Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,149
Alinda umemjibu Barubaru vizuri sana. Hapo nyuma Barubaru kasema Zitto anaandamwa.
Tulikaa kimya tukijua majibu yapo, ndiyo hayo!
Kiongozi mkuu ameitaja Arusha kama sehemu moja ya watu walioweka miguu juu.
Hawezi kusema jambo baya bila kutaja mikoa ya kaskazini kama Arusha
Huyu ndiye kiongozi anatarajiwa kuongoza taifa akijenga nyufa za chuki jukwaani
Kuanzia dakika 14.17 anaeleza uenyekiti ndio tatizo.
Hakuwaeleza wananchi wake juu yaWaraka!
Hakueleza juu yauchochezi aliousimamia miaka yote ukiwemo wa masalia, akina Shonzy n.k.
Supreme huwa anakaribisha mijadala bila kujua. Akiwa na vipaza sauti anahitaji washauri.
Ukisikiliza hiyo hotuba ukaanganisha na madudu yaliyofuata ya ACT utaweza kupata picha halisi ya mwenzetu.
Bado anahitaji muda mwingi kukua kiakili na fikra.
Unajua nimepatwa na mshangao:
kwamba wakati watu wa Kigoma wakipigwa virungu watu wa Arusha, Iringa na Singida walikuwa wamelala?? hivi ni kweli?
Kwamba watu wa Kigoma ndo wanamageuzi kuliko watu wa mkoa wowote hapa Tanzania?
Kwamba watu wa Iringa, Arusha na Singida wana midomo mirefu???
Hivi kosa la watu wa Arusha, Iringa na Singida ni nini? Wamemkosea nini Zitto?
Hivi hizi ni akili za kawaida kweli? Kwamba kiongozi anaweza kupanda jukwaani na kusimanga watu wa mkoa fulani? Yaani siku 45 za kukaa jela kwa Mzee Kasiko ndo ikufanya kudhalilisha wa mikoa fulani watu? Je watu waliopata vilema, watu waliokufa kwa ajili ya mageuzi hawa utawaitaje?
Hama kweli Zitto mwenyewe alisema "Msiwaamini wanasiasa"
Swali ninalojiuliza ni kuwa akienda Singida anatawambia kuwa "Nyie wana Singida fungeni midomo yenu mirefu kwani wakati wana Kigoma wanalalla jela nyie mlikuwa mnawakumbatia watawala?
Ila kiboko ni "Kwani mtu wa Kigoma haruhusiwi kuwa Mwenyekiti?? hii sentesi sijaielewa nini makusudi yake? Hivi alishindwa kusema "kwanini mimi Zitto siruhusiwi kuwa Mwenyekiti??" Nini siri ya hii sentensi?? Mkandara. JokaKuu , Mag3 , Adharusi na mengineo
Last edited by a moderator: