Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Ha ha ha Mkuu, je umesikia tetesi za kujipa pardon? Yeye na familia yake na washikaji wake! Follow the money inatisha.
Mkuu, mengi yanaendelea baadhi hawataki kuyasikia! ndiyo habari ya DC

Kwanza, kitendo cha kumsema AG Sessions vibaya mbele ya NYT si bahati mbaya.
Tulisema , Sessions alikuwa mtu wa kwanza kutoka senate aliyemuunga mkono

Amekuwa sehemu ya Trump kampeni kumfukuza si jambo dogo
Ile habari ya Comey kutimuliwa na Trump kusema alipanga ilikuwa mbaya.

Ime backfire vibaya sana across party line. This time alitaka ''frustrate'' Sessions ajiuzulu

Sessions amejua hilo na kwa kuzingatia amepoteza useneta hakukubali. Imenata

Pili, mmoja wa wanasheria katika jopo la Trump linaloangalia hali ya mambo amejiuzulu
Hakuna maelezo ni kwanini na pengine hatutajua kwasababu ni suala la lawyer na Mteja

Tatu, Trump ameita jopo la wanasheria kuangalia namna gani anaweza kufanya 'self pardon na familia yake' katika suala mbele ya Mueller.

Wanasheria wanaangali kutafuta vifungu vya conflict of interest ili Mueller aondoke
Kumfukuza kutazua kizazaa Capitol Hill kama ilivyokuwa kwa Comey

Nne, Rais Trump jana alisema kuchunguza financial dealings atakuwa ame cross redline
Taarifa zilizopo Mueller tayari anachunguza financial dealing kuanzia miaka 10 ya nyuma

Hapa anaangalia mambo mengi likiwemo tulilosema la tax return

Rais Trump anaingiwa na kiwewe, nyumba nyeupe (WH) ikiwa haijui nini cha kufanya nini cha kusema na kwanini mzee ana kimuhe muhe ikizingatiwa ni 'fake news'

Wachambuzi wanasema hii ilikuwa fursa nzuri ya Trump kuruhusu uchunguzi ufanyike kama hakuna lolote basi iwe proved kuwa kulikuwa na fake news

Kinyume chake tanataka 'pardon' yeye na familia. Ni kwanini 'ajisamehe' bila tatizo?

Hata hivyo huenda kuna sababu. Sakata la Bill Clinton halikuanza na Monica, lilianza na kitu tofauti na katika kufuatilia Monica akaingia yaliyotokea ni hadithi nyingine

Kukiwa na washirika wanaochunguzwa wengine wakiwa na uhusiano na Russian Oligarch linaweza kuonekana lisilotakiwa, pengine kisiasa tu, kiuchumi , kiusalama n.k.

Au ni woga tu hakuna lolote. Hofu aliyo inachagiza kudadisi kulikoni mzee ana haha hivi?
 
Mkuu kuna mengi yanaendelea ambayo baadhi hawataki kuyasikia lakini ndiyo yanazungumzwa DC...
Ndugu yetu El Jefe, akikubaliana na Donald Trump, amedai kwamba kinachoendelea ni political witch hunt na kuapa kwamba haya yote yanayoendelea ni usanii tu na kupoteza muda...yetu macho!
 
Kwa kuanzia tu nakupa alternative facts za Donald Trump katika miezi mitatu tu toka aapishwe January 20, 2017. Ingawa umetaka tatu tu mimi nakupa 56. Uongo wake kwa kipindi chote ambao ni maradufu utahitaji labda kitabu kizima...

Hujajibu swali uliloulizwa bali umejitungia swali na kisha ukalijibu, yaani umeenda OP. Lingekuwa swali la Marks 5 ulitakiwa upate 0.

Unaendekeza ushabiki hadi unashindwa kuona swali!! Jaribu kuangalia vitu 3 nilivyohitaji na 'vitu 56' ulivyoorodhesha!

Cha ajabu mwenzako naye kaenda OP, yaani ni kama vile kwenye mtihani mwenzako amekula chabo ya jibu lako bila kujua kuwa umeenda OP, halafu anasubiri kwa hamu mwalimu ampe Marks zote.
 
Ndugu yetu El Jefe, akikubaliana na Donald Trump, amedai kwamba kinachoendelea ni political witch hunt na kuapa kwamba haya yote yanayoendelea ni usanii tu na kupoteza muda...yetu macho!
Hadi sasa Don Jr na Manafort hawajathibitisha kufika mbele ya senate judiciary committee

Hata hivyo kama hawatahibitisha uwepo wao kesho, kamati ita subpoena kwa maana ya kuwaita kwa nguvu za kisheria ambapo kukataa ni kosa

Wote wawili walihiari kufika mbele ya kamati siku za nyuma, haijulikani kwanini wanasita
 
Ndugu yetu El Jefe, akikubaliana na Donald Trump, amedai kwamba kinachoendelea ni political witch hunt na kuapa kwamba haya yote yanayoendelea ni usanii tu na kupoteza muda...yetu macho!

Ningependa special counsel aachwe afanye kazi yake kwa sababu kila mtu anataka kujua ukweli. Ila kuchunguza financial dealings za 10 years ago (kabla hata Obama hajawa Rais) doesn't help him kujua kuhusu 'Russian collusion'!

Anatakiwa awe na scope ya duty ambayo ni reasonable. Nadhani kwenye tax returns za Trump kuna vitu Trump hataki watu wajue, lakini sidhani kama ni 'russian collusion'. Ila tax return zake inabidi zichunguzwe katika hiyo reasonable scope na sio nje ya hapo.
 
Kuna habari nadhani itawaudhi zaidi MSM. Russia na US zinapanga namna ya kushirikiana kwenye masuala ya cybre security.

Mkuu Tujitegemee,

Trump kupanga kushirikiana na Putin kuhusu cyber security sio jambo zuri mda huu ambapo uchunguzi wa 'Russian collusion' unaendelea. Angesubiri uchunguzi uishe. Pia cyber security ni issue sensitive sana, mambo kama haya anatakiwa kushirikisha Congress.
 
Kuna habari nadhani itawaudhi zaidi MSM. Russia na US zinapanga namna ya kushirikiana kwenye masuala ya cybre security.Russia in talks with US to create cybersecurity working group – Putin envoy
Hii habari ni ya muda sasa.

Baada ya kuzungumza kwa saa 1 wakati wa dinner kule Hamburg , Trump alimwagiza Tillerson na ku tweet kuwa wamekubaliana na Russia kuwa na cyber security unit.

Jambo hilo limeudhi sana Republicans na Dems kwa pamoja, lakini zaidi ni GOP jinsi walivyofedheheshwa
Walisema haiwezekani 'mtu avunje nyumba yako' halafu mkae pamoja kuunda unit ya kushughulikia wezi

Lakini pia Russia ni adversary wa US, cyber security ni uslama. Haiwezekani congress ikakubali upuuzi huo
In fact hili ni moja ya mambo wanahabari wana speculate yalizungumzwa na Trump bila ushauri wa

Trump ni naive sana katika uelewa wa masuala ya dunia.

Rais Trump alilazimika ku tweet na kufuta kauli hiyo siku moja baada ya kurejea kutoka G-20 (almost 3 weeks now). Hii si habari mpya, angalia source zako na ujiridhishe kwanza
 
...
Rais Trump alilazimika ku tweet na kufuta kauli hiyo siku moja baada ya kurejea kutoka G-20 (almost 3 weeks now). Hii si habari mpya, angalia source zako na ujiridhishe kwanza

Mkuu, hii habari imerudiwa jana na Russian envoy! Ni kweli ilitoka mwanzoni baadaye Trump akageuka. Lakini Russia wameendelea kudhibitisha kuwa mpango huo upo na utafanywa. Kama una muda fungua hiyo link niliyoweka ujisomee.
 
Mkuu, hii habari imerudiwa jana na Russian envoy! Ni kweli ilitoka mwanzoni baadaye Trump akageuka. Lakini Russia wameendelea kudhibitisha kuwa mpango huo upo na utafanywa. Kama una muda fungua hiyo link niliyoweka ujisomee.
Russia watasema kila kitu, ukweli ni kuwa hiyo ni DOA (dead on arrival).
Jambo la usalama kama hilo linajadiliwa na kamati za Senate, tayari wameshalikataa akiwemo Rubio

Suala hili lime expose Trump's novice and naivety katika local and international affairs
Investigation inaendelea halafu anatumbuiza kitu kama hicho, hakuna aliyemwelewa

Kibaya zaidi akamtosa sec Tillerson baada ya kukubaliana na Tillerson kuanza kupiga debe
In the end Trump aka withdraw akimwacha Tiller njia panda
 
Breaking News: WH Press Secretary, Sean Spicer, resigns...

Sean Spicer, the White House press secretary, resigned on Friday morning, telling President Trump he vehemently disagreed with the appointment of the New York financier Anthony Scaramucci as communications director.

Mr. Trump offered Mr. Scaramucci the job at 10 a.m. The president requested that Mr. Spicer stay on, but Mr. Spicer told Mr. Trump that he believed the appointment was a major mistake, according to a person with direct knowledge of the exchange.

Na bado...
 
ZILIZOJIRI KATIKA VIUNGA VYA DC

Bandiko [HASHTAG]#392[/HASHTAG] limeeleza siku ilivyoanza kwa Sec Sean Spicer kuachia ngazi

Ni baada ya WH kuajiri communication Dir. Scaramucci, Sarah H anachukua nafasi ya Spicer hakufukuzwa bali hakukubaliana na uteuzi wa Scaramucci na kujiuzulu

Don Jr na Paul Manafort
Jioni hii lawyer wa Don Jr na Manafort wamefikia 'deal' na kamati ya sheria hawata testify mbele ya kamati kwa muda.Ni baada ya 'deadline' ambapo subpoena ilikuwa njiani.

Wamekubaliana Don Jr na Manafort wafike na nyaraka zote na maelezo ya kina
Tarehe ya kukutana haijapangwa, haiondoi ukweli wanaweza itwa testify hadharani

Siku chache wawili hao walikuwa katika TV za mrengo wa kulia wakieleza utayari kufika mbele ya kamati na kwamba hakuna kilichotokea ktk mkutano na Russia

Don Jr mara nyingi amekanusha ilikuwa mkutano wa adoption ingawa Rais Trump anasema ni opposition research. Vipi wanaogopa ku testify hadharani?

Endapo hakuna cha kuficha kwanini wanagoma kuueleza umma kwanchojua ambacho wanaamini hakina tatizo isipokuwa 'fake news'

Kwa muda WH imefanikiwa kuficha tatizo, ndani ya US na hasa DC hakuna siri
Mwenyekiti wa kamati ni Republicans ambao wengi uvumilivu unaanza kuwatoka

AG SESSIONS YAMKUTA MENGINE
Baada ya kusemwa vibaya na Rais Trump juzi ndani ya NYT, leo yamemkuta mengine

Kuna 'intercepts' zikieleza balozi Kisilyak wa Russia akieleza mazungumzo yake na Session yaliyohusu kampeni kama ilivyoripotiwa na Washington Post (WAPO)

Nini kilizungumzwa hakijajulikana, lakini ukweli kuwa Sessions alishakiri taarifa za uongo mara mbili inachagiza sana uchunguzi zaidi kuhusu kinachosemwa

Kwa upande mwingine Rais Trump anafanya mambo ''yasiyoeleweka'' lakini kuna mantiki

Alimshambulia Sessions katika gazeti la NYT wengi waliona kumkosea heshima AG
Sessions akiwa Seneta wa kwanza kumuunga mkono na mshirika mkuu ilikuwa ni dhalili

Tumeeleza hapo nyuma, Trump alikuwa na nia mbili. Kwanza, kum frustrate Sessions ili aachie ngazi mwenyewe badala ya kumtimu kama Comey hivyo kupunguza joto la kisiasa

Pili, ilikuwa njia ya kumtoa Sessions aliye ji recuse kutoka Russia investigation ili achague AG ambaye hana connections na Russia ambaye atakuwa Boss wa Counselor Mueller

AG mtarajiwa ataweza kumdhibiti Mueller ikibidi kama si kutoa nyeti kwa Trump

Kwa haya yaliyomkuta Sessions jioni ya leo, Trump amepata ahueni kwani kuondoka kwa Sessions kutachagizwa na sababu nyingine ingawa Trump alitaka hilo litokee

Kesho itakuja na kitu gani?

Tusemezane
 
Mkuu, hii habari imerudiwa jana na Russian envoy! Ni kweli ilitoka mwanzoni baadaye Trump akageuka. Lakini Russia wameendelea kudhibitisha kuwa mpango huo upo na utafanywa. Kama una muda fungua hiyo link niliyoweka ujisomee.
Russia wanajua jinsi jambo kama hili lisivyowezekana na kwa sasa wameanza kuvujisha habari ambazo kwa akili zao wanaamini zinaweza kuwavuruga Wamarekani. Trump ni mateka wao na wanajua namna ya kumchezesha ngoma yao lakini wanasahau jinsi Wamarekani wanavyokuwa wamoja katika mambo yanayogusa usalama wa nchi yao.

Kwenye mambo ya msingi yanayogusa maslahi ya taifa hawana ushabiki wa kijinga kama tunaoushuhudia hapa kwetu. Hiyo ya cyber security working group eti ya pamoja sahau...ni ndoto ya Warusi isiyowezekana hata kidogo. Bila shaka uliwaona Wamarekani walivyoungana kulaani huo mapango bila kujali itikadi zao wakiufananisha na uhaini.
 
"Mag3, post: 22412884, member: 10873"]Trump ni mateka wao na wanajua namna ya kumchezesha ngoma yao lakini wanasahau jinsi Wamarekani wanavyokuwa wamoja katika mambo yanayogusa usalama wa nchi yao.
Wamarekani wameliona.

Trump yupo tayari kumsema vibaya Obama mbele ya mataifa, hakuna mahali amemsema Putin tofauti licha ya kuwa ni adversary wao.

Trump kasema mataifa yote makubwa ikiwemo UK, Ufaransa, Japan na China.
Hana rekodi ya kusema lolote kwa Russia na Putin

Kubwa zaidi ni kuhusu vyombo vya usalama na suala zima la vikwazo kama tutakavyofafanua hapa chini
Kwenye mambo ya msingi yanayogusa maslahi ya taifa hawana ushabiki wa kijinga kama tunaoushuhudia hapa kwetu. Hiyo ya cyber security working group eti ya pamoja sahau...ni ndoto ya Warusi isiyowezekana hata kidogo. Bila shaka uliwaona Wamarekani walivyoungana kulaani huo mapango bila kujali itikadi zao wakiufananisha na uhaini.
Wamarekani watasemana vibaya na kila aina ya maneno na kashfa, lakini mtu wa nje ukigusa US hakuna cha uvyama wala itikadi, wanasimama kidete dhidi yake

Hili la cyber security limekataliwa Trump akiwa Hamburg.
Hakuna cha Dems au Reps, wote kwa pamoja wamesimama na kusema liishie huko huko. Ikabidi abadili mwenendo na kumtosa Sec Tillerson

Ndivyo Congress livyofikia makubaliano ya kukaza uzi wa Vikwazo kwa pamoja.
Azimio lilipitishwa kwa maseneta 98 dhidi ya wawili waliokataa ''overwhelming none partisan''

Katika mswada huo house na seneti wamekubaliana uwekewe 'veto'
Kwamba hakuna anayeweza kuubadilisha hata kwa Exec order hadi urudi ulipoanzia

Hili wamelifanya baada ya kubaini Rais Trump anataka mswada huo ulegeze baadhi ya mambo kumfurahisha Putin na Russia ikiwemo kurudisha jengo walilotumia kwa ujasusi.

Mswada ili uwe sheria lazima usainiwe na Rais Trump. Rais anaweza ku veto mswada huo pia

Tatizo litakalotokea ni kuwa miswada ya serikali hupitia house na seneti.

Kama ata veto atakuwa ametangaza 'vita' na vyombo hivyo.
Akikubali kusaini atakuwa 'amewasaliti' jamaa zake wa Russia.

Kukiwa na sintofahamu juu ya mahusiano yake na Russia option alizo nazo ni ndogo sana.
 
ADMISSION: KAMPENI ILIKUTANA NA WATU WA RUSSIA

Kwa muda mrefu kumekuwepo na kauli za Rais Trump, washirika na surrogates kuwa kampeni haikuwa na mtu aliyewasiliana(communicate) au kushirikiana (collusion) na Russia

Kuna vitu ambavyo wengi huvichanganya katika suala zima la Russia investigation

Kwanza, kwamba Russia ilifanya interference au meddling ya uchaguzi wa 2016

Intel community 17 zimekubaliana kuwepo meddling.
Hii haina maana kuiba kura au kuvuruga uchaguzi.
Meddling inayosemwa ni ya kusambaza au kuchanganya wapiga kura

Hakuna ushahidi ni kiwango gani meddling imebadili matokeo ya uchaguzi wa 2016
Kwa uchaguzi wa Marekani, local gov zimethibitisha hakuna kura iliyoibiwa au kuvurugwa

Hivyo, kwamba Trump alishinda uchaguzi kihalali,wote wanakubaliana hadi itokeo vinginevyo

Pili, kwa vile Intel community na Congress kwa pamoja wanakubali uwepo wa meddling, hakuna shaka tukio hilo limetokea isipokuwa kwa Trump na washirika wa kampeni kuamini

Tatu, kwavile kuna ushahidi wa meddling, swali lililobaki, je, Russia ilifanya hayo ikiwa yenyewe au ikishirikisha watu kutoka ndani ya Marekani kwa maana ya collusion?

Hilo ndilo linafanyiwa kazi na kamati za house, seneta na Conselor Mueller

Rais Trump na kampeni yake wameyaweka yote kwa pamoja ili kuchanganya umma.
Hakuna anayesema Trump kampeni imefanya collusion hadi uchunguzi utakapokamilika

Kinachojulikana mwezi huu baada ya Don Jr kukiri kushiriki mkutano na Russia wa kupata dirt za Clinton, na leo Jared Kushner, mkwewe Trump kukiri alikutana (contact) na Russia mara nne, hakuna shaka tena kuwa kampeni ya Trump ilikuwa na contact na Russia

Kuwa na contact hakuhitimishi uwepo wa collusion hadi uchunguzi utakapokamilika

Kilichoitwa fake news sasa ni real news hakuna ubishi kampeni ilikuwa na contact na Russia.

Hoja ya kwamba kampeni ya Trump ilikuwa na contact na Russia ni fake news sasa imekufa
Kilichobaki kujadiliwa ni je contact zilikuwa na collusion au la. Uchunguzi utaeleza

Wamarekani wanachotaka kujua ni kwa namna gani Russia waliweza kufanya meddling na wanawezaje kuzuia isijitokeze tena. Katika hilo uchunguzi ndio unaendelea

Ukweli ulio wazi ni kuwa media zilikuwa sahihi, hakuna fake news kama ilivyoaminishwa na Trump.
Alifanya hivyo kuzima nguvu ya media kinyume chake alichochea.

Tusemezane
 
WIKI HII KATIKA SIASA ZA US

'VURUGU TUPU WH
OBAMACARE, SKINNY LEGISL, TRANSGENDER

Wiki ina matukio yasiyozoeleka katika siasa za US ikiwa ni Taifa kiongozi, kubwa na lenye nguvu

Rais Trump ameendeleza mashambuzi dhidi ya AG Session akimdhalilisha kulia kushoto
Kama tulivyowahi kujadili, lengo ni kum frustrate Sessions ajiuzulu

Kumfukuza kutazaa kizaizai kama cha Comey akihusishwa na suala la Russia investigations
Anachotaka kufanya Trump ni kumdhalilisha Session ajiuzulu ili ateue AG mwingine

Hili litamwezesha AG kuingilia katia uchunguzi wa Russia kwa kujua Counsel Mueller anaweza kutimuliwa kwa maagizo ya Trump. Ndivyo acting FBI Dir anashambuliwa na Rais

Hilo anaweza kulifanya wakati wa mapunziko ya mwezi wa nane maseneta na Wabunge wakiwa majimboni mwao na kupunguza joto la mashambulizi

Maseneta akiwemo wa kamati ya sheria ya Seneti wameonya jaribio lolote la kumuondoa Sessions ambaye amekomaa na nafasi hiyo

SCARAMUCCI Vs R.PREIBUS
Mkurugenzi wa mawasiliano mpya Ikulu bwana Anathony Scaramuci ameingia kwa gia kubwa akimtuhumu katibu kiongozi WH Bw Reince Preibus kuvujisha siri zake 'leak'

Kuja kwa Scaramucci ndiko kulipelekea kuondoka kwa Sean Spicer.
Inasemwa Prebius hakupenda ujio wa Scaramuuci ambaye ni 'swahib' wa Trump
Jana Rais, Scaramuuci na Hannity walikuwa na dinner. Hannity ni mtangazaji wa Fox News

Timbwili la wawili hao lime endeleza vurugu WH kiasi cha Republicans kumkemea Rais wa kwa kuwa un-presidential kwa tweets zinazovuruga agenda na kushindwa kudhibiti WH k 'std'

Moja ya Tweets zilizoshtua ni ile ya kufuta transgender katika jeshi bila kuwasiliana na waziri wa ulinzi au wakuu wa vyombo vya ulinzi. Ilikuwa suprise kwa kila mtu jambo lisilo la kawaida

Transgender wamekuwepo na kuna utafiti unaendele kuhusu ushiriki wao. Hadi majtokeo ya uchaguzi kutangaza major policy change kama hiyo kwa tweet imeduwaza wengi

Hayo yakiendelea mshauri wa ulinzi H.R McMaster naye anaonekana kuwa frustrated na WH
Tillerson, State sec akisemwa kachoshwa na maamuzi yanayobadilika bila mpangilio

Kubwa linalosubiriwa kwa sasa ni Obamacare, inaendelea...
 
''OBAMACARE VS SKINNY HEALTHCARE''

Kwa wanaofuatilia jitihada za Republicans kufuta Obamacare zimekwama mara nyingi
Kwanza ndani ya House na kufanyiwa marekebisho kabla ya kupelekwa Senate

Senate ikakataa Repeal and Replace ACA 'Obamacare'
Rais Trump akawaita Republicans na kuwaambi ni agenda ya miaka 7 wasimalize kipindi cha kwanza na kwenda likizo 'recess' kwavile hawatakuwa na cha kuwaambia wafuasi

Haja ya Trump si kupata Healthcare bali kufuta legacy ya Obama kwa kila kitu hata kama kufanya hivyo kuna madhara kwa nchi na wananchi.

Ndivyo alivyofanya kwa mengi kama kuondoa US katika mkataba wa Paris, hili la transgender ambalo aliahidi kulinda haki zao n.k.

Kushindwa kwa repeal and replace kukazaa kitu kingine Repeal.
Yaani wafute tu Obamacare tu.Trump alikuwa tayari kwasababu ni legacy ya Obama

Repeal nayo ikashindwa kwasababu Republicans hawakubaliani.
O'care kwa kura za maoni ni maarufu kuliko miswada yote iliyoandaliwa na Republicans

Hata wakiwa wenyewe wameshindwa ku repeal and replace au repeal alone
Hilo likazaa mswada wa kura unaolazimisha Republicans kukubaliana na repeal

Yaani Reps walilazimika kupiga kura ya kukubaliana Obamacare iwe repealed

Kura zilikuwa 50 kwa 50 lakini VP anakura na hivyo ikakubaliwa
Kura iliitwa motion to proceed, yaani hoja ya kuendelea na mchakato wa kufuta O'care

Seneti imeshindwa kuafikiana kwa miswada iliyoofikishwa na freedom caucus, moderates
Ikalazimika mwenye mswada alete ili uingizwe katika mchakato.

Ted Cruz akawa na wake na Seneta L.Graham akawa na wake na baadhi ya GOP

Hakukuwa na maafikiano, wakaamua kutengeza mswada unaoitwa Skinny O'care
kwa maana ya kuondoa baadhi ya vifungu kutoka Obamacare

Tukio hilo linaendelea sasa kukiwa na mtego. Kama mswada wa skinny, yaani kunyofoa vifungu vya Obamacare utafanikiwa, itabidi urudi katika house kwa reconciliations

Baadhi ya maseneta wanahofia ukirudi house na kwavile umepita seneti, Spika anaweza kuupeleka kwa Trump ukasianiwa na kuwa ndiyo repeal and replace Obamacare

Jioni hii maseneta 5 wakiongozwa na John Mcain na Lindsey Graham wametoa kauli ya kumtaka Spika wa house Ryan awahakikishie skinny haitapelekwa kwa Trump

Ingawa Spika amewaaambia mswada hautapelekwa kwa Trump kusaniwa kama sheria kuna wasi wasi miongoni mwa maseneta wanaoita Skinny kama kitu terrible, fraud and disaster kuliko Obamacare. Ni mswada wa kurasa 8 usieoleza kwa kina

Kwanini wanataka kupitisha mswada wa Skinny na hawataki uwe sheria?

Inaendelea
 
''OBAMACARE VS SKINNY HEALTHCARE''

Skinny ya Republicans haijajadiliwa kwa kutumia vigezo vya CBO hivyo haina score
Skinny imeletwa na seneti kwa maana tatu

1. Kuhakikisha hoja ya ku repeal and replace Obamacare inabaki hai kwa mjadala
2. Kuwafaraji wafuasi wa Republicans ahadi ya repeal and replace inafanyiwa kazi
3. Kuleta mazingira ya kujadiliana na Dems, kwani skinny ikienda house huenda kukawa na kuafikiana nini kifanyike kwa pamoja kama asemavyo McCain

Tatizo lililopo, ilishindwa kuafikiana ikiongozwa na majority GOP, na miswada imefia senate ikiongozwa na majority GOP, nini kitafanyika tofauti kwa skinny?

Kisiasa skinny ina gharama kubwa. Kwanza, haiondoi Obamacare, yaani ni kubandua tu lakini si kuangusha 'gogo'. Wafuasi wa Republicans watakuwa disappointed.

Pili, Republicans wakishaichukua skinny tayari watakuwa wamebeba mzigo wa Healthcare na madhara yote yatakuwa juu yao wakati huu ambapo Obamacare ni maarufu

Kwa mtazamo huo, skinny inayopigiwa kura sasa hivi haiwafurahishi Republicans, wanalazimika tu, wengine wakipinga wazi wazi bila uchama

Magavana bila kujali itikadi wanakubali Obamacare hasa Medicaid na medicare kwani kuondolewa ni wao kubeba mzigo wa healthcare. Wanaweka pressure kwa GOP

Kitu kimoja kinachojitokeza, wagombea wote wa Urais Dems na Reps walikuwa na sera katika wensite zao. Hizo walimaanisha zinaweza kufanyiwa kazi zaidi lakini ndio dira yao

Trump hakuwa na sera, aliaminisha watu kwa maneno ya 'believe me' something good

Hivi sasa maseneta kama Ted Cruz na Graham wana version zao wakiwemeo wengine
Hakuna version ya Trump kama ya Obama iliyofanyiwa kazi na kuzaa ACA

Trump anasubiri kuletewa chochote ilimradi tu ku repeal and replace Obamacare

Hapa ndipo tofuati ya leadership inapoonekana, kwamba, hana wataalam waliopendekeza hata kitu kidogo, anategemea entirely mawazo ya wenzake kisha kuchukua credit

Hadi sasa hata Skinny ikipita katika seneti haiwezi kuwa sheria kwani lazima imfikie Trump na tayari ameshagomewa na hata ikimfikia itakuwa kiraka, nguzo ni Obamacare

Kwa wanaofuatilia kuanzia mwanzo tulisema Obamacare haifutiki kirahisi, ni miaka 7 ya mjadala wa Reps na miezi 6 ya uongozi ugavana, house, seneti na WH hawajaweza

Tunaendelea kufuatilia kura na tutwajuza nini kinaendelea katika ''igizo'' la skinny
Ni igizo kwasababu ni sawa na joka la kisukuma lisilo na meno ingawa ni joka

Tusemezane
 
Breaking News: Obamacare has prevailed...the vote was 51-49!

The Senate has rejected a measure to repeal parts of former President Barack Obama’s health law, dealing a serious blow to President Donald Trump and the GOP agenda.

Unable to pass even a so-called “skinny repeal,” it was unclear if Senate Republicans could advance any health bill.

GOP has failed to deliver! Trump's promise to repeal Affordable Care Act has fallen flat on its face!

Cc: [B]El Jefe[/B]
 
Back
Top Bottom