Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Sehemu II

SIKU 100 ZA UTAWALA

Katika siku 100 utawala wa Rais Trump umefuta takribani 28 Exec order(EO) za mtangulizi wake
Si jambo geni ndivyo ilivyo kwa US kutokana na kampeni na platform ya uchaguzi

Hakuna mswada uliopitishwa na House au Senate katika kipindi hicho
Ahadi azliotoa za kampeni zile kubwa zinazohitaji house na senate hazijafanyiwa kazi

Katika EO zilizofanyiwa kazi baadhi yake ni Key stone pipe ambayo kwa mujibu wa Rais Trump katika mkutano wa leo inatarajiwa kutengeneza ajira 48,000.

Wataalam wanasema ni kati ya 60,000 na sehemu kubwa itakuwa upande wa Canada.

Ipo EO inayofuta marufuku ya utafutaji mafuta Arctic, kuruhusu kuchimba mafuta.
Arctic ina mzozo wa mipaka na huenda ukazuka ukihusisha nchi nyingine

Kwa mujibu wa wataalam, ili mafuta yachimbwe kwa faida bei ya pipa inatakiwa iifikie dola 150

Hili tuliliona Canada (oil sand) ambapo kuanguka kwa bei kulilazimisha kufungwa kwa shughuli.

Kuna kiwango cha bei ambacho chini ya hapo gharama za uzalishaji zinakuwa kubwa kuliko mapato.

EO ya kutumia hifadhi imesainiwa. Zipo hifadhi ambazo kwa karne haziajaguswa.
Obama aliongeza maeneo. EO imefuta sehemu kubwa, ikiacha zile zilizo na masharti mazito

Hii ni kupata maeneo ya kuendeleza. Utata ni je, nani atapewa na kwa faida gani kwa US

EO kuruhusu uchimbaji wa coal kuanza, miongoni mwa ahadi za kampeni.
Inaelezwa miradi ya clean energy iliyoanzishwa wakati wa Obama inaajiri zaidi ya coal

Je, coal itaweza kurudi, linabaki swali. Suala la coal linauhusiano mkubwa na afya
Health care ya Obama ilionekana kuwalinda wachimbaji

Healthcare iliyoshindwa ilipingwa na wachimbaji kwa hofu ya kuondolewa 'benefit'

OE tulizoeleza zinakumbana na wanaharakati wa mazingira mfano maandamano leo DC

Swali linabaki, concern ya ajira itaweza kufunika hoja za wanaharakati wa mazingira?
Je, Trump ataiondoa US katika mkataba wa mazingira duniani?

Sehemu ya II inaendelea
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Sehemu ya III

SIKU 100 ZA UTAWALA

Tunakumbuka Trump alisema yeye ni mfanyabiashara anajua kufanya 'deal'
Kwamba anakwenda DC ku drain the swamp

Ukiacha EOs yapo yaliyokuwa kipaumbele na kauli mbiu za uchaguzi

ACA (Obamacare). Ilikuwa ni hoja ya Rais Trump kama kibwagizo.

Aliahidi kuifuta siku ya kwanza. Kilichotokea ni kusaini 'symbolic EO' kufuta Obamacare
Rais Trump alifanya hivyo kupendeza kundi linalomuunga mkono kwa kutimiza ahadi

Mbele ya safari, Healthcare ikawa mwiba ikipigwa chini kabla ya kura katika House
Waliokataa si Dems ni GOP waliogawanyika , Freedom caucus na moderate na conserv

Trump akakiri hakuelewa Obamacare ilikuwa complicated kiasi hicho.
Hoja ya deal maker, anaweza ku drain swamp kwa maana ya establishment haikuwa kweli

Deal maker katika majengo si sawa na utawala. Waliomkwamisha ni the establishment

Jitihada za kuandika upya ili alau awe na kitu siku 100 zilikwama juzi.
Hakukuwa na kura kwasababu ndani ya Republican hakuna maelewano.

Ingawa hoja za freedom zimezingatiwa, moderates wanaona wamewekwa pembeni na conservative wakiona hakuna anayewasikiliza

Kwa hali yoyote kufeli kufuta Obamacare katika siku 100 ni kufeli kwa hoja kuu ya utawala

Obama alisema kama kuna mwenye Healthcare tofauti aiweke yeye ataunga mkono
Kwa miaka 7 Repu na Trump hawana, kila wanapojaribu lazima waguse Obamacare

Mgogoro uliopo, freedom caucus wanataka Obamacare ifutwe kabisa kiandikwe kitu kipya

Moderates wanasema, yapo mazuri ya Obamacare yaachwe katika mswada

Conservative yasiyoendana na values zao kama abortion,medicaid n.k. yaondolewa.
Watu waachwe huru , wapewe pesa za kujihudumia

Trump akiwa amebeba hoja kwa miaka kadhaa na ahadi za kampeni ana misimamo inayoyumba Kwanza, aliwahi kuunga mkono abortion na kupata ugomvi na conservatives na freedom caucus. Akabadili msimamo na hapo ugomvi ukawa na moderates

Aliahidi pre existing conditions zitabaki kama zilivyo, freedom caucus hawataki, conser. hawataki
Akiondoa pre existing conditions tayari ugomvi unahamia kwa moderates

Ni kwa msingi huo, suala la Healthcare limekwama ndani ya Republican si Democrats

Ingawa Trump anasema litafanikiwa, kufanikiwa kutakuja na gharama kubwa ya kisiasa

Inaendelea.....
 
Sehemu ya IV

SIKU 100 ZA UTAWALA

Tax cut ilikuwa ni jambo muhimu katika kueleza kwanini anaweza kuimarisha uchumi
Wafanyabiashara waliona fursa hiyo na hakika masoko ya wawekezaji yamezidi kuimarika

Katika siku 100 Trump ameshinda kutekeleza tax cut akiizungumzia siku za mwisho katika kupendeza tu watu wake ili kuonekana anatimizia ahadi. Tax cut kama Obamacare ni complicated sana

Trump hakujaribu kuifikisha katika house kwa kujua kufeli kwa Healthcare kungefutiwa tax cut

Kufanya tax cut si suala gumu, ugumu ni matokeo ya tax cut katika uchumi , Bajeti na madeni

Rais Trump anasema tax cut itavutia wawekezaji na kutengeneza mamilioni ya ajira
Anasema kupitia tax cut itakayozaa ajira, deni linalotokana na tax cut litajilipa lenyewe kwa kodi

Republicans wanasema tax cut itazaa 'budget deficit' na hivyo kuongeza deni la Taifa
Ikumbukwe moja ya values za Republicans ni kupunguza matumizi na deni la Taifa

Dems wanasema kama Trump anamshambulia Obama kwa kuongeza deni la Taifa, kwa tax cut anategemea nini na atalipaje deni litakalotokana na hilo?

Lakini tax cut inakuja na hoja nyingine za uchaguzi ambazo zinazidi kukwamisha

1. UKUTA:
Aliahidi kujenga ukuta kuzuia illigeal immigrants na kwamba Mexico watalipa gharama
Siku za kwanza za utawala , Mexico walimweleza wazi hawatalipa, na Trump hana la kuwafanya

Trump anapokwenda kuomba pesa za kujenga ukuta, wakati anategemea tax cut ni suala utata
Rep wanaona ukuta ni mzigo utakaongeza deni achilia mbali kuchoanganisha na wapiga kura

2. Kuna mpango wa 1Trillion Infrastructure:
Trump aanategemea kuomba Trillion kwa ajili ya miundombinu.
Hili linaungwa mkono na Rep na Dems kwani lita stimulate uchumi kila eneo

Swali linalozuka ni kuwa pesa hizo zitatoka wapi katika tax cut kubwa anayotegemea?

Ni kwa mtazamo huo ahadi ya kujenga UKUTA imekwama katika siku 100 za utawala wake

UKUTA na OBAMACARE zilikuwa 'mantra' zilizoongoza kampeni. Katika siku 100 zimefeli

Inaendelea
 
Sehemu ya V

SIKU 100 ZA UTAWALA

Katika hali isiyo ya kawaida, Rais Trump aliishambulia Canada kibiashara kupitia NAFTA
Alisema ni mkataba mbovu nyakati zote za kampeni na kwamba ataufuta kama TPP

Kujitoa kwa US katika TPP kumeipa China nafasi ya kujitanua kupitia nchi washirika

Trump alisema Jibini (cheese) inaharibu soko bila usawa wa kibiashara.
Aliyasema hayo akiwa Wisconsin, state inayozalisha jibini kwa wingi

Rais Trump hakuangalia au alisema tu kwa ajili ya kupendeza watu wake.

Jibini inayozalishwa Canada haifiki 1/3 ya Wisconsin.
Tatizo si jibini inayoingizwa bali kufurika kwa jibini na kupunguza mahitaji

Pamoja na Jibini ya Canada kuuzwa US, kuzuia kuingia hakutabadili hali ya soko
Impact ya zuio haiwezi kuwa na matokeo yanayotarajiwa kwa Badger state

Siku ya 97 , Trump akazungumzia kuzuia uingizaji wa mbao kutoka Canada
Mgogoro wa soft lumber upo miaka 10 hadi kufikishwa WTO ambako Canada ilishinda

Katika harakati za kufikia siku 100 Trump akasema atafuta mkataba wa NAFTA
Hili lilizusha sintofahamu kwa Mexico na Canada kwa wananchi na maseneta wa Marekani

Seneta McCain alisema haikuwa busara kufuta NAFTA,mwingiliano wa kibiashara ni mkubwa na wa siku nyingi. Maseneta na wabunge hasa wa states za mipakani walionyesha hofu

Rais Trump alishauriwa na 'waziri' wake wa kilimo haikuwa busara.
NAFTA ni soko , kuifuta kutaathiri biashara za wakulima, wafugaji na wenye viwanda

Katika kawaida ya kubadili misimamo, Trump akasema amepigiwa simu na viongozi wa Canada na Mexico wakimtaka asifute NAFTA. Hapa alitaka kuonyesha ameombwa, kupendeza wafuasi

Ukweli, NAFTA inanufaisha pande zote, US ikiwa na soko katika nchi hizo na kinyume
Mathalani, kufuta NAFTA kutazuia kuingia kwa Mbao (soft Lumber)

Hatua itatengeneza ajira kwa wauza mbao wa US. Hata hivyo gharama ya Mbao US itapandisha gharama za ujenzi ambazo mwisho mtumiaji ataathirika, na sekta ya ujenzi itaathirika

Ajira zitatengenezwa lakini haziwezi kuwiana na athari itakayotokana na hatua hiyo

Kufuta NAFTA kutaathiri wakulima wa mboga na Matunda.US ni wazalisha na soko ni NAFTA

Hadi sasa hatua za kuondoa wahamiaji kutoka Mexico zinaonyesha athari.
Kazi za mashambani hazifanywi na Wamarekani, na wakifanya ujira ni mkubwa

Maana yake, gharama za kuzalisha zitaongezeka, na kufidiwa na mlaji.
Suala ala ajira halitakuwa na matokeo wazalishaji watajikita kupunguza gharama kwa mashine

Ndivyo utengenezaji wa vitu kama magari utakavyokuwa na athari.
Kwa muda mfupi ajira zitatengenezwa, kwa muda mrefu wazalishaji watahamia katika mashine

NAFTA ni mkataba wa muda mrefu kibiashara kufikia dollar takribani 1.2T kwa mwaka.
Kufuta tu lazima kutaathiri system ya nchi zote husika

NAFTA, kama Obamacare na Ukuta haikufutwa kwa siku 100 kama ilivyoahidiwa

Inaendelea...
 
Sehemu ya VI

SIKU 100 ZA UTAWALA

Kwa muda msuguano si kati ya WH na Congress bali ulihusisha eneo la Sheria

Katika hoja ya kuzuia wahamiaji haramu, ikiwa ni EO imezuiwa na mahakama
Amri ya kuzuia serikali kuu kutoa pesa kwa 'miji inyohifadhi' wahamiji haram imekwama

''Mafanikio'' ni ya uteuzi wa Jaji ambayo Obama alimteua Garland na seneti haikumsikiliza.
Jaji Gorsuch amepita baada ya kanuni kubadilishwa na kuwa simple majority na si 60

Kwa kuangalia siasa za ndani na ahadi za kampeni, katika siku 100 Trump hazina lililofikiwa
Hoja ya kwamba ni deal maker haijafanya kazi,kuendesha nchi kama shirika haikufanikiwa

Kauli alizotoa katika kampeni zimebadilika akichukua misimamo tofauti kabisa, mfano

Aliyesema namba za ajira ni fake sasa anazitumia kunadi mafanikio
Alisema atakaa WH kufanya kazi. Safari za Mar alago zinaanza kutia shaka(gharama)
Trump alikemea Rais kucheza golf, katika siku 100 kacheza kuliko Marais waliomtangulia
Alimsema kuhusu transparency, yeye akikataza hata wageni wanaofika WH kujulikana
n.k. n.k.

Ugomvi na media upo pale akiizita fake kwasababu hutoa kauli zake za nyuma na za sasa na kuonyesha kuyumba kwa misimamo, hapendi.

Media zimekuwa mwiba katika kujadili suala la Russia ambalo hadi sasa limepiga hodi WH

Tulisema siku za nyuma, Russia ilikuwa inatafuta njia, ilianza mitaani ikaenda Trump Tower na sasa ipo WH baada ya kuombwa kutoa nyaraka zilizotumika kwa vetting ya Mike Flynn

Kwa namna fulani suala la Russia limechukua sura za aina nyingi katika siasa za ndani za US
1. Zimefunika habari na kumwezesha Trump kufanya EO hata zenye utata bila kujadiliwa
2. Zimefunika agenda za ndani, kile kidogo kilichopatikana katika 100 hakikuzungumzwa
3. Zimeweka wingu linaloranda randa na kumtia hofu Trump kila uchao

Hakuna ithibati kuhusu ushiriki , wasi wasi ni anapotumia mbinu kulifunika jambo hilo badala ya kuliacha limalizike ikiwa hakuna tatizo. Hili limeongeza sana curiosity

Siku 100 ni utamaduni,Trump alizishikia bango siku za nyuma ingawa anaziita ni 'foni'

Kauli hizo ndizo zimekuza jambo akitakiwa kuonyesha amefanya nini, kwa bahati mbaya hakufikia matarajio ingawa kwa kundi linalomuunga mkono hakuna tofauti

Hii haina maana ni mwisho!ana miaka 4 na nafasi kubwa tu ya kufanikiwa

Kwasasa atakuwa amejifunza somo la utawala, tofauti ya serikali na shirika binafsi

Siasa za nje zina utata mkubwa, kwa undani ni siasa za Obama zinazochagizwa na maguvu.

Tutajadili siasa za nje

Inaendelea
 
Asante kwa somo Nguruvi3...nilikuwa napitia post za nyuma nikakutana na hizi mbili za bingwa mwingine wa uchunguzi Mh. El Jefe, basi nimecheka kweli kweli! Jamii Forums kweli ni kiboko kwa kumbukumbu na mtu akichukua time akasoma tuliyokuwa tunayatabiri na upinzani tuliokuwa tukiupata kwa watu wale wale...hebu pitia hizi mbili tu...
Kuna watu wanai-support ACA bila kuzungumzia uongo wake, huku wakiuliza kuhusu alternative health plan ya Rais Trump...

House Republicans wanayo health plan yao hata kabla ya ACA, Tom Price anayo alternative plan (ukizingatia alikuwa critic mkubwa wa ACA) ambayo ndio Rais Trump anazungumzia. Kinachoendelea ni kuzi-merge ili kuja na comprehensive health plan inayoitwa 'Trumpcare'.

Ukweli ulio wazi ni kwamba ACA ya Obama haina mda mrefu, itakuwa historia.
Halafu niseme tu kwa wale watu wanaoshikilia bango Obamacare, kuwa haitafutwa na kwamba ikifutwa itafuta wengi Congress waelewe tu kwamba wataofutwa Congress mwaka 2018 ni Democrats na sio Republicans maana ni ya kwao.

Kuna watu wengi tu walimpigia Rais Trump kura kwa ahadi ya ku-repeal na ku-replace Obamacare maana ilikuwa na bado inawaumiza.

Kwa mtu asiyejua atasema Rais Trump hana mbadala wa ObamaCare ndio maana anasema Repeal na Replace inaweza kufanyika mwaka 2018. The good thing ni kwamba with President Trump, it will be done.
Kweli hujafa hujaumbika...ha ha haa! Hiyo ni healthcare tu bado immigration na tax reform! Katika siku zake mia kafanikiwa tu kusign executive orders zisizo na hesabu (kasahau alimshutumu sana Obama kwa hilo) na hata hizo nyingi zimenyongwa bila huruma na mihimili inayohakikisha Katiba haichezewi hovyo kama hapa kwetu. Nao ukuta wa kulipiwa na Mexico hata msingi wake umeshindikana.

Endelea kutupa somo Nguruvi3, wengine tunafuatilia na kufaidika sana unavyotuhabarisha. Trump angekuwa Rais wa Tanzania, mbona angepata mteremko zaidi hata ya Magufuli na hivi sasa labda Wapinzani wote wangekuwa wametekwa, wameteswa na kupotezwa hata zaidi ya Magufuli. Bahati nzuri (ila mbaya kwa akina El Jefe) Marekani ni habari nyingine na amshukuru sana huyo mnyoa kibudu wa NK...kampa breathing space ingawa kibano kiko pale pale kinamsubiri.
 
