Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Nguruvi3,
Duru za siasa inazungumziaje uamuzi wa kamati kuu ya chadema kuwavua uongozi zitto kabwe, kitila mkumbo na wengine.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Wana duru za siasa
Kuanzia kesho tutakuwa na uzi maalumu unaohusu mgogoro wa Wapinzani tukiangalia CDM kwa undani zaidi.
Tutaanzisha nyuzi maalum kwa jina la Duru: Mgogoro wa Upinzani.
Tutaangalia kwa undani mambo ya kisiasa hasa waraka uliosambazwa ambao umetoka kwa viongozi wa Chadema.
Tutachambua mstari mmoja hadi mwingine kubaini ukweli na uongo.
Tutabainisha makundi tuliyoyataja
Tutaangalia kama uongozi umetenda haki kwa wtuhumu na watuhumiwa
Tutayaangalia makosa yaliyofanyika katika kuchukua hatua
Tutabaibisha ukweli kwa ushahidi wa waraka huo na mwenendo wa matukio
Tutaangalia kama kweli CCM ina mkono au mchawi ni CDM yenyewe
Tumeshaupitia waraka huo kwa undani na kilichobaki ni kuuweka baada ya marekebisho kidogo.
Kama kawaida yetu hataonewa mtu au kuhurumiwa.
Ninachoweza kusema ni kuwa yale yaliyojadiliwa hapa tangu Ritz alipoleta hoja yote yameonekana kwa uwazi na uhakika.
Tutachambua kuanzia majina bandia yalityotumika, wahusika na mitazamo yao.
Tutaangalia mustakabali wa siasa za upinzani kwa kuichambua model ya Mchambuzi sehemu ya mwisho ya bandiko lake.
Napenda niwahakikishie kuwa mada itakuwa moto na tutawaalika wote.
cc Ben Saanane hammy D Nyakarungu sixgate Nicholas Mungi Arusha one Ritz Mchambuzi AshaDii Ngongo zumbemkuu @ EMT Mag3 Zinedine AshaDii gfsonwin Bongolander Mkandara Mimi baba Zinedine
https://www.jamiiforums.com/great-t...iasa-iii-kifo-cha-mandela-na-yaliyotokea.html. https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/572764-duru-za-siasa-sakata-la-mwaziri.htmlMkuu Nguruvi3
Naona jukwaa hili limekuwa kimya kidogo na kuna matukio mengi ya kisiasa yametokea sehemu mbali mbali duniani. Tukio kubwa la hivi karibuni ni kifo cha Mzee Madiba. Ningependa tujadili hili kwa sasa hususan hatima ya chama cha ANC na nchi ya Afrika Kusini kwa ujumla baada ya Raisi huyu wa kwanza wa SA huru kutangulia mbele ya haki.
Tuendelee kujadili...