Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

"Mag3, post: 25654229, member: 10873"]Nadhani kwanza hujui utaratibu unaofuatwa hadi FISA inatolewa.
Apewe nafasi ya kutufahamisha,huenda kuna tusilolijua wengine
Pili hata huyo Nunes mwenyewe aliyetoa hiyo MEMO hadi sasa hajui kilichomo ndani ya hiyo FISA iliyotolewa.
Hata house intel member wamekiri kutojua nini kipo nyuma ya Memo
Tatu FISA ya kwanza ilitolewa miezi mitatu kabla ya hiyo unayoiita fake dossier.
Labda atueleze Carter Page alianza kufuatiliwa lini na kwasababu gani
Nne wanaotuhumiwa kwenye MEMO wote ni wateuliwa wa Trump.
Fake dossier inakuwaje Fake ikiwa Papdopolous amekiri kudanganya FBI?FBI walikuwa na habari kabla ya dossier, kilichofanyika ni kuoanisha tu habari za Australia na dossier
Tano Trump hakuwa wire-tapped kama unavyodai na MEMO haisemi hivyo.
Nunes ali sneak WH kueleza Obama na surveillance, DOJ wametafuta hakuona tena chini ya Trump na wateuliwa.Wire tap imetoka wapi? Huyu ndugu hakumbuki 'fake voters' ikaundwa kamati chini ya Pence ambayo Trump ameivunja kwasababu hakuna ushahidi wowote.

Hili ni neno fake limewakumbuka watu bila kujua maana yake iliyokusudiwa.
Habari za Russia ziliitwa fake, hakukuwa na kitu kima hicho
Ikabainika kilikuwepo, ikasemwa fake news hakukuwa na contact, ikabainika mkutano wa June
Ikasemwa fake news mkutano ulikuwa wa adoption, well, Junior kasema 'I Love it'
Trump amefanikiwa kufanya watu mazuzu akirudia jambo moja 1000x na wanaamini
Mwisho, nakuomba uvute subira, usikurupuke
Haya mambo yakiaangaliwa kwa jicho la copy and paste kutoka RT au Hannity yanasumbua sana.
Yanahitaji kuyaelewa na weledi wa kuyapambanua.
 
Hili ni neno fake limewakumba watu bila kujua maana yake iliyokusudiwa.
Habari za Russia ziliitwa fake, hakukuwa na kitu kima hicho
Ikabainika kilikuwepo, ikasemwa fake news hakukuwa na contact, ikabainika mkutano wa June
Ikasemwa fake news mkutano ulikuwa wa adoption, well, Junior kasema 'I Love it'
Trump amefanikiwa kufanya watu mazuzu akirudia jambo moja 1000x na wanaamini
Haya mambo yakiaangaliwa kwa jicho la copy and paste kutoka RT au Hannity yanasumbua sana.
Yanahitaji kuyaelewa na weledi wa kuyapambanua.
Mkuu Nguruvi3, kama kuna mtu anafaa kupewa nishani ya kinachoitwa FAKE News ni Donald Trump. Katika historia ya Marekani hajawahi kutokea kiongozi muongo kama Trump na uongo wake ulianzia toka siku ile anaapishwa na mpaka sasa anaendelea. Uzuri ni kwamba katika nyakati hizi za teknolojia, kumbukumbu zipo (za video, audio na twitter) na hata mashabiki wake wanatamani kama angeweza kuufunga mdomo wake lakini wapi.


2000 lies in one year, 16,000 in 8?​
 
MEMO YA DEMS YATUA WH
WANASHERIA WA RAIS TRUMP 'WACHOMOA'
STOCK MARKET TAFRANI

Masoko ya mitaji yameendele kupoteza.Leo DJ imepoteza 1175, S&P na NAZDAQ nazo pia
Rais Trump amepigia upatu rekodi ya masoko kama kigezo cha uchumi mzuri

Kama mtakumbuka huko nyuma tulisema masoko hayaelezi hali ya uchumi kwa uhalisia

Hali ya masoko imeingiwa na mtafaruku kutokana na mambo mengine yanayohusiana na

Taarifa ya ajira ya mwezi uliopita inaonyesha ongezeko la ajira 200,000.
Inaashiria reserve bank inayofikiria kuongeza interest rate katika itafanya hivyo.

Pili, ashirio la mishahara kuongezeka, jambo litakalopelekea inflation

Tatu, kwa mujibu wa wachumi, masoko yalipanda kwa kasi kuliko ilivyotarajiwa na kilichotokea ni 'cooling effect'

Nne, kuna looming second gov shutdown ikiwa hakutakuwa na maafikiano

Kinachoifanya habari kuwa kubwa ni ukweli,Rais Trump ame 'anajifaragua' masoko yanashamiri kwa ushawishi wake au sera zake hata kama mwenendo ulikuwa hivyo kwa miezi zaidi ya 75 iliyopita

Tofauti ni kuwa wakati wa Obama, kulikuwa na 'steady' growth na baada ya hapo graph ikapanda kwa kasi

Kutokana na kupigia debe masoko, media zinahoji, je anguko la siku mbili lililofuta takribani point za mwaka mzima ni 'ushawishi' wa Trump?
what goes around , comes around

Wanasheria

Inaripotiwa wanasheria wa Trump wamemtaka asifike mbele ya timu ya Mueller.
Kwa wiki majadiliano yanaendelea na wanasheria wanasema 'huo unaweza kuwa mtego'

Hili linafuatilia matamko ya mwisho wa wiki kutoka kwa wanasheria hao wakisema Mueller 'hajafikia threashold'

Kilichotarajiwa kutoka kwa memo ya Nunes ,kama kumuondoa Rosenstein hayakufikiwa haraka

Rais Trump leo amemsifia Nunes akisema ni mmoja wa watakaokumbukwa kwa uthubutu.

WH ilisema lengo la kuachia memo ni uwazi, kwa namna nyingine Rais anaonekana kulifanya la kisiasa akimshambulia kiongozi wa Intel committee kwa upande wa minority Adam Schiff kwa dhihaka

Lengo la Trump ni kumdhalilisha na kumuondoa katika focus ya memo ya dems
Ni mbinu yake kuanzia nyakati za uchaguzi za kuvuta watu katika 'upuuzi' na kisha kuwashinda

MEMO
Memo ya Dems imeidhinishwa na wajumbe wa kamati na sasa ipo WH.
Ni ile iliyogomewa wiki iliyopita ikiwa ni kutoa nafasi kwa memo ya Nunes kuzungumziwa

Utata umeanza kujitokeza. Jumanne wakati wa state of union, Rais Trump alisema atai declassify memo ya Nunes hata kabla ya kuisoma.
Leo WH imeingiwa na kigugumizi kusema itasainiwa ya Dems

Hoja ya WH ni kuwa memo ya Dems itapitiwa kama ilivyokuwa ya Nunes.

Kwa kutambua utata huo Adam Schiff aliwasiliana na DOJ na FBI ili kuhakikisha memo haitatoa habari au mbinu za kiuchunguzi ili kuhakikisha hakuna excuse ya WH kupunguza

Hata hivyo, kuna uwezekano WH ikanyofoa sehemu zitakazoonekana za nguvu katika suala la siasa na Dems hawatakuwa na njia mbadala
Sababu atakayoitoa Trump ni usalama hata kama si hivyo

Lakini pia kuna mtego, kama imepitiwa na DOJ na FBI kwanza, kitakachoondolewa WH kitalinganishwa na uhalisia wa nyaraka hiyo , marekebisho ya DOJ na FB

Hali inatia shaka, chairman Nunes ameulizwa kama mem haikuandikwa kwa ushirika na WH. Kwa kuchelea leaks, Nunes kakataa kujibu swali la wazi la 'ndiyo au hapana'

Disadvantage ipo kwa Dems, kwanza, Nunes memo imezungumziwa vya kutosha ingawa impact yake haikuwa kama ilivyokusudiwa.

Trick zilizochezwa na Paul Ryan, Nunes na WH zinalipa kwa muda mfupi
Kwa muda mrefu ikibainika vinginevyo, itaonyesha kuna kinachofichwa

Ikiachwa memo ya dems itoke kama ilivyo, itaweza kukuyeyusha ya Nunes, hilo haliwezekani kwani lengo ni kupoteza umma kwa kuuchanganya uamini Russia investigation ni hoax hata kama hakuna uhusiano Russia vs memo

Tusemezane
 
MEMO YA DEMS NDANI YA WH
GEN KELLY ASEMA 'SI SAFI' ! KAMA YA REPUBLICAN

Kwanza, masoko yalianza kwa tishio la kuporomoka kabla ya kurejea katika positive territory na kupata point 500

Kisicho cha kawaida ni kupigia upatu bila kujali kuna kupanda na kushuka
Masoko si kigezo pekee ya hali nzuri au mbaya ya uchumi, kuna vigezo vingi kama tulivyowahi kujadili

Memo:
Ile memo ya Dems imeshafika WH na tayari kumeanza figisufigusu kuhusu kusainiwa kwake
Wakati Rais Trump akisema atasaini ya Nunes hata kabla ya kuisoma, amekuwa 'bubu' kwa hii ya Dems

Ilipotolewa ya Nunes hoja ilikuwa ni kuweka uwazi . Kinachoshangaza hii ya Dems imepewa mtazamo tofauti

Kama tulivyosema huko nyuma, Dems walijua WH haitaki memo yao itoke walichokifanya ni kuipeleka memo DOJ na FBI kuipitia kama kuna sensitive information kisha ikarudi katika kamati na kupigiwa kura

Sasa ipo WH, Sarah Huckabee, press sec kasema memo inapitiwa na vyombo vya usalama
Akiyekuwepo WH ni Rosenstein deputy DOJ ambaye Trump alikataa kusema ana imani naye au la 'you figure out'

Mwingine aliyeitwa WH ni Christopher Wray ambaye ni FBI Director.

Hawa wawili wiki iliyokwisha walikwenda WH kukutana na John Kelly, chief of staff kuitaka WH isitoe memo ya Nunes kwasababu ina 'gravely omission...and fundamentally misleading'. Hawakusikilizwa

Wakati huo huo Kelly anasema memo ya Nunes ilikuwa 'safi' ukilinganisha na ile ya Democrats

Hapa kuna mchezo unachezwa na WH. Kwanza kumwita Rosenstein na Wray ni kuwaweka katika mtego
Kwamba wasipokubaliana na maamuzi ya WH, wajiuzulu jambo ambalo WH na Trump wanalitaka

Pili, kauli ya John Kelly inaashiria memo ya Democrats itafanyiwa ''political editing'' ili kutofunika ya Nunes
Na itakapotokea hivyo, WH watasema aliyefanya ni Rosenstein na Wray si wao

Tatu, Gen Kelly anaandaa umma kisaikolojia kuwa memo ya democrats ina matatizo na itafanyiwa 'ukarabati'

Mtego: Kitendo cha Democrats kuipeleka DOJ na FBI kabla ya Ikulu kinamaanisha vyombo hivyo vilifanya marekebisho kabla ya kuirudisha katika kamati na kabla ya kwenda WH

Kwa mantiki hiyo, 'deductions' yoyote itakuwa imefanywa na WH bila mjadala.

Hapa Rosenstein na Wray watakuwa na wakati mgumu sana, kwamba, ima waseme WH imebadilisha na hiyo iwe tiketi ya kuwatimua, au wakubaliane kuwa wamefanya review tena na Democrats wahoji kwanini sasa na si kabla

Kwa upande wa Rais Trump, hakuna namna anayoweza kuizuia. Kitendo hicho kitamwagia 'maji' baridi memo ya Nunes kama ushahidi wa hila. Lakini pia kitakuwa kimeidhalilisha house intel committee

Trump hataweza kuizuia, atakachoweza kufanya ni kupunguza maeno yanayopingana na ile ya Nunes au kunyofoa vifungu na kuruhusu itoke.

Kwa vile chairman ni Nunes, ikisainiwa hakutakuwa na muda ataitoa ijadiliwe hata kama Dmeocrats watalalamika.

Yote hayo yanaweza kufanyika lakini kwa gharama kubwa. Hadi sasa taratibu Republican wanaanza kujitenga na memo ya Nunes wakisema haina uhusiano na uchunguzi wa Russia na haikuwa na ulazima wa kuitoa

Jambo lolote litakalokera Republican litachagiza uchunguzi wa Russia kwa kasi na mpango wowote wa kuua hoja ya Russia utakutana na upinzani kama ambavyo kumtimua Rosenstein kunavyoweza kuleta kiwewe

Kwa jicho pana, memo ya Nunes inamweka Trump katika hali ngumu kuliko faraja iliyotarajiwa

Tusemezane
 
MEMO YA DEMOCRATS 'YAPIGWA CHINI'

Wiki hii kama kawaida imetawaliwa na matukio kadhaa ya kisiasa
Kwanza, kashfa ya mtu wa karibu na msaidizi mkuu wa Rais Trump bwana Rob Porter

