Duru za siasa iii: Kifo cha mandela na yaliyotokea

Duru za siasa iii: Kifo cha mandela na yaliyotokea

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
HOTUBA YA RAIS 2013 DEC 31
https://www.jamiiforums.com/great-t...iasa-hotuba-ya-jk-mwisho-wa-mwaka-2013-a.html
KIFO CHA MANDELA NA YALIYOTOKEA
https://www.jamiiforums.com/newthread.php?do=newthread&f=11
SAKATA LA MAWAZIRI KUFUKUZWA NA KUJIUZLU
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/572764-duru-za-siasa-sakata-la-mwaziri.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...pecial-mgogoro-kambi-ya-upinzani-chadema.html
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/308989-duru-za-siasa-matukio.html
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/167157-duru-za-siasa-mgongano-wa-mawazo.html



DURU III: KIFO CHA MANDELA

Wana duru za Siasa
Yatakuwepo mabandiko matano mfululizo yakizungumzia tukio kubwa la kifo cha mwanaharakati na mwanasiasa Nelson Madiba Mandela.

Madiba alifariki tarehe 5 Dec na anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Qunu siku ya Jumapili.
Maadhimisho ya kifo chake yamefanyika na yanaendelea kufanyika katika miji ya Johanesburg na Pretoria kuelekea Cape Town katika viunga vya Qunu atakapopumzishwa milele.

Maadhimisho na kuenziwa kwa Mandela ni moja ya matukio makubwa kuwahi kutokea duniani kwa kuwakutanisha viongozi wa mataifa zaidi ya 100 marafiki na mahasimu.Vyombo vyote vikubwa vya habari duniani vilibeba habari inayomhusu Nelson Mandela.

Kumbu kumbu katika alama zinazojulikana kama London tower, Eiffel Tower, Dow Jones, English Premier league na nyingi zilisimamisha shughuli kwa heshima ya Mandela.
Ni tukio lenye mvuto wa aina yake ambalo sasa linazua maswali zaidi kuliko ilivyodhaniwa.

Wapo wanaohoji ni kwanini Mandela aliyekuwa gerezani nchi zikikombolewa Afrika apewe heshima kubwa kiasi hicho.

Zipo hoja, lipi kubwa alilofanya Mandela akilinganishwa na Manguli wengine duniani wa harakati za haki na usawa.

Mandela ana tofauti gani kubwa zaidi ya wanaharakati na viongozi wengine duniani.

Madiba amefanya nini katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi kama rais kiasi cha kupewa heshima hiyo ya kushangaza

Je, alikuwa mpigani haki na usawa au alibadilika kuwa mamluki wa nchi za Magharibi

Je, kulikuwa na mkataba kati yake na makaburu wa kulindana baada ya kuachiwa kutoka kifungoni(usaliti)

Je, Mandela ameisadia vipi jamii ya Afrika kusini iliyoishi kwa mateso kwa karne nyingi za ubaguzi wa rangi.

Maswali ambayo ni 'intriguing' yanahitaji mjadala endelevu.

Tatizo linaloonekana kwa baadhi yetu ni kuchukua jambo moja na kulifanya kama legacy ya Mandela.
Mathalani, wapo wanaodai umasikini haujabalika Afrika kusini na hilo ni dalili ya kushindwa kwa sera za Madiba.

Wapo wanaomtazama Madiba kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita na kufikia hitimisho kuhusu legacy yake.

Wapo wanaojaribu kuweka viongozi wa kisiasa katika mizani kama jiwe la kupimia na sukari upande mwingine.

Zipo hoja zisizo na takwimu zinazomhukumu Madiba.

Katika mfululizo wa mabadiko yajayo tutajaribu kuangalia historia ya Madiba kwa ufupi na kuaiangalia nchi hiyo kabla na baada ya Madiba. Tutaangalia hali na nyakati mbali mbali tukizingatia hoja zilizotolewa hapo juu kumhusu Madiba na kupitia moja baada ya nyingine kwa kupanuana mawazo na fikra.

Tutaangalia kama tuna cha kujifunza kutokana na maisha ya Madiba, harakati na ujumla wa matukio yaliyojiri.

Baada ya hapo wanajamvi mtakaribishwa ili tusemezane.
Kama ada ni hoja kwa hoja, kupingana bila kupigana, kuheshimu hoja ya mwingine hata kama hukubaliani nayo na kukosoana bila kukoseana.

Let us get started, mabandiko yataanza jioni hii na siku zinavyoendelea, tunaomba uvumulivu.

Karibuni sana.
 
Wakati tunamkumbuka na kumuenzi Mandela, tutumie fursa hii kureflect jinsi tunavyoangalia matendo ya wanaharakati na nafasi tunayoyapa matendo hayo katika kumbukumbu zetu. Nikisema hivyo naomba tujiulize je, Malcolm X si mtu anayestahili kukumbukwa kwa heshima?

Je, ni sahihi kwa "mainstream opinion" kumfuta kabisa Malcolm X kwenye historia ya wanaharakati waliopiga vita ubaguzi wa rangi?

Je, tunamuenzi Mandela kwa Urais alioupata au kwa harakati alizozifanya? Je, Mandela asingepata Urais tungethamini harakati zake?

In my view, Malcolm X anaotoa picha ni jinsi gani Mandela angekumbukwa iwapo asingeupata Urais.
 
Wanaduru,
Kabla ya kuangalia siku za nyuma na maisha ya Mandela, tungependa tuzungumzie tukio moja linalohusiana na msiba.
Tukio hilo linawiana na matukio kadhaa yaliyotokea nchini.
Tunafanya hivyo ili kuona namna gani mataifa mengine yalivyo serious katika shughuli zinazohusu maisha na taswira za mataifa yao.

Yupo mfasiri(intepreter) aliyekuwa karibu na viongozi waliotoa rambi rambi zao akiwemo Rais Obama.
Mfasiri aliteuliwa na serikali ya SA kwa kupitia wakala (Agency).
Imesemwa alishafanya ufasiri katika matamasha mengi makubwa.
Mfasiri alishindwa kutumia lugha ya kuwasiliana na watu wasiosikia(viziwi) na hicho kikawa chanzo cha kumhakiki.

Vyombo vya habari Marekani zimelishikia bango suala hili kwa kuelewa mfasiri alikuwa mita chache karibu na Obama.
Wengi wanadhani ni hofu ya US inayowasukuma kumlinda kiongozi wao.

Taatibu za secret service zinasema anayemkaribia Rais wa Marekani lazima wasifu na wajihi wake ujulikane masaa 48 kabla ya kukutana naye au kuwa na ukaribu wa aina yoyote. Ni kwa ajili ya usalama wa rais.
Kwa wamarekani rais ni taswira ya nchi, ni alama ya taifa na si mtu binafsi.

Marekani imeihoji serikali ya South Africa kuhusu mfasiri huyo na SA haikuwa na majibu zaidi ya uchunguzi unaendelea.
Wakala amefunga ofisi na hajulikani alipo. Wakati huo huo mfasiri amejitokeza na kusema anaumwa schizophrenia ambayo ni maradhi ya akili na kwamba alikuwa akiona malaika weusi wakimvamia, kwa lugha za mtaani alipoteza network

Wanaduru, FYI neno Schizophrenia linatumiwa na wataalam wa afya kwa kifupi cha schiz na watu wa mitaani wakalibeba kwa kusema ni Chizi. Ndio asili ya neno chizi. Kwa mantiki hiyo mfasiri alipata uchizi wakati akiendelea na kazi.

Kauli ya mfasiri kupata uchizi inazidi kuwachefua wamarekani kwani Obama alikuwa karibu na chizi na hiyo ni hatari kwa usalama wa rais. Sakata linaendele na huenda watu walioambatana na msafara wa rais baadhi wakapoteza kazi.

