Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

FBI DIR. COMEY AFUKUZWA KAZI
-Uchunguzi wa Russia interference ukiendelea
-Yates na Clapper wajadili uzembe wa WH kuhusu Flynn
-Sakata linaingia Oval office kwa mwendo pole

Kwanza, mjadala wa health bill unakwenda katika seneti.
Tunasubiri wakati muafaka tujadili. Kwasasa tujadili la Dir Comey

Akiwa California mkutanoni, Dir Comey alitambua amepoteza kazi kupitia TV.
Licha ya ndege yake kuwa na mawasiliano, hakupewa taarifa

Hilo limetokea siku mbili tangu aliyekuwa mkuu wa DOJ(Dept of Justice) Sally Yates na Mkurugenzi wa usalama Jimmy Clapper kueleza kamati ya bunge nini kilitokea, na walionya vipi kuhusu Flynn kuwa mshauri wa ulinzi wa ulinzi wa Taifa

Flynn alifukuzwa kazi siku 23 baada ya gazeti moja kueleza madudu yake
Yates alisema idara ilitahadharisha mara mbili kuhusu Flynn na Russia

Pamoja na hayo, Rais Obama alimtahadharisha Rais Trump kuhusu Flynn

Kitendo cha WH kumuacha Flynn licha ya tahadhari kimeiadhiri serikali, kukiwa na shaka kwanini Gen Flynn alilindwa hadi magazeti yalipoandika na si taarifa

Zipo taarifa kuwa FBI waliitisha nyaraka za Flynn kwa mamlaka 'subpoena'

Tunaeleza haya ili kuelewa kwanini haya yanatokea. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya FBI, Flynn, Yates, Comey na Washirika wengine wa kampeni ya Trump

Ikumbukwe Yates wa DOJ alifukuzwa, Sec Session (recuse)akajiweka kando kwa suala la Russia, Nunes akajiweka kando (recuse) kwenye kamati ya bunge

Kama mtakumbuka tulisema suala limeanza mitaani likitafuta njia kufika linapotarajiwa.

Kwasasa si washirika tena wa Trump bali WH inajikuta katika sakata

Inaweza kutoeleweka kwa urahisi maelezo hapo juu, sehemu inayofuata tutaunga mambo yote hadi kufukuzwa kwa Comey

Inaendelea...
 
SAKATA LA COMEY
Inaendelea...

Gen Flynn ni mhusika muhimu sana katika uchunguzi wa Russia

Secretary Sessions wa DOJ, alijiweka kando baada ya kubainika mahusiano na balozi wa Russia kinyume na kukataa kwake mbele ya kamati ya Bunge

Nunes mwenyekiti wa kamati ya Bunge alikwenda kinyemela WH na 'kumsafisha' Trump bila kuwasiliana na wenzake. Naye akatakiwa akae pembeni

Kuna mtu anaitwa Carter Page ambaye mahusiano yake na Russia yana utata sana

Kuna Manifort aliyekuwa kampeni meneja wa Trump kwa miezi 5 ambaye kama mwenzake Session anahusishwa na mazungumzo na balozi wa Russia

Hao wote na kwa uchache wao ni ''washirika'' wa kampeni ya Trump

Rais Trump alimteua Session ''kuweka' mambo sawa ndani ya DOJ
Kukaa kwake pembeni kunapunguza influence yake kwa sakata la Russia

Nunes, mbunge na m/kiti wa kamati ya bunge ya intelejensia kawekwa pembeni.

Mtu aliyebaki anayeweza kuwa msaada au kikwazo ni J. Comey wa FBI

Comey ali testify mbele ya kamati chini ya kiapo, kampeni ya Trump inachunguzwa
Kamati ya Bunge ilitaka nyaraka za Flynn kutoka WH.

WH ilikataa bila kuvunja sheria kwasababu haikutaka ijulikane nini kilichomo
James Comey akaitisha nyaraka hizo kwa mamlaka 'subpoena' kisheria

Tayari akaanza kuwa kikwazo kwasababu hakuna namna ya kumkatalia

Ili kuhakikisha uchunguzi ''unakwama'' mpango wa kumuondoa ukaandaliwa.
Tatizo likawa, Rais Trump atamfukuzaje ikiwa Comey anamchunguza?

Picha nzima ikachezwa kama tutakavyoeleza bandiko lijalo

Inaendelea...
 
SAKATA LA COMEY WA FBI

Kwavile Sec Session alijiweka kando uchunguzi wa Russia, acting akaandika barua ikapitia kwa Session ikieleza FBI kupoteza imani kwa umma kutokana na Comey alivyo handle suala la email la Clinton

Rais Trump yupo katika rekodi mara nyingi akimsifia Comey alivyoweka wazi uchunguzi wa Clinton siku 10 kabla ya kampeni.

Trump kasema anakubaliana na DOJ,FBI imepoteza imani kwa umma
Akamshukuru na kusema ' amueleza mara 3 kuwa hachunguzwi na FBI''

Kumbuka Comey alisema mbele ya kamati chini ya kiapo Trump anachunguzwa

WAPI WH IMEFANIKIWA NA WAPI IMELIKOROGA?

Kumuondoa ni mafanikio ya 'kuzuia' uchunguzi atakayemrithi atachaguliwa na Trump

Timing. Kwamba, walifanya timing nzuri Comey alikuwa aende mbele ya kamati
Tatizo: Hata kama wamefukuza bado ataitwa kama alivyoitwa Yates au Clapper

Akiwa hana cha kupoteza, na alivyodhalilishwa hili litazua jambo

Timing ni mbaya kwa upande mwingine.
Juzi tu Yates na Clapper wamemwaga habari zilizomchoma Trump.

Wiki ijayo Comey alikuwa a testify, idadi ya washirika na mawasiliano ikiongezeka
Swali, kwanini itokee sasa na kama sababu ni email kwanini isifanyike siku 100?

Na kwanini Session aliyejiweka kando alihusika na barua ya kumfukuza Comey?

Kwanini Trump amekubali kuondoka wakati Comey anachunguza Trump kampeni? Kwanini WH haikusubiri uchunguzi wa Inspector wa DOJ kuhusu Comey na emails?

Maswali yamezua tafrani viungani DC, Dems na GOP wakitilia shaka motives na timing

Moja ya shaka, Trump anataka ''cover up''kwa kutumia watu atakaowaweka.

Hili wamelifananisha na sakata la Nixon na Watergate.

Inaendelea....
 
SAKATA LA COMEY

inaendelea

Kutokana na sintofahamu ya jana, Democrats wamepata nguvu ya hoja ya independent prosecutor (IP) wa Russia meddling.

Dems wanaungwa mkono na moderate Republicans wanaohis 'cover up' inayoandaliwa na WH na uchunguzi mzima unakosa uhalali

Tatizo linalokabili hoja ya independent prosecutor ni moja.
IP anategemea habari za uchunguzi kutoka vyombo vya usalama na hapa ni FBI

Kuondolewa Comey kunatoa nafasi kwa Trump kumchagua Director 'loyal' kwake

Habari atakazohitaji IP zinaweza kuwa mislead, au zikafichwa au kufanyiwa usanii

Kwa mtazamo huo, WH imefanikiwa sana ''kuzima'' suala la Russia meddling
Si kwamba litazimika bali matokeo yake yanaweza kuwa na utata

Kwa upande wa pili, FBI dir. atakayeteuliwa na Trump lazima athibitishwe na Seneti
Kutokana na timing yenye mashaka, si rahisi kuweka mtu anayetiliwa shaka akapeta

Kwa sura nyingine, timing na maswali yanazidi kuongeza udadisi 'curiosity'
Kuna kamati ya Bunge, kuna kamati ya seneti na kuna FBI

Ni ngumu sana 'kuzimudu' kamati na FBI kwa njia za mkato. US ni tofauti

Halafu kuna media zinazofanya kazi independent.
Hizi zinaweza kuibua yasiyotarajiwa na kulazimisha uchunguzi ufanywe tofuati

Na mwisho kuna waliopoteza kazi, na wapo walio ndani ya vyombo hivyo
Cover up yoyote inaweza ku leak kama ilivyo kawaida ya DC

Kumuondoa Comey kunaahirisha tatizo na kupunguza 'maumivu' kwa muda
Kunazuia maji yasiingie ndani kwa kasi.

Ukweli utabaki kuwa suala la Russia litaendelea kuivuruga WH kila uchao

Tusemezane
 
Asante kwa somo Nguruvi3...nilikuwa napitia post za nyuma nikakutana na hizi mbili za bingwa mwingine wa uchunguzi Mh. El Jefe, basi nimecheka kweli kweli! Jamii Forums kweli ni kiboko kwa kumbukumbu na mtu akichukua time akasoma tuliyokuwa tunayatabiri na upinzani tuliokuwa tukiupata kwa watu wale wale...hebu pitia hizi mbili tu...

Kweli hujafa hujaumbika...ha ha haa! Hiyo ni healthcare tu bado immigration na tax reform! Katika siku zake mia kafanikiwa tu kusign executive orders zisizo na hesabu (kasahau alimshutumu sana Obama kwa hilo) na hata hizo nyingi zimenyongwa bila huruma na mihimili inayohakikisha Katiba haichezewi hovyo kama hapa kwetu. Nao ukuta wa kulipiwa na Mexico hata msingi wake umeshindikana.

