Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Uchunguzi kwa sasa umejikita zaidi katika mambo matatu yanayomhusu Donald Trump...
  1. Collusion with Russia
  2. Obstruction of Justice
  3. Financial dealings (crimes)
Hapa ndipo wenzetu wanatuzidi katika uzalendo na kuangalia nchi yao

Swali la kwanza lilikuwa, je, kulikuwa na meddling katika uchaguzi?
Jibu likawa ndiyo kwa mujibu wa Intel community na Congress kukubaliana na analysis ya IC

Swali la pili, je, meddling iliathiri uchaguzi wa 2016
Jibu: Hakuna kura iliyoathirika kutokana na meddling. Kulikuwa na majaribio katika state 21 lakini hazikufanikiwa wala kubadili matokeo. Kulikuwa na misleading info kutoka Russia

Swali la tatu, je, misleading info ziliathiri upigaji kura au mtazamo wa wapiga kura
Jibu: Hakuna ushahidi so far na utafiti unaendelea

Swali la nne, je, meddling ilifanywa kwa majaribio au ilikusudiwa?
Jibu: Ililenga katika 'kumtaka' mtu mmoja kwa gharama ya mwingine

Swali la tano, je,meddling ilifanywa na Russia pekee au kulikuwa na watu wa ndani?
Jibu: Kuna watu wa ndani ya kampeni ya Trump walikuwa na contact na Russia

Kuwa na contact pekee si kosa, kuna contact za kibiashara na deal nyingine halali

Swali la sita, je, contact hizo zilihusiana na uchaguzi kama usaidizi? (Collusion)
Jibu: Uchunguzi unaendelea wa Mueller na kamati za seneti na House

Swali la saba, je, kuhusu contact(swali la tano) kulikuwa na financial deal za kawaida au kulikuwa na financial deals zenye uhusiano na mambo ya election au quid pro quo?
Jibu: Uchunguzi unaendelea kubaini hayo

Swali la nane, je, habari zinazopatikana katika media zina ukweli na kama upo au hakuna kwanini watuhumiwa wanaficha habari au wanatoa habari za kupotosha?

Jibu: Uchunguzi unaendelea ili kubaini kama kuna obstruction of justice imefanyika na kwanini au kama hakuna kitu kama hicho
 
Mkuu vikwazo vile si kwa meddli.
ya uchaguzi, ni issue za deep state na biashara zao. Wanata kuchukua biashara ya Russia ya gesi anayowauzia EU. Huo ndiyo ukweli. Ebu fikiria, Kama kweli lengo ni kumuadhibu Russia kwa nini hajamuwekea vikwazo kwa mambo ambayo wanashirikiana kwa karibu sana yaani space stations! Deep state wanataka ku-weaken kampuni za EU za nishati ambazo zinashiriki katika ujenzi wa bomba la gesi linaloikwepa Ukraine. Deep state wanajua kabisa Russia hawezi kuyumbishwa na vikwazo vyao na ushahidi wanao sasa inakuwaje waiadhibu kupitia maslahi ya EU. EU nao wamestuka wanasema wazi kuwa wata'retaliate' vikwazovinavyowadhoofisha dhidi ya US .

Russia wanasema hii ni trade war tena more or less Cold war 2.0 wanasema hawawezi tena kuendelea kulea bullying ya Deep State na wamegundua DT ni dhaifu. Wameongeza kusema kuwa wana tools kibao za kuwashugulikia US kwenye toolbox yao ya kujibu mapigo.
Kumbuka meddling inaungwa mkono na Republicans na Democrats ndiyo maana senate ikapitisha 98-2, House 419-3 suala la vikwazo kwa Russia.
Kremlin agrees with Trump that Russia-US ties at ‘very dangerous low’
 
Hapana, unakosea, ilipita bila kupingwa ndiyo lakini haikupigiwa kura. The original vote was passed by a voice vote not requiring individual lawmakers to record their positions.
Obama alitaka a recorded vote of the positions of all lawmakers...kura ipigwe na kuhesabiwa ili kuweka rekodi sahihi kwa sababu alijua hiyo ya asilimia 100% haikuwa sahihi na kweli iliporudishwa ilipitishwa na Congress kwa asilimia 79% tu.

Kwani voice vote sio namna ya kupiga kura? Voice vote inatumika pale ambapo hamna controversial issues baina ya members au kupitisha routine bills. Kitendo cha Congress kutumia voice vote ni wazi hakukuwa na 'controversial issues' kwenye JASTA. Aliyekuwa na issue ni Obama pekee.

Lakini pia member(s) anaweza kuomba division of assembly/rising vote asipokubaliana na matokeo ya voice vote, hilo halikutokea kwenye JASTA. Which means hiyo asilimia 100% ilikuwa sahihi. Pia voice vote sometimes inarekodiwa.

Rais Obama ali-veto bill iliyopitishwa unanimously. Ila the main fact hapa ni kuwa hakuipenda JASTA na wala hakui-sain kuwa sheria, bali Congress ndio wali-override veto yake.

Historia inaonyesha kuwa mara nyingi Rais aki-veto bill fulani kutoka Congress, anafanikiwa kubadili maoni ya some Congress members. Ndio maana baada ya veto, aliweza kumbadilisha Senator mmoja tu na representatives 77.

Huko kutaka ku-record position ni attemp tu aliyoifanya ili kujaribu kubadilisha mawazo ya members of Congress ili kura isifike 2/3, but he failed because the vote was well ahead of 2/3.

Unadhani kuna POTUS anapenda akisha-veto legislation ikarudi Congress only to be passed into law by 2/3?. He was fighting for his position on the bill, against more than 2/3 of Congress of course and it was not 79%.
 
Ina maana uliandika kitu ambacho hukijui au unachokihisi. Kwanini wewe kwa upande wako hukuwa na 'subira kidogo' kabla ya kuandika vitu ambavyo huna uhakika navyo?




Ni mkutano baina ya Don Jr. et al. na 'meneja wa benki serikali ya Urusi' au na 'Mwanasheria aliyehusishwa na Russia'?




Grand jury imeitishwa kufumua suala la 'benki ya serikali ya Russia' na Trump?

Kitendo cha Mueller kuitisha grand jury ni kumpa uwezo wa kupata ushahidi wowote anaoutaka na kuwaonyesha grand jury ili waamue kama wanaochunguzwa wawe indicted au lah.

Sasa wewe umejuaje ushahidi ambao special counsel atau-subpoena wakati hajafanya hivyo? Au ndio muendelezo wa kuhisi?



Kwa maoni yako, kuchunguza tax return za Trump za miaka 10 iliyopita (kabla Obama hajawa Rais) ni reasonable scope inayoendana na 'Russia collusion' story?

Uchunguzi lazima uwe na scope ambayo ni reasonable kulingana na facts of the case. Maana tax returns za Trump zinaweza kuchunguzwa hata za miaka 40 iliyopita, lakini hiyo, kama siyo kupoteza mda, itasaidia vipi kujibu swali la msingi?


Special counsel kuitisha grand jury ni sehemu ya process, inayoashiria uchunguzi unaelekea mwishoni.

Kwanza inampa special counsel uwezo wa kutoa subpoena ya ushahidi (watu kuja kutoa ushahidi+documents) kama hajapata ushahidi wote lakini pia kwa wao kuamua kama kuna wrongdoing ambayo inayoweza kupelekea kuwa charged.

Badala ya kuhisihisi kama Mueller amepata documents fulani au hajapata, na kuendekeza kuwa ahead of investigations zinazoendelea, kwanini usi-deal na kile ulicho na uhakika nacho kwanza?

Time will tell. Report suggests potentially alarming development in Jared Kushner's meeting with the head of a sanctioned Russian bank
 
Hebu tuchukue time out kidogo tumsikilize Bill Maher...je hali ingekuwaje kama matendo na kauli za Trump zingetolewa na Obama?



What would have been the reaction of Trump supporters if Obama had said it!​
 
Mag3 hiyo ya Bill imechekesha sana. Najaribu kufikiri mara ngapi alisema Obama ana play golf. Well kwa kipindi kama chake amekwenda vacation ku play golf mara mbili ya Obama
Alisema akichaguliwa hataondoka WH, kwasasa anaondoka kuliko waliomtangulia

Akasema golf inatumika ku make deals, well, hakuna deal yoyote so far
Kuna chuki binafsi siyo ya sera kati yake na OB na amefanikiwa kuteka watu wengi

Rais Trump anatoka katika business na ni real professional salesman.
Anaweza kukuazima shati na kisha kukuuzia na ukalinunua kwa bei ya juu.

Watu wanasema uchumi umeongeza 209K jobs.
Takwimu za BLS zinaonyesha July 2016 kulikuwa na 255K! June 2016 ilikuwa 287

DOJ Jan 21 2016 ilikuwa 7,749 below 8K ambayo ni lowest kwa Rais yoyote aliyeahi kuingia madarakani tangu kuanzishwa kwake. Jan 21 2017 DOJ ilikuwa 20K

Wengine wanadhani DOJ ni indicator pekee ya uchumi.
Ukiacha ukweli hakuna anayeongelea S&P au NASDAQ, hizo ni sehemu tu ya indicator

Sasa mtu anaposema DOJ imefikia 22K, ni lazima ajiulize ilianzia wapi.

DOJ haijawahi kufikia 27K, sasa Rais atakayeingia madarakani ikiwa 26K halafu ikafika 27 akasema ni historical , wasiojua masikini wanashangalia!

Ukiachilia hilo, Obama akiingia kulikuwa na vita na recession. Kazi ya kwanza ilikuwa ku bail out taasisi na makampuni yaliyokuwa katika ''verge of collapse''. Trump hakukuta hayo!

Tukirudi katika media, Trump anasema kuna fake news.
Wakati huo huo WH ipo katika 'kesi' ya kushirikiana na Fox kutengeneza fake news

Orodha ni ndefu sana na inaendelea
 
Je, mnafuatilia yanayojiri Marekani kwa sasa? Naona huko Donald Trump kaliamsha dude, drip drip imekuwa flow na mambo yamekuwa mambo. Wimbo ulioshika kasi kwa sasa unasema; "keep up the good work Donald ... continue, doing whatever it is...digging your own grave.
 
Je, mnafuatilia yanayojiri Marekani kwa sasa? Naona huko Donald Trump kaliamsha dude, drip drip imekuwa flow na mambo yamekuwa mambo. Wimbo ulioshika kasi kwa sasa unasema; Let Trump continue to do whatever he is doing for he is doing quite a good job of it...digging his own grave.
Mkuu tujnafuatilia sana tu. Tutakuwa na mfululizo wa mjadiliano kuanzia kesho tukijadili mambo kadhaa yanayotokea katika duru za siasa za US

Rais Trump na sakata la Virginia
Trump na siasa za dunia, North Korea, Venezuela n.k.
 
Mkuu tujnafuatilia sana tu. Tutakuwa na mfululizo wa mjadiliano kuanzia kesho tukijadili mambo kadhaa yanayotokea katika duru za siasa za US

Rais Trump na sakata la Virginia
Trump na siasa za dunia, North Korea, Venezuela n.k.
Poor Trump, could this be the beginning of the end?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimeshasoma maandiko ya watu kadhaa wanaomfahamu Trump kuwa huwa hapendi kuonekana ameshindwa wakisema kuwa kwa vile utawala unamshinda, ataachia ngazi haraka sana kwa majigambo kusudi asitumbuliwe na watu wengine. Kama ambavyo alivyo-preempt kuvunjika kwa mabaraza ya ma-CEOs wake akijifanya ameamua kuyavunja huku ikiwa ni baada ya kuona walivyokuwa wanatimka, na alivyofanya ku-preempt rais wa Mexico kukataa kuhudhuria mkutano wa kufahamiana uliokuwa umepangwa mwanzoni mwa utawala wa Trump akisema amefuta mkutano huo; kuna kila dalili kuwa Trump ata-preempt tukio moja kubwa kwa kusema amejiuzulu White House kusudi afuatilie biashara zake binasfi kwa sababu congress na senate "are fools and stupid" na yeye "is very rich" hanufaiki chochote na kuwepo White House ila alikuwa anatoa services tu. Kwa taarifa tu, kuna mashirika mengi sana yamejiondoa kwenye uhusiano na biashara za Trump, hasa Mar-a-Lago Club!
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US

MSUKO SUKO WH, KUSHINDWA MAADILI, NA VURUGU KIUTAWALA

Wiki mbili hazikuwa nzuri na pengine mbaya zaidi katika miezi 7 ya utawala wa Rais Trump
Ni wiki iliyogubikwa na matukio mawili makubwa, mzozo na North Korea na vurugu za Charllotesville VA

NORTH KOREA
Mzozo upo muda mrefu, US na washirika wakiitaka NKorea kusitisha majaribio ya silaha za Nuclear
Rais Trump alisema ufumbuzi wa suala hilo upo mikononi mwa China hasa kuhusu vikwazo vya kiuchumi

Ni kweli tawala zote za US zilizopita ziliitumia China kushinikiza Nkorea kama mshirika mkubwa wa biashara

Tofauti na watangulizi, Rais Trump kwa kutojua siasa za Kimataifa alianza kwa kuitisha China kwa mambo mawili
1. Kwamba, ataibana China kiuchumi ili isaidie jitihada za kuiba Nkorea akiita Currency manipulator
2. Alikubali kuingilia mzozo wa China na Taiwan akionekana kubeza sera za china za One China

Kama mtakumbuka, mabandiko ya nyuma akiingia WH tulisema mzozo wa Nkorea una masilahi mapana kwa China, Russia na Iran. Ni mzozo unaohitaji uangalifu kwani mchezaji ni mmoja akiwa na timu nyuma yake

Ni mzozo mpana ukihusisha Skorea na Japan ambazo ni majirani wa Nkorea na waathirika wa kwanza wa vita
China haikuwa na haraka za kumjibu Rais Trump ikijua inashika karata muhimu sana Korean Peninsula

Muda haukupita Rais Trump akabaini ukweli na kufuta kauli ya China kama currency manipulator ili aweze kupata msaada wa kuibana Nkorea. Hili likawa ushindi wa kwanza kwa China licha ya kutishiwa kibiashara na US

Hofu ya China kwa mzozo wa Korean Peninsula ni jinsi US inavyojisogeza karibu na China kwa kuwa karibu na SKorea na Japan. Kwamba kuanguka kwa Nkorea si kuwa ni tatizo la Wakimbizi bali US kuwa mlangoni

Nkorea inafanya majaribio ya silaha za masafa ya mabara ICBM yanayoweza kufika US kwa jeuri

Kwamba Seoul chini ya KM 100 kutoka mpakani na Nkorea ni eneo la kufikika kirahisi
Ukweli kuwa makombora yanaweza kufika US unaeleza hatari inayoikabili Japan

Tishio la Rais Trump kwa tweet kuhusu Nkorea limepokelewa kwa hisia kubwa .
UN ilipitisha azimio kukaza vikwazo ambazo ni juhudi za Balozi Niki Hailey na Sec Tillerson

Hakukuwa na ulazima wa kuanza vitisho kwa kupitia tweets na mikutano na waandishi jambo lisilo la kawaida
Wanadiplomasia na Pentagon wanasema kwa uhakika suluhisho la kijeshi ni hatua ngumu na ya mwisho

Wakati huo huo Rais Trump akaeleza uwezekano wa kuingia kijeshi kwa mzozo wa Venezuela
Hili nalo lilishtua makao makuu ya jeshi Pentagon kwani hawakuwa na habari za mpango huo

Kukiwa na vita Afghanistan, Iraq na Syria ambako majeshi ya US yanashiriki, na mzozo wa Nkorea kisha kuongeza Venezuela, wataalam wa kijeshi wanasema hiyo ita 'stretch' jeshi kupita kiasi

Hoja inayojitokeza hapa ni moja, Rais Trump katika kampeni aliahidi kutokuwa Rais wa dunia na kwamba ni America first kwa kutumia rasilimali zake badala ya kulinda washirika. Sera hiyo imeishia wapi?

Kilichoonekana ni kutojua siasa za nje na kimataifa na matumizi mabovu ya diplomasia ya tweets
Vita na Nkorea ni vita ya Korean Peninsuala hadi south China. Ni mzozo mkubwa kuliko anavyodhani

Hayo yakiendelea, kukazuka mzozo katika state ya Virginia, mji wa Charllotesville, tutakaoujadili bandiko lijalo

Inaendelea...
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US

MSUKO SUKO WH, KUSHINDWA MAADILI, NA VURUGU KIUTAWALA (II)

Charlottesville, Viriginia

Mzozo ulianza na watu wawili mweupe mmoja aliyevaa kitambaa cha bendera ya confederate na mweusi aliyekemea jambo hilo akisema kwa kuitazama historia aliyevaa kitambaa hicho 'bandana' hakujua chochote

Hilo likaonekana kukuzwa kwa kualikwa kwa makundi ya weupe mrengo wa kulia mwishi alt-right katika mkusanyiko wa kulinda alama za confederate. Mkusanyiko ulioleta White supremacist(KKK) na Neo-Nazi

Kwa upande mwingine kukawepo mkusanyiko uliopinga uwepo wa makundi hayo ikikumbusha historia chungu
KKK walitumia alama ya confederate na hawa walijulikana sana na mateso hasa dhidi ya weusi

Suala zima lina mtazamo wa makovu ya kihitoria ya miaka takribani 200 iliyopita na ilionekana kama ni kutonesha vidonda. Makundi ya KKK, Nationalist na Neo-Nazi yalikuwa yanajificha, katika zama hizi yapo wazi kabisa

KKK, Neo-Nazi (alt-right) kwa neno la ujumla yaliaandaa mkusanyiko yakiimba nyimbo za kulaani Jews(Wayahudi) yakisema ''hawatakuwa mbadala wao'', blood and soil ya Nazi na white live matters.

Kwa ufupi sera za alt-right zinahusu mambo matatu, kwanza uhamiaji , pili mambo ya abortion na Rangi

Katika kupinga alt-right maandamano yalileta tukio baya. Kijana mmoja aliendesha gari na kugonga watu akiua mwanadada mmoja Heather Hayer na kujeruhi makumi ya waandamanaji. Hapo ndipo mzozo ukaingia WH

Rais Trump akalazimika kutoa kauli akisema mzozo umesababishwa na pande mbili, za alt-right na wanaopinga
Kauli hiyo ya tarehe 12 august ilizua mzozo katika vyombo vya habari, wengi wakihoji 'moral equvalency'

Kwamba alt-right walikuwa wanafanya tendo la kutukuza ubaguzi, na kundi lingine kipinga. Kimaadili makundi hayo yanawezaje kuwekwa katika mizani!! Joto likawa kubwa likimtaka Rais akemee makundi hayo kwa kuyataja

Jumatatu iliyofuata akatoa taarifa iliyoandaliwa na kuisoma ikilaani KKK, White supremacists na Nationalist kwa tendo lao la kibaguzi linalorudisha jitihada za kuunganisha Wamarekani, kufuta tofauti na kutotonesha historia

Kama ilivyotegemewa, J'nne Rais Trump akiongea na waandishi alikwenda kinyume na kauli ya J'tatu akionekana wazi kutetea alt-right kwa kulinganisha na makundi mengine. Alirudia tena siku zilizofuata

Hakika mzozo ukapamba moto watu wakihoji maadili ya kiroho ya Rais wao (moral authority) na kwamba badala ya kuliunganisha Taifa, Trump aliligawa zaidi katika hisia za kibaguzi za rangi

Hisia za watu juu ya msimamo wa Rais wao zilijengwa na historia ya Trump ya kushtakiwa kwa ubaguzi, kampeni alizofanya zilizokuwa na mwelekeo wa kibaguzi na timu yake ya WH yenye viongozi wa alt-right kama Bainnon wa Breitbart, Stephen Miller na Gorka ambao ni washauri wa WH wakijulikana wazi ni 'white supremacists'

Pressure yaongezeka, makundi yamlaani Rais wao

Inaendeleaa...
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US

MSUKO SUKO WH, KUSHINDWA MAADILI, NA VURUGU KIUTAWALA (III)

Charlottesville, Viriginia

Msuko suko wa suala la Virginia ulipelekea makundi kuandamana katika makazi ya Rais Trump , Trump Tower
Waandamanaji walimtaka alaani makundi ya alt-right yaliyosababisha kifo kwa kuyataja
Hilo likamkera Rais Trump na kuendelea na msimamo wake ulioonekana kuligawa Taifa zaidi

Shinikizo la kwanza la kulaani na kutaja makundi hayo lilitoka kwa Republicans ambao kwa muda mrefu wamehusishwa kisiri siri na agenda za white supremacists. Walichotaka ni Rais Trump kuyakana makundi hayo

Hayo yakiendelea viongozi wa KKK waliendelea kumsifia Rais Trump kwa msimamo juu yao na kuchagiza moto

Maseneta na Representative wa Republicans walimlaani Trump huku Trump akijibu mapigo kwa kila mmoja wao
Hadi tunaandika,maseneta 23 wa Republicans wamemtaja Trump kwa kukosa maadili mbali na Democrats

Makundi yha kijaamii nayo yameingila kati, makmpuni yakijitenga na kauli za Trump na taasisi za kiraia pia
Baraza la ushauri la CEO's wa makampuni makubwa lilianza kujiuzulu kama bandiko #473- Kichuguu

Kisha baraza la ushauri la sanaa na utu (arts and Humanities) huku taasisi zikivunja mikataba ya mikutano katika jumba la Mar-a-lago linalomilikiwa na Trump organization

Orodha ya watu wanaojitoa inaongezeka kila muda na baraza la kiinjilisti nalo limevunjika

Kubwa kuliko yote ni kauli mahususi iliyotolewa na joint chiefs of staff wa majeshi ya US kuhusiana na kauli ya amiri jeshi wao. Makamanda walisema jeshi halibagui na sera zake ni za ushirikishaji watu bila ubaguzi

VP pence na SoS pamoja na viongozi wengine kwa pamoja wanamtenga Rais Trump na kauli zake

NJIA PANDA
Rais Trump yupo njia panda, kwamba alaani alt-right kwa dhati apoteze ushawishi wa makundi husika, au abaki na msimamo wake apate msaada wa alt'right. Ikumbukwe alt-right ni political base ya Rais Trump

Alt right wamesimama na Trump kwa nyakati zote wakionekana 'kuvutiwa' na sera zake katika immigration, kpinga Homosexuality. Ukweli ni kuwa makundi hayo yalikuwa na agenda ya kuingiza mtu wao WH kwa kutumia kauli ya 'tuchukue nchi yetu' (take back our country) kauli iliyowahi kuleta sintofahamu wakati wa kampeni

Alt-right waliongozwa na watu kama Stephen Bannon aliyekuwa mshauri wa Rais Trump baada ya blog yake ya Breitbart kukamilisha kazi . Bannon hakwenda WH kwa bahati mbaya bali ni mchango wake

Inaendelea..
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US

MSUKO SUKO WH, KUSHINDWA MAADILI, NA VURUGU KIUTAWALA (IV)

Charlottesville, Viriginia

NJIA PANDA
Katika njia panda aliyopo, Rais Trump kaamua kuitosa Congress na Republicans ili albaki na alt-right
Raia Trump anaelewa nguvu ya alt-right siku za nyuma na kwa wakati ujao. Ni kwa vipi amtimue Bannon ?

Banno, Miller na Gorka ni 'wawakilishi' wa alt-right ndani ya WH. Kufukuzwa kwa Bannon si kwasababu ya tukio la Charlottesville. Hakuna ushahidi wa hilo bali ni kutokana na nguvu aliyokuwa nayo ndani ya WH

Taarifa za siku nyingi ni kuwa Bannon hawaelewani na Jared Kushner aliyemuoa binti wa Trump Ivanka
Lakini pia WH Chief Kelly alitaka kusafisha nyumba kwa kuondoa wakorofi kama Bannon.

Leo Banno ametimuliwa na kukidhi matakwa matatu. Kwanza, kusafisha WH na magomvi yanayotokana na Powerful man Bannon, pili kukidhi haja ya WH Chief of staff Gen Kelly na mwisho kuonyesha kuguswa kwa Trump na tukio la Charllotesvile, VA ili kujinusuru na kususiwa kunakoendelea

Hivyo si kweli kuwa Bannon ameondolewa kupinga ubaguzi.

Swali linalogonga vichwa vya wachambuzi ni kama suala la Bannon litaisha bila Trump kulipa gharama kubwa

Tutafafanua bandiko lijalo (V)
 
SIASA ZA US WIKI HII
MSUKO MSUKO WH, BANNON NJE, GOP WATIA SHAKA

Kuondoka kwa mwanamikakati Bannon kulitarajiwa kufuatia ujio wa Gen Kelly, chief of staff of WH
Bannon hakuelewana na Priebus wakati wake na Sccaramucci aliyetimuliwa siku 10 za ajira
Bannon hana mahusiano mazuri na mkwewe Trump, Jared kushner na mkewa Ivanka Trump

Wiki moja iliypita Banno alifanya mahojiano na chombo kimoja cha kiliberali na kwenda kinyume na Rais wake
Alisema hakuna suluhisho la vita Nkorea jambo linalosemwa kumuudhi sana Rais Trump

Baada ya kuondolewa, Bannon alirejea katika chombo chake cha habari cha Breitbart
Breitbart ilimpaza Trump wakati wa kampeni hasa kwa kundi la alt-right lenye msimamo mkali wa kihafidhina

Akiwa mwanamkakati wa Trump, Bannon amebeba habari nyingi. Hakupenda kuondolewa alilazimishwa

Ukiangalia wingu la timua timua kuanzia kwa Sally Yates, James Comey, Priebus,Bannon, Flynn na wengine wengi ni dhahiri kutaendelea kuwa na uvujaji wa habari zitakazomweka Rais Trump pagumu sana kiutawala

Kumfukuza Bannon hakutakuwa na matokeo mazuri ikizingatiwa anajua mikakati iliyomsaidia Trump

Hayo yakiendelea, sakata la Charlottesvill, VA. linachukua sura nyingine.
Reublicans wameshtumiwa mara nyingi kuhifadhi nadharia ya 'white supremacists'.

Hili limekuwa mwiba katika maeneo ya watu wa rangi hasa nyakati za uchaguzi.
Jitihada za Senators na Representatives kujitenga na Trump zimekuja na jingine

Kwamba, Rais Trump ana mgogoro na makundi hayo akijibu mapigo bila mpangilio
GOP wanasema handling ya sakata haikuwa katika kiwango cha Rais wa US kimaadaili

Ukiacha McCain na Graham , masenesta kama Tim Scott na Corker wamejiunga kumkemea Rais Trump

Hii maana yake ni dani ya senate, Trump anapoteza namba.

Kukiwa na ''margin of error'' ndogo si jambo jema. Miswada ya Trump haitapita kirahisi

Kosa la Trump ni kujibizana kama vile kusema 'McCain aliye block repeal and replace O'care'

Rais Trump anategemea kutuma timu maseneta husika washindwe 2018 na kufungua njia kwa Democrats, si lazima chaguo lake liwe la wananchi. Akipoteza maseneta 3 atapoteza senate

Sakata la wiki hii haikuishia kwa wanasiasa, 'CEO's wa makampuni makubwa, baraza la arts and humanities na hata la ushauri la Evangelical ikiwa ni pamoja na taasisi nyingine muhimu zimelazimika kujitenga naye

Dow Jones ilikuwa na wiki mbaya ikipoteza point nyingi dalili ya kutokuwa na imani na uongozi wa Rais Trump

Ukiyachukua yote katika kapu moja, unapata picha GOP na Independents wanamchoka

Rais Hata hivyo 36% ya watu wake tangu chaguzi za awali inasimama na Trump

Kwa mtazamo huo kuna mambo mawili yanayoanza kuchukua sura halisi ya huko twendako

1. Kwamba, 2018 kuna uwezekano Republicans wakapoteza senate na house
2. Taarifa ya Mueller kuhusu Russia ikitoa kitu chenye mashaka, itatumiwa vema kumwawajibisha

VP Pence ana misimamo tofauti na Rais akijificha kwa kusema anamuunga mkono Rais

Pence anafahamu uwezekano wa kuwa Rais bila uchaguzi unaongezeka siku hadi siku

Tusemezane
 
RAIS TEUMP AZUNGUMZIA MIKAKATI YA 'ASIA'
Charlottesville inamwandama kila aendapo

Rais Trump alianza kwa kauli zilizolenga kurekebisha bofoa ya wiki nzima ambayo bado ni gumzo Marekani
Rais amewataka wananchi wa US wawe kitu kimoja na wasigeuke kupigana wenyewe kwa wenyewe

Hii inakuja baada ya Trump kulaaniwa na jamii alivyo handle domestic crisis ya kwanza.
Kwa Charlottesvile, Trump alionyesha leadership and moral failure katika kumbumbu

Hakutaja Charlottesville wala white supremacist au nationalist
Alilazimika kuzungumzia kutokana na kauli ya joint chiefs of staff iliyomkemea kwa moral failure

Charlottesville limeonyesha udhaifu wa utawala kwa kushindwa kulileta Taifa pamoja
Polls zote zilizochukuliwa zinaonyesha disapproved hata maeneo aliyoshinda

Kauli ya leo ilifanana na iliyotolewa na joint chiefs of staff wa US military 'wakimlaani'
Kwa kutambua anaongea na askari wa aina zote, hakuwa na namna bali 'kulaani' kwa siri white supremacists

Kuhusu siasa za Afghanistan Rais Trump alisema wazi nia yake ilikuwa kutoendelea na vita
Hii ni sawa na kauli zake za nyuma alipolaani utawala wa Obama kuendelea na Afghanistan

Hata hivyo alisema kutokana na ushauri itabidi mikakati iwepo, kuondoka ghafla kutaleta tatizo kama Iraq.

Kwa maneno mengine ingawa amemlaumu Obama kwa siasa za Afghanistan mkakati alio nao hauna tofauti
Kwa sehemu kubwa alionekana kushindana kati ya dhamira yake na ushauri aliopewa na makamanda

Kuhusu Afghanistan, amesema jukumu la nchi hiyo watalichukua wananchi wa nchi hiyo ingawa US itaendelea kuongeza majeshi bila kusema ni wakati gani na kwa namna gani akiita time decision base

Trump amesinikiza Pakistan na India kupambana na magaidi akisema Pakistan inapewa pesa na US lakini ni safe heaven kwa magaidi na hivyo ifanye jitihada kupambana nayo ikizingatia ni nchi yenye Nuklia

Raia akasema India inafanya biashara na US nayo pia inapaswa kuunga mkono mapambano na magaidi

Hoja: Pakistan inapokea pesa kwa masilahi ya US. Nchi hiyo ina Nuklia na ni wajibu wa Marekani kuhakikisha Pakistan ipo mikononi mwao na si kuitisha kwa pesa zinazotolewa
Je, Pakistan ikiamua kuungana na Iran kwa 'nipe nikupe ni nani atakuwa loser'

Kuhusu India, kufanya biashara hakutoshi, India haina historia ya kuingilia mambo ya kijeshi.
Ni unlikely kuwatisha kwa biashara kutafanikiwa. Ni sawa na kosa la Taiwan kwa kuitisha China yenye karata

Asia ni eneo linalogombewa na mataifa ya Urusi , China, Iran n.k. kwa influence.
Hakuna uwezekano wa US kuliacha eneo au kutisha washirika kwani wana option ya nani washirikiane naye

Kauli za siku za nyuma kuhusu Afghanistan, Iran, Iraq na Pakistan ni tofauti na kauli za leo
Alichokilaani anakiendeleza kwa maana kuwa kutawala si sawa na kuendesha Trump Organization

Tusemezane
 
Back
Top Bottom