Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Kama kumbukumba zangu ziko sawa katiba ilibadilshwa Mwaka 2006... (I stand to be corrected)
Hivi Alinda humjui Mkandara? Anajua kabisa katiba ilibadilidhwa lini na wakati huo Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema. Anajua kabisa ni lini Zitto alitaka kugombania uenyekiti wa Chadema na kushauriwa asubiri na wazee. Anajua ni lini waraka wa usaliti ulitayarishwa. Anajua timeline ya Chadema toka kuanzishwa kwake. Anajua yote hayo.

Lakini kwa makusudi yasiyoeleweka ukimsoma ni kama vile anadai katiba ilibadilishwa baada ya Zitto kushauriwa asigombee. Kama humjui Mkandara unaweza kuumia ukijiuliza nini hasa ni lengo lake lakini kwa ambao tumebahatika kumfahamu japo kidogo, hatushtuki. Ukijaribu kumbana hapo atakuja na mengine na kuzua mapya ambayo hajaulizwa.

Mathalani ukimuuliza wakati Dr. Slaa anajiunga na Chadema na kuchaguliwa mbunge mwaka 1995, Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema na mchango gani aliweza kuutoa kulinganisha na Mbunge Dr. Slaa. Katika uchaguzi uliofuatia mwaka 2000 Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema na mchango wake ulikuwa upi katika kukiimarisha chama kipindi hicho.

Sasa humu unamkuta mtu kama Ritz anarukia hata vile asivyovijua kwa kumuunga mkono eti akina Dr. Slaa walikuwa wamelala wakati Zitto anajenga chama. Kugombea Uraisi kwa Mbowe mwaka 2005 ndiko kulikozidi kukitangaza chama hadi Zitto kuukwaa ubunge kwani mashina tayari yalikuwepo Kigoma toka wakati wa Dr. Kabourou.

Katika jukwaa hili la GT tungejitahidi kupunguza ulaghai kwa kutoandika tunayojua moyoni kwamba si ya kweli lakini kwa makusudi tunafanya hivyo. Tukumbuke kwamba wwaka 1995 Chadema haikutoa mgombea wa Uraisi na hivyo hivyo mwaka 2000. Ushupavu wa wabunge kama Dr. Slaa ndiko kulifanikisha kukiimarishana na kukijenga chama zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Mag3.

Nashukuru kwa kunitag takuambia kitu kimoja tatizo lenu nyie pro-Chadema Mbowe na Dr.Slaa wameishawapa upofu hata yale mambo ya msingi mnashidwa kuwa wa kweli.

Unasema mimi sijui chochote sasa wewe na msajili wa vyama sijui nani anajua zaidi haya masuala ya vyama msome kiduchu hapa chini msajili.

Dar es Salaam.-Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba- bila idhini na mkutano mkuu wa chama hicho. Mutungi alisema baada ya kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.“Mjadala kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao vya chini,” alisema Dk Slaa.Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba”Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.Alisema kama chama hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi kuitambua ibara hiyo.Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa kazi.“Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Dada demokrasia inamruhusu mtu yeyote kugombea Uenyekiti kwa sababu zake anazoziona yeye zinaweza kumpa ushindi. Kazi ya kamati za chama NEC ni kuchambua hizo sababu (sifa) kama kweli mtu huyo anafaa kuwa kiongozi.

Kumkataza mtu asigombee Uenyekiti kwa sababu mnazojenga wenyewe sio Demokrasia bali demokrasia ni kutomchagua mtu huyo, lakini ile haki yake ya kugombea inabakia pale pale. Mimi najua mengi sana ambayo yamefichwa fichwa kumbuka katiba ya mwanzo ya Chadema yenye kipengele hicho ya mwaka 2004, na Hivyo Ukomo wa kiongozi unaanzia pale sheria hii ilipokubaliwa lakini hawa jamaa zangu wakitetea hoja hiyo huanzia kurudi nyuma hadi mwaka 1995 kutaja viongozi wa zamani kabla ya sheria hiyo wakati kipengele hicho cha UKOMO kilikuwepo mwaka 2004, hivyo mgombea yeyote wa awali hatenguliwi na sheria kwa sababu itatazamwa nyuma alikuwepo miaka mingapi auawamu ngapi.

