbalimbali ya kijamii kama Wakulima, Wafanyakazi, Wasanii, Wavuvi, Wana michezo na wana habari.Katika safari hii ya miaka 10 kuna watu nimewafurahisha na kuna watu nimewaudhi. Kwa wale niliowaudhi ninaomba radhi. Kwa wale niliowafurahisha ninaomba wasiache kuniongoza na kunishauri kila wakati. Haikuwa safari rahisi na sikutegemea iwe rahisi. Kiuhalisia ilikuwa safari ngumu yenye mafunzo makubwa kwangu. Ilikuwa ni safari yangu kama kiongozi na pia safari yangu binafsi ya kupevuka kifikra na kupata mafunzo kuhusu maisha. Ukifika ulikokuwa unakwenda katika safari, unaweza kutathmini mengi kuhusu safari hiyo, lakini mwisho wa siku unatakiwa ujue kama safari hii ilikuwa njema ama la. Ninajivunia safari hii na ninasema kwa dhati kabisa ilikuwa ni safari njema.Ni wakati sasa wa kutoa nafasi kwa nguvu mpya kuongoza Jimbo letu. Kushika kijiti pale ninapoishia. Kurekebisha pale nilipokosea. Kuimarisha pale nilipofikia.Sitakuwa mbunge wenu baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini nitaendelea kutetea maslahi ya Mkoa wa Kigoma na Taifa letu kwa njia nyingine.Sitaacha ule uendawazimu mzuri aliyoizungumzia Thomas Sankara unaoleta maendeleo ya kimapinduzi. Na misingi ni ileile na maadui ni walewale ambao mwasisi wetu Mwalimu Nyerere aliyokuwa anasema tupambane nao, yaani umaskini, ujinga, maradhi na sasa tumeongeza ufisadi. Kizazi chetu kina jukumu la kipekee kuendeleza mapambano haya na nitaendelea kuhakikisha tunafanya mapinduzi na kuwa na Taifa lenye misingi madhubuti ya uwajibikaji ili kuondoa kila aina ya ufisadi na kutumia rasilimali za nchi kuondoa umasikini, ujinga na maradhi.

Asanteni sana Kigoma Kaskazini!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom