Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Hivi Alinda humjui Mkandara? Anajua kabisa katiba ilibadilidhwa lini na wakati huo Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema. Anajua kabisa ni lini Zitto alitaka kugombania uenyekiti wa Chadema na kushauriwa asubiri na wazee. Anajua ni lini waraka wa usaliti ulitayarishwa. Anajua timeline ya Chadema toka kuanzishwa kwake. Anajua yote hayo.Kama kumbukumba zangu ziko sawa katiba ilibadilshwa Mwaka 2006... (I stand to be corrected)
Lakini kwa makusudi yasiyoeleweka ukimsoma ni kama vile anadai katiba ilibadilishwa baada ya Zitto kushauriwa asigombee. Kama humjui Mkandara unaweza kuumia ukijiuliza nini hasa ni lengo lake lakini kwa ambao tumebahatika kumfahamu japo kidogo, hatushtuki. Ukijaribu kumbana hapo atakuja na mengine na kuzua mapya ambayo hajaulizwa.
Mathalani ukimuuliza wakati Dr. Slaa anajiunga na Chadema na kuchaguliwa mbunge mwaka 1995, Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema na mchango gani aliweza kuutoa kulinganisha na Mbunge Dr. Slaa. Katika uchaguzi uliofuatia mwaka 2000 Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema na mchango wake ulikuwa upi katika kukiimarisha chama kipindi hicho.
Sasa humu unamkuta mtu kama Ritz anarukia hata vile asivyovijua kwa kumuunga mkono eti akina Dr. Slaa walikuwa wamelala wakati Zitto anajenga chama. Kugombea Uraisi kwa Mbowe mwaka 2005 ndiko kulikozidi kukitangaza chama hadi Zitto kuukwaa ubunge kwani mashina tayari yalikuwepo Kigoma toka wakati wa Dr. Kabourou.
Katika jukwaa hili la GT tungejitahidi kupunguza ulaghai kwa kutoandika tunayojua moyoni kwamba si ya kweli lakini kwa makusudi tunafanya hivyo. Tukumbuke kwamba wwaka 1995 Chadema haikutoa mgombea wa Uraisi na hivyo hivyo mwaka 2000. Ushupavu wa wabunge kama Dr. Slaa ndiko kulifanikisha kukiimarishana na kukijenga chama zaidi.
Last edited by a moderator: