Kwanza kabisa nataka kukueleza ya kwamba hakuna mahala popote nilipo ama napowalinganisha Mandela na Nyerere. nachoandika hapa ni FACTS sasa wewe unaweza kuzipa alama vyovyote upendanyo ktk maono yako na wasomaji wengine.
Sijasema sisi tunataka kuwaandikia Wasouth Historia isipokuwa Historia ni UKWELI wa EVENTS zilizotokea hapa tunaandika tu the after math. Na wala sijasema Mandela hastahili sifa anazopewa isipokuwa nachosema ni sisi tuelewe hizi sifa zinazotoka nchi za magharibi zimetazama nini haswa na sisi tunatazama nini. Sijasema mahala popote ya kwamba hata wewe unatakiwa kumsifia Mandela kwa sifa za wazungu ama usimsifie kwa lolote. Mbona unamchambua Nyerere ambaye alikupa wewe Uhuru kwa mtazamo wako na wala sii FACTS na tunajadili hiyo mitazamo yako?... Mimi isweki mtazamo wangu hapa bali ni facts tupu kuwa Mandela anasifiwa na wazungu kwa kuwaachia wao kuendelea kutawala njia kuu za uchumi. sasa iwe ni vema au vibaya hapa ndipo tunaweza kujadili kwa mitazamo yetu.
Mandela alipotoka Jela alibadilika, Mandela alokuwa Mkomunist alikuwa mpole na kutaka tu kuondoka kwa Apartheid tofauti kabisa na Mandela alojiunga ANC na kupiga kampeni za - Amandla. Hapa nitakujibu wewe pamoja na
Nguruvi3, maana naona sasa watu mnataka kupotosha ukweli na lengo hilisi la UHURU wa South kama ilivyoanishwa ktk Charter of Freedom ya South. Na siku zote hili neno UHURU hutumiwa vibaya sana na watu kama vile UHURU ni kumwondoa mtawala mkoloni mweupe na kumweka mweusi badala ya UHURU kuwa ni hali ambayo Taifa au wananchi wake wanakuwa sii WATUMWA wa mtu ama utawala bila kujali rangi wala asili(irrespective of colour, race or nationality). Mtu mweusi anaweza pia kuwa mkoloni na mbaya zaidi ya mtu mweupe.
Nkuu Nguruvi3 ebu tuitazame hotuba ya Mandela aliposema haya:- During my lifetime I have dedicated my life to this struggle of the African people. I have fought against white domination, and I have fought against black domination. I have cherished the ideal of a democratic and free society in which all persons will live together in harmony and with equal opportunities. It is an ideal for which I hope to live for and to see realised. But, My Lord, if it needs be, it is an ideal for which I am prepared to die'
mkuu wangu nguruvi3, Mandela anaposema WHITE DOMINATION au BLACK DOMINATION alikuwa na maana gani?..
Hivyo wangu, nchi inaweza kuwa na utumwa ikitawaliwa na mtu mweusi vile vile, na zikafanyika harakati za kuuondoa utawala huo, yakafanyika mapinduzi kwa sababu hizo hizo ambazo tuliutaka Uhuru kutoka kwa wakoloni weupe. Kila binadamu anataka kuwa huru - independent of fate or necessity, kuondokana na Utumwa. Hapa ndipo tunapoanzia kuutazama UHURU wa mtu ama taifa.
Hili neno UTUMWA unapolitafsiri ndipo unaweza kuipata siri ya UHURU maana Mtumwa mara zote sii mmiliki wa ardhi ama mali bali ni mjakazi, ni mtu wa chini ambaye kudai haki za Ubinadamu pasipo kwanza kupigania kuondokana na Utumwa huo ni sawa na kutwanga maji ktk kinu. Hii ni Imani yangu mimi sii lazima nawe uamini hivyo ila naweza kukupa mifano.
Sasa turudi wa Mandela, nachoelewa mimi ni kwamba ule wito wa wasouth unaosema AMANDLA - AWETHU (POWER TO THE PEOPLE) ina maana moja tu nayo ni kujikomboa toka ktk hali ya Utumwa. Ni madai ya kuwa HURU. Ile power of self determination attributed to the will au sio?. Kwa hiyo kuungwa mkono Mandela na wahindi wayahudi na wazungu haina maana ya kwamba wahindi na wazungu wote wanapenda kuona mfumo wa kitumwa isipokuwa mtu mweusi tu. Itakuwa uongo mkubwa tukisema sisi hatupendi Utunmwa wakati kwa mrazamo wangu hakuna race inayopenda Ubwana kama sisi tena tunapitiliza kwa kuwaweka utumwani watu weusi wenzatu.
Zakumi, hata siku moja siwezi kupingana na ukweli kwamba Mandela alijitoa Mhanga kupigana haki za WaSouth hilo ni fact na tunamsifia kwa hilo kama kina Martin Luther King. Lakini pia ni muhimu kwetu ku clarify the fact kwamba watu Wasouth bado wanatawaliwa, hawako huru isipokuwa wamepewa haki za binadamu kimaandishi na uhuru wa bendera pasipo kuwezeshwa umiliki wa aedhi ama mali.
Sijasema wala sintothubutu kusema Mandela hastahili sifa zote alizopewa. Anastahili sana ila nachosema tu ni kwamba kuna mitazamo miwili hapa. Sisi tukimsifia kwa jingine na wazungu wakimsifia kwa jingine ambalo ndilo limempa umaarufu zaidi kuliko sifia zetu sisi. na siwezi sema Mandela alitakiwa afanye nini ktk miaka mitano alokuwa rais kuhalalisha mtazamo tofauti. Isipokuwa ukweli utabakia ya kwamba Mandela alokuwa Mkomunist kabla ya kwenda jela, alipotoka jela alikuwa amebadilika kabisa na kudai tu haki za binadamu Ile Power to the people ikabakia kuwa kielelezo cha mtu mweusi kuwa IKULU wakati wananchi wake bado wapo utumwani kiuchumi.
Ni sawa kabisa nikisema Historia ya Nyerere kabla ya UHURU alionekana kupiga vita Ukomunist na alikuwa pamoja na CIA na MI6 kuhakikisha ukomunist haupewi nafasi East Afrika, lakini mara tu baada ya UHURU wetu, Nyerere alibadilka na kuwa Mkomunist. Hii ndio sababu kubwa ya Nyerere kupoteza sifa na umaarufu wake kwa wazungu japo wapo wazungu wachache wanaomfagilia. These are FACTS, sio simulizi za kufikirika or my perspective!
BTW. Niwe Mohammed Said kwa chati - nauliza tu kutaka kujua... Hivi Mandela alitumikia Jela peke yake ama walikuwa viongozi wengine wa ANC? Je kwa nini hawa wengine hawapewi sifa hizo wala hakuna historia ya mateso na maisha yao wakiwa Jela ama baada yaa japo walitumikia pia miaka 27 au hawa hawastahili sifa hizo!