Mizani yangu inaonyesha kwamba Madiba amekuzwa tu na vyombo vya nchi za magharibi kwa sababu ya kuwatetea makaburu ambao ni wazungu wenzao, vinginevyo sijaona cha pekee alichofanya Mandela, pengine kinachoongelewa kusamehe ni makosa kwa upande fulani kwa maana kwamba amehalalisha maovu na mauaji yaliyofanywa na makaburu wakati wa mapambono ya ubaguzi wa rangi.
Kilichobadilika tu ni safu ya viongozi wa serikali katika ngazi ya kiifa kushikwa na weuzi badala ya wazungu, lakini kama mdau ulivyosema sijaona cha pekee cha kuwajali waafrika wenzake ambao walihitaji kwa hali na mali kupata ardhi ambayo ndiyo kitu muhimu kinachotegemewa na wengi katika maisha kama alivyofanya Mugabe.
Tazama mangapi aliyofanya Nyerere, Kaunda, Samora na wengineo kwa ukombozi wa bara la Afrika, hakuna hata mmoja wao anayeenziwa na utawala wa nchi za magharibi kwa vile tu waliwanyoshea kidole. Pengine inaweza kutafsirika kwamba Mandela aliiuza South Afrika kwa wazungu imzunguko wao wamebaki tu vibaraka.
Kwanza si kweli kuwa ametukuzwa na vyombo vya habari vya magharibi. Kila wakati alipougua habari zake zilipamba vichwa vya habari duniani.
Pengine vyombo vya habari vya Afrika vilaumiwe kwakuandika habari zake zaidi.
Msiba wa Mandela hakuna chombo cha habari kuanzia Tonga hadi Hawaii, Copenhagen hadi Captown kilichoacha habari zake. Mandela alikuwa ni habari kabla ya habari yenyewe.
Umaarufu wa Mandela si kusamehe tu, bali kuleta jamii iliyokuwa na sheria rasmi za kibaguzi, jamii iliyogawanyika kuwa taifa moja. Ni kutokana na Mandela kukaa meza moja na wabaya wake ili wajadili mustakabali wa SA.
Alifanya hivyo hata pale alipojua kuwa hana cha kupoteza tena kwasababu angeweza kufia magereza bila hofu.
Mandela alishapoteza familia na wala hakuwa na matumaini ya kuishi kama baba mwenye familia tena.
Kilichomsukuma zaidi ni kutaka kujenga misingi ya kudumu kwa vizazi vijavyo na msingi huo ni kuwa na usawa
Suala la ardhi nadhani hujaliangalia vizuri. Katika sheria za mwanzo kubadilishwa ni ile ya mwaka 1913 iliyojulikana kama Bantu Land act au Native land act iliyowazuia weusi kumiliki ardhi.
Sheria hiyo ilibadilishwa mwaka 1994 na Land restitution act iliyowapa fursa watu walionyang'anywa ardhi mwaka 1913 kudai ardhi zao. Hii ilifuatiwa na Land reform act ya Mwaka 1996 zote zikimlenga mwananchi wa kawaida.
Mandela alikuwa na choice tatu, kwanza kuwafukuza wazungu kabisa ili Waafrika wamiliki ardhi
pili, kuwanyang'anya wazungu ardhi yote na kuwapa wazawa
Tatu, kuangalia madhara yatokanayo na hatu zisizozingatia hoja mbili za awali.
Mandela alijifunza kutoka sehemu mbali mbali. Mgogoro uliozuka Kenya ni matokeo ya ardhi na ulianza wakati wa Mau Mau. Kwabahati mbaya baada ya uhuru masetla wakamiliki 90 na wachache akiwemo Kenyatta asilimia 10.
Tanzania, iliunda azimio la Arusha na kutaifisha mashamba. Tanzania haikuwa na upungufu wa ardhi bali lkilichoonekana ni madaraja ya watu. Badala ya kuwawezesha wazawa kumiliki na kuendeleza ardhi, chuki ikatawala.
Leo mashamba ya mikonge ni mapori na mashamba mengine yamebaki kuwa mbuga za wanyama.
Vipi kama serikali ingejenga uwezo kwa wazawa kwanza kwa kuwawezesha kumiliki ardhi!
Hata sasa hivi ardhi ipo lakini wangapi wanaweza kuiendeleza?
Kilichobaki ni wakubwa kujigawia mapande ya ardhi kwa kujua sehemu kubwa haina uwezo wa kuendeleza achilia mbali kumiliki.
Mandela alichokifanya ni kuweka sheria ya skills development act ili kwanza kuwajengea uwezo wakati wanawamilikisha ardhi bila kuathiri uchumi kwa namna moja au nyingine,
Zimbabwe, Mugabe amewanyang'anya ardhi. Nashangaa ukisema waafrika wamefaidika.
Sijui wamefadika na nini wakati wanazamia Tanzania na ni deal.
Uchumi wa Zimbabwe mwaka 1980 na 2013 ni sawa na 'mbingu na ardhi'
Hawa wananchi wanaosubiri mahindi kutoka Tanzania wamefaidika vipi na harakati za akina Hunzwe na Mugabe?
Mchango wa akina Samora, Nyerere na Kaunda unathaminiwa.
Unachosahau ni kuwa kwa miaka 27 Mandela alikuwa jela sijui ulitegemea ashiriki vipi katika ukombozi.
Huwezi kulinganisha role za watu mbali mbali kwa kuwaweka katika mizani kama sukari na jiwe la kupimia.
Kwa mfano unamlinganisha vipi Nyerere na Samora.
Nyerere alishiriki kuandaa mazingira, Samora alikuwa msituni.
Na wala huwezi kuweka katika mizani role ya Kaunda na Nyerere katika ukombozi hata Kaunda anakubali hilo
Nimalizie kwa kusema nipe kiongozi wa taifa moja tu duniani aliyewahi kulijenga taifa kwa miaka 5 kwa kukabiliana na kila changamoto aliyokutana nayo
Mandela hakuwa kiongozi wa kujenga taifa , alikuwa kiongozi wa kulileta taifa lililoparaganyika pamoja ili waje watakaoliendeleza.
Na kama tunadhani mandela alifanya makosa ya kutowanyang'anya ardhi wazungu, iweje sisi tuliowanyang'anya miaka 50 iliyopita tunakwenda South Afrika kuwaalika waje tuwamilikishe ardhi.
Je tumeondoa boriti machoni mwetu kwanza kabla ya kuondoa kibanzi kutoka jicho la Mandela?