Sehemu ya III

Mgogoro uliopo, freedom caucus wanataka Obamacare ifutwe kabisa kiandikwe kitu kipya

Moderates wanasema, yapo mazuri ya Obamacare yaachwe katika mswada

Conservative yasiyoendana na values zao kama abortion,medicaid n.k. yaondolewa.
Watu waachwe huru , wapewe pesa za kujihudumia

Trump akiwa amebeba hoja kwa miaka kadhaa na ahadi za kampeni ana misimamo inayoyumba Kwanza, aliwahi kuunga mkono abortion na kupata ugomvi na conservatives na freedom caucus. Akabadili msimamo na hapo ugomvi ukawa na moderates

Aliahidi pre existing conditions zitabaki kama zilivyo, freedom caucus hawataki, conser. hawataki
Akiondoa pre existing conditions tayari ugomvi unahamia kwa moderates

Ni kwa msingi huo, suala la Healthcare limekwama ndani ya Republican si Democrats

Ingawa Trump anasema litafanikiwa, kufanikiwa kutakuja na gharama kubwa ya kisiasa

Inaendelea.....
Mkuu Mag3 JF inakumbu kumbu, wakati ule hatukueleweka, anayetazama mabandiko ya nyuma ataona tofauti ya ushabiki na uelewa

Mkuu tulisema US si Tz, US system inafanya kazi na si rahisi kupeleka mambo mtu atakavyo

Trump analalamika taratibu za Congress ni mbaya, hakumbuki ndizo alizofanyia kazi Obama , Bush, Clinton , Bush, Reagan, Carter, zikamnyoa Nixon n.k.

Jana tumeandika kipande hicho hapo juu. Leo kilichotokea Hill ni kama tulivyosema.

Moderates GOP wanajiita 'Tuesday caucus' tayari wanapinga Trumpcare.
Tulisema kuondoa pre existing condition ni tatizo, wamejaribu kuwaridhisha freedom caucus na conservative. Ugomvi umehamia kwa moderates

Hiyo ni prelude ya midterm 2018 kwasababu Obamacare umaarufu wake upo katika pre existing condition na medicaid. Kuchomoa hayo ni kusaka ugomvi hata kama Trumpcare itapita kwa nguvu

By the way kwa miaka 7 hakukuwa na version nyingine zaidi ya Obamacare, waliosema itafutwa kwa kalamu kama kuchora katuni siku ya kwanza, nyuso zao zimesawajika.
JF kisima cha ufahamu

Mkuu ngoja tumalizie siasa za nje

Hapa napo tuliwahi kusema utata huu; Russia , Iran, Syria , China
Kisha tukaeleza China, Korea N, Korea S, Japan
Tukamalizia na Afghanista, Iran, Iraq, Saudia, Pakistan
Tulieza umuhimu wa NATO na kwa faida ya nani

Kinachofuata ni kunyumbua hayo katika uhalisia kama unavyotokea

Tusemezane
 
Sehemu VII

SIKU 100 ZA UTAWALA

SIASA ZA NJE

Wakati wa kampeni Rais Trump alisema US haina sababu ya kutumia rasilimali zake kulinda mataifa mengine akitolea mfano wa Japan na kwingineko

Aliahidi kutumia rasilimali kwa mambo ya ndani, ushirika kama NATO ni obsolete

Hapa JF tulieleza ,usalama wa US si hisani kwa nchi nyingine, ni muhimu kwa US
Kwamba majeshi ya US yametawanyika duniani katika kulinda masilahi yake

Tulisema ufungamano wa masuala ya dunia hauipi US nafasi ya kukaa kando
Na wala haiwezi kutenda bila kuwa na washirika hata wale US isiyowaaamini

Rais Trump akiwa mgombea aliwaahidi Israel mambo mazuri
Siasa za US mashariki ya kati zinaegemea Israel zikiangalia washirika wa karibu

Sera za kupinga upanuzi wa makazi ya Wayahudi ni za US wala si Dem au GOP
Mgogoro wa Israel na Palestina unagusa mashariki ya kati yote ukialika wasiokuwepo

Katika siku 100 Trump amekutana na ukweli,akaitaka Israel isitishe upanuzi wa makazi.
Hili ni kinyume na ahadi wakati wa kampeni akimlaani Obama

Rais Trump aliahidi kumaliza mgogoro wa ISIS katika siku 100.
Kwa muda mapambano yanaendelea kwa kutumia washirika kama Iraq

Obama anaonekana kuchelewa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya ISIS'
Alichotaka ni kujenga majeshi ya Iraq yachukue jukumu, si askari wa US

Pamoja na kukuta msingi huo, Trump hajafanikiwa kwa ISIS katika siku 100

Mgogoro wa ISIS Iraq ni complicated, si kitu rahisi. Tutajadili

Inaendelea....
 
