Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Naenda kwenye hoja zako Mwalimu wangu!

1.Poll zilitengenezwa na MSM...na wafuatiliaji wa mambo kuficha ukweli huu MSM hasa cnn.com walikuwa wanaficha picha za rally za 'mama'. Inasemekana wala alikuwa hajazi umati. Pia Democrats walikuwa wanaogopesha watu kuhudhuria kampeini za Trump (wala siyo za Republican maana walimsusia) kwa kuleta vurugu. Ushahidi upo.
2. wapiga kura wapya?Mkuu ebu fafanua.
3.No, mtu wa kuamini kwenye miracle hawezi kutamka kuwa wewe mwenyekiti wa chama endelea na kampeini nyingine mimi niachie kampeni ya Urais (Baada ya mwenyekiti wa Rep kususa); mtegemea miracle hawezi kutamka kuwa sitakubali matokeo kama sitashinda tena nchi yenyewe US. yule ni mfanyabiashara mzoefu, alishapiga hesabu zake vizuri alijua bila rigging anashinda na imekuwa (exposure ya rigging techniques za system za US kwa msaada wa WikiLeaks zimesaidia kuzuia wizi wa kura, kura zililindwa kwa namna hiyo; establishment, soros, wall Street elites et.al they were caught unprepared)
4.'Mama' asingepoteza majimbo ambayo alikuwa anajinasibu kuchukua mfano Penn ,nadhani convention yao ilifanyika huko. 'Mama' alikuwa hatakiwi
5.weka takwimu.
6.Wachambuzi wengi walikuwa 'paid ' for the job Kuhakikisha poll zinapata justification
====
Haya ni maoni yangu ,Nitaendelea kupitia post nyingine

..lakini Hillary amepata KURA NYINGI/POPULAR VOTES zaidi ya Trump.

..ukifuata mfumo wa uchaguzi wa Tz Hillary angekuwa mshindi.

..Sasa hii hoja kwamba Hillary alikuwa
"hatakiwi" mimi sikubaliani nayo.

..Trump alielekea kushindwa, lakini akaibuka ( closed the gap) baada ya FBI kuibua upya suala la e-mails.

..Inawezekana Hillary aliathirika na suala hilo kuliko ambavyo polls
ziliweza kuonyesha.
 
Mkuu Nguruvi3 na Jokakuu,
Kwa sasa kuna mjadala mkubwa kuhusu kura za maoni zinavyokwenda kinyume baada ya matokeo halisi.

Kuna haja ya kuangalia upya namna ya kutafuta hizo kura za maoni. Imetokea Brexit na sasa US. Kwa mfano ktk huu uchaguzi wamarekani walikuwa na mambo makuu 3.
1-Kilikuwa kipindi cha kufanya mabadiliko baada ya chama cha democrat kuwa madarakani kwa miaka 8,huu umekuwa km utamaduni wao.

2-Wamechoshwa na maneno matamu ya wanasiasa,miaka yote wanachagua wanasiasa wenye hotuba nzuri za kusisimua lkn wakishachaguliwa hawafanyi waliyoahidi. Hapa ndo nguvu ya Trump ilipoanzia.

3-Kwa kiwango kikubwa mambo aliyokuwa akisema Trump ndo mambo ambayo wamarekani walikuwa wanataka kuyasikia.

Wagombea wote walikuwa na dosari zao za kibinafsi ndo maana hata kashfa ya kunyanyasa wanawake haikupewa nafasi km ilivyokuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari.

Kuna tatizo kubwa sana ktk suala la kutafuta kura za maoni,taasisi nyingi zinafanya utafiti huo kwa ushabiki. Kwa sisi hapa hatuwezi kulaumu mtu,kwa sababu wote tulikuwa tukiandika kwa kufuata vyanzo vyao.

Tukubali siasa zimebadilika,watu hawahitaji tena hotuba nzuri bali wanataka mtu mwenye matendo yanayoonyesha anaweza kuchukua hatua.
Tanzania pia tuna Rais anayefanana na trump.

~Tujadiliane~
 
Maandamano

Kumekuwepo na maandamano katika miji ya New York, Chicago, Philadelphia, California ya makundi yanayompinga Trump kuchaguliwa kuwa Rais

Makundi haya hayapingi uchaguzi wala malalamiko bali kuonyesha kile wanachosema hofu na mashaka kutokana na kauli za Trump

Makundi haya yanaimba na kutoa kauli za matusi dhidi ya Trump kama 'not my president' n.k.

Interesting katika majina yanayotajwa lipo la Rudi Guillian ambaye ni mshauri wa Trump na mtu ambaye anasemekana kuchagiza sakata la James Comey

Baadhi wanaonyesha kuwa Comey aliamua uchaguzi huu , wengine wakisema wana hofu wataondolewa nchini na Trump, baadhi wakisema watu kama Waislam hawana nafasi tena n.k

Sehemu kubwa ya kundi hili inaundwa na millennial wanaosemwa ni wafuasi wa Bernie Sanders
Kundi jingine ni la Clinton linaloona ameshinda popular vote na amefanyiwa vitimbwi

Ni ngumu kidogo kueleza resentment kwa maneno machache ila, kinachoonekana na frustrations na reservations kwa Trump.

Tunafuatilia
 
Nationwide anti-Donald Trump protests marked by arrests, vandalism (VIDEO)
====
Kweli kushindwa kunaumiza. Sijui na huu ndiyo ukomavu wa kidemokrasia?
Yes ni ukomavu mkubwa sana wa kidemokrasia. Waandanamaji wamepewa fursa ya kuonyesha frustrations zao Polisi wakitoa ulinzi bila kuingia uhuru wao wa kutoa maoni. Hilo tu linakueleza

Hao wanaofanya vandalism wapo kwa kutumia fursa hiyo lakini mbele ya Trump Tower kuna utulivu
Wanaokwenda kinyume na kuhatarisha usalama wanachukuliwa hatua na kesho watafikishwa mahakamani ikibidi. Hiyo ndiyo sharia na demokrasia ya wenzetu

Ndiyo ni ukomavu wa kisiasa kwasababu wapinzani wamekubali matokeo na Rais amekubali kufanya transition smoothly

Hatuwezi kufananisha na uchafu mwingine tunaouona
 
Yes ni ukomavu mkubwa sana wa kidemokrasia. Waandanamaji wamepewa fursa ya kuonyesha frustrations zao Polisi wakitoa ulinzi bila kuingia uhuru wao wa kutoa maoni. Hilo tu linakueleza

Hao wanaofanya vandalism wapo kwa kutumia fursa hiyo lakini mbele ya Trump Tower kuna utulivu
Wanaokwenda kinyume na kuhatarisha usalama wanachukuliwa hatua na kesho watafikishwa mahakamani ikibidi. Hiyo ndiyo sharia na demokrasia ya wenzetu

Ndiyo ni ukomavu wa kisiasa kwasababu wapinzani wamekubali matokeo na Rais amekubali kufanya transition smoothly

Hatuwezi kufananisha na uchafu mwingine tunaouona
Mkuu ni ukomavu gani huo unaozungumzia!!? Hawa si ndo walikuwa wanamshangaa trump kukataa matokeo!!? Kitendo cha wao kutokubali matokeo halali ni kukubaliana na mashaka ya Trump. Tatizo bado lipo kwa Vyombo vikubwa vya habari ambavyo vilikuwa nyuma ya clinton huenda ndo vinachochea hii hali...!!

Km ni demokrasia mbona wameshindwa hata kutii kauli ya kiongozi wao aliyoitoa jana baada ya kushindwa? Hata Rais ambae alikuwa upande wao kasisitiza kuwa wamoja,wao wanapinga ushindi. Wengine hadi wameandika matusi. Eti "k****a yako kura yako. Kufuatia matamshi ya trump kuhusu kuwadhalilisha wanawake. Nadhani kuna tatizo zaidi ya demokrasia inayoimbwa!!
 
magode,

..maandamano na mikutano ya hadhara ni moja ya haki za kikatiba kwa Wamarekani.

..pia kupiga kura na kupigiwa kura ni haki nyingine ya msingi ya Wamarekani.

..Obama na Hillary hawawezi hata siku moja kukataza watu kuandamana au kukusanyika peacefully.

..waandamanaji hawapingi matokeo ya Uraisi. Wanapinga what they believe Donald Trump stands for.

..Mambo ya kutii viongozi hata pale wanapokwenda kinyume cha sheria na katiba hayapo kwa Wamarekani.

NB:

..hata Obama alipochaguliwa nina uhakika wapo walioandamana.
 
magode,

..maandamano na mikutano ya hadhara ni moja ya haki za kikatiba kwa Wamarekani.

..pia kupiga kura na kupigiwa kura ni haki nyingine ya msingi ya Wamarekani.

..Obama na Hillary hawawezi hata siku moja kukataza watu kuandamana au kukusanyika peacefully.

..waandamanaji hawapingi matokeo ya Uraisi. Wanapinga what they believe Donald Trump stands for.

..Mambo ya kutii viongozi hata pale wanapokwenda kinyume cha sheria na katiba hayapo kwa Wamarekani.

NB:

..hata Obama alipochaguliwa nina uhakika wapo walioandamana.
Ahsante sana
 
Mkuu Nguruvi3 na Jokakuu,
Kwa sasa kuna mjadala mkubwa kuhusu kura za maoni zinavyokwenda kinyume baada ya matokeo halisi.

Kuna haja ya kuangalia upya namna ya kutafuta hizo kura za maoni. Imetokea Brexit na sasa US. Kwa mfano ktk huu uchaguzi wamarekani walikuwa na mambo makuu 3.
1-Kilikuwa kipindi cha kufanya mabadiliko baada ya chama cha democrat kuwa madarakani kwa miaka 8,huu umekuwa km utamaduni wao.

2-Wamechoshwa na maneno matam
u ya wanasiasa,miaka yote wanachagua wanasiasa wenye hotuba nzuri za kusisimua lkn wakishachaguliwa hawafanyi waliyoahidi. Hapa ndo nguvu ya Trump ilipoanzia.



3-Kwa kiwango kikubwa mambo aliyokuwa akisema Trump ndo mambo ambayo wamarekani walikuwa wanataka kuyasikia.



Wagombea wote walikuwa na dosari zao za kibinafsi ndo maana hata kashfa ya kunyanyasa wanawake haikupewa nafasi km ilivyokuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari.



Kuna tatizo kubwa sana ktk suala la kutafuta kura za maoni,taasisi nyingi zinafanya utafiti huo kwa ushabiki.

Kwa sisi hapa hatuwezi kulaumu mtu,kwa sababu wote tulikuwa tukiandika kwa kufuata vyanzo vyao.

Tukubali siasa zimebadilika,watu hawahitaji tena hotuba nzuri bali wanataka mtu mwenye matendo
yanayoonyesha anaweza kuchukua hatua.
Tanzania pia tuna Rais anayefanana na trump.

~Tujadiliane~

..umepatia.

..waliompa ushindi Donald Trump ni wananchi wa rural america.

..wananchi hao hawakuwa a factor ktk chaguzi zilizopita za 2008 na 2012.

..waliokuwa wakifanya kura za maoni hawakulipa umuhimu mkubwa kundi hili la wapiga kura wanaoishi rural america.

..matokeo ya makosa hayo ktk ukusanyaji kura za maoni ndiyo yameleta hii surprise.

..kuhusu vyombo vya habari; kuna vyombo vya habari vyenye mlengo wa liberals (cnn)na vyombo vya habari vyenye mlengo wa conservatives(fox)

..lakini pamoja na hayo, cnn, fox, na vyombo vingine, hualika wageni/wachangiaji toka upande tofauti na wao ili kuleta usawa ktk vipindi vyao.

..cnn siku zote ni pro democrats. Lakini ktk uchaguzi huu walikuwa wakialika supporters wa Donald Trump ktk vipindi vyao. Fox news wao ni republicans lakini walikuwa wakitoa nafasi kwa supporters wa Clinton kutoa maoni yao.

..hilo ni fundisho kubwa kwa vyombo vya habari vya Tz. Vinapaswa kutoa coverage sawa kwa wagombea na siyo ku-black out upande wasiounga mkono.

..Marekani imegawanyika. Wananchi wamechoshwa na hali ngumu ya uchumi na jinsi ambavyo wanasiasa wameshindwa kuwakwamua.

..Sasa wako wanaoamini kwamba Marekani inakwamishwa na sera za Obama na democrats. Wanaoamini hivyo wamempigia kura Donald Trump.

..Wanaoamini kwamba Republicans ndiyo wanaomkwamisha Obama na kuirudisha nyuma Marekani wamempigia kura Hillary Clinton.

..Pia matokeo haya siyo suala la kuangalia juu juu tu.

..Kwa mfano, Donald Trump ameshinda Electoral College Votes lakini hajashinda popular votes.

..Pia kuna madai kwamba Donald Trump amepata kura chache (popular votes) kulinganisha na Mitt Romney ambaye alikuwa mgombea Uraisi wa Republican ktk uchaguzi wa Raisi wa 2012.

..Sasa hapi tayari unaona kuna changamoto kubwa sana ktk kuiongoza Marekani.

..Je, Donald Trump ataweza kuwaunganisha Wamarekani?

..Je, ataweza kuboresha maisha ya wananchi wa rural america ambao wameathirika na sera za utandawazi?

..Je, ataweza kupunguza hofu za wale ambao wanamuona ni racist na mtu asiyeheshimu wanawake?

..Changamoto ktk utawala wake ni nyingi.
 
Mkuu JokaKuu
Kuna information zinazidi kupatikana kila siku

Kuna taarifa kuwa Democrat Milioni 5 hawakupiga kura safari hii

Kule Wisconsin, Trump ameshinda kwa tofauti ya kura 27,000.
Kuna watu takriban 100-300K hawakupiga kura kwasababu ya mambo 'legal' !!!

Kama unavyojua, Dem wakijitokeza hushinda na kinyume chake

Kuhusu vijijini, ongezeko halikuwa kubwa kiasi hicho.
Kilichotokea ni kuwa maeneo waliyoshinda Republican tofauti ilikuwa kubwa.

Mfano, kipo kitongoji Romney alishinda kwa 51 kwa 49
Mwaka huu Trump kashinda kwa 67 kwa 33

Upande wa vitongoji vya Democrat, 2012 Obama alishinda kwa 63 kwa 37.
Mwaka huu Clinton ameshinda kwa 56 kwa 44.

Kuhusu vyombo vya habari, Rupet Murdoch anamiliki Fox, kuna WSJ, Washington post ambazo ni Republican. Hizi ni kwa uchache ukiangalia eneo zima hata radio

Vyombo vyote ikiwemo vya Republican vilibashiri kutokana na hali ilivyo.
Internal poll ya Reince Prebius wa RNC ilionyesha mapungufu tofauti na matokeo

Hatudhani vyombo vya habari vilipendelea au vilikuwa na ushabiki. Kilichotokea ni unusual
Kwa mfano, suala la Comey leo linaonekana kuathiri Democrat kuliko ilivyodhaniwa
1. Dem wengi walikuwa demoralized na kutopiga kura wakijua mgombea wao anashtakiwa
2. Trump alieleza umma indictment tayari hiyo ika excite GOP Base na kudemoralize Dem

Data za baadhi ya wachambuzi ''zinaeleza'' Comey alipotoa tangazo, Clinton ali loose
Hili nalo ni la kufuatilia. Ukisikiliza waandamanaji jana na jina la Rudi, kuna jambo nadhani

Kuna suala la Blacks, kwanini idadi yao ilipungua? Siyo NC, bali Michigan na kwingine

Kuna Wikileaks ambayo effect yake si emails tu, bali ilivyochonganisha Dem

Kwahiyo si factor moja au mbili ni nyingi. Insitutions na media zina scramble kutafuta what went wrong this time around hawakuwa na precision au kuwa within error of margin
 
Nguruvi3,

..halafu kuna UTITIRI WA KESI dhidi ya Donald Trump.

..kati ya kesi hizo zipo ambazo zinaweza kulazimisha impeachment process.

..kama Democrats wakiamua kumuandama Donald Trump, kama ambavyo Republicans wamekuwa wakiwaandama kina Clinton, basi tutashuhudia mengi miaka 4 inayokuja.
 
Nguruvi3,

..halafu kuna UTITIRI WA KESI dhidi ya Donald Trump.

..kati ya kesi hizo zipo ambazo zinaweza kulazimisha impeachment process.

..kama Democrats wakiamua kumuandama Donald Trump, kama ambavyo Republicans wamekuwa wakiwaandama kina Clinton, basi tutashuhudia mengi miaka 4 inayokuja.
Hizi vurugu zina madhara sana!! Wakishindwa kuzidhibiti, ninavyowajua hawa Wamarekani wataanzisha vita na nchi nyingine ili kuwaunganisha pamoja. Lazima watafute mbinu ya kuwaunganisha!!Na hotuba ya Hillary haukuwa nzuri, kama tulivyosema mwanzo kuwa huwa na kinyongo!!Jana alihimiza wafuasi wake waendelee kupambana kwa kile wanachokiamini!!Hii kauli hakuiweka Sawa. Binafsi naona kama ina kauchochezi fulani nikijaribu kuoanisha vurugu hizi.

Sema mbaya zaidi ni yule jamaa wa Trump ambaye amewaita wanaoandama ni" crybabies ".
Yaani Moto huu wasipouzima...kuna hatari mbele , kuna nchi inaweza kuvamiwa ili iwaunganishe US. Si mnakumbuka kipindi cha occupy wall Street!! nchi (US) ilibi ijiingize kwa nguvu kumuondoa Ghaddaf (R.I.P)wa Libya .
 
Hizi vurugu zina madhara sana!! Wakishindwa kuzidhibiti, ninavyowajua hawa Wamarekani wataanzisha vita na nchi nyingine ili kuwaunganisha pamoja. Lazima watafute mbinu ya kuwaunganisha!!Na hotuba ya Hillary haukuwa nzuri, kama tulivyosema mwanzo kuwa huwa na kinyongo!!Jana alihimiza wafuasi wake waendelee kupambana kwa kile wanachokiamini!!Hii kauli hakuiweka Sawa. Binafsi naona kama ina kauchochezi fulani nikijaribu kuoanisha vurugu hizi.

Sema mbaya zaidi ni yule jamaa wa Trump ambaye amewaita wanaoandama ni" crybabies ".
Yaani Moto huu wasipouzima...kuna hatari mbele , kuna nchi inaweza kuvamiwa ili iwaunganishe US. Si mnakumbuka kipindi cha occupy wall Street!! nchi (US) ilibi ijiingize kwa nguvu kumuondoa Ghaddaf (R.I.P)wa Libya .
Niliisikiliza hotuba ya Clinton, it was perfect and gracious.

Alichosema Clinton ni kuwa wafuasi wasimamie kile wanachokiamini kutokana na sera alizokuwa ana nadi. Akataja anayosimamia,kwa ufupi ni 'inclusion' ya America
Akawataka wampe Trump ushirikiano

Nimefuatili vyombo vya habari, hata wasemaji wa Trump wanatumia maneno ya Clinton na Obama kuwa sasa ni wakati wa ku 'unite' taifa.

Hakuna anayelaani au kuonyesha shaka na concession speech

America wanajua wanachotaka, na wale wanaoandamana hoja yao kubwa ni hofu

Hofu ya maneno ya Trump kuhusu immigrants, Moslems, LBGT, Women n.k.

Kibaya zaidi ni wanapokumbuka 'lock her' na kauli kama zile za kusimama na ku shoot mtu
 
Nashukuru bandugu na naona mnakasha unaendelea vizuri...bahati mbaya nilitingwa kidogo na mambo binafsi lakini bado nipo pamoja nanyi msiwe na wasi wasi. Nimepitia michango mbali mbali na bado naendelea kusoma kabla sijaweka my 50 cents nisije nikakurupuka...naomba tu subira.

Hata hivyo naomba nimjibu TUJITEGEMEE kwa maoni yake kuhusu maandamano kwamba hiyo ndiyo demokrasia yenyewe... raia kuwa huru kuonesha hisia zake matarajio yasipofikiwa. Wao huita blowing off steam na hata wanaozidisha hukamatwa lakini huachiwa bila kushtakiwa.

Ninayo mengi ya kushare nanyi ila nawaombeni mnipe muda.
 
Nguruvi3,

..halafu kuna UTITIRI WA KESI dhidi ya Donald Trump.

..kati ya kesi hizo zipo ambazo zinaweza kulazimisha impeachment process.

..kama Democrats wakiamua kumuandama Donald Trump, kama ambavyo Republicans wamekuwa wakiwaandama kina Clinton, basi tutashuhudia mengi miaka 4 inayokuja.
Kuna masuala kama la tax file, hilo wachunguzi watalifuatilia na ipo siku tutajua ukweli

Pili, kuna suala la Trump University nalo linarindima

Nadhani ni suala la muda tu Dem watatoka kwa namna itakayomsumbua
 
Hizi vurugu zina madhara sana!! Wakishindwa kuzidhibiti, ninavyowajua hawa Wamarekani wataanzisha vita na nchi nyingine ili kuwaunganisha pamoja. Lazima watafute mbinu ya kuwaunganisha!!Na hotuba ya Hillary haukuwa nzuri, kama tulivyosema mwanzo kuwa huwa na kinyongo!!Jana alihimiza wafuasi wake waendelee kupambana kwa kile wanachokiamini!!Hii kauli hakuiweka Sawa. Binafsi naona kama ina kauchochezi fulani nikijaribu kuoanisha vurugu hizi.
magode, pamoja na kuwa yawezekana una chuki binafsi na Marekani, lakini yabidi uelewe siasa ya Marekani ilivyo...kumbuka madai ya Trump alipoulizwa kama atayakubali matokeo ikitokea akashindwa, kumbuka madai ya wafuasi wake iwapo Clinton angeshinda na jinsi ambavyo wangekwamisha juhudi zake katika kutekeleza majukumu yake kama Rais na kumbuka ahadi zao wakati Obama ameshinda uchaguzi wa mwaka 2008 kwa kishindo lakini wakaapa kuhakikisha anashindwa na hivyo kuwa one term president.

Hayo hayakuwa maneno tu ya mitaani, waliyatekeleza kwa vitendo. Kuliibuka kikundi cha Tea Party ambacho kilikuwa kinafanya mikutano huku baadhi ya wahudhuriaji wakihakikisha bunduki zao zinaonekana. Na nkuapia Donald Trump angeshindwa, tunayoyaona leo yangekuwa kama cha ndimu kulinganishwa na ambacho wangekifanya. Hiyo ndiyo Marekani na hiyo ndiyo demokrasia yao inayotoa uhuru wa kujieleza, kuandamana na kupinga wazi wazi mambo wasiyokubaliana nayo.

Ushindi wa Trump pia ni wa tofauti kidogo kwani ingawa kwa popular votes wengi wamemkataa lakini kulingana na taratibu walizojiwekea kashinda Urais na chama chake kutwaa congress nzima (House na Senate). Hii kwa namna fulani inamnyima full mandate kama ilivyokuwa kwa Obama na ili aweze kufanikiwa itabidi anyenyekee kidogo lakini akiendekeza ujeuri, atapata wakati mgumu sana. Jana tu kawalaumu vijana wanaoandamana lakini leo tayari karekebisha baada ya ushauri.

Katika Jamhuri, maoni ya wachache lazima yapewe kipaumbele na siyo kwamba ukishinda basi utwae kila kitu kama hapa kwetu. Hillary Clinton keshakubali matokeo pamoja na kwamba kapata kura nyingi zaidi kutoka kwa wananchi wa Marekani. Pia tabiri (polls) zilizokuwa zikitolewa na vyombo mbalimbali hazikukosea kama unavyodai kwani ingekuwa hapa kwetu moja kwa moja Clinton angetangazwa mshindi. Hilo moja lakini la pili tabiri hizo zimepunguza kwa kiasi fulani kura za Clinton kwa sababu wengi hawakujitokeza kama ilivyotegemewa.


14937428_10157685866220285_3865324216133737442_n.jpg

Naomba uitafakari hii picha inayoonekana hapa juu ili iweze kukusaidia kuelewa kwa nini Donald Trump kaweza kuwa Rais wa 45 wa Marekani. Ni mara ya kwanza Rais anachaguliwa kwa kupata kura asilimia 26% tu za waliojiandikisha kupiga kura (registered voters)...tofauti hapa ni kwamba aliyepigiwa kuwa na wananchi wengi hakutangazwa Rais. Baadaye nitaeleza kwa nini imetokea hivyo na ni sababu zipi ziliwazuia wengi kutokujitokeza.
 
Mag3,

..ungefunguka kidogo kuhusu election circles za Marekani ili hoja yako hapo juu ieleweke vizuri zaidi.

Cc magode, TUJITEGEMEE, Mwalimu
JokaKuu, kuna mambo ya kuzingatia wakati tunafanya uchambuzi kulingana na uchaguzi huu ambao umempa Donald Trump ushindi ambao kwa kiwango chake si mdogo. Mandate aliyopata ni kubwa na kama hatafanya kosa alilofanya Obama anaweza akafanikisha mengi katika miaka miwili. Kabla ya yote naomba tulinganishe na hali ilivyokuwa chaguzi mbili za awali...

Mwaka 2008

Barack Obama - Democrat

· Popular votes...69,498,516
· Electoral votes...365
· Senate…57

John McCain - Republican

· Popular votes...59,948,323
· Electoral votes...173
· Senate…41

Pamoja na huu ushindi wa kishindo uliojumuisha na Congress (House na Senate), Obama katika kutaka kuonesha kwamba ni unifier kama alivyoahidi kwenye kampeni zake, kipaumbele chake kikawa ni kuwashirikisha Republicans. Badala ya kutumia nafasi yake kutekeleza ahadi zake huku Congress nzima ikiwa nyuma yake akaamua kutafuta muafaka kwa kila alichotaka kukifanya.

Hivyo akataka maamuzi yoyote ya serikali yapate baraka kutoka kwa pande zote na yasionekane partisan kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake. Ambacho hakutilia maanani ni kwamba Republicans walishaamua kitambo kutompa ushirikiano wowote ule lengo likiwa ni kuhakikisha anashindwa na hapati awamu ya pili na kwa kiwango fulani walifanikiwa sana katika hilo.

Baada ya kumkwamisha kutekeleza hadi zake Republicans hao hao wakaanza kumlaumu kama dhaifu kwa kutofanya lolote na huku mandate anayo. Matokeo ya uchaguzi wa mid-term mwaka 2010 kama yangehusisha ya Urais angeshindwa kwani wananchi walianza kupoteza imani naye hivyo kupoteza House na kubakiwa tu na Senate. Katika uchaguzi huo matokeo ya kura (popular votes) yalikuwa ni haya;

Mwaka 2010

· Democrats…29,110,733
· Republicans…32,680,704

Ni baada ya uchaguzi huu ndipo Obama ni kama vile alizinduka na kuanza juhudi za kuhakikisha mipango aliyokuwa nayo inatekelezwa lakini alikuwa tayari kachelewa. Akabakiwa tu na njia moja ya utekelezaki na ni kwa kutumia madaraka aliyopewa kikatiba kama mkuu wa nchi. Hata hivyo wananchi walishalishwa sumu ya kutosha na haikuwa rahisi kuwashawishi kumuunga mkono kama awali. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2012, matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;

Mwaka 2012

Barack Obama - Democrat

· Popular votes…65,915,795
· Electoral votes 332
· Senate…51

Mitt Romney - Republican

· Popular votes... 60,933,504
· Electoral votes... 206
· Senate47

Kama unavyoona hapo juu tayari alianza kupoteza wajumbe kwenye Senate na ilikuwa ni swala la muda tu apoteze kabisa na hiyo Senate. Uchaguzi wa mid-term mwaka 2014 ndio ukawa mbaya sana kwa Obama kwani safari hii akapoteza Congress (House na Senate) na hivyo kukosa nguvu kabisa ya kusimamia maamuzi ya kiutekelezaji. Kama uchaguzi huu ungekuwa wa kumpata Rais, Obama angeshindwa vibaya sana.

Mwaka 2014

· Democrats…35,624,357
· Republicans…40,081,282

Matokeo haya yalitoa indiketa kuonesha mwelekeo wa uchagzui wa mwaka huu na kweli Democrats wamevuna walichopanda. Hakuna namna Democrats wangeshinda uchaguzi wa mwaka huu na hapo ndipo Republicans wakafanya kosa moja kubwa...wakamchagua Donald Trump. Angechaguliwa mwingine yeyote yule Republicans wangeshinda kirahisi na hawangepata tabu kama walivyopata kwa Trump.

Je ni kwa nini pamoja na hilo bado Trump kashinda na kwa nini naelezea hii historia? Nitaendelea nikipata nafasi…
 
Kabla sijaingia kwenye mambo mengine naomba nieleze kwa nini vijana, millenials wa Generation Y, wako mtaani wakiandamana. Kwanza hawampendi Trump na pili wengi wao hawakudhani Wamarekani wanaweza kumchagua mtu kama Trump. Nakumbuka alivyoongea moja wao kwa hisiaa kali akieleza kwa nini hakuona umuhimu wa kupiga kura akidai eti alijua Clinton atashinda tu...! Zipo kura nyingi zimeharibika, vijana wakiandika neno harambe badala ya jina la mgombea!

Donald Trump - Republican


· Popular votes...60,261,924
· Electoral votes...290
· Senate…51


Hillary Clinton - Democrat

· Popular votes...60,828,358
· Electoral votes...232
· Senate…48

Kwa matokeo kama yalivyo mpaka sasa ni kwamba Hillary Clinton anaongoza kwa kura 566,434 (popular votes) na kwa hali ya siasa ilivyozua utata safari hii, vijana wale wale wako mitaani wakitaka majibu kwa maswali yafuatayo;

  1. Je katika kura zote zilizopigwa ziko kura za wananchi zilizo muhimu kuliko zingine?
  2. Kama kura zote zinalingana kwa nini chama kilichopata kura nyingi kipate electoral votes chache?
  3. Kama raia wote wana haki sawa inawezekanaje aliyepigiwa kura chache atangazwe mshindi?
Mpaka sasa na kwa namna Donald Trump anavyotaka kuunda baraza yake la mawaziri, yapo mambo kama hatayatilia maanani anaweza akapata shida kubwa kuliko ya viongozi waliomtangulia. Pamoja na hayo naomba niwaondoe hofu, taifa la Marekani limepitia misukosuko ya kisiasa kama hii toka liundwe na halitasambaratika kama maadui wake wanavyowaombea; sana sana itazidi tu kuimarika.

Wanajamvi nivumilieni kidogo, muda ni mfupi lakini baadaye nitajaribu kuelezea ni kwa nini mtu kama Donald Trump kapata ushindi ambao haukutegemewa kabisa.
 
TUJITEGEMEE, hii ni kwa ufahamisho tu wa Demokrasia inavyofanya kazi nchini Marekani. Ingekuwa hivyo hapa Tanzania leo hii Mwakilishi wa jiji la Arusha hangesumbuliwa na viongozi limbukeni waliokataliwa na wana Arusha.

Joint Statement from California Legislative Leaders on Result of Presidential Election


Wednesday, November 09, 2016

SACRAMENTO – California Senate President pro Tempore Kevin de León (D-Los Angeles) and California Assembly Speaker Anthony Rendon (D-Paramount) released the following statement on the results of the President election:

Today, we woke up feeling like strangers in a foreign land, because yesterday Americans expressed their views on a pluralistic and democratic society that are clearly inconsistent with the values of the people of California.

We have never been more proud to be Californians.

By a margin in the millions, Californians overwhelmingly rejected politics fueled by resentment, bigotry, and misogyny.





California_state_flag_c0-30-700-438_s885x516.png


The largest state of the union and the strongest driver of our nation’s economy has shown it has its surest conscience as well.

California is – and must always be – a refuge of justice and opportunity for people of all walks, talks, ages and aspirations – regardless of how you look, where you live, what language you speak, or who you love.

California has long set an example for other states to follow. And California will defend its people and our progress. We are not going to allow one election to reverse generations of progress at the height of our historic diversity, scientific advancement, economic output, and sense of global responsibility.

We will be reaching out to federal, state and local officials to evaluate how a Trump Presidency will potentially impact federal funding of ongoing state programs, job-creating investments reliant on foreign trade, and federal enforcement of laws affecting the rights of people living in our state. We will maximize the time during the presidential transition to defend our accomplishments using every tool at our disposal.

While Donald Trump may have won the presidency, he hasn’t changed our values. America is greater than any one man or party. We will not be dragged back into the past. We will lead the resistance to any effort that would shred our social fabric or our Constitution.

California was not a part of this nation when its history began, but we are clearly now the keeper of its future.
 
Kwa ufahamisho wa wana JF kuhusu uchaguzi Marekani.
Mpaka leo hii tunapoongea, Donald Trump bado ni Rais mteule tu wa Marekani mpaka pale atakapopigiwa kura na wajumbe wote wa Electoral College na akipata kura za kutosha atasubiri mwakani kuapishwa kuwa Rais wa 45 wa USA. Katika uchaguzi huo inategemewa kwamba kila mjumbe atapiga kura kulingana na msimamo wa chama chake na ikitokea hivyo moja kwa moja Donald Trump atasubiri tu kuapishwa.

Lakini ikitokea wajumbe kadhaa wa GOP wakaamua kutompa kura Rais wao mteule na badala yake kumpigia kura Hillary Clinton, huyo ndiye atakuwa Rais. Swali hapa ni je hali hii inaweza kutokea? Jibu ni ndiyo ingawa si rahisi kwa sababu mjumbe ambaye atafanya hivyo atakuwa amekisakiti chama chake. Imewahi kutokea kwa mjumbe moja ama wawili kubadili msimamo lakini bila madhara yoyote kwa Rais mteule.

Kwa sasa kuna petition inatembezwa mtandaoni kujaribu kuwashinikiza wajumbe wa Electoral College kutoka chama cha GOP kutompigia kura Trump. Petition hii mpaka sasa imeshapata sahihi zaidi ya 2,000,000 na watu wanazidi kujitokeza kuweka sign zao kuunga mkono. Pamoja na hatua hii kuwa na nafasi ndogo ya kufaulu, idadi ya wanaounga mkono inategemewa kukua na hata kuvuka milioni tatu inayotakiwa.

Kura hii imepangwa kupiwa tarehe 19 Desemba mwaka huu kabla ya Rais kuapishwa mwezi unaofuata. Wanaoratibu zoezi hili wanadai wanafadhaishwa na matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika na Donald Trump kushinda huku akiwa na kura chache kutoka kwa wananchi. Pamoja na hilo wanadai matokeo ya uchaguzi yamesababisha hali ya mshtuko, hofu na hasira miongoni mwa wananchi mbambali nchini Marekani na Duniani.

 
Back
Top Bottom