Tukio hilo ni kama lile la watu waliozamia dhifa ya kitaifa ya rais Obama na waziri mkuu wa India bila kualikwa, na mkuu wa shughuli za Ikulu (white house) bibi Desiree alilazimika kujiuzulu kutokana na kutokuwa makini hadi watu wanamkaribia rais wa Marekani.

Wapo watakaosema haya ni majigambo na ya Marekani. Atakayefikiri hivyo amekosea, rais ni alama ya taifa lolote.
Rais JK atakapotokea katika baraza la umoja wa mtaifa (UN) akiwa amevaa malapa na shati lisilo na vifungo, hiyo ni Tanzania si JK tena. Na kila habari itahusu Tanzania na si JK kwasababu JK ni mtu anayesimama kama alama ya taifa.

Mnakumbuka rais Kikwete alipokuwa Moshi msafara wake ulijaza mafuta ambayo yalibainika kuwa na matatizo (Chakachuliwa). Tatizo la kuchakachua ni la muda mrefu lakini lililpoingia kwa rais ilikuwa ni hatari zaidi na wake up call kwa serikali kuwa lipo tatizo la kufanyia kazi haraka.

Mwaka mmoja baada ya tukio la Moshi, tukio kama hilo limemtokea katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani Dr Slaa.
Ni takribani wiki tatu zilizopita. Msafara wake ulichelewa kufika kwasababu walijaza mafuta yaliyochakachuliwa.

Hii maana yake ni nini?
Maana yake ni kuwa hakuna kiongozi aliyewahi kufanyia kazi malalamiko ya wananchi kuhusu uchakachuaji wa mafuta.
Hakuna mtu au mamlaka iliyofanyia kazi rais wa nchi kuwekewa mafuta feki na usalama wake kwa ujumla
Hata wapinzani nao wanaonekana kuliona ukio la Dr Slaa kama la kawaida tu
Hakuna aliyewahi kuwajibishwa kwa kuchakachua mafuta
Uchakachuaji ni sehemu ya maisha yetu
Hakuna mbunge anayeliona kama tatizo

Kwa ufupi ni business as usual, hakuna usalama wala uchumi wa nchi.

Tunapata funzo gani?
Wenzetu wanafanyakazi kwa utaratibu na akili. Mamlaka zinawajibika kama ilivyo kwa vyombo vya habari.
Sisi hakuna kuwajibika kila tukio ni kazi ya mungu, hata kuchakachua mafuta ni kazi ya mungu au yatapita kama upepo

Usalama wa rais unakuwa mashakani hakuna anayewajibishwa .
Wananchi wanapoteza pesa kwa kununua vipuri vya magari yao kutokana na mafuta feki.
Ni tatizo linalogusa mtu binafsi na usalama wake, uchumi wa mtu binafasi na wa taifa.

Wenzetu wakihoji kwanini rais wao amekaribiwa na chizi, sisi hatujafika huko labda tuanze kuhoji kwanini rais wetu anawekewa mafuta feki, yeye na serikali anayoiongoza ione ni poa tu!
Tuna tatizo kubwa la nchi hii.
 
MAISHA YA MANDELA

Sehemu ya I

Mandela amefariki na umri wa miaka 95, akiwa ni muumini wa protestant (Methodist) ambalo ni tawi la Anglican.
Methodist wanaamini katika kujenga mahusiano ya waumini wao kwa njia za kutoa huduma kwa jamii.
Nelson ni jina alilopewa na mwalimu wake katika shule ya mishenari

Mandela ni wa ukoo wa Thembu, kabila la Xhosa kutoka jimbo la Eastern cape.
Madiba alizaliwa Mvezo na atapumzishwa Qunu alikokulia.Alitoka katika familia ya kifalme

Mandela ameoa mara tatu, mkewe wa kwanza akiwa Evelyn Mase,mtoto wa mwanaharakati Sam Mase.
Evelyn ni binamu yake Walter Sisulu.

Walter Sisulu alikuwa Shombe, mama yake mweusi kutoka familia ya akina Mase wa Thembu na baba yake Mzungu.
Kwa kufahamiana na Sisulu, Mandela alimfahamu Evelyn na ndio ukawa mwanzo wa ndoa.

Evelyn walitalikiana na Mandela mwaka 1957 na mwaka uliofuata alimuoa Namzamo Madikizela Winnie.
Tangu wakati huo Namzamo aliingia katika harakati za kupinga ubaguzi.
Alitalikiana na Mandela mwaka 1996 kumuoa Graca Machelle katika umri wa miaka 80

Mandela alimpoteza baba yake akiwa bado mdogo na hivyo kumlazimu kulelewa na chief.
Ni kuanzia hapo ndipo alipopata fursa ya kwenda shule za mishenari.

Katika siku za karibuni kumekuwa na kugombea nafasi katika familia ya Mandela.
Mjukuu wake anayeonekana katika mazishi mara nyingi anaitwa Mandla.
Baba yake ni Makgatho Mandela ambaye ni mtoto wa Mandela kwa Evelyn.
Mandla kwasasa ni chifu wa Mvezo alikozaliwa Mandela.
Baba yake Makgatho na bibi yake Evelyn wote ni marehemu.

Ugomvi mkubwa wa familia ni ukweli kuwa Winnie ana watoto wawili Zenani na Zindzi.
Zenani ni mwanadiplomasia na mtoto wa Maendela aliyeingia katika siasa katika kiwango cha juu.
Zindzisiwe anaonekana kuwa msemaji na mwenye umaarufu kupitia jina la baba yake.

Ugomvi wa watoto wa Namsamo Winnie na Evelyn( mjuu Amandla) na wanafamilia wengine imekuwa na mvurugano wa hali ya juu hata kuitia familia aibu wakati Mzee Mandela akiwa mahututi.

Kinacholeta taabu ni jina la Mandela, kila upande ungependa kumiliki jina hilo kwa kuzingatia umuhimu wake katika siasa za zamani na sasa. Kwa Mandela aliyewahi kupokea tuzo za heshima zaidi ya 250, jina lake si tu lina umuhimu bali ni chanzo kizuri sana cha mapato hata utajiri.

Ukiangalia maisha ya Mandela, tangu amemuoa Evelyn mwaka 1944, Madiba amekuwa katika harakati za kupinga ubaguzi akikabiliwa na misuko suko tangu mwanzo, ikipamba moto miaka ya 50 kabla ya kifungo miaka 60 hadi 90.
Ni wazi kuwa hakuweza kutumia muda wake kuishi na familia.

Hakuna mtoto wa Mandela anayeweza kusema aliishi na malezi ya Mandela kama baba kwa miaka 10.
Sehemu kubwa ya maisha yake ilikuwa ya kisiasa.
Ukichanganya na misuko suko ya ndoa mbili za awali, Madiba hakuwa na amani ya ndoa kwa muda mrefu.

Mandelea aliishi na Evelyne kwa miaka 14, Namzamo Winnie kwa miaka chini ya 6 kabla ya kifungo, Graca kwa miaka 15.
Katika umri wa miaka 95 Mandela aliishi na wanawake kwa jumla ya miaka 35 ikimaanisha miaka 60 ikiwemo ya utoto na ujana na ile ya kifungoni hakuwa na familia.

Hiyo inadhihirishwa na kauli zake mwenyewe alipohojiwa na kusema anajutia sana kutokuwa na familia imara na kwamba shughuli za kisiasa zilichukua sehemu kubwa sana ya maisha yake.

Watoto wake waliobaki wamekaririwa mara nyingi wakisema Mandela hakuwa na ukaribu na familia hata alipoachiwa.
Ilikuwa ni kama anaanza kujifunza namna ya kuishi na familia kwa mara nyingine.

Migogoro inayojitokeza ya nani arithi ni kielelezo kuwa Mandela baada ya kuachiwa alitumia muda mwingi katika shughuli za kimataifa zaidi ya za kifamilia.

Inaweza kuwepo hoja kuwa kwanini alishindwa kuwa karibu na familia hata baada ya kuachiwa.
Jibu lake ni kuwa mtu huyo alitumia muda mwingi kuwa mbali na familia na hivyo hakuweza kupitisha zile thamani za malezi kwa watoto na wajukuu hata kama walikuwa wakubwa.

Katika kuhitimisha sehemu fupi ya maisha ya Mandela, tukumbuke kuwa licha ya kutoweza kulea familia, Madiba alipoteza ndugu wengi wakati akitumikia kifungo. Ksaikolojia hilo nalo lilimuathiri sana baada ya kutoka kifungoni.

Kwa upande wa familia maisha ya mandela hayakuwa kama inavyodhaniwa, yalijaa misuko suko kwa namna tofauti.
Hata aliowategemea kama akina Winnie nao walimsaliti jambo lililoongeza uchungu katika sehemu yenye uchungu tayari.

Ni kwa bahati tu Mandela aliweza kumzika mkewe wa kwanza Evelyn Mwaka 2004, watoto wake na mjukuu aliyefariki katika usiku wa mkesha wa Kombe la dunia. Sehemu kubwa ya marafiki na ndugu waliondoka bila uwepo wake.


Hebu tuangalie maisha yake ya kisiasa kuanzia alipoingia Johansburg katika bandiko linalofuata.

Itaendelea. Sehemu Ia
 
Nguruv3;

Katika utafiti wangu, viongozi waliowahi kuwa wanasheria na kutumia ujuzi wao mahakamani wana mtazamo mwingine wa maisha na wanakuwa ni viongozi wazuri. Mfano mkubwa ni Mandela, Gandhi, na Abraham Lincoln.

Nadhani taaluma yake ya sheria na mtazamo wake wa maisha ulimpa nafasi kubwa duniani kuliko nafasi aliyopata Julius Nyerere (Kitu ambacho watanzania wengi tunashindwa kukubali).

Kama mwanasheria, Mandela alipigania uhuru na haki za kikatiba. Maendeleo ya kiuchumi ya mweusi nchini Afrika kusini au katika nchi zingine barani Afrika yatachukua zaidi ya vizazi vitano. Hivyo katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake asingeweza kufanya mambo ya ajabu kubadilisha maendeleo ya kiuchumi.

Kitu kilichowezekana katika maisha yake ni kupigania haki za binadamu. Hiki kitu ambacho kinawezekana katika kipindi cha kizazi kimoja.

Kwa upande mwingine viongozi wengine wa kiafrika akiwemo Julius Kambarage Nyerere waliona misingi ya haki imo kwenye ugawanaji mali sawa. Hivyo walikuwa tayari kukiuka misingi ya kikatiba au kubadilisa katiba za nchi hili kujaribu kugawa mali sawa na kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Kushindwa kwao kumewafanya waafrika wengi weusi kutokuwa maendelo ya kiuchumi na haki za kikatiba.
 
Sehemu ya II
Maisha ya kisiasa na harakati ya Mandela.

Katika mwendelezo ulioanza hapo juu, tumeona uhusiano wa kifamilia kati ya Walter Sisulu na Mandela, kwamba ndoa ya kwanza ya Mandela na Evelyn Mase ilianzia kwa binamu yake Walter ambaye mama yake alitoka familia ya Mase na baba yake ni mzungu. Kwa uchache ni chotara

Uhusiano wa Mandela na Oliver Tambo ulianza wakiishi bweni moja katika chuo si kisiasa kama inavyoeleweka kwa baadhi. Mandela na Tambo walishawahi kuwa na ofisi yao ya uanasheria jijini Johanesburg

Mandela aliingia Johanesburg mwaka 1941 na kuanza kazi mbali mbali huku pia akiendelea na masomo.
Ni katika muda huo Mandela alikutana na rafiki yake Tambo na yeye kuvutiwa sana na siasa za Sisulu.

Mandela alikutana na na AnthonLembende mtu aliyekuwa akiamini zaidi katika Uafrika. Ni kwa mtazamo huo Lembede aliyekuwa tayari anajulikana ANC alikorofishana na Sisulu pale alipotoa maneno ya dhihaka kwa kuelewa kuwa baba yake Sisulu alikuwa mzungu.

Lembede ni muhimu sana katika historia ya ANC kwasababu yeye ndiye aliyechagiza kuanzishwa kwa tawi la vijana la ANYL akiwa na akina Mandela. Lembede ndiye kiongozi wa kwanza wa ANCYL

Mitazamo ya Lembede na Mandela ilikuwa tofauti. Lembde akiamini Uafrika na kwamba ANC ni ya Waafrika wakati Mandela akiona tatizo ni ubaguzi na kukiukwa kwa haki za wanadamu.
Hivyo Mandela aliweza kuwafikia watu wa race, tofauti na Lembede ambaye hata Sisulu alimuona kama si kamili.

Isisitizwe kuwa Mandela alikuwa rafiki mkubwa wa Lembede ambaye alimbadilisha mawazo na kumfanya awe nationalist Kifo cha Lembede kilitokea mwaka 1947 kwa shambulio la moyo (Heart attack) akiwa na Mandela

Nafasi ya Lembde ikachukuliwa na P.Mda na Mandela akawa katibu.
Hapa tunaongelea ANCYL na siyo ANC ya Alfred B. Xuma.

Mandela alikuwa mshabiki wa siasa za akina Lenin, Nehru, Mao, Lincoln n.k.
Alichaguliwa mwanakamati ya ANC jimbo la Transvaal na kuwa sehemu iliyomuondoa aliyekuwa kongozi kwasababu tu alikuwa na msimamo wa kati kuhusu uhusiano na jamii zingine zisizokuwa za kiafrika na yeye kuchukua nafasi yake.

Mwaka 1950 Mandela akawa rais wa ANCYL. Awali alivutiwa sana na namna jamii za kiasia zilivyoendesha migomo hata hivyo yeye hakuamini katika kushirikiana na jamii zingine. Mandela alipingwa kwa msimamo huo hatimaye kukubali kushirikiana na jamii zingine.

Ukifuatilia historia ya Mandela kuna watu kama akina Ahmed Kathrada aliyeongea kwa uchungu sana kuhusu kifo cha Mandela kule Qunu jana. Harakati za kupinga ubaguzi hazikuwa kwa waafrika tu bali jamii zote ambazo ziliathirika kwa namna moja

Misuko suko ya kiasiasa ya Mandela yaanza baada ya kuwa rais wa ANCYL

Utaendelea .......
 
Nguruv3;

Katika utafiti wangu, viongozi waliowahi kuwa wanasheria na kutumia ujuzi wao mahakamani wana mtazamo mwingine wa maisha na wanakuwa ni viongozi wazuri. Mfano mkubwa ni Mandela, Gandhi, na Abraham Lincoln.

Nadhani taaluma yake ya sheria na mtazamo wake wa maisha ulimpa nafasi kubwa duniani kuliko nafasi aliyopata Julius Nyerere (Kitu ambacho watanzania wengi tunashindwa kukubali).

Kama mwanasheria, Mandela alipigania uhuru na haki za kikatiba. Maendeleo ya kiuchumi ya mweusi nchini Afrika kusini au katika nchi zingine barani Afrika yatachukua zaidi ya vizazi vitano. Hivyo katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake asingeweza kufanya mambo ya ajabu kubadilisha maendeleo ya kiuchumi.

Kitu kilichowezekana katika maisha yake ni kupigania haki za binadamu. Hiki kitu ambacho kinawezekana katika kipindi cha kizazi kimoja.

Kwa upande mwingine viongozi wengine wa kiafrika akiwemo Julius Kambarage Nyerere waliona misingi ya haki imo kwenye ugawanaji mali sawa. Hivyo walikuwa tayari kukiuka misingi ya kikatiba au kubadilisa katiba za nchi hili kujaribu kugawa mali sawa na kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Kushindwa kwao kumewafanya waafrika wengi weusi kutokuwa maendelo ya kiuchumi na haki za kikatiba.

Hii ni generalization ambayo iko skewed, data ulizotoa hazikidhi kabisa hypothesis yako. Kumbuka kuwa hata Richard Nixon alikuwa na Law degree kutoka Duke University lakini hakufuata sheria wakati wa utawala wake mpaka akafukuzwa. Nixon alianza kazi akiwa practicing Lawyer kwenye kampuni binafsi huko California kabla hajaingia kwenye siasa. Kuna mifano mingi inayopingana na hypothesis yako
 
Sehemu III
Siasa za ANC katika siku za awali zilikuwa za mashauriano (non violence) ambazo zilimpa Albert Lithuli nishani ya Nobel.

Mandela alikuwa na ushirikiano na watu wa mataifa na rangi mbali mbali.
Alipokutana na Anton Lembede alibadilika na kuwa nationaslit zaidi.
Mbele ya safari hoja zake zikapingwa na kujikuta akirudi katika ushirikiano na jumuiya nyingine

Katika kuongoza ANC jimbo la Transvaal Mandela alipata fursa ya kuzunguka na kuhutubia mikutano mbali mbali Afrika kusini licha ya vikwazo alivyokuwa anakumbuna navyo.

Ni kwa wakati huo alishiriki katika kampeni ya kuutambulisha umma kuhusu madhila ya ubaguzi.
Kama viongozi waliotangulia alijikuta akipigwa marufuku kuongoza Transvaal na kufika Jojanesburg.

Kwa kupiga marufuku asifanye shughuli zake Transvaal Mandela hakuhudhuria mkutano wa ANC
Mkutano ulipitisha azimio la kuunda vikundi vidogo vidogo ikiwa ni wazo lake.

Katika kipindi cha mwaka 1952 hadi 1959 Mandela alishiriki kuandaa migomo kadha wa kadha, akishatakiwa na hata kupigwa marufuku ya kutembelea baadhi ya maeneo.
Juhudi za migomo hiyo hazikuzaa matunda yaliyotarajiwa.

Baadhi ya wanachama wa ANC waliokuwa wamechoshwa na siasa za kugoma waliamua kuondoka ANC na kuunda PAC chini ya Sobukwe.

PAC iliamini katika utaifa (nationalist) kwamba nchi ni ya waafrika na itawaliwe na waafrika.
Pia iliamini kuwa njia nzuri ilikuwa ni mapambano na makaburu na si vinginevyo.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa PAC iliyokuwa na kambi Tanzania kule Chunya.

Mauaji maarufu ya Sharpville yalikuwa organized na PAC.
Ingawa tayari katika miaka ya mwanzo ya 1950 ANC ilishaanza kupinga sheria ya 'pass law' upingaji ulifikia kilele katika mauaji ya Sharpville ambapo watu 69 waliuawa.

Pass law ni sheria iliyomtaka mwafrika kutembea na kitambulisho kama passport ya ndani (internal passport) ili kudhibiti nyendo zao. Mandela alishawahi kushtakiwa kwa kupinga sheria hiyo hadharani.

Kutokana na kutoridhika kwa mwendendo wa ANC na kuvutiwa na siasa za PAC Mandela, Sisulu, Slovo, na wengine walianzisha tawi la kijeshi la ANC lililojulikana kama Umkhonto Wesizwe(mkuki wa taifa au MK) Mandela akiwa kiongozi wake.

MK ilihamisika kutokana na mauaji ya Sharpville kwa kutambua kuwa hakukuwa na chaguo tena kati ya kukubali uonevu au kuupinga. Njia ilikuwa ni moja tu kuanzisha mapambano.

MK ikawa na makao makuu katika eneo la Rivonia. Eneo hilo ndilo limetoa jina la kesi maarufu iliyomfunga Mandela na wenzake miaka zaidi ya 20 ikijulikana kama Rivonia trial.

MK ilianza mashambulizi mwaka 1961 siku ambayo Albert Lithuli alipewa nishani ya Nobel kama mwafrika wa kwanza na mtu wa kwanza kutoka Afrika na Marekani kwa ujumla.

Mashambulizi yalilenga majengo ya serikali, mashamba na vituo vya umeme.
Lengo lilikuwa kushambulia maeneo bila kuua raia.
Na walifanya hivyo kwa kuipa serikali ya kibaguzi taarifa za kuanza mashambulizi.

Kuanzia hapo MK ikaitwa kundi la kigaidi na serikali ya Afrika kusini na Marekani.
Hiyo ndiyo sababu iliyopelekea Mandela kuwa katika orodha ya magaidi hadi mwaka 2008

MK ilikuwa na mahusiano ya karibu na vyama vya MPLA ya Angola, SWAPO,ZANU na FRELIMO na zipo nyakati walipigana bega kwa bega kama yake mapambano ya Cuito Canavale kule Angola.

Mandela alitumwa kwenda kuomba misaada ya kusiadia shughuli za ukombozi na hiyo ndiyo sababu ya yeye kwenda Ethipia, Ghana, Algeria n.k. akipitia Tanzania.Pamoja alikwenda kuhudhuria mafunzo ya msituni (guerilla war)

MK ndiyo iliyotoa viongozi kama Chris Han aliyeuawa mwaka 1993 na kupelekea mashaka ya kuzuka vurugu kubwa. Mandela alismama na kuzuaia vurugu kutokea jambo ambalo wanasiasa na wachunguzi wa wanasema lilisaidia kuweka mustakabali wa taifa hilo.
Ni kutokana na mauaji hayo tension ya kuwa na mabadiliko ya katiba na uchaguzi iliongezeka.

Sehemu VI tutaangalia kesi maarufu ya RIVONIA na maisha ya harakati za ukombozi baada ya Mandela kwenda jela.

Katika sehemu ya III (Ijayo) tutaangalia mahusiano kati ya wasemaji katika mazishi ya Mandela kule Qunu na Umkhonto weswize na baada ya hapo tutaendelea na Rivonia trial Sehemu ya IV

Itaendeleaa.
 
Sehemu ya IV

Katika mazishi ya Mandela yaliyofanyika Qunu kijijini, kwanza yalitanguliwa na rambi rambi za washiriki na maombezi ya kidini.


Maadhimisho yaliyofanyika Johanesburg kabla ya Qunu yalikuwa kutoa nafasi kwa ulimwengu kutoa rambi rambi.

Mandela alikuwa international figure na hilo lilionekana kama tukio la kimataifa.


Johanesburg viongozi waliozungumza walitoka katika mabara yote ikiwa na maana ya kutengeneza ule umataifa


Maadhimisho ya Qunu yalilenga kutambua mchango wa watu na maeneo mbali mbali katika safari ya Mandela.


Pamoja na kutoa nafasi kwa wanandugu na viongozi wa ANC kumuongelea mwanachama wao, baadhi ya viongozi walichagulia kwa umakini sana (well choreographed) ili kutambua na kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa mataifa na wananchi wa Afrika kusini.


Viongozi

Waziri mkuu wa Ethiopia: Ingawa ni mgeni katika siasa za kimataifa na kiuongozi, alichaguliwa kwa kuwa Adis Ababa chini ya Heile Selassie ilikuwa ni sehemu muhimu ya harakati za ukombozi. Mfalme Sellasie alikuwa mtawala mwenye ushawishi na nguvu Afrika. Safari za Mandela kwenda kuomba misaada na mafunzo ya guerilla alipitia Ethiopia.


Wanaduru wakumbuke kuwa wakati Mandela anafika Ethipoia OAU ilikuwa haijaundwa.

OAU iliundwa mwaka 1963 na Mandela alifika kabla ya hapo.


Hivyo Adis Ababa hakwenda kama sehemu ya OAU bali mchango wa Haile Sellasie na wananchi wa nchi hiyo.


