Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

Mkuu Nguruvi3,

Duru za siasa inazungumziaje uamuzi wa kamati kuu ya chadema kuwavua uongozi zitto kabwe, kitila mkumbo na wengine.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu mbona wewe hujatoa maoni yako?

Mimi nimefurahia uamuzi huo kwa sababu kulikuwa na PM7 ikaondoka na akina Mtela na waalijinasibu kuwa wana mizizi ndani ya CDM kwa maslahi ya CCM Na kweli mizizi iliendelea kuchipua ikiwa na makao Kinondoni na Lumumba.

Ila Mungu si Athumani katoa fursa hata kama ni kwa ajali Mwigamba kabambwa na "operation" zote kwenye laptop. USHAHDI ambao ZZK, Kitila na Mwigamba wanakiri. Maamuzi yamefanywa na wamepewa siku 14 kujitetea. Tutaona busara zao na za Kamati kuu ya CDM.

Ila kama ni kweli hiyo ndiyo mikakati ya CCM kuhujumu vyama pinzania ni "pathetic". Kwa muumini ye yote ni kushukuru kwa "interventions" za Sir God maana usaliti si fani yenye tija.

Narudi toka Uganda mwisho wa mwezi huu wa 11. Lete thread zenye tija tuzichambue
 
Wana duru za siasa

Kuanzia kesho tutakuwa na uzi maalumu unaohusu mgogoro wa Wapinzani tukiangalia CDM kwa undani zaidi.
Tutaanzisha nyuzi maalum kwa jina la Duru: Mgogoro wa Upinzani.

Tutaangalia kwa undani mambo ya kisiasa hasa waraka uliosambazwa ambao umetoka kwa viongozi wa Chadema.

Tutachambua mstari mmoja hadi mwingine kubaini ukweli na uongo.
Tutabainisha makundi tuliyoyataja
Tutaangalia kama uongozi umetenda haki kwa wtuhumu na watuhumiwa
Tutayaangalia makosa yaliyofanyika katika kuchukua hatua
Tutabaibisha ukweli kwa ushahidi wa waraka huo na mwenendo wa matukio
Tutaangalia kama kweli CCM ina mkono au mchawi ni CDM yenyewe
Tumeshaupitia waraka huo kwa undani na kilichobaki ni kuuweka baada ya marekebisho kidogo.

Kama kawaida yetu hataonewa mtu au kuhurumiwa.

Ninachoweza kusema ni kuwa yale yaliyojadiliwa hapa tangu Ritz alipoleta hoja yote yameonekana kwa uwazi na uhakika.
Tutachambua kuanzia majina bandia yalityotumika, wahusika na mitazamo yao.

Tutaangalia mustakabali wa siasa za upinzani kwa kuichambua model ya Mchambuzi sehemu ya mwisho ya bandiko lake.

Napenda niwahakikishie kuwa mada itakuwa moto na tutawaalika wote.

cc Ben Saanane hammy D Nyakarungu sixgate Nicholas Mungi Arusha one Ritz Mchambuzi AshaDii Ngongo zumbemkuu @ EMT Mag3 Zinedine AshaDii gfsonwin Bongolander Mkandara Mimi baba Zinedine
 
Last edited by a moderator:
Wana duru za siasa

Kuanzia kesho tutakuwa na uzi maalumu unaohusu mgogoro wa Wapinzani tukiangalia CDM kwa undani zaidi.
Tutaanzisha nyuzi maalum kwa jina la Duru: Mgogoro wa Upinzani.

Tutaangalia kwa undani mambo ya kisiasa hasa waraka uliosambazwa ambao umetoka kwa viongozi wa Chadema.

Tutachambua mstari mmoja hadi mwingine kubaini ukweli na uongo.
Tutabainisha makundi tuliyoyataja
Tutaangalia kama uongozi umetenda haki kwa wtuhumu na watuhumiwa
Tutayaangalia makosa yaliyofanyika katika kuchukua hatua
Tutabaibisha ukweli kwa ushahidi wa waraka huo na mwenendo wa matukio
Tutaangalia kama kweli CCM ina mkono au mchawi ni CDM yenyewe
Tumeshaupitia waraka huo kwa undani na kilichobaki ni kuuweka baada ya marekebisho kidogo.

Kama kawaida yetu hataonewa mtu au kuhurumiwa.

Ninachoweza kusema ni kuwa yale yaliyojadiliwa hapa tangu Ritz alipoleta hoja yote yameonekana kwa uwazi na uhakika.
Tutachambua kuanzia majina bandia yalityotumika, wahusika na mitazamo yao.

Tutaangalia mustakabali wa siasa za upinzani kwa kuichambua model ya Mchambuzi sehemu ya mwisho ya bandiko lake.

Napenda niwahakikishie kuwa mada itakuwa moto na tutawaalika wote.

cc Ben Saanane hammy D Nyakarungu sixgate Nicholas Mungi Arusha one Ritz Mchambuzi AshaDii Ngongo zumbemkuu @ EMT Mag3 Zinedine AshaDii gfsonwin Bongolander Mkandara Mimi baba Zinedine

Mkuu Nguruvi3,

Nilisahau kueleza kwamba hiyo model ni kwa mujibu wa Goran Hyden, mtafiti wa masuala ya siasa, uchumi na maendeleo barani africa;
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3, nakumbuka niliwahi kutoa comment huko nyuma kwamba siko interested sana na siasa zetu za kitanzania au kiafrika kwasababu kwetu siasa ni ulaji kwa wenzetu kujenga hadhi ya moyo siyo tumbo. Ila jambo moja naloliona kwa sasa ni kwamba, kwa muda mrefu JF imekuwa mwiba kwa ccm kiasi cha kuizungumzia negatively kwenye majukwaa mbalimbali ndani na nje ya nchi. Lakini kinachoonekana sasa, JF itakuwa mwiba mkali sana kwa upinzani hasa CDM kwa kuwa wana Chadema wengi (huenda wakiwemo na viongozi) wamekuwa wakitumia taarifa za JF bila kuzichambua na kujiridhisha na uhakika wake. Kibaya zaidi katika taarifa hizo wana CDM hao wanajikita sana kwenye ushabiki badala ya uhalisia na kuongozwa zaidi na hisia na kisha (baadhi) yao kutumia hisia katika kutoa judgement au conclusion. Hii ni hatari. Matokeo yake ni kwamba, watu kuoka nje ya CDM wamebaini hilo na kulitumia jukwaa hili katika kucheza na hisia za watu kwa kuposti vitu ambavyo havijengi bali vinabomoa. Kwa mtazamo wangu, CDM wawe makini sana na Jukwaa hili lisigeuzwe kuwa jukwaa kutafuta hisia na kuamua. Ni Ni mara kadhaa tumeshuhudia taarifa za ndani za CDM (ima za vikao au za mikakati) zikilifikia jukwaa hili kupitia kwa "Anonymous" kwa njia ya Tetesi, kabla ya taarifa rasmi ya Chama, na baada ya hapo taarifa hiyo ya "anonymous" inakuja kuthibiti kwamba ni ya kweli. Je huyo anonymous ana power kiasi gani ya kuotea matukio hayo kama sio ni miongoni mwa wahusika wa mkakati au taarifa hiyo. Nadhani ni wakati muafaka kwa CDM kuongea na vijana wake waliomo humu JF ambao wengi wa wana JF tunahisi wako karibu sana na shughuli za mwendelezo wa Chama wakae mbali na the so called Tetesi" vinginevyo Jukwaa hili la JF badala ya kuwa chachu ya mabadiliko litakuwa kaburi la CDM.

Kwa kilichotokea na kinachoendelea CDM hivi sasa, niseme tu inahitajika kipindi kati ya mwaka 1-2 ili kujua kinachoua upinzani Tanzania baada ya tukio hili. Ni tukio zuri kwasababu litabainisha tatizo halisi la CDM na upinzani kwa jumla na hivyo wajuzi waje na muarobaini wake. Nasema hivyo kwasababu. Mgogoro wa NCCR uliondoa wanasiasa mashuhuri kutoka katika chama hicho, na baada ya kutoka, hatukuona "effectiveness" yyte ya chama hicho. Halikdhalika CUF ambayo haikutumika nguvu kubwa sana kuiharibu pia tumeshuhudia viongozi kadhaa wakitoka huko na kutimkia vyama vingine lakini kuondoka au (kutimuliwa) huko hakukuleta TIBA yoyote kwa CUF. Leo hii haya yamerejea CDM, na suluhu ya tatizo ni ileile ya "KUWATIMUA" au kuondoka kwa wanasiasa kadhaa ikiwa ni mbinu iliyotumiwa na vyama pinzani vya NCCR, CUF na hata UDP; ndio nasema-wacha tutumie observation power kujua nguvu za CDM baada ya kuwatimua wanasiasa hawa. Kadhalika, nimalizie kwa kutoa angalizo, Demokrasia haianzii kati, ni lazima ianzie mwanzo-mwisho bila kujali hatua ambayo taasisi inayotakiwa kutekeleza demokrasia ilipo.


Lakini vilevile niseme wazi kwamba, maandalizi ya kushika Dola yana viashiria vingi na mahitaji mengi. Kumekuwa na vijembe kadhaa ambavyo ima chama tawala au baadhi ya watu wamekuwa wakivitumia katika kuvipa majina mabaya vyama vya upinzani (ikiwa pamoja na ukabila(UDP/CDM, udini(CUF/CDM, ukanda (CUF/CDM). Kwangu naona hizi dirt political tactics tu, hata hivyo ni vema kufanyiwa kazi. Hatuchagui viongozi au watendaji kwa Dini zao au kwa makabila yao au kwa jinsia zao au kwa ukanda wao. Lakini tuseme ukweli tu kwamba mambo haya kwa nature ya Nchi yetu kama siyo Afrika kwa ujumla yana influnce kubwa sana ya stability ya nchi hivyo ni lazima yawekwe kwenye "Unwritten Law". Failure to do that, ni kujidanganya kwani ndio uhalisia ulivyo. Hivyo, CDM lazima waende hatua mbele zaidi tena evidence-based ku-apply hii "unwritten law" kwa kukifanya Chama kuwa cha Tanzania zaidi ya hapa kilivyo.

Kwa kumalizia ni kwamba, nikubaliane na Pasco katika moja ya mabandiko yake kwamba, hali ya Tanzania kwa sasa ni kama ilivyokuwa hali ya Marekani na Obama. Watanzania wamechoshwa sana na mwenendo na madhila ya CCM na wanataka mabadiliko kiasi ya kwamba upepo mdogo tu unaweza kuitoa CCM nje. Lakini kwa mtizamo wa Pasco, anaona kwamba chama kilicho tayari kuitoa CCM as if hakiko tayari japo kuna orodha ndefu ya watanzania waliokaa mguu pande wakiwa "Decided to leave CCM, but undecided to go CDM" sijui wataenda wapi, mie sijui-tusubiri hiyo 2015 ikiwa pamoja na baada ya matukio haya yanayoendelea.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3
Naona jukwaa hili limekuwa kimya kidogo na kuna matukio mengi ya kisiasa yametokea sehemu mbali mbali duniani. Tukio kubwa la hivi karibuni ni kifo cha Mzee Madiba. Ningependa tujadili hili kwa sasa hususan hatima ya chama cha ANC na nchi ya Afrika Kusini kwa ujumla baada ya Raisi huyu wa kwanza wa SA huru kutangulia mbele ya haki.
Tuendelee kujadili...
 
Last edited by a moderator:
JK na ANGUKO LA CCM

Wanaduru, katika matukio ya wiki ni pamoja na lile la CCM kuadhimisha miaka 37.
Rais Kikwete na mwenyekiti wa chama amezungumza na wana CCM na kufafanua baadhi ya hoja.

Kwanza, amemsifia katibu mkuu Kinana na sekretariati ya CCM kwa kazi nzuri ya wanayofanya
Akatoa ufanunuzi kuhusu sakata la kufukuza mawaziri mizigo.

Katika ufanunuzi amesema si kazi ya kamati kuu kufukuza mawaziri mizgo na kwamba mawaziri hao walitetewa na kamati kuu kuwa makosa hayakuwa yao.

Duru za siasa tunapenda kukumbusha kuwa mara zote tumesema Rais Kikwete ni mtu asiyependa kuudhi mtu na mara nyingi hupenda kumfarahisha kila mtu. Hilo ndilo lililotokea mjini Mbeya.

Ziara za Kinana hakika ni muhimu kwasababu zililenga kukirudisha chama kwa wanachama, kuwasikiliza na hatimaye kukabliana na wimbi la vyama vya upinzani vinavyobomoa ngome za CCM kila mara.

Kinana aliposema mawaziri mizigo alikuwa amejiridhisha kuwa hilo ni tatizo.
Kwa mfano, kuna mahali ambapo waziri husika hajawahi kutembelea si kwasababu hana usafiri bali kukosa tu hamasa na maono ya kazi

Kuna sehemu wananchi wamelalamika bila kusikilizwa si kwasababu hakuna pesa za kuwasikiliza bali hakuna watu wa kuwasikiliza.

Hoja ya Kinana ilikuwa na nguvu kabisa kuwa tatizo lipo katika serikali na alimaanisha kumshauri rais kuliangalia tatizo hilo kama serikali ya CCM.

Kikao cha CC kilipoitishwa ni wazi rais alijua ajenda zake na rais alikuwa na fursa ya kusema hilo si suala la CC. Kikwete alikubali likajadiliwa na mwisho wake akawageuga wenzake kwa utetezi laini kuwa tatizo lilikuwa ni fedha za wizara na wala si mawaziri.

Duru tunajiuliza hivi tatizo la wizara ya elimu ni kukosa pesa au ni uongozi hafifu?
Matokeo yaliyokuwa mabaya katika historia ya nchi ya kidato cha nne chini ya waziri husika hayakutokana na ukosefu wa pesa, ilikuwa ni uongozi mbaya.
Hivyo tatizo si pesa tatizo ni uongozi.

Rais alipoona ametenda kinyume na wenzake na kwamba amewadhalilisha sana ghafla akaenda Mbeya kuwasifia kwa kazi nzuri wanayofanya.
Hapa alitaka kuondoa hisia za dhalili alizozisababisha kwa wenzake akina Kinana na timu.
Wakati huo huo tayari ameshawafurahisha mawaziri na ilikuwa zamu ya kumfurahisha Kinana

Kauli za rushwa nazo zimeshangaza duru za siasa. Haiwezekani rushwa ambayo imekuwa inatendeka kila siku kwa mtindo wa harambee n.k, ionekana ni jambo baya.

Rais ana taarifa zote kuhusu suala hilo na kwa miaka 8 ameliacha liendelee kwasababu wanaofanya hivyo ni maswahiba wake.

Wiki mbili zilizopita waziri Sitta aliwashitaki baadhi ya wagombe nafasi ya 'urais' kwa kutoa rushwa.Kauli za Makonda ambazo zimeungwa mkono na wazee kama Malecela na kupingwa na wazee kama Mgheja nazo zimekiyumbisha chama.

Kwa mtazamo wa kufurahisha kila upande, rais amekemea rushwa ili hali alijua inatendeka tena usoni kwake.Kwa maneno mengine kauli za rais ni za mdomoni lakini moyoni si hivyo mtu anavyodhani.

Huko nyuma alishawahi kutoa kauli za Mgamba amabazo hadi leo zimebaki hadithi. Hii nayo ipo katika mtindo huo huo wa kufurahisha baadhi ya watu kwenye mikutano na nyuma ya pazia kuwafurahisha watu wengine kwa siri.

Zamu ya kumfarahisha EL inakuja tena kwa kisingizio cha wanachama wamemtaka.
Ukweli utabaki kuwa kauli za JK ziashiria kuunga mkono kwa siri jitihada za EL na kitendo cha kuwasifia akina Kinana na Nape ni kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Endapo yupo atakayeamini kuwa Kikwete alidhamiria kusema alichokisema Mbeya mtu huyo afikirie tena.Ni ngumu sana kumwani kiongozi anayetaka kuwafurahisha watu na si kuwaongoza.

Jk hapaswi kulalamika kuhusu rushwa akiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
Hata hivyo tunajiuliza hivi atawezaje kuwashughulikia wala rushwa kama kashindwa viongozi mizigo?

Duru za siasa tunaona mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM.
Hali hiyo itajitokeza wakati wa bunge la katiba na chaguzi za serikali za mitaa.
Kuna ombwe kubwa sana la uongozi ndani ya CCM ambalo limepita hadi ndani ya serikali.

Kwa uchache duru tunasema kifo cha CCM kinaonekana wazi na hakika JK atakuwa amesimama 'wodini' akishuhudia CCM ikikata roho.

Kitendo cha kufarahisha makundi na si kuchukua hatua za makusudi zikiwemo za nidhamu ni kukiangausha chama chake.

Kitendo cha kutumia mikutano kulalamika na si kuchukua hatua ni maafa kwa CCM
Kitendo cha kuwadhalilisha wenzake na kuwafariji huku akiwa amebeba wengine ni tatizo kwa CCM.

Laiti wapinzani wangekuwa wamejipanga vema msiba wa CCM ungefika mapema kuliko inavyodhaniwa.
Laiti wapinzani wangekuwa na uwezo wa kutumia udhaifu wa 'adui' kummaliza, pengine CCM ingekuwa imeezeka paa la matanga.

Hakuna wakati katika historia ya CCM, chama hicho kimekuwa dhaifu na vulnerable kama sasa.
Ombwe la uongozi ilikuwa silaha nzuri, rahisi na isiyo na gharama kuimaliza.

Kwa bahati mbaya wapinzani badala ya kusaidia kuondoa 'life supporting machine' wao wamebeba vimitungi vya oksijeni wakimpuliza mgonjwa. Duru hatuna uhakika kama wanajua au ni bahati mbaya.

Kama kuna anayedhani CCM ipo madhubuti basi asubiri muda maana wakati utasema.

Tusemezane

cc. Pasco Mwalimu Mchambuzi Kimweri Bongolander FJM JokaKuu AshaDii Mag3 Mkandara Gamba la Nyoka Zakumi
 
Mkuu Nguruvi3,

Ndio maana katika greatest Injustices ambazo wana Historia watakuja kuzifanyia maandika lukuki, ni kitendo cha CDM kukosa busara na vision katika kipindi ambacho CCM is the most vurnerable. CCM has never had a weaker leader than before JK before,he is plain weak, in and out. He is foremost a politician than he is a leader. CDM not being able to asses the situation are trying to out-wrestle on the political arena with political stunts.This wont take CCM and JK down.

What CDM should have done is getting to the core of the problem which is CCM and work hard to remove it strategically. instead of dancing on CCM's tunes.CDM should be setting up ajendas, not sitting by waiting for the CCM Bigwigs to make political Blunders. If ufisadi and corruption were too big a vote gainer, Slaa should have been at Magogoni now by winning 2010. They were not.

The biggest asset CDM has is the people of Tanzania, who are worse off now than they have ever been. Pumping up the chest and telling common mwananchi someone is bought by CCM is simply petty politics to them. How about you start by breaking it down really simple on how you will serve them better. And show them the team you have formed that will make sure this is going to be handle this improvement in their life. And this is where CDM really is lacking, they have a very thing leadership core. And instead of embracing strategists and capable people they have decided to take the popularity contest route.

Who in their right minds seriously believe, someone like SUGU and LEMA can serve as Ministers? these were supposed to be lumped together in propaganda team, and their team limited to that spectrum. Then CDM was supposed to introduce to the public an excellent cream of capable individuals with whom we can trust to take Tanzania to the next level.

On the other Hand what is going on in CCM shows a party that has run out of ideas. A party that is feeding on it's glory days and hedging on it's power base. even with it's absolute worst leader, CCM still has a lot of technocrats with know hows on how to make things better.

If i were CDM this would have been my key strategic angle, taking out and isolate half rotten bigwigs within CCM and give them an olive branch. There is now way CDM can win any election if CCM remains one with all it's imperfection. It's obvious there are a lot of unsatisfied souls inside CCM. these should be CDM focus, as far as destabilising CCM.

what i have seen is it's CCM who did this to CDM, ZITTO and team were unsatisfied, CCM used the window to De-stabilize them while at the same time they went on to self realization process of rebuilding their grassroots. Say what you may about Kinana, but you can easily say he is strategically superior to Mukama and Makamba. I guess that's what Harvard Education gets you. even if you decide to use it for selfish reasons.
 
Mkuu Nguruvi kwa sasa ni wazi kabisa kuwa ndani ya CCM hakuna mtu mwenye moral authority ya kumnyoonesha kidole mwingine. Wenye moral authority wako chini sana kwenye uongozi wa CCM na hawana ushawishi wowote.

Katika hali ya kawaida sidhani kama Abdulrahman Kinana ana uwezo wa kusema mtu fulani ndani ya CCM hafai kwa dosari hizi na zile, sana sana watacheka. Yeye mwenyewe jina lake kuhusishwa na pembe za ndovu, halafu anakuwa katibu mkuu wa chama ni doa kubwa sana kwa CCM yenyewe. Wanaomkebehi wanajua kuwa kwa lolote analoweza kusema haliwezi kuwa na mashiko.

Mwenyekiti mwenyewe wa chama anaongoza chama ambacho kwa sasa kinatatizwa sana na rushwa na wala Rushwa. Akiwa Rais ni haki kwake kusema tupambane na rushwa, lakini tukiangalie vitendo vya chama chake na wananchama wake sidhani kama kuna mtu anaweza kusema kwenye kauli yake kuna uhalisia, other than just a talk.

Nadhani unaweza kuona kuwa maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM kwa mwaka huu, yamekuwa hafifu kuliko maadhimisho yoyote ambayo yamewahi kufanyika. Hii inaonesha kuwa sura ya CCM na mvuto wake vina matatizo makubwa.
 
Back
Top Bottom