Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)


If this post was an opera perfomance i would call it Luciano Pavarotti last perfomance at the New York Metropolitan Opera. Grand in every way. You cut through the inner core of the issue.Well done. I sencerely hope CDM bigwigs are reading this thread.
 
I keep repeating, How can you publicly declare someone is insulting you to the public if you go to great lengths revealing what this person was writing in great secrecy?
What Kitila and Team prepared was never supposed to see the light of day save for stupidity of whoever makes decision at CDM cc.This is something that was stolen from them for God's Sake.wise men said two wrong's dont make it right. Exact opposite of What CDM did here.
For me they crossed a huge line by agreeing to go this low,worse enough they went to all that to reveal things that are 100% true and were supposed to be their internal compass.Another huge mistake all on it's own.
Even the court has to have a warranty to get information from someone.You don't just ambush people like it was the Soviet Russia. It will take a lot of convincing for me to regard CDM in the same light after this debacle. I am sure i am not alone.
Most of us who were tired of CCM are now extremely disappointed by what CDM is turning to be. In any Organization it is a very distressing sign when you have leaders who wants absolute obedience. It says if a group of people always have the same opinion, either one is not doing any thinking at all, or someone is .., you can fill that up.
 

Mkuu utasemaje Kitila na Mwigamba wametoa siri za kikao wakati waliyokuwa wanayajadili hawajamuleeza mtu aliye nje ya kikao?hivi unawezaje kusema kuwa Subset ya set ina association na another set wakati hiyo subset ni mutually exclusive na hizo set nyengine?mathematically isnt this subset still in association with it's parent set?

This was a HUGE blunder by CDM, whatever Mwigamba and Kitila Exchanged between them regarding the state of CDM CC meetings did not fall under leaking of secrets. Unless CDM has proof that these contents were leaked to a third party.So far the only guys who did this are CC themselves. They leaked their own secrets with hopes of badmouthing Kitila and Mwigamba while encapsulating ZITTO who was carefully not Mentioned as participant in the named Waraka.
 
Mkuu Kimweri , Kwa muda sasa nimewauliza wanajamvi hasa Mkandara na Pasco ambao wanahoja kama yako swali moja, Waraka uliandikwa lini?So far hakuna jibu, iliyopo ni hoja ya waraka ulikuwa wa watu wawili Mwigamba na Kitila.

Nimewahi kuweka mazingira ya kuonyesha waraka uliandikwa kati kati ya June 2013 na kwamba utekelezaji ulikuwa katika hatua za juu. Ili kuthibitisha maneno yangu na kuwathibitishieni kuwa waraka haukuwa siri na ulikuwa katika public domain nitaweka thread mjionee.

Kimweri umesema waraka haukuwa kwa ajili ya Public consumption, mimi nasema Public ilikuwa ina consume waraka.Soma haya.JULY 2013 Wakuu maneno hayo yaliandikwa katika mtandao wa JF. Sijui kama mnahitaji ushawishi zaidi kuwa waraka ulikuwa kwa public consumption na public ishaanza ku-consume vema tu na wa;a haikuwa siri tena.

Someni haya ili kujiridhisha au kukanusha kama ninachosema si kweli
OCTOBER 2013 Kabla ya waraka kunaswa
Mkulima masikini ni Mwigamba aliyekamatwa na waraka.
Maneno hayo ambayo ni neno kwa neno kutoka katika waraka yamewekwa hadharani hapa JF.

OCTOBER 19 2013 Ili kutibitisha kuwa mtandao uliozungumziwa katika waraka umekamilka na uliwa kazini Mwigamba akaandika maneno haya Nawaomba hoja zenu kama ninachokisema ni sahihi au la.
Nasisitiza tena, maneno hayo yaliyomo katika waraka yalishatolewa katika public domain kwa utthibitisho huo hapo juu na kwamba waraka haukuwa siri. Hapo ndipo hoja ya 'intent' inapoingia kuwa hizikuwa kampeni ilikuwa uharibifu uliofungwa katika kasha zuri na kuandikwa mkakati.

Wakuu kama hamtaweza kuja na hoja tofauti kwa uthibitisho basi tufunge pazia na kukubaliana neno 'waraka haukuwa siri' ulishavuja kwa makusudi katika jamii.

 
Nime prove beyond doubt kuwa mpango huo haukuwa siri. Ulishavuja katika public na kilichokuwa kinafanyika ni kuvuruga wana CDM. Nime prove na naomba usimame na kusema si kweli kwa vithibitisho.
Kama utasema mpango ulikuwa ni siri na haukujulikana inabidi utuambie waraka uliandikwa lini?

Mimi nimetoa proof za kwamba waraka ulikuwepo toka June, tueleze waraka ulikuwepo toka lini.
Kama huna uthibitisho inabidi tukubaliane kuwa waraka haukuwa siri.
 
Ndio maana nasema wenzangu mnaangalia majina na matukio halafu ndipo mnaangalia waraka. Mimi naangalia waraka kwa contents, context na intent.
Hapo ndipo naachama na wengi.

Nimeweka wazi kabisa kuwa suala lililopo mbele ya mjadala huu si nani anafanya vizuri, mwanasiasa gani mzuri, yupi ana akili ndogo nani mwenye PhD au yupi ni magumashi. Suala ni kuangalia njia za waraka ambao siyo siri na zililivyotumika kuuingiza katika public domain kwa njia ya kukimaliza CDM.

Hilo la Mbowe kuwa na uwezo au la, nadhani wana CDM ndio wenye kauli ya mwisho. Kuamua nani ana uwezo nani hana ni suala la uchaguzi na hilo CDM wana haki nalo.
Nashangaa umekimbilia kusoma hukumu badala ya kuwaachi wenyewe.
Huo kama ni utetezi wa waraka nadhani utakuwa umetoka nje ya mstari.

 
Waraka unasema hivi ''Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara. Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo''
Pasco: Wale wenye kuona mbali, na wenye nia njema ya dhati na Chadema kuingia ikulu 2015, wameyaona madhaifu yaliyopo!, kuliko kuikosa ikulu, ni bora kufanya mageuzi ya ndani, na ndipo waraka ulipobuniwa!.
Hapana! waraka ni mwendelezo wa juhudi za awali zilizokuwa zinasimamiwa na Kitila na Zitto katika kuleta 'mageuzi'. Jitihada hizo zilifyatuka na njia mbadala ikawa kuandaa waraka. Kundi la masalia ambalo mfadhili wake alikuwa ZZK lingefanikiwa kuleta vurugu kama si Ben Saanane kujitoa mhanaga.

Vurugu za Juliana Shonza zilikuwa zinaungwa mkono na Kitila na ZZK ambao walikuwa na ukaribu sana wa kisiasa na kiutendaji.

Kitila aliandika waraka wa kumtetea Juliana hata pale kila mwenye akili timamu alijua makamu mwenyekiti wa BAVICHA hawezi kuwa mkubwa kuliko mwenyekiti na hawezi kuwa msemaji wa CDM.

 
Well, hapa ndipo ninaposema tuangalie waraka kwa contents,context na intent tusitangulize hisia.

Kama jemedari ni malaya hilo siwezi kulizungumzia kwasababu sina facts.

Ninachoweza kuzungumzia ni facts zinazopatikana katika waraka. Hapa nikuonyeshe kuwa ulichokisema kuwa ni hard facts, ni ukweli na kwamba hasingiziwi, waraka umeonyesha kiwango kidogo tofauti na wewe. Soma waraka unasemaje kuhusu umalaya wa Mbowe

waraka :Mpinzaniwetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwonakama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya anayependakutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilishahata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwaketu bali hata za watu wengine

Halafu waraka huo ambao umemkemea jemedari kwa tabia mbaya unatoa tafsiri tofuati ya umalaya kwa yule 'tunayemtaka' soma hapa

waraka : Katika taasisi zetuhizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema amani haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo nihaki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damukutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakatimwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwaunaowaongoza''

Kwamba jemedari alifanya umalaya ni kosa, tunayemtaka akifanya umalaya uwe kwa siri. Hili linaonyesha jinsi gani waraka ulivyoandaliwa hovyo, ulivyokosa maono na ulivyokuwa na nia mbaya.
Sisi tunaouangalia kwa contents, context na intent tumeona hilo, ukitanguliza hisia, mapenzi na mahahba hata kama utausoma waraka miaka 10 hutaweza kuona mambo kama haya Kwanza suala la kuwa honest katika ndoa ni la mtu binafsi. Hata hivyo tukilizungumzia kwa waraka nashangaa kwasababu hao waandika waraka mbona hiyo honest, na uaminifu hawana! Nasema kuwa aliye msafi na achukue jiwe awe wa kwanza kumponda'mzinifu'
Pasco naona hilo tuliache maana tutaandika na ku cross line.

Hivi unadhani maneno haya katika waraka yalikuwa na maana gani?
:Katika taasisi zetuhizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema amani haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo nihaki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damukutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakatimwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwaunaowaongoza''

Suala la waraka kutokuwa wa public consumption nimelieza kwa uwazi na undani.
Waraka ulishaingizwa katika public domain kabla ya kukamatwa. Soma uzi hapo juu ujiridhishe.

Mwigamba kasema wazi, viongozi wa wilayani walikuwa wanamwelewa akimaanisha kazi ya kueleza waraka ambao yeye alikuwa nao ilishafanyika.

Narudi tena na tena waraka haukuwa siri ulishakuwa katika public.
Kwa anayekataa basi ajibu bandiko langu akionyesha kuwa maneno ya Hammy-D na Mkulima masikini yalifanana na ya waraka kwa bahati mbaya

Kama hakuna anayeza kuthibitisha kama nilivyofanya suala hili la waraka wa siri lifike mwisho isipokuwa tu kwa yule atakayekuwa ameamua kugoma kuelewa.
 
Mkuu Nguruvi3, kwanza asante kwa uchambuzi wa kina, nakubaliana na wewe suala la umalaya tuliache, ila waraka kwa upand wa MM haukumaanisha umalaya wa mapenzi ya ile starehe ya wanawake kwa sababu MM bado ni bachelor, hata akitanga tanga ni katika kusaka mchumba, japo nimemnote wakati wote wa kesi, alitulia na his first love ya alipokuwa UDSM na nikimuona nitamshauri aone tuu ili kutulizana!.

Ushauri wa waraka kumhusu MM ni ni ule uswahiba wake na kina Zoka na watu wa CCM!.

Sikubaliani kabisa kuziunganisha hoja za Hamy D na waraka, that was just a coincidence!.

Hebu nisome hapa kwa makini katika uzi wangu huu [h=3]CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga! - Jamii Forums
Huu uzi, niliupandisha tarehe 13 November, 2010
na hivi ndivyo nilivyosema kuhusu CCM na Chadema[/h]
Kwa hiyo hapa mimi nilikijua "kidumu" tangu 2010?,

Baada tuu ya thread hii haikupita muda CCM wakukaa na kujuiliza kulikoni?, nijidai kuwa CCM waliamua kujiuliza baada ya kusoma JF?. Sasa soma hiki nilichoishauri CCM,
Baada ya muda sii mrefu, Makamba alipigwa chini, wakamleta Nape, na January!, Jee nichukue credit kuwa CCM wamefuata ushauri wangu?!. Au angalia hapa nimesema nini kuhusu Chadema

Nilishauri Freeman aachie, hapa waraka unataka kumng'oa, unaweza pia ukadai niliujua waraka toka 2010?!. All that was only a mere coincidence!.

Sehemu ambayo sitakubaliana kabisa na wewe ni "the motive behind waraka", the manner, and the intent, wewe unasisitiza ule ulikuwa ni uhaini, with ill motive kuivuruga Chadema na ulipangwa kutekelezwa kwa kufanya mapinduzi!.

Mimi nasisitiza waraka haukuwa uhaini, ulipanga in good faith, kuisaidia Chadema kupata jemedari bora kuliko aliyepo kwa nia ya kuimarisha Chadema, mpango mzima ulikuwa ni creation ya "a new wining coalition" ili kupata viongozi bora kupitia the normal electoral process ya uchaguzi wa ndani wa Chadema!.

Kwa msimamo huu, nitaendelea kuamini we have both take sides, you've taken the sides of the wrong notion kuhusu waraka, na mimi naamini ndiye nasimama kwenye true values za ule waraka, kwa maana hiyo tutaendelea kuwa paralell,
hivyo nashauri tukubaliane kutokukubaliana, kila mtu ashikilie msimamo wake, ila siku zote, ukweli hua ndio unaosimama, na utakao simama mpaka mwisho!.

Kama ni ukweli waraka ni uhaini, then, kina Kitila, Mwigamba na Zitto, wamehukumiwa kwa haki, na baada ya kuwatimua wahaini hawa, Chadema itakuwa safi, imara zaidi na itachukua dola 2015!.

Kama hawakuhumiwa kwa haki, "the law of the karma" will take charge na kuishukia Chadema, zitatembea bakora, watenda maovu lazima waadhibiwe tena hapa hapa duniani, na 2015, ikulu watafanya kuisikia tuu kwenye bomba!.

Thanks for a good thread, fikirishi!.

Pasco
 

Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa, lakini kuna kitu cha msingi sana "we have to set the record straight here". It's very easy to connect the dots backwards. Kama Pasco alivyoainisha huko nyuma, yaliyokuwemo kwenye waraka ni mambo yaliyokuwepo kwenye public domain, actually Kitila and Team can even come out and say that, they were just compiling public domain's temperament.Of which even Pasco can become part of "muandika Waraka".Tuhuma nyingi zilizokuwemo kwenye waraka zinavunja hoja ya waandika waraka kuvujisha siri za vikao vya Chama, kwani Lawama kubwa wanayopewa ni kutoyapeleka haya mambo kwa chama kuyajadili, sasa watavujisha vipi siri za kikao ambacho wanatuhumiwa kutojadili content?Ukitazama kwa makini, na ukiusoma waraka, ukitazama reaction ya viongozi wa CDM sasa hivi, utagundua kuwa yaliyokuwemo kwenye Waraka ni hadithi za kumfunga paka kengele, hakuna aliyekuwa tayari kufanya hivyo, lakini kila mmoja wao kwa umoja wake alikuwa anayafahamu.waandika waraka walipata tu "half-courage" ya kuyaweka wazi.lakini hata wao wameonesha ni jinsi gani waliyokuwa wanayaandika yalikuwa Taboo, kiasi kwamba hayakutakiwa kusemwa na kiongozi wa chama hadharani, hence, matumizi ya pseudonyms na waraka kuwa siri.

Ukitazama kwa makini unagundua kuwa hauwezi kuwatuhumu kwa kuvujisha siri."siri" hizi hazikujadiliwa kwenye vikao.Pia huwezi kuwatuhumu kwa kuandaa uzushi,kuwashambulia viongozi wenzao.Waliyoyaandika hayakuwa mapya,kila mtu aliyafahamu.yalikuwa kwenye public domain siku mingi tu.Pasco shadihi wa hayo.Nani asiyejua Mbowe ni Tajiri mkubwa?nani asiyejua Mbowe na slaa wana mahusiano na wabunge wa viti maaalum?Nani asiyejua Mbowe hana international Exposure?

Ndio maana naendelea kusema, kama CDM wangekuwa na Busara wasingeuweka waraka kuwa public, kwani kwa kufanya hivyo wametuonesha kuwa demokrasia ndani ya Chadema ni Demokrasia yenye mapungufu makubwa.

Siwatetei kina Mwigamba moja kwa moja, lakini Viongozi wa CDM wana makosa makubwa kwenye hili, wao walishika Mpini, wao ndio walikuwa kwenye position ya make or break, and they choose to break, thinking kuwa the public will trust the same people over again.what i have learnt over the years ni kuwa Tanzanians lose their trust fast the same way they gain it.that's why CCM "A" game has always been to tarnish anyone with a squeeky clean image to the public.
 
Itakuwa ni ajabu kweli kuchukua mitazamo ya wananchi au wana JF kuhusu mambo mbali mbali yanayotokea katika nchi hii yetu kama ushahidi wa kujua ni lini waraka umeandikwa. MATHALANI NINAWEZA KUTAFUTA POSTS NYINGI SANA HAPA JF TOKA MWAKA 2006 , ZINAZOZUNGUMZIA MAMBO AMBAYO YANAFANANA NA YALE YALIYOMO KWENYE WARAKA NA NIKAYAPATA, HII HAINA MAANA WARAKA ULIANDIKWA MWAKA 2006!!!.

Nguruvi ametoa ID ya member mmoja kwa jina la Hammy-D. Sijui kama anamfahamu huyo Hammy-D ni nani, isije ikawa kwa sababu Hammy-D ana mitizamo tofauti dhidi ya Chadema moja kwa moja mtu akaconclude kuwa Hammy-D ni mmoja wapo katika kundi la kina Kitila, Je vipi kuhusu Ritz, FaizaFoxy, Simiyu Yetu, je nao ni wana waraka?.

Kitu kingine ni kwamba, kuna tofauti kati ya Waraka as a document, na Mawazo ya mtu yanayopelekea kuunda waraka, bila shaka Muunda waraka atakuwa na mtizamo wa kisiasa unaoendana na yale yaliyomo kwenye waraka. KWA HIVYO BASI NI DHAHIRI NA NI RAHISI MTU MWENYE MTIZAMO FULANI AKATOA MAONI YAKE KWA NJIA NYINGINE KABLA HATA YA KUUWEKA MTIZAMO WAKE KATIKA WARAKA!. Ninaamini Kama Tungepata kufahamu ID zote alizokuwa akitumia Mwigamba au Kitila katika mitandao ya jamii (Achilia mbali ID ya Masikini Mkulima ambayo Mwigamba alikiri kuwa ni yake) bila shaka tungeona kabisa kwamba maoni yake yanaakisi kiasi kikubwa yale yaliyomo katika waraka. HII HAIMAANISHI KWAMBA TAYARI WARAKA USHAEXIST. KWA HIYO NI VIGUMU KUJUA EXACTLY WARAKA ULIANDIKWA LINI, MPAKA WAO WENYEWE KINA MWIGAMBA WATUELEZE!.

Kuna Thread humu ndani ilikuwa ikiitwa "Chadema Must Reform" ilianzishwa na Rev Kishoka, mle ndani kuna michango mingi sana ya wana JF ambayo baadhi ya michango yake inaakisi mambo yaliyomo kwenye waraka!.

Kuna Waraka wa Marehemu Chacha Wangwe, mle ndani kuna mambo yanayoendana na yale yaliyomo kwenye Waraka wa kina Mwigamba, Je Waraka wa kina Mwigamba ulianza kuandikwa tokea enzi za Chacha na kumalizwa kuandikwa mwaka 2013?.

Na pia ni vigumu kujua kwamba Waraka uliandikwa siku moja, au katika mlolongo wa siku n.k
Ndiyo Maana Zakumi akasema, WARAKA Iikuwa ni njia ya kuyaweka katika maandishi malengo ya watu wenye dhamira fulani.

Waraka ule Hauna tatizo, Tatizo ni Ruzuku za chama, ni ukosefu wa dira wa Mwenyekiti, ni ukosefu wa maadili wa mwenyekiti pamoja na exposure, ni kushindwa kukifanya chama kuwa cha hoja badala ya matukio, hizo ndizo ishu za kudiscuss, Waraka is just a vision put on the paper!!. Kina Kitila walikuwa smart enough kujua kuwa the establishment will try to extinguish the fire of change, na badala yake itatumia advantage ya power ili kuendeleza status quo. ndiyo maana the like minded wakaja na plan, plan ambayo imekuwa aligned katika misingi ya chama ili kutafuta ushawishi ndani ya chama na hatimaye kukirudisha/kukiweka chama katika msitari, na haya yangefanyika katika uchaguzi ndani ya chama.

Mwenyekiti amekuwa muoga bila sababu na kwa bahati mbaya saga hii imemuharibia Mwenyekiti kisiasa na pia kukiyumbisha chama sana. ndiyo maana hatimaye wanatumia bilioni Moja kukodi madege kwa kampeni ya wiki moja, wakati hawana Ofisi nzuri na bora mikoana, hawana vitendea kazi vya kutosha kama magari ya chama,computer, fenicha etc. Kiufupi ni kwamba wangeboresha vitu hivyo wangeweza kuwafikia watu wengi sana na kwa muda mrefu ujao, badala ya hii populist measure ya helicopters!. Tazama hata makao makuu yenyewe hayaendani na hadhi ya Chama kikuu cha upinzani kinachotaka kushika dola!
 
Jamani mbona mnahamisha goli kila wakati?
Nimeweka maneno ya wahusika nikilinganisha na waraka neno kwa neno.
Ni sehemu tu, laiti kama mnekwenda mbali zaidi msingeweza kusema ni 'concidence'.

Pili, nimeweka waraka wa Mwigamba kama ' masikini mkulima' neno kwa neno nikinukuu hata tarehe. Hili hamsemi ni coincidence hata kidogo. Hamkanushi kwasababu hakuna mahali pa kuhamishia goli.

Ninashindwa kuelewa kwasababu nikiwauliza waraka umeandikwa lini, wenzangu hamna majibu. Nikiwaonyesha umeandikwa lini mnakataa na kuhamisha goli.
Please hebu tujaribu kuwa honest.
Mimi sipo kutetea mtu au watu nipo kuweka haya mambo wazi kabisa.

Pasco na Gamba la Nyoka, nilete ID nyingine ambayo ina maneno kama hayo tena?
Nilishafanya homework yangu vizuri na kujiridhisha.


Pasco soma tena maneno yafauatayo maana unahamisha goli tena. Waraka umemuusia MM hata kama anajihusisha na mapenzi iwe kwa siri. Soma

Katika taasisi zetuhizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema amani haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo.

Kuna mambo ambayo nihaki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damukutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakatimwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwaunaowaongoza''

Waraka unamuasa MM akifanya mapenzi iwe siri, halafu waraka huo huo unalaani mapenzi kwa wengine na kuita umalaya.Uniambie waraka huo ulikuwa wa kisiasa na kwa lengo la kisiasa! Too low, abysmal, poor and shame!!

Unapokataa kuwa waraka haukusema jinsi ya kuhifadhi umalaya kwa MM unahamisha goli.
Naomba tuishie hapa kwa suala hilo, likijadiliwa kwa uwazi litaleta matatizo katika nyumba za watu.


 
Mkuu Nguruvi3, sijahamisha goli, nilichosema malaya ni yule mwenye ndoa yake akaenda nje!, they were very right kumuita hivyo walivyomuita!. MM kwa vile hana any commitment, akipita pita ni justified kuwa ni ndege anayeruka ruka kutafuta pa kutua!. Ndege mwenye tundu lake, akiendelea kuputapita ni kutangatanga!.

Pasco.
 
Bado unahamisha goli, endapo hoja ya umalaya inahusishwa na uongozi wa chama, kwanini hoja ya mapenzi kwa 'tunayemtaka' ipewe uhalali tukijua itahusishwa na chama pia.

The bottom line ni kuwa mapenzi na uongozi havijengi taswira nzuri kwa mujibu wa waraka regardless nani anafanya hivyo. Double standards zina matatizo na ndicho chanzo cha kusema waraka ni too low, haukuandikwa kama muongozo wa kisiasa bali chuki za kujenga uhalali fulani.
 
Sasa kama hujui waraka uliandikwa lini unapataje courage ya kusema waraka ulikuwa ni siri na haukuingia katika public domain. Unawezaje kutetea hilo ukijua hujui waraka uliandikwa lini.

Pili, kufanana kwa mawazo ni tofauti na kufanana kwa neno kwa neno.
Nimeonyesha kuwa mawazo yanaweza kushabihiana lakini uwasilisha wa mawazo hayo huwa na tofauti.Kwa msingi huo nimenukuu neno hadi neno ili kutotoa nafasi ya ninyi kuleta sababu kama hizi za sasa hivi. Mnahamisha goli.

Tatu, Unesena maneno haya ''Waraka ule Hauna tatizo, Tatizo ni Ruzuku za chama, ni ukosefu wa dira wa Mwenyekiti, ni ukosefu wa maadili wa mwenyekiti pamoja na exposure, ni kushindwa kukifanya chama kuwa cha hoja badala ya matukio, hizo ndizo ishu za kudiscuss''

Nashangaa kwasababu ni nyie nyie mnaosema CDM imekuwa ya watu fulani tu.
Well, sina uhakika na hilo ninachokiona ni kuwa uhalali wa watu hao mnautoa ninyi kama unavyosemeka hapo juu.

Mwenyekiti ni kiongozi tu wa kuratibu shughuli za taasisi.
CDM kama taasisi haipaswi kusubiri na kumtumai Mbowe aandike dira,vision au atende maadili.
Yeye ni mtu na si taasisi na kumtegemea kama mtu ni yale yale mnaoyakataa kuhusu CDM kuhodhiwa na watu.

Katika kutafuta utetezi mnajikuta katika kujichanganya. Leo Mbowe ni tatizo kwasababu anahodhi chama, that being said and done tunasoma tena maoni ya watu kuhusu CDM kukosa dira na maadili kwasababu ya Mbowe. Where is your position, mtahamisha magoli hadi lini.

 
Nguruvi unazungumzia sana Context katika hoja yako kwamba ni mojawapo ya kigezo cha uchambuzi wako juu ya mada hii.
Tukirudi katika context juu ya suala la umalaya versus mahusiano binafsi. Ni nini context ya maneno hayo.

Tukiangalia Mwenyekiti yeye ana ndoa, ana commitment ya kisheria (kiapo cha ndoa), kwa vyovyote hata akitembea na mtu mmoja tu nje ya ndoa amevunja commitment NA KWA SHERIA ZETU ZA NDOA AKIKAMATWA UGONI ANA KESI YA KUJIBU MAHAKAMNI KWA SABABU UGONI NI KINYUME CHA SHERIA!.

Tukiachilia mbali hilo, NINAAMINI M1, NA M3 WANAWAJUA VIZURI SANA KUHUSU MM PAMOJA NA MWENYEKITI, BILA SHAKA WANAJUA VIDOSHO VYA MWENYEKITI NA VIDOSHO VYA MM, NASHAWISHIKA KUSEMA MAHUSIANO BINAFSI YA MM HAYAJAFIKIA LEVEL YA KUITWA MALAYA!!!. LAU KAMA MIMI NA WEWE NGURUVI HATUJUI UNDANI WA KUHUSU HILO BASI MWIGAMBA ANAWEZA KUTUFAHAMISHA!!.

Ila ni dhahiri, kuchezea wanawake ovyoovyo siyo jambo jema na la kujivunia, AKINA M1 NA M3 WAMELIONA HILO NA WAMETAMBUA UMUHIMU WA KIONGOZI MKUU KUWA CLEAN, NA KWAO USAFI WA MAADILI WA KIONGOZI MKUU NI MOJAWAPO WA NYENZO YA KUIFANYA TAASISI IAMINIKE, IKUBALIKE (KUNA WATANZANIA WANAPIGA KURA KWA KUANGALIA MISINGI YA MAADILI YA VIONGOZI WANAOOMBA KURA).

Sasa tusiwalaumu Kina M3 na M1 kwa hoja yao hiyo, bali sisi kama Great thinkers ni lazima tuwajibu kwa hoja. HOJA KAIKA KIPENGELE HIKI NI MAADILI YA VIONGOZI , JE UMALAYA NI ISHU AU SIYO ISHU. HILI NDO JAMBO LA KUANGALIA BADALA YA KUANGALIA NANI KAITWA MALAYA NA NANI HAJAITWA!. BY THE WAY KUNA USHAHIDI WA KUTOSHA KATIKA WARAKA MAPUNGUFU YA MM YAKITAJWA WAZIWAZI, BILA SHAKA HATA MM HAKUPENDA ALIVYOANIKWA MLE!!

Ni lazima tuangalie Moyo wa waraka, Moyo wa waraka ni Kufanya "Mabadiriko chanya kwa Kubadili Uongozi wa juu, kuondoa mambo ya bussiness as usual, na kukirudisha chama katika katiba,Taswira njema mbele ya umma, nidhamu ya matumizi, na kukipa nguvu ya hoja".

Unaweza kudhani kuwa kina Mwigamba walikusudia kumtukana Mwenyekiti kwa kumuita Malaya, lakini Infact huenda walikuwa wanasema kweli!. NA BILA SHAKA HILO LIKAWA LINAWAKERA KWELI KWELI KINA MWIGAMBA KWA KUWA WANAAMINI HILO LINAHARIBU TASWIRA YA CHAMA MBELE YA UMMA NA HIVYO KUCHELEWESHA UKOMBOZI!. tuliangalie hilo katika context ya Hoja badala ya context ya Matusi ambayo naamini hawakukusudia hivyo!
 
Mkuu Kimweri , hoja yangu kwa upande wa kuvujisha siri za vikao imejikita kwa Mwigamba ambaye ni mshiriki mkubwa wa waraka. Wakati Laptop inakamatwa Mwigamba alikuwa ana post habari za kikao. Sijui hilo ni jema !

Umeleta point nzuri sana kuhusu kumfunga paka kengele, half courage na taboo kwa waandika waraka.
Hili ndilo nimekuwa nalisema kilas siku kuwa waandika waraka hawakuwa tayari kuleta mageuzi ya kweli ndani ya CDM

Ingalikuwa hivyo wangefanya yafuatayo
1. Kupeleka katika vikako, wakikataliwa watoke nje wakiwa na ushahidi wa kuzuiwa kusema
2. Kujiuzulu nafasi zao ili wasiwe panya bali simba wa kumfunga paka kengele.
3. Kutumia mikutano kusema wanachodhani si sahihi bila kujali hatma.
Leo wangekuwa mashujaa

Walichokosea
Kuingia katika vikao wasivyo viamini na kufikia maamuzi wasiokubaliana nayo huku wakiwa na vikao vyao. Walikuwa wanafanya u-spy badala ya kuchochea mabadiliko wakiwa viongozi.
Si kwamba ni unafiki bali ni upungufu mkubwa wa uongozi.
Kiongozi haongozi kutokea uani, anatangulia akibainisha misimamo,wapi anadhani watu waelekee.

Kuhusu CC niliwahi kusema kuna maamuzi yalifanyika kwa jazba nika sema tatizo la kina ZZK ni la muda mrefu. Uongozi umeshindwa kumrejesha katika mstari kwasababu kuu mbili

1. Yeye ni sehemu ya uongozi na bado alikuwa anahitajika kwa CDM kwa mujibu wao
2. Kukosekana kwa ushahidi hata pale penye ushahidi na ZZK amekuwa anatumia hoja ya kugombea kama kinga.Sijui kama leo kuna mtu angeamini chochote kwa kusikia tu bila kuona.

Nilisema kabla ya CC kuwa independent organ ingekuwa na utulivu zaidi wa kulishughulikia tatizo kuliko wana CC kwasababu zifuatazo

1. Kuna watu wameguswa moja kwa moja si kwa hoja bali wingu la matusi.
Mbowe atajisikiaje akijua kuwa public ishaambiwa kuwa ana akili ndogo n.k.
Lema atajisikiaje akisikia kuwa yeye ni 'Kichaa wa Arusha'

2. Wajumbe wengine walihamaki kufahamu kuwa ndani yao wapo wenzao waliokuwa wanawaona kama mazezeta.Mipango ya maandamano inapangwa kumbe kuna sympathizers wa Polisi wanapoua au kujeruhi wanachama wao. Kwamba kuna watu wapo tayari kuuza wenzao kwasababu tu kuna 'tunayemtaka'

3. Kundi lililokasirishwa na ukweli kuwa hivi Kitila aliyepewa dhamana kubwa ya chama anaweza kuwa katika usaliti wa kiwango hicho. Nasema usaliti kwasababu hana sababu za kutoshauri chama chao. Kuna wengine wanasema this is too much, ZZK anahujumu chama kila wakati na anapewa pass, yeye ni nani na kwanini.

Matokeo ya hayo ni 'knee jerk reaction' ambayo inaweza kwenda either way.
Knee jerk reaction hutokea pasipokufahamu hapo ndipo tunaona glass zinavunjwa, fulani katandikwa ngumi n.k.

Ukweli kuwa hawa watu walikuwa wanakusanya concern za watu ingekuwa ni nzuri endapo wangesimama na kusema hadharani. Au pia wangejiuzulu nafasi zao na kubaki wakipanga mkakati wa uchaguzi, hilo ni jambo la kawaida kabisa. Lakini wakiwa viongozi na kuchukua hatua za half courage tena wakijificha ni udhaifu wa hali ya juu sana.

Kama mshauri wa chama na naibu katibu mkuu hawataweza kusimama na kuvunja taboo hadharani wanataka uongozi ili wafanye nini? Tayari kushindwa kuvunja taboo ni failure katika leadership 'tunayemtaka' angekuwa na ujasiri gani wa kurudisha chama katika mstari kama taboo tu hakuweza.



 
Ndugu yangu unachotaka kunishawishi hapa ni kuwa kuna 'kamimba kadogo na Mimba kamili' wenyewe wanasema 'little bit pregnant'

Nimesema kuwa hoja za waraka bado hizinionodi katika ukweli kuwa naungalia waraka katika hali zote.
Unaposema kuna malaya kwasababu ameoa utakuwa huna ufahamu wa def ya umalaya.
Ni hivi umalaya ni umalaya tu hakuna umalaya wa sheikh, askofu n.k.

Ukisoma waraka kwa macho angavu bila kitambaa cheusi utaona waandikaji wamekerwa sana na tabia ya mwenyekiti inayoathiri taswira ya chama. Halafu wanajisahau na kumshauri 'tunayemtaka' afanye uzinifu kwa siri sana kwasababu uzinifu una nafuu kuliko umalaya! real.

Na hapa tunaona Pasco akisema yule hajaoa akiruka ruka na vibinti vya BAVICHA au akina mama wabunge ni kughafilikiwa lakini haina athari katika taswira.

Gamba la Nyoka anasema aaa! 'tunayemtaka' anaweza kufanya uzinifu kidogo tu 'one night stand' muhimu ajifiche lakini akionekana haina taabu sana kama mwenyekiti.
Real,waungwana kuna classification za uzinifu kweli!

Point ni kwamba waraka upo vague ukiusoma una ji contradict sana.
Nikupe kionjo kingine, waraka unasema mwenyekiti ana akili ndogo na elimu ya magumashi hafai kabisa kuongoza. Waraka huo huo unasema 'tunayemtaka' hana busara na ana jazba.
Kwamba unaodoa mwiba kwa ku replace na msumari. Waraka huo!

Waraka unasema mwenyekiti anatengeneza makundi ndani ya chama.
Waraka umeshindwa kuelewa kuwa Kitila na ZZK wanatengeneza makundi kwa kutumia waraka.
Tena unampamba 'tunayemtaka' hana makundi, uongo mkubwa, ZZ ndiyte mwenye Masalia 7, Juliana, Kafulila n.k.

Usomeni waraka muone jinsi unavyojichanga, kama kuna kitu too low nimekisoma siku za karibuni waraka umeshinda.
 

Kama haya ni mambo yaliyotakiwa yabaki ndani ya pazia, CC ya Chadema kwa nini waliyaruhusu yatoke nje?obviously Kitila Mkumbo na mwigamba hawakuleak waraka ule kama viongozi wa Chama.In other words, hawaku-validate tetesi za watu mtaani. walio-validate hayo ni CC ya CDM wenyewe.

nakubalina na wewe kila sehemu, kasoro hapa kwa kusema lawama za tabia chafu za kina mbowe wapewe kina Kitila.especially wakati sio wao walio-leak waraka.

Najua utasema Member wa JF ame-post umalaya wa Mbowe. Tukienda kwa tance hiyo basi Familia ya Kikwete watakuwa Drug lords(refer Hekaya za Jason bourne), Ridhiwani atakuwa Bilionea, na Kinana atakuwa Jangili wa Kuuwa Tembo. Hakuna aliyehukumiwa kwa lolote juu ya haya. Ila ikitokea siku Kina Nape mfano wakatoa Waraka kuyasema haya, then yatakuwa Validate in the face of Public Domain.
 

Ndugu Nguruvi3 , unasema mimi na Pasco tunahamisha magoli LAKINI UKWELI NI KWAMBA WEWE NDIYE UNAYEBADILI YALIYOANDIKWA KATIKA WARAKA NA KUTUNGA YA KWAKO, MFANO HAKUNA MAHALI KATIKA WARAKA PENYE HIYO SENTENSI NILIYOIWEKEA RANGI NYEKUNDU. hakuna mahali kwenye WARAKA PANAPOSEMA TUNYEMTAKA HANA BUSARA, HAKUNA!. HAYO MANENO UMEYATUNGA MWENYEWE.

infact waraka unasema hivi na ninanukuu "
Ana uwezo wa kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama mwenzao, wanawake humwona kama mtetezi wao wakatiwazee humwona kama kijana mwenye busaraanayeweza kuelekeza kama kiongozi".

Ni vyema tunapojadili Waraka huu, tuzungumze kile kitu halisi kilichozungumzwa ndani, na kama tunatumia maneno yetu halisi tueleze bila kuumba umba maana zetu zisizokusudiwa na Waraka.


Kuhusu Hoja uliyoitaja hapo juu, Jibu lake ni kwamba Waandishi wa waraka walikuwa wakifanya SWOT Analysis, waliainisha mapungufu ya Mwenyekiti na Wakaainisha Mapungufu ya Zitto. Kisha wakapima Nguvu na Udhaifu, Nguvu zikashinda. Kiufupi ni kwamba walikuwa honest katika analysis yao!.



Mathalani madhaifu ya Zitto waliyoainisha kwa uwazi kabisa ni haya!



na Nguvu Strength) za Wanayemtaka yaani Zitto ni Hizi

Uimara wa tunayemtaka:



NARUDIA TENA, HIYO WALIYOFANYA NI SWOT ANALYSIS, NJIA YA KISOMI YA KULINGANISHA MADHAIFU NA NGUVU ILI KUFANYA MAAMUZI SAHIHI, NI JUKUMU LETU MIMI NA WEWE NDUGU NGURUVI KUSEMA, IWAPO LABDA SWOT ANALYSIS HAIKUFANYIKA VYEMA, AU LABDA PARAMETERS ZILIZOTUMIKA HAZIFAI AU HAZITOSHI AU VICE-VERSA. LAKINI KUCHUKULIA UAINISHAJI WA PARAMETERS HIZO KAMA ETI NI CONTRADICTION YA MANTIKI KUSUDIWA NI KUTOKUFAHAMU VIZURI LENGO LA SWOT ANALYSIS HUSIKA LILIKUWA NINI.

KWA MAONI YANGU, HUU WARAKA NI WA KIZALENDO, NI WARAKA CHANYA, UNAOWEKA MBELE SI TU MUSTAKBALI WA CHAMA BALI TAIFA KIUJUMLA, NA NI MIONGONI MWA DOCUMENTS AMBAZO NINGEPENDEKEZA WANAOJIFUNZA STRATERGIES ZA MABADILIKO CHANYA KATIKA VYAMA VYA KIDEMOKRASIA KUSOMA!. NA UMENIPA IMANI KUBWA KWAMBA TANZANIA TUNA VICHWA VINAVYOWEZA KUTULETEA DEMOKRASIA YA KWELI!. BINAFSI NINGEKUWA MM NINGEUPOKEA MPANGO WA WARAKA MARA MOJA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…