Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

KUSHINDWA KWA REPEAL & REPLACE OBAMACARE...
  • Trump aliaminisha watu atakuja na kitu kizuri kuliko Obamacare.
  • Rais Trump alisema atafuta Obamacare siku ya kwanza kwani ni kitu rahisi tu.
  • House na senate wanakubaliana Obamacare siyo perfect inahitaji kurekebishwa.
  • Pendekezo la Trump kufuta kwanza (Repeal) Obamacare limelenga kuwafurahisha wapiga kura wake kwamba ametimiza repeal.
  • Rais Trump kakutana na ugumu wa WH na utawala na si Trump Organization
  • Obamacare ya Obama imebaki sheria licha ya miaka 7 ya Reps kuipigia kelele...
Kwa kweli wajinga ndio waliwao...Trump hakujua hata kilichomo ndani ya Obamacare lakini akaapa kuirepeal...! Yuko jamaa yetu [B]El Jefe[/B], alituhakikishia kwamba Trump anayo healthcare nzuri tayari ya kuireplace Obamacare siku ya kwanza tu ofisini, sijui leo anasemaje!

Kwa kweli njia ya muongo fupi...Trump anayo House, anayo Senate na hahitaji hata kura moja kutoka kwa Democrats lakini bado kakwama! Kukwama kwa healthcare ina maana kwamba hoja ya tax reform nayo imekufa kifo cha mende kwani kulingana na kauli zao hoja hizi mbili zinategemeana!

Ukitaka kusema uongo utunze kumbukumbu...Awali Trump aliapa kutimiza ahadi zake zote katika kipindi kisichozidi siku 100 na bila soni anadai keshatimiza mengi kuliko viongozi wote waliomtangulia! Ukweli ni kwamba miezi sita sasa inakatika hakuna mswada wote uliopitishwa na Congress.

Mizimu ya mjaluo inaendelea kumtafuna Trump.
 
MKUTANO 'WA SIRI' WATUMBULIWA

REPEAL NAYO YAKUTANA NA KIGINGI

Counsel Mueller ametoa ruhusa kwa kamati ya Bunge kuwahoji Don Jr na Paul Manafort
Imetoa ruhusa ya kuhojiwa hadharani kwa maana, umma utaona na kusikia kila kitu

Mueller amefanya hivyo kwani kamati ilisita kuchelea uchunguzi wake
Kufanya hivyo kunawaweka wahojiwa njia panda chini ya kiapo. Kuongopa ni kosa

Wakati hayo yakiendelea chini chini, imebainika Rais Trump alikuwa na mkutano wa saa moja na Rais Putin Hamburg. Hii ni baada ya kukutuana officially kabla ya hapo

Katika mkutano huo, hakuna afisa wa US bali Trump , Putin na mkalimani wa Putin
Kinachoshtua ni kutokuwepo kwa afisa yoyote wa serikali ya Marekani

Baada ya mkutanoimefahamika Trump ali tweet kuhusu cyber security unity ya pamoja

Katika mazingira ya uchunguzi huku washirika muhimu wakiwa katika 'radar' na usiri wa mkutano huo hadi waandishi walipoutumbua, ni jambo linalotikisa habari ndani ya DC

Wakati huo huo, baada ya repeal and replace Obamacare(ACA) kushindikana, Rais Trump ametoa kauli ' Obamacare iachwe ifeli' halafu kitaandikwa kitu kipya akiwalaumu Dems

Rais Trump ameshindwa kuelewa ni Rais, kufeli kwa healthcare ni tatizo la wananchi si chama na hilo halipaswi kuwa 'political score point'

Hili limeleta ukakasi kwa wengi kuona Rais akikubali hali iharibike kwasababu za kisiasa

Trump anaposema ACA ifeli tayari ana hujumu kwa kutotoa resource za ku support.
Pamoja na hayo kauli yake inatishia makampuni ya Bima yanayojitoa

Senate Majority McConnel amefuata maagizo ya Trump ya ku repeal kwanza Obamacare
Wachunguzi wanahoji ku repeal nini kitaziba nafasi yake wakati kipya kinatengenezwa?

Maseneta watatu wameahidi kukataa mswada huo na inaonekana utashindwa kabla ya kujadiliwa wenyewe wakisema dead on arrival (DOA)

Kila uchao WH imekuwa katika 'crisis' wakati ambapo miswada muhimu imekwama

Sehemu kubwa ya kushindwa ipo kwa Trump ambaye approval rate yake ni 36% katika miezi sita ukilinganisha na marais wengine waliotawala miaka 70 iliyopita

Tusemezane
 
...Trump anaposema ACA ifeli tayari ana hujumu kwa kutotoa resource za ku support.Pamoja na hayo kauli yake inatishia makampuni ya Bima yanayojitoa
Aangalie tu asije akajiongezea kosa lingine la dereliction of duty!
 
Kwa kweli wajinga ndio waliwao...Trump hakujua hata kilichomo ndani ya Obamacare lakini akaapa kuirepeal...!

Sio kweli, Trump anajua mengi kuhusu ObamaCare. Kutopata support ya Republicans kwa 100% hakumfanyi Trump kutojua yaliyomo kwenye O'care.

Trump alifanya kampeni kuhusu 'repeal and replace' ya O'care na alipigiwa kura kwa ajili hiyo. Katika kampeni alizungumzia O'care kusababisha 'health insurance premiums' kupanda badala ya kushuka, makampuni ya bima kuweka 'deductibles' za juu hali inayosababisha mtu mwenye bima ya afya kushindwa kutumia bima yake kupata matibabu n.k

Concerns za Trump (na amekuwa consistent) ni kushusha premiums ili healthcare iwe nafuu kwa wote ili wengi waweze kumudu, kuhakikisha makapuni hayakimbii 'health insurance exchange market' katika States, kuwapa watu options au choices badala ya kulazimisha watu kutumia plan wasioitaka, kuhakikisha kuna ushindani ili kuboresha huduma zinazotolewa na makampuni ya bima ya afya, kupunguza budget deficit etc.

Yuko jamaa yetu [B]El Jefe[/B], alituhakikishia kwamba Trump anayo healthcare nzuri tayari ya kuireplace Obamacare siku ya kwanza tu ofisini, sijui leo anasemaje!

Trumpcare ni nzuri, Dems na 'obamacare republicans' wameamua kuendekeza siasa na usumbufu usio na msingi.

Hapo unaposema 'siku ya kwanza ofisini' nadhani umesahau Trump alisharekebisha hiyo kauli.

Hao Rep Senators wanne walioifanya Senate health bill kukwama hawazifanyi hizo bills kuwa mbaya. Wao wanapinga tu ila hawana proposal yoyote wanayoweka mezani kujadiliwa ili kutatua matatizo ya ACA yaliyopo.

Wanatetea vitu visivyotatua bali vinavyoongeza matatizo, wanataka kila wanachokitaka kiwemo. Kwa maana nyingine wamesimama na Dems wasiotaka 'repeal'. Ila mwisho wa siku Obamacare itakuwa repealed and replaced, nothing less than that.

Kwa kweli njia ya muongo fupi...Trump anayo House, anayo Senate na hahitaji hata kura moja kutoka kwa Democrats lakini bado kakwama!

Sio kwamba Republicans wamekwama, ila option ya 'repeal and immediately replace' ndio iliyokwama hadi sasa.

Option ya 'repeal and delay replacement in 2 years' bado haijakwama, ingawa kuna 'obamacare Republicans' a.k.a moderates ambao hawataki kutoa ushirikiano bila sababu za msingi.

Tuongee tu ukweli, kuna Rep Senators wawili (Lisa Murkowski -Alaska, Shelley Capito -W. Virginia) waliipigia kura 'ACA repeal bill' ya 2015 iliyokuwa vetoed na Rais Obama kipindi hicho, halafu leo hii wanasema wataipinga, huoni kama hawa Senators watakuwa na matatizo?

Susan Collins (Maine) hakuipigia kura ACA repeal bill ya 2015, huyu ni msumbufu tu hana lolote.

Kuna vipengele vya repeal bill katika phase za mbeleni (kwa sababu inafanyika katika phases) zitahitaji kura za Democrats.

Kukwama kwa healthcare ina maana kwamba hoja ya tax reform nayo imekufa kifo cha mende kwani kulingana na kauli zao hoja hizi mbili zinategemeana!
Hoja ya Tax reform haijakwama ingawa nayo inaweza kupata usumbufu kama huu wa Trumpcare kutokana na kuwepo kwa debates za kina.

Kupitisha vitu Congress haijawahi kuwa kazi rahisi hata kama Rais ana majority House na Senate. Obama alishindwa Immigration reform miaka yote 8 aliyokaa madarakani. Obama pia alishindwa kupitisha Buffet Tax reform n.k.

Trump ndio kwanza ana miezi sita, watu mnaanza ku-judge kama vile anakaribia re-election, wanaoenda mid-term elections 2018 nao wanatambua wanayo kazi ya kufanya, ndio maana wanajaribu kupitisha 'landmark legislations'.

Kukwama kupo katika kila jitihada, ndivyo demokrasia inavyofanya kazi na wala hakumaanishi kifo cha hoja husika wala mwisho wa kujaribu tena.

Ukitaka kusema uongo utunze kumbukumbu...Awali Trump aliapa kutimiza ahadi zake zote katika kipindi kisichozidi siku 100 na bila soni anadai keshatimiza mengi kuliko viongozi wote waliomtangulia!

Obama aliapa kufunga gereza la Guantanamo Bay siku ya kwanza ila hadi leo bado ipo wazi. Ni wapi Trump alisema atatimiza ahadi zake zote ndani ya siku 100?

Trump amesaini bills 42 kuwa sheria ukilinganisha na bills 20 alizosaini G.W. Bush na bills 39 alizosaini Obama mda kama huu. Anaweza asiwe sahihi kama anamaanisha viongozi wote waliomtangulia, lakini kawazidi wengi tu.

Ukweli ni kwamba miezi sita sasa inakatika hakuna mswada wote uliopitishwa na Congress. Mizimu ya mjaluo inaendelea kumtafuna Trump.
Miswada 42 imepitishwa na Congress na tayari Rais Trump ameshazisaini kuwa sheria.

Labda kama unamaanisha 'landmark legislations' kwa mfano healthcare, tax, immigration, infrastructure etc.

Hivi mazuri mengi yanayofanyika US chini ya Rais Trump hamyaoni au hamyajui?
 
LAWAMA KWA DEMS ??

Rais Trump alilaumu kutopata msaada wa Democrats kupitisha mswada uliokwama wa Healthcare
Kama kawaida, Trump ni mzuri sana wa kupumbuza wafuasi wake

Kwanza, Trump hakuwa na ilani ya uchaguzi ikizungumzia hoja kwa mantiki.
Hakuwa na healthcare plan, alichofanya ni kutumia jina la Obamacare kuaminisha ana kitu bora

Pamoja na hayo, Obamacare ina vitu 'core' ambavyo haviwezi kufutwa kwa namna yoyote
Pre existing condition ni kimoja na cha pili ni Medcaid n.k.

Miswada iliyokwama mara mbili sehemu kubwa ipo katika mambo hayo.
Trump alidhani anaweza kufanya hayo kwa kutumia Republicans katika house na Senate

Mswada ulipita katika house kukiwa na mashaka dhidi ya wabunge 20.
Walichokifanya ndani ya house ni kukwepa lawama na kusukuma mbele ili senate iamue

Katika seneti McConnel alitumia Republicans peke yao kupitisha mswada akiwa na uhakika wa 50 votes

Rep wapo 52, John Mcain alipougua wakaahirisha kwasababu wangekuwa na 51 votes.
Tayari masenata 2 walishasema watapiga 'no'. Uwezekano wa kumshawishi mmoja ulikuwepo

Waliojitoa wawili zaidi wakabaki 49 na Mcain alishaonyesha wasi wasi katika maamuzi
Mwisho wa siku ikawa 52-4 = 48 ambayo Mcain angepiga ndiyo inabaki 49

Hawa ni Republicans hakuna Democrats hata mmoja aliyeingilia utaratibu na mbinu za Mconnel

Kushindwa kwa mswada ni failure ya Trump kukaa pamoja na kutafuta kura kutoa kila mahali
Hoja ya Trump ni ku repeal lakini hana ufahamu wa nini kilichomo ndani ya mswada

Ilifika mahali akaita mswada 'mean' wakati huo huo anausubiri ausaini!!! Yaani ku repeal tu

Tulijdaili hapa kwanini ni ngumu kwa GOP kutokana na makundi yenye interest tofauti

Mtu anayedhani Dems wamehusika arudi akajifunze kwanza kabla ya kupumbazwa na Trump

Ni Rais Trump aliyepumbaza watu Obamacare ni disaster kama disaster ya Iran deal
Aliahidi makubwa kwa Israel tarehe 1 siku 20 kabla ya kuapishwa akisema wavumilie siku chache tu

Well, juzi Serikali ya Trump imethibitisha vikwazo alivyoweka Obama vinatekelezwa na Iran
Huyu ndiye aliyesema deal ni disaster akipumbuza watu leo hawana usemi

Tusemezane
 
Kwakuwa Republicans wana simple majority kwenye Senate, wameamua kutumia 'budget reconciliation' kujaribu ku-repeal O'care. Hawajaenda na 'bipartisan' kwa sababu Dems hawataki kusikia suala la 'repeal' ya ACA kitu ambacho Republicans waliahidi kipindi cha uchaguzi.

