YANAYOJIRI SIASA ZA US
UTEZI WA JAJI WA MAHAKAMA KUU YA MAREKANI
''BOMU' LA DOJ, HATMA YA ROSENSTEIN NA MUELLER
Siasa za viunga vya Washington zimekuwa na mengi katika kipindi cha muda mfupi
Kumekuwepo na matoleo ya vitabu na maandiko kuhusu utawala wa Rais Trump
Yamekuwepo maafa ya vimbunga ya mwaka jana na mwaka huu
Kumekuwepo na uteuzi wa Jaji wa mahakama kuu ya Marekani n.k.
Tutayapitia kuangalia maeneo yenye utata zaidi na yatakayopanda duru za habari
Mfululizo wa vitabu na maadiko magazetini kuhusu utawala huu yametia shaka juu ya hatma ya Taifa hilo katika uongozi wa nchi. Yote yanaeleza kuyumba 'wobbling' kwa shughuli za kiutawala
Jambo hilo linachagizwa sana na uchunguzi wa Mueller unaozidi kulisogelea jumba jeupe kuliko ilivyotegemewa. Washirika wa Bwana Trump wa ndani wote wamekabiliwa na mashtaka wamebwaga manyanga na kujiungana kambi ya ''ushahidi'' kujinasua na dhahama.
Kujiunga huko kuna maana moja, mengi yasiyotakiwa kujulikani yatawekwa wazi
Watu wa karibu sana kama mwanasheria binafsi Bwana Cohen, na mwenyekiti wa kampeni bwana Manafort ni sehemu ya kundi la ndani lililoamua kurudi upande wa 'mashahidi'
Jitihada za rump na mshirika Rud Giullian kupiga mzinga uchunguzi zinagonga mwamba.
Kuna jitihada chache zilizobaki zinazoanza kuzaa matunda ya kuzima uchunguzi wa Mueller
Rais Trump amekuwa akimkashfu Attorney general Bw Sessions hadharani kumkatisha tamaa. Kama mtakumbuka, tumejadili sana kuhusu hili na kwamba kuondoka kwa bwana Sessions kutatoa fursa ya kuteua AG mwingine atakayeweza kuzima uchunguzi wa Mueller
Sessions kagoma kujiuzulu na Rais Trump amesema baada ya midterm Sessions ataondoka. Kuchelewa kuondoka kwa Sessions kuna tatizo, uchunguzi unaendelea kwa ukaribu zaidi.
Njia mbadala ni kumuondoa msimamizi deputy AG Rosenstein
Kumuondoa Rosenstein kutaleta hisia za kuzima uchunguzi, na hilo limekuwa kikwazo
Leo gazeti la NewYork timeslimeandika kuhusu yale yaliyosemwa katika magazeti soma
hapa
Kwamba Rosenstein alishauri kutumika 25th ammendment ya katiba kumuondoa Bw. Trump madarakani. Habari imevujishwa kwa makusudi na mrengo wa kulia 'conservative' ambao kila siku kwa hutumia TV ya FOX wameshauri kutimuliwa kwake
Kutimuliwa kwa Rosenstein kutatoa nafasi ya uteuzi wa deputy AG mwingine atakayesimamia uchunguzi wa Mueller hadi AG atakapoondolewa.
Hii maana yake ni kuwa uchunguzi unaweza kufutwa na mteule deputy AG au AG mpya.
Habari hiyo ni njema kwa Bw Trump kwani itampa fursa ya kutekeleza azma yake
Je, azma hiyo itakuja bila maruwe ruwe au mizigo myuma yake?
Inaendelea.....