Rob anafikiriwa mwenye uwezo mkubwa katika usaidizi. Kashfa iliyomkumba ni 'kunyanyasa wake zake'
Rob ameoa mara mbili na kutuhumiwa kuwanyanyasa wake zake hata hata kuwapa vipigo

Habari iliripotiwa na gazeti kwa mara ya kwanza. Bila kujua undani, chief of staff John Kelly na Mshauri wa Ikulu Hope Hicks walitoa kauli ya kumtetea Rob. Hope ni kimada wa Rob wote wakifanya kazi WH

Habari si kubwa kiasi hicho, ukubwa ni jinsi General Kelly alivyo ''handle'' bila kujua undani wa media za US.

Leo inajulikana Kelly alikuwa na habari siku nyingi na alichokifanya ni 'cover up'
Rais Trump naye 'kadandia' kwa kutoa kauli ya kumtetea Rob wakati huu wa harakati dhidi ya unyanyasaji

Kwa mantiki hiyo, kibarua cha Gen Kelly kipo mashakani kwa kushindwa kumtetea Rob Porter

RACHEL BRAND AJIUZULU
Huyu alikuwa mtu wa tatu kwa uandamizi katika Dep. of Justice (DOJ).
Alikuwa chini ya Rosenstein anayesimamia uchunguzi wa Russia tukijua Sec. Sessions amejitoa

Ingalitokea Rosenstein akatimuliwa au kujiuzulu, mtu aliyetarajiwa kuchukua nafasi hiyo ni Rachel Brand

Inaaelezwa Rechal ameenda kufanya kazi Walmart, hata hivyo kwa nafasi yake inaonekana kuna aidha jambo halikumridhisha, shinikizo au namna nyingine yoyote iliyomlazimu

Kuondoka kwake ni nafuu kwa Rais Trump kwani kuondoka kwa Rosenstein , Rachel angechukua nafasi hiyo

Kwasasa, Rais Trump ana uwezo wa kumteua mtu mwingine na akikubalika atakuwa wa tatu kwa maamuzi
Hii maana yake ni kuwa mtu wa tatu amtakaye ataweza kurithi kazi za Rosenstein ikitokea

Kitakachofuata ni kumtimua Rosenstein ili atakayeteuliwa achukue mikoba na control ya Russia Invest

MEMO
Leo ilikuwa siku ya tano Rais alitakiwa asaini kutolewa memo ya Dems.
Kwa wiki nzima WH inasema memo ya Dems inapitia mchakato ule ule wa memo ya Nunes.

Kama tulivyowahi jadili mizengwe itatokea na imetokea

Memo imerudishwa katika kamati ya Bunge ili 'kupunguzwa' maeneo nyeti kama ilivyoshauriwa na vyombo vya usalama kwa mujibu wa WH. Ni ushauri wa vyombo vile vile vilivyokataa memo ya Nunes lakini ikatolewa

Vipi Rais Trump alidharau ushauri wa FBI na DOJ na kuruhusu memo tena akisema itatolewa hata kabla ya kuisoma na leo Rais yule yule anachukua ushauri wa vyombo vile vile alivyokataa ushauri wao?

Mtego ni kuwa memo irudishwe katika kamati kupunguzwa, Rosenstein na FBI Wray wameagizwa wasaidie hilo.

Ikumbukwe memo ya Dems ilipitia kwa watu hao hao kabla ya kwenda WH!
Mtego huu unamhusu sana Rosenstein ambaye akienda tofauti na WH atawapa sababu za kumtimua

Mkakati wa pili ni kuchelewesha memo ya Dems ili ya Nunes iendelee kuwepo.

Itakaporuhusiwa kutolewa memo ya Dem itakuwa haina nguvu kama ilivyotarajiwa.
Hapa ni kupitisha muda na kukwepa ukweli utakaoiumbua memo ya Nunes

Kama Rais Trump alitaka uwazi nini kinamzuai asitoe memo ya Dems,ya Nunes ilitoka dhidi FBI na DoJ?

Jambo moja zuri kwa namna flani. Kashfa ya WH inafunikwa na Memo iliyokataliwa ya Dems
Kashfa ya unyanyasaji iliyoibua mjadala mkubwa sasa inafifishwa na mjadala wa kukakataliwa memo

Tusemezane
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Breaking News: 13 Russian Nationals charged in Mueller Investigation!

The office of special counsel Robert Mueller says a grand jury has charged 13 Russian nationals and three Russian entities. The defendants are accused of violating U.S. criminal laws to interfere with American elections and the political process. Charges include conspiracy, wire fraud, bank fraud and aggravated identity theft.

Huu ni mwanzo tu...je nini kitafuata?
 
MUELLER AJA KINAMNA

Bandiko la Mkuu Mag3 hapo juu linaeleza kwa ufupi yaliyojiri kuhusu Russia na uchunguzi wa Mueller
Siku ya leo ilianza kwa Robert Gates, mshauri wa Trump kuelezwa ameingia 'deal' na Mueller
Gates ni mshirika mkubwa wa kampeni meneja wa zamani wa Trump Manafort

Wawili hao wanahusishwa na tuhuma na hivyo Gates anakabaliwa na kesi 'nje' ya Russia investigation na hiyo inatumika kumbana ndiyo msingi wa kuingia deal Mueller

Kwa kumbukumbu Gen Flynn anakabiliwa na mashtaka mazito kuhusu ushirika wake na Turkey

Mashtaka hayo yanamhusu mwanae Flynn Jr. Katika kumbana kilichotokea ni 'nipe nikupe' kwa maana kuwa Mueller atamfungulia mashtaka laini kama la kudanganya FBI , naye atoe ushirikiano wa Russia

Mashtaka ya leo kwa Raia hao wa Russia yana maana sana katika suala zima la uchunguzi
Kwanza, mashtaka yanaeleza kuingilia demokrasia ya uchaguzi kwa kinachoitwa 'information warfare'

Mashambulizi hayo ya 'teknohama' yanasemwa yalianza mwaka 2014.
Ni wakati ambapo US waliweka vikwazo dhidi ya Russia kuhusiana na suala la Kremia.

Pili,mashambulizi yalipangwa na washirika kutoka Kremlin kama private citizen.
Yalibadilika kuwa dhidi ya Hillary Clinton ambaye alishikia bango vikwazo dhidi ya Russia akiwa SOS.

Tatu, kumekuwa na habari kuwa uchunguzi wa Russia hauna collusion na kwamba ni Hoax

Nne, kumekuwa na figisu figisu kuhusu nama Comey alivyotimuliwa na Deputy FBI McCabe walivyoshambuliwa na Trump kampeni. Baada ya hao, Dep DOJ Rosenstein ndiye mlengwa

Tano, Ile Memo ya Nunes na jinsi memo ya Dems ilivyopigwa chini ni dhahiri kuna mpango unasukwa ili kuzima uchunguzi wa Russia kwa mbinu

Hapa ndipo hoja ya Mueller ya leo ilipo, tunajadili bandiko lijalo

Inaendelea
 
Inaendelea

Taarifaya Mueller imetolewa na Deputy DOJ Rosenstein baada ya kwenda WH kumueleza Trump
Roseinstein amefanya makusudi akijua chochote chenye utata kitampa Trump tiketi ya kumtimua

Taarifa inaeleza kwa undani jinsi Russia walivyopanga mashambulizi ya mitandao dhidi ya US
ikisema katika mashtaka hakuna Raia wa Marekani aliyehusishwa kwa ushiriki

Taarifa imeandikwa kiufundi sana kiasi ikiwa neutral na unaweza kuitafsiri kwa namna yoyote

Rais Trump kama na WH wamesema taarifa imewasafisha kuhusu Russia collusion
Katika Tweet, Trump anasema mashambulizi ya Russia yalianza 2014 kabla ya kugombea

Rais Trump ameshindwa kuelewa tweets zake zinamweka katika wakati mgumu
Kwanza, taarifa iliyotolewa na WH inatofuatiana na Tweets za Trump

Pili, Trump anajianika aliwahi kusema suala la Russia ni Hoax au magumashi.
Kwa kusema lilianza 2014 ni kukiri taarifa hiyo ni ya kweli na si hoax

Rais Trump anakubaliana na vyombo vya usalama kuhusu Russia kuingilia demokrasia
Suala la collusion ni tofauti na kuingilia.Kuna uwezekano ipo na yawezekana hakuna collusion

Yote hayo si muhimu kuliko sababu tulizoeleza bandiko 547.
Bila kujali uzito wa taarifa,muhimu ni DOJ, FBI na Mueller kuzima jaribio la kumfukuza Rosenstein

Spika Ryan, mshirika na mpiga debe wa memo ya Nunes amejitokeza na kusema lipo 'neno'

Taarifa ya leo imeeleza ''mashambulizi'' ya Russia dhidi ya US na kuwaunganisha Dems na GOP
Ukiisoma sehemu kubwa imejikita katika Utaifa si Russia investigation au Obstructions of Justice

Hili limejenga 'Kinga' kwa Rosenstein na automatic Mueller kwa kujua upo mpango wa kuwatimua

Taarifa ya leo haimaanishi kuna tatizo au la, bali imejenga mazingira magumu sana kwa Trump kuua uchunguzi wa Russia baada ya jitihada za baadhi ya Wabunge na Mseneta kwa kwa ushirika na WH

Jaribio lolote la kumtimua Rosenstein litakumbana na Impeachment, itaonekana kuna njama za watu dhidi ya Utaifa na hapo ndipo Trump na kampeni yake wanapojikuta na wakati mgumu kidogo

Tusemezane
 
  • Thanks
Reactions: BAK
MUELLER AJA KINAMNA
Bandiko la Mkuu Mag3 hapo juu linaeleza kwa ufupi yaliyojiri kuhusu Russia na uchunguzi wa Mueller
Siku ya leo ilianza kwa Robert Gates, mshauri wa Trump kuelezwa ameingia 'deal' na Mueller
Gates ni mshirika mkubwa wa kampeni meneja wa zamani wa Trump Manafort...
Uchunguzi unaofanywa na Muller sasa umeingia rasmi kipindi cha lala salama na kuna hatari ya ngoma kuwageukia wanasheria wa Donald Trump ambao wanaweza kukabiliwa na tuhuma za kusema uongo kwa nia ya kumlinda. Ushirikiano anaoutoa Robert Gates umewezesha kutiwa hatiani kwa mwanasheria wa Paul Monafort, Alex Van Der Zwaan kwa kusema uongo. Wanasheria wa Trump mwenyewe tayari matumbo moto kwani inaonekana kulikuwa na njama za makusudi kufuta nyayo katika jitihada za kuficha ushahidi.

Tunaendelea kukaa mkao wa kula...
 
Uchunguzi unaofanywa na Muller sasa umeingia rasmi kipindi cha lala salama na kuna hatari ya ngoma kuwageukia wanasheria wa Donald Trump ambao wanaweza kukabiliwa na tuhuma za kusema uongo kwa nia ya kumlinda. Ushirikiano anaoutoa Robert Gates umewezesha kutiwa hatiani kwa mwanasheria wa Paul Monafort, Alex Van Der Zwaan kwa kusema uongo. Wanasheria wa Trump mwenyewe tayari matumbo moto kwani inaonekana kulikuwa na njama za makusudi kufuta nyayo katika jitihada za kuficha ushahidi.

Tunaendelea kukaa mkao wa kula...

Huyo Alex Van Der Zwaan keshakubali yaishe!!!
 
[
Huyo Alex Van Der Zwaan keshakubali yaishe!!!
"
Mag3, post: 25880797, member: 10873"]Ushirikiano anaoutoa Robert Gates umewezesha kutiwa hatiani kwa mwanasheria wa Paul Monafort, Alex Van Der Zwaan kwa kusema uongo. Wanasheria wa Trump mwenyewe tayari matumbo moto kwani inaonekana kulikuwa na njama za makusudi kufuta nyayo katika jitihada za kuficha ushahidi.
Bahati nzuri wanasheria wa Trump hawajatoa kauli mbele ya Mueller. Bahati mbaya ni mteja wao Trump na kauli tata sana.

Kwa mfano, kuhusu kuandika statement ya Don Jr na alivyotofautiana na wanasheria wake

Kwa kutambua hilo, wanasheria wa Trump wanachelewesha muda wa mteja kukutana na Mueller

Hofu ya Sekulow na Cob ipo katika mambo kadhaa

1. Mteja wao anazungumza mambo yanayoweza kumweka matatani hasa obst of justice
2. Hawaelewi walio mikononi mwa Mueller kama Flynn, Gates, Papadopolous etc wanatoa ushirikiano gani
3. Hofu ya wanasheria wenyewe kuwa kama Van Zwaan

Wanasheria wanachelewesha Trump kukutana na Mueller wakitegemea linaweza kutokea jambo likavuruga uchunguzi mzima na kumuokoa mteja wao.

Hapa walitegemea kutimuliwa kwa Rosenstein kama ambavyo McCabe aliachia ngazi.
Walitegemea kumuandama Rosenstein kwa media kama Fox kuna weza toa jambo zuri

Kuondoka kwa McCabe kulitoa dalili za wapi Trump na timu zake wanaelekea.

Kilichofanyika wiki iliyopita ni indictment ya Russia 13 ikiwa ni statement kuwa Russia investigation si hoax
Pili, Rosenstein kutoa taarifa kulionyesha yeye ni mmiliki wa process nzima

Kilichofanyika ni kujenga uzio ili Trump asijetumia udhaifu wowote kama anavyotumia House intel ya Nunes. Kwasasa kumtimua Rosenstein ni ngumu , ikifanyika kutakuwa na kishindo

Hili linaeleza wanasheria wa Rais Trump wapo njia panda kwa kuangalia kesi ya Van Zwaan vs Mteja
 
FAKE President FAKE Administration and the CHAOS will continue.
Trump anasema watu wengi wanaitaka nafasi hiyo hivyo atampata mbadala wake hivi karibuni. Safari hii anasema atakuwa muangalifu zaidi kwenye kuchagua. Ameongeza kuwa utawala wake hauna shida ingawa anasema anaweza kufanya mabadiliko kadhaa...!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Trump anasema watu wengi wanaitaka nafasi hiyo hivyo atampata mbadala wake hivi karibuni. Safari hii anasema atakuwa muangalifu zaidi kwenye kuchagua. Ameongeza kuwa utawala wake hauna shida ingawa anasema anaweza kufanya mabadiliko kadhaa...!
TUJITEGEMEE, nilitegemea kwamba mpaka sasa utakuwa umeelewa kinachoendelea Marekani lakini yaonekana huna habari kabisaaa kuwa Trump tayari siku zake zinahesabika. Kama GOP watafanikiwa kumuepusha na dhoruba inayomkabili kwa sasa, dhoruba itakayofuatia haitamwacha salama. Kinachofanyika kwa sasa hivi ni mbinu za kuwapoza wale mashabiki wake ambao hawaamini chochote kinachosemwa juu yake.

Hatua yoyote ya kukurupuka kungeweza kuleta mtafaruku ambao madhara yake pengine ingechukua muda mrefu kuyashughulikia hadi kuyapatia ufumbuzi bila mfarakano. Kwa sasa asilimia ya mashabiki wake ndaki ndaki bado iko juu lakini taratibu idadi hiyo inasubiriwa ipungue hadi ifikie kiwango muafaka. Ni kama mgonjwa ambaye joto lake la mwili liko juu sana asivyoweza kuchomwa sindano mpaka kwanza hilo joto lipungue.

Siku njema!
 
Naona Russia collusion inaonekana kutofanya kazi...ameamua kutumia mbinu nyingine.

A White House taken by storm(y) - CNNPolitics
====
Ingawa nilishaeleza huko nyuma kuwa Trump ataizamisha US, lakini hivi visa Democrat na MSM zao wanachomfanyia si kizuri. Yaani wanataka wamchanganye ili aiue haraka US badala ya polepole.
 
Naona Russia collusion inaonekana kutofanya kazi...ameamua kutumia mbinu nyingine.

A White House taken by storm(y) - CNNPolitics
====
Ingawa nilishaeleza huko nyuma kuwa Trump ataizamisha US, lakini hivi visa Democrat na MSM zao wanachomfanyia si kizuri. Yaani wanataka wamchanganye ili aiue haraka US badala ya polepole.
Ha ha haaa, kalaghabaho! Pole sana ndugu.
 
Ha ha haaa, kalaghabaho! Pole sana ndugu.
Naona Trump anajaribu kuzima wimbi la kumfanya ashindwe haraka kuiendesha US kwa staili ya aina yake. Rex kapigwa chini kakimbizwa haraka kutoka Afrika ili akabidhiwe barua ya kupigwa chini. Rex mdomo ulizidi kichwa. Mfano Jana kurukia issue ya UK kuituhumu Russia lilikuwa kosa la ufundi. Pia msimamo wake dhidi ya mazungumzo ya US na NK nao umemletea matatizo. Nadhani pia Rex alishawekwa mtu kati na 'Deep state (DS)' wakati Trump hawataki kabisa hao DS!!

Trump fires Sec of State Tillerson, replaces him with CIA chief Pompeo
 
"TUJITEGEMEE, post: 26186398, member: 31026"]Naona Trump anajaribu kuzima wimbi la kumfanya ashindwe haraka kuiendesha US kwa staili ya aina yake.
Mkuu, kuna bandiko Mag3 kasema siasa za US zinahitaji kwenda deep na kuunganisha 'dots'. Siyo siasa za 'headlines'

Hoja ya Russia, Stormy n.k. zinasimama zenyewe kwa maana ya kuwa media zina vitengo
Ukiona habari imefifia si kwamba imekufa bali kuna timing ya muda gani habari itoke

Kwa mfano, Republican wameamua kumaliza uchunguzi wa House Intel wenyewe
Jana kuna habari zinazohusu simu za Rogerstone na mkutano wa Don Jr, June 16 zimetoka

Baada ya habari za Rex , habari za kila siku kama za akina Sotmy na Russia zitarudi pale pale
Unakumbuka email na Benghaz zilivyomtesa Hillary?

Rex kapigwa chini kakimbizwa haraka kutoka Afrika ili akabidhiwe barua ya kupigwa chini.
Hakukabidhiwa barua, alisikia kwenye tweet tu. Habari za uhakika, Kelly alimpigia simu Ijumaa arudi nyumbani. Hakuna asiyejua uhusiano wa Rex na Trump ulikuwa na mashaka
Umesahau maneno waliyotupiana kuhusu 'IQ na Moron'?
Rex mdomo ulizidi kichwa.
Nadhani hujaelewa kazi ya state dept. Hii ndiyo idara inayomshauri Rais kuhusu mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa. SoS ndiye mwenye mawasiliano yote na ukitaka kujua uzito wake tazama nyuma wakati wa Obama na jinsi Hillary alivyobeba mzigo wa Benghaz au alivyochukua credit ya Paris agreement au J. Kerry na Iran
Mfano Jana kurukia issue ya UK kuituhumu Russia lilikuwa kosa la ufundi. Pia msimamo wake dhidi ya mazungumzo ya US na NK nao umemletea matatizo. Nadhani pia Rex alishawekwa mtu kati na 'Deep state (DS)' wakati Trump hawataki kabisa hao DS!!
Alitoa kauli kama SOS baada ya kushauriana na NSA na kupata mawasiliano kutoka UK

Kwamba, ingekuwa Iran au Nk Trump angekurupuka mapema kama alivyowahi kudai kuna shambulio la kigaidi Sweden wakati ilikuwa ni documentary tu. Kwa vile ni suala la UK linalogusa 'Russia' Trump hasikiki
Hilo nalo linazidi kutia shaka sana Wamarekani kuhusu Rais wao kuwa Loyal na Kremlin. Kulikoni?

Unachotakiwa kuelewa ni kuwa SoS ni top security advisor

Sasa kuhusu kutofautiana na Trump kisera, Rex ana mitazamo tofauti kuhusu Iran,NK Paris Climate na sera nyingine kwa masilahi ya US na si 'ndiyo mzee' hivyo hakuwa loyal

Alimshauri Trump kuhusu NK na mazungumzo, kitu ambacho Trump sasa amekubali tena bila kumshirikisha. Kuhusu Iran, Rex anamuuliza Trump, option ipi iliyopo mezani ?
Climate change, Rex aliyeongoza kampuni ya mafuta anakubali.

Kuhusu deep state unayosema, nina shaka kama kweli umeielewa ni nini
Mike Pompeo unafahamu ametokea wapi? Gina Haspel unajua ametokea wapi?
Unajua wamefanya nini siku za nyuma kiasi cha kutishia confirmation yao leo hii?

Mwisho, Trump alisema ana 'hire' smart people. Je, aliachukua deep state? Na Rex unaamini ni deep state? Mabadiliko anayofanya ni kutokana na teuzi zake mwenyewe! Huoni tatizo hapo mkuu

Mkuu haya mambo si mapesi ni siasa za US
 
Mkuu, kuna bandiko Mag3 kasema siasa za US zinahitaji kwenda deep na kuunganisha 'dots'. Siyo siasa za 'headlines'...

...Mkuu haya mambo si mapesi ni siasa za US
Kwanza sina hakika kama TUJITEGEMEE kweli anajua idadi ya tuhuma zinazomkabili Trump. Pili, kwa sasa hakuna anayejua kwa uhakika hatua aliyofikia Mueller na timu yake.
 
Back
Top Bottom