Ili njia hiyo ifanikiwe ni lazima Republicans wa-prove kwamba Trumpcare ni 'deficit neutral', kwa maana kwamba haiongezi deficit kabisa (zero).

'Reconciliation bill' inatumia elements mbili kati ya 'revenue, expenditure na national debt' ku-affect 'budget'. Trumpcare inapunguza 'medicaid spending' ili kupunguza element ya 'expenditure' kwenye 'budget'.

'Obamacare republicans' wanaelewa hivi vitu ila wanakuwa wasumbufu tu. Ndio maana 'partisan bill' ya Republicans ina cut 'medicaid spending', ikizingatiwa kwamba inaongeza Spending kwa States ku-buffer 'health insurance exchange market' kutokana na high risk category (wenye pre-existing conditions).

Trumpcare inahakikisha watu wenye pre-existing conditions wanapata 'coverage' (that is spending increase).

Trumpcare inapunguza 'Medicaid spending' (spending decrease) ila watu wa kipato cha chini still wanaweza kutumia Healthcare Savings Account kununua health insurance ambayo itakuwa more 'affordable' eg. kutokana na kuwepo kwa ushindani (mfano kuweza kununua bima across State lines).

Trump akiongeza 'spending kwenye medicaid' atakuwa anai-support O'care na ni kitu ambacho 'conservatives' hawakitaki kwa sababu hawapendi kuongeza matumizi kwenye welfare programs.

Mtu ana coverage ya O'care ila hawezi kuitumia kwa sababu 'deductibles' zipo juu, still Insurance companies zinakimbia States (kuna counties zimebaki bila hata insurance player mmoja) kwa sababu wanapata hasara, wenye afya (healthy individuals) wanaachana na O'care kwa sababu ni expensive, wengine wapo tayari kulipa 'penalties' badala ya kulipia 'premiums' n.k

Dems wanasema Trump anapunguza 'medicaid spending' ili kufidia (pay for) 'tax cuts' anazotaka 'kutoa kwa matajiri'!!, sio kweli, Tax reform ya Trump ina mpango ndio wa kushusha 'corporate tax rate' kutoka 35% hadi 20-15% ila siyo kwa matajiri bali ni 'across the board'. Lakini pia kushusha taxes kwa 'middle class'. Lengo ni kukuza uchumi na kutengeneza nafasi za ajira.

Ila mpango wa kufidia (pay for) hizo 'tax cuts' ni kupitia ukuaji wa uchumi (economic growth) sio 'medicaid spending cuts' kama dems wanavyodai. Kwamba uchumi utakavyokuwa unakua na uzalishaji kuongezeka basi makusanyo ya kodi yataongezeka. Aina hiyo ya tax plan hata Mitt Romney alisimamia kwenye uchaguzi wa mwaka 2012.

Unaweza kufidia 'tax cuts' kwa njia tatu tu, (i) kuongeza kodi kwingine (ii) kupunguza matumizi (iii) ukuaji wa uchumi. Trump hana mpango wa kuongeza kodi na anahitaji nchi ifikie kwenye 'balanced budget'.

Hopefully Republican senators watamaliza tofauti zao na kuweza kufanikisha Trumpcare, au wanaweza kurukia kwenye Tax reform au Infrastructure then wakarudi tena kwenye Trumpcare.
 
Sio kweli, Trump anajua mengi kuhusu ObamaCare.Trump alifanya kampeni kuhusu 'repeal and replace' ya O'care na alipigiwa kura kwa ajili hiyo.Trumpcare ni nzuri, Dems na 'obamacare republicans' wameamua kuendekeza siasa na usumbufu usio na msingi.
Trumpcare? Ni lini umemsikia Donad Trump akiinadi hiyo Trumpcare? Ninavyojua yeye yuko tayari kusain chochote kile atakachowekewa mezani na Congress na ndiyo maana aliisifu ile iliyopitishwa na House akiamini itapitishwa pia na Senate.
Hopefully Republican senators watamaliza tofauti zao na kuweza kufanikisha Trumpcare, au wanaweza kurukia kwenye Tax reform au Infrastructure then wakarudi tena kwenye Trumpcare.
Trump hakujua Obamacare ina nini ndani yake kama ambavyo hakujua kilichopitishwa na House kilikuwa na nini hadi wananchi walipoanza kuwashambulia wawakilishi wao kwa kupitisha kitu cha hovyo na hapo akageuka na kuiita mean! Kwa kifupi Trump hana plan yoyote, anachoahidi ni kwamba itakuwa the best, the most beautiful, the greatest...believe me!
 
"Mag3, post: 22356249, member: 10873"]Trumpcare? Ni lini umemsikia Donad Trump akiinadi hiyo Trumpcare? Ninavyojua yeye yuko tayari kusain chochote kile atakachowekewa mezani na Congress na ndiyo maana aliisifu ile iliyopitishwa na House akiamini itapitishwa pia na Senate.
Akafanya 'Bash' kusherehekea kupitishwa!! Ilishangaza baadhi ya watu

Kikao cha WH na maseneta kabla ya kukwama,walieleza hakujua kilichomo wala 'kuuza' sera

Hakuna mahali Trump anaweza ku 'articulate' kama livyofanya Obama

Muda huu(leo) amewaeleza maseneta wasiende likizo ya August bila repeal

Katika maelezo hakuna mahali alipogusia hoja za msingi zaidi ya kutafuta urafiki

Alichosema 'ana kalamu' mkononi tayari kusaini chochote kitakachokuja.

Hii maana yake ni kuwa hana plan anayoijua bali kusubiri plan itakayoletwa.

Tofauti na wagombea wa Dems na Reps waliokuwa na sera zinasomeka mitandaoni

Mkutano wa leo alitarajiwa ajenge hoja, hakuna kama kawaida.

Anachotaka ni ku repeal and replace kufuta legacy ya Obama bila kujali consequences

Ndivyo alivyosema jana kuwa 'iache Obamacare ife' akimaanisha hata kama hakuna replacement watu wakafa it's ok as long as anapata political point
Trump hakujua Obamacare ina nini ndani yake kama ambavyo hakujua kilichopitishwa na House kilikuwa na nini hadi wananchi walipoanza kuwashambulia wawakilishi wao kwa kupitisha kitu cha hovyo na hapo akageuka na kuiita mean! Kwa kifupi Trump hana plan yoyote, anachoahidi ni kwamba itakuwa the best, the most beautiful, the greatest...believe me!
Nakuhakikishia mswada ukipitishwa leo Trump hana muda wa kusoma.