China anasema hataki mitambo ya THAAD pale Korea Kusini. Na amezitaka Seol na Washington wasimamishe mpago wa kuzisimka. Vinginevyo atachukua hatua, mahususi kulinda maslahi yake. Sina hakika kama Trump aliliwaza hili.
-RT.com
 
Sehemu ya VIII
SIKU 100 ZA UTAWALA

ISIS inayosemwa chimbuko lake ni Iraq na Al Zaqawi.
Ipo org katika misingi ya itikadi za imani na tofauti baina ya

Imesambaa mashariki ya kati, na kutumia mwanya wa Arab Spring kuchanganya watu
Syria inao wakimshambulia Assad, lakini pia wapo wapinzani wa Assad wasio ISIS

Assad anapigana na waasi wake na ISIS kwasababu hajui nani ni yupi, wote ni adui
Kwa maana hiyo, anasaidia vita dhidi ya ISIS

Obama alisita kuingia kwa kujua anaweza kuwasaidia waasi wa kweli au ISIS bila kujua
Russia wanataka kumlinda Assad kwa kupambana na waasi bila kujua ISIS

Huo ndio msingi wa Trump kusema Russia ni maswahiba akisahau mgawanyiko
Lakini pia ISIS wamesambaa kwasababu si organization iliyo sehemu fulani

Vita dhidi ya ISIS Iraq itaendelea hata pale miji itakapokombolewa

US kumshambulia Assad ina mchanganyiko.
Hakuna mkakati wa kumuondoa Assad kama alivyosema
Tillerson. Assad anasaidi kushambulia ISIS/Wapinzani. Kwanini ashambuliwe?

Shambulio lilikuwa kuathiri nchi kama Iran na NKorea kisaikolojia
Ndiyo maana baada ya Syria ilipigwa MOAB kule Afghanistan

MOAB ni ghali na ilitumika katika maeneo ya porini.
Madhara yake kwa Taliban hayaelezwi ukilinganisha na ukubwa wa Bomu

Hiyo ilikuwa kupeleka ujumbe Iran na Nkorea katika kuwatisha.
Tuliona baada ya Syria na MOAB, Trump alianza na Iran na Korea

Katika siku 100 za maguvu Trump amerudi kwenye Diplomasia kama Obama

Kosa alililofanya ni kutounganisha vipande husika katika 'puzzle' kwa mantiki

Mantiki ni ile tuliyosema siku za nyuma. Russia, China, Iran.
China, Nkorea, SKorea, Japan. Syria, Israel, Iran. Saudi , US, Iran

Tutajadili
 
SIKU 100 ZA UTAWALA

Kosa alilofanya Trump ni kudhani 'deal' za biashara ni sawa na deal za utawala
Kampeni-Trump alisema siku 1 ataitangaza china kama 'Currency manipulator'

Akawasiliana na Rais wa Taiwan bila kujali sera ya One China.
Trump akatangaza kusimama na Israel katika kupanua makazi na ulinzi
Akatishia umoja wa NATO, na nchi za ASIA kuhusu mambo ya ulinzi na usalama

Trump akaweka travel Ban kwa nchi za kiislam kwa mujibu wa Rudi Guillian

Yote hayo hakujua yanafungama na yanahitaji diplomasia na uangalifu kuliko vitisho

Iran: Israel ingependa US ishambulie vinu vya Nyuklia. Obama hakutaka kwasababu ya madhara yatokanayo. Akaongoza China, Russia katika meza kidiplomasia

Majenerali wanasema, Iran ni kitovu cha Waislam madhebu ya Shia.
Kuwashambulia kutazua balaa middle east yote

Trump amerudi katika meza ya majadiliano kama ilivyokuwa sera ya Obama

China:
Rais Trump baada ya kuelezwa kuhusu ushawishi wa China, amesema si currency Manipulator bali mshirika. China ni jirani na mshirika wa uchumi na Nkorea

Kuanguka kwa Nkorea kutaleta balaa China. Kubwa zaidi kutaisogeza US mlangoni mwa China kama ilivyo Seoul. Huo ndio msingi wa China kuwa mshirika wa mzozo Nkorea

Majeshi ya US, Japan na Seoul si hisani, ni ulazima kuwa karibu na China na Nkorea.
Hii ni tofauti na Trump alivyodhani kuwa ni hisani kwa nchi hizo

China inatumia Nkorea kama ''bargaining chip'' na US.
Hivyo China ni mlinzi wa masilahi ya Iran na Nkorea na yale ya kibiashara na US

Utashngaa kuwa SouthKorea na Japan hawataki mvutano wa Korea Peninsula
Ni kwanini ikiwa wanalindwa na US? Tutajadili

Inaendelea....
 
