Mzuvendi
JF-Expert Member
- Apr 28, 2009
- 561
- 545
Mkuu kuna wakati nakushangaa kidogo.
Hili jambo nimelizungumzia mabandiko mawili au matatu yaliyopita hasa la Stormy
Stormy na Karen wanasema wamefanya mapenzi na Trump wakieleza hadi vyumba walivyoingia
Michael Cohen, wakili wa Trump amekiri kutoa 130,000$ kuziba midomo
Michael Avinnati, wakili wa Stormy, anasema Trump au wakili wake wasimame kukanusha.
Hakuna anyekanusha. Wanachotaka ni arbitrations nje ya court, kwamba suala limalizwe kiutu uzima
Malipo yaliyofanywa na Cohen kukiri siku 13 kabla ya uchaguzi yakazua swali kama ilikuwa ni sahihi kwa kuzingatia sheria za uchaguzi na kwamba gharama hizo ni sehemu ya pesa za kampeni au la
Fukua fukua ikamkuta Mueller ambaye aliona kuna `crime`na kupeleka kwa FBI, nao wakata kupata kibali cha kumpekua Cohen.
Walimtumia prosecutor aliyeteuliwa na Trump kutaka ruhusa ya mahakama ya Jaji aliyeteuliwa na Trump. Kumbuka FBI ipo chini ya Wray aliyeteuliwa na Trump, AG aliyeteuliwa na Trump na Deputy AG Pia. Hapa kuna nani ana `twist`
Tatizo linalojitokeza, ukisharuhusu kupekuliwa chochote na lolote linaweza kutokea
Nikupe mfano rahisi unaoweza kuulewa, Polisi wanaweza kuja kkukupekua nyumbani kwako kwa hisia kuwa una nyaraka zilizotumika kuiba pesa ofisini.
Katika upekuzi wakakutana na kichwa cha mtoto au mguu wa mtu
Usitegemee Polisi wataacha hilo kwasababu eti wanatafuta nyaraka. Umeelewa!
Jaribu kuwa na information za kutosha kuhusu mada, usiwe na `bias blind`
There's no deep state or group of people who have conspired to overthrow Trump's presidency. The problem with Trump is he came to power with a lot of baggage and he wants his opponents to cut him some slack. It doesn't work that way. Besides, he gets a taste of his own medicine. What did think when he used to trash his opponents during the primaries and general election? This isn't the guy who linked Ted Cruz's father to the assassination of JFK?