Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

Mkuu Nguruvi3 sikuwa na nafasi ya kufuatilia mdahalo wa wagombea uRais wa Marekani tafadhali tudadavulie yaliyojiri.
 
Last edited by a moderator:
MDAHALO WA UCHAGUZI MAREKANI

Mdahalo wa kwanza wa wagombea urais ulifanyika usiku jana. Mitt Romney akiingia huku akiwa na pressure kali kutokana na kuwa nyuma katika kura za maoni 'polls' katika majimbo yanayobadilika katika upigaji kura (swing states).

Sehemu kubwa ya madahalo ilitawali na mambo ya uchumi na afya.
Kufuatana na vyombo vingi vya habari, Mitt Romney alionekana kumzidi Barak Obama katika kujenga hoja.
Haina maana kuwa Obama alikuwa hana hoja, hapana! lakini mdahalo ni jinsi unavyokuwa na nguvu, ushaiwishi na hamasa katika jukwaa ikiwa ni pamoja na kuetetea hoja zako.

Tatizo la Obama ambaloni kuwa yeye ni mwelezaji wa hoja kwa undani sana.
Anatumia logic katika kujenga hoja zake wakati Romney alikuwa 'forceful' hata pale alipowakilisha hoja nyepesi au zisizo na mashiko.Kwa muktadha huo, Obama alionekana kama kupwaya.

Kwa wasomi na watu wanaoangalia mambo kwa undani, Obama alijenga hoja za msingi kabisa.
Aliweza kumbana mpinzani wake katika mambo ambayo amekuwa akibadilika badilika. Obama alimbana kwatika 'specific' za details za plan zake.Hata hivyo alikuwa defensive katika sera zake na hilo kumfanya ashindwe kumshambulia Romney kikamilifu.

Kwa uchaguzi wa Marekani mbako kuna wapiga kura washabiki kama Tanzania, mdahalo wa jana haukumsaidia Obama na ilionekana wazi kuwa mshindi alikuwa Romney.

Kitu kilichoonekana ni jinsi Romney alivyokuwa anabadili 'position' zake kuhusu mambo aliyoyakubali au kuyakataa siku za nyuma na hilo linaweza kuonekana kama jambo dogo lakini kwa wenye weledi linamjengea utata wa maamuzi.

Obama alionekana kupwaya kwasababu:
1. Matarajio ya watu yalikuwa ni kwa Obama kummaliza Mitt katika mdahalo. Hilo halikutokea

2. Kuwasiliana na average American hilo nalo halikutokea kwasababu si kila mmoja anaweza kuchambua data za kisayansi ili aweze kupata majibu. Ni sawa na hapa nyumbani ambapo akitokea mgombea mwenye vision na mission anaweza kuonekana hafai kwasababu tu kuna political opportunists wanaoweza kujenga hoja nyepesi kwa shangwe na shamra shamra hata kuonekana za maana. Kwahiyo suala si data bali kitu kinaitwa passions

3. Katika mdahalo huo Obama alikosa ili passion ya kuwahamasisha wafuasi wake kama afanyavyo katika kampeni.
Kwa ufupi Romney ameweza kuihamasisha ngome ya Republican iliyokuwa imeanza kukata tamaa.
Obama ameleta tashwishi na sintofahamu katika ngome yake.

Muhimu ilikuwa kundi la wapiga kura wasio na mrengo(independent voters). Kuna uwezekano mkubwa sana Romney amemega sehemu kubwa ya kundi hili jana na siku zijazo tutaona kura za maoni zikionyesha kuzibika kwa pengo kati yao.

Ikumbukwe kuwa wakati mdahalo ukiendelea kura zimeanza kupigwa katika baadhi ya majimbo.
Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema wale Republican waliokuwa wamekata tamaa wanaweza kurudi katika sanduku la kura.Kwa hakika mdahalo huu umemuumiza Obama kwa kiasi fulani na sasa pressure ipo upande wake katika mdahalo utakaofuata wa Urais.

Tarehe 11 kutakuwa na mdahalo wa wagombea wenza. Hapa pia Democrat wanawakati mgumu. Joe Biden anajulikana kwa kusema hovyo 'gaffe' na mpinzani wake Ryan ni mtu organized na mwenye uwezo wa kujenga hoja.
Hapa Democrat watakuwa katika wakati mgumu pia.

Mdahalo umebadili sura ya uchaguzi in favor of Republican. Ni jinsi gani wapiga kura wamepokea hoja za wagombea hao, tutaendelea kuwaletea.
 
WINGU NENE LATANDA UCHAGUZI WA MAREKANI

Baada ya mdahalo kumalizika na kushuhudia Mitt Romney akiibuka kidedea kamapeni zimeendelea tena.
Uchunguzi wa vyombo vingi vya habari umeonyesha kuwa Mitt Romney alitumia takwimu na hoja ambazo zinakinzana na misimamo yake ya awali. Ni dhahiri alishinda mdahalo kwa nguvu hoja za nguvu na si nguvu za hoja.

Pamoja na hayo mwelekeo wa uchaguzi umeonekana kubadilika kiasi fulani ukiwa unaegemea upande wa Republican.
Mitt ameweza kuhamasisha ngome ya Republican na kuweza kukusanya pesa zaidi za uchaguzi. Kwa wiki moja tu ametumia nafasi hiyo kutoa matangazo yenye thamani ya dollar milioni 12. Huu ni mkakati wa kimbunga cha mdahalo ambao umeiumiza ngome ya Obama kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande mwingine mwangi wa ushindi wa Romney umedumu kwa muda mfupi kutokana na matukio kadhaa.
Kwanza Obama ameweza kukusanya pesa nyingi kuliko kipindi chochote cha makusanyo ya kampeni yake.
Hili litamwezesha kuingia katika mashambulizi ya matangazo 'ad'.
Hata hivyo kuna wingu nene kuhusiana na waliomchangia ingawa hoja haijaingia rasmi katika vyombo vya habari na kushikiwa bango.

Habari njema kwa Obama ni kuhusu takwimu za ajira na kiwango cha ajira.
Mwezi uliopita ajira zipatazo 114,000 zilitengenezwa na kiwango cha ukosefu wa ajira kilifikia 7.8 % ambacho ni cha chini tangu amekuwa Rais. Kiwango hicho kimeshuka kutoka 8.3%.

Historia inaonyesha kuwa ni nadra sana rais wa marekani kuchaguliwa muhula wa pili kiwango kikiwa juu ya 8.1
Wapiga debe wa Republican wanasema huenda kiwango hicho kimeingiliwa na wanasiasa.
Ukweli ni kuwa bureau of statistic ni taasisi inayojitegemea, rais na makamu wake hupewa taarifa masaa 12 kabla ya kutangazwa. Lakini pia hakukuwa na sababu za msingi za kuingilia uchaguzi huo kwasababu takwimu za mwezi mmoja haziwezi kubadili ukweli wa takwimu zizlizopita zinazoonyesha kiwango kuwa juu ya 8.2.

Habari hizi zimebadili na kupunguza nguvu ya msisimko wa Romney.
Alhamisi ni mdahalo wa wagombea wenza na hakika Joe Biden wa Obama ana wakati mgumu kwa Paul Ryan wa Romney.
Kuna uwezekano Joe Biden akavuruga hali kabisa kutokana na kusema hovyo.

Kwa muktadha huo hali bado ni tete na ngumu sana kwa Rais Obama. Hadi pale atakapobadilika upepo unaonekana kuvuma kuelekea upande wa pili.

NYUMBANI:TANZANIA
Katika matukio ya kisiasa ni pamoja na lile la mh Zitto kujitangaza kugombea nafasi ya urais.
Suala hili linazidi kuleta sintofahamu miongoni mwa wadau wa siasa. Inaonekana kuwa Zitto anafanya siasa za jeshi la mtu mmoja.

Katika harakati hizo inahofiwa kuwa huenda akaleta mzozo usiotarajiwa ndani ya chama.
Mzozo utatokana na kujengeka kwa makundi ndani ya chama na kudhoofisha juhudi za chama kujiimarisha.

Kwa taarifa za karibuni kuna kundi la vijana ndani ya BAVICHA linaloshadidia juhudi za Zitto, na hili limekuwa likitumika katika kuleta mtafaruku na kundi jingine.
Kuna mtifuano unaoendelea chini kwa chini ambao hauonekani kuleta maridhiano ndani ya chama.

Wapo watetezi wa Zitto wanaosema anachokifanya ni kubadili siasa za Tanzania kutoka katika mazoea kuelekea katika siasa za kisasa. Hofu inayotokana na nadharia hii ni kuwa ujenzi wa siasa hizo mpya unaonekana kulenga katika kutafuta madaraka na si kuungwa mkono na wananchi.

Tatizo linalokikabili chama cha Chadema ni lile linalovikabili vyama vingine. Kwamba, nidhamu ndani ya chama haizingatii sheria au kanuni bali wajihi na wasifu wa mtu. Tumeshuhudia mara kadhaa watovu wa nidhamu wakitetewa kwa hoja nyepesi wakati ambapo kuna wanasiasa ndani ya chama wanaadhibiwa kikamilifu.
Taratibu huu wa double standard unakikwaza chama kwasababu huwezi ukawa na chama kilichojengwa kwa personalities na sio kanuni au sheria.

Hakuna tatizo kw mtu kutangaza ndoto zake kama afanyavyo Zitto. Tatizo ni je,amefanya hivyo kwa nia njema? Je, kufanya hivyo kunakisadia chama? na je. amezangitia masilahi ya chama kabla ya kuzingatia yake binafsi?

Kwa vyovyote iwavyo safu ya duru matukio inapenda kukumbusha historia za CUF na NCCR, ikiwa ni pamoja na CCM inayokaribia kufumuka. Migogoro katika vyama hivyo haikuanza siku moja ni zao la kuleana kwa muda mrefu.
Ni lazima CDM ijiendeshe kama taasisi yenye kuzingatia demokrasia, kanuni na sheria na ijengwe na wanachama siyo personality.

Hali isipodhibitiwa mapema duru matukio inatabairi machafuko makubwa ndani ya chama kati ya June 2013 na Jan 2014.
 
MDAHALO WA UCHAGUZI MAREKANI NA TAARIFA ZA MAUAJI YA MWANGOSI

Mdahalo wa uchaguzi umemalizika kati ya Joe Biden na Paul Ryan.
Mdahalo ulihusu mambo ya ndani ya marekani na siasa za nje.
Kwa hakika Joe Biden ameweza kuwatoa kimaso maso Democrat kwa kutoa tuition kwa kijana Ryan.
Ameonyesha weledi wa hali ya juu sana katika siasa za nje na za ndani na mara zote ameongozwa na facts zaidi ya siasa.

Kinyume na matarijio ya wengi kulikuwa hakuna kuropoka kutoka kwa Joe Biden kwasababu hiyo ni hulka yake.
Kilichojitokeza ni yeye kuingilia kati wakati mwenzake anajenga hoja.

Hilo lilifanyika makusudi ili kumzuia Rayan asiweze kuweka hoja za kupotosha kama alivyofanya Mitt Romney kwa Obama.
Inonekana kuwa Biden alikuwa na maandalizi mazuri kuliko mwenzake.

Pamoja na hayo historia inaonyesha kuwa mdahalo wa makamu wa rais haubadilishi sura ya uchaguzi.
Mdahalo unaofuata ni Obama na Romney tena, na hapa ndipo wanaposema make or break.

Obama anatakiwa aje akiwa amejiandaa pamoja na facts. Aongee kwa mamlaka kama mtu anayeijua ofisi ya rais na majukumu yake. Mdahalo uliopita umemuumiza sana katika kura za maoni na ana kazi kubwa kujibu mapigo.
Uchaguzi ni wa karibu sana na hakika uwezekano wa Obama kurudi white house sasa upo njia panda.

TANZANIA
Wakati hayo yakiendelea wiki hii nchi yetu imekumbwa na simanzi tena. Simanzi iliyosababishwa na taarifa mbili za matokeo ya uchunguzi wa kifo cha mwangosi.

Taarifa ya kwanza ni ile iliyoandaliwa na baraza la habari Tanzania(MCT) pamoja na jukwaa la wahariri(TEF)
Taarifa hiyo ilijaa mtirirko wa tukio zima kama tunavyofahamu kwa mpangilio mzuri.
Imeonyesha kina cha uchunguzi na kuleta picha halisi ya tukio hata kama tulilijua.

Tatizo la taarifa ile lipo katika majumuisho(Conclusion). Majumuisho hayakuwa na kitu kizito kama ailivyotarajiwa.
Tulitaraji kusikia chanzo cha tatizo zaidi ya mauaji, nani wamehusika kwa uzembe huo, nani wawajibike na kwanini, na mwisho nini hatima ya taaluma ya habari.

Taarifa iliyoandaliwa na kamati ya Nchimbi.
Kuanzia mwanzo kamati hii iliitwa tume hadi pale wanasheria walipohoji mamlaka ya tume hiyo kisheria kuundwa na waziri ambaye hapaswi kufanya hivyo. Ghafla ikibadili jina na kuitwa kamati.
Hili tu linaonyesha kuwa Nchimbi alikuwa anafanya asichokijua.

Nchimbi aliunda kamati baada ya shinikizo la yeye kujiuzulu. Shinikizo hilo lilikuwa na hoja kuwa yeye akiwa waziri mwenye dhamana anapaswa kuchunguzwa na hivyo hawezi kuunda chombo kitakachotoa taarifa kwake akiwa mtuhumiwa.

Ukweli ni kuwa nia ya waziri Nchimbi ilikuwa kuunda kamati ili kuwapumbaza Watanzania.
Hilo amefanikiwa kwasababu mijadala inayomtaka ajiuzulu imekufa.
Ikumbukwe kuwa kamati hii ni kama kamati ya harusi kwasababu haina nguvu ya kisheria.
Mapendekezo yake yanaweza kuwekwa kabatini na Nchimbi na ukweli hivyo ndivyo atafanya bila kubanwa na sheria yoyote.

Kamati hiyo iliongozwa na jaji mstaafu Ihema. Ni jaji aliyewahi kutuhumiwa na mbunge Tundu Lisu kwa kiwango chake cha weledi. Makamu mwenyekiti alikuwa mhariri Theophil Makunga akiwakilisha jumuiya ya waandishi wa habari.

Taarifa ya kamati hiyo ni ya kiwango cha chini sana na cha kipuuzi kisichoeleweka kwa urahisi.
Ni taarifa ambayo ingeweza kuandikwa na kijana mwerevu wa kidato cha sita.
Taarifa imejaa habari za watu wa mitaani na kutuhumu vyama vya upinzani na hapa CDM.

Inasema kuwa hakuna nguvu yoyote kubwa iliyotumika kule Iringa. Huu ni ujinga wa kiwango cha kutisha kuandikwa na watu wenye taaluma zao kama majaji na Waandishi. Haiwezekani mtu auwawe kinyama chini ya askari sita halafu ionekane nguvu ya kawaida.

Ujinga mwingine wa kutisha ulioandikwa na Jaji Ihem na Theophil makunga ni ule wa kusema waandishi wapewe mafunzo katika maeneo ya hatari. Hapa walimaanisha kifo cha mwangosi kilitokana na ujuha wa taaluma na si uonevu.

Kwa kifupi ni kuwa taarifa iliyoandikwa na Jaji na Mhariri inatia aibu taifa na taaluma zao.
Kama kuna kituko cha mwaka basi hiki ni kimojawapo.

Tunafahamu kuwa Jaji Ihema ni mstaafu kwahiyo kazi yake ni kutafuta kitu cha kufanya hata kama ni kulamba miguu ya viongozi. Kibaya sana ni mwandishi wa habari Theophil Makunga ambaye tulimuonya kushiriki kamati hizi za kipuuzi.

Kwa njaa na bila kuongozwa na taaluma Makunga amaeamua kufuata vi-allowance na kuisaliti taaluma yake.
Haiwezekani mwandishi asijue kipi cha kushiriki na kipi ni haramu.
Haiwezekani mwandishi ashiriki kuandika utumbo ule unaotia kinyaa kiasi kile.

Makunga ameidhalilisha sana taaluma ya habari. Ili taaluma hiyo ijisafishe na uchafu huu wa Makunga inabidi kumtenga Theophil katika taaluma, kumkemea kwa upuuzi na kumdharau. Makunga asishirikishwe katika shughuli za uandishi katika vyama vya kiandishi. Huyu ni mpuuzi na mjinga wa kiwango cha kusikitisha.

Kwa Jaji Ihema, wale wote waliopitia hukumu zake na wako vifungoni ni vema wakajiuliza kama walihukumiwa na mtu sahihi. Taaluma ya sheria nayo ipo katika majaribu kwasababu kama Jaji anaweza kuandika utumbo ule basi kuna tatizo kubwa sana.

Wakati tunaomboleza kifo cha Mwangosi, lazima Watanzani tujiulize, hivi ujinga huu wa akina Nchimbi, Ihema na Makunga utaisha lini? Ni lazima tuwaambie ukweli bila hivyo wataendelea kutudharau.

Ni lazima wapate ujumbe kuwa sasa tumechoka na hapa ndipo nasema tunapaswa kusimama na kusema bila haya, soni au kificho kuwa waziri Nchimbi ipo siku utakuja jibu haya. Jaji Ihema njaa inadhalilisha taaluma ya sheria, Makunga wewe ni msaliti mkubwa unayeongozwa na njaa wala siweledi.

Tusemezane.
 
MATUKIO YA WIKI NCHINI.
Matukio makubwa ya kutisha yaliyotokea nchini wiki hii ni pamoja na Mauaji ya kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Vurugu za Mbagala na Uchaguzi wa CCM.

Tuangalie uchaguzi wa CCM.
Niwakumbushe wasomaji kuhusu haya tuliyoyaandika katika mabandiko yetu hapa duru za matukio siku za nyuma:
Makongoro Nyerere ambaye ni maarufu kwa 'kule site' wanasema mafisadi..... naye ni victim. Tofauti na wenzake yeye ana ngao ya jina kubwa na huenda kumwacha nje ya sytem kunaweza kuzua makubwa. Wamiliki wa CC na NEC kwasasa hapendi arudi katika uongozi, wakati huo huo wapo wanaotaka jina hilo libaki kama heshima kwa Nyerere. Ni kazi nzito kumuengua kwa mizengwe lakini tayari jitihada zinaendelea ili aenguliwe mapema huko Musoma kabla hajafika NEC au CC kukwepa lawama
Matokeo ya uchaguzi mkoa wa Mara kwa mujibu wa taarifa,Makongoro Nyerere ameangushwa katika uenyekiti wa mkoa. Kama taarifa hizo ni kama tulivyozipokea basi tuliyosema sasa yanatimia. Kuondolewa kwa Makongoro hakutokani na kundi la Mtandao bali ni kundi ndani ya chama linaloongozwa na wakubwa wa chama wa kutaka aondoke kwasababu ya misimamo yake ndani ya NEC.
Njia ya 'kisayansi' ni kuhakikisha anamalizwa huko huko ili kuosha mikono mapema.

Mkoa wa Dar es Salaam umeshuhudia mabaliko ambako Ramadhani Madabida amemuengua Joh John Guninita.
Madabida amekuwa mwanachama wa NEC kwa muda mrefu.
Madabida anaungwa mkono na kundi linalojulikana kama wazawa wa Dar es Salaam likiwashirikisha akina Idd Simba,Sophia Simba, Sykes n.k.Ni dhahiri kuwa ipo nguvu ya ziada nyuma yake.

Ikumbukwe, Guninita alichukua wadhifa huo kutoka kwa mzee Hemed Mkali ambaye pia alikuwa mwanachama wa kundi la wazawa. Kuingia kwa Guninita kulikuwa na Chapuo la juu ambalo safari hii halikufanya kazi.
Hii pia inaonyesha ni jinsi gani siasa za chama zinavyobadilika kutoka katika sera na kuegemea makundi.

Adam Kimbisa aliyewahi kuwa Meya wa jiji naye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Dodoma.
Matokeo yanayoendelea yanaonyesha wazi kuwa ndani ya NEC kuna upungufu w kundi la mtandao ukilinganisha na siku za nyuma. Katika makundi ya kuelekea 2015 kundi la Sitta linaonekana kupata nguvu huku kundi la Lowasa likiwa na majeraha mkubwa.

Hata hivyo kwa uzooefu wa siasa za mitandano, kundi la Lowasa haliwezi kuondolewa katika mbio kwasababu lina uwezo mkubwa wa kucheza karata za kisiasa. Sasa hivi kuna jitihada za makusudi zinaendelea ili kurikruti wanachama wapya wa NEC kwa kutumia gharama kubwa.

Vurugu za Mbagala:
Tukio hilo limesababishwa na watoto wawili wenye umri wa miaka 12 na 14. Ni tukio la kukojolea kitabu kitakatifu cha Kurani. Inasemwa kuwa baada ya tukio hilo wazazi wa pande mbili waliyamaliza kama wazazi, lakini pia hatua zikachukuliwa kwenda katika vyombo vya sheria.

Kilichotokea ni Ijumaa iliyopita waamuni kuvamia kituo cha polisi ili kumtoa mtoto huyo na kumwadhibu huenda kukatisha maisha yake. Baada ya jaribio hilo kushindwa ndipo waumini wakavamia makanisa na kuanza kufanya uhalifu.

Duru za matukio zina amini kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuishi kwa kuhesimu kile mwingine anachokikubali au kukikataa.
Imani ni jambo nyeti sana katika jamii hasa jamii zetu ambazo ufahamu wa mambo ni tatizo.
Ni vema wazazi wakaanza kuwalea watoto kutambua umuhimu wa kuishi kwa utangamano katika jamii moja.

Duru matukio inaamini kuwa umri wa miaka 12 na 14 ni mdogo kuweza kuchambua madhara ya jambo fulani.
Nakumbuka nikiwa katika umri wa miaka hiyo niliwahi kufanya michezo ya kuchezea mahindi yaliyokuwa katika stoo. Furaha yangu ilikuwa kuwasha kiberiti ili 'nywele; za mhindi ziungue na hapo nilijisikia raha.
Matokeo ya hili yalikuwa kuchoma ghala zima na kusababisha hasara kubwa.

Umri wa miaka hiyo ni umri wa majaribio ya kila jambo ikiwa ni pamoja na kuchungulia watu wakioga, kufuatilia sauti zisizo za kawaida vyumbani, kukimbilia katika matukio kama ya watu kuuawa n.k.

Ni umri unaosikia na kuona lakini hauna uwezo wa kupambanua zuri na baya.
Ni kwa ukweli huo sheria nyingi kama upigaji kura, kujamiiana n.k. zinalitenga kundi hili.
Inafanyika hivyo kwa kuelewa kuwa ni umri unaojua aina ya vyama, bendera za vyama na wapi sanduku la kura lilipo, lakini haujui ni kwanini wamachague kiongozi A na siyo B.

Hatukabali kwa namna yoyote tabia mbaya na wala si vema kutoa excuse kwa tabia chafu kwa kisingizo chochote tukielewa kuwa hayo yaweza kuwa matatizo ya ulezi, jamii n.k.
Kinachosikitisha ni pale watu wazima wanapokuwa na uelewa mdogo katika kupambanua mambo na hoja.

Sidhani kuwa mtoto alyefanya hivyo alitumwa na kundi lolote la jamii. Siamani hivyo!
Na kama nitaamini hivyo basi itanibidi niami kuwa kibaka aliyeiba nyumbani kwangu naye alitumwa na wazazi au familia. Itabidi niende mbali ili kufahamu jina la kibaka huyo na kama ni Mohamed basi atakuwa ametumwa na Waislam, kama ni Chiristian basi atakuwa ametumwa na Wakristo.
Nitakwama endapo jina la kibaka wangu ni Gugutioh Mwanoga maana halina kiashiria cha dini.

Ni ujinga wa hali ya juu kuchukua jina na kulifanya dini. Hili ndilo tatizo tulilorithishwa Waafrika.
Tunadhani kuwa jina peke yake linamfanya mtu kuwa mcha mungu.Vitabu vitakatifu havisemi ukiitwa John Samson Jacob basi automatic wewe ni mtu wa ufalme wa mungu.
Wala havisemi kuwa ukiitwa Abdul Mohamed Hussein wewe ni mtu wa peponi.

Sijui ni kigezo gani kilitumika kutambua kuwa kijana aliyetenda kosa hilo ni muumini wa dini fulani. Sijui ni kigezo gani kilitumika kujua kuwa ametumwa kufanya uhalifu huo na dini yake. Na sijui ni kigezo gani kilitumika kujua kuwa yeye au wazazi wake ni wafuasi wa dini fulani.

Matokeo ya kutokuwa na majibu ya maswali hayo achilia mbali kujiuliza ndiyo yamepelekea watu kuvamia na kuchoma makanisa moto. Hakika hiki ni kitendo cha uovu kilichokosa busara kabisa.

Hata kwa kutumia busara za kawaida tu hili lisingefika lilipofikia. Ni suala ambalo lingezungumzwa na kufikia tamati bila kuwa na mikwaruzo au vurugu. Hakukuwa na busara ya aina yoyote katika kuvamia sehemu nyingine na kuleta uharibifu.

Kinachoonekana hapa ni uwepo wa matatizo mengine yanayosubiri sababu, lakini tatizo lililokuwepo halikuwa katika kiwango kilichotokea. Lazima tukiri kuwa kuna watu wameachwa katika jamii yetu kujenga chuki baina ya watu na watu, dini na dini na pengien kabila na kabila.

Tumelikemea sana hapa JF pale mijadala iliyolenga kuleta vuru ilipoletwa. Nakumbuka Mohamed Said ambaye ni kinara wa chuki hizi za jamii aliposema, 'tuangalie tusijejikuta AU, EU wanakuja kutusuluhisha'.
Hoja ya namna hiyo ililenga kuleta chuki na nadhani ni wakati Mohamed Said ajitokeze na kueleza furaha yake kwa kupandikiza chuki hizi.

Kinachosikitisha sana ni kuona watu wenye nia mbaya ya kulichonganisha taifa na jamii wamepewa fursa ya kufanya hivyo hadi tumefikia hapa. Hapa tulipo ni mahali pa baya kwasababu inapotokea mtu anaamua kwenda kuchoma moto nyumba za dini nyingine bila kujua kwanini anafanya hivyo inatisha.

Duru matukio inalaani dhihaka za imani na pia inalaani matumizi ya nguvu yasiyozingatia weledi au busara.
Two wrongs never make one right.

Iko wapi Tanzania niliyoishi nikiwa na marafiki wengi wa imani tofauti na yangu, marafiki wengi wa makabila yasiyokaribiana na langu?

Ukweli usemwe, kuogopa kusema ni kulea tatizo.

Tusemezane
 
MDAHALO MAREKANI
Leo ilikuwa siku ya pili ya mdahalo uliomalizika hivi punde.
Kuna hali mbili zilizokuwa zinatarajiwa
1. Obama kurudi kama nyati aliyejeruhiwa
2. Romney kubalisha mwelekeo wa Uchaguzi kabisa.

Hadi sasa kura za maoni nchini Marekani zinampa Obama kiwango kikubwa kuliko mpinzani wake(hata hivyo ukiangalia takwimu wao wanasema ni close call au tie) katika kuwania viti 270.

Obama amerudi akiwa amejiandaa na kwa hali yoyote mdahalo wa leo amekuwa bora zaidi kuliko wa mwanzo na kwa mtazamo wangu upepo ulikuwa upande wake.

Mitt Romney alitumia udhaifu wa uchumi kutaka kumbana Obama ambaye alikuwa mwerevu kujibu mapigo.
Romney alitumia shambulizi la Benghazi kutaka kuonyesha udhaifu wa Obama katika mambo ya usalama.
Hoja hii imekuwepo katika vyombo vya habari kwa wiki sasa kama sehemu ya kampeni.
Obama ali ichukua hoja kama president kitu kilichomfanya Romney anywee hasa pale alipoongea kama Rais.

Suala la shambulizi la Libya lilionekana kama mwiba, kwa bahati nzuri au mbaya Romney hakuweza kulichukua kama ilivyotarajiwa na Obama akachukua udhaifu huo ku-score political point.

Kwa upande wa mambo ya jamii, Romney alionekana kupwaya sana hasa katika haki za akina mama.
Obama alitumia udhaifu wa rekodi ya Romney ambayo inabadilika badilika ili kuwaonyesha Wamerakani undumila kuwili.

Nafasi ya swali la mwisho Mitt Romney aliumizwa pale Obama alipokuwa na fursa ya mwisho ambayo alioongelea 47% aliyowahi kuisema Romney kuwa haipo responsible. Kwa vile lilikuwa swali la mwisho Romney Hakuweza kujibu kwahiyo linabaki kumuumiza.

Kosa jingine kwa Mitt ni pale aliposema akina mama (single moms) nao wanachangia kuzagaa silaha kwa kutokuwa na akina baba. Japo hakumaanisha jambo baya lakini katika uchaguzi mpinzani anaweza kuchukua maneno na kujenga chuki na wapiga kura. Tayari tunasikia kuwa watu wakisema Romney amewatukana ma-single mom kama watu wanaochangia kuzagaa silaha kwa kutokuwa na waume.

Kwa upande mwingine, Romney aliishambulia rekodi ya Obama katika mambo ya uchumi.
Kwa ufupi Romney alikuwa defensive na Obama offensive.
Ile performance ya Romney ya mdahalo wa awali ilikosekana na kama wanavyosema Obama came back swinging.

Historia inaonyesha kuwa hakuna mgombea wa Republic aliyewahi kuwa Rais bila kushinda Ohio. Huko ndiko Romney alipooelekeza pesa za matangazo wakati huo huo Obama akimbana pia ili asiweze kupata wasaa wa kwenda sehemu nyingine.

Historia pia inaonyesha kuwa ni mara mbili tu katika uchaguzi wa marekani Marais wawili wamekuwa na vipindi viwili.
Nina maana Bush alikuwa na vipindi viwili akimfuatia Bill Clinton. Historia haimpi nafasi Obama kwasababu atakuwa Rais wa tatu katika vipindi viwili viwili jambo lisilo la kawaida.

Hata hivyo Historia hugeuga kwasababu hakuna kiongozi aliyewahi kushindwa zhaguzi za awali katika jimbo la Ohio na kuwa Rais. Obama alishindwa na Hillary na kuwa Rais.

Hii ni katika hints tu, chochote kinawezekana kutokea

Tutaendelea kudadavua kadri tunavosonga mbele.
 
Asante sana nguruvi kwa analysis yako...Kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwenye midahalo hii, hususan jinsi wagombea wanavyochambua sera na mikakati yao na jinsi watakavyoperform wakipewa madaraka. Baada ya kufunikwa katika debate ya kwanza Obama alijipanga upya na ndio maana ameweza kumdhibiti mpinzani wake vilivyo. Tunasubiri kwa hamu mdahalo wa mwisho next week...
 
Last edited by a moderator:
Kwenye mdahalo huo walikusoana mara kwa mara huku Obama, akimtuhumu Romney, kwa kusema uongo Romney, alikuwa anatafuta point kwenye suala la tukio la mauaji ya balozi wa Marekani nchini Libya, na kusema limefedhehesha sana sera za Obama, Mashariki ya Kati. Naye Obama, alilisisitiza kuwa atafanya kila awezalo kuwakamata wauaji...ngoja tusubiri mdahalo wa mwisho jumatatu kwa njia ya TV.
 
UCHAGUZI MAREKANI NA UCHAGUZI CCM
Turejelee kwa haraka habari za uchaguzi wa ndani ya CCM. Matokeo ya UWT yanampa Sophia Simba nafasi ya uenyekiti kuelekea uchaguzi wa 2015. Kama tulivyowahi kusema huko nyuma, tawi la akina mama ni muhimu sana katika kuwaleta wananwake ambao ni wapiga kura pamoja.

Sophia Simba ni mmoja wa wale wanaojiita Wazawa wa Dar es Salaama, kundi la akina Kitwana Kondo, Sykes, Madabida kwa uchache wa kuwataja. Katika siasa Sophia ni mshiriki mkubwa wa kundi la Mtandao linaloongozwa na Waziri mkuu aliyejiuzulu EL. Duru zetu zinatuonyesha kuwa pesa ilitumika vilivyo katika kumrudisha madarakani.

Kwa hili tunaweza kusema Sophia ana kofia mbili, moja ya uzawa na nyingine ya mtandao.
Kurudi kwake ni jitihada za mtandao na haijulikani ataegemea wapi, lakini ni dhahiri kuwa baada ya kundi la EL kupata majeraha mikoani sasa limefarjikika ingawa Sophia ni mtu wa kubadilika na anaweza kuwatosa na kujiunga na wazawa wanaompigia chapuo mgombea mtarajiwa mzee.

Kuanguka kwa Makongoro Nyerere ni afueni nyingine kwa wana mtandao. Makongoro alikuwa mwiba mkali kwao.
Lakini pia ni ahueni kwa serikali iliyokuwa inakasirishwa na mijadala yake ya kusimamia kwa dhati itikadi za chama.
Kuanguka kwa Guninita hakuna madhara ya wazi zaidi ya yale ya kurudisha uzawa katika uongozi wa jiji.

Tukiangalia UVCCM, kule kunaonekana kuwa na matatizo makubwa sana. Uwepo wa watoto wa vigogo ambao wengi ni sehemu ya kambi zinazohasimiana unaleta mpasuko mkubwa sana ndani ya chama.
Kisiasa, uwepo wa watoto wa vigogo unazidi kukiuumiza chama cha mapinduzi kwasababu sasa ni dhahiri kuwa uongozi umebaki kurithishana na si sifa za mtu. Hili linaondoa matumaini kwa vijana wenye uwezo na nia ya kukitumikia chama.

Zaidi ya hayo, ile dhana ya wananchi kuwa CCM ni kundi teule na si chama cha wafanyakazi na wakulima sasa inashika kasi na hakika kuna chuki inayojijenga dhidi ya chama kwasababu tu ya sura ya uongozi.

Kwa kiasi tulichoweza kupata matokeo ya chama, ni wazi kuwa uchaguzi ndani ya CCM umezidi kukibomoa chama zaidi ya kukijenga. CCM wana karata moja muhimu sana wanayoitegemea. Karata ya safu ya juu ya uongozi kitaifa, na sekretariati za chama. Endapo kutakuwa na mabadiliko huenda wakaweza kuzuia uharibu unaoendelea. Kinyume chake hiyo ndiyo itakuwa safari kuelekea katika kambi ya upinzani.

Katika safu ya kitaifa hatutarajii mabadiliko makubwa. Mwenyekiti JK atabaki kuwa mwenyekiti, na Makamu Zanzibar atakuwa Dr Sheni. Swali linalobaki ni je, Pius Msekwa atabaki kuwa makamu Bara? Je,Kinana anaweza kurudi katika nafasi ya uongozi kama Makamu mwenyekiti?

Eneo lingine linaloweza kuwa na mabadiliko makubwa ni nafasi ya katibu mkuu. Nafasi hii imepwaya baada ya Wilson Mukama kukaa pembeni na kumwachia Nape achukue nafasi za kazi za katibu mkuu. Inavyoelekea kuna mgongano mkubwa sana kati ya hawa wawili. Ni matarajio ya wanachama kuwa kutakuwepo na katibu mkuu mpya na safu nyingine kama ya katibu uenezi n.k.

Tatizo litakuwa ni kupatikana kwa wajumbe wa sekretariati . Itategemea kundi gani litakuwa na 'upper hand'' katika idadi ya wanachama wa NEC. Hilo litaamua sekretariati iweje na kutoa kiashiria nani atabeba bendera.

Hebu tugeukie siasa za Marekani, inaendelea.......
 
UCHAGUZI USA
Mdahalo wa tatu na wa mwisho unategemewa kufanyika jumatatu usiku saa za Marekani.
Huu unafuatia ule wa pili ambapo Obama alionekana kuwa mshindi kwa kiasi kidogo.
Hata hivyo kwa kura za maoni zinaponyumbuliwa kisayansi kwa kuangalia issues na makundi bado Romney ameonekana kumzidi Obama.

Kwa mfano watu walipoulizwa kuhusu uchumi wengi walionyesha kuwa na imani na Romney zaidi ya Obama, vivyo hivyo katika mambo mengine. Hata hivyo kura za maoni zinategemea sana idadi ya washiriki wanaegemea mrengo gani.

Mdahalo wa pili hauonekani kumpa Obama adavantage zaidi ya kuzuia momentum aliyokuwa nayo Romney.
Mdahalo wa pili haukurudisha watu waliohamia kwa Romney lakini umezuia kundi lingine kuhamia huko(stop bleeding).
Kikubwa zaidi ni kuwa Obama aliweza kuamsha hamasa kwa Democrat walionyong'onyea sana kutokana na mdahalo wa mwanzo.

Ikumbukwe kuw wakati midahalo hii ikiendelea upigaji kura katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi unaendelea.
kwa namna moja au nyingine hili litakuwa limemuumiza sana Obama hasa kutokana na performance ya mdahalo wa mwanzo iliyokuwa hafifu sana.

Katika kura za maoni zilizotolewa na taasisi ya Gallup inaonyesha kuwa kitaifa Romney sasa anaongoza.
Ingawa si kigezo cha mwisho, mara nyingi kura za maoni hufanywa kisayansi na matokeo yake ni nadra kupishana na ukweli.

Kura za maoni za kituo cha CNN zinaonyesha kuwa Romney anamzidi Obama kwa asilimia 1 katika jimbo la Florida.
Miezi miwili iliyopita Obama alikuwa anaongoza kwa asilimia 4. Kwa maneno mengine advantage aliyokuwa nayo sasa haipo.

Kura nyingine zinaonyesha kuwa katika jimbo la Ohio, wanawake sasa ni 50/50.
Kwa kawaida wanawake wamekuwa wanapigia kura Democrat na Obama alikuwa anaongoza kwa 68 kwa 32, sasa ni 50/50

Ohio na Florida ni majimbo yenye wajumbe wengi wanotoa matokeo ya viti 270 vinavyoweza kumpa mgombea Urais.
Kwa Romney ni lazima ashinde Ohio na Florida ili kumbana Obama na jitihada zinaonyesha kuwa hilo linawezekana.

Ni kwa mtazamo huo mdahalo wa kesho kule Florida ni Muhimu sana. Mdahalo huu utakuwa ni kuhusu mambo ya nje.
Kwa asili ya midahalo hii mambo ya nje ni usalama wa taifa kisilaha, mahusiano, ulinzi wa ndani,uchumi n.k.
Tutarajie kuwa mdahalo utagusa mambo ya uchumi pia kwasababu wenzetu usalama ni pamoja na uchumi si maderaya ya jeshi na vifaru.

Eneo kubwa litakalojadiliwa litakuwa mashariki ya kati, Libya, Syria, Israel na Palestina. Pia litagusa maeneo ya China na Russia kwasababu hizo ni strategic area za ulinzi na usalama wa Marekani.

Obama ana advantage kwa siasa za mashariki ya kati hasa alivyo-handle Arab Spring bila Marekani kupeleka askari.
Hata hivyo suala la Libya linaonekana kuwa mwiba mchungu kwake.
Tatizo ni jinsi ambavyo utawala wake ulilitolea taarifa za kubadilika badilika. Hakika majibu yake yanatakiwa yawe maridhiwa vinginevyo hili litaharibu kabisa taswira yake katika ulinzi na usalama.

Kinachofanywa na Republican ni kutaka Obama amwajibishe Hillary au Balozi wake UN. Kwa kufanya hivyo Obama atawaudhi wanawake na hiyo itakuwa ni advantage kwa Romney.
Sijui Obama atawezaje kulimazia suala hili kwasababu kila kukicha kuna taarifa zinaokinzana.
Inatosha kusema kuwa suala hili liatkuwa mwiba kwake Jumatatu jioni.

Kuhusu Syria, hakuna tofauti kati ya Romney na Obama. Obama anaweza kutumia nafasi hiyo kuonyesha kuwa yupo sahihi na kama sivyo basi Romney asema atafanya nini tofauti. Option ya Romney ni kusema atapeleka majeshi na hakika hatasema hivyo kwasababu kitu cha mwisho Wamerekani wanachokihitaji ni vita nyingine.

Kuhusu Iran, inaonekana kuwa Romney hana makali kwa kuzingatia taarifa za taasisi za usalama zinazopingana na hoja zake kuwa Iran ipo karibu kutengeneza bomu la Nyuklia. Hili ni eneo la Obama kama atalitumia vema.

Israel nayo itakuwa mwiba mkali kwa Obama. Mahusiano yake na BB Nyahu si mazuri kutokana na Benjamin kuamini kuwa ni lazima Marekani iwasaidie kuilipua Iran, wakati Obama akipinga hilo kwa kuangalia hali ya uchaguzi

Katika siku za karibu viongozi maarufu wa Israel wamejitokeza na kusema kuwa hakuna wakati wowote ambapo Marekani imeipa Israel msaada wa Silaha zaidi ya kipindi cha Obama.

Tatizo ni mahusiano kati ya BB Nyahu na Obama ambayo Romney anayatumia vema kuvutia wapiga kura na wenye vyombo vya habari vya Israel kumsaidia.

Kwingineko tutasikia siasa zile zile za kawaida kuhusu mvutano wa magharibi na mashariki.

Pamoja na mdahalo kuwa wa kimataifa, bado hoja kubwa inabaki kuwa Uchumi.
Kwahiyo mshindi wa kesho hatarajii kuvuna sana. Kwa Romney inaweza kumuongezea sifa kuhusu siasa za nje na kuendelea kumega pande la wapiga kura wa Obama.
Kwa Obama hili litamweka mahali pazuri zaidi kwasababu so far siasa zake za nje zinaonekana kuridhisha sehemu kubwa ya jamii.

Kwa kumalizia, hadi sasa hivi uchaguzi na mchuano ni mkali sana. Upepo unavuma kwa kasi kuelekea kwa Romney.
Obama yupo katika wakati mgumu sana na ushindi wake kama utakuwepo utaamuliwa kwa kura ya mwisho kuhesabiwa.
Kwasasa uwezekano wa historia kujirudia ni mkubwa na Obama anaelekea kushindwa unless something happen katika siku 22 zijazo.
 
Obama atajilaumu sana kwa kushindwa kumdhibiti Romney kwenye mdahalo wa kwanza kiasi cha kumpa ushindi kwenye mdahalo ule, Hapo ndipo Romney alipopata momentum ya kumkimbiza mchaka mchaka Obama...japo alijitahidi kwenye mdahalo wa pili lakini ushindi wake haukuwa wa kishindo kama wa Romney kwenye mdahalo wa kwanza. Obama bado anayo nafasi ya kumbwaga Romney akipanga vizuri kwenye mdahalo wa tatu na wa mwisho....Suala la Libya ndilo pekee litakalompa shida lakini kwenye masuala mengineyo ya nje yatampandisha chari kama kumuua Osama.
 
MDAHALO WA MWISHO MAREKANI
Mdahalo uliohusu siasa za nje za Marekani umemalizika.
Kama ilivyotarajiwa Rais Obama ameibuka kidedea kwa mpinzani wake.
Kwa wale walioona mdahalo ni wazi kuwa Mitt Romney alikuwa katika wakati mgumu na mara zote alikubaliana na hoja za Obama.

Hili lilihusu eneo ambalo Obama ni mzuri zaidi kuliko mpinzani wake.
Kilichomsaidia Obama ni kuwa katika kiti cha Urais na hivyo kuwa uptodate na habari zote za vyombo vya intelejensia.
Hata hivyo Mitt Romney alimvuta Obama aingie katika eneo la uchumi.
Cha kushangaza hata huko Obama alionekana kuwa mzuri zaidi ya Mitt kuliko alivyofanya awali.

Mdahalo huo umeonyesha kuwa Obama ameshinda katika maeneo mengi, lakini ushindi huo haukuwa mkubwa sana huku akipishana na mpinzani wake kwa point chache.
Kama kuna kitu Obama anapaswa ajilaumu ni mdahalo wa mwanzo. Ule ndio uliompa Romney momentum ya kumkaribia.

Ni vigumu kutabiri matokeo ya mdahalo huu kwa wapiga kura kwa vile uligusa sana mambo ya nje.
Hata hivyo mdahalo huu pamoja na kuwa na tija kidogo, umeweza kuwaonyesha watu uongozi (leadership) na hapo Obama amefanikiwa.
Tatizo ni kuwa je, momentum ya Romney itapungua?

Kwa hali ilivyo kwa sasa kuna maeneo matatu makubwa ya vita(battle ground) ambayo ni Ohio, Florida, Colarado.
Kwa upande wa Florida upepo unaelekea kwa Mitt Romney na anaweza kushinda jimbo hilo.
Obama bado anaongoza Ohio na mdahalo wa leo alijaribu kuwagusa sana watu wa Ohio kama sehemu muhimu ya uchaguzi. Obama anahitaji Ohio na Colorado ili aweze kurudisha kiti chake.

Mdahalo ulitawaliwa na mjadala wa Israel. Umuhimu wa Israel ni nguvu ya kiuchumi ya jews waliyo nayo katika majimbo muhimu kama Florida. Ni nguvu ya vyombo vya habari wanavyovimiliki. Eneo hilo ambalo Mitt alimshambulia Obama katika kampeni, Obama alilimudu vizuri kwa kuonyesha mahusiano yake ya kijeshi na Israel.

Kuhusu Iran, Mitt Romney alionekana kukubaliana na sera za Obama kama ilivyokuwa kwa Afghanistani na Iraq.
Hata hivyo Mitt Romney amenonekana kubadili misimamo na Obama alikuwa mwepesi sana kumshambulia kwa sera zake.

Obama pia alitumia vema mauaji ya Osama kuonyesha ubabe wa Marekani ikiwa ni mkakati wa kuwavuta kundi linalosubiri kuamaua dakika za mwisho.
Kura zinaendelea kupigwa katika baadhi ya majimbo na hilo nalo ni la kuzingatia sana.

Katika kipindi cha siku 14 zilizobaki wagombea watafany kampeni zao kisayansi. Maana yake ni matumizi ya fedha za matangazo katika maeneo wanayoona wanaushindi ili kujiimarisha, wanaelekea kushinda ili kupata ushindi na hata kuacha baadhi ya maeneo ili kuelekeza rasilimali katika maeneo muhimu.

Baada ya mdahalo huu timu za wagombea zitakaa na kuamua wapi wapeleke nguvu zaidi na wapi wajikite wenyewe.
Uchaguzi unatoa matokeo ya kukaribiana sana kiasi cha kuleta kiwewe miongoni mwa wana timu.

Endapo Obama ataweza kumbana Mitt kule Ohio basi anaweza kurudi white house.
Ushindi wa Romney Florida na Ohio utakamilisha safari ya Obama ya miaka minne.

FUNZO
Ukifuatilia mijadala na jinsi wenzetu wanavyoendesha kampeni, basi hutachele kusema sisi bado tupo enzi za mawe(stone age). Mambo muhimu ya kitaifa na kimataifa yanajadiliwa huku rekodi za wagombea zikiwekwa wazi.
Timu za kampeni zinafanya kazi kisiasa na kisayansi kuliko uwepo wa wapiga debe wasiojua mkakati wala mbinu.

Tunatakiwa tujifunze kutoka kwa wenzetu. Inashangaza kuona watu wanaibuka kutoka katika vitanda vyao wakiongozwa na njozi njema na kutueleza mgombea fulani anafaa. Watu hawa ukiwauliza rekodi ya 'mtu' wao hawawezi kusema hata neno moja bali kubaki wakisema 'fulani anajituma sana, anasimamia shughuli n.k''
Utamaduni huu ndio unatupelekea tupate viongozi wasiojua kwanini sisi ni masikini.

Ni utamaduni unaotuletea viongozi wasioijua hata historia ya nchi. Inashangaz kuona kiongozi wa sekta muhimu kama ya elimu hajui Tanzania imetokana na nini.

Kiongozi huyo aliyesema Tanzania ni muungano wa Pemba na Zimbawe alichaguliwa miongoni mwa wabunge.
Ni wabunge hawa waliokuwa wanapita wakisema nichagueni nitawaletea maendeleo kana kwamba maendeleo yapo bandarini na anachopaswa kufanya ni clearance ya kontena wala si sera au maono

Viongozi wa aina hii hawakutokea kama uyoga au kunyesha kama mvua. Ni matokeo ya mfumo wetu mbaya wa kupata viongozi bila kuwajua. Ni matokeo ya kuwa na taratibu mbaya za uchaguzi na pengine ni matokeo ya kukosa elimu ya uraia.

Wakati haya ya Marekani yakiendelea, viongozi wa upinzani wanatakiwa wakae chini na wafanye tafiti za kuona jinsi gani siasa za kileo zinapaswa kutekelezwa. Haitoshi tu kuwa na orodha ya mafisadi, ni zaidi ya hapo.
Na wala haitoshi kukurupuka na kuutaka urais huku tukijua fika kuwa bila kubadili baadhi ya mifumo katika jamii yetu hiyo itakuwa ndoto.
Je, wapinzania wana mkakati wa kupata viongozi kwa kushindanisha hoja?

Kuna somo linapatikana kwa kuangalia wenzetu wanafanya nini.

Tutaendelea kudadavua takwimu na mwenendo mzima wa uchaguzi wa Marekani kila siku hadi siku ya uchaguzi kupitia safu hii.

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3,
Ni kweli kabisa mjadala ulikuwa mkali tumeona Romney akimlaumu Obama kwa kushindwa kutoa uongozi unaofaa kwa dunia na ameruhusu amani mashariki ya kati kuvurugika. Obama alimkosoa Romney akisema amekuwa akipinga sera zote kuu za Marekani ikijumisha kuivamia Iraq.

Wagombea hao wamezungumza sana kuhusu suala tete la harakati za mageuzi katika nchi za kiarabu. Nimevutiwa sana jinsi hawa jamaa wanapokuwa mstari wa mbele kwenye maslahi ya nchi yao.

Pale Obama alivyokuwa anaelezea walivyopambana mpaka kuwezesha makambuni ya Marekani kuuza chuma nchini China pamoja na kuyabana makampuni ya China kuingiza matairi ya magari nchini Marekani...sidhani kama viongozi wetu wanajifunza.
 
Last edited by a moderator:
UCHAGUZI MAREKANI

Baada ya madahalo wa tatu hakuna mabadiliko makubwa sana yaliyotokea.
Kilichojiri ni tajiri Donald Trump kurusha dongo kwa Obama eti atoe vyeti vya shule na barua ya kuombea passport ya Marekani. Ingawa hili halichukuliwi serious, kisiasa lina athari kwa sababu linavuruga mada ya Mitt Romney ambaye amekuwa anapanda chati kwa kasi sana. Watu wanajadili Donald zaidi ya hoja za wagombea na kumpa nafasi Obama.

Kura za maoni bado zinaonyesha uchaguzi mkali kati ya wagombea. Nikumbushe kuwa kuna mashirika zaidi ya 100 yanayotoa kura za maoni nazo hubadilika kila mara. Ingawa zimekuwa na ukaribu sana na uhalisia hilo halizifanyi ziwe sahihi muda wote.

Kura za maoni za shirika moja zinaonyesha kuwa kwa upande wa akina mama sasa ni 50/50. Hili ni pigo kwa akina Obama kwasababu nguvu ya Democrat imekuwa kwa wanawke siku zote. Miezi miwili Obama alikuwa anaongoza kwa 68 dhidi ya 32. Hadi hapo utaona kuwa kama ni kweli basi uchaguzi utaamuliwa na makundi mawili.
1. Independent voters- ambao huwa wanabadili misimamo hata kama ni dhidi ya vyama vyao
2. Undecided voters ambao huwa wanasimama katika hoja na si ushabiki au upenzi wa vyama.

Katika majimbo yanayobadilika(swing states) jimbo la Carolina kaskazini linaonekana kwenda kwa Mitt Romney kama ilivyo Florida. Hili linamuongezea sana nguvu ya kutafuta kura za majimbo mengine na linapunguza nguvu ya Obama.

Katika jimbo la Ohio ambalo Romney anapaswa kushinda, hakuna shirika lolote la kura za maoni linaloonyesha makali ya Romney. Hapa ndipo Obama alipokaza uzi akijua kuwa hilo tu litamfunga mikono Romney kwenda sehemu nyingine kama Colarado na Wisconsin au Viriginia. Hata hivyo Romney anatumia mamilioni ya pesa katika matangazo.

Ohio wameanza kupiga kura leo kama walivyo Chikago. Hii inaitwa early voting.
Kuna mambo mawili yanayojitokeza hapa.
1. Kwa wale wa majimbo yaliyoanza kupiga kura baada ya mdahalo wa kwanza, ni dhahiri Romney atakuwa amewapata.
2. Kwa wale waliosuburi kidogo ambao ni undecided na independent voters basi huenda wakageuza mawazo baada ya midahalo miwili iliyofuata na hapa Obama atakuwa na advantage.

Kitu kingine kilichojitokeza wiki hii ni kuwa katika jimbo la Ohio, Obama amehamasisha watu kupiga kura mapema na hadi sasa idadi ni 2:1 ikilalia kwa Obama. Unless jambo lingine litokee katika siku 16 zilizobaki uwezekano wa Obama kushinda Ohio unaonekana kuwa mkubwa.

Katika baadhi ya majimbo kumewekwa vituo vya watu wasiojiandikisha kwenda kujiandikisha na kupiga kura.
Idadi yao imeonekana kuwa ni kubwa mno na hawa wanasadikiwa kuwa watu wa Obama. Hili ni jambo la halali kwahiyo nalo pia litalalia kwa Obama kama inavyotarajiwa.

Kura zitakazoamua mshindi si za republican au Democrat, ni za unregistered, independent na undecided voters.

Katika mazingira ya kawaida Obama alitakiwa awe mbele japo kwa point 5 hadi 10. Hali inavyoonekana si nzuri kwa upande wake na uwezekano wa Romney kuwa Rais unazidi kuongezeka kila siku.

Katika maisha ya siasa siku 1 ni kubwa sana, kwahiyo wiki mbili ni nyingi sana. Lazima tukiri kuwa lolote linawekana kutokea. Kilicho dhahiri ni kuwa mchuano ni makali sana.

Mambo mawili yanawekana:
1. Kupata rais kwa idadi ya viti 270
2. Aliyeshindwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliompigia kura (popular vote)

Duru matukio inafuatilia kwa ukaribu na itakuletea kila kinachojiri kwa muda muafaka.








0
 
SUDAN KUISHTAKI ISRAEL KWA UN.

Sudan imesema kuwa inapanga kuishtaki Israel kwa Umoja wa Mataifa kuhusiana na madai ya mashambulizi dhdi ya kiwanda chake cha silaha mjini Khartoum hapo jana usiku.

Balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa Daff Alla Elhag Oman, amesema kuwa Israel imevamia kiharamu anga zake mara tatu katika miaka ya hivi karibuni. Sudan hata hivyo bado haijatoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yake na Israel nayo haijatoa tamko lolote kuhusu madai dhidi yake.

Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema inaaminika kuwa kiwanda hicho kilikuwa kinatengeza roketi na zana zingine kwa niaba ya Iran ili kuzipeleka kwa wapiganaji wa Hamas. Na kwa hivyo Israel iliona umuhimu wa kusitisha shughuli za kawanda hicho badala ya kuchukuwa hatua ambazo zingeiudhi Misri.

Serikali ya Sudan inaungwa mkono na Iran na inatumiwa kama kivukio cha silaha kupitia Misri na kwenda kwa Hamas.
 
SUDAN KUISHTAKI ISRAEL KWA UN.

Sudan imesema kuwa inapanga kuishtaki Israel kwa Umoja wa Mataifa kuhusiana na madai ya mashambulizi dhdi ya kiwanda chake cha silaha mjini Khartoum hapo jana usiku.

Balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa Daff Alla Elhag Oman, amesema kuwa Israel imevamia kiharamu anga zake mara tatu katika miaka ya hivi karibuni. Sudan hata hivyo bado haijatoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yake na Israel nayo haijatoa tamko lolote kuhusu madai dhidi yake.

Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema inaaminika kuwa kiwanda hicho kilikuwa kinatengeza roketi na zana zingine kwa niaba ya Iran ili kuzipeleka kwa wapiganaji wa Hamas. Na kwa hivyo Israel iliona umuhimu wa kusitisha shughuli za kawanda hicho badala ya kuchukuwa hatua ambazo zingeiudhi Misri.

Serikali ya Sudan inaungwa mkono na Iran na inatumiwa kama kivukio cha silaha kupitia Misri na kwenda kwa Hamas.

Actually Sudan ni lazima ithibitishe madai haya.
Na Sudan ikiweza kuthibitisha kwamba Israel Imekiuka sheria za Kimataifa suala hilo linapelekwa UNSC.Hiyo inatasiriwa kama act of aggression.Kwenye International law(Criminal agression article 39).It's a breach of peace and violation of UN Charter on territorial Intergrity

-Hata hivyo suala hilo huko UNSC sitarajii Israel kuchukuliwa hatua yoyote kwani Susan Rice na washirika wake UN atapinga na most likely China kwenye hii scenario aka-abstain kupiga kura kwenye resolution yoyote
-Atakachoongea muda wowote sasa Ehud Barack kama ataona uwezekano wa Sudan kuwa na ushahidi atasema amefanya pre-emptive attack in defence of self existence
-pia shuttle diplomacy na rhetorics zitatumika kuitaka dunia kuungana katika kusimamisha harakati za kigaidi
 
Actually Sudan ni lazima ithibitishe madai haya.
Na Sudan ikiweza kuthibitisha kwamba Israel Imekiuka sheria za Kimataifa suala hilo linapelekwa UNSC.Hiyo inatasiriwa kama act of aggression.Kwenye International law(Criminal agression article 39).It's a breach of peace and violation of UN Charter on territorial Intergrity

-Hata hivyo suala hilo huko UNSC sitarajii Israel kuchukuliwa hatua yoyote kwani Susan Rice na washirika wake UN atapinga na most likely China kwenye hii scenario aka-abstain kupiga kura kwenye resolution yoyote
-Atakachoongea muda wowote sasa Ehud Barack kama ataona uwezekano wa Sudan kuwa na ushahidi atasema amefanya pre-emptive attack in defence of self existence
-pia shuttle diplomacy na rhetorics zitatumika kuitaka dunia kuungana katika kusimamisha harakati za kigaidi
Hapo ndipo utaona dunia isivyokuwa na haki. Double standard.
Ben ninyi watu wa inter affairs mnajua Israel imekiuka maazimio mangapi ya UN bila kuchukuliwa hatua.

Shambulizi hilo limefanyika wakati wa kampeni za uchaguzi kwa kujua kuwa Jews wana upper hand katika ku-influency siasa za marekani. I can imagine kama Rocket ingetoka Tunisia leo habari zingekuwaje.
 
Hapo ndipo utaona dunia isivyokuwa na haki. Double standard.
Ben ninyi watu wa inter affairs mnajua Israel imekiuka maazimio mangapi ya UN bila kuchukuliwa hatua.

Shambulizi hilo limefanyika wakati wa kampeni za uchaguzi kwa kujua kuwa Jews wana upper hand katika ku-influency siasa za marekani. I can imagine kama Rocket ingetoka Tunisia leo habari zingekuwaje.

Ofcourse Israel ni miongoni mwa Mataifa vinara wa kwenda kinyume na maazimio ya UN

Unless UN imefanyiwa reforms hii double standard haitaondoka.Veto power iondolewe na badala yake UN security council iwe expanded

Pia with the rise of China na EU intergration at least tutakuwa na multipolar power ingawa EU intergration bado ni wajomba wa US katika international politics

Israel ni wazuri kwa Timing.Siyo Republican au Dems watakaothubutu kulaani shambulio la Israel ingawa halikubaliki katika sheria za kimataifa

Shambulizi lingetoka Tunisia hadithi ingekuwa ni sanctions faster.Baada ya kushindwa kufanya lobbying ya New International Order(NEIO) ,nchi zinazoendelea zimeshindwa kushirikiana wenyewe (South-South Relation) .

Reform UN zinaonekana tishio kwa hegemony ya mabeberu kwa kuwa idadi kubwa (zaidi ya 2/3) ni kutoka South Block.

UN ni vein ya watekaji nyara (mabeberu) wa ulimwengu huku IMF na World Bank zikitumika kama kisu na WTO kama chumba cha kuwafanyia ufedhuli waliotekwa(nchi zinazoendelea)
 
Back
Top Bottom