Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu historia ya marekani ndivyo ilivyo.Huu ulinzi wanaopewa sasa si wa bure.Marais wameshauwawa kwasababu za tofauti ambazo zinafanana na hii niliyoitaja(kuwa kinyume na Israel)
Ni muhimu sana watu muelewe kwamba ktk Utawala huu kuna world Order.. Kuna watu juu yetu ambao ndio hupanga na kuamua wafanye nini..Al Pasino ktk Scarface alisema kwanza unahitaji uwe na Fedha ambayo itakupa nguvu na ukisha pata nguvu utaitawala dunia. Fedha - ni Principal ya Wayahudi hata kabla ya Yesu japokuwa alijaribu sana kuwaasa wasifikiria fedha itawapatia pepo ama uzima wa milele, na pengine yawezekana hii kuwafuata ktk fedha kuwa sababu kubwa ya Wayahudi kuto mkubali Yesu..
Mkuu hayo matatizo tunayo sana sisi waafrika, kuna wanaojinasibisha na uarabu, u jewish etc.Mkuu Nguruvi3,
Kweli Obama hana matatizo na Waisrael watu wengi hasa waafrika wanajidanganya kumnasibisha Obama na uafrika, Obama kalelewa na bibi yake na kusomeshwa mpaka apo alipofika ni matunda ya bibi yake Madelyn Lee ambaye ni jewish alikuwa mfanyakazi wa benki...hata ukiangalia Obama wakati anagombea urais 77% jewish walikuwa upande wake wakimuunga mkono.
Jewish wamekuwa na nguvu Marekani na Ulaya sababu wana nguvu za kiuchumi makampuni makubwa wanayamiliki wao Banking and finance, Cosmetics, Food and ratail, Newspapers and publishing, Real estate, Technolgy, Televion, film and vedeo...halafu idadi yao ni ndogo sana Marekani wapo 2.5% baadhi ya raia wa Marekani wanapiga kelele kwa nini nchi yao imekuwa ikitumiwa na jewish hata kwenye mambo yasiyokuwa ya lazima.
Ni suala la muda tusubiri tuone siasa mpya za Mashariki ya Kati.
Somewhat true, but not all the way true, kwa mfano, mataifa mengi ya kiarabu yametumia mafuta kama silaha ya kuinfluence culture and so forth.
HALI YA MISRI BADO TETE
Rais Morsi alitangaza kurudishwa kwa bunge lililovunjwa na baraza la kijeshi.
Mtafaruku umeendelea baada ya mahakama kupinga agizo la Morsi na kwamba kuliita bunge ni kukaidi amri ya mhimili mwingine. Siku za nyuma tulisema Brotherhood walikaa kimya wakati wa uchaguzi bunge likivunjwa ili wa-focus katika hatua yao ya mwisho ya kuchukua utawala.
Taratibu tunaona kucha za Brotherhood zikichomoza. Ni ukweli usiopingika kuwa Brotherhood walishinda viti vya bunge na Urais. Ni ukweli kuwa baraza la kijeshi chini ya Tantawi halikupaswa kuvunja bunge halali lililochaguliwa na wananchi.
Tunajua kuwa hata uapishwaji wa Morsi ulifanyika mara mbili, moja ikiwa ni mbele ya jengo la mahakama linaloelekeana na Hospitali maarufu ya kijeshi. Hospitali hiyo ndipo alipotangazwa kufariki Anwar Sadat, ndiyo hospitali aliyofia Shah wa Iran na ndiyo anapotibiwa Hosni Mubarak.
Baraza la kijeshi lilitaka Morsi aelewe kuwa kuna mihili mingi ya kikatiba na mingine isiyo rasmi.
Msuguano wa Mhakama, serikali, bunge na baraza la kijeshi unaonekana kupamba moto.
Hili ndilo changamoto tulilosema siku za awali kuwa linamkabili Morsi.
Jambo la kushangaza ni kuwa nchi za magharibi hazijalikemea jeshi kwa kuingilia serikali iliyochaguliwa kihalali.
Huu ni ushahidi kuwa jeshi linaungwa mkono kama lilivyoungwa mkono wakati wa kumuondoa Mubarak.
Bado nchi za magharibi hazijaridhika na uchaguzi halali wa Misri. Wanawajua Brotherhood vema na hakika hawana usingizi
Siku za karibuni tutashuhudia makundi Tahariri Square kumuunga mkono Morsi, na mengine kuunga mkono Jeshi.
Jeshi halitaki kuachia 'utamu' kwasababu linapata msaada wa dola Bilioni 10 kutoka marekani kila mwaka. Hayo ni sehemu ya mkataba wa Camp David.
Uwezekano wa Morsi kupata 'ajali' ya kisiasa ni mkubwa sana hasa kwa jinsi jeshi lilivyochukia kuporwa madaraka.
Ukitaka kujua jinsi jeshi linavyoendesha mambo kichini chini ni pale Mubarak akiwa mfungwa kama wengine bado anatibiwa katika Hospitali ya jeshi. Muda wote wa mashataka alikuwa katika Hospitali ya kijeshi.
Hali ya Misri bado haijatengemaa na tutaendelea kujadili kadri itakavyojuzu
Tusemezane
Mkuu Nguruvi3,
Ni kweli hali bado tete nchini Misri, baada ya rais Mohamed Morsi kutoa agizo bunge kulejea kwenye vikao vyake, Baraza la Kijeshi linalotawala limesema kuwa ni sharti raia wote wa nchi hiyo waheshimu uamuzi wa mahakama ya katiba, kama unavyosema tutashuhudia makundi ya raia wa Misri kwa mara nyingine tena wakielekea kwenye viwanja vya Tahariri.
Walikuwa wakishare philosphy ya "Pan Africanism", walikuwa the strongest believers and the champions for the cause at that period and time.Hopefully imesaidia...Kama niko wrong, basi watanisahihisha waungwana uliowataja.
Nilikuwepo mwaka 1966 alipokuja Gamal Abdel Nasser kutembelea Tanzania. Nilijipanga mstari pale Forodhani na wanafunzi wenzangu karibu na Kilimanjaro Hotel. Nasser na Mwalimu walipita kwenye gari iliyokuwa wazi na nilimwona Nasser kwa karibu. Great times, great memories.
Ni kweli jmushi1, wenyewe siku hizi wanaita 'Umajumuhi' kama siajakosea (Pan Africanism).Walikuwa wakishare philosphy ya "Pan Africanism", walikuwa the strongest believers and the champions for the cause at that period and time.Hopefully imesaidia...Kama niko wrong, basi watanisahihisha waungwana uliowataja.
Kama alivyoeleza JMushi1, hawa jamaa kwanza kabla ya Uhuru wa nchi zetu walikuwa wakikutana na kuzungumza juu ya Uhuru wa nchi za Kiafrika na kuunda Umoja wa nchi hizo kama USA ilivyo..Na walifikia maamuzi haya kutokana na kwamba kuikomboa Afrika tu yaweza kuwa rahisi lakini ku sustain uhuru huo wakati Mali na Utajiri wote uko Afrika itakuwa ngazi ngumu sana hivyo kuungana kwa Afrika tu ndio kunaweza kuleta nguvu ya pamoja ktk kujitetea against mataifa Makubwa.
Mkandara,Kama alivyoeleza JMushi1, hawa jamaa kwanza kabla ya Uhuru wa nchi zetu walikuwa wakikutana na kuzungumza juu ya Uhuru wa nchi za Kiafrika na kuunda Umoja wa nchi hizo kama USA ilivyo..Na walifikia maamuzi haya kutokana na kwamba kuikomboa Afrika tu yaweza kuwa rahisi lakini ku sustain uhuru huo wakati Mali na Utajiri wote uko Afrika itakuwa ngazi ngumu sana hivyo kuungana kwa Afrika tu ndio kunaweza kuleta nguvu ya pamoja ktk kujitetea against mataifa Makubwa.
Lakini tukakutana namatatizo makubwa zaidi ya kuunda Umoja huo maana ikumbukwe tu ya kwamba hakuna nchi ambayo zimeungana pasipo vita na maguvu isipokuwa muungano wa Tanzania na Zanzibar. Union karibu zote duniani zimetangauliwa na vita na kutekana iwe Ethiopia, Somalia, Nigeria, USA, Russia au Uingereza na zote leo hii zinatafuta kutengana kama hazijatengana tayari.. NI Marekani na UK tu ndio wamebakia wagumu kutokana na sheria zao kali kwa yeyote anayehubiri au kwenda kinyume cha Union zao..
We failed na ndio maana leo hii Afrika tumerudi ktk kutawaliwa Kiuchumi. Na inasikitisha sana kuwasoma watu wengi wakidhania kwamba kuwa na uhuru wa mipaka ndio hasa maana ya Uhuru ama waasisi wetu walipigania. Vita ya uhuru wetu ilityokana na umiliki wa rasilimali na maliasili zetu (UCHUMI) nje ya hapo tungeendelea kutawaliwa hadi kiyama maana swala la uongozi bora na kulinda mipaka hakuna kama wazungu wakoloni isipokuwa tatizo lao ni kupora rasilimali zetu kuendeleza nchi zao ndio hasa sababu ya kuutafuta Uhuru lakini maajabu leo ni jambo la kawaida kabisa.. Viongozi wetu wakisema tena bila aibu kwamba hatuna mtaji hivyo sii sii vibaya kutawaliwa kiuchumi ikiwa wananchi watapewa ajira...