VIUNGANI DC WIKI HII
WH YAKATAA WATUMISHI KUHOJIWA
Huko nyuma katika uzi tulisema kinachoitwa collusion si tishio kama obstruction of justice
Tutumie maneno yalio kwenye ripoti ya Mueller, ambayo ni "conspiracy" na "coordination", kwa sababu "collusion" imechunguzwa kama "conspiracy". Kwahiyo labda useme conspiracy sio tishio. Ina maana Volume I nzima sio tishio?
House watashughulika na "Obstruction of justice" na sio "conspiracy" au "collusion".
Tulitoa mfano wa sakata la Bill Clinton liloanza kwa mambo ya nje, ngono na kuhitimishwa na obstruction of justice. Kinachoendelea DC si tofauti na tulichozungumza
Kesi ya Bill Clinton ni tofauti kwa sababu yeye alitenda kosa (underlying crime) ambalo alitumia mamlaka ya Rais kuzuia haki (obstruction of justice). Trump hajatenda kosa ambalo anatuhumiwa kuzuilia haki.
Clinton alikuwa na kesi nne (2 za perjury, obstruction of justice na abuse of power) ambazo Independent Counsel Ken Starr aliamua kwenye ripoti yake awe impeached. Huku, Mueller ameshindwa kuamua kuhusu kesi ya Obstruction of Justice.
Clinton alikuwa impeached na House (Republican majority) kwa makosa mawili kati ya manne lakini zilishindwa kupita Senate (Republican majority, Dems wote wakapiga kura ya Hapana) na hivyo akaonekana hana hatia. Leo majority kwenye House ni Dems ila Senate ni Republicans, unaweza kupiga hesabu!
Wiki tatu zilizopita tulisema AG Barr anatumika tu na WH na ile credibility yake imeondoka
Barr alisimama na kusema hakuna collusion ingawa si neno la kisheria
Taarifa ya Mueller inaeleza mahusiano yalikuwepo kati ya kampeni ya Trump na Russia
"Collusion" sio neno kisheria ndio, what difference does it make? Mahusiano yote yamechunguzwa na yamehibitika sio makosa kisheria.
Credibility ya Barr imeondoka mbele ya nani, Democrats?
Barr akasambaza vihabari vya kutunga ( Bandiko 765) na kurudia tena alhamisi iliyopita
Katika mengi yaliyomo, Barr alidai Mueller hakufikia tamati kuhusu obstruction of justice
Taarifa inaonyesha kinyume kabisa kwani Mueller aliweka mazingira ya mashtaka Congress
Kwani Mueller amefikia tamati kuhusu Obstruction of Justice? Ni page namba ngapi ya ripoti?
Congress imeona tatizo na hivyo kuamua kuita akina McGahn, Barr na Mueller kueleza kwa kina
Wakwanza atakuwa AG Barr ambaye hakuna shaka akaangwa kama firigisi kwa kulisha umma matango pori. Halafu atafuata Mueller atakayeitetea taarifa yake.
Mpangilio huo haumpi Barr nafasi ya kujificha chini ya kivuli cha Mueller wala kuongopa tena
Don Mcgahn naye ataitwa kutetea ushahidi wake wa masaa 30 kwa tume ya Mueller
House Judiciary Committee ime-issue subpoena kwa ajili ya ushahidi wa McGahn sawa! Ila hebu tujiulize, huyu mtu ameshahojiwa na Mueller kwa zaidi ya masaa 30 na ushahidi wake upo kwenye ripoti ya Mueller, kuna kitu gani cha ziada ambacho Democrats wanatafuta ambacho Mueller alishindwa kukipata kwake? Jibu ni hakuna! Kwanini wasitumie ushahidi aliokwishatoa?
Mueller atazungumzia ripoti yake! So hamna kipya!
Barr atasimamia alichokisema.
Lakini swali la msingi, kama Democrats wana uhakika na wanaona Obstruction of Justice kwa Trump kwanini wasiendelee na hitimisho la uchunguzi tuone watakapofika! Badala ya kurudia kuhoji watu ambao wameshahojiwa!!
WH imeshtuka kwani suala la obstruction of justice limeelezwa kwa kina na Mueller
Sasa Rais Trump na WH hawataki washauri kuitwa mbele ya kamati za Bunge
Wanataka kutumia executive privilege ingawa ina ukomo wake kwa hali ilivyo.
Swali linarudi kwa AG Barr, ikiwa alihakikishia umma kwamba WH ilitoa ushirikiano 100%, ni vipi basi WH hiyo hiyo haitaki watu kuhojiwa na kamati za Bunge?
Swali kwa Rais Trump. Ikiwa taarifa ilimsaifisha nini kinamtisha hadi kuzuia watu kutoa ushuhuda mbele za kamati za Bunge? Nini anahofia na nini anaficha ikiwa taarifa ilimsafisha!
Kwanini House Judiciary Committee wasitumie ushahidi ambao Mueller anao kufanya maamuzi? Tumeambiwa "Mueller alitaka kesi ya Obstruction of Justice iamuliwe na Congress". White House wanachotaka ni Dems waamue chochote kutokana na hiyo ripoti, Dems wanashindwa nini kuamua hadi kutaka kuanza kurudia kuhoji watu?
White House watoe ushirikiano mara ngapi? Trump angekuwa na nia kuficha mawasiliano ya maafisa wa WH angetumia executive priviledge kuyaficha kwenye ripoti ya Mueller! Hao Dems wanashindwa nini kuendelea na hitimisho la uchunguzi wao?
Kama mtakumbuka tulisema drip drop zitammaliza Trump. Kila uchao magazeti yanadonsha kitu hata kumpelekea Mzee atoe tweet 50 katika masaa 24. Hili si bure kuna kihororo na mshawasha
Tatizo Dems wanahangaika na Trump sana! Kiasi kwamba wanajichanganya hawajui wanachokitafuta.