Hivi u Ukaskazini mnautoa wapi?maana nautafuta siuoni, nimesoma maelezo ya Zitto sioni, ndio maana nazidi kupata mashaka sana na Utanzania wa baadhi yetu, maana kutafsiri jambo la kisera na kimfumo kwa muktadha wa Ukaskazini?hii inasikitisha sana.
Na kingine hiki kinanishangaza zaidi, kwanini Lindi isiwe issue?maana alipotaja Kilimanjaro ndipo alipotaja Lindi pia?sasa kwanin iibuke hoja tu ya Ukaskazini lakini isiibuke hoja ya Ukusini?kuna tatizo kubwa hapa.
Ni wazi kuwa kuna watu wanatafuta excuse ya kuonyesha jinsi wasivyo wa-taifa kwa kulazimisha ata kisichokuwepo.Tunahitaji kuondoa hii kitu mioyoni mwetu, maana wakati mwingine unaweza ukakiona kitu sio kwa sababu kipo kwa mwingine bali ni kwa sababu kipo ndani yako.Hiki tukiondoe!!
Na pia tusiwawekee watu maneno ambayo hawajayasema, mfano wa Ukaskazini na chuki kwa Ukaskazini, kama tunahitaji Ukaskazini tuseme wazi kama Nassari, tusiwasingizie wengine. Ebu tulishike neno hili la busara la Alinda hapa chini.
Hayo ya power struggle ndani ya Chadema sio rahisi kwetu ku-conclude lolote.
Kwenye taasis yeyote kuna vitu vya ndani ambayo kwa mtu asiye kwenye inner-cycle hawezi kujua.
Ndivyo ilivyo ngumu kwangu na labda kwetu juu ya hayo ya chumba cha ndani cha Chadema.
Ni vizuri tu tuweke benefit of doubt kwa pande zote kisha tusonge mbele.
Hakuna mtu yeyote utamsikia analalamikia Usingida wala U-Iringa.Mtu yeyote atatambua kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa dhidi ya Msigwa na Lissu.
Nguruvu, Alinda: Najua mu watu makini sana, na yawezekana kabisa mna Utanzania ndani yenu.Lakini kauli hizi humu ndani badala ya kujenga zitazidi kujenga utengano wa kijamii.
Kuna watu humu wanaosoma ambao kwa maelezo ya humu watapata picha tofauti na badala ya kujenga ndio kwanza tunabomoa zaidi.Tusiwe watetezi wa Kanda.Tuwe wa Tanzania kwanza.
Mkuu kwanza, lazima ukumbuke zilikuwepo hisia za udini na ukanda katika chama cha Zitto.
Alinda yupo hapa, aliwahi kufanya mazungumzo naye na hakukanusha. Karata hiyo imetumiwa sana na CCM.
Hivyo suala la ukanda chimbuko lake ukiliangalia kwa undani si CCM
Pili, Kama uliangalia hotuba zote zilizoletwa hapa jamvini, ile ya Shinyaga Zitto alikwenda moja kwa moja Kilimanjaro na Arusha bila kuwa na utaratibu. Mfano, aliongelea Mikoa hiyo kuchangia pato kidogo na kuwa na maendeleo. Akasema katika uchangiaji ni namba 7 na 9 na maendeleo ipo juu. Hakueleza nafasi katika maendeleo, neno juu ni la jumla.
Lengo lilikuwa kuwaacha wasikilizaji waamue juu ni namba 1 ,2 au 3.
Katika uchangiaji, tukauliza mbona amekwenda namba 7 na 9 akiacha 1-6? Tukapewa majibu ya kubabaisha
Tunaweza kusema kwa dhati kabisa hilo la Lindi, sijui umelitoa wapi, hotuba ya Shinyanga au Mwanza maana kuna version nyingi.
Hata taarifa ya habari ya TV(clip ipo nadhani ilikuwa Tabora) , ilipofika katika eneo la mikoa tajwa ilikatwa haraka ili kuondoa hisia na kujenga utaifa. Tunaelewa hilo.
Suala la Lindi tunadhani unalileta kufunika uchafu, ukweli ni kuwa Zitto alikwenda straight kwenye maeneo anayolenga yeye
Kuhusu power struggle, hilo hatujui na ndio maana tunasema yeye na wenzake wamalizane huko bila kuwahusisha wananchi.
Ukiangalia clip ya Alinda, kwa tafsiri yako Zitto alikuwa katika mtifuano wa ndani na watu wake. That's ok.
Hatukubali mtifuano huo uchukue sura ya mikoa. Huwezi kumfanya Lissu kama Singida kwa kisingizio cha tifu la chama.
Huwezi kuwaendelea kombo wananchi wa Iringa kwasababu ya Msigwa. Zitto ndiye anajenga hisia na chuki zote hizo
Kuhusu Utanzania wetu, nakuhakikishia kwangu Tanzania ni alpha and Omega.
Ndiyo nchi niliyozaliwa nakikakulia na ninaishi. Tumekuta wananchi wanaishi kwa Utangamano mkubwa.
Nimeishi nje ya mkoa wangu karibu asilimia 70 ya miasha.
Leo akitokea mjinga anaanza kutugawa kwa ukabila na ukanda, sitafumba macho
Katika vita ya kumpigania mama Tanzania, tutakuwa watu wa mwisho waliosimama kabla ya 'silaha' zetu hazijawa kimya.
Yes silaha ya kukemea na kupingana na wale wanaotaka kuivuruga Tanzania .
Tunaomba watu wanaosoma, waelewe kuwa hoja hapa ni kujenga Utanzania, kukemea aina au kiashiria chochote kile kinachochoea hisia au utengano.
Tusemezane