Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

jmushi1

Mkuu naomba ufafanuzi zaidi na ikiwezekana tupatie mifano hai kama ipo.
Mkuu historia ya marekani ndivyo ilivyo.Huu ulinzi wanaopewa sasa si wa bure.Marais wameshauwawa kwasababu za tofauti ambazo zinafanana na hii niliyoitaja(kuwa kinyume na Israel)

Ukiwa kinyume na Israel kwasasa, ni sawa na wakati ule wa vita kati ya South na North, ambapo South walitaka utumwa uendelee where as North walikuwa wakipinga, however marais wa dizaini hiyo ya kupinga utumwa waliuwawa, mfano Abraham Lincolin,(na siyeye peke yake, listi ni ndefu ya marais waliouwawa kwasababu zinazofanana na hizo),hilo lilitokana na kwamba wadau wakubwa ie mapebari na wanausalama wa maslahi yao, walikuwa ndo wenye power na kucall the shots.

Same as now, wadau wakubwa ie CIA nk, hao sidhani kama watakubaliana na issue ya kuwa kinyume na Israel, hizo propaganda za wananchi za kisiasa ambazo wanasema Obama haipendi Israel si za kweli, pengine hata wao wanazipenda kwasababu zinawapa leverage kwenye kusuluhisha migogoro ya middel east espeacially huo wa Palestine.
 
jmushi1

Mkuu naomba ufafanuzi zaidi na ikiwezekana tupatie mifano hai kama ipo.
Ni muhimu sana watu muelewe kwamba ktk Utawala huu kuna world Order.. Kuna watu juu yetu ambao ndio hupanga na kuamua wafanye nini..Al Pasino ktk Scarface alisema kwanza unahitaji uwe na Fedha ambayo itakupa nguvu na ukisha pata nguvu utaitawala dunia. Fedha - ni Principal ya Wayahudi hata kabla ya Yesu japokuwa alijaribu sana kuwaasa wasifikiria fedha itawapatia pepo ama uzima wa milele, na pengine yawezekana hii kuwafuata ktk fedha kuwa sababu kubwa ya Wayahudi kuto mkubali Yesu..

Waswahili wanasema Mchagga akisikia mlio wa fedha lazima ageuke, basi Myahudi ndiye huitengeneza fedha hiyo hivyo sii mlio tu anaijua hadi harufu yake. Fedha ikifika mkononi mwako jua imepitia kwake.. They control world Economy na ukisha kuwa na nguvu hiyo bila shaka uta control dunia. Leo hii huwezi kufika hata wagombea wawili wa mwisho ktk Urais wa Marekani kama hukubaliani na Israel...

Na pengine nisikutishe zaidi.. soon Tanzania pia tutakuwa tunachaguliwa marais na kundi hilo hilo baada ya kuruhusu taasisi fulani ya Kimarekani (jina kampuni) kuingia nchini.. And for that tusitegemee tena mkombozi kutoka vyama vya siasa! hadi hapo atakapotokea Chavez au Kagame wetu..Another sign wameingia wapi - Ukiona kiongozi yeyote nchi maskini anasifiwa sana na Marekani au nchi za magharibi basi jua wameisha mweka mikononi, (The weakest) na yule anayechukiwa sana basi huyo hakubali kununuliwa na kuendeshwa (The strongest). watatafuta njia ya kumwondoa hivyo sii swala la Marekani tu sasa hivi limekuwa kiongozi yeyote duniani asitekubaliana nao lazima aondolewe..
 
jmushi1

Mkuu naomba ufafanuzi zaidi na ikiwezekana tupatie mifano hai kama ipo.

Ngongo,

Siasa za Misri zina historia ndefu sana na viongozi wake wamepitia misukosuko mingi sana kutokana na mgogoro wa Mashariki ya Kati kwenye orodha ya Marais wa Misri hakuna hata mmoja ambaye kauuliwa na Marekani au na Israel kuanzia..

1. Ali Muhammad Naqib 1953

2. Gamal Abdel Nasser 1970

3. Anwar As-Sadat 1981

4. Sufi Abu Taleb 1981 huyu alikuwa mtendaji tu.

5. Muhammad Hosni Mubaraka 1981 mpaka 2011

6. Mohamed Morsi
 
Last edited by a moderator:
Kwa watu wanaodhani kuwa Obama ana matatizo na Israel wanadanganyika kidogo. Obama licha ya kuwapa mamilioni ya fedha katika kipindi chake amewapa teknolojia ya juu sana ya kijeshi.

Waisrael wametawala sehemu kuu ya uchumi wa nchi za Magharibi. Ili kuweza kufanisha azma zao wameteka vyombo vya habari vingi sana na hivyo kuweza kueleza kile wanachokitaka ukiamini.

Ujio wa televisheni ya Aljazira umewasumbua sana kwasababu habari za pande zote zinapatikana. Siku za mwanzo nchi za magharibi zilipinga kuruhusu Aljazera, utashangaa sasa hivi wengi wanaipenda hasa wale wanaotaka kuona pande zote mbili za shilingi.

Mtangazaji kama Larry King na Wolf Blitzer wote ni jews. Hadi hapo usitegemee waeleze habari nyingine tofauti na utashi wa masilahi yao. Mfano mwingine ni gazeti la the SUN hili linamilikiwa na jews n.k.

Tofauti ya Obama na Israel inakuja pale Waisrael wanapotaka kufanya ubabe unaokinzana na mtazamo wa Obama.
Kwa mfano, Obama aliitaka Israel isitishe ujenzi katika jiji la Jerusalem ili kuwashawishi Wapalestina warudi mezani.
Hakuwa na maana ya kuwapendelea bali kuwepo na hatua za kurudi mezani kama alivyofanya Bill Clinton.

Waisrael wakamdharau kwa kutangaza ujenzi zaidi siku makamu wa Rais Joe Biden alipowasili Tel Aviv. Hili liliwakera sana Wamarekani na wengine kujiuliza Israel ni kwanini inaleta jeuri na dharau hata White House.
Obama alimwita Netanyahu White House na kumpa mapokezi ya dharau sana kama njia ya kujibu kiburi.
Netanyahu alipokelewa na afisa mahusiano na wala hapakuwepo 'press' pale Rose Garden

Ugomvi mwingine ni pale Israel inapotaka kuchukua hatua za kumshambulia Iran. Obama anafahamu kuwa hilo likitokea basi Marekani haina budi bali kuingia vitani tena kumlinda Mwisrael. Katika kipindi hiki ambacho Wamarekani wamechoshwa na vita hilo hakuna anayelikubali. Wakati huo huo kuna shinikizo kutoka Tel Aviv kufanya shambulio.

Kuna mtu amesema katika nyuzi moja kule jukwaa la siasa kuwa Israel ina nguvu kuliko taifa lolote.
Hapa kuna kupotoka sana kwasababu nguvu za Israel zipo mgongoni mwa Marekani. Ni kweli wana nguvu lakini si kiasi hicho. Lakini pia mtu anaposema wana nguvu lazima aangalie vigezo vingi sana na siyo matukio machache.

Tukio kama la mwaka 1967 la vita ya siku sita, ukweli ni kuwa CIA walikuwa wameji-infiltrate na mpango mzima wa akina Gamal Adel Nasar ulikuwa unajulikana. Hilo lilimpa sana nafasi Mwisrael kushinda vita.

Kipimio kizuri tu ni kile cha Hezbollah ambao Israel imekiri kuwa pamoja na kutumia nguvu kuwa vita ile walishindwa. Walishindwa kwasababu ilibaki bomoa bomoa na hakuna mkakati. Kuna wakati walipata kipigo na kulazimika kurudi nyuma jambo lisilo la kawaida.
 
Mkuu Nguruvi3,

Kweli Obama hana matatizo na Waisrael watu wengi hasa waafrika wanajidanganya kumnasibisha Obama na uafrika, Obama kalelewa na bibi yake na kusomeshwa mpaka apo alipofika ni matunda ya bibi yake Madelyn Lee ambaye ni jewish alikuwa mfanyakazi wa benki...hata ukiangalia Obama wakati anagombea urais 77% jewish walikuwa upande wake wakimuunga mkono.

Jewish wamekuwa na nguvu Marekani na Ulaya sababu wana nguvu za kiuchumi makampuni makubwa wanayamiliki wao Banking and finance, Cosmetics, Food and ratail, Newspapers and publishing, Real estate, Technolgy, Televion, film and vedeo...halafu idadi yao ni ndogo sana Marekani wapo 2.5% baadhi ya raia wa Marekani wanapiga kelele kwa nini nchi yao imekuwa ikitumiwa na jewish hata kwenye mambo yasiyokuwa ya lazima.

Ni suala la muda tusubiri tuone siasa mpya za Mashariki ya Kati.
 
Mkuu hayo matatizo tunayo sana sisi waafrika, kuna wanaojinasibisha na uarabu, u jewish etc.

On the other note, huwa najiuliza, kati ya hao "Ten percent" wa US wanaopigiwa kelele na wale wa "99%", wangapi ni jewish?

Ukweli ni kwamba Jewish wameshikilia kitu kitu except mafuta ya mwarabu ambayo ni baadhi tu wameyashikilia indirectly...

Hata Bin Laden hakupiga New York kwa bahati mbaya, nenda New York utajuwa, ni ya Jews.Ndo wenye pesa pale na everywhere else...
 
jmushi1,

Kwenye suala la mafuta ni vita vya kidunia Mataifa matano wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi, hawa ndio wanaomiliki makampuni makubwa sana ya mafuta duniani.

Makampuni haya yanashikilia sasa soko la mafuta kutokana na mitaji yake mikubwa sana ya mafuta duniani, makampuni haya ni Petrochina, British Petroleum (BP), Royal Dutch Shell, Exxon, Texaco, Gulf, Mobil, makambuni ya Kirusi yaliyo chini ya Ikulu, Yukos, Sibneft, Lukoil, kuna Chevron, Total na mengine huunganisha mitaji ili kulikamata soko la mafuta duniani..

Mataifa ya kiarabu yanatumia mafuta yao kama silaha katika uchumi wa dunia.
 
Last edited by a moderator:
jmushi1,

Mataifa ya kiarabu yanatumia mafuta yao kama silaha katika uchumi wa dunia.
Somewhat true, but not all the way true, kwa mfano, mataifa mengi ya kiarabu yametumia mafuta kama silaha ya kuinfluence culture and so forth.

Na ndiyo maana huwa wanaliana timing haya mataifa ya kiarabu vs. West.Kila mmojawapo akitaka kuwa influential, siyo tu economically, but also culturally...

Hata silaha walizonazo mataifa ya kiarabu, huwa limited, haijalishi hata kama wana uwezo wa kuzinunuwa, hawaruhusiwi kuzinunua zote.

Kwahiyo unaweza kuona kuwa kama ingekuwa ni biashara peke yake, basi kusingekuwa na matatizo mengi kuhusiana na mafuta kama ilivyo sasa.
 
HALI YA MISRI BADO TETE

Rais Morsi alitangaza kurudishwa kwa bunge lililovunjwa na baraza la kijeshi.
Mtafaruku umeendelea baada ya mahakama kupinga agizo la Morsi na kwamba kuliita bunge ni kukaidi amri ya mhimili mwingine. Siku za nyuma tulisema Brotherhood walikaa kimya wakati wa uchaguzi bunge likivunjwa ili wa-focus katika hatua yao ya mwisho ya kuchukua utawala.

Taratibu tunaona kucha za Brotherhood zikichomoza. Ni ukweli usiopingika kuwa Brotherhood walishinda viti vya bunge na Urais. Ni ukweli kuwa baraza la kijeshi chini ya Tantawi halikupaswa kuvunja bunge halali lililochaguliwa na wananchi.

Tunajua kuwa hata uapishwaji wa Morsi ulifanyika mara mbili, moja ikiwa ni mbele ya jengo la mahakama linaloelekeana na Hospitali maarufu ya kijeshi. Hospitali hiyo ndipo alipotangazwa kufariki Anwar Sadat, ndiyo hospitali aliyofia Shah wa Iran na ndiyo anapotibiwa Hosni Mubarak.

Baraza la kijeshi lilitaka Morsi aelewe kuwa kuna mihili mingi ya kikatiba na mingine isiyo rasmi.
Msuguano wa Mhakama, serikali, bunge na baraza la kijeshi unaonekana kupamba moto.
Hili ndilo changamoto tulilosema siku za awali kuwa linamkabili Morsi.

Jambo la kushangaza ni kuwa nchi za magharibi hazijalikemea jeshi kwa kuingilia serikali iliyochaguliwa kihalali.
Huu ni ushahidi kuwa jeshi linaungwa mkono kama lilivyoungwa mkono wakati wa kumuondoa Mubarak.
Bado nchi za magharibi hazijaridhika na uchaguzi halali wa Misri. Wanawajua Brotherhood vema na hakika hawana usingizi

Siku za karibuni tutashuhudia makundi Tahariri Square kumuunga mkono Morsi, na mengine kuunga mkono Jeshi.
Jeshi halitaki kuachia 'utamu' kwasababu linapata msaada wa dola Bilioni 10 kutoka marekani kila mwaka. Hayo ni sehemu ya mkataba wa Camp David.

Uwezekano wa Morsi kupata 'ajali' ya kisiasa ni mkubwa sana hasa kwa jinsi jeshi lilivyochukia kuporwa madaraka.
Ukitaka kujua jinsi jeshi linavyoendesha mambo kichini chini ni pale Mubarak akiwa mfungwa kama wengine bado anatibiwa katika Hospitali ya jeshi. Muda wote wa mashataka alikuwa katika Hospitali ya kijeshi.

Hali ya Misri bado haijatengemaa na tutaendelea kujadili kadri itakavyojuzu

Tusemezane
 
Ni kweli hali bado tete nchini Misri, baada ya rais Mohamed Morsi kutoa agizo bunge kulejea kwenye vikao vyake, Baraza la Kijeshi linalotawala limesema kuwa ni sharti raia wote wa nchi hiyo waheshimu uamuzi wa mahakama ya katiba, kama unavyosema tutashuhudia makundi ya raia wa Misri kwa mara nyingine tena wakielekea kwenye viwanja vya Tahariri.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara, Nguruvi3, joka Kuu, Jasusi, Wakuu kwa nini Rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Nasser washirika wake wa karibu walikuwa ni Rais wa zamani wa Ghana Kwame Nkrumah na Rais wa Tanzania wa zamani Mwl Julius Nyerere 1966 Gamal Abdel Nasser alizuru Tanzania akatembelea Mwanza na Zanzibar.
 
Wakuu yanayoendelea Misri yananifanya kujiuliza iwapo kilichotokea North Africa yalikuwa mapinduzi ya wananchi au wanajeshi walimgeuka kiongozi wao na kumweka pembeni.

Yanayoendelea Misri wote tunaona, kule Tunisia; pamoja na kufanya uchaguzi kwa amani tunashuhudia wananchi wakirudi barabarani kuonyesha kutoridhika kwao na mambo yanavyokwenda. Kule Libya ndio kwanza wanajaribu kuchaguana huku central government ikiishia Tripoli na Benghazi na maeneo mengi ya nchi yakiwa chini ya vikundi tofauti. Hata ukiangalia Yemen, muafaka wa Raisi kumkabidhi mararaka Makamu wake umetuliza maandamano lakini haikuleta majibu yalifanya watu waingie barabarani.

Swali langu hapa ni iwapo hii dawa waliyoitumia wenzetu inatufaa huku kwetu kusini mwa Sahara? Baadhi ya majirani zetu watu walihamasika lakini wakakosa moyo wa kuvumilia mkono wa chuma wa serikali zilizopo. Je bado kuna wanaofikiri hata sie hapa kwetu tufuate njia hii? Kama sio, kuna njia mbadala kuleta mabadiliko? Nasema hivi kwa sababu tumefanya experiment ya multi-party demokracy kwa miaka 20 na hatuoni matunda yake.
 
Mkandara, Nguruvi3, joka Kuu, Jasusi, Wakuu kwa nini Rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Nasser washirika wake wa karibu walikuwa ni Rais wa zamani wa Ghana Kwame Nkrumah na Rais wa Tanzania wa zamani Mwl Julius Nyerere 1966 Gamal Abdel Nasser alizuru Tanzania akatembelea Mwanza na Zanzibar.
Walikuwa wakishare philosphy ya "Pan Africanism", walikuwa the strongest believers and the champions for the cause at that period and time.Hopefully imesaidia...Kama niko wrong, basi watanisahihisha waungwana uliowataja.
 
Nilikuwepo mwaka 1966 alipokuja Gamal Abdel Nasser kutembelea Tanzania. Nilijipanga mstari pale Forodhani na wanafunzi wenzangu karibu na Kilimanjaro Hotel. Nasser na Mwalimu walipita kwenye gari iliyokuwa wazi na nilimwona Nasser kwa karibu. Great times, great memories.
 
Walikuwa wakishare philosphy ya "Pan Africanism", walikuwa the strongest believers and the champions for the cause at that period and time.Hopefully imesaidia...Kama niko wrong, basi watanisahihisha waungwana uliowataja.
Ni kweli jmushi1, wenyewe siku hizi wanaita 'Umajumuhi' kama siajakosea (Pan Africanism).
Walikuwepo akina Huari Boumediane, William Tolbet aliyeuawa na Doe Kinyama sana tena akiwa mwenyekiti wa OAU.
 
Mkandara, Nguruvi3, joka Kuu, Jasusi, Wakuu kwa nini Rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Nasser washirika wake wa karibu walikuwa ni Rais wa zamani wa Ghana Kwame Nkrumah na Rais wa Tanzania wa zamani Mwl Julius Nyerere 1966 Gamal Abdel Nasser alizuru Tanzania akatembelea Mwanza na Zanzibar.
Kama alivyoeleza JMushi1, hawa jamaa kwanza kabla ya Uhuru wa nchi zetu walikuwa wakikutana na kuzungumza juu ya Uhuru wa nchi za Kiafrika na kuunda Umoja wa nchi hizo kama USA ilivyo..Na walifikia maamuzi haya kutokana na kwamba kuikomboa Afrika tu yaweza kuwa rahisi lakini ku sustain uhuru huo wakati Mali na Utajiri wote uko Afrika itakuwa ngazi ngumu sana hivyo kuungana kwa Afrika tu ndio kunaweza kuleta nguvu ya pamoja ktk kujitetea against mataifa Makubwa.

Lakini tukakutana namatatizo makubwa zaidi ya kuunda Umoja huo maana ikumbukwe tu ya kwamba hakuna nchi ambayo zimeungana pasipo vita na maguvu isipokuwa muungano wa Tanzania na Zanzibar. Union karibu zote duniani zimetangauliwa na vita na kutekana iwe Ethiopia, Somalia, Nigeria, USA, Russia au Uingereza na zote leo hii zinatafuta kutengana kama hazijatengana tayari.. NI Marekani na UK tu ndio wamebakia wagumu kutokana na sheria zao kali kwa yeyote anayehubiri au kwenda kinyume cha Union zao..

We failed na ndio maana leo hii Afrika tumerudi ktk kutawaliwa Kiuchumi. Na inasikitisha sana kuwasoma watu wengi wakidhania kwamba kuwa na uhuru wa mipaka ndio hasa maana ya Uhuru ama waasisi wetu walipigania. Vita ya uhuru wetu ilityokana na umiliki wa rasilimali na maliasili zetu (UCHUMI) nje ya hapo tungeendelea kutawaliwa hadi kiyama maana swala la uongozi bora na kulinda mipaka hakuna kama wazungu wakoloni isipokuwa tatizo lao ni kupora rasilimali zetu kuendeleza nchi zao ndio hasa sababu ya kuutafuta Uhuru lakini maajabu leo ni jambo la kawaida kabisa.. Viongozi wetu wakisema tena bila aibu kwamba hatuna mtaji hivyo sii sii vibaya kutawaliwa kiuchumi ikiwa wananchi watapewa ajira...
 
Mkandara,
Siyo sisi tulioshindwa. Viongozi wetu ndio waliotuangusha. Baada ya kina Nkrumah, Nyerere, Sekou Toure, viongozi wote waliofuata hawana vision jinsi ya kuendeleza harakati za kujikwamua kiuchumi. Leo unasika tuna viongozi wanaodhani kwamba Wamarekani na wazungu ndio watakaotusaidia kujikwamua kiuchumi huku wakisahau kwamba ni hao hao ndio waliotuweka kwenye ukoloni ili waendelee kutonyonya kiuchumi. Haiingii akilini kabisa. Siku moja nimemuuliza Mzee Nyerere, hivi mbona uongozi wa wakati wenu, (nikimweka Mandela katika kundi hilo hilo kwa sababu kiumri Mandela alikuwa kundi moja na akina Sekou Toure, Nyerere, na Nkrumah.) ulikuwa na vision nzuri tu kuhusu Afrika lakini mbona viongozi wa sasa ni kama wanaturudisha kwenye ukoloni? Mwalimu aliniangalia kwa dakika kadhaa, akasema ni kweli enzi zao ilikuwa rahisi kuwa na vision ya ukombozi kwa sababu kila mtu aliona jinsi Waafrika walivyonyanyasika chini ya utawala wa kikoloni, lakini ni jukumu la uongozi uliofuata kutambua kwamba manyanyaso hayo hayajamalizika kiuchumi na wao kuja na vision itakayowasaidia Waafrika kujikwamua kiuchumi. Leo, hiyo vision hatuna kabisa.
 
Mkuu Mkandara,
Naafiki kabisa hoja zako. Nikiwakumbuka akina Nkrumah, Dauda al Jawara,Wiliam Tolbert, Sekotoure,Nyerere, Kaunda n.k. nakumbuka wakati huo waliposimama pamoja kuikomboa Afrika. Hata pale Pan Africanism iliposhindwa bado walisimama kwenye kanda na vikundi vidogo wakitambua kuwa kizazi kitakachowapokea kitaweza kuja na mkakati mkubwa wa kuisadia Afrika kiuchumi baada ya ukombozi

Mkuu Jasusi, kushindwa kwa viongozi wetu kuna sababu za ndani na za nje. Bahati mbaya sababu za nje zinakuzwa zaidi na hata kufunika zile za ndani. Viongozi wetu wamenunuliwa kirahisi sana na mataifa makubwa.
Akina Nkrumah na wenzake walikataa hata kama ilikuwa kwa gharama, walisimamia walichokiamini ni sahihi.
Kikubwa zaidi ni sababu za ndani hasa kukosa uongozi wenye uadilifu na mtazamo.

Chukulia mfano tu wa nchi yetu. Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi masikini kama yetu imeshindwa kutumia fursa zake kujiendeleza. Hii ni kwasababu genge la viongozi limejikita katika kulimbikiza mali huku likilindana.
Hivi kiongozi kama wazIri wa nchi masikini kama yetu anawezaje kuwa na dola laki tisa bila kuhojiwa au kuulizwa!
Hivi Mkapa angesimama kwa hakimu mkazi kutueleza Kiwira ilikuwaje nani angethubutu tena kuiba.
Kwa bahati mbaya sivyo, aliyetangulia atalindwa na afutataye na inakuwa ni mzunguko.
Hakuna vision bali mission za kuibia taifa. Wananchi tumeonekana kuridhika pamoja na chuki na manung'uniko tuliyo nayo

Mkuu Kakalende, yaliyotokea katika ulimwengu wa waarabu yalitarajiwa.
Kwa bahati mbaya au nzuri ni mimba iliyozaliwa kabla ya wakati na kumchukua kila mmoja kwa kiwewe!
Nchi za Misri, Libya, Tunisia n.k. zilikuwa na wananchi wenye manung'uniko kwa muda mrefu sana.
CIA waliwahi kuionya nchi yao kuwa muda wa kutegemea marafiki sasa unafikia kikomo na Marekani ijiandae kwa njia mbadala.

Maandalizi yakiendelea ndipo Tunisia ilipoanza na kuambukizi eneo zima la mashariki ya kati hadi Saudi Arabia. Hili linadhihirisha manung'uniko ninayosema yapo. Kilichokuwa kinatafutwa ni sababu ambayo ilipatikana kwa bahati nzuri au mbaya haraka sana bila maandalizi.

Kukosa maandalizi ndiko kumepelekea nchi kama Libya kuunda serikali za haraka haraka na matokeo yake ni kutokuwa na 'institution' za kuongoza nchi bali wanaharakati tu. Tunaona hali ilivyo tete.

Misri na Tunisia wao walikuwa na 'institution' zisizokuwa rasmi kama Brotherhood na chama cha waislam cha Tunisia ambao walichukua nafasi ya ombwe la uongozi kuingia madarakani.
Lakini tatizo lipo pale pale kuwa hawakuwa na maandalizi na tunaona nchi hizo zinavyoyumba hadi sasa na kuna kipindi kirefu tu kijacho bado kutakuwa na mtafaruku.

Mazingira ya kwetu hayatofautiani sana na yale ya nchi za kaskazini kwa hiyo hatujawa na 'institutions' mbadala kama yakitokea yale ya jasmine revolution. Lakini haiondoi kweli kuwa 'beyond yield point' anything can happen.

Sasa swali ni je kwanini majirani walijaribu na wameshindwa! sidhani kama wameshindwa kwasababu katiba mpya ya kenya inayowafanya wawe katika speed kutuzidi ni matokeo yake. Na kule yapliposhindwa kulikuwa na sababu. Mfano, Sudan walijaribu wakiwa katika mtafaruku wa kuigawa nchi. Kwingineko tunaweza kusema ni sleeping giant na ipo siku kutapambazuka.

Je tuige ya jasmine revolution! Nakataa kuiga lakini tunaweza kuazima vitabu ili tufanye mambo kwa mazingira yetu.
Unajua, ukombozi wa kweli unaanza kwa mtu na si suala la mkusanyiko. Hadi wananchi watakapoelewa (na wameanza) kuelewa kuhusu tatizo lao hasa hapo ukombozi unawezekana.
Lakini Kakalende naona kama kuna jasmine in low profile! huenda ita-mature na kuwa jasmine kweli muda muafaka ukifika.
Tunaweza kusema siyo photocopy lakini final drawing inaweza kushabihiana na jasmine, ni muda ndio utatuambia ukweli
 
Makandara Mkuu wangu,

Tunashukuru sana kwa uchambuzi wako marua nimejifunza mengi sana kwenye ili pandiko lako, na pia Mkuu Nguruvi3, msichoke kutupa darsa.

JF Daima.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom