General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,064
Mkuu kuna mambo yanayotokea ambayo huko nyuma ima hayakuangaliwa, au yaliangaliwa ''for granted'' kwa kuangalia ukubwa wa ofisi n.k.
Katiba imetenga mihimili kwa uwazi, executive, Judicial and Legislative.(co equal branches of government). Kwa mantiki hiyo Rais anaondolewa madarakani kwa njia ya impeachment tu
Impeachment ni utaratibu mgumu sana, kwamba, House itaandika article of impeachment kama inavyotokea sasa hivi.
Halafu article itapelekwa mbele ya senate kwa mjadala.
Kama kutakuwa na mashtaka kutokana na mijadala ya senate, atakaye preside ni Chief Justice
Ipo katika katiba kwamba lazima kupatikane 2/3 ya wajumbe wa senate ambao ni 99 na VP ili kumuondoa Rais.
Hilo liliwezekana zama hizo si kwa nyakati hizi ambapo senate imepoteza ile nguvu yake (inherent powers) kama tunavyoshuhudia sasa hivi.
Katiba haisemi kama Rais anaweza kushtakiwa akiwa madarakani. Watalaam wanasema ingalikuwa haiwezekani basi walioandika katiba wangeweka kifungu cha'' immunity''
Kwa tafsri ya idara ya sheria imekubalika Rais akiwa madarakani hawezi kushtakiwa
Ieleweke kutoshtakiwa ''is not enshrined in the constitution '' ni legal opinion kutoka DOJ na OLC
Kitu kikiwa ''enshrine'' katika katiba hakiwezi kukwepeka, ni andiko lisilo na utata wa kisheria
Ni kwa msingi huo, Robert Mueller akifikisha uchunguzi wa Russia alisema katika kamati ya Bunge kwamba hawakuweza kumshtaki Rais Trump kutokana na ukweli kuwa Rais aliye madarakani hawezi kushtakiwa kama DOJ inavyosema
Alipoulizwa endapo anaweza kushtakiwa baada ya kumaliza muda wake, Mueller alisema ''Yes''
Swali hilo aliulizwa na Nadler mwenyekiti wa kamati ya sheria ya House kwa sasa
Baadhi ya wasomi wanasema kuna utata katiba haikusema hivyo kwahiyo ni suala lililobaki wazi
Wengi wa Wasomi wa sheria wanakubaliana na maoni ya Mueller kwamba anaweza kushtakiwa
Kitu kilichowazi ni kuwa Rais baada ya muda wake anaweza kushtakiwa kwa ''criminal'' kesi kwani muda huo anakuwa Raia na nguvu au kinga inakuwa haiopo.
Huo ndio msingi wa DOJ kusema Rais aliye madarakani hawezi kushtakiwa
Mkuu,
Rais hawezi kushtakiwa baada ya kustaafu?
Kama anakinga ya kutoshtakiwa akiwa madarakani, vipi akimaliza muda wake?