Tarehe 17 inaweza kuwa na matokeo mawili, kwanza, kumsafisha Trump once and for all. Pili, kumtia katika matatizo makubwa sana ya impeachment.
Baada ya taarifa yake kuwekwa hadharani, Mueller alisema hatasema zaidi nje ya ripoti. Hicho ndicho kilichotokea, Mueller hakujibu maswali takribani 206 akitumia privilege ya kutozungumza baadhi ya mambo ambayo mengine yapo katika uchunguzi na mengine yakiwa yamefichwa na AG Barr hadi leo
Mara nyingi Mueller alishindwa kuelezea hata yaliyomo kwenye ripoti yake (redacted). Mda mwingine aliulizwa maswali ili kuthibitisha jambo anakataa kujibu wakati maelezo yapo wazi kwenye ripoti.
Mueller alitegemewa kukazia hoja ya Dems ya "impeachment" lakini matokeo yake mahojiano yake yameanika uwezo wake usioridhisha wa kujibu hoja na kupelekea kuwapa credit zaidi Republicans.
Mueller hakuzungumzia chanzo cha uchunguzi wake na ule wa FBI dhidi ya Trump sio kwasababu yamefichwa kwenye ripoti yake na AG Barr, hapana! Ni kwa sababu ya uchunguzi unaondelea wa AG Barr ulioanza baada ya ripoti ya Mueller.
1. Trump alikuwa anadai kuwa Mueller ana conflict of interest kwani alimuomba awe mkuu wa FBI siku moja kabla ya uteuzi wake
Mueller: Alithibitisha kuwa hakuomba kazi kama madai ya Trump yasemavyo. Hapa ikumbukwe Mueller alikuwa chini ya kiapo na hivyo kauli yake ina uthabiti. Kuanzia siku hiyo hoja ya conflict of interest imekwisha
(A) Hoja ya 'conflict of interest' ya Mueller haijaisha, kwa kifupi mambo mengi hayajaisha. Kwahiyo kusema kwamba imekwisha kwa sababu Mueller alikuwa chini ya kiapo, sio hoja kwa sababu watu wanaweza kusema uongo chini ya kiapo pia.
Lakini pia nafasi ya mkurugenzi wa FBI ni nafasi ya uteuzi ambayo Rais anapendekeza jina ili kupigiwa kura na Senate. Kwa kuwa sio nafasi inayotangazwa ili watu waombe, unaweza kukuta Rais ana mtu wake au anachambua baadhi ya watu kwa kuzungumza nao. Lakini pia wanaohitaji nafasi kama hizi za uteuzi huwa wanazungumza na watu walio karibu ya Rais ili wawapendekeze kwake. Kitendo hiki kimantiki ni sawa na kuomba nafasi hizo.
Mueller alimwambia Mike Pence (VPOTUS) kuwa nafasi ya Mkurugenzi wa FBI ndiyo inaweza kumfanya arudi kufanya kazi serikalini.
"FBI director is the only job I'll come back for"
Hii kauli ni sawa na kuomba aangaliwe katika nafasi ya Mkurugenzi wa FBI, ndio maana Mike Pence alimkutanisha na Trump ili apigwe interview ya nafasi hiyo, ila Trump akampiga chini.
Mueller alipigwa chini "leo", "kesho" yake akateuliwa na Rod Rosenstein (Deputy AG) kuwa Special Counsel kumchunguza Trump. Yaani mtu kakupiga chini leo kesho yake unaanza kumchunguza!!!
(B) Ukisikiliza mahojiano ya Mueller na Rep. Louie Gohmert (R-TX), Mueller alizungumza na Trump kuhusu kufukuzwa kazi kwa James Comey (Frm FBI Director) katika interview yake siku moja kabla ya kuteuliwa kuwa Special Counsel. Kufukuzwa kwa Comey ndio chimbuko la uchunguzi Mueller dhidi ya Trump kuhusu Obstruction of Justice. Unachunguzaje suala ambalo wewe ni shahidi??
(C) Muller aliteua wasaidizi 13 katika uchunguzi wake, wote wakiwa ni wanachama wa Democrat na wanachangiaji wazuri wa kampeni zao! Mmoja wa wasaidizi aliowateua ni Peter Strzok ambaye sms zake na mpenzi wake Lisa Page zilizonaswa kwenye uchunguzi mwingine zilionesha kuwa ana chuki dhidi ya Trump na walikuwa na nia kumzuia Trump kuwa Rais. Unateuaje wasaidizi ambao unafahamu wana chuki ya wazi dhidi ya unayemchunguza?
Mueller hajajibu haya maswali kwa ufasaha.
Mueller: Taarifa yake haiku ''total exoneration'' Trump kwa maana haikumsafisha Trump
Hii ni kuikana kauli ya Trump ya ''taarifa kuwa na total exonerations and vindication''
Mueller hana mamlaka ya kufanya au kutofanya "exoneration". Trump alitumia neno hilo kisiasa ila Mueller amelitumia kwenye ripoti yake kwamba hajamu-'exonerate' Trump. Lakini pia Prosecutor kama Special Counsel hana mamlaka ya kutimisha hatia ya anayemchunguza.
Mahojiano ya Mueller na Rep. John Ratcliffe (R-TX) na Rep. Michael Turner (R-OH) yalimfumbua macho Mueller kuhusu mamlaka ambayo hana kisheria, ambayo alikuwa anafikiri anayo.
2. Mueller : Alithibitisha kuwa Russia iliingilia uchaguzi na hadi sasa wanaendelea na kazi hiyo kwa nia ya kumsaidia Trump ashinde uchaguzi. Hii inathibitika kwa kauli ya Putin akiwa na Trump nchini Finland akisema ni kweli Russia ilitaka ashinde uchaguzi.
Mueller alishindwa kumjibu Rep. Tom McClintock (R-CA), alipoulizwa kwanini hakutoa ushahidi mbele ya jaji wakati wa uchunguzi wake, unaoonyesha uhusiano wa IRA (Internet Research Agency) na Serikali ya Russia, ingawa kwenye ripoti yake anasema uhusiano huo upo!!
Marais wangapi walitaka Hillary ashinde? Au Trump ashinde? Marais wengi hawawezi kusema kwa kuhofia mahusiano mabaya iwapo waliyemtaka hakuwa Rais.
Hadi sasa Russia wanamsaidia Trump ashinde? Una ushahidi mkuu au ni hisia tu?! FBI walishasema hakuna ushahidi wa "impact" ya "Russia influence" kwenye uchaguzi wa US. Anayesababisha Trump ashinde ni utekelezaji wa ahadi zake.
3.Mueller: Alithibitisha kuwa Trump alikataa mahaojiano na kamati kinyume na madai ya Trump kwamba hakuitwa na kwamba kama angeitwa angalikwenda kwani hana la kuficha
Kwa mazingira yale Trump alifanya uamuzi sahihi wa kujibu kwa maandishi.
4.Obstruction of justice: Mueller akathibitisha uwepo wake na kusema taratibu za kisheria zilimzuia kumshtaki Rais kama ilivyo utaratibu wa DOJ.
Mueller hajathibitisha uwepo wa Obstruction of Justice katika testimony yake. Wala hakusema taratibu za kisheria zilimzuia kumshtaki Rais bali masuala magumu (difficult issues) ndizo zilizomzuia kuamua kushtaki au kutoshtaki.
Ukisikiliza mahojiano ya Dems na Mueller kwa mfano Rep. Hakeem Jeffries (D-NY), utagundua kuwa Mueller hakuthibitisha uwepo wa Obstruction of Justice. Rep. Hakeem kama Dems wengine alitaka Mueller athibitishe lakini Mueller hakuthibitisha.
Lakini huo unaoitwa "utaratibu wa kisheria" aliotumia Mueller kwenye Obstruction of Justice haupo kisheria, maana kwanza, kutokana na kanuni zinazomuongoza Special Counsel, anatakiwa afikie uamuzi wa kushtaki au kutoshtaki na sio uamuzi wa kutoamua kushtaki au kutoshtaki. Pili, hamna kanuni yoyote ya DOJ inayomruhusu Special Counsel 'kutoku-exonerate' mtu kwa sababu ameshindwa kufikia uamuzi kuhusu 'hatia' ya anayechunguzwa.
5. Conspiracy: Mueller alisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa mashtaka.
Hapa alithibitisha kauli kuwa conspiracy ilikuwepo lakini haikuwa na ushahidi wa kimashtaka
Kama tendo fulani halijafikia kiwango cha kuwa kosa kisheria, unawezaje kusema tendo hilo ni kosa kisheria?. Na kama tendo hilo sio kosa kisheria, linawezaje kuwa kosa kwa misingi ya haki?
Viwango vya kutambua kosa kisheria vimewekwa kulinda haki. Mueller amehitimisha hakukuwa na conspiracy, ina maana ni mahusiano ya kawaida. Kutaka kufanya mahusiano ya kawaida yawe "conspiracy" kutahitaji definition nyingine ya "conspiracy" ambayo sio ile iliyotambulika kama kosa.
5. Mueller: Hakujibu baadhi ya hoja kwa kusema hatakwenda nje ya taarifa na kwamba habari nyingine ni nyeti kuwekwa hadharani
Mueller alisema hatazungumzia unredacted materials (zile catogory nne). Tusi-insinuate kuwa kwa kusema kwamba "habari nyingine ni nyeti kuwekwa hadharani" kunamaanisha kuna taarifa mbaya inafichwa kwa makusudi.
Maana kuna baadhi ya watu humu walidhani AG Barr alitoa redacted report ili kumbeba Trump na sio kufuata sheria na kanuni za DOJ.
Katika hali isiyotarajiwa Mueller alisema ''Rais Trump anaweza kushtakiwa baada ya Urais'' ingawa baada ya mapunziko alisahihisha kauli yake baada ya kuulizwa na mjumbe wa GOP.
Mueller hakusahihisha kauli yake kuhusu kumshtaki Rais baada ya kuondoka madarakani, alisema inawezekana na hakubadilika. Aliulizwa kuhusu hili na Rep. Ken Buck (R-CO).
Ila Mueller alisahihisha swali la Rep. Ted Lieu (D-CA) aliyemuuliza Mueller kama hakumshtaki Trump kwa sababu ya maoni OLC yanayosema Rais aliye madarakani hawezi kushtakiwa, mara ya kwanza alijibu ndio, halafu baadae akarekebisha kuwa hawakufikia uamuzi kama Rais alitenda kosa.
Kuna shahidi muhimu aliyewekewa uzio na utawala wa Trump. Huyu ni bwana Macgahn ambaye ni shahidi muhimu sana katika jaribio la obstruction of justice.
Huyu bwana ametajwa zaidi ya mara 50 katika taarifa ya Mueller. Mchakato wa kumwita una ugumu wake ingawa suala limeenda mahakamani
Mueller ameshindwa kuwapa Dems wanachokitafuta sasa wamehamisha nguvu kwa McGahn, sijui baada ya McGahn atafuata nani? Maana Dems walituambia Mueller ndiye alikuwa "mtu wa muhimu sana" na kwamba Trump na AG Barr walikuwa wakimzuia kuhojiwa Congress. Hata huko mahakamani Dems wanafikiri wanahujumiwa! Mara wanamtaka Jaji huyu, mara Jaji huyu hawamtaki, ili mradi wapate wanachokitaka.
Nawaza tu kwa sauti haya maamuzi yakipelekwa Supreme Court, sijui Dems watampanga Justice gani kule?
Hayo ni baadhi ya yaliyojiri yakiacha swali, je, kuna sababu za impeachment?
Katika mazingira ya kawaida jibu ni ndiyo! Uchunguzi ungeachwa hadharani na AG Barr uchafu mwingi ungetosha. Kama mashahidi wangeatikana kwa urahisi ingalikuwa dhahma. Kwasasa jibu la ndiyo lina tatizo na hilo ndilo linawasumbua Democrats
Mueller aliulizwa na Dems na Republicans kuhusu "impeachment", vikiwemo vile visententensi tulivyoambiwa humu kuwa tafsiri zake ni "Congress waamue" au "impeachement", lakini alikataa kuzielezea au kutoa mapendekezo hayo. Juhudu za akina Rep. Veronica Escobar (D-TX) ziligonga mwamba.
Again, AG Barr analaumiwa kwa ku-hide grand jury materials (among others) na watu ambao hawajasoma Fed. Rules of Criminal Procedures 6(e).
Tatizo la Dems sio mashahidi, tatizo ni kwamba kesi haina nguvu dhidi ya wanaemchukia a.k.a Trump. Wasingekuwa wanadunduliza na kutumia nguvu nyingi kushawishi watu kuwa Trump ametenda kosa.
Karata kubwa ipo katika Senate!
Kwenye Senate hamna "karata" yoyote huko labda kama hamuwasikilizi Republicans. Ni 'far-fetched' hata kuwaza kuwa Republicans walio Senate watadandia treni ya 'impeachment' ya Dems!!