SIKU 100 ZA UTAWALA

US inapeleka manowari Korean Peninsula ili kulazimisha NKorea kurudi mezani
Wakati huo huo, US inajenga missile defence system SKorea na Japan

Ieleweke umbali kutoka Seol hadi mpakani na Nkorea ni chini ya KM 100
Kwa maana nyingine ni karibu kuliko Dar na Chalinze

Japan ina mgogoro na China wa visiwa visivyokaliwa na watu vya Senkaku na Diaoyu
Licha ya rasilimali visiwa hivyo vipo katika lango la Asia-Pacific na vizuri kimkakati

Nkorea inatambua kusimama na US katika vita kuna madhara makubwa.
Wanasema, shambulio la US litapelekea Skorea kuzama na Japan kutekekea

US inazitumia Japan na Skorea kuhakikisha mgogoro wowote unaishia huko
Inazitumia kwa hesabu za kuwa karibu na China wakati wowote

Hilo linawafanya wakazi wa Seoul na Tokyo kuingiwa na hofu na Nkorea
Nkorea inakaribia kuwa na uwezo wa Intercontinental ballistic missile

Kuzifikia Japan na SKorea ni suala la muda si umbali au silaha

China haipo tayari kuona Japan na Skorea zikitumika na US, ni tishio la usalama
Japan haipo tayari kuona China inatumia mzozo, itazusha mzozo wa Senkaku

Kwa kutambua hilo , Jana Trump kasema yu tayari kukaa meza moja na Kim UN

Dhana ya Trump kuizogoa China na kudhani Silaha zina majibu haijatoa jibu siku 100.
Trump anarudi katika Diplomasia kama alivyofanya Obama.

Kwanini mzozo wa Korea Peninsula unaingia 'middle east'? Tutajadili

Inaendelea
 
SIKU 100 ZA UTAWALA

Uwepo wa majeshi ya US Korean Peninsula sijambo linaloipa raha China
China inasema mzozo umalizwe mezani, si kuweka makombora Japan na Skorea

US inawakusanya washirika wa Ulaya kuhakikisha shinikizo Nkorea linafanikiwa
EU wana wasi wasi na msimamo wa US kwani ilishaonyesha NATO ni obsolete

Trump alimwalika kiongozi wa NATO na kusema bado ni chombo muhimu cha ulinzi
Katika siku 100 kauli ya NATO ni obsolete imefutwa, ni felia nyingine kwa utawala

China ina karata ya Iran ambayo EU ni washirika.
Karata hiyo itatumika endapo shinikizo la Nkorea litaendelea.

Ingawa Iran inaheshimu mkataba wa Nuke kauli za Trump zinaweza tibua

Hofu ya Iran kuwa na Nuke si kwa US bali mshirika wake Israel
Tayari kuna kauli kwanini Israel iruhusiwe kuwa na Nuke wengine wakatazwe

Hayo yakiendelea kuna mzozo wa Ukraine ambapo nchi za Ulaya zimeonyesha hofu
Kwa upande mwingine US iliyotakiwa kuongoza eneo hilo ipo kimya dhidi ya Russia

Russia ina karata nyingi za kucheza. Inahusika na Ukraine moja kwa moja, ina masilahi Syria, ni mshirika wa mazungumzo-Iran, na mshirika wa China kiuchumi

Tusisahau kuwa sakata la uchaguzi US na Russia lina sehemu muimhu ya maamuzi
Hakuna anayejua kina cha tatizo, kauli dhidi ya Russia kutoka US zinatiliwa shaka

Mwingiliano huo wa mtaifa na taasisi kama NATO umeleta hofu kuliko utulivu
Dhana kwamba mabomu yanamaliza migogoro ya dunia ina feli at least siku 100

Mivutano inayotokea ina sababu nyingine,ni kuondoa focus ya matatizo ya ndani
Katika siku 100 hakuna kilichofikiwa cha kujivunia ukilinganisha na watangulizi

ISIS wapo, Obamacare haikufutwa siku ya kwanza, UKUTA hautalipwa na Mexico au walipa kodi US, Tax cut ipo kiporo,NAFTA ipo, namba ya ajira hazina tofauti n.k.

Trump yupo frustrated akisema hakujua mambo ni magumu kiasi hicho

Je, amewaacha wapi mashabiki walioamini bila tafakuri?

Waliosema kuna wenye chuki dhidi ya, nyuso zao zipo wapi? Wanajifunza?

Tusemezane
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Eti Trump kafanikiwa kutimiza ahadi yake...ni ahadi gani hiyo TUJITEGEMEE? Je umemuona akisaini muswada wowote? Hebu leta habari kamili...
Wakuu Ebu nifafanulie hii, uwenda nimeelewa tofauti.

House Republicans squeaked by with a one-vote victory to repeal and replace the Affordable Care Act, better known as Obamacare, after months of negotiations and failed attempts to unite the conservative and moderate factions of the party.
With four empty seats in the House of Representatives, the GOP needed 216 votes to pass the American Health Care Act and fulfill their seven-year-old promise to rid the country of Obamacare. The AHCA passed 217-213, with no Democrats voting for it.


It is one of the first major legislative victories for President Donald Trump, who made repeal-and-replace a cornerstone of his campaign.

The bill is the first part of a three-pronged approach to repealing and replacing Obamacare. The second prong would allow Health and Human Services Secretary Tom Price to take administrative steps to remove regulations that Republicans say are driving up costs and decreasing options for Americans. The third part is reforming the healthcare system through additional legislation.

====
Hii si ni nyota njema kwa Trump?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
TUJITEGEMEE unapolizwa swali kisha ukaleta nukuu inaleta taabu kueleweka

Kuna swali la msingi, ametimiza ahadi ya kampeni. Ni kwa vipi?
Hapa ndipo panahitaji 'inputs' zako ili kila anayefuatilia aelewe ulimaanisha nini

Pili, unaelewa hiyo proposal ina kitu gani ndani?
Pengine utufafanulie mwenzetu umeona nyota njema eneo gani katika hiyo ''act''?
 
Mkuu TUJITEGEMEE

Siasa za US muundo ni tofauti na wetu.US wana upper and Lower house

Sheria zinavyotungwa ni tofauti na lugha ''Westminster'' tuliyozoea

Kwa mfano ni mara chache kusikia neno 'sequestration' kwa mabunge ya commonwealth kwasababu utaratibu ni tofauti

Kwa mtazamo huo lengo hasa ni kubadilishana mawazo na kuyafanya mambo yasiyoeleweka kirahisi kueleweka kwa wasomaji ili kila mmoja apate faida

Katika kurahisisha mambo kila jambo linaangaliwa kwa undani.
Ni hatari sana kuangalia mambo kwa mtazamo wa blog au paper fulani

Tangu jana tulikuwa kimya, hatukujua nini kilichomo katika act pendekezwa

Pili, tulisubiri kuona reaction ya jamii ili tathmini iendane na hali ilivyo

Tatu, tuliangalia nini kinafuata baada ya kura katika House

Tulisema, kufuta ACA ni process. Healthcare ni sehemu kubwa ya bajeti ya US

Tukasema Republican wana majority kuanzia magavana, house na seneti

Hata hivyo umeona ugumu uliopo katika siku 100 na kura 1 kutoka kuokoa jahazi.
Wapo Republican waliopinga, sina hakika kama umeliona hilo

Nina uhakika ulichokielewa,mswada umepita ACA itafutwa na ni nyota njema.
Sivyo! kuna mengi yanafuta baada ya hapo

Mkuu, kilichotokea jana ni hatua za awali katika house.

Inafuata seneti kupitia tena mswada huo na katika hilo kuna mambo mawili.
Mswada unaweza kufutwa au ukafanyiwa mabadiliko wakiita reconciliations

Baada ya kujua nini kimo ukilinganisha na ACA ya Obama tunaweza sema;
1. Nini kilitokea jana, kwanini mjadala ulikuwa masaa 3
2. Tunaweza kusema kwanini hakukuwa na CBO score
3. Tutarajie nini katika seneti
4. Ikitokea ABCD katika seneti nini kinafuata

Kwa sasa kusema 'anatimiza ahadi, ni nyota njema is nothing but 'jump the gun'

Tusemezane
 
Haya, mambo yamekuwaa mambo...! Wakati kitanzi kinaaza kukaza...

Breaking News: Trump fires FBI Director Comey!

FBI Director James Comey has been fired, according to the White House.

"Today, President Donald J. Trump informed FBI Director James Comey that he has been terminated and removed from office," the White House statement reads.

"President Trump acted based on the clear recommendations of both Deputy Attorney General Rod Rosenstein and Attorney General Jeff Sessions," the statement said
.
 
Back
Top Bottom