Ni utetezi wa kijinga tu maana mwisho wa siku yale yale walokuwa wakiyakataa kuwa ndio malengo yao na kusema haiwezekani wamerudi wenyewe kuchukua tena Uongozi. Haiwezekani katiba iandikwe mwaka 2004, ghafla miaka miwili tu baadaye Katiba mpya inaandikwa tena upya mkitegemea wanachama wataisoma yote na kuelewa kila kitu ndani yake. Mimi hapa hadi leo Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 sijaiweka kichwani iwe hiyo ya chama na yapo mambo nayagundua leo kuwa hayako sawa!.

Mambo ya katiba tutayaongelea wakati mwingine..

Kwa sasa tujikite katika hiyo video hapo juu.. Je ni haki mwanasiasa kukashfu wakazi wa eneo fulani kwa sababu yeyote ile?
 
Kama kuwaambia wananchi wa Arusha, Iringa na Singida wana midomo mirefu!

Aliposhambulia kanda anayoichukia tuliambiwa tuna chuki. Sasa waje akina Mkandara watueleze Iringa na Singida midomo mirefu yao ni ipi? Hapa anaaminisha nini!
 
Kwani Uongo? Kuna kosa gani ikiwa mkoa mzima ulikuwa chini ya CCM wakiishangilia na kuwachagua wabunge wake. Mbona Kamanda wenu alipokuja Dar alisema wakazi wa Pwani wamelala? akasema hadi chakula wanachokula ndio sababu? au hadi tuseme majina..

Ni mkoa gani huo ambao ulikuwa chini ya CCM na watu wote wakishangilia?

Katika kumbukumbu zangu, uchaguzi wa vyama vingi Mwaka 1995 Nccr ndicho chama kilichokuwa kina nguvu Tanzania bara na CUF Zanzibar na katika uchaguzi huo vyama vya upinzani viliweza kupata wabunge 55.

Nccr wabunge 19, CUf wabunge 22, UDP 3, Chadema 3 na 10 viti maalum.

Miongoni mwa wabunge hawa kuna Makongoro Nyerere Arusha mjini, Mabere Marando Rorya, James Mbatia Vunjo, Makidara - Siha, Kibaso Iringa, Joseph Mtui Moshi na nk. Sina kumbukumbu kuwa 1995 Kigoma waliweza kupata mgombea kutoka Upinzani.

Sasa swali kwako Je ni kweli wakati wanakigoma wako atika harakati za mageuzi, Arusha, Iringa na Singida walikuwa wamelalal?

Na kama walikuwa wakishangilia CCM ilikuwaje Makongoro na Kibaso wakachanguliwa kuwa wabunge kutoka Nccr?

Na katika kura za urais Mrema alipata asilimia 27.7 wakati Ben Mpaka akiwa na asilimia 61.... Je unataka kusema hizi kura alizopata Mrema zilitoka Kigoma tu?
 
Kama kuwaambia wananchi wa Arusha, Iringa na Singida wana midomo mirefu!

Aliposhambulia kanda anayoichukia tuliambiwa tuna chuki. Sasa waje akina Mkandara watueleze Iringa na Singida midomo mirefu yao ni ipi? Hapa anaaminisha nini!

Siasa za Zitto zitanichukua muda mrefu kuzielewa..
 
Ninachokiona hapa kuna watu wanaugua Zittophobia.

Wakati mwingine uwa nabaki nasoma tu na kuwasikitikia maana bila shaka Zitto amewapa makovu makubwa sana mioyoni mwao au anawatisha sana. Vinginevyo isingewezekana kwa karibu mwaka sasa Nguruvi, Alinda, Mchambuzi, Mag3, wao wakijadili ni Zitto, Zitto,Zitto,ZItto, please ebu mmove on, mnaweza kumpata Zitto mwingine, muacheni huyu Zitto aende njia aliyoichagua yeye.Chuki ni sumu.

Kwenye hiyo video nimeisikiliza tena na tena, na sioni ina ajabu gani kisiasa, unless kama hamtaki kutambua lugha za kisiasa.

Mosi, ni kweli ni mkoa wa Kigoma ndio mkoa wa kwanza Tanganyika kuonyesha upinzani haswa dhidi ya CCM, wakati mikoa mingine yote ikiwa ata hakuna dalili ya upinzani wowote, kwa lugha ya kifasihi ikiwa imelala, hii ni fact!

Pili, haihitaji ata kufika form 4 kujua kuwa "midomo mirefu" ni "lugha ya picha", kuweka hiyo kama issue ni kudharirisha ufahamu wetu."midomo mirefu" maana yake "anayeongea sana maneno ya uongo".

Sasa huishii hapo, hii ni lugha inayokurejesha kwenye tukio la "wanaongea sana uongo", inakuleta ni nani hao??anasema "ni hao wanaosema kuwa yeye ni msaliti na kuwa wao ndio wapinzani sanaaa", kuondoa doubt ya ni nani hao ndio anamalizia "yule anayetokea mkoa wa Arusha, Iringa n.k).Jamani!!hizi chuki zinafanya lugha rahisi kama hizi pia zisieleweke?kama mkirudi darasa la fasiri mkatafsiri hivyo basi zero ni halali yenu.

Otherwise, ushauri ni muhimu, lakini chuki ikizidi inaondoa maarifa.
 
Ni mkoa gani huo ambao ulikuwa chini ya CCM na watu wote wakishangilia?

Katika kumbukumbu zangu, uchaguzi wa vyama vingi Mwaka 1995 Nccr ndicho chama kilichokuwa kina nguvu Tanzania bara na CUF Zanzibar na katika uchaguzi huo vyama vya upinzani viliweza kupata wabunge 55.

Nccr wabunge 19, CUf wabunge 22, UDP 3, Chadema 3 na 10 viti maalum.

Miongoni mwa wabunge hawa kuna Makongoro Nyerere Arusha mjini, Mabere Marando Rorya, James Mbatia Vunjo, Makidara - Siha, Kibaso Iringa, Joseph Mtui Moshi na nk. Sina kumbukumbu kuwa 1995 Kigoma waliweza kupata mgombea kutoka Upinzani.

Sasa swali kwako Je ni kweli wakati wanakigoma wako atika harakati za mageuzi, Arusha, Iringa na Singida walikuwa wamelalal?

Na kama walikuwa wakishangilia CCM ilikuwaje Makongoro na Kibaso wakachanguliwa kuwa wabunge kutoka Nccr?

Na katika kura za urais Mrema alipata asilimia 27.7 wakati Ben Mpaka akiwa na asilimia 61.... Je unataka kusema hizi kura alizopata Mrema zilitoka Kigoma tu?

Mikoa mingine imeanza kuamka kisiasa katika uchaguzi wa 1995, Kigoma upinzani ulishakomaa immediately baada ya vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, kama ulikuwa unasoma magazeti wakati huo utakuwa ulikuwa unasikia mshikemshike wa Ujiji,wakiongozwa na Kabourou.Mikoa mingine wakati huo kulikuwa hakuna upinzani wowote wa maana kwa CCM.
 
Unajua nimepatwa na mshangao:

Kwamba watu wa Iringa, Arusha na Singida wana midomo mirefu???

Swali ninalojiuliza ni kuwa akienda Singida anatawambia kuwa "Nyie wana Singida fungeni midomo yenu mirefu kwani wakati wana Kigoma wanalalla jela nyie mlikuwa mnawakumbatia watawala?

Ni kweli, ni mpaka utakapoanza kuzifuatilia ukiwa open-minded, kwa sasa huwezi maana chuki imetawala akili.
 
Ninachokiona hapa kuna watu wanaugua Zittophobia.

Wakati mwingine uwa nabaki nasoma tu na kuwasikitikia maana bila shaka Zitto amewapa makovu makubwa sana mioyoni mwao au anawatisha sana. Vinginevyo isingewezekana kwa karibu mwaka sasa Nguruvi, Alinda, Mchambuzi, Mag3, wao wakijadili ni Zitto, Zitto,Zitto,ZItto, please ebu mmove on, mnaweza kumpata Zitto mwingine, muacheni huyu Zitto aende njia aliyoichagua yeye.Chuki ni sumu.