Endelea kutupa somo Nguruvi3, wengine tunafuatilia na kufaidika sana unavyotuhabarisha. Trump angekuwa Rais wa Tanzania, mbona angepata mteremko zaidi hata ya Magufuli na hivi sasa labda Wapinzani wote wangekuwa wametekwa, wameteswa na kupotezwa hata zaidi ya Magufuli. Bahati nzuri (ila mbaya kwa akina El Jefe) Marekani ni habari nyingine na amshukuru sana huyo mnyoa kibudu wa NK...kampa breathing space ingawa kibano kiko pale pale kinamsubiri.

Hii thread imejaa mihemko na ushabiki usio na msingi.

Kuna watu wanajadili siku 100 kana kwamba walitegemea kila kitu kifanyike ndani ya siku 100, na bahati mbaya hawajui historia ndefu ya Congress na Administrations za US toka 1776 zaidi ya kuanza kufuatilia serikali za US kipindi cha Bill Clinton na zaidi zaidi kipindi cha G.W. Bush na Obama.

US politics ina historia yake na kadri siku zinavyoenda ina-jitwist kuendana na wakati na wanaoelewa wanajua haya mambo. Ndio maana wagombea wengi wa Urais- US wamekua wakihubiri Washington kubadilisha namna inavyofanya kazi ili kuleta maendeleo kwa haraka.

Lakini huo uharaka haupo US ukilinganisha na nchi kama China, US wanaendekeza u-vyama zaidi, wao kila kitu ni siasa. Ndio maana China kuipita US ni suala la muda tu.

Nilichozungumza kuhusiana na Healthcare sikukosea. Republicans lazima wata-repeal na ku-replace ACA, iwe mvua iwe jua Obamacare haina mda mrefu. Unaweza kuona walivyoipania na kwenye Senate wana option ya 'budget reconcilliation' kuitupa huko kwa simple majority, its just a matter of time.

kwa US, Healthcare, Immigration, tax reform na almost everything ni political issue.

Republicans hawataki kujaza watu wasio raia US, wala kuwapa watu Uraia au hifadhi kirahisirahisi na wana-favor massive deportations, suala la Uraia na mipaka wanaichukulia serious n.k. Democrats wapo tofauti ndio maana 'immigration reform' ya Obama ilishindikana kwa miaka yake minane.

Democrats lazima wataipinga immigration reform ya Trump kama ambavyo wanaleta arguments zisizo na uzito kwenye Border wall na Executive orders. Ila mwisho wa siku itapita.

Kwenye tax reform, vile vile, democrats wanaleta arguments zisizo sahihi kuwa Trump anataka kuwapa matajiri tax cuts kwa gharama za watu wa chini. Lakini kuna Senators wa Democrats wanaamini US ni moja kati ya nchi zenye kodi kubwa kwenye mataifa yanayoongoza kiviwanda na watamuunga mkono. Obama alifeli kwenye tax reform alitaka kuwaongezea kodi top 1% inayoajiri 80% ya watu, aliona akizunguka na Warren Buffett atapata business support lakini wapi!. Anyway, Obama knew less about taxes na economy hakujua hata alichotaka kukifanya na madhara yake.

Huko kwenye foreign policy Tillerson anapiga kazi fresh tu, kumbuka Trump anataka Millitary Spending iongezwe na ma-establishments, media (hata liberal) na raia wanaopenda vita wanamuunga mkono akifanya matukio yanayoonesha matumizi ya nguvu. Liberals na Establishments wanafanya juu chini Trump achukie Russia ndio maana wamemganda na suala la Russia ambalo kwa wanaoelewa na wanaojua wanaona limejaa siasa tupu na litaisha kama lilivyoanza.

Wasioelewa na wasiojua wanaona suala la Russia linaelekea Oval Office kumu-affect Trump, wanaohubiri hizi habari wanawaaminisha media hivyo na wanaoshinda kwenye hizo media hawana information tofauti na wanayolishwa. Dawa ni kuwaacha tu waendelee kufukuzia tembo mweupe.

Halafu mkuu, unavyosema Trump angekuwa kiongozi wa Tz angeteka au kutesa wapinzani ni dhahiri hujui kwamba Trump sio mtu wa kuweka maslahi ya chama mbele kama viongozi wengi wa Tz. Upinzani wa US unaweka vyama mbele, POTUS wengi hawaupendi. Pia Trump alikuwa republican, akahamia democrat, then akarudi republican na kugombea na kushinda sidhani kama anawachukia wapinzani.
 
El Jefe , kwanza kabisa ulishaaga ukumbi kumbe bado unachungulia! te te te

Usione haya na karibu. Muhimu ni kusaidia kuelewa kwa kidogo Tulichonacho.
Hatupo hapa kushabikia, kushindana au kufanya spinning za kipuuzi

Umerudi ili kuvunja mtiririko wa mabandiko 241 ambayo kwako hupendi kuyasikia.
Unataka ku 'divert' mjadala kwa kuingiza mambo irrelevant kwa wakati

Tumekueleza mara nyingi kama hukubaliani au huna hoja au unakereka, una hiari

Kuhusu siku 100, Trump alipigia upatu katika kampeni atatenda katika siku hizo
Tumeeleza siku 100 zilianzaje halafu tukaonyesha ahadi za mgombea Trump

Siku 100 ni ahadi za Rais Trump akitumia utamaduni huo, hatuzushi,rekodi zipo

Upo katika rekodi ukisema siku ya kwanza atafuta Obamacare kwa kalamu
Tunaofahamu tukakwambia pamoja na magavana, house na seneti si rahisi.

Kauli iliungwa mkono na Trump aliyesema 'hakujua ni complicated kiasi hicho' .
Aliposema atafuta siku ya kwanza ulidakia, hukujua ni complicated kiasi gani.

Uliongozwa na kauli tu si weledi, leo umebaki mtupu, Trump akiungana nasi

Huna ufahamu nini kimeondolewa ACA, nini kimeachwa na kwanini mvutano.
Hiyo act wamepitishwa kwa kura 1, jiulize kwanini

Nina uhakika unafahamu kwasababu unafuatilia uzi huu na hilo si kosa, jifunze

Hayo mengine ya Obama, tax, economy ni yako na irrelevant kwa wakati huu

Ni kuondoa watu katika suala la Comey, yapo siku nyingi, hukujadili iwe leo!

Ukija hapa uje na kitu cha kusaidia watu kuelewa hata kama ni kidogo

Habari za wewe kufuatilia hoja na spinning bila substance zinachefua
Haina mantiki wewe kusubiri wengine ili upate cha kusema.

Lini umma utajifunza hata neno moja kutoka kwako?

Kwasasa tulia ujifunze, lau kana una kitu kipya andika tusome.
Hili si eneo la innuendos, una hiari wala hujalazimishwa kusoma au kuchangia

Ahsante kwa kutojibu bandiko , na shukran kama utakuja na jipya la maana.
 
KOSA LA KIUFUNDI SAKATA LA COMEY

Katika barua WH iliyoandika, Trump anamshukuru Comey kwa utumishi
Anamshukuru pia 'kwa kumeleza nyakati tatu tofauti , FBI haimchunguzi'

Kauli hiyo ya kutochunguzwa na FBI ina matatizo kifundi
Kwanza, Comey ali testify katika kamati ya Bunge na kuthibitisha uchunguzi upo

Comey alikataa kueleza kwa kina akisema habari hizo ni classified information
Alimaanisha ni wale tu wenye security clearance wanaweza kupata ikibidi, si public

Rais Trump kujua kama anachunguzwa au la kutoka kwa Comey si kosa
Rais ana access na classified information na huenda alimweleza

Tatizo linapotokea ni , je, alimtaarifu kabla ya ku testify au baada ya hapo?
Alimtaarifu kwa maneno au zipo kumbu kumbu?

Kitendo cha Rais kusema 'alitaarifiwa na Comey wa FBI' tayari kina comporomise uchunguzi. Hilo ni sawa na ku declassify information zinazofanyiwa kazi

Ipo siku Comey ataulizwa kuhusu hilo na itabidi akubali au akanushe

Kwa upande mwingine, tayari Rais anaonekana ''amesafishwa''
Kusema maneno hayo ni kujisafisha mwenyewe wakati uchunguzi ukiendelea

Swali wanalojiuliza wengi ni kwanini Trump anaonekana kuwa na hofu ikiwa mwenyewe anathibitisha hakuna tatizo?

Tusemezane
 
Busted! Despite repeatedly denying that he met with the Russians during his 2016 campaign, it has been revealed that Presidential candidate Donald Trump spoke with and “warmly greeted” Russian Ambassador Sergey Kislyak prior to giving a foreign policy speech on April 27, 2016.

trump_ambassador-800x430.jpg

And then last night President Trump welcomes the Ambassador and there's no press release. (picture released by the Russian Embassy)

trump-kislyak-800x430.jpg

Busted! AG, Jeff Sessions (R-Ala.) spoke twice last year with Russia’s ambassador to the United States, encounters he did not disclose, when asked about possible contacts between members of President Trump’s campaign and representatives of Moscow during Sessions’s confirmation hearing to become attorney general.

blog_zuma_kislyak_sessions_0.jpg

Nguruvi3, nikiwa na mda kama ilivyo kwa watu wengine naangalia majukwaa tofauti ya JF, na niki-quotiwa sehemu huwa najibu kama kuna cha kujibu.

Hii thread yako huwa inanifurahisha tu jinsi wewe na mag3 mnavyojitahidi kutabiri hatma ya Trump na serikali yake. Actually huwa sioni tofauti kati ya unayoandika humu na yaliopo kwenye liberal media za US.

Mkuu, mi sipo kwa ajili ya kuvunja mtiririko wako, wanaokufuatilia wanajua maandishi yako.

AMERICAN HEALTH CARE ACT/AHCA (TRUMPCARE) vs AFFORDABLE CARE ACT/ACA (OBAMACARE).

Kuhusiana na Obamacare (ACA) umesoma hizo quotes za mag3?, Trump alirekebisha ahadi yake ya repeal na replace ya ACA hata kabla hajachaguliwa kuwa Rais, jaribu kuwa updated.

'Complication' ya healthcare unayozungumzia wewe ni tofauti na aliyozungumzia Rais Trump. Wewe huifahamu vizuri healthcare system ya US ilivyo ndio maana ni 'complicated' kwako.

Healthcare system ya US imegawanyika sehemu kuu mbili program za afya za (i) serikali mfano Medicaid (SHIP), Medicare, Federal employees HBP, Prescription Assistance, Millitary Health System/TRICARE, CHIP, PACE, Veterans Health Administration (ii) za Binafsi mfano Consumer driven health care/ CDHC (eg Health savings Account, Health Reimbursement Account, Flexible Spending Account etc), Health Insurance, etc.

Haya mabadiliko kama ACA na AHCA yanagusa baadhi ya health plan za watu na kuleta mabadiliko kadha wa kadha, lengo ni kuleta unafuu kwa watu.

Baadhi ya vitu vinavyobadilishwa ACA:

(ii) Kuhusiana na watu wenye pre-existing conditions. Kupitia ACA, makampuni ya bima hayawezi kuacha kutoa coverage kwa watu wenye pre-existing conditions (high risk pools).

Lengo la ACA ilikuwa ni kwamba watu wengi wenye afya (healthy/less risk pools/low premiums) wangejiunga (enroll) pamoja na wachache wenye afya mgogoro (unheathy/high risk pools/high premiums) ingepelekea mamilioni ya wananchi ambao hawakuwa na bima ya afya kabla kupata bima ya afya kwa bei ya chini (affordable).

Kwa maana hiyo ili ACA iwe affordable ilihitaji sign up nyingi za watu wengi sana wenye afya nzuri. Lakini pamoja na push ya Obama enrollment hazikufikia target ya CBO (Congressional budget office). Matokeo yake watu wenye pre-existing conditions wakasababisha premiums zikapanda kwa watu wengi.

Kupitia AHCA, makampuni ya bima yanaruhusiwa kucharge bei (premium) kwa watu hawa kulingana na medical underwritting (uchunguzi wa kina wa taarifa ya afya ya muhitaji bima). Ila watu hawa wenye pre-existing conditions wanahitajita kuwepo katika mfumo wa huduma ya bima ya afya (siku 63+ katika mwaka uliopita) na sio wasubiri mpaka waugue sana au wazidiwe ndio watafute bima ya afya. Wakisubiri kuna penalty (premiums zao zinaongezeka kwa 30%).

Ili ku-counter na ku-stabilise madhara ya hawa watu wenye pre-existing conditions (high risk pools) kwenye soko la bima ya afya (health insurance exchange market) kama kuongezeka kwa premiums ,AHCA inatoa fedha kwa makampuni ya bima kupitia States (majimbo), $ 15 Billioni kwa mwaka 2018 na 2019 na $10 Billioni kwa miaka inayofuata hadi 2026 wakati ACA inatoa $20 Billioni kwa mwaka.

Kwa hiyo Republicans wakitaka kuipitisha AHCA kwa 'budget reconcilliation', CBO watakuja na analysis yao ambayo kama haiongezi deficit (deficit neutral) inakuwa rahisi kupita Senate kwa simple majority.

(ii) Pia kuna mabadiliko (MacArthur Amendment) yalifanyika kutoka AHCA original ambapo majimbo (States) yanaweza kuomba serikali kuu (federal gov) kutengua kanuni kadhaa za ACA/Obamacare kama wakiweza kuthibitisha kuwa kutotumika kwa hizo kanuni kunaweza kupunguza gharama za bima ya afya. Majimbo yatakayotuma maombi hayo yatapata kiasi cha ziada $8 Billioni kwa miaka 5 (Upton Amendment) ili kuwawezesha kushusha bei ya bima ya afya katika health insurance exchange market hasa kwa watu wenye pre-existing conditions.