Joyce Banda:

Ni mwenyekiti wa SADC ambayo chimbuko lake ni Frontline states zilizokuwa zinaunga mkono wapiganaji na kuachiliwa kwa wapigania uhuru kama Mandela na wenzake


Nchi hizo ni pamoja na Tanzania na Zambia.Hivyo Banda alikuwa anawakilisha frontline states ingawa Malawi haikuwemo lakini ni kwa hadhi ya uenyekiti na busara inasema isingekuwa vema kufanya tofauti na hivyo.


Kenth Kaunda

Katika viongozi wa frontline states walio hai ni Kaunda tu. Wengine wameshafariki

Kaunda aliongea kwa heshima yao na ndiyo maana alimtaja mama Maria kama sehemu ya kumbu kumbu ya enzi hizo.


Rais Kikwete

Ni kutambua mchango wa Tanzania katika kusaidia ukombozi kusini mwa Afrika yakiwa makao makuu na sehemu yenye kambi nyingi za wapigania uhuru.

Ni eneo lililokubali kuchukua ‘risk' ya kuwahifadhi umkhonto weziswe pamoja na wengine kutoka nchi za kusini mwa Afrika.


Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watu wa Afrika kusini kuhusu wasichokielewa kuhusiana na fadhila walizopewa na Watanzania. Na pia kuwakumbusha wanachama wa SADC mahusiano ya muda mrefu katika ukombozi.



Tuendelee na kesi ya Revonia sehemu ijayo

 
Hii ni generalization ambayo iko skewed, data ulizotoa hazikidhi kabisa hypothesis yako. Kumbuka kuwa hata Richard Nixon alikuwa na Law degree kutoka Duke University lakini hakufuata sheria wakati wa utawala wake mpaka akafukuzwa. Nixon alianza kazi akiwa practicing Lawyer kwenye kampuni binafsi huko California kabla hajaingia kwenye siasa. Kuna mifano mingi inayopingana na hypothesis yako

kwikwikwi. Sikutumia data yoyote hile na wale sikusema kuwa alikuwa na taaluma ya sheria havunji sheria. Rais Nixon alivunja sheria. Lakini alikuwa ni mmoja wa progressive minds kutoka Republican Party. Ni yeye aliyefungua uhusiano kati ya USA na China.

Kati ya marais 44 wa Marekani, 26 ni wanasheria. Hiyo ni namba kubwa na sio ya kubahatisha. Hivyo kuna ukweli kuwa kutokana na taaluma yake ya sheria, Mandela aliangalia uhuru wa watu wake kwa kutumia darubini nyingine.
 
Sehemu ya V

Mwaka 1962 Mandela alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi wa migomo ya wafanyakazi pamoja na kuondoka nchini kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo Mandela alitumia fursa kuelezea ubaguzi badala ya kujitetea.Alihukumiwa kifungo cha miaka 5.

Mwaka uliofuata polisi walivamian eneo la Liliesleaf na kuwakamata washirika wa Mandela na nyaraka za Umkhonto.
Kesi hiyo ilichukua sura ya kimataifa na taasisi mbali mbali kwa kupewa jina la Rivonia trial.
Licha ya kuombewa msamaha Mandela na wenzake walihukumiwa kifungo cha maisha.

Kama ilivyokuwa kwa kesi ya awali, kuanza kwa kesi hii kulitanguliwa na hotuba ya Mandela ambayo alimnukuu Fidel Castro kwa maneno 'History will absolve me' na kuwa kivutio katika vyombo vya habari.

Katika mkutano wa Transvaal ambao Mandela hakuhudhuria, hotuba yake ilipambwa na maneno kutoka kwa Nehru yaliyosemwa 'No easy walk to freedom'

Siku chache kabla ya kuhukumiwa, Mandela alifahamu wazi kilichokuwa kinakuja ni hukumu ya kifo.
Akatoa msemo maarufu unaosema
'It is an ideal for which I have lived,it is an ideal for which I hope to live and see realised. But if needs be, it is an ideal for which I am prepared die' Maneno haya yalienea sana duniani na kuendelea kuupasha ulimwengu nini kinaendelea kule Afrika kusini.Mandela alitumia kesi kuendeleza ajenda za kisiasa bila kujali hatima yake.


Ukimuacha Kantor na Bernestein, Mandela aliambatana na G.Mbeki baba yake Thabo, Ahmed Kathrada, Walter Sisulu, Andrew Mlangeni, Raymond Mhalaba na Elias Motosoaledi kuelekea kisiwa cha Robben.
Pamoja na kuwa kifungoni Madiba alitembelewa na wageni kadha kutoka nje ya nchi na serikali ya makaburu.

Mkewe Winnie Mandela aliendeleza harakati za kisiasa akifungwa mara kadhaa na kuwekwa katika vizuizi vya kusafiri.
Winnie alikuwa kiongozi wa ANC tawi la akina mama na hivyo kuendeleza kukuza sauti zaidi juu ya kuachiwa mumewe.

Katika miaka ya 70 siasa za Afrika kusini zilibadilika kutokana na kifo cha Mwanaharakati Steve Biko.
Biko hakuwa mwanachama wa ANC, alikuwa mwanafunzi wa medical ambaye alianzisha BCM (Black conscious movement) akiegemea katika kujitambua.

Kifo cha Biko akiwa mikononi mwa polisi kilizungumzwa sana dunia na kuendele kumulika akina Mandela wakiwa Robben Island. Baadhi ya wanachama wa BCM walifungwa na Mandela, Madiba hakukubaliana nao kwa dhana ya ubaguzi hata kwa wazungu waliopinga ubaguzi.

Mauaji ya June 16 ya SOWETO hayakuwa na uhusiano wa siasa za wakati huo moja kwa moja.
Ilikuwa ni wanafunzi wanapinga matumizi ya lugha ya Afrikaner.
Mauaji hayo nayo yaliendelea kuimulika Afrika kusini katika jicho la ubaguzi na uonevu.

Hayo yalilazimisha mazungumzo na Mandela, kwani serikali ya Afrika kusini iliendelea kutengwa na jumuiya ya kimataifa.
Vikwazo vya kiuchumi na sauti za manguli kama Nyerere, Kaunda, Khama, Machael, Kaunda, Huari boumedien na wengine ziliendelea kuiweka serikali ya kibaguzi katika wakati mgumu.

Mwandishi wa habari mweusi Qoboza ndiye aliyeufahamisha ulimwengu kwa dhati nini kilitokea SOWETO.
Kutokana na kuvuta hisia za wasomaji Qoboza aliandika wimbo wa 'free Mandela' ambao uliimbwa kwa lugha nyingi ikiwemo kiswali 'Afunguliwe Mandela'.

Qoboza alifariki mwaka 1988 baada ya kurejea kutoka Marekani.
Kabla ya kwenda huko Qoboza alitumikia kifungo cha miezi 6 bila kufunguliwa mashtaka.

Wakati huo huo mashambulizi kutoka Umkhonto yalikuwa yakipamba moto uzi yakiendeshwa na vijaana akina Chris Han.
Mwaka 1985 ujumbe wa watu saba mashuhuri kutoka jumuiya ya madola ulimtembelea mzee Mandela gerezani kwa
majadiliano. Ujumbe huo pia ulikutana na Botha na kumweleza hali ya Mandela kuwa ni ya amani na yenye ari.

Kuundwa kwa ujumbe huo kunafuatia kikao cha jumuiya ya Madola kule Nissau, Bahamas ambako waziri mkuu wa Uingereza alikuwa katika mbinyo wa hali ya juu kuwekea vikwazo Afrika kusini.
Mbinyo huo ulitoka katika nchi za Afrika hasa frontline states.

Ni jambo la kushangaza kuona Kikwete hakuandamana na mzee Malecela ambaye alikutana na Mandela yeye akiwa bado ni mchanga sana katika siasa. Mzee Malecela alistahili nafasi na hatufahamu ni kipi kilitokea hakuwepo katika ujumbe.
Mwingine aliyekuwepo ni Olusgunu Obasanjo wa Nigeria na wengine watano.

