Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
AshaDii, asante sana, nimekusoma ila naomba upitie kwa makini kidogo sehemu hii inayoelezea awamu tatu za namna ya kufanikisha mkakati kama ulivyoandaliwa kwenye waraka;
Kwa kumalizia nina maoni machache kwa watu wanaojaribu kujenga hoja kwamba kuna mgogoro ndani ya Chadema na hivyo njia ya usuluhishi na suluhu zingefaa kuliko ya kuwatimua wasaliti! Kwamba kwa kufanya hivyo CC imezidisha mgogoro na kuzidi kukidhoofisha chama au kwamba CC wamekurupuka kuchukua hatua walizochukua. Kufikiria kwamba kamati nzima ya Chadema ilichukua maamuzi kwa shinikizo la mtu moja k.m. kiongozi mkuu wa Chadema, ni kutoitendea haki kamati hiyo. Kufikiria kwamba mtu kama Tundu Lissu ambaye tulibahatika kumfahamu muda mrefu hata kabla ya Mbowe na Zitto katika harakati zake za kupigania haki au John Mnyika na wengineo eti leo hii wanakuwa misukule ya Mbowe ni kutokuwatendea haki. Je ni kweli wanaoeneza haya wanaitakia mema Chadema?
Hapa waandaaji wanapanga kufanya haya yote wakiwa sehemu ya uongozi wa juu wa Chadema kwa kuanzisha mtandao na kuunda kundi lililoaminifu linaloweza kutunza siri. Je lengo ni kuimarisha chama ama kudhoofisha chama?Awamu ya kwanza ni kuanzia sasa mpaka uchaguzi wa ngazi ya matawi utakapoanza said:Kulingana na muda hii ni kazi inayotakiwa kufanyika sasa lakini kwa uangalifu mkubwa. Ni muhimu kukumbushana hapa kwamba katika awamu hii hakuna anayetakiwa kujua mpango mzima zaidi ya kamati ya kitaifa na MMili kuhakikisha uwezekano wa mkakati wetu mapema kwa wapinzani wetu unakuwa minimized to almost zero.
- Kuhakikisha kwamba mtandao mzima umekamilika mpaka kwenye ngazi ya mkoa.
- Kuspot makada kwenye wilaya na mikoa ambao tayari wana mtazamo tulio nao ama ambao wanaweza kuingiziwa kirahisi mbegu hii ya mabadiliko na wakawa tayari na wana uwezo na sifa za kushinda uongozi kwenye wilaya na mikoa yao bila kusahau sifa ya kuwa waaminifu wenye uwezo wa kutunza siri.
Wakiwa bado ni sehemu ya uongozi wa juu wanaohudhuria vikao vya pamja wanapanga safu zao kwenye kata na wilaya na kuhakikisha wanaochaguliwa ni makada wao? na si Chadema? Je lengo ni kujenga chama au kubomoa chama?Awamu ya pili ni kipindi kuanzia uchaguzi wa matawi mpaka uchaguzi wa mikoa unapokamilika said:Hapa ndipo kwenye kazi kubwa ya mkakati wetu na hapa ndipo tutakapohitaji kuingia gharama zaidi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia angalau 80.
- Kusaidiana na waratibu wa kanda na mikoa kuhakikisha makada tuliowaspot kwenye wilaya wanapanga safu zao kwenye kata ili kuhakikisha watakaochaguliwa kwenye kata ni watu wao ili waje wawachague kwenye wilaya.
- Kuhakikisha wanaochaguliwa kwenye wilaya ni wale makada wetu ili nao waje wawachague kwenye mikoa yao.
AshaDii, hakuna lugha yoyote inayoweza kutumika kuelezea lengo la waandaaji wa huo waraka zaidi ya hujuma! Sasa hapa waandaaji watakuwa wanalalamikia nini kama na wao lengo ni kuunda makundi ndani ya chama ya wao na sisi. Sina hakika ungekuwa wewe ndio kiongozi mkuu wa Chadema ungejibu hoja gani hapo. Hebu urudi nyuma tujikumbushe moja ya madai yao kwa nini mabadiliko yalihitajika ndani ya Chadema;Awamu ya tatu ni kuanzia baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mikoa hadi uchaguzi wa kitaifa utakapoitishwa said:Aidha katika awamu zote tatu kazi ya kuianalyze ofisi kuu itakuwa non stop kwa kuzingatia kwamba mabadiliko ya wakurugenzi na maofisa yatakuwa yanatokea na watu nao watakuwa wanabadilika kimtazamo. Analysis ya ofisi kuu ni kuhakikisha tunajua nani na nani wako na sisi na nani na nani wako against na pia nani na nani wanaweza kupandikiziwa mbegu kwa ustadi na wakaungana nasi.
- Katika kipindi hiki kwa ustadi mkubwa tutakuwa tukiwaandaa makada wetu waliochaguliwa tayari kuja kufanya mabadiliko makubwa kitaifa.
- Ni wakati huu ambapo tutawaingizia mkakati taratibu lakini kwa ustadi mkubwa tukijikita hasa kwenye kuonyesha kwa nini tunahitaji mabadiliko.
- Ni katika kipindi hiki ambapo kwa ustadi mkubwa tunaweza kuwaspot wale waliochaguliwa ambao hatukuwaandaa na kuwaingizia pia mbegu ya mabadiliko ili kuwawin na kuwarecruit kwenye mkakati.
Hawa, narudia, walikuwa ni viongozi wa juu ndani ya chama, je ni juhudi gani walifanya katika kulitafutia ufumbuzi hoja hii kama sehemu ya uongozi au ni mpaka pale wameukamata uongozi wenyewe? Chadema imeshuhudiwa ikiandaa "operations" mbali mbali nchini kwa lengo la kujiimarisha na kutoa elimu kwa wananchi mbali mabli, je wao wameshiriki vipi katika harakati hizo katika kukijenga, kukiimarisha na kukitangaza chama?...watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi, nk na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo.
Kwa kumalizia nina maoni machache kwa watu wanaojaribu kujenga hoja kwamba kuna mgogoro ndani ya Chadema na hivyo njia ya usuluhishi na suluhu zingefaa kuliko ya kuwatimua wasaliti! Kwamba kwa kufanya hivyo CC imezidisha mgogoro na kuzidi kukidhoofisha chama au kwamba CC wamekurupuka kuchukua hatua walizochukua. Kufikiria kwamba kamati nzima ya Chadema ilichukua maamuzi kwa shinikizo la mtu moja k.m. kiongozi mkuu wa Chadema, ni kutoitendea haki kamati hiyo. Kufikiria kwamba mtu kama Tundu Lissu ambaye tulibahatika kumfahamu muda mrefu hata kabla ya Mbowe na Zitto katika harakati zake za kupigania haki au John Mnyika na wengineo eti leo hii wanakuwa misukule ya Mbowe ni kutokuwatendea haki. Je ni kweli wanaoeneza haya wanaitakia mema Chadema?