Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Kuna watu wanaongozwa na hisia zaidi kuliko FACTS kwenye suala zima la kutolewa ripoti ya Mueller. Kwa sababu mtu hajamsikiliza Bill Barr anasemaje tayari ameshaandika atachokisema au atakachokimaanisha!! Amazing!

Barr anachokifanya ni kufuata sheria na kanuni za DOJ, asipozifuata haohao Democrats ndio watakuwa wa kwanza kumtaka aondoke kwenye nafasi yake kwa kushindwa kufuata sheria na kanuni za DOJ.
FACTS and Trump? Are you for real dude? I doubt it, I really doubt it very very much. Anyway, I don't blame you...maybe you are listening too much to Trump's mouthpiece, FOX NEWS just like TUJITEGEMEE and company...😁!
 
TAARIFA 'NUSU' HADHARANI
NI MBAYA , INA MATATIZO NA ITAENDELEA

Sehemu ya I

Kwa wafuatiliaji wa uzi huu, lengo kubwa ni kujaribu kwa kiasi kinachowezekana kuwapa Wananchi popote walipo habari za siasa ndani ya viunga vikubwa vya DC

Uzi una miaka zaidi ya miwili na mabandiko mengi tu. Uzi haukusudii kuleta ushidani bali kufafanua mambo ambayo katika siasa za nchi masikini ni nadra kuyaona

Lengo kuu kama ilivyosema si kukata habari zilizoandikwa kishabiki, si kuweka picha wala si kuzogoana. Kila mwenye mtazamo na mwenye kitu tofauti ni vema akakianisha

Ile taarifa ya Mueller iliyohaririwa sasa ipo wazi. Ni taarifa nusu kwani mengi yamefichwa katika mwamvuli wa classified info, intelligence, Grand jury and Witness ambao si indicted

Nitoe tahadhari tu kuwa mtiririko hautafuta habari iliyopo bali yaliyojiri bila mpangilio maalumu
Kutakuwa na mabandiko mengi tukiunga vipande.
Kwa kuanzia turudi na kuudurusu uzi toka mwanzo

1. Tulisema zipo habari za Russia kuingilia uchaguzi wa Marekani kwa lengo la kumsaidia Trump kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari. Mueller amethibitisha hilo katika taarifa

2. Tukaeleza vyombo vya habari vya Marekani si kama vya nchi masikini. Kuna professional journalist ambao hata kama ni miaka 20, habari za uchunguzi watazikamilisha
Tuliambiwa ni Fake news kwa msemo wa Trump uliodakwa na wafuasi wanaomeza
Mueller amethibitisha hilo

3. Tukasema katika nchi ya Marekani sheria hufuata mkondo wake. Mueller kalionyesha hilo

4. Tukasema Rais Trump anatishika sana na uchunguzi. Mueller kalieleza vizuri sana

5. Tukasema collusion si uhalifu. Leo wafuasi na mashabiki wa Trump hawataki kulitumia neno hilo isipokuwa wale wasioelewa nini wanasema. Hata Lawyer wa Trump wanalikimbia
Mueller kaeleza hilo

6. Tukasema collusion si tishio, tishio ni obstruction of justice. Leo hoja ya obstruction of justice imemnyong'onyeza Trump na ni tishio kubwa kuliko alivyodhani. Mueller kaeleza hilo

7. Tukafafanua kuhusu taarifa ya Bill Barr kuwa ilikuwa ya kisiasa na kwamba ile summary yake ilikuwa kutafuta headlines. Leo taarifa inamsuta bila kupepesa
Tukasema analisha mazezeta matango pori, Mueller kaanika kila kitu

8. Tukasema kuna uchafu unafichwa. Pamoja na taarifa iliyohaririwa bado uchafu unaonekana achilia mbali ulio chini ya kapeti. Mueller kaonyesha

9. Tukasema Mueller anajua mengi kuliko tweets na habari za kila siku. Mueller kaonyesha hilo

Kwa ufupi kila kilichojadiliwa kimetoka na majibu iwe sahihi au la , majibu yapo

10. Tukasema kuna sababu za Mueller kutotoa hatma ya obstruction of justice
Sasa tunajua ni kwanini na sababu tulizosema zinasimama wima. Mueller kathibitisha

Tukasema ''the devil is in the details'' Je, leo kuna aliyeona devil? Au ni kusikiliza FM station

Sasa tunakwenda hatua ya kujadili nini Mueller alikusudia na siyo habari za AG Barr aliyepoteza heshima yake. Tulionya habari za taarifa zake zilikuwa za kisiasa kizushi na kupotosha
Walioelewa wakiwemo Republicans na WH walikaa kimya, masikini nyumbu waliendelea tu

Inaendelea....
 
TAARIFA HADHARANI
Sehemu ya II

Taarifa ya Mueller imeandikwa kiufundi sana na kitaalamu kiasi kwamba anayesoma hataweza kuona uzito wake. Anayesoma na kuelewa anasoma nini ni taarifa mbaya sana

AG Barr leo ameita mkutano wa vyombo vya habari baada ya kukaa kimya taarifa yake ikipotosha umma kwa wiki 3. Rais Trump alisema no collusion no obstruction bila watu kuwa na taarifa

AG katika summary yake alieleza mambo mawili, no collusion no obstruction kama Trump
Leo tena katika kukimbia ukweli karudi maneno hayo mara zaidi ya 6 huku akieleza jinsi Rais alivyokuwa frustrated n.k. kana kwamba ni lawyer wa Trump. Tulijua njia ya muongo ni fupi

Collusion: Huko nyuma tulisema ka tafsiri collusion si neno linalomtia mtu hatiani, ni kutenda jambo kwa njia za siri. Hivyo Russia collusion ni msemo wa Trump akipoteza watu

Hata wanasheria wake na wasaidizi walidaki neno hilo bila kujua maana yake
AG Barr naye kadakia tu bila kujua kwa tafisri halisi collusion haina maana ya uhalifu

Kitu kilichokuwa kinaangaliwa na Mueller ni conspiracy ambayo kisheria ni kosa
Taarifa ya Mueller imesema haiku ''establish'' collusion kati ya Trump na Russia.

Hata hivyo imeonyesha uwepo wa mawasiliano ambayo si lazima yawe uhalifu

Mueller anasema Russia waliwazengea akina Trump kampeni kwa lengo ovu
Kampeni ya Trump ilijua na haikuchukua hatua zozote za kutoa taarifa kuhusu nchi hasimu kuingilia uchaguzi kwa lengo la kumsaidia Trump

Kampeni ya Trump ilifahamisha na vyombo vya usalama kuhusu Russia, kampeni haikuchua hatua. Taarifa ya Mueller inaonyesha contact zilizokuwepo kati ya Trump kampeni na Russia

Mueller anamalizia hilo kwa kusema Russia walingilia uchaguzi kwa lengo la kumsaidia Trump. Mueller kaonyesha kauli ya Trump na mahusiano ya kutolewa emails kutoka Russia

Hapa kuna hoja ya kisheria. Hata kama Rais Trump alishirikiana na vyombo vya usalama vya Russia, ni lazima uwepo ushahidi wa kutosha kuhusu hilo.

Kwahiyo ukitazama taarifa ya Mueller, inasema hakuna collusion, lakini inaonyesha mahusiano kati ya kampeni ya Trump na Russia. Soma hapa
Hapa ndipo neno 'establish' linapoingia, kwa maana ni lazima uwepo ushahidi wa kutosha.

Kwa kuelewa tofauti ya collusion, conspiracy na yaliyojiri, ni wazi kulikuwa na lengo ovu, kuachia Russia ambayo ni nchi hasimu kuingilia uchaguzi wa Marekani

Wanasheria wa Trump wanakimbia neno collusion kwasababu ikiwa hakuna collusion, contact zilizopo zinageuka kuwa conspiracy kama alivyoonyesha Mueller.

Hivyo, kuwepo kwa interference kumethibitishwa. Kushiriki kwa kukaa kimya kumethbitishwa

'' They also discussed the status of the Trump campaign and Manafort's strategy of winning democratic votes in mid western states. Months before that meeting, Manafort had caused internal polling data to be shared with Kilimnik and the sharing continued for some period of time after their August meeting''

Na kwamba kukaa kimya kuliepusha collusion imethibitishwa, hata hivyo hiyo haimaanishi kampeni ilitenda jambo jema. Ilipaswa kutolewa taarifa kwa vyombo vya habari

Ukimuona mtu anatumia neno collusion basi hajui uzani wake ulivyo mwepesi.
Neno halisi lenye maana ni no conspiracy. Tuliwahi kusema siku ningi collusion si uhalifu

Inaendelea,
 
TAARIFA HADHARANI

Sehemu ya III

AG Barr katika taarifa yake ya mwanzo na leo anasema hakuna obstruction of justice
Taarifa ya Mueller imeonyesha kwa kina suala hilo na kwamba haikueleza Barr atoe ufafanuzi

Barr alijivika mamlaka kwa kusema ''sheria za DOJ' zinamtaka ikiwa hakuna hitimisho basi yeye afikie hitimisho hilo. Huu ni uongo wa hali ya juu ambao leo unamwacha Barr uchi wa mnyama

Tulieleza huko nyuma kuwa Mueller ni mwajiriwa wa DOJ na kwamba, kanuni za DOJ zinasema haiwezi kumshtaki Rais aliye madarakani. Mueller na timu yake walielewa hilo
Hapa anasema

'' And apart of OLC's (office of legal council) constitution view, we recognized that a federal criminal accusation against sitting president would place burdens on the president's capacity to govern and potentially pre empty constitution processes for addressing presidential misconduct''

Ukisoma taarifa ya Mueller, ni kwamba ameanisha mambo 10 kwa kina yanayoonyesha ushahidi wa kutosha wa obstruction of justice. Mueller akasema ikiwa Rais asingekuwa amefanya kosa la obstruction of justice tungesema hivyo. Mueller akaachi hapo

Maana yake ni kuwa Mueller hakufikia tamati kwasababu angefanya hivyo ingelazimu DOJ afungue mashtaka kinyume na kanuni za kumshtaki Rais aliye madarakani

Mueller akawezaka facts akijua suala hilo litashughulikiwa na congress kimamlaka
Ndiyo msingi wa kusema hivi potentially pre empty constitution processes for addressing presidential misconduct''


Ushahidi ulitolewa na watumishi wa WH hauna shaka kuwa walimzuia si mara moja au mbili, ni mara nyingi Rais Trump asimfukuze Mueller . Hiyo ni obstruction of justice

Kitu kimoja kilichojionyesha, wakati Trump akiwa bingwa wa tweets na majigambo kumbe hana ''guts' za kufukuza bali kuwatumia watu waliomkatalia wakijua ni ukiukwaji wa sheria


Barr na jitihada zake wamejikuta wakiangukia pua, ni wazi Mueller hajamsafisha Trump na kwamba kuna tuhuma nzito sana za Obstruction of justice

Leo Trump hakuongea na waandishi kama ambavyo angeongea ikiwa ni jambo la ushabiki
No collusion no obstruction ni kitu kigumu sana kwasasa kwa upandw wa Trump

Leo AG Barr alikuwa na deputy Roseinstein.
Hakuna mahali Mueller anatokea kwasababu maalumu. Mueller anajua kuna upotoshaji

Hata suala la obstruction of justice , AG Barr amekubali kuwepo kwa tofauti ya tafsiri kati yake na ile ya Mueller kwa maana kuwa kama alivyoandika kabla ya kuwa AG maoni yake ndiyo anataka yawe ya Mueller

Ngoma inakuwa nzito kwasababu kamati za bunge zitamwita Mueller.
Taarifa ipo wazi na ile iliyofichwa italetwa kwa ulazima.
Mueller ataendelea kumwaga radhi itakayomtafuna Trump

Republicans wamelalamika kuwa mkakati wa Barr unachagiza sana habari kuliko kuzima

Taarifa ya awali na ya leo vimeondoa imani ya watu kwake, na kwamba sasa watu wanautafuta ukweli wenyewe.

Hapo lazima taarifa nzima na madudu yake yatakuwa hadharani

Je, si kweli kuwa tulisema drip drop zitaendelea na kumtafuna Trump?
Leo kibao kimebadilika kabisa, Russia imechukua sura mpya, donda ndugu!

Inaendelea....
 
AG BILL BARR NA UNAZI WA KISIASA

Sehemu ya IV

Ikumbukwe kuwa AG Barr aliandika barua kwa wanasheria wa Trump kuhusu obstruction of justice akipinga uwepo wa jambo hilo.

Kupitia barua hiyo ya kurasa 19 ndipo alipoteuliwa kuwa AG na Trump kwa imani ya kumlinda

Barr amekuwa shabiki mzuri wa Trump na kutelekezaa majukumu yake ya AG wa US
Jana alikutana na waandishi kabla ya taarifa akijua yapo maswali mazito yanayomkabili

Barr alisema WH imetoa ushirikiano wa kila aina kwa Mueller. Well sasa inajulikana Trump alikataa kwenda mbele ya kamati, na majibu aliyotoa 30 ni yale ya ''sikumbuki, sina kumbu kumbu''. Trump hakutoa ushirikiano kama Barr alivyosema

Orodha ya uzushi wa Barr ni ndefu na taratibu anaandamwa aachie ngazi.

Huenda hataweza kuachia lakini hali inayomkabili kwenda mbele ni mbaya
Ameshaitwa mbele ya kamati ya sheria na usalama ya Bunge

Hayo yakiendelea Dems wamemtaka Barr atoe taarifa yote kwa lazima subpoena
Wametaka Mueller aende mbele ya kamati kupata undani zaidi

Barr ataumbuka, ineleweka alikuwa na mgogoro na taarifa kuhusu obstruction of justice
Mueller ataeleza nini alifikiri na Barr atatokea upande mwingine bila fursa ya kufinyanga uongo

Msome Mueller hapa chini

''The evidence we obtained about the president's actions and intent presents difficult issues that would need to be resolved if we were making a traditional prosecutorial judgement. At the same time , if we had confidence after a through investigation of the facts that the president clearly did not commit obstruction of justice, we would state so.
Based on the facts and the applicable legal standards , we are unable to reach the judgement''


AG Barr akatoka na page 4 (bandiko 765) akiwatia watu kimuhe muhe kuwa Mueller ameshindwa kufikia tamati ya suala hilo, hola ! hakuna kitu n.k bila kujua details.
Ndiyo maana tuliwakubusha ule msemo wa watu '' the devil is in the details''

Of course Barr akifanya kazi ya Trump alijua atawazoa tu, wapo.

Wajuvi wa siasa za viungani DC walijua shauku ile ya Barr ni ya kisiasa na haina ukweli wowote

Mbele ya kamati Barr hana pa kukwepa, atakutana na kamera na utaona aanavyohangaika na kujivunjia heshima yake. Taarifa ya Mueller ni mbaya kwa kila mtazamo, Trump ameiona na sasa ana tweet hovyo hasa akikumbuka alivyokaangwa na wasaidizi wake

Inaendelea..
 
Taarifa ya Mueller ni mbaya kwa kila mtazamo, Trump ameiona na sasa ana tweet hovyo hasa akikumbuka alivyokaangwa na wasaidizi wake
Mkuu Nguruvi3, tofauti ya taarifa ya Mueller na ile ya Barr ni kama mbingu na nchi. Taarifa ya Mueller imemkaanga Trump kweli kweli na kumuacha uchi wakati ile ya Barr ni kama inamtupia kipande cha kanga aweze kujisetiri. Hii ndiyo sababu wapo watu kutoka ofisi ya Mueller walisikika wakilalamika kuwa Barr anapotosha ripoti nzima. Uongo wote wa Trump na wafuasi wake umeanikwa na utaendelea kuanikwa hivyo sasa wakae wasubiri tu moto uwake uwachome na kuwaumbua . Ndiyo maana nilimwambia ndugu yangu TUJITEGEMEE kuwa asipende sana kujadili mambo ya Marekani kwa jicho la Kitanzania. Nixon alikuwa na kiburi kuliko Trump lakini alikwenda na maji.

trumplies-jpg.1076084

Hayo ni baadhi tu ya uongo wa Trump lakini inayofunga mwaka ni ya Barr. Ripoti ya Barr imedai Mueller hakushauri ripoti yake ishughulikiwe na Congress baada ya kuona madudu ya Trump. Alishauri na kuwaachia wawakilishi wa wananchi ndio walishughulikie ripoti hii na si AG aliyeteuliwa na mtuhumiwa.
 
