Ha ha ha Mkuu, je umesikia tetesi za kujipa pardon? Yeye na familia yake na washikaji wake! Follow the money inatisha.
Mkuu, mengi yanaendelea baadhi hawataki kuyasikia! ndiyo habari ya DC
Kwanza, kitendo cha kumsema AG Sessions vibaya mbele ya NYT si bahati mbaya.
Tulisema , Sessions alikuwa mtu wa kwanza kutoka senate aliyemuunga mkono
Amekuwa sehemu ya Trump kampeni kumfukuza si jambo dogo
Ile habari ya Comey kutimuliwa na Trump kusema alipanga ilikuwa mbaya.
Ime backfire vibaya sana across party line. This time alitaka ''frustrate'' Sessions ajiuzulu
Sessions amejua hilo na kwa kuzingatia amepoteza useneta hakukubali. Imenata
Pili, mmoja wa wanasheria katika jopo la Trump linaloangalia hali ya mambo amejiuzulu
Hakuna maelezo ni kwanini na pengine hatutajua kwasababu ni suala la lawyer na Mteja
Tatu, Trump ameita jopo la wanasheria kuangalia namna gani anaweza kufanya 'self pardon na familia yake' katika suala mbele ya Mueller.
Wanasheria wanaangali kutafuta vifungu vya conflict of interest ili Mueller aondoke
Kumfukuza kutazua kizazaa Capitol Hill kama ilivyokuwa kwa Comey
Nne, Rais Trump jana alisema kuchunguza financial dealings atakuwa ame cross redline
Taarifa zilizopo Mueller tayari anachunguza financial dealing kuanzia miaka 10 ya nyuma
Hapa anaangalia mambo mengi likiwemo tulilosema la tax return
Rais Trump anaingiwa na kiwewe, nyumba nyeupe (WH) ikiwa haijui nini cha kufanya nini cha kusema na kwanini mzee ana kimuhe muhe ikizingatiwa ni 'fake news'
Wachambuzi wanasema hii ilikuwa fursa nzuri ya Trump kuruhusu uchunguzi ufanyike kama hakuna lolote basi iwe proved kuwa kulikuwa na fake news
Kinyume chake tanataka 'pardon' yeye na familia. Ni kwanini 'ajisamehe' bila tatizo?
Hata hivyo huenda kuna sababu. Sakata la Bill Clinton halikuanza na Monica, lilianza na kitu tofauti na katika kufuatilia Monica akaingia yaliyotokea ni hadithi nyingine
Kukiwa na washirika wanaochunguzwa wengine wakiwa na uhusiano na Russian Oligarch linaweza kuonekana lisilotakiwa, pengine kisiasa tu, kiuchumi , kiusalama n.k.
Au ni woga tu hakuna lolote. Hofu aliyo inachagiza kudadisi kulikoni mzee ana haha hivi?