Kwenye hiyo video nimeisikiliza tena na tena, na sioni ina ajabu gani kisiasa, unless kama hamtaki kutambua lugha za kisiasa.

Mosi, ni kweli ni mkoa wa Kigoma ndio mkoa wa kwanza Tanganyika kuonyesha upinzani haswa dhidi ya CCM, wakati mikoa mingine yote ikiwa ata hakuna dalili ya upinzani wowote, kwa lugha ya kifasihi ikiwa imelala, hii ni fact!

Pili, haihitaji ata kufika form 4 kujua kuwa "midomo mirefu" ni "lugha ya picha", kuweka hiyo kama issue ni kudharirisha ufahamu wetu."midomo mirefu" maana yake "anayeongea sana maneno ya uongo".

Sasa huishii hapo, hii ni lugha inayokurejesha kwenye tukio la "wanaongea sana uongo", inakuleta ni nani hao??anasema "ni hao wanaosema kuwa yeye ni msaliti na kuwa wao ndio wapinzani sanaaa", kuondoa doubt ya ni nani hao ndio anamalizia "yule anayetokea mkoa wa Arusha, Iringa n.k).Jamani!!hizi chuki zinafanya lugha rahisi kama hizi pia zisieleweke?kama mkirudi darasa la fasiri mkatafsiri hivyo basi zero ni halali yenu.

Otherwise, ushauri ni muhimu, lakini chuki ikizidi inaondoa maarifa.

Ungefanya home work yako sawa sawa ungegundua katika hii topic watu tumejifunza mambo mengi sana na nafikiri ndicho kinachokufanya kuingia kuchungulia humu mara kwa mara.

Pili kinachojadiliwa hapa ni matendo ya Zitto na kauli zake.. Hakuna kashfa, hakuna matusi na hakuna kejeri.

Tatu hakuna mtu yeyote mwenye Ziittophiobia hizi kejeri zipeleke katika jukwaa la siasa. Hapa ni hoja tu bila kejeri au viloja.

Nne si kweli kuwa Arusha, Singida na Iringa walikuwa wamelala wakati Kigoma wanapigania mageuzi, rejea matokea ya mwaka 1995.

Tano hili ni swali. Je haya maneno aliyosema anaweza kwenda Singida, Arusha au Iringa kuyaongea?.. Hapa ninamaaanisha je anaweza kwenda Singida akawambia nyie mlikuwa mmelala wakati wanakigoma wako kwenye harakati za mageuzi hivyo acheni midomo mrefu?

Sita je hizi ndo aina za siasa kwa kizazi chetu kijacho?
Ni hayo tu.
 
Mikoa mingine imeanza kuamka kisiasa katika uchaguzi wa 1995, Kigoma upinzani ulishakomaa immediately baada ya vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, kama ulikuwa unasoma magazeti wakati huo utakuwa ulikuwa unasikia mshikemshike wa Ujiji,wakiongozwa na Kabourou.Mikoa mingine wakati huo kulikuwa hakuna upinzani wowote wa maana kwa CCM.

Kama walikuwa wameisha komaa kuliko mikoa mingine ilikuwaje katika hiyo mikoa ambayo upinzani ulikuwa haujakomaa/hakuna (kauli za Zitto haupo) wakapata wabunge wa upinzani na mkoa ambao siasa zimekomaa wakakosa mbuge hata mmoja wa kuwakilisha?
Naomba ufafanuzi wako tafadhali.
 
Kapwela, hebu twende taratibu...upepo wa mageuzi umeanza lini na wakati huo Kabourou alikuwa wapi? Unaweza kunitajia magazeti mawili tu yaliyokuwa mstari wa mbele katika harakati za mageuzi.
 
Last edited by a moderator:
Ungefanya home work yako sawa sawa ungegundua katika hii topic watu tumejifunza mambo mengi sana na nafikiri ndicho kinachokufanya kuingia kuchungulia humu mara kwa mara.

Pili kinachojadiliwa hapa ni matendo ya Zitto na kauli zake.. Hakuna kashfa, hakuna matusi na hakuna kejeri.

Tatu hakuna mtu yeyote mwenye Ziittophiobia hizi kejeri zipeleke katika jukwaa la siasa. Hapa ni hoja tu bila kejeri au viloja.

Nne si kweli kuwa Arusha, Singida na Iringa walikuwa wamelala wakati Kigoma wanapigania mageuzi, rejea matokea ya mwaka 1995.

Tano hili ni swali. Je haya maneno aliyosema anaweza kwenda Singida, Arusha au Iringa kuyaongea?.. Hapa ninamaaanisha je anaweza kwenda Singida akawambia nyie mlikuwa mmelala wakati wanakigoma wako kwenye harakati za mageuzi hivyo acheni midomo mrefu?

Sita je hizi ndo aina za siasa kwa kizazi chetu kijacho?
Ni hayo tu.

Kama walikuwa wameisha komaa kuliko mikoa mingine ilikuwaje katika hiyo mikoa ambayo upinzani ulikuwa haujakomaa/hakuna (kauli za Zitto haupo) wakapata wabunge wa upinzani na mkoa ambao siasa zimekomaa wakakosa mbuge hata mmoja wa kuwakilisha?
Naomba ufafanuzi wako tafadhali.
Kapwela, hebu twende taratibu...upepo wa mageuzi umeanza lini na wakati huo Kabourou alikuwa wapi? Unaweza kunitajia magazeti mawili tu yaliyokuwa mstari wa mbele katika harakati za mageuzi.

Nishakujibu huko mwanzo, juu ya "midomo mirefu", sitaki kuamini kama bado lugha ya picha hiyo haieleweki.

Pili, nimeishasema hapo juu, mikoa mingi hasa hasa Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mara na Kigoma kulikuwa na upinzani mkali kwenye uchaguzi wa mwaka 1995.Hakuna mtu atakataa hili.

Hoja hapa sio uchaguzi wa 1995, hoja iliyotolewa hapa ni kuwa "wakati kigoma upinzani umekomaa kwingine CCM ilikuwa imetamalaki", sasa la kujiuliza ni je hii ni kweli?jibu ni NDIYO, kabla ya mwezi wa 4 mwaka 1995 hakukuwa na upinzani wowote wa kuitisha CCM mikoa mingine.Ni kuanzia April 1995 ndipo takribani nchi nzima ilifufuka ghafla na kimbunga cha Mrema.

LAKINI Kigoma tayari kuliishakuwa na upinzani mkali sana toka mapema baada ya 1992, masuala ya kupigwa mabomu na watu kufungwa yaliishaanza Kigoma kabla ya mkoa mwingine wowote. Mwaka 1994 mbunge wa kwanza wa upinzani Tanganyika alichaguliwa Kigoma Mjini..Hii ni fact. Kukataa hili ni kuikataa historia.Weka kumbukumbu zako sawa.Katika uchaguzi wa mwaka 1995 Kigoma ilipata atleast wabunge watatu wa upinzani(sina kumbukumbu nzuri hapa).

Otherwise, ninaelewa ilivyo ngumu kuelewa kitu kama tayari umeishatanguliza "jibu" unalolitaka.ndilo tatizo lililoko hapa.
 
Nakumbuka hii kauli ya Obama akimzungumzia Hillary Clinton mwaka 2008 kuwa "YOU CAN PUT LIPSTICK ON A PIG. IT'S JUST A PIG", kwa mlinganisho usio rasmi hapa inamaana tungesema Obama kamuita Hillary Clinton kuwa ni nguruwe. Lugha za picha.
 
Huko sahihi Mbunge wa kwanza kukaa upande wa upinzani baada ya vyama vingi kuruhusiwa ni Kaburu, mwaka 1994 Alinda amelisishwa ubishi na wenzake,maana ukisoma maelezo yake,anataja wabunge wa upinzani wa Arusha,Kilimanjaro,ila kwa kigoma hajataka kujishughulisha,wakati hizo amegoogle,kwanini hasigoogle na kigoma,nilichogundua,baada ya kutuvutiwa na Zitto,sasa hivi wanaichukia hata na historia ya upinzani kutoa mbunge wa upinzani kutoka kigoma,wanatamani angetoka mikoani kwao huko,huzi ulishapotea njia huu,tokea Zitto alipo amia ACT
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka hii kauli ya Obama akimzungumzia Hillary Clinton mwaka 2008 kuwa "YOU CAN PUT LIPSTICK ON A PIG. IT'S JUST A PIG", kwa mlinganisho usio rasmi hapa inamaana tungesema Obama kamuita Hillary Clinton kuwa ni nguruwe. Lugha za picha.
Hivi mtu asimame na kusema mikoa fulani ina maendeleo, hata hivyo mikoa inayochangia abcd inapata zaidi. Hakuna ushahidi, tumeomba hapa jamvini hakuna aliyeleta
Takwimu zote zinakataa, hesababu za darasani, kijiograifia n.k. zinakataa

Leo utuambie kauli hiyo ni 'lip stick...''

Tatu, hivi unataka tukae kimya huyu kijana akilimega taifa eti tu move on! nani atakemea!

Nne, kauli zinatoka kwa nani, sisi au yeye? Kwani hukumbuki mshauri wake Kitila alisema nini na mlezi wake Baregu alisema nini.

Tano, huyu mtu anayetaka uongozi wa taifa huku nyuma akimega mega taifa anatufaa kwa mtazamo wako?
 
Ni mkoa gani huo ambao ulikuwa chini ya CCM na watu wote wakishangilia?

Katika kumbukumbu zangu, uchaguzi wa vyama vingi Mwaka 1995 Nccr ndicho chama kilichokuwa kina nguvu Tanzania bara na CUF Zanzibar na katika uchaguzi huo vyama vya upinzani viliweza kupata wabunge 55.

Nccr wabunge 19, CUf wabunge 22, UDP 3, Chadema 3 na 10 viti maalum.

Miongoni mwa wabunge hawa kuna Makongoro Nyerere Arusha mjini, Mabere Marando Rorya, James Mbatia Vunjo, Makidara - Siha, Kibaso Iringa, Joseph Mtui Moshi na nk. Sina kumbukumbu kuwa 1995 Kigoma waliweza kupata mgombea kutoka Upinzani.

Sasa swali kwako Je ni kweli wakati wanakigoma wako atika harakati za mageuzi, Arusha, Iringa na Singida walikuwa wamelalal?

Na kama walikuwa wakishangilia CCM ilikuwaje Makongoro na Kibaso wakachanguliwa kuwa wabunge kutoka Nccr?

Na katika kura za urais Mrema alipata asilimia 27.7 wakati Ben Mpaka akiwa na asilimia 61.... Je unataka kusema hizi kura alizopata Mrema zilitoka Kigoma tu?
Kuweka kumbukumbu sawa NCCR Mageuzi hawakupata viti hivyo 19.

Uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi 1995, Chama tawala cha CCM kilipata viti 186, CUF viti 24, NCCR MAGEUZI viti 16, CHADEMA viti 3, UDP viti 3 na TLP kiti 1.
 
LAKINI Kigoma tayari kuliishakuwa na upinzani mkali sana toka mapema baada ya 1992, masuala ya kupigwa mabomu na watu kufungwa yaliishaanza Kigoma kabla ya mkoa mwingine wowote. Mwaka 1994 mbunge wa kwanza wa upinzani Tanganyika alichaguliwa Kigoma Mjini..Hii ni fact. Kukataa hili ni kuikataa historia.Weka kumbukumbu zako sawa.Katika uchaguzi wa mwaka 1995 Kigoma ilipata atleast wabunge watatu wa upinzani(sina kumbukumbu nzuri hapa).

Otherwise, ninaelewa ilivyo ngumu kuelewa kitu kama tayari umeishatanguliza "jibu" unalolitaka.ndilo tatizo lililoko hapa.
Kapwela uchaguzi wa kwanza kabisa kufanyika baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na upinzani kushinda ulikuwa ni wa serikali za mitaa mwaka 1994. Aliyeshinda uchaguzi huo na kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa kijiji kupitia chama cha Chadema aliitwa Simon Kibola aliyeshinda na kuwa Mwenyekiti wa Kijiji kinachoitwa Gongali huko Karatu.

Chama cha Mapinduzi hakikuamini kwamba kingeweza kushindwa na hivyo uchaguzi kurudiwa mara nne chini ya usimamizi wa defenda za polisi kutoka Arusha. Ilibidi uchaguzi wa wazi ufanyike baada ya wana Karatu kukomaa na kumkataa kabisa mgombea wa CCM.

Kwa kumbukumbu Dr. Slaa mwaka 1995 alichaguliwa kuwa mbunge pia kupitia Chadema alikohamia baada ya chama chake cha CCM kumletea mizengwe. Katika uchaguzi huo wabunge machachari Masumbuko Lamwai na Mabere Marando walichaguliwa kupitia chama cha NCCR Mageuzi.

Sijui hii ya Kabourou kuchaguliwa mwaka 1994 unaipata wapi lakini ni wazi watu wa Karatu ndio wanaweza kupewa sifa kwa kuvunja mwiko wa CCM kushindwa kwenye uchaguzi wowote ule. Sasa na wewe naomba uje hapa na facts jinsi wana Kigoma walivyopigwa virungu kwa kuunga mkono mageuzi.

Katika wabunge waliochaguliwa mwaka 1995 kutoka Upinzani, wengi kwa ulafi walirudi CCM isipokuwa wanamageuzi wa kweli ambao walikataa vishawishi vya CCM na hadi leo tunao wakiongoza Upinzani katika nyadhifa mbali mbali.
 
Last edited by a moderator:
Huko sahihi Mbunge wa kwanza kukaa upande wa upinzani baada ya vyama vingi kuruhusiwa ni Kaburu, mwaka 1994 Alinda amelisishwa ubishi na wenzake,maana ukisoma maelezo yake,anataja wabunge wa upinzani wa Arusha,Kilimanjaro,ila kwa kigoma hajataka kujishughulisha,wakati hizo amegoogle,kwanini hasigoogle na kigoma,nilichogundua,baada ya kutuvutiwa na Zitto,sasa hivi wanaichukia hata na historia ya upinzani kutoa mbunge wa upinzani kutoka kigoma,wanatamani angetoka mikoani kwao huko,huzi ulishapotea njia huu,tokea Zitto alipo amia ACT
Na mwaka 1993 wakati Zitto anajiunga na Chadema alikuwa kidato cha tatu Dr.Slaa alikuwa anawakumbatia watawala "CCM" Tundu Lissu huko Singida sijui alikuwa wapi.
 
Last edited by a moderator:
Kapwela uchaguzi wa kwanza kabisa kufanyika baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na upinzani kushinda ulikuwa ni wa serikali za mitaa mwaka 1994. Aliyeshinda uchaguzi huo na kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa kijiji kupitia chama cha Chadema aliitwa Simon Kibola aliyeshinda na kuwa Mwenyekiti wa Kijiji kinachoitwa Gongali huko Karatu.

Chama cha Mapinduzi hakikuamini kwamba kingeweza kushindwa na hivyo uchaguzi kurudiwa mara nne chini ya usimamizi wa defenda za polisi kutoka Arusha. Ilibidi uchaguzi wa wazi ufanyike baada ya wana Karatu kukomaa na kumkataa kabisa mgombea wa CCM.

Kwa kumbukumbu Dr. Slaa mwaka 1995 alichaguliwa kuwa mbunge pia kupitia Chadema alikohamia baada ya chama chake cha CCM kumletea mizengwe. Katika uchaguzi huo wabunge machachari Masumbuko Lamwai na Mabere Marando walichaguliwa kupitia chama cha NCCR Mageuzi.

Sijui hii ya Kabourou kuchaguliwa mwaka 1994 unaipata wapi lakini ni wazi watu wa Karatu ndio wanaweza kupewa sifa kwa kuvunja mwiko wa CCM kushindwa kwenye uchaguzi wowote ule. Sasa na wewe naomba uje hapa na facts jinsi wana Kigoma walivyopigwa virungu kwa kuunga mkono mageuzi.

Katika wabunge waliochaguliwa mwaka 1995 kutoka Upinzani, wengi kwa ulafi walirudi CCM isipokuwa wanamageuzi wa kweli ambao walikataa vishawishi vya CCM na hadi leo tunao wakiongoza Upinzani katika nyadhifa mbali mbali.
Na wabunge wa kwanza wa Chadema kuingia bungeni wanatoka mikoa gani?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom