Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Mkuu kuna wakati nakushangaa kidogo.
Hili jambo nimelizungumzia mabandiko mawili au matatu yaliyopita hasa la Stormy

Stormy na Karen wanasema wamefanya mapenzi na Trump wakieleza hadi vyumba walivyoingia
Michael Cohen, wakili wa Trump amekiri kutoa 130,000$ kuziba midomo

Michael Avinnati, wakili wa Stormy, anasema Trump au wakili wake wasimame kukanusha.
Hakuna anyekanusha. Wanachotaka ni arbitrations nje ya court, kwamba suala limalizwe kiutu uzima

Malipo yaliyofanywa na Cohen kukiri siku 13 kabla ya uchaguzi yakazua swali kama ilikuwa ni sahihi kwa kuzingatia sheria za uchaguzi na kwamba gharama hizo ni sehemu ya pesa za kampeni au la

Fukua fukua ikamkuta Mueller ambaye aliona kuna `crime`na kupeleka kwa FBI, nao wakata kupata kibali cha kumpekua Cohen.

Walimtumia prosecutor aliyeteuliwa na Trump kutaka ruhusa ya mahakama ya Jaji aliyeteuliwa na Trump. Kumbuka FBI ipo chini ya Wray aliyeteuliwa na Trump, AG aliyeteuliwa na Trump na Deputy AG Pia. Hapa kuna nani ana `twist`

Tatizo linalojitokeza, ukisharuhusu kupekuliwa chochote na lolote linaweza kutokea

Nikupe mfano rahisi unaoweza kuulewa, Polisi wanaweza kuja kkukupekua nyumbani kwako kwa hisia kuwa una nyaraka zilizotumika kuiba pesa ofisini.

Katika upekuzi wakakutana na kichwa cha mtoto au mguu wa mtu
Usitegemee Polisi wataacha hilo kwasababu eti wanatafuta nyaraka. Umeelewa!

Jaribu kuwa na information za kutosha kuhusu mada, usiwe na `bias blind`

There's no deep state or group of people who have conspired to overthrow Trump's presidency. The problem with Trump is he came to power with a lot of baggage and he wants his opponents to cut him some slack. It doesn't work that way. Besides, he gets a taste of his own medicine. What did think when he used to trash his opponents during the primaries and general election? This isn't the guy who linked Ted Cruz's father to the assassination of JFK?
 
There's no deep state or group of people who have conspired to overthrow Trump's presidency. The problem with Trump is he came to power with a lot of baggage and he wants his opponents to cut him some slack. It doesn't work that way. Besides, he gets a taste of his own medicine. What did think when he used to trash his opponents during the primaries and general election? This isn't the guy who linked Ted Cruz's father to the assassination of JFK?
Donald Trump is busy digging a grave...what he doesn't know is that it is his own!
 
Donald Trump is busy digging a grave...what he doesn't know is that it is his own!

This guy thrived on bad publicity. Before he became the president, he was one of those people who believe that there's no such thing as bad publicity. It worked well for him. For example, he used to stir up controversies so his name could stay relevant and in people minds. So personally I believe that now it's time he gets the taste of his own medicine.
 
This guy thrived on bad publicity. Before he became the president, he was one of those people who believe that there's no such thing as bad publicity. It worked well for him. For example, he used to stir up controversies so his name could stay relevant and in people minds. So personally I believe that now it's time he gets the taste of his own medicine.
Pres. Trump was a staunch proponent of birther for 8 years unabated
It was a political stunt to keep his name in the media 'afloat'
Now,chicken are coming home to roost, he is whining on fake news and the so called deep state

The deep state conspiracy is merely a hogwash to lure the public on assumption of masking the Russian probe,infidelity and other ''financial dealings'' of public interest

We may recall senate Majority leader,McConnell, once said, he will make sure Obama'' is a one term pres''
Mitch and congress blocked every move including infrastructure program and supreme court nominations

Revamping the dilapidated infrastructure was Obama's agenda. Mitch and GOP blocked it on the pretense of rising national debt. Ironically, Pres Trump and Mitch are the cheerleaders of the same!

Whilst congress handcuffed Obama,tycoon cum media Mogul,DT, was on the streets affronting him incessantly
Pres Trump leveled unfounded allegations, criticism and derogatory remarks for publicity

It's suffice to say, If the ''deep state'' is a viable concept, then, Trump, McConnell and GOP are the founders
Apparently Paul Ryan, another 'deep state' so to speak has read the writings on the wall
 
Deep State is just a figment of imagination perpetuated by conspiracy theorists majority of whom have no confidence to the established machinery of justice , law and order
Bahati mbaya maneno haya 'Deep State' yametumiwa na chombo cha habari cha Russia kwenye habari yao hii.
----
Former Democratic Congressman Dennis Kucinich told RT’s Politicking that there are ‘deep state’ elements influencing US foreign policy, citing examples from the Trump, Obama, and Bush administrations.
The current Ohio gubernatorial candidate claimed there are elements in the Pentagon, the State Department, and the CIA trying to influence the Trump administration to be “more hawkish, more interventionist.”
------
‘Deep state’ elements pushing for Syrian conflict – Dennis Kucinich tells Larry King on RT (VIDEO)
 
Trump tabu sana! Kumbe ndiyo maana chemistry yake na Merkel haikuwa sawa hivi majuzi!
===
The European Union was formed to rip off the US, President Donald Trump said during a rally, as he vowed to “take on” the bloc and China, saying that the days of “disastrous trade deals” are over.
Trump unleashed a tirade aimed at the European Union at a campaign-style rally in Michigan on Saturday. Taking aim at the EU's trade policies, Trump said that the bloc “was put there to take advantage of the United States.
Not anymore, we told them that yesterday, actually the exact same words, not anymore, those days are over,” Trump said to a round of cheers.

The US leader hinted that he would stop at nothing to fix the trade imbalance, warning the crowd that they should expect some temporary setbacks on the way to a bright future for the US economy.

“In short term you may have to take some problems, long term – you're going to be so happy, we're going to get it opened up, or we’re not doing business with these other countries,” Trump said.

While blasting the EU, China and Japan over trade, Trump said that his criticism of the “disastrous trade deals,” which he is busy “straightening out,” does not mean he has a personal grudge against those countries' leaders.

EU was created to rip US off, Trump says as allies brace for trade war
--------------
 
Donald Trump is busy digging a grave...what he doesn't know is that it is his own!
Vipi na hili hapa ni 'kaburi' lingine la Trump ?
-----
Trump aitaka DOJ kufanya uchunguzi dhidi ya FBI kuingilia kampeni zake za urais.
....
US President Donald Trump says he’s ordering a probe into claims Barack Obama pushed for his 2016 campaign to be surveilled by FBI for alleged links to Russia.
“I hereby demand, and will do so officially tomorrow, that the Department of Justice look into whether or not the FBI/DOJ infiltrated or surveilled the Trump Campaign for Political Purposes - and if any such demands or requests were made by people within the Obama Administration!” tweeted Donald Trump on Sumday afternoon.

This week, the New York Times and the Washington Post revealed that an operation, codenamed Crossfire Hurricane, was conducted by the FBI from the summer of 2016. As part of it, an agent, who has since been outed as experienced spy and academic Stefan Halper, was charged with wheedling out potentially compromising information from George Papadopoulis, Sam Clovis and Carter Page, and possibly other members of the Trump campaign. Popadopoulos later pled guilty to making false statements to the FBI over his Russian links.

In the past few days, Trump has claimed that this story is “bigger than Watergate” particularly considering accusations that any agency involvement may have been prompted not only by officials sympathetic to the Hillary Clinton-supporting Democrats, but also on the basis of evidence collected at their behest.

“Reports are there was indeed at least one FBI representative implanted, for political purposes, into my campaign for president. It took place very early on, and long before the phony Russia Hoax became a “hot” Fake News story. If true - all time biggest political scandal!” Trump wrote on Friday.

Trump to demand DOJ probe into FBI ‘infiltration’ of Trump campaign
 
NDANI YA SIASA ZA US
Kwa muda yamekuwepo matukio yanayoendelea katika siasa za ndani za nchi ya Marekani

1. Sakata la Stormy Daniel
Sakata lilianza kama jambo la mahaba kati ya Rais Trump na mwanadada huyo.
Mwanzoni halikuonekana kuwa ni tatizo, kadri siku zinavyozidi kwenda mbele timbwili linakufukua mengine yasiyotarajiwa

Wakili binafsi wa Rais Trump alipekuliwa na FBI baada ya kupata 'taarifa' kutoka kwa mchunguzi Mueller. Tulijadili hili

Kinachoonekana ni Bwana Cohen kuwa 'mfreji' au conduit wa miamala ambayo haijulikani inaanzia na kuishia wapi
Kwa namna moja inamhusisha Rais Trump kwavile Cohen alidai kuwa na uwezo wa kufanikisha 'lobbying' mambo

Hilo nalo limezaa mengine kwa baadhi ya washirika kutajwa katika mikutano wakiwemo Qatar na UEA
Haijulikana kwa uwazi ni kitu gani kilichokuwa kinataka kufanyika kupitia kwa Bw Cohen kama mshirika wa Rais

Rais Trump anajaribu kujitenga na Cohen lakini pia anachelea kwa kujua Cohen ni 'mwandani' wake, akiamua kutoa ushirikiano na wachunguzi, huenda jahazi likaingia maji. Hili linamtia hofu ingawa kwasasa linaonekana kupoa kidogo

2. Kamati ya Bunge yatoa taarifa
Kamati ya bunge la wawakilishi imetoa taarifa ya uchunguzi ikiwa ni ya upande wa Republican peke yake
Democrats walikataa wakisema baadhi ya mashahidi hawakuitwa makusudi na tume chini ya GOP
Tume hiyo inamshirikisha Bwana Nunes ambaye uadilifu wake unatiliwa mashaka

Nunes ndiye alikwenda WH na kusema ipo taarifa ya Rais Obama kudukua 'wiretap' maongezi kutoka Trump Tower
Ilikuja bainika taarifa hiyo iliandikwa na WH na haikuwa na usahihi wa aina yoyote

Nunes ndiye pia alitaka maafisa wa serikali ya Obama waitwe kwa kuweka wazi 'unmask' majina ya baadhi ya watu katika kile kile kilichoitwa FISA. Mshauri wa mambo ya usalama wa serikali ya Obama Bibi Rice aliitwa na hoja ikafia hapo

Nunes katika jitihada nyingine anamtaka Deputy AG apeleke taarifa ya wigo wa uchunguzi katika suala la Russia

Ametishia kumshtaki mbele ya kamati ikiwa hatafanya hivyo, ingawa Roseinstein amegoma
Kugoma ni katika kuchelea kuwa Nunes anatumika kuiba siri za uchunguzi na kuzipeleka WH

Taairfa ya kamati ya Nunes ilizimika ghafla kutokana na vyombo vya habari kutoa taarifa siku hiyo hiyo kuwa mwanadada wa Russia (Natalia V) aliyeomba mkutano Trump Tower alikuwa ni shushu wa Russia, wakimkariri mwenyewe akikiri hilo

Media zilikuwa na taarifa kilichokuwa kinasubiriwa ni 'timing' tu ya kuthiitisha ubatili wa taarifa ya Nunes

3. Kamati ya Seneti yatoa taarifa
Kamati ya seneti imetoa taarifa 'bipartisan' ikieleza wazi kuhusika kwa Russia katika uchaguzi na kumsaidia Bwana Trump

Hili halikupendeza upande wa Trump kama ilivyokuwa taarifa ya Nunes na wala halikuongelewa kwa nguvu
Trump alisifu taairifa ya Nunes kwavile inamsafisha bila kujali ilikuwa ya upande mmoja,ya seneti amekaa kimya

4. Rudy Giulian ajiunga na Team Trump
Huyu ni meya wa zamani wa NY na Mgombea Urais wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa GOP
Rudy alitegemewa kuwa mwanasheria mkuu (AG) katika serikali, akakataa nafasi hiyo na amekiri anajuta kwa uamuzi huo

Tangu aipojiunga na timu ya wanasheria, Giulian amekuwa 'tatizo' akiongelea mambo bila mpangilio na nje ya eneo lake
Katika aliyeongelea mengine yanamweka Rais Trump katika wakati mgumu yakipingana na wanasheria wake wa kawaida

Inaendelea....
 
5. Taarifa ya 'spy' katika kampeni ya Trump
Gazeti la NY Times limeandika makala kuhusu uwepo wa afisa wa FBI akichunguza kampeni ya Trump
Taarifa hiyo ilibezwa na Rais Trump mwanzoni kama fake, lakini sasa anaitumia vema katika kubadili mwelekeo

Inasemwa, afisa huyo alionana na baadhi ya maafisa wa kampeni ya Trump.
Kwa habari zaidi, inasema maafisa hao waliingia katika kazi baada ya taarifa za awali ya ile dossier ambayo chanzo ni Papadopolous, afisa wa kampeni ya Trump aliyekwenda London na kukutana na afisa wa Australia akimweleza Russia wana 'zigo' la habari za Hillary Clinton

Rais Trump na washirika wake akina Rudy wanasema afisa huyo alikuwa 'spy' akichunguza kampeni kupeleka habari kwa upande wa pili na hivyo wanaitaka DOJ ichunguze.

Deputy Roseinstein ametoa taarifa kuwa kama lipo jambo kama hilo litachunguzwa.
Ingawa Rosenstein amepata habari kupitia tweet, kuna sababu za yeye kufanya hivyo

Tuhuma zinaangukia DOJ zikuhusisha Russia ambayo yeye ndiye msimamizi.
Rais Trump ameahidi kukutana na DOJ Jumatatu ili kuwataka wafanye uchunguzi

Hapa kuna hoja.
Kwanza, Rudy na Trump wanataka jina la afisa huyo liwekwe wazi.
Huko nyuma ni Rais Trump na washirika wake walilaani majina kuwekwa wazi 'unamask' ya maafisa wanaochunguza ili kuwalinda. Vipi hoja hiyo imebadilika?

Pili, inawezekana alikuwepo afisa, lakini je, alikuwa anachunguza suala la Russia au alikuwa anafanya u'spy wa kampeni?

Tatu, DOJ pamoja kuwa ipo chini ya Rais kwa utaratibu wa Marekani ni idara huru inayojitegemea.
Kumekuwepo na kuituhumu idara ambayo kiongozi wake kiuhalisia ni 'Rais' kwani yeye ndiye mteuzi wa watendaji

Nini kinaendelea
Baada ya jitihada za Nunes na washirika kuidhalilisha tume ya Mueller kugonga mwamba kwa namna nyingi hapa panaonekana kuwa na upenyo.

Mtakumbuka text za maafisa wawili zilivyopigiwa debe na mwisho wa siku ikaonekana hakuna lolote.
Ilikuwa ni kuadhirika sana kwa timu Trump, fox news, Nunes na washirika wengine

Hesabu zinazofanyika ni kutaka kumlazimisha Deputy Rosenstein akiri kuna us-spy chunguzi wote uonekana ni hila tu.

Rais Trump ameuita 'witch hunt' mara nyingi sana, katika hali ya kushangaza FBI Dir bwana Wray wiki hii amekanusha na kusema hakuna witch hunt. Huyu ni mteuliwa wa Rais Trump

Kamati ya seneti ikiwa na pande zote imethibitisha kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa sahihi kusema Russia iliingilia uchaguzi na kwamba ilifanya hivyo kumsaidia Rais Trump

Itakapotokea Deputy AG Rosenstein 'akakaidi' maagizo ya Rais Trump kwa kutosema anachotaka, huenda ndio ukawa mwanzo wa mwisho wake na kutimuliwa.

Kutimuliwa kwake kutampa Rais Trump nafasi ya kuchagua amtekakaye ili kuzima uchunguzi wa Mueller

Ni katika jitihada hizo za kuua suala hilo, Trump na timu yake walivujisha maswali kwa media kutoka kwa Mueller
Maswali yalikuwa takribani 49 na sasa inasemekana yamepunguzwa

Hata hivyo bado kuna tatizo na wanasheria wake hawataki atokeo mbele ya Mueller kwa kuogopa 'kusema hovyo'

Wiki hii itakuja na nini? Tutawajuza

Tusemezane
 
SIASA ZA US WIKI HII

Kinachojiri katika habari ni suala la 'FBI' kuchunguza kampeni ya Rais Trump kama tulivyowahi kujadili
Rais Trump na washirika wake wameita suala hilo kama u 'spy' dhidi ya kampeni yao

Kauli ya spy inatumika makusudi kuonyesha ushushushu uliofanywa na FBI dhidi ya kampeni kwa ajili ya mpinzani

FBI wanafanya kazi kwa kutumia informant pale wanapopeleza habari. Katika sakata linaloendelea inasemwa FBI walikuwa wanafuatilia nyendo za 'Russia' na washirika wa Trump baada ya kupata habari za Papadopolous

Juzi Rais Trump alimwita FBI Dir na Deputy AG Rosenstein akiwataka wachunguze suala analochunguzwa!
Katika hali isiyo ya kawaida kwa DOJ, AG alikubali mkaguzi 'auditor' kufanya uchunguzi wa suala hilo la 'FBI Spy'

Huu ulikuwa mtego kwa Deputy AG. Ingalitokea amekataa ushauri wa Rais hatua inayofuata ni kujiuzulu.
Hilo ndilo Trump alilitaka, kuondoka kwa Roseinstein kungemfungulia milango ya kumteua atakayemsimamia Mueller

Kumetengenezwa mpango mwingine, kwamba, kamati ya Bunge 'intelligence house ''chini ya Nunes ilitaka kupata habari za ndani 'classified information' jambo ambalo Roseinstein alikataa.

Kwa shinikizo imekubalika kuwa kamati ikiwa na wajumbe wa Republican tu na Chief of Staff wataonyeshwa classified information zinazohusiana na uchunguzi

Republican na Rais Trump wamekataa Democrats wasiwepo na hivyo hawataweza kuona classified information hizo

Jambo hilo linafanyika makusudi. Kamati ya Nunes ilipotoa memo, Demo walitoa mbadala 'rebuttal' na kuua hoja

Ikumbukwe, Nunes ndiye alianzisha suala la Obama kufanya wiretap lililoishia bila kuwa na matokeo yaliyokusudiwa
Nunes ndiye aluimtuhumu Suzane Rice, mshauri wa Obama kuhusu usalama kama mtu aliye unmask majina ya watu kinyume na taratibu za FISA. Rice aliitwa na suala likaishia hapo bila matarajio husika
Nunes alishikia bango suala la text, ambalo nalo lili isha bila matarajio husika kwao

Na juzi Rais Trump akiwa WH alimsifu Nunes kama mtu 'courageous'

Nunes na washirika wake wamejifunza kosa, kwamba kuwashirikisha Democrats kunaharibu mipango

Mpango ni kuonyesha uchunguzi unaondelea si halali,una hila za kisiasa tu katika kumnasua Rais Trump na kampeni yake dhidi ya uchunguzi wa Mueller. Hoja yao ni kutaka kuua uchunguzi huo kabisa

Kitendo cha kutaka classified info bila kushirikisha Democrats ni kutaka kufanya jambo moja.
Baada ya alhamisi, kwa pamoja watatoka wakisema kuna jambo baya wameliona limefanywa na FBI dhidi ya Trump

Kwavile hakuna Democrats waliolikwa hoja yao itashikiwa bango na kuonekana 'ni ukweli'

Kuanzia hapo watamshambulia Dep AG Roseinstein wanayemwita deep state ajiuzulu na huo ndio utakuwa mwanzo wa kuua hoja ya Mueller. Hili linafanyika makusudi wakati timu ya wanasheria wa Trump ikisusua sua ili kupitisha muda wa Rais kuhojiwa na Mueller. Hivyo, baada ya Alhamisi, huenda vyombo kama Fox vikashikia bango na pengine wiki ijayo Roseinstein anaweza kuwa nje ya ofisi. Baada ya hapo Mueller anazimwa na uchunguzi unafikia hatma

Hesabu hizo zinaweza kufanikiwa lakini pia zinaweza kuja na gharama kubwa.
Mwaka jana mshauri wa WH bwana Don McGahn litishia kujiuzulu ikiwa Roseinstein atatimuliwa.
Na baadhi ya maseneta hawakubaliani na hatua hizo

Kitendo cha kamati ya seneti kuja na taarifa ya pamoja 'bipartisan' ikithibitisha ushiriki wa Russia na kuunga mkono taarifa za intel community zinaonyesha tatizo linaloweza kumkabili Rais Trump ikiwa atamtimua Roseinstein

Tegemeo kubwa lipo katika House ambako sehemu kubwa wanamuunga mkono Rais Trump hasa kuelekea midterm election. Je, kumtimua Mueller kutawezekana kwa mkakati uliopo bila gharama?

Tusemezane
 
Yanayotokea US yanafurahisha sana na yanatoa somo kubwa kwa wanaofuatilia jinsi demokrasia iliyokomaa inavyofanya kazi. Wanasheria wetu hapa Tanzania wana mengi ya kujifunza lakini nina wasi wasi kama kweli wanafuatilia kwa umakini wa kutosha mambo yanayojitokeza huko. Natoa pongezi kwa [B]Nguruvi3[/B] kwa namna anavyozidi kutuhabarisha yanayoendelea nchini Marekani na hasa siasa za huko.

Kinachoshangaza zaidi ni jinsi Mueller alivyoweza kuzuia kuvuja kwa taarifa zozote kuhusu utendaji wa kazi ofisini kwake. Machache yanayojitokeza ni yale ambayo walishayashughulikia zaidi ya miezi mitano iliyopita. Pamoja na kwamba si rahisi kutunza siri Marekani, watu wengi wanapiga tu ramli na hakuna anayejua kwa uhakika hatua aliyofikia katika uchunguzi wake. Watu wanamsema lakini yeye yuko kimya kama vile hawasikii!

Nina hakika siku atakayotoa taarifa rasmi, things will never be the same again! Kwa kweli nampa big salute kwa namna ofisi yake inavyofanya kazi. Pamoja na uchokozi wote kutoka sehemu mbali mbali, yeye anaendelea kuchapa kazi kimya kimya. Pamoja na kutukanwa na kuitwa kila jina na wasiompenda; kutuhumiwa na kuchokozwa hadi na Rais wa nchi...yeye na timu yake wapo tu kazini.

Ni kama vile wameweka pamba masikioni na kima kimya wanaendelea kuchapa kazi! Kitu kimoja hata hivyo kiko wazi, ripoti yake itawashangaza wengi! Na kwa hali inavyozidi kujitokeza siku hiyo haiko mbali na wengi wameanza kujitayarisha na kuchukua tahadhari kwa kuchagua upande. Lakini ni kama vile wanapapasa gizani, hawajui washike lipi na hata wale waliotegemewa kuwa makini wanajikuta wanakurupuka hovyo tu! Yetu macho, tuendelee kusubiri!
 
NDANI YA SIASA WIKI HII, YANAYOJIRI

Rais Trump na washirika ikiwemo TV ya Fox wameshikia bango hoja ya 'spy' katika kampeni za uchaguzi
Hakuna anayetoa ushahidi, ni tuhuma tu.Rais Trump akisema mkutano wa DOJ,WH na Nunes 'utatoa mengi'
Mkutano wa Alhamisi ni kupitia nyaraka za siri za DOJ na FBI kumbaini nani alikuwa, na alitumwaje

Ni utamaduni wa US 'classified information' hutolewa kwa wajumbe wa mabunge mawili
Wajumbe hao wa seneti na house hujulikana kama Gang of 8, kwa maana kuwa Republican 8 na Democrats 8
Gang of 8 inaundwa na viongozi wa vyama kutoka seneti na wawili kutoka House kwa kila upande,jumla ya nane

Gang of 8 kwa lugha nyingine linaundwa na wajumbe 8 wa Congress.
Hata hivyo si kila siri inayoweza kutolewa kwa Gang 8 kama Rais ataona ni muhimu kuhifadhi.
Kwa ufupi, intelligence za US huonwa na Gang of Eight

Katika hali isiyo ya kawaida na kinyume cha utamaduni, kikao cha Alhamisi ni kati ya DOJ, FBI na WH wakiwa na wajumbe wawili wa Republican akiwemo Nunes, mpiga debe wa Trump

Ile memo iliyozungumzia 'ubaya' wa FBI ambayo Rais Trump alidhinisha itoke 'declassified' haraka ni kazi ya Nunes
Dems walikuja na memo iliyoonyesha upotoshaji uliofanywa na Nunes, hoja ikafa

Mchezoulikuwa kutoa memo ya Nunes na kuchelewesha ya Dems upotoshaji ushike kasi. Haikusaidia
Nunes ndiye alikwenda WH na hoja ya wire tap kufanywa na Obama, ikafa haraka

Nunes alisema Suzane Rice, mashauri wa usalama wa Obama alianika majina ya watu hadharani kinyume na FISA. Rice akaua hoja mbele ya kamati ya Bunge iliyoongozwa na Republican

Mchezo unaotaka kuchezwa Alhamisi ni Nunes na kuona classified information kisha kufanya upotoshaji kwa kujua hakuna mwingine atakayeweza kuona na kueleza tofauti.

Ndicho Trump anakisubiri apate hoja akijua inaweza kuwa ni upotoshaji kama alivyofanya katika hoja tulizoeleza hapo juu

Dems na baadhi ya Republican wametaka kuona classified information na kushikilia bango wao nao washirikishwe. Hii ni baada ya kuambiwa wasubiri hadi september
Kilichotaka kufanywa ni kutoa miezi ya kutosha kufanya upotoshaji.

Imekubaliwa kuwa na vikao viwili katika nyakati tofauti za masaa mawili kesho

Kikao cha kwanza ni Nunes , DOJ, FBI na WH ambaye wanasema ataondoka
Baada ya masaa mawili kikao kingine cha Gang of 8, DOJ, FBI ambacho Nunes ataingia

Trick hapa ni Nunes kuona classified information kwanza, ili akienda kikao cha pili aweze kutengeneza 'narrative' itakayoweza kuwiana na mpango anaotaka kuutengeneza

Hilo litakutana na kikwazo. Gang of eight wameomba makusudi kushiriki kwa kuchelea kwamba upotoshaji utakuwepo, itakuwa ni kinyume cha desturi na itaweka mwanzo mbaya 'bad precedent' katika kushughulikia mambo ya usalama

Lakini pia kuna jambo Rais Trump na washirika wake hawajalisoma.
Kama alivyoeleza Mag3, Mueller amefanya kazi kwa usiri sana.
Kila habari inayopatikana inakuwa si chini ya miezi 3. Mueller yupo miezi 3 hadi 5 mbele ya tulipo

Leo kumevuja habari, Papadopolous, yule coffee boy anayesemwa na Trump kampeni, kwamba atafikishwa mahakamani kwa hukumu

Hii ni baada ya kutoa ushirikiano wa kutosha na kuhakikishiwa adhabu ya mashtaka itapungua na Mueller ameridhika Papadopolous hana alichobakiza katika kunyetisha

Huyu ni chanzo cha mambo yote ikiwemo kuingia kwa FBI kuchunguza Kampeni na uhusiano na Russia. Kuna ujumbe unapelekwa hapa!

Imebainika Jared Kushner, mkwe wa Rais alihojiwa tena na Mueller kwa masaa zaidi ya 7

Kila linapozushwa jambo kuua uchunguzi, kuna jambo 'linavujishwa' kuhakikisha propaganda zinadhibitiwa

Tutawahabarisha nini kitajiri siku ya Alhamisi

Tusemezane
 
NDANI YA SIASA ZA US WIKI HII

KASHFA YA ''SPYGATE '' YAUMBULIWA (DEBUNKED)
KUTA ZA UCHUNGUZI ZINAZIDI KUBANA

Wiki iliyopita tulieleza kampeni iliyoanzishwa na Trump akishirikiana na Rudi Gulian.
Kampeni ililenga kuonyesha FBI walipenyezwa kuchunguza kampeni kwa faida ya Clinton.

Kwa pamoja waliita tukio hilo 'spygate' kuonyesha ukubwa na ubaya wake

Ni kweli FBI walikutana na watu wa Trump kampeni baada ya kupata habari kuwa Russia wanaingia katika kampeni, hawakwenda kuchunguza kampeni bali Russia kama informant na siyo spy kwani neno spy linaonyesha 'uhalifu' zaidi

DOJ, FBI walikutana na makundi mawili kwa nyakati tofauti, lile la Nunes akiwa na Trey Gowdy, wote wa Republican, kisha walikutana na gang of 8 la Republican na Democrats

Matokeo ya classified information hayaonyeshi kuwepo kwa 'u-spy'.
In fact Trey Gowdy wa Republican amesema 'Trump angejua FBI walifanya nini angewashukuru badala ya kutuhumu, kasema FBI walifanya kilichopaswa kwa lengo jema

Pamoja na hayo Rais Trump ameendelea kusema kuna spygate akishirikiana na Rudi Gulian
Rudi amekiri kuwa huo ni mkakati tu wa kubadilisha mawazo ya watu

Nunes hajaonekana tena licha ya kwamba ndiye aliyepiga debe sana classified info hiyo
Kama tulivyowahi sema mpango mzima ni kutaka kumfukuza Mueller, umeshindwa tena

Kuna mbinu nyingine imetengenezwa, ni nzuri lakini ina tatizo, tuijadili

KUTA ZINAFUNGA 'WALLS ARE CLOSING IN'

Uchunguzi wa Mueller unaendelea kupunguza wigo ukizibana kuta za White house na kumsogelea Rais Trump kwa ukaribu zaidi

Kuna habari zimevuja aliyekuwa deputy FBI Andrew McCabe amempa memo bwana Mueller ikieleza nini kilitokea wakati wa kumfukuza James Comey

McCabe anasema, aliongea na Roseinstein (Deputy DOJ) baada ya kufukuzwa kwa Comey.
Roseinstein alimueleza kuwa Rais Trump alimtaka aandike barua ya kumfukuza Comey kwasababu ya suala la Russia siyo email za Clinton

Hapa ndipo mchezo mzuri unapogeuka kuwa shubiri

Inaendelea...
 
KUTA ZINAFUNGA
Sehemu ya II

Republican wamevujisha habari ili kuwepo na mjadala kuwa Roseinstein alijua nini kinaendelea lakini alifumbia macho na lingemlazimu ajitoe 'recuse' kama alivyofanya AG Session.

Kwamba media na Congress watamtuhumu kwa cover up

Kumbuka lengo ni kumuondoa Roseinstein ili apatikane mwingine atakayemsimamia Mueller.
Jitihada za kum-furstrate Session zimekwama, haonekani kujali dhalili kutoka kwa Trump

Mkakati wa kuvujisha siri ili Roseinstein ajitoe umeingia shubiri.

Endapo Roseinstein atajitoa kwasababu alijua Rais Trump alimuagiza amfukuze Comey kwasababu ya Russia, itakuwa tatizo kubwa kweli kwa Rais Trump

Kuna hoja mbili, kwamba, Mueller anachunguza Russia na ilivyoingilia uchaguzi, na pili, Mueller anachunguza obstruction of justice jambo ambalo ni baya haswa kwa nchi kama US

Hivyo Roseinstein akijitoa utakuwa ni ushahidi kuwa Rais Trump alimfukuza Comey kwasababu ya kutakuwa kuua uchunguzi wa Russia na hiyo ni obstruction of justice

Waliovujisha habari badala ya kumsaidia Rais Trump wanamweka mahali pagumu zaidi

Kwa kutambua hilo, leo Rais Trump amekana, hakumfukuza Comey kwasababu ya Russia kupitia tweet ya asubuhi. Trump anafahamu hilo ni tatizo kubwa na anajaribu kujiondoa

Kwa bahati mbaya sana, huko nyuma Rais Trump alisema katika mahojiano 'pamoja na mambo ya email nilishafikiri kumtimu Comey kwasababu ya hili jambo la Russia'

Rekodi zinafumuliwa akitamka kwa maneno yake, atawezaje kukana hilo sasa hivi?

Wanasheria walimuonya mara nyingi kuwa uchunguzi ukiendelea si vema kusema sema hovyo
Hakika ushauri ulikuwa wa maana kwasababu leo anakana alichosema, akionyeshwa rekodi

Kibao kimegeuka, mkakati wa kumtimua Roseinstein unageuka kuwa wa kumlinda

Kumlinda kuna maana moja, kwamba, asije jitoa kwasababu ya ''obstruction of justice''
Akifanya hivyo, tayari Rais Trump atakuwa katika mtego wa obstruction of justice

Lakini pia kuna kosa jingine la kifundi. Rais Trump na wapambe walipopiga debe Andrew McCabe atimuliwe walipuuza ukweli kuwa anaweza kuwa shahidi mzuri kama ilivyo sasa

Kwa hali ilivyo, pressure ya public kutaka Roseinstein ajitoe inamtia kiwewe Rais Trump
Kumwacha aendelee ni kuruhusu Mueller akamilishe kazi inayomtia kiwewe pia

Kiwewe si Russia collusion, bali nyaraka zinaweza kutoboa siri nyingi zinazomhusu
Kiwewe ni pamoja na obstruction of justice hasa wakati Mueller akimtaka kwa mahojiano

Kuta zinazidi kubana kutoka kila pande

Tusemezane
 
'Impeachment' ya Trump bado tu??
Impeachment ya Trump iko pale pale...GOP kwa unafiki na woga wao wanaweza kumsave temporarily kama tulivyotabiri lakini akae akijua hatma yake inategemea matokeo ya mid-term elections. Kabla ya hapo Mueller anategemewa kukamilisha kazi na GOP kama hawatazinduka na kuacha woga, uchaguzi utawaumbua. Au wewe, mpenzi wa Trump, unasemaje?
 
Mag3 katika kipindi cha wiki kadhaa yamepita mengi muhimu. Bado tunayafanyia kazi

Baada ya Nunes na Trey Gowdy kutaka kuona nyaraka za DOJ, walionyeshw.
Trey , Spika Ryan na McConnel kwa wakasema hakuna kitu kipya au walichoona kuhusu FBI

Taarifa iliyosubiriwa ya OIG nayo haikuwa na jambo lolote la maana linalo implicate FBI

Mueller ameendelea licha ya kusakamwa na GOP na Trump. Uchunguzi unachukua hatua mpya hasa panapokuwa na ushirikiano kati ya FBI South district NY na Mueller kuhusu Cohen

Kesi ya Cohen haihusiani na Russia investigation bali mwanadada Stomy Daniel.

Hata hivyo Cohen alikuwa mwanasheria wa Rais Trump kwa kila alichoitwa Fixer.
Uhusiano wa wawili hao umetetereka na kwamba Cohen huenda aka flip

Hofu ya Trump team si Stomy Daniel tu, bali kiasi anachojua Cohen na pengine kikihusishwa na malipo au miadi au maongezi yanayohusu Russia.

Hali inakuwa ngumu pale Russian Oligarch kuwa na mahusiano na Cohen
Hii ina maana moja, uchunguzi wa Mueller unaendelea. Haijulikani ana nini au hana nini

Kutokana na hofu, mipango inasukwa kumuondoa Roseinstein kisha kufunga uchunguzi

Devin Nunes anataka nyaraka zaidi za FBI wakati Roseinstein anasema kufanya hivyo ni kuharibu uchunguzi. Hili, GOP ya Nunes , Jordan na wengine wanalifanya makusudi

Wanachotaka ni kuingia katika malumbano na pengine kufanya kitu kuonyesha amedharau kamati ya Bunge, na kupitia hilo Rais Trump atapata cover up ya kumfukuza Roseinstein

Kulekea midterm, GOP hawataki Trump afanye makosa kwani gharama watazilipa wao
Rais Trump ana nguvu sana katika Republican, akiwatishia kadri anavyoweza

Kashindwa kumfukuza Jeff Sessions kuna hofu ya backlash kutoka Senate.
Hili la Roseinsten halionekani tofauti. Kadri muda unavyosonga Mueller anachimba

Jambo moja linalowahangaisha watu kuhusu hii Russia investigation ni kuwa endeapo hakuna tatizo, mbona kuna jitihada za kila aina kutaka kulifukia au kuliharakaisha?
 
TAARIFA YA MAJASUSI WA URUSI

Katika kuendelea na uchunguzi wa Russia, wiki hii Deputy AG Rosenstein ametoa taarifa ya mashtaka (indictment) dhidi ya majasusi wa Urusi wanaotuhumiwa kujihusisha na chaguzi wa Marekani. Majasusi hao ni askari na wapo nje ya nchi

Rosenstein alisema taarifa hizo alimpa Rais Trump kabla ya kuelekea Brussels. Aliendelea kusema ilikuwa vema kwa Rais kuzijua kwa kuzingatia anakutana na Rais wa Russia

Taarifa ilisema hakuna Raia wa Marekani anayetuhumiwa kwa mujibu wa taarifa hiyo
Kauli hiyo ilizua propaganda hasa mrengo wa kulia wakisema 'no collusion' kutoka kwa Trump kampeni. Taarifa ikiangaliwa kwa undani imeandikwa kiufundi sana na inaeleza kitu

Kwanza, ilikuwa ni kumweleza Rais Trump na wapambe wake kuwa Russia walitenda hilo kama ilivyoripotiwa na vyombo vya ulinzi na salama. Maana yake hakuna witch hunt

Pili, idadi ya Warusi na Wamerekani wanaochunguzwa inazidi kuongezeka

Tatu, taarifa imeonyesha mawasiliano kati ya mshirika wa Trump bwana Roger Stone na mtu aliyejulikana kama Gulcifer 2. Huyu Gulcifer ana mahusiano na Wikileaks na Kremlin

Nne, taarifa imetoa muda halisi wa nini kilitokea. Inaporejewa nyuma, ni wazi kuna siku Rais Trump alisema 'Russia kama wanamsikia watoe emails za Clinton' na muda unaowiana kitendo kiltokea. Dep.AG Kuweka muda katika taarifa kuna mantiki isiyoonekana kirahisi

Wachunguzi wanasema inawezekana ilitokea tu (coincidence) au ilikuwa ni ishara (signal) ya mawasiliano kati ya kampeni na Russia. Hili linafanyiwa kazi hasa likimhusu Roger Stone

Lakini pia wachunguzi wanarudi nyuma na kujiuliza. Siku ilipotoka tape ya Hollywood ikimuonyesha Trump akijifaragua kukamata nyeti za wanawake, ni siku hiyo hiyo email za kampeni meneja wa Clinton bwana Podesta zilimwaga hadharani na Wikileaks

Kinachoulizwa, matukio hayo yanakuwaje na 'bahati' tu kila mara?

Hili la majasusi linashadidiwa na taarifa ya leo ya gazeti la Washington Post inayosema majasusi hayo yanahusishwa na tuhuma za matumizi ya gesi za sumu yaliyotokea Uingereza

Katika mazingira ambayo Rais Trump anaonekana 'kuikumbatia' Russia, tukio la taarifa ya Rosenstein na hili la majasusi kuhusishwa na ujasusi mwingine linamweka mahali pagumu

Taarifa ya AG ina mambo yakiangaliwa kwa kudodosa kunaitia shaka kambi ya Trump.

Hakuna anayejua nini kimepatikana katika ofisi ya mchunguzi Mueller, inatosha kusema kuwa uchunguzi huo unaonekana si witch hunt au fake, lipo jambo

Kwa upambe wa Bunge nako kunasongombingo.
Zile text za Strzok na Page zimeshikiwa bango na Republican ili kuonyesha uchunguzi mzima wa Russia ulijaa upendeleo. Kumbana strzok kunazua hoja na kueleza mengine

Tusemezane
 
Impeachment ya Trump iko pale pale...GOP kwa unafiki na woga wao wanaweza kumsave temporarily kama tulivyotabiri lakini akae akijua hatma yake inategemea matokeo ya mid-term elections. Kabla ya hapo Mueller anategemewa kukamilisha kazi na GOP kama hawatazinduka na kuacha woga, uchaguzi utawaumbua. Au wewe, mpenzi wa Trump, unasemaje?
Trump akipigwa chini, Kunaweza kukatokea 'Civil War' Marekani, sidhani kama intels za US zinaweza kufanya uzembe wa namna hiyo!
 
Katika kuendelea na uchunguzi wa Russia, wiki hii Deputy AG Rosenstein ametoa taarifa ya mashtaka (indictment) dhidi ya majasusi wa Urusi wanaotuhumiwa kujihusisha na chaguzi wa Marekani. Majasusi hao ni askari na wapo nje ya nchi
Nyongeza: Russia imekubali kutoa ushirikiano kwa raia wake kufanyiwa uchunguzi hata mahojiano juu ya hili lakini pia na yenyewe imetaka ukubaliwe kuwahoji Christopher Steele, Michael McFaul juu kumsaidia Bill Browder kutorosha kiasi kikubwa cha ela kutoka Russia. Ikumbukwe kuwa hawa wanaotakiwa kuhojiwa na Russia walikuwa washirika wakaribu sana na Hillary R. Clinton mpaka kuelekea kwenye uchaguzi.
 
Back
Top Bottom