Moja ya kanuni ya ACA iliozua mvutano ni kuhusiana na 'community rating' ambapo makampuni ya bima yanapaswa kutoza bei sawa ya bima ya afya kwa eneo fulani bila kujali 'medical underwritting'. Kwenye AHCA, majimbo yanaweza kuomba serikali kuu kuitengua hii kanuni.

Freedom caucus walipenda hii provision kwenye AHCA na kusababisha ongezeko la kura 20 kwenye House. Moderate Republicans waliona kama hii provision inaweza kusabisha Majimbo kuondoa matumizi kwenye baadhi ya program na kuharibu mfumo wa mwajiri kutoa bima ya afya.

(iii) Tax credits ya kuwezesha watu kupata bima ya afya kulingana na mapato na makazi yao. American Health Care Act (AHCA) itatoa tax credits kwa wamarekani kulingana na umri.

Kwa mfano:
Chini ya miaka 30: $2,000 kwa mwaka
30- 39 : $2,500 kwa mwaka e.t.c

Lakini pia kuna income category mbili ambazo (mtu aliye na kipato juu ya $75,000 kwa mwaka na kaya/household yenye kipato juu ya $150,000 kwa mwaka) tax credit yao itapungua.

Tutaendeleza discussion ya US HealthCare. Then tuta-discuss Tax reform na Immigration reform.

KUHUSIANA NA COMEY

Aliyetoa recommendation kuwa Comey apigwe chini ni nani kama sio Rod Rosenstein (Deputy AG)?

Je huyo Rosenstein si alipata bi-partisan support katika Senate kuchaguliwa kuwa Deputy AG (94-6)?

Chuck Schumer, Nancy Pelosi na Democrats mara ngapi wamesema hawamkubali James Comey kwenye nafasi ya Director wa FBI? Sasa hivi wanajitoa fahamu kama kawaida kuendekeza siasa.

Huyo Chuck Schumer anamwambia Rosenstein kuwa yeye ndio tegemeo lao (Dems) kuhakikisha 'haki inatendeka' na anasahau ni kuwa ni huyo huyo Rosenstein alipendekeza Comey atoswe, funny.
 
Aliyetoa recommendation kuwa Comey apigwe chini ni nani kama sio Rod Rosenstein (Deputy AG)?
Kama hujui kitu ni heri kunyamaza. Uamuzi wa kumpiga chini Comey ulichukuliwa na Trump mwenyewe...Rosenstein na bosi wake Sessions waliagizwa tu kutafuta visababu vya kuridhisha na kazi hiyo waliifanya pamoja karibu usiku kucha.
Huyo Chuck Schumer anamwambia Rosenstein kuwa yeye ndio tegemeo lao (Dems) kuhakikisha 'haki inatendeka' na anasahau ni kuwa ni huyo huyo Rosenstein alipendekeza Comey atoswe, funny.
Yawezekana ulimsikiliza Schumer lakini hukuelewa kabisa sababu zilizomfanya kumtahadharisha huyo Rosenstein.
 
Kama hujui kitu ni heri kunyamaza. Uamuzi wa kumpiga chini Comey ulichukuliwa na Trump mwenyewe...Rosenstein na bosi wake Sessions waliagizwa tu kutafuta visababu vya kuridhisha na kazi hiyo waliifanya pamoja karibu usiku kucha.
Punguza jazba mkuu, una ushahidi gani kuwa Trump aliwaagiza Rosenstein na Sessions kutafuta 'vijisababu vya kuridhisha' na kwamba kazi hiyo waliifanya usiku kucha ili Comey apigwe chini?

Umesoma memo ya Rosenstein? Je ulimsikiliza Rosenstein wakati wa Senate Hearings zake? Ulipata kufahamu kuhusu position yake kuhusiana na Comey's handling ya email server ya Hillary toka mwaka jana?

Turudi nyuma kidogo, ina maana miezi sita baada ya kuapishwa kuwa Rais (July 19, 1993), Bill Clinton alipompiga chini William S. Sessions (Director wake wa FBI) kwa kufuata recommendations za Janet Reno (Attorney General), aliwaagiza Janet Reno (AG) na Philip Heymannn (Deputy AG) kutafuta 'vijisababu vya kuridhisha' ili William Sessions apigwe chini?

Yawezekana ulimsikiliza Schumer lakini hukuelewa kabisa sababu zilizomfanya kumtahadharisha huyo Rosenstein.

Chuck Schumer anahitaji Rod Rosenstein ateue 'independent prosecutor' kwa sababu ana mamlaka hayo bila approval ya Congress baada ya Jeff Sessions kuji-recuse na 'investigations za Russia'.

Kwa akili zao (Schumer et al.) wanaona kama Trump ana 'control' na uchunguzi huo ukiendelea kuendeshwa na FBI. Lakini Mitch McConnel (Senate Majority Leader) amemueleza Chuck Schumer (Senate Minority Leader) kuwa hicho kitu kitaharibu uchunguzi ambao umekwishafanyika na unaendelea kufanyika.

Tukirudi nyuma kidogo, mwaka 1993, hata Senate Minority Leader wa kipindi hicho, Robert J. Dole (R-Kan) pia alipinga uamuzi wa Bill Clinton kumfukuza kazi William Sessions (FBI director wa kipindi hicho) na kumtahadharisha AG.
 
Kama hujui kitu ni heri kunyamaza. Uamuzi wa kumpiga chini Comey ulichukuliwa na Trump mwenyewe...Rosenstein na bosi wake Sessions waliagizwa tu kutafuta visababu vya kuridhisha na kazi hiyo waliifanya pamoja karibu usiku kucha.
Yawezekana ulimsikiliza Schumer lakini hukuelewa kabisa sababu zilizomfanya kumtahadharisha huyo Rosenstein.
Mkuu nimemueleza mara nyingi sana. Kama hajui akae kimya. Mabandiko 241 etc tulieleza picha yote, mwenzetu hana habari

Kwanza, kitendo cha kusema ni kwasababu za emails za Clinton si kweli kwa mujibu wa Trump
Trump anasema hakufanya kazi nzuri, Roseinstein anasema emails.

Ukiangalia kulikuwa hakuna strategy ya kwanini Comey aliondolewa ndio maana kuna majibu tofuti kila asubuhi
Muulize Sessions anawezaje kuingia katika sakata lenye uhusiano na Russia ikiwa ali ji recuse?
 
Hata huyo Rosenstein mwenyewe sasa hivi anajaribu kutafuta namna ya kujiweka mbali na uamuzi wa kumfukuza Comey! Anasema hayakuwa mapendekezo yake per se...ni kama swala na kuku na yai!

Update...(Trump's own admittance in an interview)

It is now confirmed that President Trump had already made up his mind to fire FBI Director Comey even before his meeting with both AG Sessions and his Deputy Rosenstein!

[B]El Jefe[/B], ambalo halijathibitishwa ni Roenstein kutishia kujiuzulu kama atahusishwa moja kwa moja na maamuzi hayo.
 
...

And then last night President Trump welcomes the Ambassador and there's no press release. (picture released by the Russian Embassy)​
This is conspiracy Sir, White House photographer was also present during closed door meeting!
Ushahidi huu hapa chini
==========​
After the photos began circulating, members of the White House press corps inquired whether the Russian media had been allowed into the closed meetings.

The White House responded, according to a White House pool report, by saying, "On background, our official photographer and their official photographer were present, that's it."
Source: usatoday.com
 
Je, umejiuliza kwa nini WH wamechukizwa na hiyo picha kuoneshwa na TASS news agency?

The White House Is Apparently Upset That Russia Published Photos of Trump and Its Ambassador
 
Hata huyo Rosenstein mwenyewe sasa hivi anajaribu kutafuta namna ya kujiweka mbali na uamuzi wa kumfukuza Comey! Anasema hayakuwa mapendekezo yake per se...ni kama swala na kuku na yai!

Update...(Trump's own admittance in an interview)

It is now confirmed that President Trump had already made up his mind to fire FBI Director Comey even before his meeting with both AG Sessions and his Deputy Rosenstein!

Ambalo halijathibitishwa ni Roenstein kutishia kujiuzulu kama atahusishwa moja kwa moja na maamuzi hayo.
Mkuu, Katika mahojiano na NBC Rais Trump anasema alipanga kumfukuza Comey kabla ya kuonana na Sessions na deputy AG

Nashangaa hata hili linafanyiwa spinning, kwamba kuna mtu anaamini kwa dhati kabisa kuwa FBI dir aliyekuwa confirmed na Senate anaondolewa na Act AG!

Ndiyo maana nawaambia wengine kama mtu hajui aulize au akae kimya ajifunze.
 
KOSA LA KIUFUNDI SAKATA LA COMEY

Katika barua WH iliyoandika, Trump anamshukuru Comey kwa utumishi
Anamshukuru pia 'kwa kumeleza nyakati tatu tofauti , FBI haimchunguzi'

Kauli hiyo ya kutochunguzwa na FBI ina matatizo kifundi
Kwanza, Comey ali testify katika kamati ya Bunge na kuthibitisha uchunguzi upo

Comey alikataa kueleza kwa kina akisema habari hizo ni classified information
Alimaanisha ni wale tu wenye security clearance wanaweza kupata ikibidi, si public

Rais Trump kujua kama anachunguzwa au la kutoka kwa Comey si kosa
Rais ana access na classified information na huenda alimweleza

Tatizo linapotokea ni , je, alimtaarifu kabla ya ku testify au baada ya hapo?
Alimtaarifu kwa maneno au zipo kumbu kumbu?

Kitendo cha Rais kusema 'alitaarifiwa na Comey wa FBI' tayari kina comporomise uchunguzi. Hilo ni sawa na ku declassify information zinazofanyiwa kazi

Ipo siku Comey ataulizwa kuhusu hilo na itabidi akubali au akanushe

Kwa upande mwingine, tayari Rais anaonekana ''amesafishwa''
Kusema maneno hayo ni kujisafisha mwenyewe wakati uchunguzi ukiendelea

Swali wanalojiuliza wengi ni kwanini Trump anaonekana kuwa na hofu ikiwa mwenyewe anathibitisha hakuna tatizo?

Tusemezane
Mag3 kama ni ''utabiri'' huu sijui tuiiteje.
Ninachoweza kusema ni kuwa hakuna utabiri ni uelewa wa mambo tu.

Jana tuliandika bandiko hilo, leo linaleta tabu kwa akina McCabe.

Huo ni mwanzo tu Comey atatakiwa athibitishe au akanushe kuwasiliana na Rais kwa simu na katika hafla akimweleza Trump hachunguzwi wakati akieleza kamati tofauti

Hili la Comey limefunika na kuongeza curiosity.
Hata kama hakuna collusion bado litaisumbua serikali kwa muda mrefu

Kamati ime subpoena faili la Flynn. Kuna Carter Page, Paul Manufort, Rogers
Hao wote ni wapambe wa Trump kwa namna moja au nyingine.

Zipo ''habari '' kuwa Comey aliomba resource zaidi ili achunguze Russia meddling
Hilo linaweza kuwa moja ya sababu za Comey kuondolewa

Tayari kuna kutupiana mpira kuhusu Comey. Hakuna aliyedhani litakuwa kubwa kiasi lililpofikia.
Jitihada za kuingiza mambo mengine zinaonekana kukwama

Leo Trump amerudisha suala la ''illegal voters'' haionekana kama litafunika la Comey

Kinachotia wengi shaka ni jitihada za kutaka 'kuzima' suala zima.

Katika mazingira ya kawaida WH ingeruhusu uchunguzi umalizike ili usiharibu agenda nyingine

Kufukuzwa kwa Comey hakuta pita bila 'gossip au leak' .Inaweza isiwe leo lakini itatokea tu
 
Mkuu Nguruvi3, kuna wakati nilisema huko Marekani watu hawakurupuki hovyo na kwa bahati mbaya sana kwa sasa wanaye Rais ambaye kukurupuka ni jadi yake. Matokeo yake ni kwamba yuko shimoni na huko kidogo kidogo anatupiwa zana na yeye bila kujiuliza hizo zana za nini, anaanza tu kuzitumia...masikini anachimba huku tayari yuko shimoni. Wenzake hawana haraka, wanachungulia tu kutoka juu anavyojididimiza...!

Leo yuko huyu binti wa aliyewahi kuwa gavana wa Arkansas Gov. Mike Huckabee, Sarah, anajitahidi kuzuia tsunami kwa kiganja cha mkono akidai Rais ana haki ya kumtimua Comey! Ndiyo yawezekana ana haki hiyo lakini swali linalofuatia ni hili, je hiyo haki ni pamoja na kumtimua mkuu wa kikosi kinachomchunguza? Hii inaitwa gross abuse of power na inapingana na utawala wa kidemokrasia unaoheshimu sheria na kufuata haki.

Yako mambo yanawezekana tu katika nchi za kifashisti na si Marekani...Trump watu wameshamuelewa na mbinu zake za kubalisha gia hazitafanikiwa. Nasikia anapata wazimu anapoona watu walivyomvalia njuga hadi wale aliotegemea watamtetea, hata akiamua kuvua nguo na kutembea uchi mtaani, wako kimya. Comey mwenyewe alianza kujiuliza kama kweli huyu mtu ana akili timamu kwa vitendo na kauli zake zisizoeleweka!
 
After the photos began circulating, members of the White House press corps inquired whether the Russian media had been allowed into the closed meetings.
Yes, it is true Russian TV made its way into the Oval Office!

920x920.jpg

The White House responded, according to a White House pool report, by saying, "On background, our official photographer and their official photographer were present, that's it."
No, not true. A photographer for a Russian state-owned news agency was allowed into the Oval Office on Wednesday during President Donald Trump's meeting with Russian diplomats, a level of access that was criticized by former U.S. intelligence officials as a potential security breach.

The officials cited the danger that a listening device or other surveillance equipment could have been brought into the Oval Office while hidden in cameras or other electronics. Former U.S. intelligence officials raised questions after photos of Trump's meeting with Russian Foreign Minister Sergei Lavrov were posted online by the TASS news agency.
 
Back
Top Bottom