Tamasha la kuadhimisha miaka 70 ya kuzaliwa Mandela nalo lilizidisha ufahamu wa dunia juu ya Mandela hasa kizazi kipya. Tamasha hilo lilifanyika London.

Tamasha hilo ilikuwa kama kuamsha hisia za uhusiano wa kimasomo uliokuwepo kati ya Mandela na Univ of London alipokuwa anafanya masomo kwa njia ya posta akiwa gerezani.Alipohukumiwa ilifanyika sala maalumu ya kumombe jijini London.

Msukumo wa mambo yote hayo ulimweka Mandela kama mtu muhimu sana kwa mustakabali wa taifa lao.
Ni ukweli usiopingika kuwa katika wote aliokuwa nao gerezani yeye ndiye alikuwa kiongozi kwa matendo.

Mandela aliiondoa ANC na kuipeleka hatua mbele kuanzia ANCYL na Umkhonto huku pia akiwa mwanachama wa SACP, siri iliyowekwa wazi katika siku si zaidi ya tano zilizopita.

Tutaendelea kuangalia majadiliano kati ya Mandela na Makaburu na kuachiwa kwa wenzake
 
kwikwikwi. Sikutumia data yoyote hile na wale sikusema kuwa alikuwa na taaluma ya sheria havunji sheria. Rais Nixon alivunja sheria. Lakini alikuwa ni mmoja wa progressive minds kutoka Republican Party. Ni yeye aliyefungua uhusiano kati ya USA na China.

Kati ya marais 44 wa Marekani, 26 ni wanasheria. Hiyo ni namba kubwa na sio ya kubahatisha. Hivyo kuna ukweli kuwa kutokana na taaluma yake ya sheria, Mandela aliangalia uhuru wa watu wake kwa kutumia darubini nyingine.

Wingi wa wanasheria katika siasa za Marekani ni kutokana na wingi wa digrii za sheria nchini humo; kwa hiyo namba hiyo siyo kipimo tosha. Ni kutokana na wingi huo ndiyo maana unaweza kukuta unatibiwa na daktari ambaye pia ana digrii ya sheria; kuna rafiki yangu anafundisha computer science lakini pia ana digrii ya sheria. Maseneta karibu wote wana digrii za sheria pia. Jambo la muhimu ni kama nilivyosema hapo awali kuwa wote wamekuwa na matatizo yao kama wale wasiokuwa wanasheria, kwa hiyo hakuna clear line inayotofautisha performance ya wanasiasa wenye background ya sheria na wanasiasa wasiokuwa background hiyo. Marais wote wa marekani wamekuwa na mazuri na mabaya yao, hakuna aliyeacha clean record nzuri isipokuwa wachache sana ambao utakuta walitoka katika background tofauti tofauti, siyo sheria tu.
 
Zakumi,
Kumradhini, waswahili wanasema Ashakum sii matusi..
Leo mimi na wewe maana nataka watu wanisikie vizuri kuhusu huyu mwanasheria - The Great Leader. Ni kweli kabisa kapigania haki za binadamu na ndio upeo wake ktk maono tofauti kabisa na Mchumi. Mandela hakutazama sana upande wa miliki ya utajiri wa mali na ardhi kama kina Mugabe,Nyerere, Kaunda na wengineo bali alichogombania zaidi ni weusi wawe treated sawa na wazungu not second or third class citizen.

Kama mwanasheria alipoahidiwa hilo tu mzee wetu alikubali na kushusha gloves, hizi sifa zote anazomiminiwa hasa na nchi za magharibi sii kwa sababu ya mateso yake ama Huruma alokuwa nayo kutolipiza kisasi..Watakuwaje na huruma leo wakati wao ndio walomweka Jela na kumweka ktk list ya Terrorist hadi majuzi tu. Sifa kubwa ya Madiba kwao ni kukubali kuacha Utajiri wa nchi hiyo ukamatwe bado na wakoloni - BASI!

Ni kiongozi pekee duniani alopigania UHURU na akaweza kuwaacha wakoloni waendelee kukamata ardhi na njia kuu za uchumi. Huo ndio mtazamo wa viongozi wa nchi za magharibi, japo hawatasema hivyo ila eti huruma yake kutolipa kisasi maana huo Urais wangeweza kabisa kumnyima nafasi hiyo. Na sidhani kama kuna mtu humu anajua in details yaliyomi ktk Memorandum of Understanding walofanya baina Kaburu,nchi za Magharibi na Mandela kwani hadi anatoka jela ANC ilikuwa bado banned!
 
Wakuu Zakumi Mkandara Kichuguu
Nawasoma kwa umakini kabisa na hoja zenu zitaangaliwa kwa jicho pevu.
Hakika hatuwezi kueleza au kuandika kila jambo kwa ukamilifu, hata hivyo ni vema tukapata japo picha kidogo.

Wakati mfupi sana ujao tutasoma mashtaka, tutaita watetezi na hukumu itatolewa.
Tunachokifanya kwa sasa ni kuweka baadhi ya mambo katika muktadha unaoekana ili kuepuka kusoma 'hukumu' bila mashtaka au uetezi. Tunafanya hivyo ili kuzingalia hoja kwa undani na si kama nilivyowahi kusoma hapa JF baadhi yetu wakihoji umaarufu wa Mandela zaidi ya Steve Biko. Hukmu ilisomwa haraka hata bila kujua wasifu wa wawili hao.

Nawashukuru na tuendelee kujadiliana.
 
Last edited by a moderator:
Zakumi,
Kumradhini, waswahili wanasema Ashakum sii matusi..
Leo mimi na wewe maana nataka watu wanisikie vizuri kuhusu huyu mwanasheria - The Great Leader. Ni kweli kabisa kapigania haki za binadamu na ndio upeo wake ktk maono tofauti kabisa na Mchumi. Mandela hakutazama sana upande wa miliki ya utajiri wa mali na ardhi kama kina Mugabe,Nyerere, Kaunda na wengineo bali alichogombania zaidi ni weusi wawe treated sawa na wazungu not second or third class citizen.

Kama mwanasheria alipoahidiwa hilo tu mzee wetu alikubali na kushusha gloves, hizi sifa zote anazomiminiwa hasa na nchi za magharibi sii kwa sababu ya mateso yake ama Huruma alokuwa nayo kutolipiza kisasi..Watakuwaje na huruma leo wakati wao ndio walomweka Jela na kumweka ktk list ya Terrorist hadi majuzi tu. Sifa kubwa ya Madiba kwao ni kukubali kuacha Utajiri wa nchi hiyo ukamatwe bado na wakoloni - BASI!

Ni kiongozi pekee duniani alopigania UHURU na akaweza kuwaacha wakoloni waendelee kukamata ardhi na njia kuu za uchumi. Huo ndio mtazamo wa viongozi wa nchi za magharibi, japo hawatasema hivyo ila eti huruma yake kutolipa kisasi maana huo Urais wangeweza kabisa kumnyima nafasi hiyo. Na sidhani kama kuna mtu humu anajua in details yaliyomi ktk Memorandum of Understanding walofanya baina Kaburu,nchi za Magharibi na Mandela kwani hadi anatoka jela ANC ilikuwa bado banned!

Mkuu Mkandara,

Umeelezea point muhimu sana kuhusu msimamo wa Madiba baada ya kutoka gerezani....

Kwa kuongezea tu ni kwamba msimamo huu ulipata upinzani kutoka baadhi ya kada ndani ya ANC ambapo baadhi waliona kuwa ni usaliti baada ya miaka nenda rudi ya mapambano ya kumwondoa kaburu.
 
Last edited by a moderator:
Sehemu ya VI

Ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika ulipamba moto katika miaka ya 70 na 80.Mreno aliachia makoloni yake yote.
Afrika kusini ikawa na mpaka mkubwa na maadui karibu mlangoni kwa nchi kama Zimbabwe, Angola, Namibia na Botswana. Pressure ya kukabiliana na mapambano ilizidi kuwa kubwa.