Anachotaka ni kutoka kwenda kwa mshabiki wake na kusema ametimiza ahadi.

Ikiwa mswada ni mzuriii kwanini wananchi wanaupa asilimia ndogo kuliko Obamacare?

In fact watu wanaotumia medicaid sehemu ni wapiga kura wake!
 
Trumpcare? Ni lini umemsikia Donad Trump akiinadi hiyo Trumpcare? Ninavyojua yeye yuko tayari kusain chochote kile atakachowekewa mezani na Congress na ndiyo maana aliisifu ile iliyopitishwa na House akiamini itapitishwa pia na Senate.

Mbona Trump anazungumzia 'repeal and replace' Plan kote anakoenda na kupitia twitter account yake. Hata leo aliwaalika Senators wa Republican lunch WH kuzungumzia healthcare.

Sio kwamba Trump yupo tayari ku-sign chochote, bali ana washauri na anajua anachokitaka, lakini pia anahitaji kuondoa Obamacare haraka iwezekanavyo. Labda pengine hiyo haraka aliyonayo ndio inakufanya uone kama yupo tayari ku-sign chochote kile!

Hata Obama aliwahi kuonesha kalamu (Nanukuu: I've got a pen ready to sign) kuwa yupo tayari ku-sign 'Medicare Access and CHIP Reauthorization Bill ya mwaka 2015', ila hiyo haikumaanisha kuwa ange-sign chochote kile bali ni kuonesha utayari na uharaka wa ku-sign bill akishaletewa kutoka Congress.

Trump hakujua Obamacare ina nini ndani yake kama ambavyo hakujua kilichopitishwa na House kilikuwa na nini hadi wananchi walipoanza kuwashambulia wawakilishi wao kwa kupitisha kitu cha hovyo na hapo akageuka na kuiita mean! Kwa kifupi Trump hana plan yoyote, anachoahidi ni kwamba itakuwa the best, the most beautiful, the greatest...believe me!

Hivi Obama alivyokuwa akisema "if you like your plan, you can keep your plan" ina maana yeye mwenyewe hakujua vilivyomo ndani ya Obamacare? Alikuwa anazunguka kunadi kitu ambacho hakukisoma chote? Na aka-sign bila kujua? Obama aliahidi Plan yake itakuwa 'affordable', mbona sio affordable?

Trump anaweza asiwe anajua kila kurasa katika sheria ya Obamacare ina nini, ila anatambua vitu vya msingi vilivyomo na matatizo yake.

Obama mwenyewe hakuwa na Plan yake, Obamacare ilikuwa drafted na akina Robert Creamer, Elizabeth Fowler n.k. O'care ilijazwa uongo mwingi hata Obama mwenyewe alishindwa kujua kila kilichomo. Ndio maana hata Bill Clinton aliita 'crazy thing'. Unajua kwanini Dems wengi walikubali kusign 'O'care repeal bill ya 2015' na wakamwekea Obama kwenye desk yake? Kwa kuona aibu 'legacy' yake kupotea aka-veto!!

Hivi unakumbuka Nancy Pelosi alivyokuwa akisisitizia Congress kupitisha Obamacare ili watu wajue kuna nini ndani yake?
 
Mbona Trump anazungumzia 'repeal and replace' Plan kote anakoenda na kupitia twitter account yake. Hata leo aliwaalika Senators wa Republican lunch WH kuzungumzia healthcare.

Sio kwamba Trump yupo tayari ku-sign chochote, bali ana washauri na anajua anachokitaka, lakini pia anahitaji kuondoa Obamacare haraka iwezekanavyo. Labda pengine hiyo haraka aliyonayo ndio inakufanya uone kama yupo tayari ku-sign chochote kile!

Hata Obama aliwahi kuonesha kalamu (Nanukuu: I've got a pen ready to sign) kuwa yupo tayari ku-sign 'Medicare Access and CHIP Reauthorization Bill ya mwaka 2015', ila hiyo haikumaanisha kuwa ange-sign chochote kile bali ni kuonesha utayari na uharaka wa ku-sign bill akishaletewa kutoka Congress.



Hivi Obama alivyokuwa akisema "if you like your plan, you can keep your plan" ina maana yeye mwenyewe hakujua vilivyomo ndani ya Obamacare? Alikuwa anazunguka kunadi kitu ambacho hakukisoma chote? Na aka-sign bila kujua? Obama alihaidi Plan yake itakuwa 'affordable', mbona sio affordable?

Trump anaweza asiwe anajua kila kurasa katika sheria ya Obamacare ina nini, ila anatambua vitu vya msingi vilivyomo na matatizo yake.

Obama mwenyewe hakuwa na Plan yake, Obamacare ilikuwa drafted na akina Robert Creamer, Elizabeth Fowler n.k. O'care ilijazwa uongo mwingi hata Obama mwenyewe alishindwa kujua kila kilichomo. Ndio maana hata Bill Clinton aliita 'crazy thing'. Unajua kwanini Dems wengi walikubali kusign 'O'care repeal bill ya 2015' na wakamwekea Obama kwenye desk yake? Kwa kuona aibu 'legacy' yake kupotea aka-veto!!

Hivi unakumbuka Nancy Pelosi alivyokuwa akisisitizia Congress kupitisha Obamacare ili watu wajue kuna nini ndani yake?
Hivi kwa akili yako unataka kumlinganisha Obama na hii takataka, you've got to be kidding! Yaani upuuzi wote unaofanyika toka Trump aapishwe unaufumbia macho huuoni! Pamoja na Upresidency, Trump ana House na Congress achilia magavana kibao yet the negotiator-in-chief kama ulivyowahi kumuita hawezi kufanikisha lolote linalohitaji ushawishi. Dunia nzima kwa sasa inaicheka Marekani au huoni Trump anavyodhihakiwa kila pembe ya dunia.

funny-world-map-donald-trump-latest-raw.jpeg




trump_map_1.jpg


Donald%2BTrmp%2Bas%2Bseen%2Boutside%2Bthe%2BUS.jpg


20151116-PG05-MAP.jpg



1500327570_129_9-charts-that-capture-how-the-rest-of-the-world-feels-about-Donald-Trump-MarketWatch


Trump_Respect.png

 
Hivi kwa akili yako unataka kumlinganisha Obama na hii takataka, you've got to be kidding!
Obama alizunguka nchi nzima kumfanyia kampeni Hillary, akishirikiana na Bill Clinton, ila mwishoni alishindwa na huyo 'Takataka' KO !! Ndio maana aliwasisitizia 'don't underestimate him'.

Obama hakuwa malaika kama unavyofikiri, ndio maana sera zake zilishindwa na Trump.

Nimemlinganisha Trump na Obama kwa sababu vipo vya kulinganisha kama hivyo nilivyo-note.

Yaani upuuzi wote unaofanyika toka Trump aapishwe unaufumbia macho huuoni!

Iko hivi, nikiona Trump amekosea nasema hapa kakosea, wala siendekezi ushabiki, unaweza kuangalia posts zangu za nyuma.

Ila pia akifanya jambo zuri nasema hapa kafanya jambo zuri. Lakini pia sihangaiki na phony stories za kwenye media, kama media hawana FACTS habari zao zinakosa nguvu kwangu.

It's just a matter of FACTS, what are the FACTS with regards to Trump's Presidency, that's all.

Pamoja na Upresidency, Trump ana House na Congress achilia magavana kibao yet the negotiator-in-chief kama ulivyowahi kumuita hawezi kufanikisha lolote linalohitaji ushawishi.

Kwani umeona Trump ameachana na Healthcare baada ya kukwama mara mbili au ndio kwanza anazidi kukomaa nalo ili afanikishe? Atafanikisha legislations nyingi tu, it's just a matter of time. Na akishafanikisha healthcare mtarukia kingine!

Negotiations bado zinaendelea na mda si mrefu utaona Republicans wana-compromise. Hiyo ndio demokrasia.

Dunia nzima kwa sasa inaicheka Marekani au huoni Trump anavyodhihakiwa kila pembe ya dunia.
Kusema kwamba dunia nzima inaicheka U.S. sio kweli, labda utoe ushahidi.

Trump hadhihakiwi, media kadhaa ndio zinaaminisha watu hivyo. Kwa mfano, mke wa Rais wa Poland alimpa mkono Trump wao kwa makusudi kabisa wakaripoti kuwa alibaniwa mkono.

Katika hizo polls ulizo-attach hapo, kuna wengine ni mabingwa wa kukana tafiti zao e.g Pew, so trust but inspect.
 
subiria, siku ya kumu ' impeach ' Trump kama tulivyoaminishwa hapa kutokana na issue ya 'Russia collusion'.
Si kweli! tunachofanya hapa ni kuhabarisha nini kinatokea, kujifunza wenzetu wanafanya nini na kutafsiri mambo katika lugha rahisi ili wengi waweze kunufaika. Hatupo hapa kutuhumu, kuendesha mashtaka au ushabiki wa simba vs Yanga

Nitakupa mfano, tazama jinsi congress inavyofanya checks and balances Rais hawezi ku 'abuse' power.
Laiti ingelikuwa shaghalabala, Trump angefuta Obamacare kabla hajaingia WH

Hayo yanatokana na nguvu ya wananchi kwa wawakilishi wao.

Obamacare ni mfano mzuri, Rep seneti wanafanya maamuzi kwa kuangalia constituents inasema nini. Ndivyo inavyokuwa litakapokuja suala la infrastructure kwa Dems

Maana yake tunawaeleza watu wa nchi yetu bado wana nafasi ya kuiwajibisha serikali wakiamua

Hawajaamua kutumia nguvu ya sanduku la kura, kuwajibisha walioweka masilahi ya vyama mbele n.k.

Tutakapoweza kupata Wabunge bila kujali uchama, tutafanikiwa kuwadhibiti wakijua uwepo wao ni kwa ajili yetu na si kwa watawala.

Hapo tutakuwa tumevunja supremacy ya vyama na kuvifanya loyal kwetu

Mfano wa pili, US kuna mambo yanayoweza kufanywa kwa EO ya Rais, na mengine yanahitaji kupitia mchakato wa Bunge.

Si suala la mtu kuamka na kusema chochote nje ya katiba kikakubalika

Mambo kama hayo ndiyo tunayaelenga na ili kufikia lengo la kusaidia taifa kujielewa tunafuatilia nini wenzetu wanafanya kizuri, kipi kibaya, tuchukue kipi na tuache kipi
 
YANAYOJIRI SIASA ZA US

Jana CBO walitoa tathmini kuhusu repeal Obamacare,watu 22M watakuwa uninsured
Repeal haina maana kufuta sheria nzima ya afya, itaondoa mafao baadhi

GOP wamekutana kujadili pamoja wafanikishe repeal au repeal and replace.
Hakuna Dems aliyeshiriki, kuonyesha wanaolaumu pengine hawajui kinachoendelea

Sera kubwa anayoeleza ni ubaya wa Obamacare. Kama ilivyo kawaida, Trump ni 'obsessed' na Obama kiasi yeye na surrogates wake kumfanya Obama kama std

Mkutano na maseneta hakueleza sera bali urafiki na kuwatisha wanaopingana naye

Trump katika kampeni hakuwa na andiko la sera, anategemea senate na house
Ni tofauti na wagombea wengine wa GOP na Dems waliokuwa na japo template

Trump hajui nini tatizo na yanapotokea hujitenga kama alivyojitenga kwa Spika Ryan

Don Jr:
Don Jr na Manafort wanategemewa kukutana na kamati ya senti Jumatano kuhojiwa
Jared Kushner atahojiwa J'tatu nyuma ya kamera kutokana na nafasi katika serikali

Don Jr atakuwa chini ya kiapo. Hoja yake ya awali ilikuwa 'mkutano wa adoption'

Hoja iliungwa mkono na msemaji wa WH Sarah Huckabee siku zilizofuata
Rais Trump aka tweet, mkutano ulihusu opposition research! contradiction ikatokea

Kubwa kwa Jared ni lini alijua na kwanini alifanya marekebisho yaliyoibua emails.
Hili litaeleza Rais na Don Jr walijua lini kuhusu emails, tofauti na kauli zao za awali

Matumizi ya mitandao, na disorganization ya WH itazua maswali na huenda kutakuwa na kujichanganya au kukanusha au kuzua mengine. Mahojiano yatato picha nyingine

Rais Trump anena

Akihojiwa na NYT, Trump amesema angalijua Sessions ataji recuse asingemchagua.
Kauli iliyomdhalilisha Sesssions,licha ya kuacha useneta amesisitiza kuendelea na wadhifa

Siku za nyuma tulijadili uchaguzi wa Sessions ulilenga mahususi kwa Russia

Rais Trump akamshmbulia Comey kuhusu 'taarifa alizompa'akiwa mteule kuhusu Russia
Habari hiyo Trump aliita fake ingawa leo anakiri ilisemwa. Hapa Jamvini tulijadili hilo

Trump akamshambulia special counselor Mueller, uchunguzi usiingilie maeneo ya fedha
Alisema kufanya hivyo kutakuwa 'too much' akimaanisha anaweza kumfukuza

Mueller anawajibika idara ya sheria inayowajibika kwa Rais.

Katika hali ya kawaida idara hizo humshauri Rais zikiwa 'independent'.
Kwasasa Trump anataka kuzihodhi pengine kwa mtazamo wa Trump organization

Trump anaweza kumfukuza Mueller ni special counselor na siyo independent investigator
Hatua inaweza kuzua utata mkubwa kama uliopo sasa kuhusu 'financial interest zake'

Hakuna anayejua tax returns za Trump na kauli kuhusu hilo zinachagiza udadisi kulikoni kati ya tax return, Russia investigation n.k.

Suala la tax linarudi kwa nguvu ingawa halionekani na litamsumbua

Sehemu kubwa ya matatizo anayasabisha mwenyewe kwa kuzungumza bila mpangilio na bila kujua legal implications za kauli zake.

Mahojiano ya 'wanawe yatakuwa magumu kutokana na flip flop za Mzee''

Tusemezane
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Karibu tena mwalimu wangu wa Tuisheni.
------
Mimi nasubiria, siku ya kumu ' impeach ' Trump kama tulivyoaminishwa hapa kutokana na issue ya 'Russia collusion'.

Asante mkuu Tujitegemee,

Kusubiria 'impeachment' ya Trump kutokana na 'Russia collusion' ni sawa na kwenda mbugani kusubiri kumuona Tembo Mweupe.

Nimesoma post uliojibiwa hapo juu ila mtu akisoma posts za kwanza kabisa za uzi huu anaweza akabaini hasa lengo la uzi huu ilikuwa ni ipi.

Labda niulize, kama lengo lilikuwa zuri hivyo mbona haikuandikwa mwanzoni mwa uzi badala yake posts ni za kuhusu 'utata', 'timbwili', 'crisis','Russian collusion','kuboronga' 'kufeli' kwa Trump? Chuki level za akina Rosie O'donnell na mastaa wengine wa Hollywood!!

Media walituambia Rais Trump alikutana na Rais Putin wakafanya mazungumzo ya siri peke yao kwa mda mrefu walipokuwa kwenye mkutano wa G-20!! Hii yote ni katika kujaribu kuanganisha vipisi vya Russian collusion conspiracy, kama kawaida baadhi ya wenzetu humu huwa wanakubali tu kwa sababu hawaamini kuwa media za US zinaweza ku-ripoti 'fake news'.

Hivi Trump yupo dinner walioalikwa na Chancellor Angela Merkel na ndiye aliyepanga hata namna watakavyokaa halafu wanamtaka asizungumze na Putin kwa sababu za 'conspiracy' zao? Wanasema wamekutana kisiri wakati viongozi wote wa G-20 na wake zao walikuwepo hapo, mara wameongea masaa wakati Trump amesema waliongea kama robo saa. Hizi 'fake news' balaa!.

Hata video ya CNN ilivyo-leak, ikibainisha kuwa 'russian collusion' story ni kwa ajili ya ratings, baadhi ya wenzetu humu wameendelea kushikilia misimamo yao.

Sasa sisi wote tunasubiri 'impeachment' ya Trump kwa sababu ya 'Russian collusion' iliyokuwa inasogea na sasa 'imetua' rasmi White House.

Labda Trump bado 'anajitundika kitanzi mwenyewe drip drip' maana wenzetu humu wametuambia kuwa 'ugomvi wake' na media na Intelligence Community mwisho wake ni 'impeachment' na kwamba ni suala la muda tu.

'Russian collusion' isipozungumziwa kwenye media hata kwa siku moja tu, hawa wenzetu humu huwa wanatuhabarisha sababu. Kila siku humu tunahubiriwa Russia, Russia, Russia!. Nitashangaa sana kama hawa wenzetu leo hii hawasubirii 'impeachment' ya Rais Trump itakayosababishwa na 'Russian collusion'!!!!

Nafurahi tu jinsi hiyo greatest political witch hunt inavyoendelezwa na Liberals. Wanatafuta vitu ambavyo havipo, wana-force dots zao zilete maana lakini wapi!! Wafuasi wao wengi washaanza kukata tamaa ila kuna wachache bado wanaamini hizo phony story za Russia!!
 
Asante mkuu Tujitegemee,

Kusubiria 'impeachment' ya Trump kutokana na 'Russia collusion' ni sawa na kwenda mbugani kusubiri kumuona Tembo Mweupe...

...'Russian collusion' isipozungumziwa kwenye media hata kwa siku moja tu, hawa wenzetu humu huwa wanatuhabarisha sababu. Kila siku humu tunahubiriwa Russia, Russia, Russia!. Nitashangaa sana kama hawa wenzetu leo hii hawasubirii 'impeachment' ya Rais Trump itakayosababishwa na 'Russian collusion'!!!!

Nafurahi tu jinsi hiyo greatest political witch hunt inavyoendelezwa na Liberals. Wanatafuta vitu ambavyo havipo, wana-force dots zao zilete maana lakini wapi!! Wafuasi wao wengi washaanza kukata tamaa ila kuna wachache bado wanaamini hizo phony story za Russia!!
Kama kuna kitu kimoja tumesisitiza ni kwamba mambo ya Marekani hayaendi kwa kukurupuka na mpaka sasa hakuna anayejua kwa undani ushahidi uliopatikana mpaka siku special counsel atakapotoa ripoti.

Tayari Trump ana wasi wasi mpaka na watu aliowateua yeye mwenyewe kuanzia kwa Mwanasheria Mkuu, msaidizi wake, wakuu wa inteligensia na hata special counsel aliyeteuliwa na DOJ.

Yawezekana wengine wenu hamkufuatilia yaliyomkuta Richard Nixon ambaye alikuwa na kiburi labda zaidi ya Trump! FYI Uchunguzi ulichukua zaidi miaka miwili sembuse hii miezi mitatu ya special counsel!

El Jefe, mpaka sasa ni Trump anayeongoza kwa fake news ambayo msemaji wake aliibatiza alternative facts; naona na wewe umetumia neno witch hunt...incidence or coincidence, believe me!
 
"Mag3, post: 22379387, member: 10873"]Kama kuna kitu kimoja tumesisitiza ni kwamba mambo ya Marekani hayaendi kwa kukurupuka na mpaka sasa hakuna anayejua kwa undani ushahidi uliopatikana mpaka siku special counsel atakapotoa ripoti.
Kuna watu wanatafiti kifo cha Martin Luther na JF Kennedy hadi sasa. Marekani jambo halipiti kienyeji enyeji kama sisi ambapo leo ukiuliza nini kilimtokea Mwanasheria Sengondo Mvungi hakuna jibu. Marekani itachimbua na kuna siku itajulikana nini kilitokea au hakikutokea

Tayari Trump ana wasi wasi mpaka na watu aliowateua yeye mwenyewe kuanzia kwa Mwanasheria Mkuu, msaidizi wake, wakuu wa inteligensia na hata special counsel aliyeteuliwa na DOJ.
AG Sessions ni Seneta wa kwanza kumuunga mkono Trump.
Sessions alifanya kile kinachotarajiwa, kwamba kwavile kuna 'tuhuma' hataweza kusimamia haki kwani hana public trust. Ndiyo maana akaji recuse

Rais Trump bila kujua kauli ina ramifications gani kwa WH na yeye binafsi katika wingu lililotanda kasema wazi 'angalijua AG ata recuse' asingemchagua. Anachoeleza umma AG yupo kwa ajili yake na si nchi. Kutawala nchi si sawa na kuendesha Trump Organization!

Yawezekana wengine wenu hamkufuatilia yaliyomkuta Richard Nixon ambaye alikuwa na kiburi labda zaidi ya Trump! FYI Uchunguzi ulichukua zaidi miaka miwili sembuse hii miezi mitatu ya special counsel!
Kuna kitu kinaitwa Saturday massacre kilichotokea October 20 1973, wengi walikuwa pengine hawajazaliwa.
Wenye kutaka ufahamu google
Trump anayeongoza kwa fake news ambayo msemaji wake aliibatiza alternative facts; naona na wewe umetumia neno witch hunt...incidence or coincidence, believe me!
Jana kasema amekutana na Putin kwa dakika 15 wakati wachunguzi wakiwemo watu wa WH wanasema ni saa moja. Fake news?
Illegal immigrants milioni 5 wame vote isivyo halali. Fake news
Obama ame tape Trump Tower. Fake news
Hakuna mtu wa kampeni yake aliyewahi kuwasiliana na Russia. Fake news
Atawaadabisha wa Iran. Sasa anathibitisha vikwazo vya Obama. Fake news

Orodha inaendelea......

Jambo moja watu wanataka umma uamini, media za US ni fake except Fox.
Well, kila mara zime prove habari kiasi kwamba sasa hivi haamini mtu yoyote ndani ya WH
 
Kama kuna kitu kimoja tumesisitiza ni kwamba mambo ya Marekani hayaendi kwa kukurupuka na mpaka sasa hakuna anayejua kwa undani ushahidi uliopatikana mpaka siku special counsel atakapotoa ripoti.

Tayari Trump ana wasi wasi mpaka na watu aliowateua yeye mwenyewe kuanzia kwa Mwanasheria Mkuu, msaidizi wake, wakuu wa inteligensia na hata special counsel aliyeteuliwa na DOJ.

Yawezekana wengine wenu hamkufuatilia yaliyomkuta Richard Nixon ambaye alikuwa na kiburi labda zaidi ya Trump! FYI Uchunguzi ulichukua zaidi miaka miwili sembuse hii miezi mitatu ya special counsel!

El Jefe, mpaka sasa ni Trump anayeongoza kwa fake news ambayo msemaji wake aliibatiza alternative facts; naona na wewe umetumia neno witch hunt...incidence or coincidence, believe me!
Unavyotoa mifano ya uchunguzi naona unajipa matumaini kama liberals wengine kwa uchunguzi wa Watergate uliomuondoa Richard Nixon! mbona kuna chunguzi kadhaa zilizotoka hola bila kumuondoa Rais? Hivi vitu haviendi kwa hisia kuwa liberals wengi wangependa Trump awe impeached, bali ni FACTS ambazo ni 'beyond reasonable doubt'.

Special counsel hawezi ku-present 'conspiracy theory' inayoungwa ungwa kila kukicha na media zilizowekeza nguvu zao kwa ajili ya ratings. Wakiona chochote chenye alama au uhusiano na Russia wanaona kama ni crime ! Ndio yaleyale ya Trump kuzungumza na Putin ni ku-commit 'treason'.

Walioanza kuwa na concerns na special counsel ni wengine wala sio Trump hasa baada watu kujua kuwa uhuru wake utaathiriwa na urafiki wake na Comey, that's just common sense.

Naku-challenge uandike list za fake news tatu (3) zilizoripotiwa na media dhidi ya Trump au serikali yake, ukiweza kila mtu atajua huna ushabiki kwenye huu uzi, ukishindwa basi jua huwezi constructive discussions zaidi ya kuendekeza ushabiki. Kama hamna sema hamna ili niku-challenge na list ya fake news.
 
...Naku-challenge uandike list za fake news tatu (3) zilizoripotiwa na media dhidi ya Trump au serikali yake, ukiweza kila mtu atajua huna ushabiki kwenye huu uzi, ukishindwa basi jua huwezi constructive discussions zaidi ya kuendekeza ushabiki. Kama hamna sema hamna ili niku-challenge na list ya fake news.
Kwa kuanzia tu nakupa alternative facts za Donald Trump katika miezi mitatu tu toka aapishwe January 20, 2017. Ingawa umetaka tatu tu mimi nakupa 56. Uongo wake kwa kipindi chote ambao ni maradufu utahitaji labda kitabu kizima...


1. Jan. 21 “I wasn't a fan of Iraq. I didn't want to go into Iraq.”

2. Jan. 21 “A reporter for Time magazine — and I have been on their cover 14 or 15 times. I think we have the all-time record in the history of Time magazine.”

3. Jan. 23 “Between 3 million and 5 million illegal votes caused me to lose the popular vote.”

4. Jan. 25 “Now, the audience was the biggest ever. But this crowd was massive. Look how far back it goes. This crowd was massive

5. Jan. 25 “Take a look at the Pew reports (which show voter fraud.)”

6. Jan. 25 “You had millions of people that now aren't insured anymore

7. Jan. 25 “So, look, when President Obama was there two weeks ago making a speech, very nice speech. Two people were shot and killed during his speech. You can't have that.”

8. Jan. 26 “We've taken in tens of thousands of people. We know nothing about them. They can say they vet them. They didn't vet them. They have no papers. How can you vet somebody when you don't know anything about them and you have no papers? How do you vet them? You can't.”

9. Jan. 26 “I cut off hundreds of millions of dollars off one particular plane, hundreds of millions of dollars in a short period of time. It wasn't like I spent, like, weeks, hours, less than hours, and many, many hundreds of millions of dollars. And the plane's going to be better.”

10. Jan. 28 “The coverage about me in the @nytimes and the @washingtonpost has been so false and angry that the Times actually apologized to its dwindling subscribers and readers.”

11. Jan. 29 “The Cuban-Americans, I got 84 percent of that vote.”

12. Jan. 30 “Only 109 people out of 325,000 were detained and held for questioning. Big problems at airports were caused by Delta computer outage.”

13. Feb. 3 “Professional anarchists, thugs and paid protesters are proving the point of the millions of people who voted to MAKE AMERICA GREAT AGAIN!”

14. Feb. 4 “After being forced to apologize for its bad and inaccurate coverage of me after winning the election, the FAKE NEWS @nytimes is still lost!”

15. Feb. 5 “We had 109 people out of hundreds of thousands of travelers and all we did was vet those people very, very carefully.”

16. Feb. 6 “I have already saved more than $700 million when I got involved in the negotiation on the F-35.”

17. Feb. 6 “It's gotten to a point where it is not even being reported. And in many cases, the very, very dishonest press doesn't want to report it.”

18. Feb. 6 “The failing @nytimes was forced to apologize to its subscribers for the poor reporting it did on my election win. Now they are worse!”

19. Feb. 6 “And the previous administration allowed it to happen because we shouldn't have been in Iraq, but we shouldn't have gotten out the way we got out. It created a vacuum, ISIS was formed.”

20. Feb. 7 “And yet the murder rate in our country is the highest it’s been in 47 years, right? Did you know that? Forty-seven years.”

21. Feb. 7 “I saved more than $600 million. I got involved in negotiation on a fighter jet, the F-35.”

22. Feb. 9 “Chris Cuomo, in his interview with Sen. Blumenthal, never asked him about his long-term lie about his brave ‘service’ in Vietnam. FAKE NEWS!”

23. Feb. 9 “Sen. Richard Blumenthal now misrepresents what Judge Gorsuch told him?”

24. Feb. 10 “I don’t know about it. I haven’t seen it. What report is that?”

25. Feb. 12 “Just leaving Florida. Big crowds of enthusiastic supporters lining the road that the FAKE NEWS media refuses to mention. Very dishonest!”

26. Feb. 16 “We got 306 because people came out and voted like they've never seen before so that's the way it goes. I guess it was the biggest Electoral College win since Ronald Reagan.”

27. Feb. 16 “That’s the other thing that was wrong with the travel ban. You had Delta with a massive problem with their computer system at the airports.”

28. Feb. 16 “Walmart announced it will create 10,000 jobs in the United States just this year because of our various plans and initiatives.”

29. Feb. 16 “When WikiLeaks, which I had nothing to do with, comes out and happens to give, they’re not giving classified information.”

30. Feb. 16 “We had a very smooth rollout of the travel ban. But we had a bad court. Got a bad decision.”

31. Feb. 16 “They’re giving stuff — what was said at an office about Hillary cheating on the debates. Which, by the way, nobody mentions. Nobody mentions that Hillary received the questions to the debates.”

32. Feb. 18 “And there was no way to vet those people. There was no documentation. There was no nothing.”

33. Feb. 18 “You look at what's happening in Germany, you look at what's happening last night in Sweden. Sweden, who would believe this?”

34. Feb. 24 “By the way, you folks are in here — this place is packed, there are lines that go back six blocks.”

35. Feb. 24 “ICE came and endorsed me.”

36. Feb. 24 “Obamacare covers very few people — and remember, deduct from the number all of the people that had great health care that they loved that was taken away from them — it was taken away from them.”

37. Feb. 27 “Since Obamacare went into effect, nearly half of the insurers are stopped and have stopped from participating in the Obamacare exchanges.”

38. Feb. 27 “On one plane, on a small order of one plane, I saved $725 million. And I would say I devoted about, if I added it up, all those calls, probably about an hour. So I think that might be my highest and best use.”

39. Feb. 28 “And now, based on our very strong and frank discussions, they are beginning to do just that.”

40. Feb. 28 “The E.P.A.’s regulators were putting people out of jobs by the hundreds of thousands.”

41. Feb. 28 “We have begun to drain the swamp of government corruption by imposing a five-year ban on lobbying by executive branch officials.”

42. March 3 “It is so pathetic that the Dems have still not approved my full Cabinet.”

43. March 4 “Terrible! Just found out that Obama had my ‘wires tapped’ in Trump Tower just before the victory. Nothing found. This is McCarthyism!”

44. March 4 “How low has President Obama gone to tap my phones during the very sacred election process. This is Nixon/Watergate. Bad (or sick) guy!”

45. March 7 “122 vicious prisoners, released by the Obama Administration from Gitmo, have returned to the battlefield. Just another terrible decision!”

46. March 13 “I saved a lot of money on those jets, didn't I? Did I do a good job? More than $725 million on them.”

47. March 13 “First of all, it covers very few people.”

48. March 15 “On the airplanes, I saved $725 million. Probably took me a half an hour if you added up all of the times.”

49. March 17 “I was in Tennessee — I was just telling the folks — and half of the state has no insurance company, and the other half is going to lose the insurance company.”

50. March 20 “With just one negotiation on one set of airplanes, I saved the taxpayers of our country over $700 million.”

51. March 21 “To save taxpayer dollars, I’ve already begun negotiating better contracts for the federal government — saving over $700 million on just one set of airplanes of which there are many sets.”

52. March 22 “I make the statement, everyone goes crazy. The next day they have a massive riot, and death, and problems.”

53. March 22 “NATO, obsolete, because it doesn’t cover terrorism. They fixed that.”

54. March 22 “Well, now, if you take a look at the votes, when I say that, I mean mostly they register wrong — in other words, for the votes, they register incorrectly and/or illegally. And they then vote. You have tremendous numbers of people.”

55. March 29 “Remember when the failing @nytimes apologized to its subscribers, right after the election, because their coverage was so wrong. Now worse!”

56. March 31 “We have a lot of plants going up now in Michigan that were never going to be there if I — if I didn’t win this election, those plants would never even think about going back. They were gone.”

Kuanzia mwezi wa April uongo wa Trump uliongezeka mara mbili, kila siku alisema uongo na hakuna hata siku moja aliweza kupata ujasiri wa kuomba radhi. Kwa mfano alidai hakuna mtu yeyote kwenye timu yake ya kampeni aliwahi kuwa na mazungumzo na Warusi na sasa tunakuta hata mtoto wake na mkwe wake wanahusika. Hata Mkuu wake wa Kampeni na makamu wake Pence naye andai hivyo hivyo na watu bado wamemnyamazia tu wakimsoma.
 
Mag3 Nasubiri ujibiwe maana baadhi yetu dah ! Pengine yupo atakayesema hiyo list ni fake! teh teh
 
Back
Top Bottom