DON McGAHN ALIVYOMNUSURU RAIS TRUMP
GOLDEN STD YA MUELLER SASA NI SHUBIRI

Siasa kongwe ndani ya jimbo la DC na viunga vyake hazihitaji kubeba kila kitu kama mwenge

Baada ya AG Barr kutoa headline aliyoiita summary ulimwengu ulibaki na mshangao mkubwa

Watu makini hawakudandia treni kwa mbele, walivuta pumzi wakijua nini kinajiri viungani DC

Watu 2 waliamua kujitoa Muhanga kwa kuelewa au kutoelewa, Trump na Kellyanne Conway

Rais Trump alibadili kibao ghafla akimwita Mueller kama mtu smart anayejiheshimu
Trump akaisifia taarifa ya Mueller kupitia summary mbovu ya Barr masikini bila kujua

Mpambe wake ambaye ni mshauri mwanamama Kellyanne akaiita taarifa kama golden std

Wazoefu na wajuvi wa siasa za DC walivuta pumzi wakijua 'the devil is in the details''

Walijua kusomewa habari na AG Barr ni sawa na kufakamia matango pori

Taarifa ya Barr ikasambazwa kila kona ya duru za siasa kama mwenge!

kila aiyepa fursa aliinukuu kwa kicheko, hakuna kitu, hola, no collusion no obstruction

Baada ya taarifa iliyohaririwa kutoka siku ya alhamisi madhari ya kisiasa DC ina uelekeo mpya

Waliovuta pumzi wakitafuta details wamefanikiwa kuona 'the devil''.

Mwanamana Kellyanne katoweka katika anga za habari akiikwepa taarifa aliyoiita golden std

Trump aliyekuwa aongee na vyombo vya habari baada ya uzushi wa Barr aliingia mitini Florida

Asubuhi ya leo ni kama alinyweshwa pombe ya ndaza. Ameamka akiandika tweet za kuilaani taarifa ya Mueller na yaliyomo kwa kina, ghadhabu na jazba. Mzee ni kama kapagawa

Tumaini lililobaki ni AG na DOJ kugoma kutoa sehemu ya taarifa iliyofichwa ambayo kuna Wikileaks na taarifa nyingine za 'counter intelligence' ambazo tayari inajulikana zilimtaja Mzee

Taarifa zilizokatwa ''redacted' inaelezwa ni chafu ambazo Republicans wasingesubiri tena

Ndani ya DC hata hiyo redacted part ya taarifa itavuja. Kilichokuwa kinasubiriwa ni DOJ kutoa redacted ili wajuvi wamwage radhi kwani wakati huo haitajulikana kama ni watu wa Mueller au wa DOJ. Hoja itakuwa moja, walioiona ni wengi na hakuna atakayebainika ikiwa ataitoa

Rais Trump anapotafkari kombora la kwanza, na kujiuliza kombora la mafichoni limebaba nini anabaki na hofu na kutweta.

Kichekesho kikubwa ni tweet ya leo akilaani lawyer kuchukua notisi wakati wa maongezi naye
Huyu alikuwa mshauri wake Bwana McGahn

McGahn ndiye aliyemsaidia kuitwa Rais hadi siku ya leo.

McGahn alikataa hoja za Trump za kumfukuza Mueller akitishia kujiuzulu.
Laiti isingalikuwa hivyo, kungekuwa na Saturday massacre namwisho wa Urais kama alivyotabiri

Huku mambo ya Trump yakiangaliwa kwa jicho pembe na wapi pa kumtokea, mtu anayepumua kwa mashine ni AG Barr.

Pamoja na jeuri yake leo hana credibility na kamati za Bunge zinamsubiri kumvua kile kinguo kidogo cha ndani, na pengine hatasubiri kuchutama!

Tusemezane
 
VIUNGANI DC WIKI HII
WH YAKATAA WATUMISHI KUHOJIWA

Huko nyuma katika uzi tulisema kinachoitwa collusion si tishio kama obstruction of justice

Tulitoa mfano wa sakata la Bill Clinton liloanza kwa mambo ya nje, ngono na kuhitimishwa na obstruction of justice. Kinachoendelea DC si tofauti na tulichozungumza

Wiki tatu zilizopita tulisema AG Barr anatumika tu na WH na ile credibility yake imeondoka
Barr alisimama na kusema hakuna collusion ingawa si neno la kisheria
Taarifa ya Mueller inaeleza mahusiano yalikuwepo kati ya kampeni ya Trump na Russia

Barr akasambaza vihabari vya kutunga ( Bandiko 765) na kurudia tena alhamisi iliyopita
Katika mengi yaliyomo, Barr alidai Mueller hakufikia tamati kuhusu obstruction of justice
Taarifa inaonyesha kinyume kabisa kwani Mueller aliweka mazingira ya mashtaka Congress

Mueller alieleza kuhusu jitihada za Rais Trump kufanya obstruction of justice akiokolewa na washauri wake waliokataa kutekeleza maagizo wakijua madhara yake
Mmoja wa watu walioeleza kwa kina ni Don McGahn ambaye kiuhalisi aimnusuru sana Trump

Congress imeona tatizo na hivyo kuamua kuita akina McGahn, Barr na Mueller kueleza kwa kina
Wakwanza atakuwa AG Barr ambaye hakuna shaka akaangwa kama firigisi kwa kulisha umma matango pori. Halafu atafuata Mueller atakayeitetea taarifa yake

Mpangilio huo haumpi Barr nafasi ya kujificha chini ya kivuli cha Mueller wala kuongopa tena
Don Mcgahn naye ataitwa kutetea ushahidi wake wa masaa 30 kwa tume ya Mueller

WH imeshtuka kwani suala la obstruction of justice limeelezwa kwa kina na Mueller
Sasa Rais Trump na WH hawataki washauri kuitwa mbele ya kamati za Bunge
Wanataka kutumia executive privilege ingawa ina ukomo wake kwa hali ilivyo

Swali linarudi kwa AG Barr, ikiwa alihakikishia umma kwamba WH ilitoa ushirikiano 100%, ni vipi basi WH hiyo hiyo haitaki watu kuhojiwa na kamati za Bunge?

Swali kwa Rais Trump. Ikiwa taarifa ilimsaifisha nini kinamtisha hadi kuzuia watu kutoa ushuhuda mbele za kamati za Bunge? Nini anahofia na nini anaficha ikiwa taarifa ilimsafisha!

Kama mtakumbuka tulisema drip drop zitammaliza Trump. Kila uchao magazeti yanadonsha kitu hata kumpelekea Mzee atoe tweet 50 katika masaa 24. Hili si bure kuna kihororo na mshawasha

Tusemezane
 
Ripoti ya Mueller imegawanywa sehemu mbili:
Volume I: Matokeo ya uchunguzi wa Special Counsel wa Russia kuingilia uchaguzi wa Urais wa mwaka 2016 na mahusiano na Kampeni ya Trump (Page 1-198)
Volume II: Matendo ya Rais dhidi ya uchunguzi wa FBI wa Russia kuingilia uchaguzi wa Urais wa mwaka 2016 na mambo yanayohusiana na hayo, na matendo yake dhidi ya uchunguzi wa Special Counsel (Page 1-182)

Volume I:
Nimesoma ripoti maana nilitaka nijiridhishe kwanza na sio kusikiliza vyombo vya habari vinasemaje kisha kuandika maoni yao humu. Uchunguzi umemalizika kwa Special Counsel kusema hakuna njama (conspiracy) au ushirikiano (coordination) baina ya Timu ya kampeni ya Trump na Serikali ya Russia kuingilia uchaguzi wa US mwaka 2016.

"The investigation did not establish that members of the Trump Campaign conspired or coordinated with the Russian government in its election interference activities" (Page 2, Parag 1.Vol I).

Wale wenzetu waliokuwa wanadai Trump anamtumikia Putin au Russia wameumbuka na watarukia kwingine.

Ni upotoshaji kusema "collusion" ni msemo wa Trump akipoteza watu. Ukisoma ripoti Mueller anasema neno "collusion" ilitumika katika mawasiliano yake na Acting AG na katika mawasiliano ya umma juu ya uchunguzi.

"the word collude was used in communications with the Acting AG confirming certain aspects of the investigation's scope and that the term has frequently been invoked in public reporting about the investigation" (Page 2, Parag 4, Vol I).

Pia kuhusu neno "coordination", Muller akaamua ili kuwepo "coordination" lazima kuwepo na makubaliano baina ya serikali ya Russia na Kampeni ya Trump kuingilia uchaguzi. Kitu ambacho kimethibitika hakikuwepo.

"Like collusion, coordination does not have a settled definition in federal criminal law. We understood coordination to require an agreement- tacit or express- between the Trump Campaign and the Russian government on election interference" (Page 2, Parag 4, Vol I).

Kwahiyo, maneno "collusion" au "coordination" sio ya Trump per se, Trump aliyachukua kutoka kwenye Media na Congress, pia katika Order No. 3915-2017 (Appendix A ya Ripoti ya Mueller) ya kumteua Mueller hakuna neno "conspiracy"!

Kusema kuwa watu wanakimbia au wamedakia neno "collusion" au wanaogopa "conspiracy", ni upotoshaji, kwa sababu mtu anaogopaje kitu kilichochunguzwa tayari na hamna aliyepatikana na hatia nacho? Tusipotoshe! Wanaokimbia collusion na conspiracy hasa ni Democrats na wafuasi wao maana imethibitika hamna kitu. Haya ndio madhara ya kubeba kila unachokisikia kwenye vyombo vya habari kama maoni binafsi bila kusoma ripoti.

Kwamba ikiwa hakuna collusion contacts zilizopo zinageuka kuwa conspiracy, ni upotoshaji mwingine na ni kitu kisicho na maana, imeonyeshwa wapi kwenye ripoti ya Mueller?

Ni vizuri kuelewa kwanini Mueller alitumia "conspiracy" badala ya "collusion" kwenye ripoti yake. Kosa la "Collusion" halimo kwenye sheria na pia sio neno linalotumika kwenye sheria za jinai ambazo hutumika kwenye mashtaka, sio suala la uzani.

"In evaluating whether evidence about collective action of multiple individuals constituted a crime, we applied the framework of conspiracy law, not the concept of collusion" (Page 2, Parag 4, Vol I)

"Collusion is not a specific offense or theory of liability found in the U.S. Code, nor is it a term of art in federal criminal law"(Page 2, Parag 4, Vol I).


Sio kwamba "collusion" sio kosa, ni kosa, ila kwenye sheria linatumika "conspiracy" ambalo kimantiki lina maana ileile, ndio maana Mueller amelitumia. "Collusion" ingekuwa sio kosa kusingekuwa na haja ya uchunguzi.

Mawasiliano yote baina ya maafisa wa Kampeni ya Trump na watu wanaohusiana na Russia, yamechunguzwa kama yanaweza kuwa na "conspiracy".

"The office considered in particular whether contacts between Trump campaign officials and Russia linked individuals could trigger liability for the crime of conspiracy- either under statutes that have their own conspiracy language or under general conspiracy statute (Page 180, Parag 2. Vol I).

Na Mueller hajaona ushahidi wa "conspiracy" au makosa yoyote kisheria kwenye hayo mawasiliano . Ukisoma uamuzi wa kushtaki wa Special Counsel, hajaona ushahidi wa kosa kisheria.

"While investigation identified numerous links between individuals with ties to the Russian government and individuals associated with the Trump campaign , the evidence was not sufficient to support criminal charges" (Page 8, Parag 7. Vol I)

Kusema kwamba Timu ya Kampeni ya Trump wamekosea kwa kukaa kimya bila kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu nchi hasimu kuingilia uchaguzi na hivyo kuepusha "collusion" ni upotoshaji wa taarifa ya Special Counsel kwa sababu hayajaelezwa popote kwenye ripoti ya Mueller.

Kwahiyo, Trump na AG Barr wapo sahihi kusema hakuna "collusion", hakuna "conspiracy" wala hakuna "coordination" baina ya Team Trump na watu wanaohusishwa na Serikali ya Russia, maana hayo ni maneno ya Mueller na yapo kwenye ripoti yake.
 
2. Tukaeleza vyombo vya habari vya Marekani si kama vya nchi masikini. Kuna professional journalist ambao hata kama ni miaka 20, habari za uchunguzi watazikamilisha Tuliambiwa ni Fake news kwa msemo wa Trump uliodakwa na wafuasi wanaomeza Mueller amethibitisha hilo
Vyombo vya habari vya Marekani vimeegemea vyama na itikadi za kisiasa, professional journalism hamna katika vyombo hivyo, ndio maana ukiwasikiliza unatakiwa uchanganye na zako. Vinginevyo utashindwa kuegemea ukweli. Neno "Fake News" limekuwa maarufu kwa sababu watu wanaona wanavyopewa taarifa zenye maslahi fulani huku taarifa zingine zikiminywa kwa makusudi.
3. Tukasema katika nchi ya Marekani sheria hufuata mkondo wake. Mueller kalionyesha hilo
Nchi yoyote inayofuata utawala wa sheria, sheria hufuata mkondo wake.
4. Tukasema Rais Trump anatishika sana na uchunguzi. Mueller kalieleza vizuri sana
Mueller hajatumia neno "kutishika" katika ripoti yake, bali Trump "kukasirishwa" au "kulalamika" kwa kuwepo kwa uchunguzi na taarifa kwa umma kuwa yeye binafsi anachunguzwa.

"President was angered by both existence of Russia investigation and the public reporting that he was under investigation, which he knew was not true based on Comey's representations" (Page 61, Parag 4, Vol II).

"President complained to his advisors that if people think Russia helped him with the election, it would detract from what he had accomplished" (Page 61, Parag 4, Vol II).

"President complained that the perception that he was under investigation was hurting his ability to conduct foreign relations , particularly with Russia" (Page 61, Parag 5, Vol II).


5. Tukasema collusion si uhalifu. Leo wafuasi na mashabiki wa Trump hawataki kulitumia neno hilo isipokuwa wale wasioelewa nini wanasema. Hata Lawyer wa Trump wanalikimbia Mueller kaeleza hilo
Mueller hajasema kuwa collusion sio uhalifu bali amesema kosa la "Collusion" halimo kwenye sheria na pia sio neno linalotumika kwenye sheria za jinai ambazo hutumika kwenye mashtaka.

"Collusion is not a specific offense or theory of liability found in the U.S. Code, nor is it a term of art in federal criminal law"(Page 2, Parag 4, Vol I).

Kusema kwamba wafuasi na mashabiki wa Trump hawatumii neno "collusion" sio kweli, kwa sababu hata Trump bado analitumia. Na sasa hivi wameongeza na "no conspiracy" baada ya Muller kusema (Page 2, Parag 1.Vol I) kuwa hamna conspiracy pia.

6. Tukasema collusion si tishio, tishio ni obstruction of justice. Leo hoja ya obstruction of justice imemnyong'onyeza Trump na ni tishio kubwa kuliko alivyodhani. Mueller kaeleza hilo.
Mueller amechunguza "conspiracy" badala ya "collusion" wakati kwenye Order No. 3915-2017 (Appendix A ya Ripoti ya Mueller) alielekezwa achunguze "links" na "coordination", lakini ameeleza vizuri sababu kwanini amefanya hivyo. Kwahiyo kusema kwamba "collusion" sio tishio ni upotoshaji maana angepatikana na hatia nayo tungekuwa tunaongea mengine sasa hivi.

Hoja ya "Obstruction of Justice" Mueller mwenyewe kachemka, akawa anatafuta pa kushika kwenye ripoti yake, kama alivyoeleza "difficult issues" kwenye "Overaching Factual Issues" (Page 156-158 Vol II).
7. Tukafafanua kuhusu taarifa ya Bill Barr kuwa ilikuwa ya kisiasa na kwamba ile summary yake ilikuwa kutafuta headlines. Leo taarifa inamsuta bila kupepesa Tukasema analisha mazezeta matango pori, Mueller kaanika kila kitu
Taarifa ya Barr ambayo ilikuwa ni summary ya ripoti ya Mueller ime-capture vitu muhimu sana kama ukisoma ripoti ya Mueller na hauwezi kuibeza. Barr na Rosenstein walichofanya ni ku-summarize ripoti na conclusions za Mueller. Kitu gani alichokisema Barr ambacho hakipo kwenye ripoti ya Mueller? Hayo "matango pori" ya Barr ni yapi? Hebu tuwe specific.
8. Tukasema kuna uchafu unafichwa. Pamoja na taarifa iliyohaririwa bado uchafu unaonekana achilia mbali ulio chini ya kapeti. Mueller kaonyesha
Uchafu upi uliofichwa? Barr alieleza kuwa hakuna Obstruction of Justice, Mueller ameshindwa kuhitimisha kwa sababu ya yale aliyoyaita "difficult issues".
9. Tukasema Mueller anajua mengi kuliko tweets na habari za kila siku. Mueller kaonyesha hilo Kwa ufupi kila kilichojadiliwa kimetoka na majibu iwe sahihi au la , majibu yapo
Uchunguzi wa karibia miaka miwili na kuunguza karibia USD 30 Millioni, kutoa zaidi ya subpoenas 2800, karibia search warrants 500, zaidi ya Order 230 za mawasiliano, zaidi ya Order 50 za matumizi ya Pen Registers, maombi 13 kutoka nchi za kigeni, kuhoji karibia mashahidi 500 (Page 13, Parag 3.Vol I). Lakini mwishowe collusion na conspiracy hakuna! Obstruction imebaki inaelea hewani bila kosa la msingi (underlying crime)!.
10. Tukasema kuna sababu za Mueller kutotoa hatma ya obstruction of justice Sasa tunajua ni kwanini na sababu tulizosema zinasimama wima. Mueller kathibitisha
Kwamba aliachia Congress? Ingawa naunga mkono Congress wakatolee uamuzi suala la Obstruction of Justice ila hamna sehemu yoyote kwenye ripoti ya Mueller ambapo amesema ameshindwa kutoa hatma kwa sababu ameliachia Congress. Tusipotoshe.
 
Volume II: Matendo ya Rais dhidi ya uchunguzi wa FBI wa Russia kuingilia uchaguzi wa Urais wa mwaka 2016 na mambo yanayohusiana na hayo, na matendo yake dhidi ya uchunguzi wa Special Counsel (Page 1-182).

Uchunguzi wa kuzia haki (obstruction of justice) ulilenga kujua kama Rais Trump alizuia haki katika uchunguzi wa FBI uliohusu Russia na katika uchunguzi wa Special Counsel dhidi yake. Mueller ameelezea namna hatia ya kuzuia haki inavyopatikana kisheria (legal framework of obstruction of Justice) na kutaja mambo matatu (3) ya msingi yanayoangaliwa mara kwa mara (Page 9-10, Vol II).

Ameyataja kuwa ni tendo la kuzuia (obstructive act), uhusiano wa tendo la kuzuia na uchunguzi unaoendelea (a nexus between the obstructive act and an official proceeding) na nia ya uovu (corrupt intent). Lakini pia ameandika mengineyo kama kuingilia mashahidi (witness tampering), majaribio na jitihada (attempts & endeavors).

Uchunguzi pia umesema kuwa uthibitisho wa kuwa kuna "nia ya uovu" huwa unapatikana kwenye ushahidi wa kimazingira (circumstantial evidence).

"In assessing the evidence we obtained, we relied on common principles that apply in any investigation. The issue of criminal intent is often inferred from circumstantial evidence" (Page 13, Parag 3, Vol II).

Kwenye "Factual results of the Obstruction Investigation" (Page 15-156 Vol II), ripoti imeelezea ushahidi uliokusanywa kwenye maeneo kumi na moja kuhusiana na suala la kuzuia haki (Obstruction of Justice).

A. The campaign's response to reports about Russian support for Trump
B. Conduct involving FBI Director Comey and Michael Flynn
C. The President's reaction to the continuing Russia investigation
D. The President's termination of Comey
E. The Appointment of Special Counsel and efforts to remove him.
F. Efforts to curtail the Special Counsel's investigation
G. Efforts to prevent public disclosure of evidence
H. Further efforts to have the Attorney General to take control of the investigation
I. Efforts to have McGahn deny that the President had ordered him to have the Special Counsel removed.
J. Conduct towards Flynn, Manafort,
K. Conduct involving Michael Cohen


Wakachambua ushahidi waliokusanya kulingana na mambo matatu (3) ya msingi yaliyopo kwenye sheria kuhusu "obstruction", kwa maana ya tendo la kuzuia, uchunguzi unaoendelea na nia ya uovu.

"We summarized the evidence we found and then analyzed it by reference to the three statutory obstruction-of-justice elements; obstructive act, nexus to a proceeding, and intent" (Page 15, Parag 2, Vol II).

Lakini ukichunguza uchambuzi wa Mueller katika kila eneo katika hayo maeneo kumi na moja, ameshindwa kufikia hitimisho usio na shaka kwenye eneo moja moja kulingana na hayo mambo matatu ya msingi kama kuna "Obstruction of Justice". Ndio chanzo cha kushindwa kutoa uamuzi wa jumla kama kuna "obstruction of justice" au la! Alikuwa na uoga wa kukosea.

Hayo mambo mengine aliyoandika kuwa ameshauriana na OLC (Office of Legal Counsel) kuwa hawezi kumshtaki Rais aliye madarakani ni mbwembwe tu, kwa sababu kwanini aseme hivyo kwenye Volume II, halafu ashindwe kusema hivyohivyo kwenye Volume I? Wakati Rais angeweza kupatikana na hatia hata kwenye Volume I?

Special Counsel ameandika kuhusu uoga wake wa kutoa uamuzi kwenye kipengele alichokiita "Overarching Factual Issues (Page 156-158, Vol II).

A: Ameelezea mambo 3 ambayo "sio ya kawaida" kwenye mashataka ya DOJ, ameyachambua na kutoa maoni yake ila inaonekana hakuwa na uhakika na maoni yake.

1. Kwamba kuna matendo aliyoyafanya Rais Trump ambayo yapo ndani ya mamlaka yake kikatiba kwenye Article II.
2. Kwamba kesi nyingi za Obstruction of Justice huwa zinalenga kuficha kosa lililofanyika (underlying crime). Ila kwenye hii kesi hakuna kosa linalofichwa, kwa sababu amethibitisha mwenyewe kwenye Volume I kuwa hakuna kosa lililofanyika.
3. Kwamba matendo mengi ya Rais dhidi ya mashahidi yalifanyika mbele ya umma.

B: Baada ya kushindwa kuona nia ya uovu kwenye matendo ya Trump, Mueller ametoa maoni:

1. Kwamba kuangalia matendo ya Trump kwa ujumla na sio mojamoja kunaweza "kutoa mwanga" kuhusu nia yake!
2. Kwamba kuangalia matendo ya Trump kabla na baada ya kumfukuza kazi Comey (FBI Director wa zamani) kunaweza kuonyesha kubadilika kwa nia yake!

Hamna mtu anayeweza kufurahia kuchunguzwa hasa pale unapojua wapinzani wako ndio wamekutengenezea kesi yenyewe ili wakumalize. Kwahiyo kukasirika au kulalama ni kitu cha kawaida katika mazingira hayo.
 
VIUNGANI DC WIKI HII
WH YAKATAA WATUMISHI KUHOJIWA

Huko nyuma katika uzi tulisema kinachoitwa collusion si tishio kama obstruction of justice
Tutumie maneno yalio kwenye ripoti ya Mueller, ambayo ni "conspiracy" na "coordination", kwa sababu "collusion" imechunguzwa kama "conspiracy". Kwahiyo labda useme conspiracy sio tishio. Ina maana Volume I nzima sio tishio?

House watashughulika na "Obstruction of justice" na sio "conspiracy" au "collusion".

Tulitoa mfano wa sakata la Bill Clinton liloanza kwa mambo ya nje, ngono na kuhitimishwa na obstruction of justice. Kinachoendelea DC si tofauti na tulichozungumza

Kesi ya Bill Clinton ni tofauti kwa sababu yeye alitenda kosa (underlying crime) ambalo alitumia mamlaka ya Rais kuzuia haki (obstruction of justice). Trump hajatenda kosa ambalo anatuhumiwa kuzuilia haki.

Clinton alikuwa na kesi nne (2 za perjury, obstruction of justice na abuse of power) ambazo Independent Counsel Ken Starr aliamua kwenye ripoti yake awe impeached. Huku, Mueller ameshindwa kuamua kuhusu kesi ya Obstruction of Justice.

Clinton alikuwa impeached na House (Republican majority) kwa makosa mawili kati ya manne lakini zilishindwa kupita Senate (Republican majority, Dems wote wakapiga kura ya Hapana) na hivyo akaonekana hana hatia. Leo majority kwenye House ni Dems ila Senate ni Republicans, unaweza kupiga hesabu!

Wiki tatu zilizopita tulisema AG Barr anatumika tu na WH na ile credibility yake imeondoka
Barr alisimama na kusema hakuna collusion ingawa si neno la kisheria
Taarifa ya Mueller inaeleza mahusiano yalikuwepo kati ya kampeni ya Trump na Russia

"Collusion" sio neno kisheria ndio, what difference does it make? Mahusiano yote yamechunguzwa na yamehibitika sio makosa kisheria.

Credibility ya Barr imeondoka mbele ya nani, Democrats?

Barr akasambaza vihabari vya kutunga ( Bandiko 765) na kurudia tena alhamisi iliyopita
Katika mengi yaliyomo, Barr alidai Mueller hakufikia tamati kuhusu obstruction of justice
Taarifa inaonyesha kinyume kabisa kwani Mueller aliweka mazingira ya mashtaka Congress

Kwani Mueller amefikia tamati kuhusu Obstruction of Justice? Ni page namba ngapi ya ripoti?


Congress imeona tatizo na hivyo kuamua kuita akina McGahn, Barr na Mueller kueleza kwa kina
Wakwanza atakuwa AG Barr ambaye hakuna shaka akaangwa kama firigisi kwa kulisha umma matango pori. Halafu atafuata Mueller atakayeitetea taarifa yake.
Mpangilio huo haumpi Barr nafasi ya kujificha chini ya kivuli cha Mueller wala kuongopa tena
Don Mcgahn naye ataitwa kutetea ushahidi wake wa masaa 30 kwa tume ya Mueller

House Judiciary Committee ime-issue subpoena kwa ajili ya ushahidi wa McGahn sawa! Ila hebu tujiulize, huyu mtu ameshahojiwa na Mueller kwa zaidi ya masaa 30 na ushahidi wake upo kwenye ripoti ya Mueller, kuna kitu gani cha ziada ambacho Democrats wanatafuta ambacho Mueller alishindwa kukipata kwake? Jibu ni hakuna! Kwanini wasitumie ushahidi aliokwishatoa?

Mueller atazungumzia ripoti yake! So hamna kipya!

Barr atasimamia alichokisema.

Lakini swali la msingi, kama Democrats wana uhakika na wanaona Obstruction of Justice kwa Trump kwanini wasiendelee na hitimisho la uchunguzi tuone watakapofika! Badala ya kurudia kuhoji watu ambao wameshahojiwa!!

WH imeshtuka kwani suala la obstruction of justice limeelezwa kwa kina na Mueller
Sasa Rais Trump na WH hawataki washauri kuitwa mbele ya kamati za Bunge
Wanataka kutumia executive privilege ingawa ina ukomo wake kwa hali ilivyo.
Swali linarudi kwa AG Barr, ikiwa alihakikishia umma kwamba WH ilitoa ushirikiano 100%, ni vipi basi WH hiyo hiyo haitaki watu kuhojiwa na kamati za Bunge?
Swali kwa Rais Trump. Ikiwa taarifa ilimsaifisha nini kinamtisha hadi kuzuia watu kutoa ushuhuda mbele za kamati za Bunge? Nini anahofia na nini anaficha ikiwa taarifa ilimsafisha!

Kwanini House Judiciary Committee wasitumie ushahidi ambao Mueller anao kufanya maamuzi? Tumeambiwa "Mueller alitaka kesi ya Obstruction of Justice iamuliwe na Congress". White House wanachotaka ni Dems waamue chochote kutokana na hiyo ripoti, Dems wanashindwa nini kuamua hadi kutaka kuanza kurudia kuhoji watu?

White House watoe ushirikiano mara ngapi? Trump angekuwa na nia kuficha mawasiliano ya maafisa wa WH angetumia executive priviledge kuyaficha kwenye ripoti ya Mueller! Hao Dems wanashindwa nini kuendelea na hitimisho la uchunguzi wao?

Kama mtakumbuka tulisema drip drop zitammaliza Trump. Kila uchao magazeti yanadonsha kitu hata kumpelekea Mzee atoe tweet 50 katika masaa 24. Hili si bure kuna kihororo na mshawasha

Tatizo Dems wanahangaika na Trump sana! Kiasi kwamba wanajichanganya hawajui wanachokitafuta.
 
Blah, blah, blah...Kwamba aliachia Congress? Ingawa naunga mkono Congress wakatolee uamuzi suala la Obstruction of Justice ila hamna sehemu yoyote kwenye ripoti ya Mueller ambapo amesema ameshindwa kutoa hatma kwa sababu ameliachia Congress. Tusipotoshe.
Sina hakika kama kweli umepitia ripoti ya Mueller neno kwa neno hivyo nakushauri utafute muda maalum uipitie ukiwa umetulia kwani huu mtizamo wako hakika si wa kweli...Mueller aliitaka Congress ndiyo iwe mwamuzi.

Hilo moja lakini la pili ni kwamba ripoti ya Mueller imeonesha wazi kabisa kati ya WH na Press muongo ni nani. Mambo mengi yaliyoandika na magazeti na Trump kudai ni FAKE News, ripoti ya Mueller imeeleza vinginevyo.

Ingekuwa Tanzania habari kama hii ingekuwa imezikwa baada ya ripoti ya Mueller kwani kwa upuuzi wa Barr katika kumlinda Rais hakuna ambaye angehoji zaidi.lakini kwa Marekani kazi imebaki kwa wawakilishi, Congress.
El Jefe said:
Tatizo Dems wanahangaika na Trump sana! Kiasi kwamba wanajichanganya hawajui wanachokitafuta.
Ni kama vile unaishi dunia ya peke yako, strategy waliyo nayo Democrats katika kumshughulikia huyo mhuni, wewe subiri tu uone moto wake. Watu hawakurupuki hovyo kama unavyodhani. Ya Nixon yalichukua muda mrefu zaidi na aliweza hata kuchaguliwa kipindi cha pili lakini hakukimaliza. Taratibu hata Republicans wenyewe wataanza kumkimbia Trump, vuta subira...
 
VIUNGA VIKUU VYA DC NA YANAYOJIRI
RAIS TRUMP ATHIBITISHA TAARIFA HAITOKI KWA WITO WA KISHERIA

Tunaendelea kuipitia taarifa ya Mueller. Hakuna mtu makini anayeweza kusema ni nzuri.

Kuna mkanganyiko katika kambi ya Trump, wanaitumia taarifa hiyo ikiwafaa na wanampiga madongo Mueller inapobana. Ndiyo taarifa ilivyo, ni moto ni baridi, ndio utaalam unavyotaka

Taarifa ya Mueller imeandikwa kwa utaalam na ufundi wa hali ya juu. Ukiisoma kama hadithi hutabaini nini kimesemwa. Ukiisoma na jicho angavu ni taarifa mbaya sana kwa Trump

AG Bill Barr alimlisha Trump matango pori kwa ile taarifa aliyoitoa ikatembezwa kama mwenge(#765). Baada ya kuelezwa kwa kina hakika machungu ya taarifa ni makubwa

Kwanza, Mueller amemueleza WH sec. Bi Sarah Sander akieleza kuwa alichosema ni uongo,hakuna kiongozi wa FBI aliyempongeza Rais kuhusu Comey

Mueller aliiweka taarifa makusudi akionyesha kinachosemwa ni ''fake news' siyo media

Fake news ni WH yenyewe. Ni utaalam wa Mueller kumvua mtu mavazi bila kurupushani

Ukitaka kujua watu wanasoma volumes hawaelewi mantiki soma hapa chini na tutafafanua

'The evidence we obtained about the president's actions and intent presents difficult issues that would need to be resolved if we were making a traditional prosecutorial judgement. At the same time , if we had confidence after a through investigation of the facts that the president clearly did not commit obstruction of justice, we would state so.
Based on the facts and the applicable legal standards , we are unable to reach the judgement''


Mueller anasema '' Ushahidi tulioupata juu ya Rais na dhamira ya vitendo vyake ina mambo magumu yanayohitaji kushughulikiwa kama tungefanya taratibu za kawaida za uamuzi wa mashtaka'' Mueller ana maana ugumu wa kufuata taratibu za kufikia maamuzi ya mashtaka unakuja na suala moja, wao watamshtaki vipi Rais wakiwa watumishi wa DOJ?

Anaendelea kusema
'' Wakati huo huo kama tungekuwa na uhakika kupitia ukweli wa uchunguzi kwamba Rais hakuzuia mkondo wa sheria, tungesema hivyo''

Mueller anasema ikiwa wangekuwa na ushahidi wa kumsafisha Rais wangetamka.
Hii maana yake, ule ugumu wa kushughulikia suala kimashtaka unamzuia kusema Rais alifanya abcd. Maneno muhimu ni '' we would do so'' Yaani tungefanya hivyo!

Anaendelea
''kwa msingi wa ukweli na taratibu zilizopo hatuwezi kufikia uamuzi''
Mueller anamaanisha ukweli uliopo kuhusu suala hilo(ukweli ni vitendo) na kwa taratibu zilizopo(taratibu ni zile za DOJ kutomshtaki Rais) hawakufikia uamuzi.

Maana yake hawakufikia uamuzi wa kumshtaki kwa kuzuia mkondo wa sheria kwa hoja za kwao ni sehemu ya DOJ.
Hapa hana maana uamuzi wa hatia, ana maana uamuzi wa kufungua mashtaka.

Kwa mantiki hiyo, Mueller amelicha wazi kwa kujua anayeweza kufungua mashtaka atafanya hivyo. Alichokifanya ni kutoa dondoo kumi za kumsaidia atakayefungua mashtaka pa kuanzia

Ndiyo maana Mueller alisema hivi
'' And apart of OLC's (office of legal council) constitution view, we recognized that a federal criminal accusation against sitting president would place burdens on the president's capacity to govern and potentially pre empty constitution processes for addressing presidential misconduct''

Kwamba
'' Licha ya mtazamo wa kikatiba waofisi ya sheria (OLC) tunatambua kwamba tuhuma za jinao dhidi ya Rais aliye madarakani zitakuwa mzigo katika kutawala na utatangulia mbele zaidi dhidi ya hatua za kikatiba katika kushughulikia ukosefu wa Rais''

Mueller hapa anaeleza kuhusu taratibu za kikatiba kushughulikia makosa ya Rais na kwamba wao hawakutaka kutangulia utaratibu huo. Utaratibu anaouzungumzia ni kupitia congress

Laiti Mueller angetaka DOJ ishughulikie suala hilo, angesema wazi analirudisha idarani

AG Barr kamwekea maneno katika summary ya kurasa nne.
Alijua wapo wanaosoma na kuelewa na wanaobeba vitu ilimradi tu waonekane

Taarifa ya Mueller ni ya kitaalam, si ya kuisoma kama kijarida.

Unaweza kuchangia taarifa hiyo ukawaacha watu na maswali siyo yatokanayo na taarifa bali juu ya uwezo wa kuielewa

Tusemezane
 
Kuna uwezekano kuna kosa la "obstruction of justice" na pia kuna uwezekano halipo. Tusome ripoti "impartially" na kwa makini.

Hamna aliyesema kuwa ripoti ya Mueller ni nzuri kwa ujumla wake. Lakini Volume I ya ripoti imesema Trump na washirika wake hawana hatia na walichokuwa wanatuhumiwa nacho. Kwenye Volume II, uchunguzi wa "Obstruction", Mueller hakuhitimisha kama Rais ana hatia au lah!

Kwanza, kwa sababu ya maoni ya OLC kuwa POTUS aliye madarakani hawezi kushtakiwa kwa kuwa inaleta madhara kwenye utendaji kazi wake na kukiuka kwa misingi ya "seperation of powers," lakini anaweza kuchunguzwa.

Kwa sababu hiyo, Mueller hakufanya uchunguzi wake kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa DOJ ambao pengine ungekuwa na uwezekano wa kuhitimisha kuwa Rais ana hatia!

"a traditional prosecution or declination decision entails a binary determination to initiate or decline a prosecution, but we determined not to make a traditional prosecutorial judgement" (Page 1, Parag 4, Vol II)

"We considered whether to evaluate the conduct we investigated under the Justice Manual Standards governing prosecution and declination decisions, we determined not to apply an approach that could potentially result in a judgement that the President committed crime. The threshold step under the Justice Manual Standards is to assess whether a person's conduct constitutes a federal offense" (Page 2, Parag 2, Vol II)

Ndio maana kwenye Volume II, Mueller amechunguza kujua ukweli na kujua kama kuna kosa limefanywa lakini sio kuamua kama kuna hatia au lah!.

Pili, katika kuchunguza ukweli wa "Obstruction", Mueller amekutana na masuala magumu (difficult issues) ambayo yalimfanya ashindwe kuhitimisha kuwa Trump hajatenda kosa!

"The evidence we obtained about the President's actions and intent presents difficult issues that prevent us from conclusively determining that no criminal conduct occured. Acordingly, while this report does not conclude that the President commited a crime, it also does not exonerate him." (Page 2, Parag 4, Vol II)

Mueller amesisitiza kuwa hayo "masuala magumu" yanabidi yasuluhishwe kama wangetaka kuhitimisha kuwa Trump ana hatia au lah!

"The evidence we obtained about the President's actions and intent presents difficult issues that would need to be resolved if we were making a traditional prosecutorial judgement".(Page 8, Parag 4, Vol II)

Kwakuwa Mueller hakutaka njia au utaratibu (approach) wa uchunguzi ambao ulikuwa na uwezekano wa kuhitimisha kuwa Rais ana hatia kwa sababu alizoainisha, ni wazi Rais asingekuwa na hatia bila hayo "masuala magumu" kuwepo angesema. Neno la muhimu (Keyword) hapo ni "clearly".

"At the same time if we had confidence after a thorough investigation of the facts that the President did not clearly commit obstruction of justice, we would so state" (Page 8, Parag 4, Vol II)

Lakini ameshindwa kusema kwa sababu hayo "masuala magumu" hayajasuluhishwa.

Kwahiyo, hakuna hitimisho popote pale kwenye ripoti ya Mueller kwamba Trump amepatikana na kosa la "obstruction of justice" bali ni watu binafsi kwa maoni yao ndio wanahitimisha.
 
NDANI YA VIUNGA VIKUU VYA DC

MUELLER 'THE HONORABLE'' SASA NI GROUP OF DEMS
MCGAHN AZUIWA KUFIKA MBELE YA KAMATI, TRUMP AMNANGA

Katika taarifa ya Mueller iliyohaririwa '(siyo ya Barr bandiko 765) imeeleza kuhusu taratibu zilivyokuwa ngumu kushughulikia suala hilo na kuliacha lishughulikiwe na mamlaka nyingine

Mueller alisema '' kama ingalikuwa wazi hakuzuia mkondo wa sheria, tungesema hivyo''
Akaendelea kusema '' taarifa haimsafishi '' akitumia neno does not exonerate him

Ugumu wa obstruction of justice unaonyeshwa pale mshauri wa WH Mcgahn alipotajwa zaidi ya mara 100 huku mueller akimueleza kama mkweli na asiye na sababu ya kuzua kwa nafasi yake

Si Mcgahn tu, wapo wawili zaidi waliotoa ushahidi na yapo mazingira yaliyoanisha tendo hilo

Rais Trump kaamka kumshambulia Mcgahn kwa kumwita Muongo na kwamba taarifa inayosambaa kumhusu ni fake news!! Yaani media zimekuwa fake kueleza taarifa ya Mueller

Trump anakana kuwa hakumwambia Mcgahn amfukuze kazi Mueller.
Kwa hili wafuasi wake watamwamini na kubeba tweet bila kufikiri. Hoja ipo hapa

1. Mgahn hakuwa peke yake wapo wengine waliotumwa na walitoa ushahidi wa hilo
2. Mcgahn alitoa taarifa chini ya kiapo (oath) , Trump anazungumza katika tweet
3. Trump hakuwahi kutokea katika kamati, vipi anaweza kumwita Macgahn Muongo?

Katika mahangaiko ya kutambua kina cha obstruction of justice, Rais Trump anataka kutumia executive privilege kumzuia Mcgahn asitokee mbele ya kamati ya Bunge

Swali, kuna hofu gani kwa Mcgahn ku testify ikiwa Trump na kundi linalomfuata linaamini kwa dhati kabisa kuwa hakuwa na hatia na kwamba taarifa ilimsafisha!!

Lakini pia hili linaonyesha jinsi Trump asivyojua mambo ya utawala.

WH ilipomruhusu Mcgahn kutokea katika kamati tayari ilishaondoa exec privilege wakisema ''waive the privilege''

Mcgahn sasa si mwajiriwa wa WH ni raia, exec privilege kwa sehemu kubwa haina maana

Haya yanaendelea kuonyesha udhaifu wa Trump katika kuelewa mambo ya viunga vya DC

Juzi ali tweet akisema ikiwa Dems wataamua impeachment yeye atakwenda supreme court(SC)

Trump haelewi kuwa congress ni equal branch na executive na kwamba kikatiba ina mamlaka ya kuchukua maamuzi bila kuingiliwa na supreme court

Kilichomchanganya Trump ni uwepo wa chief justice(CJ) wakati wa impeachment kama itatokea

CJ ndiye anayeongoza mchakato wa impeachment, haina maana SC imeingia. Ni utaratibu

Baada ya kuisoma taarifa kwa kina au kuhadithiwa kwa uyakinifu Trump amebaini ni chafu na siyo ile ya Barr (bandiko 765) iliyokuwa na kihoro ikiwalenga wabebaji waichukue na kuimeza tu

Baada ya kurasa 4 za Barr kutoka Rais Trump aliita taarifa powerful na Mueller is honorable person na kwamba kwa muda wote alijiheshimu.

Leo Trump amamwita Mueller kama genge la democrats 14 lililoandika taarifa ya kuzua
Kama kawaida, Trump kawavuta manazi wake kisha kuwaacha njia panda!

Tusemezane
 
Kuna uwezekano kuna kosa la "obstruction of justice" na pia kuna uwezekano halipo. Tusome ripoti "impartially" na kwa makini...

Kwahiyo, hakuna hitimisho popote pale kwenye ripoti ya Mueller kwamba Trump amepatikana na kosa la "obstruction of justice" bali ni watu binafsi kwa maoni yao ndio wanahitimisha.
El Jefe, haya mapenzi yako kwa huyo mhuni na muongo kaa nayo. Lakini mpaka sasa ujue Fox News imegawanyika kama Republican Party ilivyogawanyika. Very soon Trump ataanza kukimbiwa...vuta subira! Mpaka majuzi kabla ya ripoti ya Mueller, Judge Andrew Napolitano alikuwa mshauri mojawapo wa Trump kwa mambo ya kisheria huko Fox News!

Fox News' Judge Napolitano skewers Trump: His obstruction's "unlawful, defenseless and condemnable"
Andrew Napolitano, a former judge and Fox News' senior judicial analyst, said that Attorney General Bill Barr was "wrong" to absolve President Trump of obstruction of justice based on the evidence in the Mueller report in a Fox News op-ed on Thursday. Napolitano called Trump's actions "unlawful, defenseless and condemnable" and said it was up to House Democrats to decide whether or not to impeach Trump on obstruction charges.

The president's job is to enforce federal law. He said, “If [Trump] had ordered his aides to violate federal law to save a human life or to preserve human freedom, he would at least have a moral defense to his behavior,” the judge said in the video. “But ordering them to break federal law to save him from the consequences of his own behavior? That is immoral, that is criminal, that is defenseless, and that is condemnable.”


On obstruction, the report concluded that notwithstanding numerous obstructive events engaged in by the president personally, the special counsel would not charge the president and would leave the resolution of obstruction of justice to Congress. Congress, of course, cannot bring criminal charges, but it can impeach.
 
El Jefe, haya mapenzi yako kwa huyo mhuni na muongo kaa nayo. Lakini mpaka sasa ujue Fox News imegawanyika kama Republican Party ilivyogawanyika. Very soon Trump ataanza kukimbiwa...vuta subira! Mpaka majuzi kabla ya ripoti ya Mueller, Judge Andrew Napolitano alikuwa mshauri mojawapo wa Trump kwa mambo ya kisheria huko Fox News!

Fox News' Judge Napolitano skewers Trump: His obstruction's "unlawful, defenseless and condemnable"
Andrew Napolitano, a former judge and Fox News' senior judicial analyst, said that Attorney General Bill Barr was "wrong" to absolve President Trump of obstruction of justice based on the evidence in the Mueller report in a Fox News op-ed on Thursday. Napolitano called Trump's actions "unlawful, defenseless and condemnable" and said it was up to House Democrats to decide whether or not to impeach Trump on obstruction charges.

The president's job is to enforce federal law. He said, “If [Trump] had ordered his aides to violate federal law to save a human life or to preserve human freedom, he would at least have a moral defense to his behavior,” the judge said in the video. “But ordering them to break federal law to save him from the consequences of his own behavior? That is immoral, that is criminal, that is defenseless, and that is condemnable.”


On obstruction, the report concluded that notwithstanding numerous obstructive events engaged in by the president personally, the special counsel would not charge the president and would leave the resolution of obstruction of justice to Congress. Congress, of course, cannot bring criminal charges, but it can impeach.
Huko kugawanyika kwenye vyama ni kitu cha kawaida Mag3, Dems wamegawanyika vilevile, ila mwishoni Republicans wanakuwa kitu kimoja.

Judge Napolitano anatoa maoni yake binafsi kama Fox News Judicial Analyst. Ken Starr kama mtu aliyewahi kuwa "independent counsel" anasema Trump alikuwa kwenye "brink" ya Obstruction ila haku-obstruct justice.

Ripoti ya Mueller nampa (A) kwa uchunguzi wa kina (thorough investigation).

Ken Starr (whitewater) na Leon Jaworski (watergate) walihitimisha kuwa kuna "obstruction of justice" na mambo mengine katika chunguzi zao. Cha kushangaza kwenye "whitewater", Dem Senators wote (45) walikuwa kitu kimoja kukataa "perjury" na "obstructions" za Bill Clinton.

Leo hii Dems wanawahitaji Republicans kwenye Senate ili wafanye kile walichoshindwa kufanya wao!!Funny! Kesi yenyewe ya "obstruction" ina "difficult issues".

Nancy Pelosi anaota mchana kweupe na huo mkakati wake! Hata CNN wanajua Dems wameshafeli, kesi haina nguvu.
 
Huko kugawanyika kwenye vyama ni kitu cha kawaida Mag3, Dems wamegawanyika vilevile, ila mwishoni Republicans wanakuwa kitu kimoja.

Nancy Pelosi anaota mchana kweupe na huo mkakati wake! Hata CNN wanajua Dems wameshafeli, kesi haina nguvu.
Naona humjui Nancy Pelosi, DEMS wako pamoja tena sana tu. Impeachment itaendeshwa na House na hapo ndipo ushahidi wote wa alichonuia Mueller utakapoonekana wazi hata kwa waliopofuka kimapenzi na Trump.

Nancy anawataka DEMS kutokurupuka, anataka kwanza ripoti kamili ya Mueller ikiwepo kuwa-subpoena wahusika pamoja na Barr, Rosenstein na Mueller mwenyewe lakini mwisho ni impeachment, hakuna namna.

Kumbuka hata hiyo ripoti iliyotolewa na Barr bado ni redacted...zinazopenyezwa ni kwamba ripoti nzima ya Mueller ambayo lazima itapatikana kwenye impeachment process imemkaanga vibaya Trump mpaka kwenye tuhuma za conspiracy. Collusion is a non-issue.

Issue ya Rais Clinton ilikuwa ni ndogo sana kisheria labda kimaadili...eti kufanya mapenzi na intern. Kama Senate haitaafiki maamuzi ya House, hilo ni jambo lingine lakini halizuii House kutekeleza wajibu wake. Je unasemaje kuhusu Richard Nixon?

Je aliyofanya Trump angefanya Obama, kweli leo Republicans wangekaa kimya? Je unakumbuka walivyotaka kum-impeach kwa kutumia tu Executive Action kwenye swala la DACCA?
 
Back
Top Bottom