KOSA LA KIUFUNDI SAKATA LA COMEY
Katika barua WH iliyoandika, Trump anamshukuru Comey kwa utumishi
Anamshukuru pia 'kwa kumeleza nyakati tatu tofauti , FBI haimchunguzi'
Kauli hiyo ya kutochunguzwa na FBI ina matatizo kifundi
Kwanza, Comey ali testify katika kamati ya Bunge na kuthibitisha uchunguzi upo
Comey alikataa kueleza kwa kina akisema habari hizo ni classified information
Alimaanisha ni wale tu wenye security clearance wanaweza kupata ikibidi, si public
Rais Trump kujua kama anachunguzwa au la kutoka kwa Comey si kosa
Rais ana access na classified information na huenda alimweleza
Tatizo linapotokea ni , je, alimtaarifu kabla ya ku testify au baada ya hapo?
Alimtaarifu kwa maneno au zipo kumbu kumbu?
Kitendo cha Rais kusema 'alitaarifiwa na Comey wa FBI' tayari kina comporomise uchunguzi. Hilo ni sawa na ku declassify information zinazofanyiwa kazi
Ipo siku Comey ataulizwa kuhusu hilo na itabidi akubali au akanushe
Kwa upande mwingine, tayari Rais anaonekana ''amesafishwa''
Kusema maneno hayo ni kujisafisha mwenyewe wakati uchunguzi ukiendelea
Swali wanalojiuliza wengi ni kwanini Trump anaonekana kuwa na hofu ikiwa mwenyewe anathibitisha hakuna tatizo?
Tusemezane
Bandiko hilo tulileta kabla ya interview ya Trump na NBC siku ya alhamisi
Habari inayozungumzwa ni kosa hilo la kifundi ambalo Trump amelifanya kwa kujua au kutokujua
Tulisoma barua ya Trump na kujiuliza kama kweli alijua ABCD za Washington,DC
Rais Trump ametaja mara 3 alizoambiwa na Comey kuwa 'hachunguzwi'
Kwanza, katika dinner ambayo haukueleza nani aliandaa kwa undani na ilikuwa kujadili nini
Pili, Comey alimpigia simu kwa mujibu wake
Tatu, Trump alimpigia simu kumuuliza kama anachunguzwa
Kumbuka, Comey ali testify mbele ya kamati kuwa Trump kampeni ilikuwa inachunguzwa.
Hivyo ima Comey atalazimika kueleza ni kwa vipi na kama credibility ya uchunguzi ilikuwepo
Mahojiano na NBC Trump alibanwa kuhusu kauli alijitetea alimuuliza kama mtu binafsi 'anachunguzwa'
Rais Trump anasahau ni mkubwa wa kampeni na hakuna namna wanaomzunguka wakahusika bila kubeba dhamana.
Kwa maneno mengine Rais Trump anaanza kuwakana washirika wa kampeni kama kama kampeni, 'anajitoa'
Tatu, Trump amesema alipanga kumfukuza Comey siku nyingi kabla ya taarifa ya Roseinstein na Sessions.
Hili ni tofauti na kauli zilizotolewa na VP Pence, Msemaji wa WH Sarah Sanders, Mshauri Kellyanne Conway na mwenzetu 'JF El Jef' ambaye anayepewa benefit of doubt kama mhanga wa propaganda
Kauli ya Trump imewatosa waliojitokeza kushadidia Roseinstein alishauri au alimfukuza Comey kwama wasemavyo
Ukweli upo wazi kutoka kwa Trump kuwa emails za Clinton hazikuwa sababu.
Roseinstein hakuwa na sababu za kushauri Comey aondolewe wakati inspector general anamchunguza Comey
Katika mahojiano na NBC Rais Trump amesema FBI ilikuwa katika 'turmoil' kutokana na uongozi wa Comey
Wakati huo huo McCabe anasema kazi ya Comey ilikuwa nzuri na hakuna kasheshe ndani ya FBI!!!
Trump alisema hakuna 'collusion' yake au kampeni yake na Russia. Hii kauli nayo ina matatizo na itamsumbua
Watuhumiwa wakubwa ni washirika wake wengine wakishiriki kampeni, ana uhakika gani kama hawakushiriki?
Zipo habari kuwa ofisi ya Comey imewekewa utepe kama ule wa 'crime scene'.
Haielweki ni kwanini, na nini kimetokea wakati Comey aliporudi kutoka California alikopata habari za kufukuzwa kwake
Ulitazama suala zima, kuna tatizo linaloendelea ambalo haijulikani mwisho ni upi
Tusemezane