TRUMP RAIS WA 45 WA MAREKANI
Akiwa na umri wa miaka 74 , mzee zaidi kuwa Rais ameapishwa leo kama Rais wa 45 wa US
Sherehe ya kuapishwa iliambatana na kuondoka kwa Rais Obama kuashiria zama mpya za Trump
Tukio la kubadilisha madaraka lilikuwa na sura mbili, furaha na huzuni kwa kila upande
Kila hatua ilifanyika kwa kuzingatia utamaduni wa Marekani wa miaka nenda rudi
Kubwa ni kubadilishana madaraka kwa njia ya amani na utulivu kwa wahusika kwa kufuata sheria
Pamoja na uwepo wa kupingwa kwa Trump na makundi, kwa US hiyo ni sehemu ya demokrasia
Katika uchaguzi uliokuwa na mazonge zonge ya kila aina, bado sheria zilifuatwa bila shurti
Hata kama kuna aliyechukizwa na lolote, sheria ilikuwa mwongozo katika demkorasia iliyokomaa
Mara nyingi tumeeleza, demokrasia ya US hailinganishwi na vinchi vinavyoendelea.
Katika nchi hizo, Rais huondoka kwa nguvu za kijeshi au chaguzi kufutwa n.k. ubabaishaji tu
Kwa US hata mahasimu wa kisiasa, huweka tofauti zao pembeni na kuliweka Taifa mbele
Tuangalie sura mbili za tukio, Obama na Trump sehemu inayofuata