Nchi za Afrika zikaungana zaidi katika kupinga utawala wa makaburu.
Jumuiya ya Madola ikawa hatiani kuvunjika kwa suala la ubaguzi na kuachiwa huru kwa akina Mandela na wenzake.
Afrika ya kusini ikaendelea kutengwa na mataifa na kubaki na washirika wachache kama Marekani.

Ingawa vita baridi ilikuwa inaelekea ukingoni, ilikuwa dhahiri nchi za mrengo wa kushoto zilikuwa na ushawishi sana katika kumuondoa mreno.

Mataifa zaidi ya Cuba na Urusi yalijitokeza kuunga mkono wapigania uhuru.
Mahathiri Mohamed na Suarhato wakaonekana wazi kuunga mkono vyama vya ukombozi.

Ni katika kipindi hicho mataifa ya Asia mashariki yalianza kupata nguvu za kiuchumi na kuitwa Asian Tiger huku nchi za magharibi zikianza kuparaganyika.

Tukio la kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin na mataifa mawili kurudi kuwa taifa moja ilikuwa ni kielelezo kizuri kuwa nguvu ya umma ilikuwa haizuliki tena.

Hadi wakati huo kukawa na nguvu za ndani zinaotoka kwa wapigania uhuru na nguvu za nje zinazotokana na vikwazo vya uchumi na kutengwa na jumuiya ya kimataifa.

Mazungumzo yaliyokuwa yamekwama upande wa serikali na Mandela yalianza tena.
Kuna nyakati Mandela alitaka akutane na P.W.Botha kwa sharti kuwa lazima ANC iache mashambulizi.
Mandela alikataa kwa kusema serikali ya makbauru iache vurugu kwanza.

Majadiliano yaliendelea na baadhi ya wafungwa kuanza kuachiwa

Govan Mbeki aliachiwa mwaka 1987
Walter Sisulu aliachiwa mwaka 1989
Raymond Mhalaba 1989
Ahmed Kathrada 1989

Hatimaye Mandela naye akaachiwa baada ya De Klerk kuingia madarakani.
Mazungumzo ya makaburu na Mandela yaliendelea kabla ya kuachiwa kwake na hasa alipoondolewa Robben Island.

Mandela aliendelea kuwa na umaarufu hata alipopata ugonjwa wa TB hilo likabaki kuwa mwiba mkali kwa makaburu kwa hofu ya kifo chake akiwa mikononi mwao. Ilikuwa dhairi kuwa kifo cha BIKO kiliitisha Afrika kusini na pengine cha Mandela kingepelekea maafa zaidi.

Nikumbushe kuwa kifo cha BIKO kilikuwa maarufu kutokana na kufia mikononi mwa polisi tena kwa mateso makali huku makaburu wakificha na kudai alifariki kwa Pneumonia. Aliyefichua kifo hicho ni mzungu ambaye alichukua picha ya Biko akiwa chumba cha maiti na majeraha.

Hilo lilichochea sana Afrika kusini kuoenakana madhalimu zaidi hasa kwa waliokuwa na wasi wasi. Hata hivyo Biko hakuwa maaurufu kwa kutokana na mapambano bali kundi lake la BCM

Kuachiwa kwa Mandela hakukusitisha mauaji au mapaigano ya ndani.
Kifo cha Chris Han ambaye alikuwa kiongozi wa Umkhonto tena akipigwa risasi na mzungu kilionekana kama mtihani kwa Mandela.

Hali tete ilimlazimu Mandela aongee na taifa na kuwataka wawe watulivu licha ya mauji hayo.
Imeelezwa kuwa mauaji ya Han ilikuwa ni kulipa kisasi kwa kazi kubwa aliofanya dhidi ya hujuma kwa serikali ya makaburu. Na pia ulikuwa mtihani kwani vurugu zingezuka zingehusishwa na kuachiwa Mandela.

Hali haikuwa nzuri kwani mapambano yaliendelea kama alivyoahidi Mandela katika mkutano baada ya kauchiwa.
Jambo lililobadilika lilikuwa makaburu kuwatumia Inkhata ya Wazulu kuleta mapambano na ANC.
Mauaji yalikuwa makubwa kutokana na mapambano ya wapiganaji wa ANC na yale ya Mongustu Buthelezi.

Mandela alibainisha wazi kuwa hizo zilikuwa hujuma za serikali ya makaburu na kuomba wawepo wasimamizi wa amani kutoka umoja wa mataifa.

Yakafikiwa makubaliano kati ya Inkhata, Mandela na De klerk kusitisha mapambano.
Uamuzi huo haukuwapndeza wenye msimamo mkali wa ANC lakini Mandela aliona ni bora katika kuelekea katika uchaguzi.
Hatua za awali za SA kuelekea uchaguzi ilikuwa kuunda katiba ya mpito na hilo lingewezekana tu ikiwa kungalikuwa na amani baina ya makundi hayo hasimu

Pamoja na vurugu za Inkhata yalikuwepo makubaliano ya wazungu wachache kutonyang'anywa haki zao kama ajira.
Msimamo huo pia haukuwapendeza wana ANC wakereketwa na ilionekana kana kwamba Mandela amewauza kwa kuachiwa huru. Ndani ya ANC kukawa na mitafaraku ambayo ilimlazimu Mandela kutumia busara kusawazisha.

Hoja kubwa ya Mandela ilikuwa ni Afrika ya kusini ya kila mmoja isiyo na ubaguzi.


itaendelea... sehemu ya mwisho
 
Sehemu ya VII

Kutoka kwa Mandela kulileta matarajio makubw kwa Waafrika.
Walimtaka Madiba achukue Urais wa ANC uliokuwa chini ya Oliver Tambo, mwanaharakati na rafiki yake.

Mandela aliwaambia alipokuwa Magereza waliongozwa na Tambo, hakukuwa na ulazima wala uharaka.
Ilikuwa ni busara kwasababu Tambo alikshaanza kudhoofika kwa maradhi na lilikuwa suala la muda.

Muda ulipowadia Mandela akachukua uongozi wa ANC huku makundi yenye msimamo mkali yakiendelea kumtaka achukue hatua za haraka. Mandela alibaki na msimamo wa kile alichoona ni bora kwa wananchi

Mapambano kati ya ANC, Inkhata na AWB yalikuwa yanaendelea na watu kupoteza maisha.
Weupe wachache waliingiwa hofu iliyotokana na msukumo wa wanaharakati wa ANC wenye msimamo mkali.

Hatimaye maridhiano ya mikutano ya vyama yalipatikana kuipitia kwa kutengeneza katiba ya mpito kuelekea uchaguzi. Yapo matatizo yalitokea na kupatiwa ufumbuzi hata kama haukufurahisha wanachama wa makundi mbali mbali. uchaguzi kufanyika mwaka 1994, Mandela alichaguliw rais wa Afrika kusini.

Mandela alielewa kuwa hawezi kuongoza kukiwa na kutoelewana.
Akatengeneza serikali ya umoja wa kitaifa na kutoa nafasi kwa vyama pinzani ikiwemo Inkhata ambayo Buthelezi alipewa wizara ya mambo ya ndani.

Buthelezi alipewa wizara hiyo makusudi ili aweze kudhibiti Inkhata bila manung'uniko ya uonevu na kundi jingine. De Klerk akawa makamu wa rais akisaidiana na Thabo Mbeki .
Mbeki ndiye alikuwa anaendesha shughuli za serikali za kila siku.

Mandela na ANC akakabiliwa na changamoto mbele yake.
Kwanza kulileta taifa lililogawanyika kwa misingi ya urangi kwa miaka mingi pamoja.
Kuleta mabadiliko yatakyomwezesha mtu wa kawaida kuona tofauti ya ubaguzi na wakati alio nao
Kuendelea na jitihada za kuandaa katiba ya kudumu ya nchi hiyo itakayoliacha taifa kama kitu kimoja.
Kuleta usawa na kuounguza pengo kati ya walionacho na wasio nacho.

Sheria zifuatazo zilifanyiwa marekebisho miongoni mwa nyingi
i)Kubadili sheria ili ziwiane na mazingira yaliyopo bila kuleta tafrani.

ii)Madiba alibadili sheria ya ardhi ya mwaka 1913 iliyokuwa ya kibaguzi na kutengeneza inayotambua ardhi za watu walionyng'nanya, kulinda masilahi ya watu wanaoishi au kufanya kazi katika mashamba

iii)Katika wakati wake ilipitishwa sheria ya kuwawezesha watu kujenga nguvu kazi yenye ubora
Kutoa huduma za afya ya msingi

iv) Sheria ya kuondoa ubaguzi wa kijamii kama kwa wazee, walemavu n.k

Kupitishwa kwa sheria hizo hakukuwafurahisha wapinzani na wanaharakati ndani ya ANC.
Kwa mfano wanaharakati walitaka wazungu wanyang'anywe ardhi, wakamatwe na kufunguliwa mashtaka na hata kunyimwa haki zao .

Mandela alitambua kuwa taifa lilikuwa linapita katika kipindi kigumu na busara zilihitajika zaidi. Aliweza kutambua makosa ya nchi nyingine katika kuleta mabadiliko ya haraka hasa katika suala la ardhi.

Pamoja na majukumu yake Mandela alikuwa na kazi ya kuileta jumuiya ya kimataifa kuitambua SA mpya.
Alifanya hivyo kupitia michezo, ushiriki wa shughuli mbali mbali, makongamano na mikutano.

Kwa mara yakwanza jeshi la Afrika kusini lilishiriki katika kulinda amani kule Kongo.
Mandela akawa mwenyekiti wa SADC na mwenyekiti wa nchi zisizofungamana.

Madiba hakutaka kuwania uongozi kwa kipindi cha pili kwasababu,
kwanza alitaka kuwa na ukaribu na familia kama ilivyoelezwa katika bandiko I.
Kujenga familia upya baada ya ndoa yake kuparaganyika

Pili, kutoa nafasi kwa kizazi cha sasa kuongoza taifa kwa vile hakuwa na cha ziada baada ya ajenda ya ubaguzi.
Hata hivyo Mandela alitambua kuwa yeye ni mtu maarufu na aliapaswa kutumia umaarufu wake kama gundi.

Mandela hawezi kupimwa kwa miaka 5,10 au 20. Miasha yake yalitawaliwa na misuko suko kuanzia ya kifamilia, harakati na kisiasa. Na wala haiwezekani kumweka katika mizani na kiongozi mwingine kwasababu mazingira ya kisiasa, utamaduni na harakati hubadilika kutoka eneo moja hadi jingine.

Miasha ya Mandela ni marefu kwa umri na muda. Si rahisi kuorodhesha kila jambo kwa ukamilifu wake.
Ningeomba wanajamvi walio na mchango mwingine au tofauti waulete hapa jamvini tubadilishane mawazo.

Tulichokijadili ni kutupa tu mwanga wa kuanzia katika majadiliano.
Katika bandiko la kwanza tulisema tutajibu hoja ikiwa ni pamoja na za wakuu Zakumi Kichuguu Mkandara
Tuziangalie hoja zao kwa mantiki na kustahamiliana.

Wanaukumbi karibuni

Tusemezane
 
Swali la kwanza
Kwanini Mandela aliyekuwa kifungoni apewe hsehima kubwa kuliko waliosaidia kuachiwa kwakwe?

Kwanza tutambue ukoloni wa Afrika kusini ulikuwa mkubwa tofauti katika eneo letu .Ubaguzi ulikuwa sheria za nchi.
Kwa mfano kulikuwa na sheria ya 'pass law' ambayo mtu alitembea jimbo moja hadi jingine kwa 'passport'.
Sheria ya kunyang'anya ardhi ya mwaka 1913. Sheria za kazi n.k.

Mandela aliwakuta akina Lithuli na Sisulu wakiwa katika harakati.
Kwa muda mfupi alishiriki katika harakati kwa mambo mengi lakini makubwa ni kuipeleka ANC katika level nyingine.

Akiwa na akina Lembede na Sisulu walianzisha ANCYL. Halafu akawa mwanzilishi wa Umkhonto Wesizwe.
Umkhonto ilibadilisha mwelekeo wa kisiasa hata kuwazidi PAC ambao kwao mapambano yalikuwa ni sera.

Matukio ya Mandela yalikuwa kivutio cha habari na kuutanabaisha ulimwengu kilichokuwa kinaendelea SA.
Hata alipofungwa jina la Nelso Mandela lilikuwa mbele kama alama ya kupinga ubaguzi.

Nguvu yake ya kuwaunganisha watu waliokuwa katika kina cha ubaguzi kama SA ilikuwa ni muhimu sana kwa mustakabali wa taifa hilo. Licha ya madhila yaliyomkuta Mandela aliamini kuwa Afrika kusini ni ya wote kilichokuwa kinakosekana ni usawa uliopelekea ubaguzi.

Haiwezekani kuwaweka katika mizani viongozi wa kisiasa kama tunavyopima sukari.
Nyerere hakupigana kwa bunduki, alipigana kwa fikra.
Kuwaweka katika mizani ni sawa na kusema embe na chungwa kipi kitamu.

Historia ya south Afrika, Mandela kabla na baada ya kufungwa vinampa umaarufu wa kipekee.
Si kwamba alifanya mambo tofauti na wenzake lakini aliyafanya katika mazingira tofauti.
 
Wingi wa wanasheria katika siasa za Marekani ni kutokana na wingi wa digrii za sheria nchini humo; kwa hiyo namba hiyo siyo kipimo tosha. Ni kutokana na wingi huo ndiyo maana unaweza kukuta unatibiwa na daktari ambaye pia ana digrii ya sheria; kuna rafiki yangu anafundisha computer science lakini pia ana digrii ya sheria. Maseneta karibu wote wana digrii za sheria pia. Jambo la muhimu ni kama nilivyosema hapo awali kuwa wote wamekuwa na matatizo yao kama wale wasiokuwa wanasheria, kwa hiyo hakuna clear line inayotofautisha performance ya wanasiasa wenye background ya sheria na wanasiasa wasiokuwa background hiyo. Marais wote wa marekani wamekuwa na mazuri na mabaya yao, hakuna aliyeacha clean record nzuri isipokuwa wachache sana ambao utakuta walitoka katika background tofauti tofauti, siyo sheria tu.

Mkuu Kichuguu;

Hoja ya kuwa wingi wa digrii za sheria si ya kweli. Zipo takwimu za kuonyesha hilo. Vilevile Yale na Harvard law schools ndizo zinazoongoza kwa kutoa viongozi wa juu. Vilevile wanaojiunga na law schools ni top performers katika mambo mengi tu. Hivyo kilichopo hapa ni a selective group of people.

Ukisoma hotuba na historia za Nyerere na Mandela utaona kuwa taaluma na professional zao zilijenga mitazamo yao ya mawazo. Kwa mfano hotuba nyingi za Nyerere zilikuwa na mtazamo wa kukufundisha au kumwelewesha mtu. Kwa upande wa Mandela,alikuwa anatafuta a winning position au commoni grounds.
 
Mkuu Zakumi
Kwa vile umesema Mandela alikuwa smart katika uongozi kwasababu alikuwa lawyer swali ni kuwa wafuatao hawakuwa ma lawyer, sijui nao unawaongeleje.

Winston Churchil
Roosevelt
Kennedy
G.Washington
Reagan

Mkuu Mkandara
Kuhusu suala la Mandela kuwaacha wakoloni wakimiliki ardhi
a) Mandela alipaswa kufanya nini kuhusu suala la ardhi zaidi ya ilivyo sasa
b) Ni nchi gani iliyowahi kwanyang'anya wakoloni ardhi ikapata mafanikio?

Ahsanteni
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom