Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Mkuu Mkandara.Ritz,
Shukran sana sasa sina sababu ya kuendelea na ubishi huu baada ya kutazama bandiko lako na Adharusi kuwa sawa kabisa japo Adharusi kachukua vipande vipande. Tazama sehemu nilizo highlight.. Ama kweli nimeamini watu wamepania kumharibia jina kwa sababu wewe umetoa hotuba kamili, Adharusi kazungumzia wapi takwimu zake zinapatikana maana waliuliza Zitto kazipata wapi kwa sababu hawakuamini. sasa wamepewa bado wamekazania kipande ambacho hakipo ktk hotuba yake.. iweje wewe na Adharusi ndio muwe na hotuba lakini hawa jamaa na madai yao hawana hotuba hiyo? Kumbe alicholinganisha Zitto ni mkoa wa Lindi na Shinyanga sio kama walivyodai eeeh...
Hotuba ya zitto uloitoa wewe;-
" Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP. Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba. Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.'
Alichoandika Adharusi:-
Nanukuu maelezo ya Zitto
"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa,pia akasema Mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.
Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.
" Zitto akasisitiza ndio mana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi,huwezi kuwa na mkoa unashika nafasi ya 4 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namna 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu,Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi,ina Ng'ombe na Pamba.
Tunavita moja tu,kufanya Mapinduzi ya mfumowetu was uchumi kutoka mfumo wa kinyonyaji na kifisadi na kujenga uchumi shirikishi.
Zitto aligusia Takwimu za watu wenye elimu ya sekondari simiyu ni 3.7%, na Dar ni 29% inaongoza nchi mzima(THDR2014)
Hii hotuba ya Zitto ni ulimbo lazima unase kwenye mtego ndiyo maana makamanda hawataki hata kuiona achalia mbali kuisoma.
Last edited by a moderator: