Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

AshaDii, asante sana, nimekusoma ila naomba upitie kwa makini kidogo sehemu hii inayoelezea awamu tatu za namna ya kufanikisha mkakati kama ulivyoandaliwa kwenye waraka;
Awamu ya kwanza ni kuanzia sasa mpaka uchaguzi wa ngazi ya matawi utakapoanza said:
  • Kuhakikisha kwamba mtandao mzima umekamilika mpaka kwenye ngazi ya mkoa.
  • Kuspot makada kwenye wilaya na mikoa ambao tayari wana mtazamo tulio nao ama ambao wanaweza kuingiziwa kirahisi mbegu hii ya mabadiliko na wakawa tayari na wana uwezo na sifa za kushinda uongozi kwenye wilaya na mikoa yao bila kusahau sifa ya kuwa waaminifu wenye uwezo wa kutunza siri.
Kulingana na muda hii ni kazi inayotakiwa kufanyika sasa lakini kwa uangalifu mkubwa. Ni muhimu kukumbushana hapa kwamba katika awamu hii hakuna anayetakiwa kujua mpango mzima zaidi ya kamati ya kitaifa na MMili kuhakikisha uwezekano wa mkakati wetu mapema kwa wapinzani wetu unakuwa minimized to almost zero.
Hapa waandaaji wanapanga kufanya haya yote wakiwa sehemu ya uongozi wa juu wa Chadema kwa kuanzisha mtandao na kuunda kundi lililoaminifu linaloweza kutunza siri. Je lengo ni kuimarisha chama ama kudhoofisha chama?
Awamu ya pili ni kipindi kuanzia uchaguzi wa matawi mpaka uchaguzi wa mikoa unapokamilika said:
  • Kusaidiana na waratibu wa kanda na mikoa kuhakikisha makada tuliowaspot kwenye wilaya wanapanga safu zao kwenye kata ili kuhakikisha watakaochaguliwa kwenye kata ni watu wao ili waje wawachague kwenye wilaya.
  • Kuhakikisha wanaochaguliwa kwenye wilaya ni wale makada wetu ili nao waje wawachague kwenye mikoa yao.
Hapa ndipo kwenye kazi kubwa ya mkakati wetu na hapa ndipo tutakapohitaji kuingia gharama zaidi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia angalau 80.
Wakiwa bado ni sehemu ya uongozi wa juu wanaohudhuria vikao vya pamja wanapanga safu zao kwenye kata na wilaya na kuhakikisha wanaochaguliwa ni makada wao? na si Chadema? Je lengo ni kujenga chama au kubomoa chama?
Awamu ya tatu ni kuanzia baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mikoa hadi uchaguzi wa kitaifa utakapoitishwa said:
  • Katika kipindi hiki kwa ustadi mkubwa tutakuwa tukiwaandaa makada wetu waliochaguliwa tayari kuja kufanya mabadiliko makubwa kitaifa.
  • Ni wakati huu ambapo tutawaingizia mkakati taratibu lakini kwa ustadi mkubwa tukijikita hasa kwenye kuonyesha kwa nini tunahitaji mabadiliko.
  • Ni katika kipindi hiki ambapo kwa ustadi mkubwa tunaweza kuwaspot wale waliochaguliwa ambao hatukuwaandaa na kuwaingizia pia mbegu ya mabadiliko ili kuwawin na kuwarecruit kwenye mkakati.
Aidha katika awamu zote tatu kazi ya kuianalyze ofisi kuu itakuwa non stop kwa kuzingatia kwamba mabadiliko ya wakurugenzi na maofisa yatakuwa yanatokea na watu nao watakuwa wanabadilika kimtazamo. Analysis ya ofisi kuu ni kuhakikisha tunajua nani na nani wako na sisi na nani na nani wako against na pia nani na nani wanaweza kupandikiziwa mbegu kwa ustadi na wakaungana nasi.
AshaDii, hakuna lugha yoyote inayoweza kutumika kuelezea lengo la waandaaji wa huo waraka zaidi ya hujuma! Sasa hapa waandaaji watakuwa wanalalamikia nini kama na wao lengo ni kuunda makundi ndani ya chama ya wao na sisi. Sina hakika ungekuwa wewe ndio kiongozi mkuu wa Chadema ungejibu hoja gani hapo. Hebu urudi nyuma tujikumbushe moja ya madai yao kwa nini mabadiliko yalihitajika ndani ya Chadema;
...watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi, nk na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo.
Hawa, narudia, walikuwa ni viongozi wa juu ndani ya chama, je ni juhudi gani walifanya katika kulitafutia ufumbuzi hoja hii kama sehemu ya uongozi au ni mpaka pale wameukamata uongozi wenyewe? Chadema imeshuhudiwa ikiandaa "operations" mbali mbali nchini kwa lengo la kujiimarisha na kutoa elimu kwa wananchi mbali mabli, je wao wameshiriki vipi katika harakati hizo katika kukijenga, kukiimarisha na kukitangaza chama?

Kwa kumalizia nina maoni machache kwa watu wanaojaribu kujenga hoja kwamba kuna mgogoro ndani ya Chadema na hivyo njia ya usuluhishi na suluhu zingefaa kuliko ya kuwatimua wasaliti! Kwamba kwa kufanya hivyo CC imezidisha mgogoro na kuzidi kukidhoofisha chama au kwamba CC wamekurupuka kuchukua hatua walizochukua. Kufikiria kwamba kamati nzima ya Chadema ilichukua maamuzi kwa shinikizo la mtu moja k.m. kiongozi mkuu wa Chadema, ni kutoitendea haki kamati hiyo. Kufikiria kwamba mtu kama Tundu Lissu ambaye tulibahatika kumfahamu muda mrefu hata kabla ya Mbowe na Zitto katika harakati zake za kupigania haki au John Mnyika na wengineo eti leo hii wanakuwa misukule ya Mbowe ni kutokuwatendea haki. Je ni kweli wanaoeneza haya wanaitakia mema Chadema?
 
Ahsante sana Mag3
Niseme kuwa wale 'wanaotuhumiwa' kuchukua upande katika mjadala nikiwemo wanatumia waraka kuonyesha udhaifu dhahiri shahiri bila kificho, haya au soni.

Wale wanaosema waraka ni saafi! hawautetei kama ulivyo, wanautetea kwa hisia zao( jambo la haki kabisa).

Ni vema tungesaidiana kuuchambua ili tupate vipengele vyenye utetezi utakaojenga uhalali wa waraka.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana Mag3
Niseme kuwa wale 'wanaotuhumiwa' kuchukua upande katika mjadala nikiwemo wanatumia waraka kuonyesha udhaifu dhahiri shahiri bila kificho, haya au soni.

Wale wanaosema waraka ni saafi! hawautetei kama ulivyo, wanautetea kwa hisia zao( jambo la haki kabisa).

Ni vema tungesaidiana kuuchambua ili tupate vipengele vyenye utetezi utakaojenga uhalali wa waraka.
Nguruvi3, wapo wanaowatuhumu wenzao kwa kuchukua upande wakati wao katika huu mjadala wameonesha wazi kabisa kwamba kuna upande wanaouegemea. Mimi naunga mkono Kamati Kuu ya chama yenye wajumbe zaidi ya 30 kukaa na kuchukua maamuzi haraka dhidi ya kikundi kinachokiri kilikaa gizani kwa siri kupanga kuuhujumu uongozi halali wa chama. Lazima hapa tukumbuke kwamba hakuna namna waraka kama huu ungeweza kufanikiwa Chadema ikabaki salama bila kumeguka na kubaki vipande vipande.

Kwa vyovyote vile lengo hasa la waandaaji wa waraka lilikuwa ni kupanda mbegu ya uasi ndani ya chama na hivyo kuwezesha wanachama kugawanyika kimakundi...wao na sisi au kwa maana nyingine kusambaratisha chama. Kwamba kuna watu wanaendelea kutetea usaliti huo kinazidi tu kuthibitisha jinsi hatua iliyochukuliwa na uongozi ilikuwa sahihi na ilifanywa kwa wakati muafaka. Nina hakika kuwa madhara ambayo Chadema ingeweza kuyapata kama hatua za dharura zingechelewa kuchukuliwa ni makubwa zaidi.
 
Mag3 pengine kwa kuangalia ukakasi wa waraka ndio maana wengine wanasema ni vema pande zote zikaangaliwa.
Maana ya kauli hiyo ni kuweka mizani ili kuficha uvundo ndani ya waraka.
Nimeusoma zaidi ya mara 20, sijaona mahali penye nia ya kuisadia CDM au makakati wa kisiasa kwa maana hiyo.

Nilichoona ni mipasho tu, lakini mkakati wa kisiasa hakuna.
Nimeuliza maswali hapo nyuma ili kurahishisha mjadala, nadhani waungwana bado wanatafakari.
 
Last edited by a moderator:
Mag3 pengine kwa kuangalia ukakasi wa waraka ndio maana wengine wanasema ni vema pande zote zikaangaliwa.
Maana ya kauli hiyo ni kuweka mizani ili kuficha uvundo ndani ya waraka.
Nimeusoma zaidi ya mara 20, sijaona mahali penye nia ya kuisadia CDM au makakati wa kisiasa kwa maana hiyo.

Nilichoona ni mipasho tu, lakini mkakati wa kisiasa hakuna.
Nimeuliza maswali hapo nyuma ili kurahishisha mjadala, nadhani waungwana bado wanatafakari.
Ulishajibiwa na wana duru labda useme majibu hayajikufurahisha au kulizisha,wewe unataka sisi tukubali kuwa waraka ulikua hatari huko mbele ya safari,kitu ambacho sikubali zaidi ya hisia,kwani waraka usingevuja na Zito akagombea alafu akashindwa kwa kura je angefanya Mapinduzi!naeshimu mnacho andika,lakini tusitengeneze Athari sisi alafu tudai hali ingekua hivyo
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana Mag3
Niseme kuwa wale 'wanaotuhumiwa' kuchukua upande katika mjadala nikiwemo wanatumia waraka kuonyesha udhaifu dhahiri shahiri bila kificho, haya au soni.

Wale wanaosema waraka ni saafi! hawautetei kama ulivyo, wanautetea kwa hisia zao( jambo la haki kabisa).

Ni vema tungesaidiana kuuchambua ili tupate vipengele vyenye utetezi utakaojenga uhalali wa waraka.
Nguruvi3,
Mkuu kwanza nizungumzie hili swala la waraka na kwa nini nasema sii kosa wala hakuna Uharamu. Nitakueleza kwa kirefu na mifano nitaitoa wazi kabisa ili upate kuelewa kama nilivyoelewa mimi.

Katika chama chochote ikiwa mjumbe/wajumbe hawaridhiki na Uongozi wa juu kwa kuona kwamba uongozi huo unapwaya ama unapoteza dira, sii haramu kabisa ikiwa wajumbe hao watafanya mpango wa mageuzi ktk ngazi hiyo kupitia uchaguzi ujao na pasipo kuuweka ktk vikao vya chama unless wajumbe hao wameona kwamba yanayotokea ni makosa tu ya kiutendaji ambayo hayakudhamiriwa na uongozi. Lengo na nia ilikuwa nzuri isipokuwa makosa yamefanyika na sii wale walokusudia kukitumia chama kufanya yalokuwa haramu.

Kwa maana hi,i utashauri tu uongozi walofanya kosa pasipo kujua madhara yake hivyo ushauri wako utawaonyesha makosa na athari zake mbeleni ili wakirekebishe lakini sii wale walodhamiria kufanya kosa wakiona ni sawa na kwa faida yao ama wachache wakati wakiwaacha wengine kizani. Na kama utawashauri ilihali wao waliifanya siri basi elewa wataweka madai kuwa wewe ni muongo na ulete ushahidi, na kama unao ushahidi basi elewa watakaa chini na kufikiria mbinu za kukumaliza maana walichokifanya hawaoni uharamu wake isipokuwa siri ilofichuka..

Na kibaya zaidi basi ni kwamba, watu wa aina hii hawashauriki kwa sababu wameisha azimia kama vile JK au CCM na swala la wawekezaji toka nje. Viongozi wote wa CCM toka enzi ya Mwinyi walikuwa wakijipanga kuchukua miradi ya serikali kupitia Ubinafsishaji. Wameiuza nchi kwa kupitia 10% ktk uuzaji wa viwanda vyetu, wamechukua hisa toka mashirika ya nje ktk kuwapa vibali vya uchimbaji wa madini, mafuta na gas na sasa wameingia ktk umiliki wa ardhi na wanyama pori. Hii habari ya majangili na Unga unafikiri hawajui ama haina dawa? wanajua vizuri lakini ndio wameisha ifumbia macjho kwani hamjui wao wanahusika vipi, hadi siku atakapotoea mtu wa ndani na kuiweka hadharani.. Huyu atakuwa hatarini aidha kisiasa ama maisha yake.

Sasa usinambie kwamba mshauri wa JK ambaye anapingana na ufisadi huu anatakiwa kuyazungumzia haya ktk vikao vya chama ilihali viongozi wenyewe wameisha amua kujitajirisha wao kwanza wakati nchi inaingia kizani. Kiana huu uongozi ni wa Kidikteta, aidha uko nao ama utafute pa kutokea maana hapa kila mtu atachukua chake mapema. Katika mazingira haya unataka kunambia akitokea mtu ama kundi la watu ambao wameona yanayofanyika sii UTU wala haki na kuwa wanapoteza kabisa maana ya mrengo wa SIASA ya chama, wakajipanga ili uchaguzi unaofuata wawaondoe viongozi hawa ktk madaraka ya chama, hawa watu watakuwa WAHAINI?.

Hvi kweli wewe unamuona mtu kama Mnauye ni Mhaini maana kwa kila alolifanya toka mkakati (waraka)akiwatuhumu kina Lowassa, Rostam na wengineo. Na nina hakika nyuma ya Mnauye kuna sauti ya watu ambao wao wana chaguo lao la mtu ambaye wao wanamuona ataweza kuiongoza CCM kama chama kilichoasisiwa na mwalimu. Ama nikuulize wewe hivi kweli unaafikiana na wizi unaofanywa na viongozi wetu dhidi ya Watanzania ilihali umaskini wao sasa hivi unapanda kama presha ni zaidi ya asilimia 60. Halafu kwa kila kosa linalowatokea wao hutafuta Bangusilo ili kuwatuliza wananchi wakati watendaji haswa wa Ufisadi bado wapo madarakani?..

Je, ikiwa wewe hukubaliani na Mungu amekujalia umekuwa ktk wadhifa ambao unaweza kabisa kufanya mabadiliko (mageuzi) hutaitumia nafasi hiyo kuandaa mkakati utakao lenga kuwakomboa Watanzania?. Bila shaka mkuu wangu utajitahidi kadri ya uwezo wako kuokoa rasilimali zetu, utaifanya siri ama sii siri kuhakikisha Utawla huu unaondoka japo hutakuwa na lengo la kuiangamiza CCM. Na hakika uongozi huu wakigundua njama zako bila shaka watakuita Mhaini na msaliti maana unachotaka kufanya ni kinyume cha Kanuni pasipo kuona kwamba wao wenyewe walikiuka kanuni ya chama kwa kutokuwa wawazi, wakifanya mipango ya siri ambayo haikupitia kikao chochote cha chama. Na hakika ukiitwa Mhaini ama msaliti ktk kupinga Ufisadi basi ndio kwanza watakuongezea sifa na umaarufu.

Mkuu wangu hivi ndivyo nilivyouelewa waraka wa kina Kitila, na kama kweli yaloandikwa ktk waraka ule ni UONGO basi hawa watu wachukuliwe hatua zozote zile hata kufukuzwa chama kwa tunzi kama hiyo, lakini maadam hatuna majibu na inaonyesha kuna ukweli kuwa vitu hivyo vinafanyika ama vilifanyika, kumfukuza Zitto ktk uongozi na uanachama ni kufunika kombe mwana haramu apite kama JK alivyofanya ktk teuzi 3 za baraza lake ya mawaziri. Mara zote kafanya hivyo kufunika kombe na kweli sisi wanaharamu tumeyapita wakati ufisadi umewekwa mezani watu wanakula kwa mrija..

Nawaomba sana wenzangu nasi tusiwe double standard, tujaribu sana kuona nje ya box na kufuata misingi ya UTU wetu ambao accountability ndio kipimo halisi cha ufanisi wa kila mmoja wetu. Ebu litupie jicho hilo baraza jipya la mawaziri, naraza hili ni maandalizi ya uchaguzi wa 2015, hata kipofu ataliona akimbiwa. Kuna watu wamelalamika au wanalalamika kumuona Mwigulu ktk list ya manaibu waziri wakidai ni mwana siasa, sijui lele lele lakini CCM itaweza ipi kushinda uchaguzi pasipo fedha ya Takrima kutoka Hazina kama miaka ilopita? je na sisi CDM kama tukiwa IKULU mbona viongozi wote wa chama ndio watakuwa mawaziri!.

Nilipokishauri chama kuwa viongozi wa chama hawatakiwi kuwa wabunge wengi hawakuliona hili lakini ukweli unabakia kwamba kama sisi tutaingia madarakani hivi sasa basi itakuwa ni kama Ukomunist, maana viongozi wa juu wa chama ndio watakuwa viongozi wa juu wa serikali. Na hii inatisha hata kuifikiria tu kama vile tunavyoshangaa Mwigulu kuwa naibu waziri.
 
Last edited by a moderator:
Nimekuelwa Nguruvi3, wewe ni moja ya wadau wenye Michango mingi ambayo ni ushauri Chanya kwa Chadema toka kitambo. Na ninaposema Chanya I mean it ‘Literally'… Kwa misingi kuwa ingekuwa kweli Viongozi wa Chadema husoma yaliyopo hapa Great Thinkers (yakiwa yameelekezwa kwao) basi ina maana huyasoma kana kwamba wanasikuliza muziki. Yaani kwao ni burudani tu na wala hawana la kujishughulisha Zaidi ya kufurahia burudani hiyo na kuiacha hapo hapo. Kuna mifano ya mada nyingi sana, na kwa kutaja moja wapo ni (https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/167157-duru-za-siasa-mgongano-wa-mawazo.html) ambayo pia ipo applicable katika sakata hili la waraka. Chadema walikurupuka mno! Hawakujipanga. Matendo yao ni wazi yalikua yakifikiria vya hapo hapo na si mbele.

Lengo la Waraka (Kuwa na niya mbaya ama nzuri)

Kinachofanya kuwa na mgongano wa mawazo kama waraka ni sawa ama si sawa, ni kwa misingi tu ya namna ipi huo waraka ulipaswa kuchukuliwa.

Tatizo la Waraka lilipaswa kutazamwa kwa angle zote; nani kaandika, nani kaandikwa, nini kimeandikwa, kilicho andikwa kina ushahidi wowote? Na kila angle kufanyiwa kazi ipasavyo. Kufanikisha kulitatua hili tatizo ambalo linaendelea saizi Chadema ilipaswa wote walio guswa katika Waraka huo (Hasa Mbowe na Slaa) wasiwepo katika maamuzi juu ya Waraka, juu ya walio uandaa waraka na juu ya nini kifanyike in relation na waraka huo. Ingefanywa hivyo; then tungesema kweli Chadema kuna Demokrasia ya kweli!

Hatua ambazo zilipaswa kufuatwa katika kuelewa na kuamua endapo waraka ulikua na nia mbaya ama nzuri ni hizi;

1. Kuwepo waraka uliolenga mabadiliko ndani ya Chama ukihusisha watu wachache moja kwa moja hilo kimsingi ni kosa na kwa haraka sana inaweza eleweka kuwa Waraka ulikua na nia mbaya sababu kubwa ni kuwa ulikua wa siri. Hiyo ni hatua ya kwanza kabisa. Hili linafanya adhabu kuwa lazima kwa walioandaa waraka, ingawa narudi pale pale kuunga mkono hoja ya Mkuu Kichuguu – adhabu waliopewa ni kubwa mno!

2. Suala la msingi pia; waliohusika kuandika huo waraka walikua akina nani? In this case ni Mwigamba (Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Arusha na inaesemekana ni Accountant ambae aliingia Chadema kwa lengo la kurekebisha ufujaji wa pesa katika Chama) AND Kitila Mkumbo ambae kwa ufupi ni mtu ambae aliyekuwa akiaminika na wote katika mipango na maamuzi sahihi kwa maslahi ya Chadema. Hayo majina mawili tu, ni tosha kwa Waraka huo kutazamwa content na kuufanyia kazi tokana na FACT kua kuna uwezekano mkubwa sana kilichopo humo ni valid mana wahusika wote wanaielewa Chadema vilivyo kuliko mwanachama yeyote yule wa kawaida wa Chadema.

3. Ilipaswa kuangalia madai yote ya Waraka huo, hatua kwa hatua ili kuangalia endapo madai hayo yalikua valid ama haupo valid. Kitendo hicho kingetoa nafasi ya kufanyia kazi yaliyomo, na baadae ingewezekana hata kutoa adhabu pia kwa viongozi husika pale ingepo dhihirika kuwa yale walioandikwa ni kweli. Ni sawa na askari anapo ingia nyumbani kwako bila warrant - anapokukuta na kile alichokua anatafuta kikihusisha uhalifu (mf, madawa, mali ya wizi, mtu alouwawa n.k) - Kisheria ana uwezo wa kupewa adhabu (licha ya kuvumbua na kulitatua tatizo); ila hilo halizuii mhusika kuto adhibiwa.

4. Waraka ule ungejibiwa kwa hoja na kugusa kila kipengele. Ndio maana narudi kuwa Chadema walikurupuka. Walipo ona ule waraka wakachanganyikiwa mno na kutaka kuenda public ili kujisafisha juu ya Mwigamba ionekane walifanya maamuzi sahihi (Kumbuka suala la Mwigamba ilionekana wazi hata baadhi ya Wana Chadema hawakuridhishwa na maamuzi ya Viongozi juu yake). Wakaenda haraka sana public, mwisho wa siku walipotulia na kusoma content na kuona ina hoja za msingi wakakurupuka tena kuukataa kua ni feki. Hadi leo hii huo ambao ni original kwao wameshindwa ku deliver. Imebaki wazi kuwa huo waraka ndio hasa waraka wenyewe.


Tatizo tokana na hayo juu ni haya;


  • Waraka unazungumziwa sana kuwa ni kosa sababu ni wa siri; ila wengi hawataki kujadili yaliyo ndani ya waraka huo endapo ni kweli ama si kweli.
  • Viongozi walioshutumiwa katika waraka ndio walio husika kutoa maamuzi, sielewi hili limekaa vipi. Mwisho wa siku naona CC imeshindwa kufanya wajibu wao ipasavyo.
  • Namna sakata lote hili lilivyoendeshwa; Chadema imeumia zaidi kuliko Kiongozi yoyote yule wa Chadema. Wengi wanataka kuamini kua it was worth it sababu tu wanaona kana kwamba itammaliza Zitto kisiasa. Tafsiri hii si nzuri kwa Chadema, kwa namna moja ama nyingine inakua kana kwamba wanakubalia kuwa Zitto ni zaidi ya Chadema.

Naomba ni address maswali yako kwangu;



Mkuu, ni halali kabisa. Ni lazima uingie katika kikao – kukubaliana ama kukataliana na yaliyopo huja baada ya ushiriki na si vinginevyo.



Umeshakiri kuwa Kitila is Bright (whether directly ama through Insinuation); Huo Waraka unadhihirisha kabisa kuwa kuna uwezekano mkubwa sana wahusika (Waandaaji) wamejitahidi hapo nyuma kutumia njia sahihi na zilikwama. Kukwamba kwa njia hizo sahihi ikafanya kuwe na wale ambao wametaka mabadiliko kwa lazima; na hivyo kuandaa waraka kufanikisha hilo.

Ni rahisi kuamini hivyo tokana na nyenendo za Chadema zinaonyesha wazi viongozi wa juu wana sifa hizi ambazo ni maumivu na hulemaza Demokrasia.


  1. Hawashauriki – Hili wewe ni shahidi pia. Chadema (Viongozi na Wanachama) wanajitahidi sana katika ushiriki wa JF. Ni wazi ushauri wote wanaopewa uliolenga kujenga Chama wanausoma ila tu hawaufanyii kazi.
  2. Hawakosoleki – Chadema kuna double Standards, kuna viongozi wanaoruhusiwa kusemwa vibaya bila kujalisha ni kweli ama uongo, na kuna wale ambao hairuhusiwi kabisa kusemwa vibaya bila kujalisha ni kweli ama uongo. Hili unaliona wazi kabisa kila pale itokeapo Kiongozi wa Chadema (hasa Mbowe, Slaa, Lema na Lissu) wakisemwa vibaya – vile harakati za kufanya haraka ku clear hizo tuhuma zinazofanywa haraka sana. Tumeona mfano mzuri Zitto akisemwa vibaya mara zingine hata na vijana ambao inajulikana kabisa wapo katika payroll ya Chadema huwezi kuta harakati hizo zikifanywa.
  3. Mlolongo wa wale ambao wamesimamsihwa uongozi Chadema kwa makosa mbali mbali. Wao hutazama issues in black and white; wao hakuna shades of grey. Hilo ni tatizo kwao.



Utumiaji wa mitandao haukwepeki. Na hapa ndio narudi kwako Nguruvi3, where is the line crossed? Nani ana ruhusa ya kutumia mtandao na nani hana? So far katika matumizi ya Mtandao wote from Mbowe, Slaa, Zitto, pamoja na followers wao wote wana bidii ya kutumia mitandao kusambaza habari.

Nawalaumu Sana viongozi wa Chadema kwa haya;

Wapo too selfish! Wapo so busy kujitazama wao kama individuals, nani ni Zaidi ya nani? Hawana habari kabisa na Chadema kama taasisi; hilo ndilo linawafanya kufanya maamuzi mengi ya kukurupuka, pengine hata kuinua reputation ya mtu Fulani katika chama ila Chama kama chama kuzidi kudhoofu. Hilo ndilo linafanya hata Chadema kukosa collective agenda. Wana Agenda gani kama chama ambayo inawaunanisha viongozi wote? Ni lini mara ya mwisho Chadema walipigania kitu cha msingi kwa ajili ya jamii kwa pamoja kama chama? Kila kiongozi kashika lake kwa jitihada na nguvu zake, Ukija agenda ya Maji na Umeme ni Mnyika pekee, Ukija agenda ya ardhi ni Mdee pekee, ukija agenda ya tax evasion and Accountability ni Zitto pekee, kila mmoja akiwa na lake but hakuna lile ambalo ni collective.

If in any way nimegusia kurudisha nyuma kilichojadiliwa tayari, I apologize in advance.


Wakuu Kakalende & Mkandara, nimewasoma. Asante.


AshaDii;

Heri ya mwaka mpya. Nimeeleza katika posti kadhaa kuwa waraka sio tatizo na nafurahi kuona kuwa sipo peke yangu katika msimamo huo. Tatizo kubwa hapa ni failure of the party to rise up to the occassion.

CDM wamehamua kuwa ni chama cha kidemokrasia. Ukiondoa chaguzi la wengi, demokrasia ina misingi mingine mikubwa. Chama cha kidemokrasia ni lazima kifuate katiba ya nchi. Katiba na taratibu za chama hazitakiwi hata siku moja kuzidi katiba ya nchi. Katiba ya nchi inawaruhusu watu kushiriki katika political processes. Je kuandika waraka sio political processes?

CCM iliundwa kujenga Ujamaa na sio kuwapa nafasi watanzania au wanachama wake watimize wajibu haki zao za kikatiba. CDM na vyama vingine vya upinzani vilitakiwa kujitofautisha na CCM kwa kuwapa wanachama wake nafasi za haki kikatiba. Hivyo matatizo ya waraka yanakuja kwa sababu watu wanauwangalia waraka kwa mazoea yao.

Zitto akitangaza kuwa atagombea urais, tayari watu wanapata wasiwasi. Ukweli wa mambo haki ya kutangaza kuwa rais ni haki ya mtanzania yoyote. Katiba ya nchi haikatazi mtu kufikiri au kuwa na matamanio. Katiba ya nchi inakataza mtu asiye na sifa za kuwa rais kuwa rais.

Kuhusiana na utendaji ndani ya CDM, tayari chama kina mtu atakayegombe urais 2015. Hili ni tatizo kwa sababu vyama vingi vya siasa barani Afrika vinajiingiza kwenye matatizo kwa kuwa na wateule. Na mtu yoyote anaitishia nafasi ya uteule anakuwa msaliti japokuwa anachofanya kipo within the legal framework. Na waraka unaonekana kuwa na matatizo kwa sababu chama tayari kina safu zake za mapambano.

Hili kundoa migogoro kama hii, CDM inatakiwa ifanye mabadiliko ya kimuundo na kiutendaji. Kimuundo, chama kiwe shirikisho la watu wenye interest mbalimbali asa katika kipindi hiki cha mpito. Kama chama kilikubali kupokea rogue politicians kama Shibuda, ni lazima wakubali kuwa awa watu atakuwa free to express themselves. Na usipotaka utatumia muda mwingi katika PR damage control.

Kiutendaji wakubwa wa chama wawe na ambition za kujenga chama na sio kuwa viongozi wa serikali. Na wawe wanatoa nafasi kwa watu wengine ku-shine. Kwa sasa Dr. Slaa anapotembelea sehemu mbalimbali ana nia mbili. Kwanza anajiwekea mazingira ya kuwa rais. Pili anajenga chama. Hivyo mtandano anaojenga unaweza kuwa mzuri au kuleta matatizo ndani ya chama. Mtu akisema anataka mabadiliko ni sawa na kutukana juhudi alizofanya toka 2010.

Kwa maoni yangu, migogoro ya CDM ni ya kujitakia. Hakuna mchawi.
 
Ahsante sana Mag3
Niseme kuwa wale 'wanaotuhumiwa' kuchukua upande katika mjadala nikiwemo wanatumia waraka kuonyesha udhaifu dhahiri shahiri bila kificho, haya au soni.

Wale wanaosema waraka ni saafi! hawautetei kama ulivyo, wanautetea kwa hisia zao( jambo la haki kabisa).

Ni vema tungesaidiana kuuchambua ili tupate vipengele vyenye utetezi utakaojenga uhalali wa waraka.

Nguruv3;

Kuna kundi la tatu katika mjadala. Kundi hili aliangalii udhahifu au nguvu za waraka. Kundi hili linaangalia je waraka ulitakiwa kuleta migogoro ndani ya chama? Jibu hapana. Waraka ni kisingizio tu na kilichomo ndani ya waraka hakina umuhimu wowote ule.
 
Heri ya mwaka mpya. Nimeeleza katika posti kadhaa kuwa waraka sio tatizo na nafurahi kuona kuwa sipo peke yangu katika msimamo huo. Tatizo kubwa hapa ni failure of the party to rise up to the occassion.

CDM wamehamua kuwa ni chama cha kidemokrasia. Ukiondoa chaguzi la wengi, demokrasia ina misingi mingine mikubwa. Chama cha kidemokrasia ni lazima kifuate katiba ya nchi. Katiba na taratibu za chama hazitakiwi hata siku moja kuzidi katiba ya nchi. Katiba ya nchi inawaruhusu watu kushiriki katika political processes. Je kuandika waraka sio political processes?

CCM iliundwa kujenga Ujamaa na sio kuwapa nafasi watanzania au wanachama wake watimize wajibu haki zao za kikatiba. CDM na vyama vingine vya upinzani vilitakiwa kujitofautisha na CCM kwa kuwapa wanachama wake nafasi za haki kikatiba. Hivyo matatizo ya waraka yanakuja kwa sababu watu wanauwangalia waraka kwa mazoea yao.

Zitto akitangaza kuwa atagombea urais, tayari watu wanapata wasiwasi. Ukweli wa mambo haki ya kutangaza kuwa rais ni haki ya mtanzania yoyote. Katiba ya nchi haikatazi mtu kufikiri au kuwa na matamanio. Katiba ya nchi inakataza mtu asiye na sifa za kuwa rais kuwa rais.

Kuhusiana na utendaji ndani ya CDM, tayari chama kina mtu atakayegombe urais 2015. Hili ni tatizo kwa sababu vyama vingi vya siasa barani Afrika vinajiingiza kwenye matatizo kwa kuwa na wateule. Na mtu yoyote anaitishia nafasi ya uteule anakuwa msaliti japokuwa anachofanya kipo within the legal framework. Na waraka unaonekana kuwa na matatizo kwa sababu chama tayari kina safu zake za mapambano.

Hili kundoa migogoro kama hii, CDM inatakiwa ifanye mabadiliko ya kimuundo na kiutendaji. Kimuundo, chama kiwe shirikisho la watu wenye interest mbalimbali asa katika kipindi hiki cha mpito. Kama chama kilikubali kupokea rogue politicians kama Shibuda, ni lazima wakubali kuwa awa watu atakuwa free to express themselves. Na usipotaka utatumia muda mwingi katika PR damage control.

Kiutendaji wakubwa wa chama wawe na ambition za kujenga chama na sio kuwa viongozi wa serikali. Na wawe wanatoa nafasi kwa watu wengine ku-shine. Kwa sasa Dr. Slaa anapotembelea sehemu mbalimbali ana nia mbili. Kwanza anajiwekea mazingira ya kuwa rais. Pili anajenga chama. Hivyo mtandano anaojenga unaweza kuwa mzuri au kuleta matatizo ndani ya chama. Mtu akisema anataka mabadiliko ni sawa na kutukana juhudi alizofanya toka 2010.
Kwa maoni yangu, migogoro ya CDM ni ya kujitakia. Hakuna mchawi.
Zakumi , katiba ya nchi inatoa uhuru wa kushiriki political processes kama ulivyosema.

Hakuna shaka juu ya hilo, shaka ni kuwa hukuangalia vipengele vingine vya katiba vinavyomwekea mtu vikwazo pale anapokwenda nje ya mstari.

Katika waraka kama kungekuwa na sehemu inayozungumzia kuua 'wapinzani wetu' huo ungechukuliwa kama uhalaifu. Kwa nchi za wenzetu Polisi wangeingia kuuchunguza waraka bila mwaliko wa CDM. Ni katiba hiyo inayotoa uhuru kwa mkono wa kulia inazuia kwa wa kushoto

Katiba inayotoa uhuru wa kushiriki ndiyo iliyompa uwezo msajili wa vyama vya siasa kuikemea CDM kutokana na vipigo miongoni mwa wanachama wao wanaotekeleza Political processes.
Iweje msajili awazuie?

Katiba ya nchi imetoa uhuru wa kuanzisha vyama, hiyo haiondoi ukweli kuwa uanzishwaji na uendeshaji wa vyama lazima ufuate taratibu.

Unajichanganya kwasababu waandika waraka hawakuwa katika political processes walikuwa katika mkakati wa SIRI.

Waraka kama nyaraka ni sehemu ya Political process, tunaungalia katika contents, context na intent. Tukiyaangalia kwa pamoja waraka haukidhi yaliyokusudiwa kisiasa. Ni skeleton without flesh. Hakuna red meat in it at all. Contents ni horrible, context ni poor na intent ni abysmal

Hoja ya kwamba waandishi wa waraka walichokifanya kipo katika legal framework ina ukweli.
Hakuna sheria inayozuia wanachama kukihujumu chama chao.

Kuna maadili yanayoongoza taasisi yoyote ile. Maadili huambatana na taratibu ni mambo muhimu katika uaminifu, uadilifu na ustaarab.

Hakuna sheria inayomzuia daktari kucheza muziki. Yapo maadili yanayomzia kufanya hivyo katika katika baadhi ya maeneno. Medical ethics zinalenga kuweka standards ambazo ni accepted katika professional. Ethics ni tofauti na Law au regulations.

Kuhusu ZZK kugombea Urais au Uenyekiti,binafsi nipo katika rekodi za kusema mwenye matamanio na mwanachama wa chama cha kisiasa apewe fursa ya kuchagua na kuchaguliwa.

Hakuna sababu zozote za kumzuia mtu kama ZZK mwenye ambitions zake kufikia ndoto zake.

Lakini basi kila jambo lina mahali pake na wakati wake. Ni jambo la kushangaza kuona askari wapo vitani kamanda mmoja yupo bize kuandaa ndoa.
Ndoa ni halali na haki ya mtu lakini je, kuna busara za kuondoka mstari wa mbele wa vita na kwenda kufunga hiyo ndoa?

Wakati CDM wapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ZZK alikuwa bize akitangaza nia ya kuwania uenyekiti. Jambo hilo lilizua tafrani na kupeleka ujumbe tofauti kwa wapiga kura waliokuwa na fikra za CDM bila uhakika.
Kulikuwa na sababu zozote za ZZK kufanya hivyo kwa wakati huo? Kulikuwa na busara zozote kwa hilo?

Utetezi wa kila aina utatafutwa lakini hautafuta ukweli kwa waraka ulikuwa ni tatizo.
Kitila na ZZK wamethibitisha hilo kwa kukutaka kujiuzulu hata kabla Zakumi hajafikiria mbinu za kuhalalisha waraka
 
Nguruv3;

Kuna kundi la tatu katika mjadala. Kundi hili aliangalii udhahifu au nguvu za waraka. Kundi hili linaangalia je waraka ulitakiwa kuleta migogoro ndani ya chama? Jibu hapana. Waraka ni kisingizio tu na kilichomo ndani ya waraka hakina umuhimu wowote ule.
Well wakati ukiwa siri hilo halikuwa tatizo, ulipoingia katika public domain hilo ni donda.
Hivi Kitila angekaaje meza moja na Mbowe aliyemwita Magumashi, akili ndogo na malaya.
 
Tunapojadili waraka huu ni muhimu kuutazama waraka wenyewe na maudhui yake bila kutazama personalities za wanaotuhumiwa kuhusika na waraka. Mgongano wa fikra ninaouona hapa unabebwa zaidi na anayetuhumiwa kuwa mhusika mkuu ZZK. Sina uhakika kama ingekuwa ni mwanachama mwingine tu wa CDM angekuwa ndio mhusika wa waraka ule reaction yetu dhidi ya hatua zilizochukuliwa ingekuwaje...tungesema kuwa ameonewa au ameadhibiwa stahili yake?
 
Nguruvi3, nafurahi kuwa ni mengi ambayo tunakubaliana tunapokuja yale ambayo yanahusiana na Chadema. Likija suala la Waraka tunapishana padogo tu. Unazungumzia Waraka kuwa haramu na kutupia lawama zote kwa akina Kitila, kwa kukusoma hapa kaka naona kana kwamba hutaki kwenda nje ya (a) Kuona waraka ni Haramu (b)Kulaumu akina Kitila Mkumbo kuuandaa.

Tukienda hatua kwa hatua; hayo mimi nakubaliana nayo (a) & (b) ikiwa tunalitazama hili suala kwa ‘Right' and ‘Wrong' ila tu mimi nataka tuende Zaidi ya hapo kaka. I am sorry to say this; ila kiukweli umewapa credit kubwa sana akina Mbowe and Company na kuwanyima kabisa Kitila and Company. Hapa ndipo tunapishana. Mie nakubali waraka ni haramu na waandaaji ni sawa kuadhibiwa – LAKINI naenda a step Zaidi; yaliyomo kweye waraka (tuhuma kwa viongozi) yazingatiwe na kufuatiliwa (na body nje ya uongozi) . Yakizingatiwa yatatoa majibu yote… Naamini hivyo.

Ok, ume insinuate mahala Kitila alipwaswa ajitoe nafasi aliyopo endapo alikua hakubaliani na yale ambayo viongozi waliopo juu yake walikua hawafanyi? Naomba nikuulize haya;


  1. Huoni kama kujitoa ni dalili ya mtu kukata tamaa haraka katika kutaka kuleta mabadiliko chanya? Kwa mtazamo wake aliona kuwa hao viongozi wanaharibu; giving Mkumbo benefit of the doubt (tokana na umakini na busara aliyo onyesha siku zote huko nyuma)ni wazi katumia njia zote ambazo ni sahihi na hazikuzaa matunda – Unaniambia kuachia ngazi ndio ilikua njia sahihi? Nakataliana na wewe katika hilo! Change haiji kirahisi hivyo, ni lazima upiganie kuweza kufanikisha hasa kama imelenga kheri mwisho wa siku. Kuna msemo wa mmoja wa Thomas Jefferson unaingia vizuri hapa! ""The Democracy will cease to exist when you take away from those who are willing to work and give to those who would not." Hiki ndicho kimetokea Chadema. Na hiki si kwa Chadema tu! Tunapoelekea tokana na kukosa Chama makini ambacho ni mbadala wa CCM ili waweze kung'olewa madarakani, kuna hatari kikatokea kwa upana hata CCM.
  2. Ki mantiki na kwa misingi ya haki; toka kumkamata Mwigamba, kutangwazwa kupatikana kwa Waraka hadi kujulikana kwa MM wote - Nini maoni yako ya namna hili suala lote limeendeshwa na maamuzi yaliyotolewa? Unakubaliana na hatua na maamuzi yote yaliyochukuliwa na viongozi wa Chadema pamoja na CC kwa ujumla?

Tukija suala la Mwigamba; mfano mzuri sana ambao pia Chadema walikurupuka. Mwigamba aliweka mada hapa JamiiForums iliyo gharimu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha kwa kupitia jina ID name ya Maskini Mkulima. Aliweka mada ya "Kwa nini mabadiliko Chadema ni ya Lazima" ikiwa ni mwendelezo wa mada (WITO KWA CHADEMA) October 25, saa 18:56 (kama post inavyo onyesha) - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/540858-wito-kwa-wana-chadema-wote.html#post7652142.

Siku hiyo hiyo saa 23:53 Kurugenzi ya Habari ya Chadema ikatangaza kumsimamisha nafasi ya uongozi - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...baada-ya-kukiri-kusema-uongo.html#post7654260.

Naomba tuliangalie hili na tulitafakari kwa kujiuliza haya;


  1. Ilisemekana kikao cha Baraza la Uongozi kilikaa na kujadili. Baraza la Uongozi wa Chadema ni akina nani? (Kwa haraka haraka habari siku hiyo zinasema aliyekuwepo hapo ni Mbowe, Lema, Israel Natse, na viongozi wengine wa hapo Arusha) ndani ya masaa 3, mhalifu kakamatwa, waamuzi wamesha mobilise na maamuzi kuchukuliwa?
  2. Why maamuzi ya haraka hivyo? Ikiwa tayari walishachukua PC yake, tayari ishajulikana alichofanya, Kiongozi mkubwa kama Mwigamba hasa ukizingatia katoka eneo ambalo Chadema lina influence kuliko sehemu yoyote nchini – Walikua wanakimbizwa? Hapa ndio huwa nashangaa pale followers baadhi wa Chadema waki condemn viongozi wengine kutumia mitandao ya kijamii na hali pia wapo so Active.
  3. Nguruvi, naamini wengi hawajasoma content ya Mwigamba, na wengi hawajajua hasa ni ipi mada ilifukuzisha. Ukisoma hiyo content yake unapata picha ipi kuhusu Chadema na Uongozi wake? Unaichukulia vipi hiyo content – Kweli/Uongo/nusu ukweli ama nusu Uongo?

Disclaimer:-

Uwakilishi wangu wa suala hili la Mwigamba, Sina maana kuwa Mwigamba hakustahili kuvuliwa Uongozi. Nimetaka tuangalie utendaji wa such cases na viongozi wa Chadema na zaidi nataka tuende a step ahead – Kwa nini akili, maoni na maudhui mengi yanaelemea kutaka kuliangalia tendo na mtu mwenye ila hakuna anae taka kurudi kwenye contents za hivi vitu ili kuwaelewa viongozi wa Chadema na Chadema yenyewe?

Nina concern; Kuna mahala ambapo sijakuelewa ama nimekuelewa vibaya. Nguruvi una maana unasema matatizo yote yakivurugu yaliyopo CDM sasa causative ni ZZK? Take note nilipokua naungumzia suala la shades of grey nilikuwa silengi tu Zitto; I meant utendaji wa ujumla.

*Apologies on the delay in responding.
 
Nguruvi3,
Mkuu wangu waraka ulikuwa siri kama ilivyokuwa siri ktk utendaji kazi na matumizi ya ndani ya chama. Labda nitumie mtazamo wako na kusema ya kwamba Zitto, Kitila na wengineo wanaoitwa kundi la ZZK walifichwa vile vile ktk maswala ambayo waraka umeyagusia. Kama kweli ilikuwa uongo nina hakika kabisa viongozi waliopo wangeweka kila kitu wazi kuwasuta wakionyesha ukweli ili uongo ujitenge lakini wameshindwa na wameshindwa kwa sababu wanajua kuwa siri nzima imefichuka kama alivyoshindwa Kitila ktk kikako cha chama.

Tatizo kubwa la Chadema sasa hivi ni Zitto ambaye hakubali kumalizwa, yuko tayari kumwaga mboga tofauti na kina Kitila. Na hii ndio athari nilikuwa nikiizungumzia kila mara humu JF japo sikuwa muwazi zaidi. Chadema haikutakiwa kufikia hapa ilipo leo kwa sababu tu ya kugombania nafasi ya uongozi. Na nitasema tu kwamba Uharamu wa yote haya ni ile ari ya kila mmoja wao kutaka kuwa kiongozi wa Chadema kutokana na mfumo walokuwa nao ambao unawapa Ulaji. Kiongozi wa chama ndani ya Chadema ni hatua moja mbele inayokupa nguvu kubwa ya kujitangaza majukwaani kupata umaarufu ambao utamsaidia mtu ktk uchaguzi wa kitaifa.

Watazame hata vijana wake utawaona kila siku wanagombea nafasi ya uongozi BAVICHA,na wakishapata tu kesho wanagombea Ubunge! zaidi ya hapo kiongozi yeyote wa chama hata bavicha tu, ana sauti kubwa kitaifa kuliko wanachama wenye uwezo wa kiutendaji. Hivyo basi ni mfumo uliopo ambao unavuta shari zote hizi laa sivyo hakuna mtu angependa kuwa Mwenyekiti wa chama ikiwa mwenyekiti huyo angekuwa mtumishi wa chama tu na sii kuwania Ubunge, Uwaziri ama Urais maana pasipo kujijua hawa watu wanajipanga utafiri Chadema itachukua nchi kesho.

Mwisho labda nikuulize wewe swali moja. Huu ni mfano tu nautoa na sii hali halisi maana sijui ukweli ni upi..
1. Ikitokea Ukateuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, kisha ukakuta kuna madudu yanafanyika humo na wahusika wakuu ni JK, Mwinyi, Mkapa na viongozi wengine wakubwa wa CCM - Utafanya nini?
- Usinambie utajiuzuru tafadhali!
 
Last edited by a moderator:
Well wakati ukiwa siri hilo halikuwa tatizo, ulipoingia katika public domain hilo ni donda.
Hivi Kitila angekaaje meza moja na Mbowe aliyemwita Magumashi, akili ndogo na malaya.

Nitajibu kwa kuunganisha na posti iliyotangulia. Chadema inaongozwa kama CCM na kama chama cha siasa cha kwenye nchi yenye mfumo wa chama kimoja. Matukio yaliotokea yananikumbusha vita vya wahujumu uchumi. Watu walikamatwa kwanza na baadaye sheria ikatungwa.

Unachofanya wewe ni kutafuta makosa baada ya fact. Lakini wangeachia watu kutumia haki zao za kikatiba, kusingekuwa na kosa. Huwezi kuongoza chama kwa kutumia rumors.

Watu wanafanya juhudi za kijasusi kupata waraka. Wanapata waraka na kuona mambo wasiyotaka wanaona ni makosa.

Kwa mfano: Unampomtamani mke wa rafiki yako kwa sababu unazozijua na kuyaweka matamanio yako moyoni, kisheria hujafanya kosa lolote. Na ukirudi nyumbani na kuanza kuandika mashahiri kuelezea fantasies zako kuhusu mke wa rafiki yako, bado utakuwa hujafanya kosa lolote lile.

Rafiki yako ana haki ya kukushuku. Lakini akiamua kuja nyumbani kwako kutafuta ushahidi kwa kuiba mashahiri yako, yeye ndiye atakuwa chanzo cha mgogoro.

Kwa aibu ya mashahiri yako unaweza kuvunja urafiki. Lakini hiyo haikufanyi kuwa ulivunja sheria. Unavunja urafiki kwa sababu imani kati yako na rafiki yako imepotea. Imani kati ya kundi la Kitila na kundi jingine imepotea. Hivyo kujiuzuru kulikuwa ni kwa masuala ya kiutu uzima baada ya kutoaminiana.
 
Zakumi, Mwalimu, AshaDii, Mkandara, Nguruvi3, Mag3,

..je, amani inaweza kurudi ktk chama ikiwa Zitto na Mbowe watakaa pembeni ktk kinyanganyiro cha uenyekiti wa CDM?

..je, yupo kiongozi yeyote anayekubalika na Zitto na Mbowe na wapambe wao anayeweza kurudisha amani na umoja ndani ya CDM?

Jokakuu;

Kheri za Mwaka mpya. Wakiwa transparent katika matumizi ya chama na uendeshaji wa chama amani na umoja itarudi.
 
Hawa, narudia, walikuwa ni viongozi wa juu ndani ya chama, je ni juhudi gani walifanya katika kulitafutia ufumbuzi hoja hii kama sehemu ya uongozi au ni mpaka pale wameukamata uongozi wenyewe? Chadema imeshuhudiwa ikiandaa "operations" mbali mbali nchini kwa lengo la kujiimarisha na kutoa elimu kwa wananchi mbali mabli, je wao wameshiriki vipi katika harakati hizo katika kukijenga, kukiimarisha na kukitangaza chama?
Mag3 nashukuru kwa maoni yako. Nakubaliana nayo kabisa, ila bado mie msimamo wangu upo pale pale kua yapaswa hata yaliyomo kwenye waraka kutiliwa maanani in relation na wale walio husishwa. Ni kwa misingi hiyo silaumu maamuzi ya Viongozi wa Chadema ingawa bado wana mapungufu makubwa kwa namna walivyo liendesha suala zima.

Mag3 naomba nikumbushe kuna tofauti kubwa ya kujenga chama nje ya chama na kujenga chama ndani ya Chama. Upande wa Chadema naweza nikasema wanafanikiwa kujenga chama nje ya chama chao lakini jitihada hizo ni hafifu ndani ya chama kiasi kwamba hata kinawadhoofisha once in a while. Hivyo in this case hatuangalii hilo kwa akina Kitila.

Kuelewa juhudu zao katika kujenga chama ndani ya chama - hapo ndipo tatizo linakuja, hatuwezi kujua ni juhudi zipi zilifanywa bila kuwauliza wao moja kwa moja. Hilo linatufanya watazamaji tujigawe katika makundi mawili. (a) wale ambao wanaamini Kitila & Co walishafanya juhudi nyingi ikashindikana hadi kuwasukuma kuuandaa waraka. (b) wale ambao wanaamini moja kwa moja kuwa hakufanya juhudi zozote alichagua tu njia ya kuandaa waraka. Whatever the case akina Kitila wanaelewa Zaidi hapa kuliko yeyote anayeweza liwakilisha hapa.

Sina hakika ungekuwa wewe ndio kiongozi mkuu wa Chadema ungejibu hoja gani hapo. Hebu urudi nyuma tujikumbushe moja ya madai yao kwa nini mabadiliko yalihitajika ndani ya Chadema;

Kuna hoja za kujibu sana; hizo hoja ni nzito na ni hoja ambazo zimekua zikijirudia mara kwa mara. Hoja ambazo ikiwa kuna vielelezo ilipaswa tu viwekwe sawa. Hasa katika vipengele vinavyohusiana na pesa… Mana tunajua fika kiongozi yeyote yule ambaye ni mroho wa pesa na anajiingiza kujinyakulia pesa ambazo si zake kwa njia ambazo si halali – Ufisadi katika uongozi wake hauepukiki! Kwa maneno mengine kiongozi kama huyo akichaguliwa kuiongoza nchi kutakua hakuna tofauti na sasa.

Madai ambayo yanapaswa kufuatiliwa kwa karibu na kutolewa ufafanuzi ni haya;

  1. Matumizi ya pesa ya taasisi – Chadema siyo ya watu watatu tu (so far ndio watu wanaojua matumizi hayo ya pesa yanavyoenda); kwa taasisi kubwa kama hiyo ni lazima iwe accountable hizo pesa zinatumika vipi, na record ya matumizi hayo yawe public (hilo ni wazi na halina ubishi); kama waraka unavyojieleza, maamuzi na matumizi yapo mikononi mwa wachache. Hilo ni tatizo kubwa else kama mnali underestimate ukubwa wake.
  2. Njia haramu za kubaki Madarakani – Na hili kwa mtazamo wangu ndio linaleta matatizo makubwa Chadema; Uongozi wa juu, upatikanaji wake na ushiriki wa wengine katika nafasi hizo. Kwa wale ambao huwa mnafuatilia habari hapa JF mara kwa mara liliwahi kuletwa hili hapa kama tetesi (kua Viongozi wa Chadema kuna kipengele wamekitoa katika katiba ya Chama ili ku prolong muda wa uongozi uliopo), na mdau aliyeleta hii habari alitukanwa sana kuwa katumwa. Kwa haraka sana tokana na udhaifu wa Chadema ya kila mmoja kutaka kuwa msemaji - Hiyo habari ilikanushwa haraka na mmoja wa viongozi wa Chadema. Habari ililetwa tena safari hii ikiwa na ushahidi wa Kipengele kilivyokuwa awali na kilivyo sasa (baada ya kubadilishwa), hapo sasa Chadema wakaja na utetezi wa kwa nini hicho kipengele kilirekebishwa, safari hii wakikubali kua mabadiliko yalifanywa. Mag3 hayo mambo madogo madogo, yakikusanywa ndiyo yanayozidi kui discredit CHADEMA.
  3. Baadhi ya utendaji wa Uongozi mkuu.

Kwa kumalizia nina maoni machache kwa watu wanaojaribu kujenga hoja kwamba kuna mgogoro ndani ya Chadema na hivyo njia ya usuluhishi na suluhu zingefaa kuliko ya kuwatimua wasaliti! Kwamba kwa kufanya hivyo CC imezidisha mgogoro na kuzidi kukidhoofisha chama au kwamba CC wamekurupuka kuchukua hatua walizochukua. Kufikiria kwamba kamati nzima ya Chadema ilichukua maamuzi kwa shinikizo la mtu moja k.m. kiongozi mkuu wa Chadema, ni kutoitendea haki kamati hiyo. Kufikiria kwamba mtu kama Tundu Lissu ambaye tulibahatika kumfahamu muda mrefu hata kabla ya Mbowe na Zitto katika harakati zake za kupigania haki au John Mnyika na wengineo eti leo hii wanakuwa misukule ya Mbowe ni kutokuwatendea haki. Je ni kweli wanaoeneza haya wanaitakia mema Chadema?

Maoni yako haya naomba niende na wewe tofauti. Believe you me Chadema kama taasisi kubwa walikua na uwezo wa kuwamaliza akina Kitila & Co. kwa njia alternatives na taratibu ambazo zingekua ni za kujenga kuliko kubomoa.

Hivi unadhani kuwa baada ya wao kujulikana nia yao wangetengwa huko na kutupiliwa mbali bila kuhusishwa kungekua na tofauti yoyote ile na kama walivyofukuzwa? Inawezekana ndio wamefanya sawa ila huu ulikua si wakati wake. Hawajawa calculative, na ndio narudi pale pale hilo ni tatizo la kutazama mtu badala ya kuitazama taasisi. Na ndio maana kunakua na discussions za kiongozi is bigger than Chadema. Kufika kote huko kwa namna moja ama nyingine hiyo ni insult kwa Chadema as a whole na si sit u kwa viongozi wa CHADEMA.


Nimekupata Nguruvi3, pamoja saana. Wakuu Zakumi and JokaKuu nitarejea hizo post, nashukuru kwa maoni yenu.
 
Zakumi, Mwalimu, AshaDii, Mkandara, Nguruvi3, Mag3,

..je, amani inaweza kurudi ktk chama ikiwa Zitto na Mbowe watakaa pembeni ktk kinyanganyiro cha uenyekiti wa CDM?

..je, yupo kiongozi yeyote anayekubalika na Zitto na Mbowe na wapambe wao anayeweza kurudisha amani na umoja ndani ya CDM?
JokaKuu
Sidhani kama mgogoro uliopo unaweza kumalizika kwa Zitto & Mbowe kukaa pembeni pekee...suluhisho halitapatikana kutokana na majina ya watu fulani tu.

Nimewahi kusema huko nyuma kwamba CDM pamoja na kuwa hivi sasa ina nguvu na ndio chama kikuu cha upinzani lakini bado haijafikia ultimate goal...ambayo ni kuchukua dola! Ili kufikia lengo hili kuu ni lazima wasimame kama kitu kimoja na kutekeleza malengo yao kwa pamoja. Huu sio wakati kwa wao kulumbana kuwa nani anafaa kuwa zaidi kuwa mwenyekiti au nani anafaa zaidi kugombea urais...inawapoteza taratibu kutoka kwenye lengo kuu.

Tumetumia muda mwingi kujadili uhalali au uharamu wa waraka huu lakini one this is for sure. Endapo mkakati huu ungefanikiwa sidhani kama ungeondoa mgawanyiko na makundi ndani ya chama zaidi ya kuzidisha mpasuko. Hao ambao wangeng'olewa sidhani kama wangekubali kuondoka kimya kimya bila kupigana, mwisho wa siku 2015 inawakuta wakiwa sio wamoja na kwa hilo hawawezi kufanikiwa.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,
Mwisho labda nikuulize wewe swali moja. Huu ni mfano tu nautoa na sii hali halisi maana sijui ukweli ni upi..
1. Ikitokea Ukateuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, kisha ukakuta kuna madudu yanafanyika humo na wahusika wakuu ni JK, Mwinyi, Mkapa na viongozi wengine wakubwa wa CCM - Utafanya nini?
- Usinambie utajiuzuru tafadhali!

Kuna option nzuri zaidi ya hiyo?
 
Back
Top Bottom